KIZA KINENE
MSIMU WA KWANZA
SEHEMU YA KWANZA
Director13
Weekend moja tulivu sana ya siku ya Jumamosi,Maeneo ya Mikocheni,Nilikua Saloon kujiandaa na harusi yangu,na hiyo ilikua siku yangu mbaya pia katika maisha yangu.Nilikua nikijiaangalia kwenye kioo jinsi nilivyopendeza na kila aliyeingia alinishangaa na alinisifia kua nimependeza sana.Nilijisikia vizuri kusifiwa ila chozi lilinidondoka kwa ujasiri niliotaka kuonyesha siku ya leo nikajifuta ili nisiharibu makeup yangu.Nilichukua simu yangu nikajipiga selfie mbili kali za kumbukumbu.Nikawatumia rafiki zangu wa karibu kuwajulisha kama niko tayari kwa siku ya leo,na hiyo ilikua mara yangu ya kwanza kupaka makeup na pia mara yangu ya kwanza kuona nimependa.Sauti ilipita kichwani ikisema
“Weee Queen,Mtoto wa Mama Ntilie,leo hii uko ndani ya shela la bei mbaya,hakika umeweza”
Nilishusha pumzi na kujiongelesha mwenyewe kimya kimya
“Mtoto wa Mama Queen,Relax,Usipanic,Usiniangushe,Mfurahishe mama yako”
Ghafla,simu yangu iliita na hakua mtu mwengine zaidi ya Mama yangu mzazi,Mama Queen alikua akinipigia simu.
Mama:Mwanangu,Nakujua ila nakuomba usinitie aibu kwa siku ya leo jikaze tu hii siku ipite kimya kimya baadae tutajadili vizuri.
Queen:Mamaaa,Nafanya hivi vyote kwa ajili yako lakini sio sawa kabisa,sio sawa.
Mama:Mwanangu,najua ila unapenda hizi dhiki ziendelee,Nimechoka mwanangu maisha ya dhiki,maisha yasiyo na mwanga.
Queen:Naelewa Mama ila mbeleni naona Kiza Kinene,Kiza Kinene sana Mama.
Mama:Mwanangu ndio maana nimekupigia,chonde,chonde chonde,usiniangushe
Queen:Ulimcheck Kaka Albert maana nimejitahidi sana kumtafuta toka week mbili ziliyopita ila hapatikani.
Mama:Atakua busy na issues zake,akipatikana tu nitamjulisha.
Queen:Sidhani kama Kakaangu atafurahia hili jambo.
Mama:Tutaongea Mwanangu.
Mama alikata simu,na Mimi nilifatwa na Matron wangu akinitaka nitoke tuelekee kanisani kwa ajili ya ndoa.Nilimpatia simu Dada yangu kipenzi ambaye nilishare nae Baba,Dada Julieth ndiye pekee anayeshirikiana na sisi na tumefanana sana na Dada yangu.
Julieth:Usiogope Queen,Mdogo wangu,naamini Sebastian ni Mwanaume mzuri sana na atakua mzuri pia kwako.
Queen:Okay Dada,Ahsante
Nilimkumbatia Dada yangu na kuanza safari ya kuelekea kanisani,Tulielekea Maeneo ya Mbezi Beach na nilikuta tayari Bwana harusi yaani Mume wangu mtarajiwa alishafika ukumbini akiwa ananisubiri kwa ajili ya kuingia kanisani.
Tuliingia kanisani na kuanza taratibu zote za ndoa,katikati ya taratibu hizo aliingia msichana mrembo sana,mwenye shape nzuri akiwa amevalia gauni nyekundy na alipendeza sana,kunukia vizuri kila mtu alimuangalia yeye kwasababu alivaa viatu vya juu juu na vilikua vikitoa sauti sana alivyokua anatembea.Alikaaa na kuendelea kusikiliza zoezi la ndoa likiendelea.
Kama ilivyopangwa zoezi la ndoa lilitimia na rasmi nikawa Mke halali wa Sebastian Shayo.Marafiki zangu na ndugu zangu walinipongeza sana na nilionyesha furaha mbele yao na pia tulipata picha za ukumbusho pamoja na Mume wangu na ndugu,jamaa na marafiki.
Ila Mume wangu hakua na furaha kabisa hata ya kuzuga,Mda wote alimuangalia yule Msichana aliyevalia nguo nyekundu.Mpaka aliamua kumfata na kuanza kuongea nae kama anambembeleza na yule Msichana anamjibu kwa dharau fulani,Nilivyoona hivyo nilikua busy kuongea na Dada yangu Julieth ila dadaangu hakusita kuniuliza kuhusu Mume wangu.
Julieth:Mdogo wangu,Unatakiwa uwe makini na mume wako.
Queen:Naelewa Dada
Julieth:Sijui yule Msichana ni nani?
Queen:Nadhani ni Msichana wake
Julieth:Msichana wake? Kivipi?
Queen:Da’Julieth,Hii ni story ya siku nyengine tukikutana.
Julieth:Mmmhhh,Sawa ila kua makini na Mumeo.
Mara niliona Mama yangu Mkwe,aliwafata Sebastian na yule Mdada na kuongea nao,Ghafla niliona Sebastian anakuja upande wangu huku akiwaacha Mama yake na yule msichana wakiongea.Sebastian alinifata hadi nilipo na kunishika mkono kunisogeza pembeni na kumuacha Dada yangu Julieth akiwa amesimama peke yake.
Queen:Sebastian,Nini lakini,mbona tunavutana hiviSebastian:Unatakiwa ujue nimekuoa kwasababu ya Mama na Baba yangu ila vyenginevyo nisingekuoa,nina sababu ya kufanya hivi.
Queen:Hilo najua kwani kuna lingine tofauti na hilo,Maana hata mimi unajua nimeolewa na wewe kwasababu ya Mama yangu na Wazazi wako.
Sebastian:Na Tamaa zako za pesa
Queen:Mimi sitaki kubishana na wewe hapa,tutakutana nyumbani kwetu.
Sebastian:Twende ukabadiki nguo,Tujiandae kwa ajili ya White party kwa ajili ya kuagana na rafiki zangu.Si unajua hakuna party ya usiku.
Nilimuangalia Sebastian wala sikumjibu,alizuga kwa kunishika mkono na kuelekea kwenye gari zuri la kifahari.Niliingia kwenye gari nilinyamaza kimya ila yeye alikua busy na simu kuongea na Msichana wake.Niliwasha simu yangu na ziliingia msg kutoka kwa Boyfriend wangu ambaye nilikua niko nae kimapenzi.
“Queen,kweli kabisa kipenzi changu mimi,umekubali kuolewa na Mwanaume mwengine na kuniacha mimi kwa sababu ya Pesa”
Nilijisikia vibaya sana na niliumia moyo kuona text aliyonitumia Damian wangu.
Kiukweli nilimkosea sana ila hajui ni kiasi gani ninampenda ila ni shida tu ndio zilizopelekea yote haya ila siwezi kumsahau Damian wangu hata siku moja na lazima nihakikishe natoka katika hii ndoa.
Hatimaye,Tuliingia kwenye hotel moja ya kifahari hapa Bongo,Mume wangu Sebastian,alinishika mkono na kunipeleka chumbani kwetu ambako tutalala kwa siki hiyo.
Nilifurahia mazingira na nilitamani ningekua na Mpenzi wangu Damian Damian.Nilichunguza kila kona ya chumba kila kitu kilikua poa sana,niliingia bafuni nikaoga na kuvaa nguo nilizochaguliwa na huyo Mume wangu.
Nilivaa kiukweli nilipendeza,aliingia Mdada wangu wa Makeup na kunipamba kiasi,Nilipendeza mno na kila kitu nilichokivaaa nilionekana kinaendana na mimi,Baada ya nusu saa alikuja Sebastian na kuniamrisha tutoke kama niko tayari.Nilitoka na kuelekea nae hiyo sehemu waliyoandaa party na rafiki zake.Hapo niliona vijana tu hakukua na watu wazima,kila aliyekuwepo hapo alikua yuko na Mpenzi wake na wote walikua wamependeza ila baada ya mda waliingia wasichana watano wakiwa wamevalia vizuri pia ila hawakua na watu wao.lakini pia waliingia wakaka watatu nao hawakua na wasichana wao.
Party ilianza ila nilikua na hofu sana kwasababu hakukua na mtu hata mmoja ambaye nilimfahamu.Kila aliyeingia alienda kuongea na Sebastian ila hakukua na mtu wa upande wangu na wakati niliwapa taarifa,nilijisikia vibaya kama dakika kumi zilipita aliingia rafiki yangu mmoja na Dada yangu Julieth.Nilifurahi sana hatimaye nimepata watu wakuniweka busy na mimi.
Queen:Nimefurahi nilipata hofu,nikajua hamtokuja.
Janice:Siwezi acha kuja kwenye party ya rafiki yangu,japo uyo mumeo chizi,alitufata Mimi na Diana,akatuambia tusije,Diana kasema umsamehe hawezi kuja sababu ya huyo mumeo
Queen:Khaaaa,kwanini aliwazuia.
Janice:Ndio hapo,na ndio maana tumekuja hapa,Mimi siwezi acha kuja sehemu unanihitaji eti kisa Bwana ako kanizuia,tena anikome kabisa,alitaka akule nyama na rafiki zake eeeeh yaaan silipendiiiiiii
Julieth:Ulikataaa kunihadithia ila Janice kanielezea kila kitu kuhusu wewe na Sebastian
Queen:Janiceee jamaniii,kila siku nakwambia fridge lako haligandishi
Janice:Babu weeee,nisharopoka
Queen:Khaaa Binti,Haya karibuni,mjihudumie wenyewe,kuna kila kitu hapa
Janice:Mambo ninayoyapenda mimi
Queen & Julieth:Hahahahha hahaha
Walikula na kunywa walienjoy,wakati tukiendelea na party aliingia yule mdada aliyevalia nyekundu wakati tuko kanisani.Usiku huo alivalia white kama wengine,kila mtu alimuangalia tena na wote walijua hapo amekuja kwa ajili ya Sebastian na Sebastian alimfata bila aibu na kumkumbatia na kumkiss mabusu mazito mbele za watu.Watu waliniangalia na mimi,nilituliza akili nikafanya kama sijaona kitu,nilikua busy sana kuongea na watu wangu,Janice na Dada Julieth,walinitia moyo na waliniahidi watakua upande wangu siku zote.
Queen:Basi tu ila Sitofanya na huyu mwanaume kitu chochote kile,Damian ndio mwanaume wangu wa kwanza na ninampenda sana sidhani kama nitakuja kupenda kama ninavyompenda D,Janice mwambie Damian,Mimi ni wake.Naona kiza kimetanda mbele yangu sijui nifanye nini mungu wanguJanice:Queen usijilaumu,wewe tulia tuliii,acha waone wametukomoa ila tutamaliza hili swala kirahisi tu.
Queen:Nahitaji kuishi nao kwa akili sana ili tu nisimuweke mama yangu kwenye hatari.
Julieth:Mdogo wangu,umejikuta umeingia kwenye matatizo kisa tu roho na tabia mbaya za Mama yangu,Sasa hivi tungekua nyumbani kwa Baba yetu unaishi kwa amani tu.
Queen:Acha tu dadaangu usijali,ukiwa wewe kwenye Maisha yangu na Mama nyie mnanitosha.
Niliongea na ndugu na rafiki yangu.Alinifata kijana anaefanana kwa mbali na Sebastian na alijitambulisha kwa jina la Samson.
Samson:Shem,Kaka ameniagiza nikwambie kama umechoka,nikusindikize hotel ili ukapumzike maana yeye amesema hatoondoka sasa hivi.
Queen:Ni sawa Sam,tunaweza kuomdoka sasa hivi,Mimk niko tayari.
Niliwachukua Janice na Da Julieth tukaondoka hadi hotel,wao waliniacha hapo,niliingia chumbani na kuanza kuchat na baadhi ya marafiki na ndugu walionipa hongera.Nilipoingia Status niliona watu wengi wamenipost picha zangu tu,maana picha nilizopiga na Sebastian hakua na furaha kabisa.
Nilimpigia Damian,tukaongea ila alikua anaongea kwa kuumia mno.Nilimuumiza sana Damian,ili ilibidi iwe hivyo na kijana wawatu bado alikua akinipokelea simu zangu na tuliongea vizuri ila alikua akinikumbusha kua Mimi ni Mke wa Mtu sasa.Ilikua inaniuma mno,sema nilishafanya maamuzi wakati huo kwa ajili ya Mama yangu,na nilishamuahidi kaka yangu,nitamlinda Mama yetu kwa lolote lile ili tu awe salama.Nilichezea simu hadi nilipitiwa na usingzi mzito maana nilichoka sana na hekaheka za harusi.
nipe maoni niendelee au
********
𝙆𝙞𝙯𝙖 𝙠𝙞𝙣𝙚𝙣𝙚
GREEN HACKER
0
Tags
Simulizi za kali
Chapisha Maoni
TOA MAONI YAKO HAPA