Secret Love🖤🖤
Sehemu ya 1 na 2
Ni jioni moja tulivu mimi na rafiki yangu Mary tulikuwa tumekaa beach tukila upepo wa bahari baada ya kutoka chuo, mara ghafla niliweza kumuona mpenzi wangu Kelvin akiwa na msichana mwingine pembezoni kidogo na bahari...nilishtuka lakini nilihisi huenda labda si yeye nimemfananisha tu nilipotezea nikaendelea kupiga story na Mary
Lakin kadri walivyokuwa wakitembea niliweza kugundua kuwa yule ni Kelvin na wala sikumfananisha niliskitika kwanini sasa kelvin wangu anatembea na msichana mwingine tena eneo la starehe🥹🥹 na Kwa jinsi walivyokuwa wameshikana mikono ni wazi kuwa ni wapenzi, nilitamani kumshirikisha Mary kuhisu hilo lakin tatizo ni kwamba mimi na Kelvin tulikubaliana mapenzi yetu yatakuwa ya Siri hakuna mtu yoyote tulipanga ajue kuhusu uhusiano wetu🥹🥹 nifanyeje ili kuficha hisia zangu hizi za huzuni
Mary alinishtukia baada ya kuona nimekaa kiunyonge alinitikisa magegani akasema unashida gani rafiki yangu Hamisa mbona umepoa ghafla??!!, nilikosa cha kujibu zaidi niliangalia upande wa pili na kusema hakuna kitu Mary☺️☺️ Mary alijua wazi kuwa siko sawa alikuwa ananilazimisha niongee lakin niligoma katakata Kwa sababu ningesema ingekuwa ndo nimevunja makubaliano ya mimi na Kelvin kuwa na mapenzi ya Siri....tuliendelea kupiga story lakini macho yangu mimi yalikuwa yakiwatizama tu Kelvin na yule mwanamke aliyekuwanaye macho yangu hayakukauka kwake kabisa😫😫 ukweli ni kwamba nampenda sana kelvin nitawezaje kuvumilia kumuona akiwa na mwanamke mwingine mbona kama najitesa😣
Mary alikuwa busy kujisnap lakin mimi macho yangu yalikuwa bado busy kumtizama tu Kelvin wangu huku nikiumia ndani Kwa ndani😣😣 baadae nilijikaza ili Mary asiweze kugundua kitu ila nilikuwa naumia sana sio siri...tulikula mishkaki pale then wakati wa kuondoka nilikuwa
nawahi kuondoka ili kelvin asijue kama nimemuona wakati huo nishampoteza machoni
Nilifika Kwa mbele nilisimama ili nimsubiri Mary maana Kasi niliyokuwanayo nilikuwa nimemuacha nyuma sana....kelvin ni mwanaume ambaye tunasoma wote chuo ila ye mtoto wa kishua kuliko mimi kwao Wana hela chafu Kwa haraka haraka huwezi kuamini kama kelv ni mwanachuo , Mary alikuja akasema nimemuona rafiki yako bwana😊😊 mimi nilishangaa nikamuuliza rafiki gani huyo??
"Si kelv maana naonaga anakufuatilia siku nyingi sijui kwanini hujawahi mkubali aisee"
"Mmh niliguna tu moyoni nikasema ungejuaaa😝😝" nikamwambia akuu mi wa nini sasa hata simtaki halafu yule ni rafiki tu kwangu wala hanitaki kama unavyohisi"
"Ooh vizuri basi tuondoke au tunakaa hapa hadi muda gani"
"Tunaenda Mary just a minute...karoho kangu kalikuwa hakataki tena kuondoka bila kumuona Kelv sjui kwanini😣😣 mwanaume kaniteka huyu nyie acheni tuuu, lakin natakiwa kuondoka hakuna kitu naweza kufanya kuzuia nilichokiona leo....nilianza kuondoka tena speed nikamuacha hatua nyingi Mary
Nilitoka hadi nje wakati huo Mary yupo nyuma yangu ananishangaa tu jinsi nilivyo speed ya 5G Cha ajabu wakati ndo nataka kumaliza eneo hilo nilikutana uso Kwa macho na Kelvin.....
Je unafikiri nini kitatokea kati ya Hamisa na Kelvin mahali hapo??? """usiache kufatilia sehemu inayofuata"""
Itaendeleaaa......
Sehemu ya 2
Nilianza kutetemeka Kwa hasira sikutegemea kabisa kama ningemuona Kelvin hapo nilihisi kuishiwa nguvu mwilini mwangu hasira za ajabu zilinipanda🥹🥹 muda huo yule mwanamke aliyekuwanaye alikuwa hayupo hapo nilikuwa natetemeka kama nimenyeshewa mvua ya mawe, wakati huo Mary anashangaa tu hajui nini kinachoendelea na alihisi kelvin ananitaka kumbe watu tunadate long time😝😝....nilimsukuma kelvin mbele yangu nikaanza kutembea haraka sana kutoka maeneo hayo....
Mary alinikimbilia akawa ananiuliza Kuna nini kinaendelea kati ya mimi na Kelvin....nilimwambia Mary my friend please naomba uachane na huyo mjinga tuongelee mambo yetu sitaki kabisa kuongea kuhusu kelv sasa hivi nilianza kuliaa😭😭😭
Rafiki yangu alikuwa haelewi hili wala lile akaanza kunibembeleza nimwambie ni nini kinachoendelea, nilikosa nguvu ya kuendelea kutembea nilikaa chini kama mzigo,,,Marry nae alikuwa yupo upande wangu alikaa akawa anataka kujua kile kinachonisibu.....
"Hamisa sweetheart am your only one close friend please tell me what you'are going through(Hamisa mpenzi mimi ni rafiki yako wa pekee wa karibu tafadhali niambie unapitia nini)
Nilimjibu marry, I know but please let's go!
Kabla hata hatujanyanyuka pale chini Kelvin alikuja akaninyanyua akaniweka begani nilikuwa narusha miguu ili aniachie lakin alinizidi nguvu akaenda kunipakia kwenye gari lake mi nalia sanaa muda huo.....
Alianza kudrive sikujua anaelekea wapi lakin mimi moyo wangu ulikuwa unauma sana sikutaka hata maongezi na yeye, alifika sehemu akapaki akaanza kuniuliza Misa why are you pretending like crazy(Misa kwanini unajifanya kama chizi)....nilichukia huyu si kanikera mwenyewe now anaanza kuniambia am pretending like crazy surely🥹🥹
"Please kelvin naomba uniache niende nyumbani kwetu sitaki kuongea chochote kile na wewe"
"Oooh really so why hutaki kuongea na mimi chochote what's wrong??!....alikuwa anachukulia simple sana alichokifanya na hicho ndo kilizidi kunikera hajui hata kuomba msamaha aaarghhh😫😫
"Listen Misa let's go tutaongea zaidi nyumbani kwangu right?!
"Nooo sitaki kuongea na wewe chochote kelv wewe ni playb😔y tu you'are nothing to me anymore sikutaki tena kelv am done with youu
Hakuelewa chochote kelvin eti alidrive mpaka nyumbani kwake masaki, alifika akanifungulia mlango alikuwa ameniweka nyuma ya gari lake....nilikuwa nimevuta mdomo ulitaka kufanana kama wa kunguru😁😁 alinibeba eti akanipeleka ndani kwake mi ata nilikuwa sitaki lakin ndo nshabebwa sasa, aliniambia come to my bedroom Misa tunatakiwa tuweke sawa kila kitu kuhusu mahusiano yetu na sitaki uumie kuhusu mimi haya njoo, alitanua mikono yake ishara ya kutaka nimkumbatie.....
Nilipita pale silumkumbatia wala niliongoza njia hadi chumbani kwake nilifika nikaangalia kioo cha chumbani kwake huku nalia alikuja akaanza kunifuta machozi, nilimsukuma huko nikakaa kitandani nikaendelea kulia....nilikuwa nashauku tu ya kuambiwa kwanini alikuwa anatembea na mwanamke sehemu za starehe kama zile??!!! hilo ndo swali nililohitaji majibu yake ya kina,,,aliwasha PC yake kitu nilichokiona pale juu ya computer yake ni picha ya mwanamke ndo ilikuwa kama wallpaper nyieee alivyovaa sasa ni bkn na t🥺p pekee imagine....Je unafikiri picha hiyo ni ya nani?? na itasababisha nini?? Kaa karibu sehemu inayofuata
Itaendeleaaa.....
FULL STORY UNAIPATA KWA KULIPIA
Secret love
GREEN HACKER
0
Chapisha Maoni
TOA MAONI YAKO HAPA