BINTI YANGU*1 NA 2
SEHEMU YA.....1
****************
ilikuwa ni mida ya jioni kiasi saa 11 katika kijiji kilichofahamika kwa jina la milengwe lengwe kilichopo mkoani morogoro, basi alionekana Binti mmoja ambae alifahamika kwa jina la Asma alikuwa akitokea shamba kwani alibebe jembe lake begani, amevaa sketi yake iliyochoka sana na shati iliyofubaa na nnje alijifunga lubega khanga iliyochanika chanika na miguuni alikuwa peku hana hata ndala alionekana kuwa na maisha magumu sana.
Lakini mbali na hali duni aliyoonekana nayo Binti huyo bado alionekana kuwa na mawazo yaaani alitembea huku akionekana kabisa kuwa akili yake haipo hapo alikuwa akiwaza jambo fulani akilini mwake.
Mala gafla akisikia akiitwa na mtu,
"Asma... Asmaaa".
Ndipo Binti akasimama na kuangalia ni rafiki yake ndo alikuwa akimwita alieitwa Sikitu.
"Vipi shooga mbona unatembea lakini akili yote inaoenekana haipo hapo jamaniii ndo mawazo ya msiba wa baba yako hayajaisha tu".
" Ahhhh we acha tu sikitu sio rahisi kiivyo hata siku moja lakini nashukuru siku zinaenda"
" Pole buana usiwe hivyo sasaivi ni kupambana kama hivyo unalima zako muda wa mavuno unavuna unapata pesa yako unajikimu baba tumuombee salama huko alipo"
" Sawa Sikitu nashukuru kwa kunipa moyo rafiki Yangu basi wacha nifike nyumbani"
" Sawa basi kesho tutaonana".
Basi Asma aliendelea zake kurudi nyumbani na yule rafiki yake ambae ni tausi nae akaendelea na safari zake.
Kumbe ndo tunapata kujua kuwa asma ana mawazo kwa sababu hivi karibuni alipata msiba wa kuondokewa na baba yake hivyo sasaivi yupo kama mkiwa.
Alifika mpaka nyumbani lakini alishangaa kukuta kuna watu wafika wanne wamekaa nnje kuonesha walikuwa wakimsubiri kwa hamu sana.
Asma alipowatazama aligudbua kuwa ni ndugu zake yaaani baba wakubwa na wadogo hivyo akainama chini kupiga goti kuwapa heshima yao.
"Shikamoo baba".
"Hakuna mwenye shida ya shikamoo yako unaondoka nyumba unaifunga utadhani ni ya kwako? Nyumba hii ni ya kaka yetu na leo tumekuja na mteja huyu tunataka kuiuza tugawane ela".
Aliongea mmoja wa watu wale.
Asma alishangaa,
" Bamdogo Jitu unaongea nini mbona sikuelewi? Mnataka kupauza hapa mbona gafla usitoshe mimi hamjaniambia"
" Tukuambie wewe kama nani? We si chokolaa tu mama yako mwenyewe alipokuzaa akakuleta hapa kwa kaka yetu akakutelekeza na kukimbia kijiji haijulikani yuko wapi mpaka leo je utasema na wewe una thamani? "
Aliongea bamdogo Mwingine tena maneno ambayo yalimchoma Asma na kumuumiza mpaka akaanza kulia.
Basi wote wakachachamaa kuwa afungue mlango akatoe nguo zake nyumba inauzwa.
Asma alikuwa ni mpole na mtaratibu sana hivyo akaingia ndani akachukua nguo zake na kutoka akaona jinsi watu wanavyouziana nyumba ile ya udongo Shilingi laki moja hivyo kila bamdogo alipata Shilingi elfu 25.
Asma alibaki anawatizama jinsi walivyouziana pale wakapeana mikono na yule mnunuaji kisha wakamtaka Asma aondoke bila hata kumpa shilingi 10.
"Bamdogo jamani sasa mimi naenda wapi nilitegemea labda sawa mnauza hapa hata mtanichukua lakini mnanifukuza niende wapi?"
" Nani akuchukue? Hivi umechanganyikiwa? Ulishatelekezwa tokea zamani wewe ondoka zako bwana".
Asma aliamua kuondoka zake huku akilia kwanza alienda kwenye karibuni la baba yake na kuanza kulia pale maana hajui hata ataenda wapi alilia mala mbili baba yake ambae ndo amemlea bila mama nae amemuacha siku hazijapita Nyingi anafukuzwa na nyumba inauzwa japo ya tope lakini watu kumbe walikuwa wakiitolewa macho wapate ela.
Binti alilia mpaka giza lilipoingia kabisa ndipo akaamua kuondoka kwenda kwa Kina sikitu rafiki yake ambapo alipokelewa vizuri na akawasimulia yaliyotokea kwani sikitu alikuwa akiishi na wazazi wake.
Mama yake Sikitu alisikitika sana kusikia vile akimuonea sana huruma Binti huyo,
"Nakwambiaje hao baba zako wadogo na ulevi wao wasitusumbue kabisa hawana lolote tamaa tu hapo wameuza nyumba ili wapate ela ya kwenda kunywa pombe nakwambiaje nitawakomesha kesho tuende serikali za mitaa".
" Hapana nawaacha tu nimechoka kutukanwa wananitukana sana mpaka najisikia vibaya mimi basi waache tu"
" Sawa Usijali mwanangu weee utakaa hapa na mwenzio sikitu kijisikie upo nyumbani hatuwezi kubali uhangaike mitaani na sisi jirani zako tupo sawa".
Basi Asma alipokelewa na kupata hifadhi hapo kulala.
Basi zilipita siku tatu Asma aliendelea na majukumu yake walau ndo alikaa sawa kwani alikuwa ni mtu wa kulia tu.
Siku hiyo aliamua kwenda shambani kwake ndo kitu cha thamani pekee ambacho akibakia nacho Binti akitegemea kulima na kupata mazao yamsaidie kujikimu kimaisha, lakini alipofika alishangaa kukuta kuna vibarua wapya wanalima yaaani ni kama kuna watu wengine wameajiriwa hapo.
Asma alizidi kushangaa ndipo akamsogelea mmoja wapo na kujaribu kuuliza akaambiwa kuwa wao pale ni vibarua tu boss wao mkubwa yupo mbele kidogo anakagua kazi inavyoenda.
Asma alielekezwa huyo boss akamfuata na kumsalimia,
"Samahani mama hapa ni shambani kwangu"
"Shambani kwako? Hapana Binti umejichanganya hapa ni kwangu nimepanunua juzi shahidi mwenyekiti nimeuziwa na wababa wanne ambao wamesema ni kwao ndo maana leo nimeleta vibarua nawasimamia walime".
Asmaa pozi lilimuisha wala hakutaka kubisha aliamini hao ni baba zake wadogo.
Asma alilia sana hakuamini pamoja na upole wake lakini aliona katika hilo wamezidi sasa akatoka mbio kuelekea kwa mwenyekiti akashtaki.
Alifika Binti akiwa analia kupita maelezo na kumueleza mwenyekiti hali halisi lakini mwenyekiti alionesha kuwa upande mmoja na wale baba zake wadogo na Asma kwa sababu alimuwekea vikwazo Asma kuwa alete ushahidi unaoonesha umiliki wake wa shamba lile na binti alikuwa hana kwani alichokuja anajua aliachiwa na baba yake hivyo ni vya kwake.
Hakuwa na msaada wowote binti huyo akaamua kuondoka zake kurudi kule nyumbani kwa kina sikitu akiwa analia na kuwaelelezea Hali halisi ambapo nao wasikitika lakini hawakuwa na jinsi zaidi ya kumbembeleza Asma na kumtaka aachane nao watampatia eneo jingine la kulima na maisha yatakwenda.
Miezi mitatu ilipita ambapo Asma ilikuwa tofauti na vile ambavyo familia ya sikitu walimuahidi hawakumpa eneo la kulima zaidi alikuwa kama mfanyakazi wao pale ambae alilazimika kuwapikia, kwenda shamba kuwalimia bila kulipwa chochote jambo ambalo lilimchosha akaamua nae kutafuta muda wa ziada kufanya vibarua vya kulima kuliko mashamba ya watu kujipatia viela vya kujikimu lakini pia haikusaidia kwani Mama Sikitu alibadilika alipochunguza na kugundua kuwa Asmaa amepata vibarua huwa anajibana bana anakwenda alikuwa akimsubiri akirudi akampokonya ela na kumtukana juu.
Basi hali ile iliendelea baada ya wiki mbili Asmaa alichoka na kuamua kutoroka nyumbani pale alishaona anapitia yote hayo kwa sababu wale sio wazazi wake aliamua kuondoka zake.
Alikuwa na akiba yake kidogo kama elfu 15 aliitumia kwenda mpaka morogoro mjini huko akajikuta ameingia kwenye basi linaloitwa Abood ambalo lilikuwa linakwenda dare salam na kuondoka kutokomea huko japo hajui atafikia wapi na kwa nani aliona atajua mbele kwa mbele lakini kwanza akahangaike huko huwenda ipo siku atakutana na mama yake ambae aliambiwa kuwa alimtelekezaga akaenda mjini zamani tokea akiwa mdogo hivyo hajui hata uso wake unafananaje ila alichoamini ni kwamba kwa kuwa mama yake akiondoka na hakurudi pengine alipata maisha huko hivyo aliamini na yeye atayapata....
Simulizi hii ndiyo itakuwa kila asubuhi na mchana inafuatiwa na Sonia kisha usiku Ndoa ya siwa .
Je atafanikiwa?
*BINTI YANGU*
Sehemu ya.... 2
Tulipoishia....
Aliambiwa kuwa alimtelekezaga akaenda mjini zamani tokea akiwa mdogo hivyo hajui hata uso wake unafananaje ila alichoamini ni kwamba kwa kuwa mama yake aliondoka hakurudi pengine alipata maisha huko hivyo aliamini na yeye atapata........
SONGA NAYO.........
Asmaa alifika Daresalam jiji lenye kila maajabu kwa yule mgeni ambae anafika bila kuwa na muelekeo hivyo binti alikuwa akishangaa tu hajui wapi aelekee huku njaa inamuuma.
Kwa kuwa Binti alikuwa na chenchi kidogo alienda katika duka moja na kununua mkate na maji kisha akakaa palepale nnje ya duka lile na kuanza kula hakuwa na pakwenda hivyo hata alipomaliza kula aliamua kukaa hapohapo.
Basi ilifika mpaka usiku wakati muuza duka yule sasa akiwa anafunga duka maana tayari ni saa 3 usiku, akashangaa kumuona binti akiwa anasinzia pale amejifunika kakanga chepesi kilichopauka ilibidi amuamshe,
"Dada...dada samahani nahitaji kufunga duka ondoka tafadhali"
"Kaka weee funga tu naomba nilale hapahapa ni mgeni hapa sina pa kwenda"
" Haaa sasa wewe unakuja huku bila kuwa na ndugu au ndo nyie mnaodhania maisha ya mjini ni mepesi eti? Ebu ondoka buana kwanza usije kuwa muongo ni mwizi wewe"
" Hapana kaka mimi sio mwizi tafadhali naomba usinifukuze nisaidie nakuomba".
Alilia Asmaa huku akipiga magoti lakini pia haikusaidia kijana yule akimfukuza kwa ukali mpaka kama mbwa mpaka Asmaa akaamua kuondoka tu na kusogea kwa pembeni hajui hata aende wapi alitamani hata kurudi kijijini lakini ilikuwa ngumu kwake.
Basi kijana yule alifunga duka lake na kuondoka, lakini kabla hajafika mbali mala gafla moyo wa kiubinaadamu ulimuingia ikabidi arudi tena mpaka alipokuwepo Asmaa.
"Dada umesema wewe ni mgeni hicho unachokiongea ni ukweli isije kuwa ni tapeli wewe"
" Kweli tena kaka mimi sio tapeli niamini nimetokea kijijini nimekuja tu naomba nisaidie kakangu".
Basi kijana yule alimtaka Asmaa ainuke na kuondoka nae waongozane huko Ambapo anakwenda.
Walifika mpaka katika nyumba moja ambayo alikuwepo mwanamama mmoja ana banda lake la kuuza chakula yaani mama ntilie kijana yule alionesha kufahamiana nae hivyo akamwita,
"Mama kola eeeeh leo nimechelewa naona unamalizia malizia"
"Yaaani ndo nilikuwa nakusubiri wewe chakula chote kimeisha kimebakia cha kwako tu".
" Daaa sawa nipe tu maana leo nina mgeni huyu"
" Hata mimi nilivyomuona nikataka kuuliza huyu mgeni wako".
Palepale Asmaa akapiga goti na kusalimia,
" Shikamoo mama"
" Marhaba karibu".
Basi kijana yule alieitwa vicent alisogea kwa pembeni akamtaka na Asmaa akae chini wale chakula kile huku mwanamama yule ambae aliitwa mama kola akawa anawatizama tu.
Walipomaliza Vincent akamsogelea mama kola na kumwambia,
"Kiukweli mama huyu msichana nimemkuta tu huko hana pa kwenda ni mgeni hapa jijini?"
" Heeee amekuja kutafuta maisha ivi maisha ya dar anayajua kweli? Tatizo watu huwa wanadhania Daresalam maisha marahisi wanakuja tu sasa ataenda wapi huyu? "
" Mama naomba msaidie alale ata hapa kwako asubuhi awe anakusaidia kazi mbili tatu".
" Mimi hapa nina wafanyakazi watatu wametosha uwezo wa kuongeza mfanyakazi wa nne sina la hasha awe tu anafanya kazi anakula na kulala hapa bandani".
Asmaa alikubali kwa moyo mmoja hivyo Vincent akamuacha na kumtaka awe makini aanze maisha pale kwani yeye hakuwa na uwezo wa kwenda kukaa nae.
Basi maisha mapya yalianza kwa Binti Asmaa ambapo kukipambazuka alikuwa akifanya kazi jumlisha ni mgeni na hakuwa mbaya isipokuwa maisha tu yalimpiga ndo akawa anatumiwa kwenda kutafuta wateja waje kula na kweli waswahili husema kipya kinyemi, wateja waliongezeka kwa mama kola siku hadi siku kutokana na Ukaribu na heshima aliyokuwa nayo Asmaa katika kuita wateja waje kula chakula.
Lakini pamoja na jitihada zote hizo za asmaa bado mama kola hakuwa akimlipa Binti zaidi ya chakula ambacho siku kikisha anaambulia ukoko au wakati Mwingine anakosa kabisa anakula usiku ni maisha ambayo alikuwa akiyapitia Binti huyo lakini hana pa kwenda hivyo ilimlazimu kuwa mstaamilivu.
Sasa zilipita kama siku tatu kutokana na uchovu siku hiyo Asmaa alikuwa akijisikia homa Hivyo masufuria aliyopewa na wenzake kusugua alikuwa akifanya taratibu kwani hayupo sawa kiafya.
Mala walifika mabinti wawili katika mgahawa huo ambao walionekana kuvaa kupendeza kama ni wafanyakazi katika eneo ambalo ni zuri.
Mabinti hao walikaribisha na kukaa kwenye viti kuagiza chakula.
Binti mmoja aliitwa Selin na mwingine aliitwa Mena lakini Selin alionekana kuwa na mawazo ni kama hayupo sawa kabisa Ndipo yule mwenzie mena akamwambia,
"Selin ebu tule kwanza leo nimekuleta hapa katika mgawaha tofauti uwe huru niambie nini kinakusibu mpaka haupo sawa kabisa".
" Acha tu mena naumia sana ni kwamba.... ".
Kabla Selin hajaanza kumsimilia rafiki yake huyo mala walishtuka baada ya kusikia kelele na walipotazama ni Binti Asmaa alikuwa anapigwa na mama kola kwa sababu hasugui masufuria kwa wakati.
Alimpiga na kumsukua Binti akaanguka chini.
Selin na Mena wote wakainuka na kwenda kuamulia ambapo selin alifika na kumuinua Asmaa alionesha kuchukia zaidi akamvaa mama kola.
"Mama mbona umekosa ustaarabu kiasi hiki kweli binadamu mwenzio unampiga mbele za watu na kumsukuma namna hii? "
" Nyie hamjui anakula Kwangu, analala kwangu bado anakuwa mzembe mzembe".
Alijibu mama kola kwa jazba sana na kumtaka Asmaa haraka aoshe viombo laa sivyo atafute pakulala.
Selin aliona hapana kama tatizo ni kula na kulala hata yeye anaweza kusaidia akamwambia Asmaa,
"Samahani kama hutojali naomba twende nyumbani kwangu nimeumia sana kuona haya unayofanyiwa ni chakula tu hiki mtu anakuwa hivi".
Asmaa alishukuru akapiga magoti kumshukuru selin huku watu Wengine waliokuwa wanakula waliinuka na kumpongeza Selin kwa kuwa na moyo wa huruma na wengi wakimlaani mama kola kwa kitendo kile alichokifanya.
Basi kutokana na lile Selina alimtaka rafiki yake yule ambae ni Mena watakutana kesho kazini na atamuelezea alichotaka kuongea nae ila kwa wakati ule wacha aondoke na Asmaa ampeleke nyumbani kwake hivyo Binti aliondoka huku mama kola akibaki anashangaa.
Selin ni Binti ambae alijaliwa Kusoma na kufanya kazi nzuri pia alikuwa mpole, mstaarabu, mwenye utu ndani yake hakuwa na majivuno kwanza aliendesha gari mpaka katika despensary moja kumpeleka asmaa kwanza akachunguzwe kama alivyoanguka kaumia au laa na kwa kuwa Binti alikuwa anaumwa kweli ikawa ni Faida kwake.
Alifanyiwa vipimo na kupatiwa dawa kisha wakarudi nyumbani.
Ilikuwa ni nyumba nzuri ya kupendeza ndiyo aliyokuwa akiishi Selin Hivyo kufika walishuka Kwenye gari na kuingia mpaka ndani huku Asmaa akiwa anashangaa tu kwake aliona ni maajabu hayo.
Ndani walipoingia alikuwepo mwanamama mmoja ambae ni mama mzazi wa Selin na alipomuona Binti yake ameingia akiwa na Mgeni tena mchafuuu alishangaa.
"Heeew Selin wanangu naona umeanza kuokota wehu njiani unawaleta au? "
" Hapana mama punguza ukali wa maneno mamangu laiti ungemuona mazingira niliyomkuta nayo acha tu hata wewe ungemuonea huruma ebu acha kwanza akaoge hayupo sawa anywe dawa apumzike mimi nakuja tuongee".
Asmaa akapiga goti kumsalimia mwanamama yule lakini wala hakuitika alimtazama kwa nyodo na dharau iliyopindukia.
Selin hakujali akaingia Ndani katika chumba kimoja wapo na kumuelekeza Binti aoge.
"Huku ni bafuni utaoga sawa wacha nikitafutie nguo za size yako nakuletea utakuta nimekuwekea hapa kitandani ukitoka bafuni...lakini unaitwa nani"
" Naitwa asmaaa asante sana dada kwa moyo wako huo"
" Usijali kaoge kwanza unatakiwa kupumzika tutaongea historia yako na mengi baadae sawa".
Basi Asmaa akaingia bafuni huku selin akaenda chumbani kwake na kumchagia baadhi ya magaoni yake, mafuta ya kupaka akampelekea chumbani akitoka apate kuvaa kisha akarudi sebleni kuongea na mama yake.
"Mama lakini amekusalimia Binti wa watu ungeitikia basi"
"Aiiiii anipishe mie wewe huo wema wako utakuponza dunia ya sasaivi hakuna kusaidiana ngoja aje aujue mji akufurahishe ndo akili itakukaa sawa".
" Hapana mama usiwaze hayo yote kwa sasa tuangalie namna ya kumsaidia anatia huruma sana".
Kisha Selin akainuka na kwenda zake jikoni.
Mwanamama yule kitendo cha kumuona asma alijikuta anakumbuka zamani kuwa na yeye aliwahi kuja mjini kutafuta maisha akiwa mchafu vilevile lakini akapotezea akaona hakuna haja ya yeye kuendelea kufikilia jambo ambalo limeshapita.......
Full 1000
3----4
BINTI YANGU*
SEHEMU YA ...... 3
Tulipoishia.......
Mwanamama huyo kitendo cha kumuona Asmaa alijikuta anakumbuka zamani kuwa na yeye aliwahi kuja mjini kutafuta maisha akiwa mchafu vilevile lakini akapotezea akaona hakuna haja ya yeye kuendelea kufikilia jambo ambalo limeshapita......
SONGA NAYO......
Asmaa alioga na kubadilisha nguo kisha Selin alimpelekea chakula ambapo alikula na kumeza dawa zile alizopewa kisha akamtaka apumzike kwanza.
Asmaa hakuamini kama. Na yeye ipo siku ataishi katika nyumba kama ile na kupewa ukarimu kama ule pamoja na hali ya umaskini aliokuwa nao.
Sasa majira ya usiku Selin akiwa mezani na mama yake pamoja na Asmaa alishaamka nae akaungana nao kukaa mezani, ndipo alirudi kijana mtanashati yupo smart alifahamika kwa jina la Martin aliingia ndani hapo na Selin akainuka kwenda kumpokea,
"Waooo my love karibu"
Akambusu pale na kumpokea begi lake la kazini inaonesha ni mumewake na Binti selin.
Martin akasogea mezani na kumsalimia mama yule ambae aliitwa mama Selin ni mkwe wake kisha akamsalimia na Asmaa japo hamfahamu kisha akaelekea chumbani aliamini mkewe ataenda na kumuelezea habari za mgeni yule kwani siku zote wastaarabu huwa hawaulizii hapohapp husibiri wakiwa faragha ndipo wanaulizia.
Kweli Selin nae akaenda chumbani ndipo Mumewe akamuuliza,
"Mhhh naona tumetembelewa na mgeni ambae anaonekana ni wa karibu yetu sana mpaka amevaa gaoni yako? "
" Mmewangu jamani acha hizo inamaana mpaka awe mtu wangu wa karibu sana ndo anaweza kuvaa nguo zangu? "
" Mhhh Hapana siwezi jua"
" Ok leo wakati natoka ofisini na rafiki Yangu yule mena alinipeleka katika mgahawa fulani huwezi amini tulimkuta huyi Binti katika mazingira ambayo hata ingekuwa ni wewe mmewangu ungemuonea huruma na kumchukua sio siri alikuwa anaosha majombo huku anaonekana kabisa amechoka kama haitoshi boss wake akampiga hicho kilichoniuma zaidi inaonesha ni mgeni hapa naomba tumsaidie yaanai jinsi alivyo tu haina haja ya maelezo yake anaonesha ana shida"
" Mhhh mimi sina shaka katika hilo madam wewe ndo mama Mwenye nyumba Chochote utakacho we fanya kwa sasa akili yangu, fikra zangu zote lipo katika... ".
Kabla martin hajamalizia kuongea mkewe ambae ni Selin akamziba mdomo na kumwambia,
"Najua mawazo yako ndio mawazo yangu, wote tunahitaji mtoto naomna usinifanye nijione mnyonge Mmewangu itafika tu".
Basi Martin alimkumbatia mkewe huyo walionesha wanapendana kupita maelezo.
Sasa baada ya wiki moja Asmaa alikaa Sawa ambapo nae alinunuliwa mavazi mazuri na akawa angalau anavaa na kuonekana anapaka mafuta mazuri nae akawa anang'aa weusi wa kijijini ukawa unaondoka nae akanawiri.
Alikuwa anabakia anasaidia kazi za pale nyumbani.
Sasa mama Selin bado alikuwa Hampendi anamfokea kila mala lakini kwa maisha aliyopitia aliona wacha avumilie tu.
Sasa siku hiyo majira ya mchana Binti aliandaa chakula akaandaa kwa ajili ya mama kula,
Kwa wakati huo mama selin alikuwa amekaa sebleni akiangalia Tv akawa anamtaza jinsi Binti anavyoandaa mpaka alipomaliza akaenda kupiga goti kumkaribisha,
"Mama chakula tayari"
"Mhhh hivi katika wapishi na wewe unajiita mpishi kabisa mshamba wewe unapika unakoroga? Yaaani ungejua nilivyo sikupendi tokea uje nyumba yote imebadilika harufu eti unasaidiwa na mwanamke mwenzako ingekuwa rahisi si ungejisaidia Mwenyewe".
Sasa wakati mwanamama huyo anamsema Asmaa Mpaka Binti machozi yakawa yanamtoka martin nae alikuwa amerudi gafla siku hiyo alirudi mapema kidogo.
Akashangaa kuona Asmaa amepiga magoti pale huku analia,
"Vipi mama kuna tatizo?"
"Hapana mwanangu si unajua tena watu wanaoonekana wametokea kijijini huwa hawajui Chochote ukisema umuelekeze analia kutwa anatia hasara humu ndani".
" Ohhh msamehe mama nahisi atakuwa ameshakuelewa sasaivi eti Asmaa nenda kaendelee na shuhuli zako nadhani umemuelewa mama alichokuwa anakuambia".
Asmaa alitingishwa kichwa kuonesha ameelewa kisha akainuka na kuondoka zake Sebleni hapo.
Sasa wakati Binti katoka alienda kukaa nnje kabisaaa akawa analia, alijiona yeye ni mkosaji kila mahali anapokaa anakutana na maneno tu.
Mala alitoka martin kwani alikuwa anatoka zake tena akamuona binti akiwa amekaa kinyonge akaona amfuate,
"Pole sana Asmaa japo sijui umemkosea nini mama lakini nahisi haujafanya baya pole Usijali sawa? "
Martin akatoa kiasi cha pesa kama laki moja na kumpatia Asmaa kama kumfariji na kumbembeleza kisha akaondoka zake.
Asmaa mpaka machozi yalikatika hajawahi kumuliki pesa Nyingi kiasi kile tokea azaliwe hivyo siku hiyo kwake yalikuwa ni kama maajabu.
Sasa Upande wa Selin siku hiyo akiwa zake kazini kwani alikuwa ni muhasibu, mala rafiki yake yule mena akamfuata,
"Vipi shooga sijakuulizia siku nyingi kuhusu yule Binti vipi anaendeleaje?"
"Ohhh hajambo kabisaa yaaani tena ni mchapakazi sana sema changamoto moja tu mama sijui kwanini lakini nahisi kama Hampendi"
" Ohhj usijali si unajua tena wazazi wetu kuna muda kuwavumilia kidogo kidogo atamkubali tu... Mhhhh tuachane na hayo siku ile kuna kitu ulitaka kuniambia hapa kati kati tukatingwa na ubize hatujaongea tena"
" Mhh weee acha tu rafiki Yangu kuhusu suala la Mtoto tumefanya chekup wote tupo sawa kabisa lakini kila nikijaribu bado"
" Usijali rafiki Yangu kama ni ivyo kikubwa ni dua tu punguza ubize pata muda wa kuomba sana kila kitu kitakaa sawa tatizo upo bize sana na kazi unatakiwa uuachie mwili kila kitu kitakaa sawa".
" Sawa shoga angu nitajitahidi kwa ushauri wako maana hizi ndoa wee acha tu".
"Usijali buana shoga angu".
Basi waliendelea na story zao za hapa na pale.
Upande wa Pili Martin alirudi zake kazini kwani alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa hivyo alikuwa akisimamia mwenyewe kama boss.
Sasa alikuja rafiki yake mmoja ambae ni kama msaidizi wake hapo,
"Boss umerudi? Kuna mtu alikuwa anakuulizia nikajua haupo"
"Yah nilitoka kidogo nilirudi nyumbani mala moja"
" Sasa mchana unarudi nyumbani kufanya nini akati shem yupo kazini saa zote anachezea ela tu muhasibu wote mpo bize mkikutana usiku mmechoka vibaya".
Sasa utani ule wa rafiki yake huyo alieitwa sam uliendana na ukweli kabisa.
"Ujue weee acha tu kuna kitu kinaniumiza kichwa mimi na mkewangu tunahitaji familia na tumefanya chekup tupo sawa ila sielewi tatizo nini?"
Sam alicheka kisha akamjibu,
" Kwa ubize mliokuwa nao mke yupo huku mume yupo kule mnakutana usiku mmechoka hakuna Muda wa kuomba pamoja kikubwa subira kila kitu kitakaa sawa ila muda huu upate mtu wa kukupotezea hayo mawazo etiii tafuta kidemu kikaliiii kanakutoa mawazo mwanaume hutakiwi kuwa na mawazo kuna mambo mambo yanapungua shauri yako".
Basi walicheka wote kwa pamoja maana utani ule kwao vijana uliwavutia zaidi.
Siku zilizidi kwenda Martin akajikuta kila mala akimuona Asmaa akajikuta anavutiwa nae na ukiangalia na mawazo aliyokuwa nayo kwa mkewe kutokubeba mimba alianza kumfikilia Asmaa ambae aliona hana ubize wowote atamfaa kwa matumizi yake kwa kile anachokihitaji.
Sasa Siku hiyo asubuhi Selin aliamka na kujiandaa Kwenda kazini alipomaliza aliagana na mumewe lakini gafla akakumbuka kitu,
"Mmewangu leo ni siku ya mama Kwenda hospital kufanya chekup ya presha yake wewe si ndo njia hiyo utampeleka basi"
" Ohhh haina shida nitamuacha kisha nitaenda kazini sababu leo kuna mizigo mingi mipya inaingia nahitaji nikaikague"
" Sawa haina shida tutawasiliana nisaidie mmewangu kwa hilo maana leo kuna mahesabu yanatakiwa kuwasilishwa Asubuhi hii"
" Usijali mkewangu".
Basi waliagana kwa mabusu kisha Wakatoka wote na walipofika sebleni walimkuta mama Selin ameshaamka zamani amejiandaa amekaa anasubiri kwani anajua siku yake ya kwenda hospital.
Walitoka pamoja Mama selin alipanda gari moja na mkwewe na selin akapanda la kwake wakaondoka nyumbani alibaki Asmaa kama kawaida akifanya shuhuli zake.
Basi Martin alimfikisha mama mpaka hospital akamkabidhi eneo husika hivyo alibaki anamsubiri daktari wake.
"Mama wacha niwahi kazini nitakuja kukufuata Doctor atanipigia simu"
"Sawa haina shida baba wahi kazini".
Martin aliondoka zake na kumuacha mwanamama huyo hapo.
Sasa Upande wa Nyumbani Asmaa akiwa anaendelea na majukumu yake na sasa alikuwa nnje akimwagia maji maua.
Mala akasikia geti likigongwa ndipo kwenda kufungua alikuwa ni Martin,
"Shem karibu"
"Asanteee".
Martin alirudi nyumbani bila hata gari inaonesha aliliacha sehemu akaja na usafiri mwingine.
Basi Martin akaingia mpaka ndani na Asmaa akabakia nnje anaendelea na kazi zake mala gafla akasikia Martin akimwita ndani haraka akaenda kumsikiliza maana anamuheshimu sana lakini alishangaa hamuoni pale sebleni Binti alishindwa kujua anamwitia akiwa wapi.....
Sijui itakuwaje?
Tukutane sehemu ya 4
*BINTI YANGU*
SEHEMU YA.... 4
Tulipoishia....
Mala gafla akasikia Martin akimwita ndani haraka akaenda kumsikiliza maana anamuheshimu sana lakini alishangaa hamuoni pale Sebleni Binti alishindwa kujua anamwita akiwa wapi....
SONGA NAYO.....
Asmaa ilibidi asimame palepale sebleni na kuitikia,
"Abee shemeji nipo hapa sebleni unasemaje?"
"Pita huku ndani mala moja".
Asmaa akaenda mpaka kordoni huku akiitikia abe shemeji,
Ndipo akagundua kuwa Martin yupo chumbani kwake na yeye Asmaa.
"Abee shemeji upo chumbani Kwangu?"
"Ndio pita usijali".
Asmaa alipata wasiwasi alihisi au kuna kitu Martin amekiona chumbani kwake kibaya ndio maana lakini akaona hapana kwani hana baya alilolifanya basi akaingia.
Martin alikuwa amesimama mlangoni Asmaa alipoingia tu akafunga mlango na kumshika kumtupia kifuani kwake.
Asmaa akaanza kupiga kelele,
"Hapana shemeji hapana shemeji hapana".
Huku mapigo ya moyo yakibadilika akaanza kupiga kelele lakini martin akamzuia kwa kuanza kumbusu mdomoni Binti asijue cha kufanya huku taratibu akimsogeza kitandani na wakati huo Asmaa alikuwa amevaa khanga tu chini akijua yupo nyumbani hakuna mtu amebaki peke yake hivyo kazi haikuwa ngumu kwa Martin kufanikisha kile alichokidhamiria.
Zilipita kama nusu saa Ndipo kazi ilikuwa imemalizika wahenga husema majuto ni mjukuu Asmaa alibaki akilia na Martin aliondoka na kurudi chumbani kwake kuoga huku alijilaumu sana tamaa zimepelekea amemsaliti mkewake.
Kwa aibu Martin alioga zake haraka haraka na kuondoka zake Huku Asmaa bado alibaki akilia ameharibiwa leo usichana wake na mwanaume ambae ni shemeji yake.
Alianza kukumbuka jinsi Selin alivyomsaidia na hajawahi kumuonesha ubaguzi hata siku moja je vipi akigundua kuwa leo wamemtumia mwanaume mmoja hapo ndo Binti aliishiwa nguvu.
Asmaa alitamani atoroke ili Selin akirudi asimkute hapo lakini alipokumbuka kuwa kijijini hana pa kukaa na Daresalam hapo hana ndugu zaidi atanyanyasika ndo alizidi kuchanganyikiwa.
Martin alirudi mpaka kazini nae akiwa hana raha alijionea kabisa aibu mpaka yeye Mwenyewe alikaa tu kwenye kiti na kujiinamia.
Mala yule rafiki yake ambae ni Sam alimfuata,
"Oyaaa mkuu vipi mbona leo upo taratibu taratibu sana au kabla haujaondoka shem kakupa mambo mazuri mpaak umechoka".
Sasa utani ule wa Sam ndo kama ulizidi kumchanganya Martin,
" Sam acha utani ujue kitu serious kimetokea?"
"Kitu gani?"
"Huwezi amini kuna Binti mmoja yupo pale nyumbani aliletwa na mkewangu leo ibilisi kanipitia nimelala nae sijui huko alipo Binti wa watu anafanya nini nina wasiwasi asije hata kujidhuru sababu leo ndo mala yake ya kwanza"
" Ohooooo... Umekua babaaaaa aaaaah siamini kabisa maana tulikuwa hatupumui kila mala selin, selin, selin bola sasa kapata msaidizi si kama ivyo umechangamsha damu kipya kinyemi kama nakuona"
" Sam plzzzzz kuwa mtu mzima wakati mwingine acha utani ujue roho inaniuma Sijui hata nitamtazama vipi Selin wangu"
" Kwani wewe unataka umtazameje kwa mfano mwanaume jikaze buana huo mwanzo tu baadae utazoea kabisa".
Martin aliona kama sam anazidi kumchanganya akaondoka akamuachia maagizo na kuondoka zake kwani muda wa kumfuata mama Selin hospital ulikuwa umefika.
Basi Majira ya Usiku Familia yote walikuwa mezani wakipata chakula Martin alijitahidi kujikaza na kuwa kawaida lakini Asmaa kwake ilikuwa ngumu alikuwa akila huku aibu mpaka anaangalia chini.
Mama Selin kama kawaida yake kwani huwa hampendagi Binti huyo akamwmabia,
"Na wewe kulikoni leo unatazama chini utadhani umefumaniwa".
Asmaa alishtuka mpaka chakula kikampalia wacha aanze kukohoa.
Haraka ilibidi Selin ampatie maji ya kunywa na huo ndio huwa uhalisia kwa mtu Ambae anakuwa amefanya Jambo la siri sasa likiongelewa huhisi kama siri yote ipo nnje ndicho kinachomkuta Asmaa.
Selin akamtazama mama yake,
"Mama sio vizuri huwezi kumuambia maneno makali kiasi hiki jamani mbele ya mkweo mama usiwe Hivyo... Ok Asmaa nina habari ya kukufurahisha kuna kitu nimefikilia ujifunze ikiwezekana na wewe uwe mjasiriamali mimi na shemeji yako tutakuandalia kitu na shemeji yako ni mfanyabiashara atakupa mtu wa kukuelekeza au yeye mwenyewe atakuelekeza".
Asmaa ndo alizidi kuchanganyikiwa kuona mtu anamjalia kiasi gani akati ameshamuingilia Kwenye ndoa.
Mama Selin alizidi kuchukia akainuka na kwenda zake chumbani maana anaona wanae hao wanamjali sana Asmaa utadhani ni ndugu yao.
Basi zilipita kama Siku tatu ambapo Siku hiyo Martin alimkuta Asmaa akiwa kwa nnje anaosha viombo na mama selin alikuwa amejipumzisha hivyo akaona ni wakati wa yeye kuongea na Asmaa.
"Najua nimekukosea sana elewa ni shetani tu naomba nisamehe tafadhali Asmaa sitorudia tena nitajitahidi kuwa mbali na wewe ili isije kutokea"
" Sawa shemeji nafurahi kusikia hivyo na naomba ahadi yako iwe kweli kuwa hautorudia tena sababu naumia sana"
" Usijali na kitu kingine kama alivyokwambia Selin kuwa kuna biashara tunataka kukufungulia lakini inahitaji ujuzi kuna mtu kutoka kazini Kwangu nitampa kazi hiyo na kila siku atakuwa akija kukufundisha"
" Asanteee shemeji nashukuru sana".
Basi walikubaliana na kumaliza maduku duku yao.
Kweli baada ya wiki moja Asmaa alianza kufundishwa biashara jioni alikuwa akija mtu na kumfundisha jinsi ya kuendesha biashara, kukarimia wageni hivyo kila siku akawa anajifunza kidogo kidogo japo mama Selin alikuwa hapendezwi na lile alikuwa akikasirika sana lakini hakuna namna.
Siku ziliendelea kwenda hatimae ulipita mwezi mmoja Asmaa maendeleo yalizidi kuwa mazuri na yule anaemfundisha alikuwa akirudisha majibu kwa Martin kuwa Asmaa anaelewa sana hivyo kimya kimya martin na mkewe wakaanza maandalizi ya kutafuta frame nzuri na kuijenga kisasa zaidi kuvutia zaidi wateja, Kisha wakakaa mezani na kupanga vitu vya kumuwekea dukani wote wakapendekeza liwe duka la nguo za watoto hivyo walianza Maandalizi ya kuweka order kutokea nchi za nnje kufungiwa Mzigo ili Asmaa akifuzu mafunzo wamfanyie surprise".
Basi Siku hiyo Asmaa akiwa anaendelea na masomo yake jioni akiwa ameshachangamka nae siku hizi, mala gafla akajihisi kichefu chefu na kabla hajainuka kufika mbali Binti alianza kutapika hata yule mwalimu wake kwa kuwa ni mtu mzima alielewa.
"Pole sana mbona unatapika hivi una mimba au?"
Asmaa alishtuka kusikia vile haraka akakanusha,
"Hapana hapanaaaa kwanini?"
"Ohhh basi labda malaria inabidi upime sasa kama ni kweli uanze dozi".
Asmaa hali alizid kuwa mbaya akaenda ndani kabisa bafuni.
Sasa yule mwalimu wake ikabidi aondoke maana alishaona kwa hali hiyo siku hiyo hakuna kusoma akaamua kuondoka.
Wakati anatoka akakutana na Selin nae siku hiyo ndo alikuwa amerudi mapema.
"Habari yako mwalimu mbona mapema au ndo huwa mnamaliza sasaivi? "
" Hapana leo naona hayupo sawa anatapika tu sijui ana homa au malaria".
Hata selin alishangaa ikabidi ashuke kwenye gari asiliingize ndani ili kama kweli anaumwa waende hospital.
"Sawa asante wacha nikamsikilize".
Selin aliingia kweli mpaka ndani akamtafuta Asmaa alikuwa ametapika nguvu zimemuishi kajilaza tu kitandani.
"Asmaaa asmaaa nini cha mno mumy nasikia unaumwa? "
Basi selin akaanza kumpapasa shingoni kuangalia joto lake akaona waende tu hospital hata Asmaa nae kwa kuwa dalili hizo kwake ni ngeni aliona wacha waende tu hospital aliamini huwenda ikawa ni malaria.
Walipofika kweli Binti alichukuliwa vipimo vyote cha mkojo, cha damu na Kwenda kuchunguzwa maabara huku Asmaa amewekwa mapumziko na Selin akiwa pembeni yake.
Baada ya muda Nurse alileta majibu na kumpatia Selin kwani aliona wapo Pamoja hivyo ni watu wa karibu.
Selin alianza kusoma kuwa malaria negative, UTI negative lakini UPT ikawa positive.
Selin hakuamini akarudia kusoma mala mbilimbili lakini jibu likawa ni lilelile hata Asmaa akabaki anashangaa tu.
"Hongera una mimba".
Asmaa alishtuka mpaka akainuka kitandani,
"Vipi mbona unashtuka nooo usijali utapata presha bulee tukifika nyumbani tutaongea sawa, wewe ni mdada najua hawezi kukosa boy friend utanielezea vizuri ikibidi tutamwita na shemeji yako tuone msimo wake na nikutoe hofu tu vijana wa mtaaani Tabia zao zinajulikana usiwaze kuwa atakataa akikataa basi tutalea wenyewe sawa Mumy".
Kisha Selin akainuka na kwenda kupeleka Majibu yale kwa daktari wapewe kama kuna dawa au vipi.
Asmaaa alianza kulia huku akivuruga nywele zote, nguvu zilimuishia moyo ulimuenda mbio alibaki njia panda asijue cha kufanya, alitamani dunia dunia ipasuke aingie maana yajayo kwake anajua kuwa ni mazito....
Sijui itakuwaje?
Tukutane sehemu ya 5
like na ku comment tu
Chapisha Maoni
TOA MAONI YAKO HAPA