Simulizi ya MY KING ❤️❤️

"1__5" MY KING❤️❤️❤️

SEHEMU YA 01

Ngoja niwape kisa changu na huyu mjeda mtata kupita maelezo😁😁siku Moja nilikuwa nyumban najiandaa kutoka na marafiki zangu 😍😍 Tulipanga siku hiyo twende zetu beach Huko coco beach,kama mnavyojua ndio beach za hadhi yetu....😁😁

Muda ilikuwa saa tisa na hapo nilishamuaga mama karibu wiki nzima kanikubalia😁😁mama yangu huwa hapendi tutoke hovyo nyumban,na ukitaka kutoka usimkurupushe inatakiwa uanze kuomba ruhusa mapema😁😁😁

Sasa wakat najiandaa bwana nikashangaa mama huyoo karudi maana hakuwepo,tena karudi na ndoo iliojaa samaki 🙄🙄na wakat huo ilikuwa ni saa nane na nusu nina nusu saa tu za kufika eneo la tukio, kwakuwa nilishamuaga mama nikajua Ile kazi ya kusafisha wale samaki haiwez kuwa kazi yangu,maana kwanza naishi na binamu yangu nikajua ataambiwa yeye ndio asafishe😌😌.

Sasa nimeshauramba zangu nataka nitoke nikasikia "Sajda OSHA hao samaki ndio uende kwenye mambo yako😕😕. Nikawa kama sijasikia vizuri nikamuuliza mama unaongea na mimi?? "OSHA hao samaki ndio uende kwenye safar zako,akasema mama na safar hii aliongea Kwa msisitizo mkubwa mpaka nikajikuta nimenyong'onyea ghafla😔😔 . "Lakin mama Anita si yupo🙄🙄,Kwann asioshe yeye na haendi popote🙄🙄,na unajua kuwa mm natoka na nilishakuaga mama😔😔nikaanza kusema Kwa sauti ya kulalamika😔😔. "Unabishana na mama yako wewe umekuwa ee,haya mama yangu ambae umeninyonyesha nenda maana ww ndio mkubwa kwenye hii nyumba,akasema mama Kwa sauti ya ukali🤔. "Lakin mama si nilishakuambia kuwa natoka🤨🤨 "Unataka kunipangia si ndio🤔🤔 au Kwakuwa ww ulitoka bila taarifa kwenye Tumbo langu ndio unataka kurudia tena😳😳, "Sasa maneno yote hayo yanatoka wapi,haya naosha hao samaki nikasema Kwa sauti ya kulalamika Huku nikiwa nimevuta mdomo😒😒

Mama aliniangalia Kisha akasema,"wenzio wanavuta bangi ww unavuta mdomo,hakikisha ukitoa mguu wako kwenye hii nyumba basi samaki wote wawe tayar ni wasafi laa sivyo utanambia kuwa uliniweka tumbon miaka mingapi maana wewe ndio utakuwa mama yangu Sasa... Wamama wa uswahilin ndio wako hivyo na binafsi nimeshamzoea mama yangu na kauli zake,so nikaanza kuosha samak Huku nimenuna balaa Na hata mabest zangu walipokuja kunichukua nikawaomba sana wanisubiri,maana nisipotoka siku hio kuja kumuomba mama yangu ruhusa mpaka akubali sio kazi ndogo😒😒,

Na kingen siku hio tulikuwa tunaenda Kukutana na mpnz wa rafiki yetu Jamila,ambae ni cameraman so siku hio tulikuwa tunaenda kupigwa picha za bure bure🙄😀. Basi nikaosha wale samaki Huku nikiendeleq na mnuno wangu,mpaka SAA tisa na robo nikawa nimeshamaliza kuwaosha wote😍😍. Nikawaanika wale samaki kisha nikachukua beseni lenye shombo na kwenda kumwaga kwenye mtaro ambao watu mtaa mzima ndio tulikuwa tunamwaga maji machafu hapo😁😁, Wakati namwaga maji sikuangalia alieko mbele anaekatiza wala anaepita mimi nilikuwa najali muda wangu tu😁😁😁 Sasa nikamwaga haraka haraka na hata sikuwa naangalia nyuma maana nilichokuwa nakiwaza wakat huo ni safar yetu ya beach pekee🙄🙄.. Nilimwaga maji nikageuza zangu na beseni kurudi ndani nimepiga hatua mbili nikasikia naitwa sajda..nikasimama..

"Mbona umemwagia kaka wa watu shombo??,aliniuliza dada mmoja jirani yetu niligeuka haraka haraka kuangalia nilikomwaga maji.. Toba toba toba😳😳😳nilimuona mkaka Mmoja akiwa ameloana shombo za samaki anajaribu kujipangusa usoni maana nilimchafua kutoka kichwani mpaka miguuni🙄🙄

Alikuwa mrefu hivi mweusi kapanda hewani bodi fulani hivi la jimu mmhhh niliogopa😳😳sasa the way alikuwa amechafuka na ule uchafu usoni nikajikuta nashindwa kuzuia kicheko🤣🤣

nilicheka kidogo Kisha nikamfata na kuanza kumuomba msamaha pole🙄😁🙈 sikukuona wakati namwaga uchafu🙄🙄🙄 kiukweli hakuni semesha aliniangalia tu kisha akaondoka zake😌😌,Sasa namna ambavyo Yale ya mautumbo yanadondoka nikajikuta naanza kucheka kwa nguvu🤣🤣🤣🤣

Yule mkaka Wala hakutia neno🙄🙄nilirudi zangu ndani nikanawa nikavaa vizuri nikajipodoa zangu kwa ajili ya safari beach 😍 Wakati natoka nikakutana na mmoja wa marafiki zangu akaniuliza sajda nimeambiwa umemwagia kaka yangu uchafu na hajatoka bafuni mpaka sasa hivi😒😒 Hivi unamjua kaka yangu ni nani??? Mmmhh jamani pole kumbe yule ni kaka yako nisamehe kpnz mi sikumuona et😔😔niliomba msamaha pale tukaondoka zetu beach.. Tulimaliza mizunguko yetu na siku hio tulipiga picha za kutosha Kisha kwenye mida ya kama SAA Moja tukaanza kurudi nyumban😍😍

Siku hio ilipita,na hatimae asubuh kulipambazuka,mimi huwa nasomaga hotel management so asubuh nikajiandaa nikaenda chuoni, wakat narudi kutoka chuo nikawa nahisi kama Kuna mtu ananifatilia nyuma😳😳nikiwa bado sijamjua ni nani maana nilikuwa natembea nikashangaa nabebwa juu juu na kuingizwa kwenye gari😳😳, na nilipoingia kwenye gari nikamkuta yule kaka niliemmwagia uchafu jana🥹🥹🥹 nilishtuka😳 alikuwa na wenzake wawili dereva na mwingine mmoja😔😔

Niacheni🗣🗣🗣msaaada msaaada nisaidieni nisaidieni nilianza kupiga kelele naomba msaada ghafla nikashangaa napgw bonge na mkofi🥹 Kaa kimya usiongee chochote😠😠 nilipewa bonge la onyo kisha wakawasha gari wakaondoka namimi..🙄🙄 Je nini kitafuata??? Itaendeleaaaaa Full 1000

SEHEMU YA 02❤️❤️ Baada ya gari kuondoka nilianza kulia nikawa nawauliza mnanipeleka wapi naombeni mnisamehe nilimwambia yule kaka nilommwagia uchafu naomba unisamehe mdogo wako Jamila ni rafiki yangu😭😭😭 Aliniangalia kwa ukali akaniambia kaa kimya🥺🥺 nilikaa kimya nikawa nalia kimya kimya mara nikashangaa gari inaingia kwenye kambi ya Jeshi tumeingia huko nikashushwa kama kikaragosi🥹

nyie adhabu nilizopewa siku ile 😭😭nilimchukia yule kaka nilimuona kama mnyama🥹🥹istoshe mimi sikummwagia uchafu maksudi mbona ananitesa hivo🥹🥹 Alinipa adhabu ngumu sana mpaka nikaingia period bila kutarajia🥹🥹

Nakumbuka baada ya kushushwa kwenye gari nililetewa ugali na yule kaka yake Jamila maana sikuwa namjua hata jina😔😔, Baada ya kuleta ugali akanambia unatakiwa kula huu ugali na hii mboga ilikuwa ni nyama choma, nikamwambia mi nimeshiba😔😔. Akacheka sana,Kisha akasema huwez kuacha kula,nikaona isiwe tabu nikamwambia haya Lete Nile😔😔,akanambia hauwez kula kirahisi hivyo nikashangaa why?? Alinipiga piga mgongoni akaniambia haujaja hapa kustarehe umekuja kulipia ulichokifanya jana nataka nikufundishe kuwa na heshima siku nyingine usirudie kuleta utovu wa nidhamu kwa watu usiowajua.. Baada ya kuniambia hivo aliuchukua ule ugali akaenda kuuweka hatua mia mbili kutoka nilipo na mboga ikawekwa upande mwingine😔😔 Alipomaliza akanifuata akaniambia unatakiwa kuruka kichura chura kutoka hapa ulipo mpaka sehemu ulipo ugali ukishamega tonge ruka mpaka sehemu ilipo mboga kula tonge lako na mboga kisha unarudi hapa ulipo unaanza kuruka tena upya mpaka ugali utakapoisha kwenye sahani nyieee🥹🥹

Nilianza kulia,na kuomba msamaha, yule Mjeda kaka yake na Jamila aliniwasha kibao kichungu Kisha akanambia nianze kazi😭😭😭 Ilibidi niache ubishi,so nikaanza kuruka kichura nafata ugali, Kisha naruka kichura kufata mboga,na wao walikuwa kama watano hivi wananiangalia tu🥹🥹 Wengine wakawa wanacheka tu,kiukweli nilikuwa najisikia vibaya sana...sikustahiri kutendewa vile au kisa wao wanajeshi ndo waninyanyase vile?? Niliendelea kuruka kichura ikafikia hatua nikawa siwezi tena kuruka vitu viliwekwa mbali mbali sana miguu ilianza kuuma mpaka nikashikwa na tumbo la period 😭😭😭 hakuna hata mmoja ambae alikuwa ananionea huruma,nilijivuta mpaka nikamaliza😭😭

Nikashangaa naletewa mche wa sabuni Kisha nikaambiwa nisivue nguo ila nioge mpaka ule mche uishe,nikawa nalia mno na kuomba msamaha ila hawakunisikiliza ikabidi nianze kuoga. Nimeoga Kwa takriban masaa matano maana ilikuwa SAA SITA mpaka SAA Moja usiku bado mche haujaisha🥹🥹, Sasa yule kijana ni kama akaanza kunionea huruma😔😔alinifuata na kuniambia kuwa niondoke🥹🥹🥹,aliniletea nguo ya kubadilisha sijui hata aliitoa wapi.., Aliniletea kijola kilikuwa kipya nilibadilisha Kisha Nikatoka lakin nilikuwa na mawazo sana nilikuwa najiuliza narudi vipi nyumban maana sikuwa hata na Hela ya kunitoa pale kunipeleka nyumban.. Wakati nawaza ghafla nyuma yangu nikashangaa muungurumo wa gari alikuwa ni yule mjeda akanambia nipande kwenye gari,nikapanda Huku nikiwa natetemeka maana sikujua amepanga Nini kingine kuhusu mm😔😔.. Basi akaanza safari ya kunipeleka nyumban,tukiwa njian akasema Kwa sauti kavu kuwa,"Tariq hachezewi so nahisi umeshajifunza kuwa ulikuwa unapambana na mtu wa aina gani😠😠 hata sikumjibu maana nilikuwa Nina hasira balaa,na nimetulia tu maana niliogopa kumfanyia chochote kile maana sikutaka anitese tena maana hata pale nilipo nilikuwa hoi bin taaban..

Nilifika nyumban nikakuta rafiki yangu Jamila yuko pale nilipoingia ndani nikashangaa mama ananipa pole na hapo sijui hata ananipa pole ya nn Jamila alinikonyeza akaniambia itikia nishampanga.. Basi nilimwambia mama asante kisha nikapitiliza chumbani kwangu kulala,asubuh nimeamka na homa kali mnooo😔.. Nilienda pharmacy kuchukua dawa,Sasa wakat natoka kununua dawa,nikakutana na Jamila na shoga yangu mwingine wakaanza kuniuliza Jana nilikuwa wapi??.. Na nini kilitokea waliniambia mama aliwapigia simu kuniulizia ikabidi wadanganye kuwa kuna rafiki yangu alianguka darasani nikamsindikiza hospital... nilianza kuwahadithia namna nilivyopewa mche mzima wa sabuni na kuambiwa nioge mpaka uishe na namnà nilivyokula ugali kwa kuruka kichura🥹 Kila Mmoja alianza kunicheka😔😔nilimwambia Jamila kaka yako ni shetani ila subiri namtafutia dawa yake yaan ni lazima nimkomeshe😔, Hawz kunitesa mm kiasi chote hichi,wakati tunaongea ghafla tukasikia mtu anakohoa nyuma yetu kugeuka nitariq😳😳, Wee niliogopa nikaanza kutetemeka ile nataka kukimbia Tariq akanishika mkono akaniambia hakuna haja ya kuniogopa mimi na wewe tushamalizana 😍😍 Vipi mnajua kuogelea?? Nikajiuliza anataka kutupeleka swimming pool?? Wote tukajibu hapana,.. "Sasa mnatakiwa mfanye kitu kimoja,muogelee hapo na mtafute samaki Kila Mmoja samaki watano kheee😳😳, Tukashangaa😳😳tunaogeleaje hapa kwenye michanga samaki tunawatoa wapi hapa kwenye michanga???.. Wakati tunaulizana tukashangaa tunapigwa mitama wote tukaanguka chini puuh tukaanza kuogeleakwenye mchanga 🥹🥹 Tariq alisema zoezi la kuogelea liendelee mpaka tutakapopata samaki watano watano🥹🥹Bora hata ningekaa kimya kamdomo kameniponza ona sasa navozidi kuumia🥹🥹 Itaendeleaaaaaaa

SEHEMU YA 03❤️❤️

tumeogelea kwenye vumbi wee mpaka tukawa hatutamaniki🥹🥹🥹,Tariq alikaa pale mpaka alipohakikisha tumefanana na michanga ndo akaondoka zake😔😔, Niliondoka pale hasira zimenipanda mno yaan nataman hata nimkate Kate vipande vipande alafu nimkaange mpaka aungue nikamtupe jalalani,Kwa namna ambavyo nilikuwa namchukia. Basi maisha yakawa yanaenda na sikuwa naonana na Tariq mara Kwa mara,na hata sikuwa nataka kumuona maana ananitiaga kichefu chefu tu yaan. Na kwa vile Yuko jeshini nikawa namuomba Mungu hata aumie kwenye mazoezi akufie Huko maana kushare pumzi Moja nae ni kama kero. Siku Moja usiku mama yangu alikuwa anaumwa sana kiasi kwamba akawa anagaragara Huku akiwa ameshika Tumbo,ilikuwa kama SAA Saba usiku,na kiukweli tusingeweza kulala nae mpaka asubuh maana Hali yake ilikuwa inatuogopesha sana. Nikaenda Kwa akina Jamila na Tariq hapo nimevurugwa nimevaa tu kinight dress na sion hata kama nimevaa uchi,nikaenda kugonga kengele,Huku nikiwa natetemeka Kwa hofu. Akaja Tariq kufungua na alikuwa kana kwamba anafanya mazoezi usiku ule,nikajikuta nimeropoka kama lichawi vile,ila hakunisikia. "Shida nn usiku wote huu,akasema Tariq Kwa sauti kavu...yani linafokaga tu😔😔 "Nikaanza kulia mpaka nikawa nashindwa hata kujielezea,ndio binamu yangu akamwambia kuwa mama anaumwa sana na tunaomba msaada wa kumpeleka hospital,basi akaenda kwenye gari lake Kisha akaliwasha na kutuambia twende tukamuandae mama,kweli tukaenda kumuandaa Kisha mm na yeye tukaenda hospital na kumuacha binamu yangu nyumban. Hapo masaa yote sikuwa nawaza kama sijavaa nguo ya maana,kwakuwa nilikuwa kama nimechanganyikiwa,sasa pale hospital tukaambuwa turudi asubuh na tuwaachie kazi madaktar na watamalizana nae,basi kinyonge nikaanza kuondoka hapo Tariq Yuko nyuma yangu. "Umevaa je hivyo,akasema Tariq Kwa Ile sauti yake ya ukavu.
Sindio nikasema niangalie,nikaanza kushusha shusha nguo,na Tariq alikuwa amevaa sweta akalivua na kuanza kunifunga kiunoni,akawa ananiangalia Huku kalegeza macho,ila hata sikumzingatia maana hofu yangu kubwa ilikuwa n mama yangu. Tumefika nyumban kwetu nikawa nataka kushuka nikashangaa Tariq ameshuka na kwenda kunifungulia mlango,hata sikumzingatia,mara akanishika mkono na kunivuta Kisha akanikumbatia na kusema,"usijali mama atakakaa sawa tu. "Wewe vipi ulisikia kuwa mama yangu atakufa au,embu niache na haka kamsaada Kako usikute unataka kukatumia vibaya,maana hata sijafurahia kusaidiwa na wewe maana shetan hata kama akitaka kuwa malaika basi ni lazima ataonesha tabia zake za kisheta,nikashangaa Tariq kanywea Kisha akaangalia chini na kinyonge akaondoka zake. Mm sikulala nikaanza kumuandalia mama chai maana tunatakiwa kwenda kumuona SAA Moja kamili,na kama tunavyojua jam za dar,so nikamaliza kuanda Kila kitu kwenye kama SAA 11 na nusu,bado ilikuwa Giza ila nikaanza kutoka,Ile nafika nje nashangaa Tariq huyo. Nikasunya Kisha nikaendelea na safar zangu,nikashangaa ameshuka Kisha akanifata na kusema "naomba nikupeleke hospital Sajda,naomba nikusaidie. Nikashangaa huyu vipi,yaan Leo atake kunisaidia lazima Kuna kitu kitakuwa hakiko sawa kabisa,nikaanza kumuandalia Kisha nikasema, "tangu lini wewe ukanisaidia kabisa mm,au ndio unataka ukanipe zile adhabu zako Kwa sababu nilikujibu vibaya,embu niache na maisha yangu maana hapa penyewe nimeshavurugwa zangu,nikasema Huku nikiwa naendelea kwenda.
Nikashangaa ametoa pesa kama elfu 50 Kisha akanambia Kodi basi usafiri,nikachukua zile pesa nikazitupa chini,yeye akaenda kupanda zake gari akawa anaondoka,hapo nimezitupa pesa ila sijasogeza mguu wangu nikawa nazilinda,maana kupata elfu 50 ya haraka haraka sio kitu kidogo,so alipoanza kuondoka nikaziokota na kuziweka kwenye maziwa,kumbe Tariq alikuwa ananiangalia Kwa side mirror so aliniona. Nimefika mbele nikashangaa tena naona gari la Tariq,akashusha kioo Kisha akasema,aseee twende nikupeleke maana wewe mwenyewe unajua kuwa naweza kukuteka na hata ukipiga kelele hakuna mtu atakusaidia,nikajifanya sijamsikia,hapo tuko barabarani na naona watu nikajiambia kuwa nitapiga kelele asinisumbue mm,yaani sijui hata ilikuwa SAA ngapi nikashangaa nimepigwa taksi bega na mkono mwingine kashika mfuko wa chakula,Kuna baba akamfata akasema unafanya nn kijana. "Ni mke wangu huyu Mzee tumepishana KAULI kidogo,so usiwe na shaka,akasema Tariq NAKUJA...
SEHEMU YA 04❤️❤️

Basi Tariq Akaniingiza kwenye gari Kisha akasema " tulia,Kwa sauti ya ukavu kidogo Kisha akakaa kimya akawa anaendesha gari hapo mm nalia kimya kimya. Tumefika hospital tukakuta hali mama Iko sawa kidogo,mm nikaingia ndani ila Tariq akabaki nje na niliamin kuwa ana mambo yake,hivyo nikitoka sitomkuta. Basi akaja ness akasema kuwa mama anatakiwa kuruhusiwa, Kwa hio nimuache ale mm nimfate,kweli Nikamfata mpaka caunter ambapo Kuna baadhi ya document nikazijaza,na mara baada ya kumaliza kuzijaza hizo document,nikatakiwa nilipe,nikatoa zile pesa ambazo Tariq alinipa nikazitupa,maana sikuwa na pesa nyingine yoyote zaidi ya pesa ya usafiri tu. Basi baada ya kulipa nikapewa risiti Kisha nikarudi alipo mama na nikamkuta ameshamaliza kula,nikaanza kumuandaa ili turudi nyumban. Basi baada ya kujiandaa tukatoka mpaka mapokezi,nashangaa nafika hapo namkuta Tariq amekaa na alipotuona akatabasamu Kisha akasimama na kuanza kuja uelekeo ambao tupo. Nilijikuta napandwa na hasira sana maana niliona kweli alikuwa anakuja kwetu. "Shikamoo mama,nilikuja na Sajda hivyo sikuona busara kuondoka bila kuwarudisha nyumban,akasema Tariq Nikamshangaa maana hakuwa hata anajua kama mama ataruhusiwa na maana yake alikuwa ananisubiri mm na sio mm na mama. "Marhaba mwanangu unaadabu sana,yaan SIKUTEGEMEA kama ungekuja kuniona,hakika PONGEZI zote ziende Kwa wazaz wako,akasema mama nikajikuta nimesunya na Tariq aliniangalia Kisha akatabasamu na kimsogelea mama yangu,na kuanza kumsaidia kutembea maana hata mm nilikuwa nimeshika wakat namtoa wodini. Akawa anamuelekeza kwenye gari lake,Nikamfata mama na kumuambia kuwa tunatakiwa kupanda daladala na tuache kuwaamin watu tusiowajua. "Mwanangu huyu si mtoto wa Mzee filambi namfahamu na nimehamia Huku na marehemu baba yako alikuwa na Miaka kama mitano hivi,na nimemuona akikuwa,Sasa Kwann useme hatujuan au ni mpita njia,akasema mama "Kweli mama wewe ni mama yangu na mm ni mwanao nashangaa huyu Sajda anashida gani,na kama hataki yeye akapande daladala mm nitakupeleka nyumban akasema Tariq. Siwez kuongozana na shetan mm,nikasema ila mama hakusikia akadakia tu,Sema usikike sio unanong'ona tu hapa,ila Tariq akatabasamu bila kujibu kitu. Nikawaacha na kuanza kwenda kwenye kituo Cha daladala. "Unaenda wapi ww,akasema mama Kwa ukali ila hata sikumjibu nikawa zangu kimya tu naendelea na safar,sijui hata walipanga nn maana mm nilidhamiria kutokupanda gari la Tariq. Basi nafika nyumban nakutana na mafurushi, mm Michele,mafuta,unga na matunda na mablueband yaan mpaka biscuit. Nilipoingia ndani nikamkuta Tariq anapiga story na mama wanacheka,yaan hata mzuka wa kuingia ndani sikuwa nao. "Oww mdogo wangu Sajda umekuja,embu njoo tumpikie mama maana binamu yako sikumkuta,akasema Tariq maana nilitaka kuondoka bila kuingia ndani ila huyu Mwanaume anamacho kama darubin vile. Sikutaka kuongea ila nikasikia mama anasema,kumbe Sajda karudi. "Weee Sajda embu njoo unipikie au unafikiri kale ka uji ulichoniletea kamenishibisha,akasema mama na sikuwa na namnà zaidi ya kuingia ndani,ambapo nikafika na kuanza kuandaa vitu,hapo nikapanga nimpike zangu ugali na kachumbar nikanunue vikalusungu tule,nahisi Tariq alielewa Hilo akadakia Kuna samak hapa mchemshie mama supu naenda kununua viazi,akasema Tariq Kisha akawa anatoka nje,akatoka nje ila alipokuwa nje nikashangaa kasimama maana jikon Kuna dirisha kubwa akawa kana kwamba kaduwaa ananiangalia nikasonya Kisha nikachuchumaa maana sikutaka kumuona na nilikuwa nashangaa sana Kwann ANAKUWA mwema kiasi hichi kwangu. NAKUJA . SEHEMU YA 05❤️❤️❤️ Nikachuchumaa Kwa dakika kadhaa na nilipoamka sikumkuta,basi taratibu nikaanza kusafisha samak,na kuandaa viongo vingine,Sasa nilikuwa busy mno kiasi kwamba sikumuona hata Tariq alivyorudi,nikawa naendelea na kazi zangu. Mara nikawa nahisi kama mtu kasimama nyuma yangu,kugeuka saa ngapi nisimpamie akanikaka hapo nilikuwa nimeshika bakuli la maji machafu naenda kumwaga yakamwagikia,akawa amenidaka ananiangalia tu,nikajikuta natetemeka maana nilijua tatizo lingine linakuja,maana sikuwa namuamin kabisa yaan. Nimeleta viazi mpikie mama,akasema Kisha akaniachia . Kwann unanifanyia wema,n kwamba unajisafisha Kwa ukatili ulionifanyia au unanitaka,kama unanitaka si unitongoze tu kuliko kunifata fata nyuma kama mkia nikasema ila nikashangaa Tariq anatabasamu. "Na kama nakupenda utafanya nn,akauliza Tariq "Yaan ni Bora hata niolewe na shetan kuliko wewe,maana nakuchukia,nilisema hivyo nikijua nitamkera maana ni MTU WA majazba ila badala yake akacheka na kusema"umeshawah kuona wapi ndg wanaoana. "Ww mpuuzi kweli Kwa hio mm shetan ni ndg yangu nikasema Kwa jazba ila Tariq hakunisikiliza akaondoka zake na mm nikaendelea na mapishi yangu. Basi siku hio ilipita na siku zikasonga,Sasa nilikuwa natongozwaga na kaka flan hivi dereva Toyo,nikawa namzungusha zungusha maana simnajua tena aibu za kike,ila nilikuwa nimemuelewa kitambo,maana hata safar zangu ndogo ndogo alikuwa ananisave yeye,yaan naenda sehemu buree Kwa raha zangu. Na mwenyewe alishaona ishara zote za kukubaliwa na ndio maana alikuwa anajileta leta,siku hio Sasa nimetoka zangu nyumban nimejikwatua mwenyewe,Sasa Ile natoka naona gari la Tariq Hilo saa hio nilikuwa naenda college,nikabinua mdomo maana nikimuonaga Tariq nashikwaga na hasira tu bila sababu. Akashusha kioo kisha akanambia naomba nikupeleke,hata sikumjibu nikawa naelekea zangu Kwa Toyo wangu hapo najitingisha na natembea Kwa nyodo Kali. Tariq akawa amesimamisha gari akawa kana kwamba ananiangalia Kwa side mirror,na mm wakat huo Sina habar,ila nilivyogeuka nikaona gari ya Tariq bado imesimama,sijui nilipatwa na Pepo gani,yaan nikaenda kumkumbatia yule dereva Toyo alikuwa anaitwa Arash,Kisha nikamkiss kwenye shavu,aisee alichekelea huyo,bila kujua alikuwa anajichumbia shimo. Huyo akanibeba kwenye Toyo,sie hao tukapepea na wakat wote huo gari ya Tariq imesimama tu ila hata sikumjali,nikawa namuona wakuja tu asie na maana. q

Sasa tulipanga na Arash kuwa nikitoka atanifata tukafurahie penzi letu Kwa mara ya kwanza,maana wakat alipkuwa ananipeleka college nikamkubali,ila unafika muda wa kutoka nashangaa mtu simuon,nikaanza kumtumia sms hazijibiwi, nikipiga simu hapokei. Nikaanza kupatwa na mashaka mno maana nilihisi lazima atakuwa amepatwa na kitu kibaya maana nilikuwa hata nikibip bahat mbaya anapiga au anakutumia sms ndefu ya mapenzi na anaanza kujielezea namna anavyonipenda Ila siku hio haikuwa hivyo na hapo ndio Kwa mara ya kwanza nataka kuzama PENZINI. Nikamtumia sms inasema "nilidhan Leo ndio itakuwa siku yetu ya furaha,na nikaamin zile sms zako Tamu za mapenzi ambazo huwa unanitumia Kila nikibip utatuma tena ila badala yake umekuwa kimya naomba unambie umepatwa na nn. Nikashangaa inaingia sms ikisema usiniponze Sajda,nikasema nipimpigie ila safar hii hakuwa anapatikana kabisa,nikarudi zangu nyumban mwenyewe Kwa daladala tu maana sikuwa na namnà. Basi siku hio ikapita kesho yake nikamuona kijiwen kwake,ila nilivyomfata nikashangaa ananikwepa,si ndio Toyo mmoja akaropoka,usimsogelee maana utamponza mwenzio maana kilichomkuta ni balaa. Nikamfata nikamuuliza kimekukuta nn,akanambia tu mm Sina Hela na sijui napambana na nani,maana hata sijui wajeda wametokea wapi nikashangaa tu napewa adhabu na wakawa wameichukua simu yangu,ila Kuna muda nikasikia wanataka jina lako ila hawakujua kama nimesikia nikahisi labda bwana ako katuona ndio akaja kunipa mateso. "Wamekufanyia nn,nikauliza Kwa sauti ya wasiwasi. Akaangalia chini Kisha akanambia "Sajda nakupenda sana ila Sina nguvu ya kupambana na WENYE vipato,nikamuomba tutoke twende sehemu tukazumgumze,akakubali kweli akawaachia Toyo wake watu Kisha tukaondoka tukiwa tumeshikana mikono,yaan new couple mtaan mtatuambia nn,Sasa Kuna muda nageuka nikashangaa namuona Tariq kasimama getin kwao Kisha anaangalia usawa wetu ila nikampuuza maana namuonaga kama ng'ombe katoliki tu.

Tukaenda kwenye mgahawa Kisha tukaagiza soda,na mara badaa ya kuagiza akanambia kuwa wajeda walimfata kisha wakamjazia mafuta full tank Kisha wakamchukua wakampeleka kwenye uwanja hata sijui n wapi nikaambiwa niendeshe Ile Pikipiki mpaka mafuta yaishe hapo sijui hata nimekosea nn.

Nikasikitika sana,nikahisi ni Tariq ila nikasema hapana maana haiingiia akilini maana hamna sababu ya yeye kufanya hivyo,ila tukiwa tunajitafakari,mara wakaja wanaume wawili wamejazia alafu wamevaa mashati meusi yamewabana vizuri vifua vyao na surual za jinsi,yaan Arash alipo waona tu alishtuka sana Itaendeleaaaaa Full 1000

"6__10" MY KING❤️❤️❤️ SEHEMU YA 06 "Tulikuambia nn wewe,wakasema. "Mpenzi wangu kawafanya nn nyie,Kwann mnamfanyia hivi,Mmoja akawa kama anataka kuniweka kibao ila akajizuia,mwenzie akamzuia,mara akapokea simu akawa anajibu tu mhhh,mhhh sawa Kisha wakatuacha hapo wakaondoka zao. Basi kuanzia siku hio Arash hakuwa anataka kabisa mazoea na mm,nikaona isiwe kesi kwani Mwanaume ni yeye pekee yake asinisumbue mm. Basi Tariq akawa hayupo Kwa takriban miezi miwili,maana Jamila alikuwa RAFIKI yangu na taarifa za kwao nilikuwa nazipata na Hilo lilikuwa jambo jema sana kwangu maana nilikuwa sipendi kumuona maana Kila nikifikiria alichowah kunifanyia najikuta ñakuwa na hasira tu. Basi muda ukaenda na yule Toyo alihama kijiwe na akawa hataki kabisa mazoea na mm,yaan nikawa najitahidi kujipendekeza kwake ila hakuwah kutaka shobo,akawa hata hawez kumpakia mama yangu au mtu yoyote wa kwetu kwenye Toyo yangu,yaan Hadi marafiki zangu hakuwa anataka mazoea nao. Siku Moja Jamila akaja kunialika kuwa kesho yake kutakuwa na party nyumban kwao maana kaka yake Tariq anarudi siku hio na Wazaz wanataka kufanya kama ki maulid uchwara hivi na Dua kwaajili ya Tariq maana Kuna coz alikuwa amemaliza kuisoma. Nikamwambia kama Tariq atakuwepo basi mm siwez KWENDA,maana siwez KWENDA Kwa hasimu wangu kusharehekea nae,Jamila alinibembeleza sana lakin niligoma kabisa kwenda maana siwez kushangulia ushindi wa Tariq mm. Basi mama yangu nae alialikwa pamoja na binamu yangu na wote waliokubali kwenda na mama akawa anajaribu kunishawish lakin niligoma. Basi muda ulienda na pale Nyumban kwetu wakaanza kujiandaa,mama yangu alivaa zake dira na mtandio mkubwa na binamu yangu akavaa hijab lake na raba na kamtandio chake Cha kichokozi na alivyokuwa amebarikiwa umbo zuri,alipendeza balaa. Basi hào hao wakatoka na kuniacha Nyumban mwenyewe kama mwanga ila sikujal,nikaweka zangu movie nikaanza kuangalia yaan Sina habar. Mara nilasikia mlango unagongwa,nilishtuka maana Kwa ninavyojua mtaa wangu,watu wote watakuwa kwenye Dua maana hawapitwagi na usikute mpaka sare wameshona maana hawanaga dogo. Nikajikuta napatwa na wasiwasi nikajua labda mwizi,nikaenda kuchukua mwiko Kisha nikazima taa,Kisha nikasogea mpangon taratibu na kuanza kukushika kitasa Cha mlango na kukizungusha Kwa lengo la kufungua mlango,ila nilipofingua nikashangaa anaingia Jamila. "Mbona imezima taa ww,akaniuliza "Nilijikuta napatwa na wasiwasi nikajibu. "Basi shoga angu Huko kumenoga,nikasema walau nije kukuita ukale maana Leo Kuna vitu vyako vile,akasema Jamila. Kiukweli sikutaka kabisa kwenda ila Jamila akanilazimisha mno,mpaka nikaona isiwe tabu acha niende tu. Nimefika nikamuona Tariq na alivyonioana akatabasamu na wakat huo akashika mic,Kisha akaanza kusalimia watu na kuwashukuru Kwa kufika, Kisha akasema baba mwanamke wa kumuoa nimeshampata na akikubali tu nitamleta kwako. Wamama wakaanza kupiga vigelegele na baba yake akataka amtaje ila Tariq hakutaka. ila muda wote alikuwa ananiangalia tu. Sasa Kuna muda si wakaweka mziki,aisee mm siwezag kujivunga nikaingia Katikati na kuanza kukata mauno. Aiseee nilishikwa mkono nikaanza kuburuzwa,kuangalia vizuri ni Tariq Unafanya nn ww,nikamuuliza "Acha kujidhalilisha kama unasikia usingizi si ukalale kuliko kufanya mambo ya ajabu kama mlevi,Akasema Tariq . " Kwan nimekuambia nataka kulala nikasema ila Tariq hakunijibu akawa anaondoka zake tu bila kusema jambo lolote Lile NAKUJA SEHEMU YA 07 Basi siku zikawa zinaenda,na maisha yakawa yanaendelea. Siku Moja nipo nyumban ilikuwa ni weekend,nikawa napika,mara akaja Jamila akanambia anaomba nikakaae nae nyumban kwao,nikakataa maana nilikuwa napika alifu nilikuwa nimechoka kutokana na kazi za nyumban. Akamfata mama na kumuomba,mama akakubali ila akasema Kwa nikishamaliza kupika nikakae na mwenzangu,Sasa sikuwa na namnà zaidi ya kukubali kwenda kukaa nae. Kweli akaanza kunisaidia kupika Kwa maana aoinikuta namenya nyanya,basi akanipokea na kuanza kumenya nyanya Kisha akakwangua karot na kukata kata vitunguu,Kisha akaanza kupika mboga mm Wakat huo nasonga ugali Kwa maana mm nilikuwa napikia mkaa yeye alikuwa anapika kwenye gesi. Tumemaliza akanambia nitaenda kula kwao so nisile,nikakubali maana kwao kunakuwaga na mapocho pocho sio mchezo. Nimefika nyumban kwao,nikashangaa kana kwamba anawahka wa kufa mtu,ila sikujal maana kawaida yake huwa ana mawenge, basi nikaingia mpaka ndani na kukaa,na mara baada ya kukaa akanambia kuwa ameagiza chips mayai na mishkaki anaomba akachukue na mm nimsubiri hapo. Nikakubali maana mm ukishanitajia chips tu unanivuruga tu yaan ikabidi nitulie na Jamila akawa anatoka ila kana kwamba anawasiwasi sana ila sikujal kabisa KUHUSU wasiwasi wake,nikawa nimekaa ukumbini naangalia movie Moja inaitwa the promice ya kikorea KIMYA,nikaamin ndani hakuna mtu so nikawa nimekaa Kwa kujiachia kabisa yaan. Sasa Ile nyumba kulikuwa na mlango wa mbele na WA nyuma,Sasa kwenye mlango wa nyuma nikawa nahisi unafunguliwa,kweli ukafunguliwa na akaingia Tariq. Sikumjali maana anajuaga kabisa kuwa simshobokeag hata siku Moja,akaingia chumban kwake kulikuwa ni ghorifan Kisha akashuka akiwa amevaa singlend,ilikuwa imemkaa vzr na vile anakifua Cha mazoezi ila hata sikumuangalia maana sitakag mazoea nae. Basi Tariq akawa kana kwamba ameficha kitu nyuma yake,ila sikumjali pia akaja akakaa pemben yangu nikasimama nikawa nataka kuondoka nikashangaa Tariq ananishika mkono. Tukawa tunaangaliana,nikashangaa Tariq katoa ua Kisha akapiga goti,nikabaki nimeduwaa tu Kisha akasema,"Sajda naomba nisamehe Kwa Kila nililofanya. "Mbona mm nimeshakusamehe kitambo tu,ila naomba niondoke,nikasema nikashangaa kasimama Kisha akanikumbatia,nikamsukuma Huko,ila hakuuacha mkono wangu akanipa lile uwa,Kisha akasema ni zawad kwaajili ya kukubali msamaha alioniomba,na anaomba nisimuwekee chuki moyon mwangu. "Hayo yameshaisha lakin naomba uachane na MAISHA yangu Tariq,mm sitaki matatizo,nikasema. "Kama sitaki,akasema Tariq "Hutaki nn?,nikamuuliza "Kama sitaki kuwa mbali na maisha yako,kama sitaki kuondoka karibu yako,kama nataka niwe pemben yako milele utafanya nn?,akauliza Tariq. Nikacheka Kisha nikasema,"umekunywa nn Leo,maana naona kama akili yako haifanyi kazi,achana na mm maana naweza kuropoka neno hapa ukaja ukanifanyia mambo yako ya ajabu,nikasema. Tariq akaniangalia Kwa dakika kadhaa Kisha akasema,"siwez kukufanyia jambo lolote Lile baya Kwa sababu nakupenda,nakupenda sana Sajda,sikutaka niende haraka haraka hivi ila nimeshindwa kuendelea kukaa kimya maana naogopa kuendelea kukosana na ww,maana naogopa kukufanya uzidi kunichukia na wakat najiona kabisa kuwa siwez kuishi bila wewe Sajda maana nakupenda sana. NAKUJA.......... SEHEMU YA 08 Nikatoa macho nikawa namuangalia tu maana hata SIKUJUA nimjibu Nini,nikawa naondoka nikashangaa amenivuta Kisha akanikumbatia Kwa dakika kadhaa,nikawa najaribu kujitoa mwilin mwake ila ndio hivyo kajazia huo ubavu wa kujitoa nautolea wapi😀. Ikabidi nitulie kama maji kwenye mtungi tu niwe nasikilizia mapigo yake ya moyo,ni kweli n mhandsome ila tatizo Kwann aniogeshe kwenye vumbi,na kwann aniogeshe na sabuni mche mzima,akwende huko,nikawa najiambia. "Naomba niondoke,nikasema "Uondoke uende wapi na ww,embu kwanza niambie unataka nifanye Nini ili uamin kuwa najutia Kila nililofanya,sijui hata niliwaza Nini ila ukweli ni kwamba nakupenda sana na Hilo sitanii",akasema. "Nenda kariakoo Kisha uogelee kwenye vumbi,ukimaliza chukua mche wa sabuni uogee katikati ya soko Kisha nikusingee ugali nifanye kama ulivyonifanyia,nikasema nikashangaa Tariq anacheka,Kisha akasema "acha utoto mm siwez kufanya hivyo ulivyosema,maana mm Nina hadhi yangu so siwez KWENDA kujidhalilisha mbele za watu, akasema "Labda tufanye jambo Moja,Kwa maana najutia sana Kwa Kila nililofanya,unipe hizo adhabu Ila tukae mm na ww,niamin nitafanya Kila unalolitaka,akasema "Kwa maana ulivyokuwa unanifanyia mm udhalimu wako ulikuwa pekee yako,ulikuwa na marafiki zako,tena wakawa wananicheka na kufurahia kuona nateseka,Sasa Kwann mm nikuonee huruma,na kwann wewe ufanye sehemu iliyojificha,naomba uachane na mm maana naona kabisa huwez kubaliana na mm,so siwez kukulazimisha na siwez pia kuwa na ww,maana sio Siri nakuchukia,nikasema Kisha nikaondoka zangu na Muda wote huo Tariq alikuwa kimya sana na akaniacha niondoke zangu. Basi nilirudi nyumban na kumkuta mama ananisubiri,nikaingia jikoni nikapika Kisha baada ya hapo nikatenga chakula ukumbini tukala na mara baada ya kumaliza kula nikaanza kuelekea kwenye chumba changu Kwa sababu ya kupumzika. Nilipofika chumban nikaishika simu yangu nikakuta sms imeingia,ilikuwa ni namba ngeni na kiukweli SIKUJUA kabisa ni nani, sms ilisema. Sajda mwanamke mwenye macho mazuri mfano wa mbalamwezi,nataman niwe nakuita macho mbalamwezi wangu,una sauti Tamu sana,yaan nataman kuisikia Kila wakat maana sauti yako pekee unanitosha kunitibu maradhi ya moyo wangu. Mwanamke mwenye adabu,ambae Niko huru kumpeleka mbele ya wazaz wangu Kwa sababu naamin watanisifu Kwa kumchagua mke ambae anapaswa kuwa mke wangu. Nakupenda na naahidi kukupenda siku zote za maisha yangu. Ile sms ilinishangaza sana nikajaribu kuipigia Ile namba ila haikupatikana,nikajaribu kuitumia sms ila hata sms hazikuwa zinaenda. Nikajaribu kuangalia kwenye tigo pesa,muhusika aliesajili Ile lain alikuwa anaitwa Mwamfupe yusuph,na kiukweli sikuwah kuwa karibu na mtu mwenye jina kama Hilo. Kuna muda nikawa nadhan labda amekosea namba Ila mbona ametaja jina langu,nikawa nahisi ni mtu anaenifahamu kabisa. Nikampuuza na kulala zangu. Basi Siku ilienda na hatimae kukapambazuka,nikaamka na kuanza kufanya usafi,maana huwa TUNAKuWA na zamu mm na binamu yangu,na zamu ni wiki nzima,hio wiki unaosha vyombo,unadeki,unapika yaan kiujumla unafanya kazi zote pekee yako,nikafanya kazi zangu Kisha nikaanza kujiandaa kwenda college. Nikashangaa nikiwa njian Toyo inasimama,Sajda twende,akasema dereva Toyo. Ni Toyo ninae mfahamu kabisa,ila sikuwa na mazoea nae,nikashangaa Kwann ananambia anibebe kwenye Toyo na Hali ya kuwa sijamuomba. "Hapana mm siendi,nikamwambia. "Naelekea kariakoo so nimeona sio vibaya kama nikikusogeza sogeza,akasema na kwakuwa na mm nilikuwa naelekea Huko Huko basi nikakubali. Akanipeleka mpaka college Kisha akaondoka zake. Basi nikaingia coLlege na kuendelea na masomo,Sasa hapo nilipokuwa nasoma kulikuwa ni ghorofani,na Kwa chini Kuna kaka alikuwa anaitwa mwedi,anakaangaga chips na anakachumbari pambe,nashangaa wakat naenda nyumban ananiita akanifungashia chips mayai na kuku nusu,nikamwambia mm Sina Hela,akanambia usijal umeshalipiwa. " Na nani,nikauliza "Siwez kujibu Hilo maana hata mm simfahamu, ww chukua mzigo wako,akasema mwedi na mm Wala sivungagi nikabeba nikawa najiambia kama alikuwa amekosea na hakupaswa kunipa mm atajijua mwenyewe,nikabeba zangu chips zangu na kuanza kurudi zangu nyumban. Sasa nikiwa nimesimama kwenye kituo Cha daladala,nikaona kama gari la Tariq limepita maana nilikuwa nalifahamu ila sikujal,mara likaja mpaka nilipo Kisha nikaona kioo kimeshushwa,alikuwa Tariq na Jamila. Jamila akaniita, twende mama Nina ubuyu wako,akasema Jamila na kwakuwa alikuwa ni Jamila nikaona nipande nikashangaa anataka nikae mbele pamoja na Tariq na Tariq kweli akanifungulia mlango wa mbele ila sikutaka,nikahisi Hawa wanamipango Yao Hawa. Mm siend bana nimekumbuka Kuna mtu namsubiri. Aweee twende bana akaanza kunilazimisha Jamila nikaona isiwe kesi nikapanda ila nyuma ambapo alikuwa Jamila,ila wakat wote Tariq alikuwa ananiangalia Kupitia side mirror nikajikuta hata siwez kuchangamka. Basi wakanipeleka mpaka nyumban na wao wakaenda kwao. Ila Ile nafika nyumban nikashangaa sms kutoka kwenye Ile namba ngeni ilionitafuta usiku inaingia ikisema Your so beutifull,ila nilipojaribu kupiga kutaka kujua ni nani bado haikupatikana na sms pia ikawa haiendi . NAKUJA SEHEMU YA 09 Nikawa najiuliza anaweza kuwa nani ila nikawa nampotezea tu Kwa sababu sikuwaza mtu yoyote yule ambae angeweza kunitumia sms kama zile. Maisha yangu yakawa yanaendelea ila Kila siku asubuh najion nilikuwa natumiwa sms za MAHABA kutoka kweñye Ile nàmba ngeni mpaka nikamsave Mr ghost maàna ukituma sms we haziend na ukipiga haipatikani Kila siku,mpaka nikawa nimezoea Ile Hali. Siku zilienda na Ile nàmba ikawa inaendelea kunitumia sms za Mahaba Kila siku,na sikuamgaika nayo maàna najua haya nikisema nijibu nitakuwa najisumbua na haiwezekan sms zikamfikia. Tariq alikuwa anapambana Sana kuweka ukaribu na mm,mwisho nikakubali kimsamehe ila sikutaka kuwa na mahusiano nae kabisa na alionekana kunielewa,so nikawa naweza kwenda kwaakina Jamila nikafika tukawa tunapiga story na Tariq bila HATA Jamila kuwepo na Tariq alikuwa anaonekana mstaarabu Sana,Kwa maàna Toka alivyosemaga ananipenda hakuwah HATA siku Moja tena kuniambia Hilo neno na akinitreat kama anavyimtreat mdogo wake,nikamuamin mpaka nikawa namuita kaka. Basi siku hio usiku nilikuwa nachart na Jamila,nikawa namuambia kuwa kesho yake ni birthday yangu so asisahau kunipost. Basi tukawa tunapiga zetu story za kimbea na Jamila,maàna kazi pekee tunayoweza kuifanya ni kusengenya watu. Mara ikaingia sms kutoka kwenye Ile namba ngeni na sms ikawa inasema. Sajda kipenzi changu Kuna Muda nataman sana nije ulipo maana nateseka sana nisipokuona Maanà uzuri wa sura yako sijawah kuifananisha na sura ya mwanamke yoyote yule dunian Maana Mwenyezi Mungu amekuumba Kwa namna ya kipekee sana na nadhan kakuumba hivyo kwaajili yangu, Maana Kuna muda nataman hata nikufiche ili usionekane na mtu yoyote yule ili asije kuona nilichokiona kwako,na akaja kuninyang'anya.. Na nikisema nianze kukusifu amini siwez kumaliza maana sifa zako kwangu haziwez kuisha maana wewe ni wakipekee na baraka kubwa kwenye maisha yangu Usiku mwema kipenzi changu na hakika nakupenda sana😘 "Wewe ni nani ambae kutwa unanitumia sms alafu sikujui,labda nikujibu kuwa nakupenda sana na nitakupenda zaidi nikisikia sauti YAKo,nikatuma hio sms Nikijua kuwa najifurahisha na sms haitoenda ila Kwa mara ya kwanza nikaona message sent na wakat huo huo akareply na kusema. "Ukiisikia sauti yangu hautonichukia maana sijui kwann Mwanaume MWENYE nguvu na ninaejiamin kama mm niwe namuogopa mwanamke ninae mpenda,ikaingia sms nyingine kutoka kwenye Ile namba. Nikaona usinitanie,Kwan kupiga Bei gani. Basi nikapigia Ile namba niliyoisave Mr ghost. Nikashangaa inaita,na baada ya sekunde kadhaa ikapokelewa. Sauti niliisikia ilikuwa kama sio ngeni hivi ila sikutaka kujiumiza kichwa,alikuwa anaongea sauti flan ya kibezi hivi,alafu ilikuwa ni sauti ya utulivu mno,kiukweli Ile sauti ilinisisimua na kutaman kuongea na yule Mwanaume. Tukaanza kuongea na sio Siri nilikuwa nafurahia sana kampan yake kiasi kwamba nikawa nataman kuongea nae Kila dakika kutokana na namnà alivyokuwa anasauti Tamu. Nilianza kumpenda Hali ya kuwa siku namfahamu na kama mnavyojua mapenzi ni kokohozi kutaficha huwez,basi mashoga zangu wakajua na hata Tariq akajua na alionekana kufurahia sana mm kuwa na mahusiano na hata nilipowaambia kuwa NAMPENDA Mwanaume nisiemjua walikuwa wananiambia kuwa nimuamin kama NAMPENDA na Kila siku wakawa wananiombe,Tariq na Jamila kuwa nidumu nae,mpaka nikawa naona marafiki si ndio Hawa. NAKUJA

SEHEMU YA 10.

basi mapenzi mubasahara yakaanza kati yangu na Mr ghost,nikawa namuomba Kukutana nae ila hakuwa anataka yaan Kila Siku akawa ananipa udhuru,mara hivi mara vile,yaan Kila Siku akawa ananipa visingizio. Nilijikuta na fall in love na sauti na zile sms zake Tamu za mahaba,nikawa nataman sana nimuone maana nilijikuta NAMPENDA mtu nisiemfahamu hata anamuonekano gani. Siku Moja ilikuwa ni birthday yangu nikashangaa Toyo kaja kaniletea keki,nikamuuliza imetoka Kwa nani akanambia hata yeye hajui ila ameambiwa ailete tu kwangu. Sasa wakat napokea Ile keki Kuna mashoga zangu wengine wakaona,si ndio wakaja kuniuliza Kunani na Ninani huyo ambae ameniletea keki,nikasema kuwa hata mm simjui maana sijawah kumuona ila naishia kuongea nae na kuchart nae tu. "Mzimu mzimu huo,shoga angu kama sio mzimu unaweza ukajikuta una majini mahaba,usiwe unakula vitu vya watu usiowajua wewe,akasema shoga yangu Mmoja alikuwa anaitwa Melisa na siku hio Jamila hakuwepo. "Bwana weee,hata kama ni wewe una uwezo wa kuacha Hela bana,kama ni Hilo jini kitajijua lenyewe maana mm ananipa pesa na ananitumia sms Tamu atajijua mwenyewe na ujini wake,na.ww kama unaona ni jini achana na mm, na usile vitu vyangu,maana sijui ulifikiri nn Kwa maana kutwa nawanunuliaga chips na mnakula,na mnasifia tu mnafikiri hizo pesa zinatoka wapi,nikasema. Ila usipuuze,unaweza kukuta ni jini kweli,akasema Melisa nikasonya Kisha tukaingia ndani na kuendelea na birthday na siku hio mama yangu alikuwa amesafiri ameenda msiban,Sasa hapo tupo mm na mashoga zangu pamoja na binamu yangu,yaan tulingurumisha Birian maana pesa ndogo ndogo sikuwa nakosa,tukafungulia disco tukaanza kucheza.

Saangapi umeme usikatike,yule Melisa akadakia kuwa, "jini kaja kuchukua watu wake,tumekaa tunashangilia pesa za shemeji ambae hatumjui na hata huyo mwanamke wake hamjui,tumeisha sisi,tukaanza kusali😀😀😀 maana Hadi mm mwenyewe niliingia upepo maana ni kweli sikuwah kumuona Sasa naachaje kuamin kuwa ni jini. Basi tulikaa hapo,ila kuangalia nje tunaona Kuna umeme,ndio tukazidi kuogopa,yaan tukajikuta tunakumbatiana mpaka asubuh,na uzuri Kila aliekuwa pale aliaga kwao na nikawaida kwenda kulala sehemu yoyote tunayotaka hivyo haikuwa shida. Basi hakuna alielala siku hio,tulikesha tunasali mpaka asubuh,na kulipipambazuka,Melisa akanambia twende Kwa mganga nikatilewe hilo jini maana huenda likanitesa. Nilivyo ndezi nikakubali,ila kwanza tukashirikiana kufanya usafi wa nyumban na tukamaliza,maana mm nilishika vyombo pamoja na Melisa,binamu yangu akawa anadeki,wengine wakawa wanapika chai na wengine wakawa wanafua maana nyumban kwetu hatunaga tabia ya kurundika nguo hata siku Moja. Basi tumemaliza mm na Melisa tukaanza kukokotana mpaka Kwa mganga maana aliongea sana usiku mpaka kweli nikajikuta naogopa maana n Mwanaume gan atakuwa anahudumia mwanamke ambae hamjui,nikawa najiambia kuwa yeye ananijua ila mm ndio simjui so natakiwa kuamin maneno ya Melisa. Basi hao mpaka Kwa mganga,akatuambia tulete kuku,kweli tukaenda kimnunua,akaanza kumzungusha,akamzungusha weee Kisha akamuweka chini,yule kuku akawa kama kalewa akaja kuangukia kwangu,tukashangaa yule mganga anacheka,Kisha akasema "nimeona ..nimeona mwanangu. "Nikawa nimetoa tu macho maana hata SIKUJUA mganga atakuwa kaona nn,si ndio akasema tumueleze shida yetu. Nikamuanza kumsimulia Kila kitu kuhusu yanayonitokea,akawa ananisikiliza Kwa makini Kisha akaanza kucheka,akacheka Sana Kisha akaanza kusema,"umependwa na mtoto wa jini wa bahar nyeusi na hakuna uwezo wa kumuacha so natakiwa nikubali kuolewa na jini.

"Jini? Mimi na Melisa tukauliza wote Kwa pamoja maana hatukutegemea kabisa kama atasema ety mm niolewe na jini nikaona ananiletea maskara huyu. Akatupa dawa zake za kupaka na kunywa,ila aliniogopesha Kisha hao tukarudi zetu nyumban na siku hio nilikuwa na mawazo sana. Kwenye mida ya kama SAA 11 Jamila alikuja kuniomba niende nae kwao Kuna kazi niiamsaidie,nikakubali ila nilikuwa na mawazo sana na Jamila alililijua Hilo,maana kawaida yangu huo nimechangamka sana.

"Una shida gani ww,akauliza Jamila ila kabla sijamjibu akaitwa ndani na mama yake akaniacha kwenye garden.sasa nikawa natembea tembea tu. Saa ngapi nisihisi nimekumbatiwa Kwa nyuma,alafu nikazibwa mdomo,huyo aliefanya hivyo alikuwa na harufu nzuri sana na hakuwa anasema chochote kile zaidi ya kunikiss nyuma ya shingo yangu na mkono wake mwingine akawa anafanya utalii kwenye mwili wangu Huku akiwa anahema kama jenerator mbovu. Itaendeleaaaaa..

"11__15" MY KING❤️❤️❤️ SEHEMU YA 11 nikataman kupiga kelele ila ndio hivyo nilikuwa ninezibwa mdomo,na hata sikuwa naweza kugeuka nyuma,alifanya hivyo Kwa takriban dakika tano,nageuka hivi sion mtu,aisee nilitimua mbio,maana nilijua jini Hilo limekuja,mpaka Kila alieniona akawa ananishangaa. Basi bana Jamila akanifata na kuanza kuniuliza Nina shida gani, si NDIO nikamsimulia kuhusu tulivyoenda Kwa mganga na alichonambia na kilichomkuta siku hio,aisee aliangua kicheko. Alicheka sana Kisha akasema twende ukaombewe Sasa Kwann umeenda Kwa mganga. "Unacheka Nini Nini Sasa Jamila,nitamuuliza maana niliona kama hakupaswa kucheka na badala yake alitakiwa kunionea huruma na sio kucheka vile alivyocheka. "Usijisikie vibaya Sajda Kwa kucheka kwangu ni Kwamba sikutegemea kabisa kama utaenda Kwa mganga Kwa swala kama hili,ila usijal nitakusaidia Kwa Kila litakalo kutatiza,akasema Jamila huku akiwa anajizuia kucheka. Basi siku hio ulienda na Ile namba iliyokuwa inamtumia sms za mahaba Kila siku Sajda,Sajda akaacha kuijibu yaan akajikuta anakuwa na wasiwasi sana nayo. Mara ikapiga,Sajda akajikaza na kunipokea,akasikia Ile sauti tamu ya kiume anayoipenda ikisema,"nipo tayar kuonana na wewe Sajda ila nihakikishie kuwa utanipenda Kwa namna nilivyo maana mm NAKUPENDA sana,ukàsema hio namba mpya. Sajda akakubali japo ilikuwa ni kishingo upande,hakuwa anaiman nae tena. Basi wwkapanga sehemu ambayo wataenda kuonana,na kweli kesho yake Sajda akajiandaa vizuri na kwenda mpaka alipoelekezwa kuwa atakutana na Mwanaume ambae hakuwa anaefahamu,alipofika akawa anaangaza angaza ili kuangalia kama anaweza kumuona MTU yoyote ambae angehisi ndio huyo anaemtafuta ila hakumuona,akachukua simu na kumpigia,kweli simu iliita Kwa sekunde kadhaa na kupokelewa, na Ile sauti inayosisimua moyo wangu Kwa aina ya kipekee sana. "Hellow upo WAPI maana mm nimeshafika muda mrefu tu,kwenye hii sehemu tulio kubaliana,nikasema. "Nimeshafika pia kipenzi changu na hapa nakuona umevaa gauni zuri lenye mauwa mekundu na mtandio mweusi,si ndio wewe,ukasikika upande wapili. Nikaamua kugeuka kuangalia huyo anaeongea hivyo yupo wapi,lakin bado sikumuona. "Upo wapi? maana sikuoni,nikamuuliza. Akacheka Kwa sekunde kadhaa Kwa Ile sauti yake,nyie mpaka nikajikuta nafunga macho,maana sijui Kwa nn inanisisimua hivyo,sijui ndio ananifanyia makusudi kwakuwa anajua Sina ubavu nikisiisikia,akasema " nipo kwenye mishipa yako,kwenye wekundu wa damu yako,Niko kwenye Kila pumzi unayoitoa,Niko kwenye maisha yako milele,Niko kama kivuli chako Kwa maana popote utakapokuwa na Mimi nitakuwepo nakupenda Sajda naomba tuyaanze maisha yetu Mimi na wewe,na tuujenge upendo wetu mpaka TUJE kuandikwa kwenye vitabu vya historia kuwa hakuna watu waliotufikia sisi Kwa namna tunavyopendana ,ukasikika upende wapili. "Sawa lakin upo wapi,nikasema. "Nyuma yako",ukasikika upande wa pili,na kweli nikageuka Kwa shauku kubwa sana maana nilikuwa nataman sana kumuona huyo Mwanaume ambae alikuwa anasababisha mapigo yangu ya moyo yaende kasi,Kila ninaposikia sauti yake. Laahaula! Nilitahamaki mara baada ya kugeuka nyuma na kumuona huyo Mwanaume ambae nilikuwa nikitaman sana kumuona,alikuwa ni Tariq. "Nikahisi labda sio yeye,maana inawezekana vipi nisiijue sauti yake siku zote hizo, Nikawa sijakataa simu Kisha nikasema mbona sikuoni. " Mbele yako Sajda,ni mm unaeniona mbele yako,akasema Tariq. Nikawa napima Ile sauti na nikweli ilikuwa ni sauti yake,nikageuka na kutaka kuondoka. "Tariq akanikumbuoia na kunishika mkono Kisha akapiga magoti,hapo Kuna watu wengine kwenye hilo eneo wanatuangalia,Sajda mamaa ni kwamba unataka chuki itawake kwenye maisha yako Kwa kiasi chote hicho,ni kweli huwezi kusamehe na kukubali kuanza upya,Leo nimepiga magoti mbele yako maana niliamin kufanya hivi walau unaweza ukanielewa,sijawah kubembeleza mwanamke kama ninavyofanya kwako, nakupenda sana sajda na hili sitanii,akawa anasema Huku kanishika mkono. Nilianza kuona aibu maana watu walizidi kitushangaa,nikamuomba asimame. "Siwez kusimama kabla hujanisamehe Sajda,akasema Tariq. "Sawa nimekusamehe Amka nikasema Basi akasimama na kunikumbatia Kwa nguvu na kusema, "Nina hisia sana na ww,hapa nimekushika lakin Hali yangu sio shwari kabisa,nikashangaa ananikiss kwenye lips na watu waliokuwa pale wakawa wanatushangilia,na hata hakuwa anaona aibu,mara wakaja wakaka wawili waliovalia gwanda za jeshi Kisha wakampa heshima yake pale na mara baada ya kumpa heshima wakaondoka,yaan ndio kama wakazidisha shangwe Kwa watu hapo mm naona aibu vibaya mno. "Akanishika mkono Kisha tukawa tunaelekea kwenye gari lake,nikapanda maana sikuwa nachaguo zaidi ya Hilo maana nilikuwa naona aibu kukaa kwenye Lile eneo. Tumepanda kwenye gari,nikashangaa Tariq anapandisha vioo Kisha akawa ananiangalia,akasogeza mkono wake akanishika mkono Kisha akaukiss na kusema unataka nikupeleke wapi kipenzi changu. Bado sikuwa na jibu la kumpa maana niliona Kila kitu kilitokea haraka haraka sana na sikuwa nimejipanga Kwa lolote Lile. "Kauli yangu ni Ile ile bado,kama unataka nikusamehe twende ukafanye ulichonifanyia na mm sitokuwa na kisasi na ww na huenda ikafikiria kukupenda. Tariq akatabasamu Kisha akasema sawa malkia wangu kauli yako ni amri yangu nitafanya utakacho mpenzi,nikaanza kuchekelea na kuona nimemkomoa Nikijua kuwa ety Tariq ataenda kariakoo aoogee na sabuni mche mzima kumbe nilikuwa najidanganya tu na alikuwa ameshapanga mambo yake,ila Mwanaume huyu simuwezi😀 NAKUJA SEHEMU YA 12 basi akanirudisha mpaka kwetu,nashangaa natoka namuona mama yangu akaanza kupiga vigelegele,nikashangaa huyu mama vipi na yeye,nikashangaa Tariq kashuka kwenye gari Kisha akaenda Moja Kwa Moja mpaka Kwa mama yangu Kisha akamshika mkono na kusema, "shikamoo mama mkwe,mama yangu aliitikia Ile salamu Kwa bashasha kubwa na kusema karibu sana kijana wangu na najivunia sana Kwa kutaka kumuoa mwanangu na nawaombea muishi pamoja siku zote za maisha yenu,akasema mama yangu na mm nikabaki nimetoa macho tu,Kwa sababu SIKUJUA hata alikuja kuongea Nini na mama yangu na lini... "Mama lakin hatuna mahusiano Kwann unamuita mkwe wako,nikasema nikashangaa Tariq kadakia. "Usione aibu bana maana muda sio mrefu Kila mtu atashuhudia ndoa yetu,akasema Tariq Kisha akanisogelea na kininong'oneza na kusema alafu utabeba mimba na Kila mtu atajua nakukulaga. "Unasema nn wewe,nikauliza Akanishika mkono Kisha akasema "mama Kwa ridhaa yako naomba kesho nitoke na mke wangu mtarajiwa. "Usijal mwanangu,maana posa yako tumeshaipokea naomba ndoa isiwe muda mrefu maana siunajua umuhimu WA kufunga ndoa mapema,akasema mama Kisha akaniachia na kunikonyeza Kisha akaondoka zake. Kila kitu kulikuwa kama ndoto kwangu,maana sikuwa naelewa chochote kile kinachoendelea,SIKUJUA hata ni lini alikuja kutoa posa,maana sikuwah kuona watu wakija nyumban kwetu,ila sikutaka kuhoji na kujiambia kuwa lazima nipambane Kisha nimalizane na Tariq. Sikuwa na uhakika kama NAMPENDA au laa,sikuwa najua kama bado Nina hasira au Nina upendo,maana moyo wangu na akili yangu ni kama hazikuwa zinaongea lugha Moja,moyo unataman kuendelea kusikia Ile sauti yake na kuona zile sms zake tamu za kusisimua,ila akili yangu ilikuwa inaniambia kuwa hafai Kwa vile vitendo ambavyo alinifanyia. Nikiwa bado nawaza nifanye Nini mara ikaingia sms,kutoka kwenye Ile namba na hapo ndio nilikuwa nimeshamjua kuwa siku zote zile nilikuwa nachart na Tariq. Kipenzi siulisema unanipenda sauti yangu au umeshabadilisha mawazo baada ya kuniona,ila unajua kabisa umeshaniloga maana najikuta kwako sipindui kabisa sijui hata Kwann nakupenda kiasi chote hichi,naomba nipe nafasi niwe mume wako,naomba nipe nafasi niwe Mwanaume wa maisha yako na baba wa watoto wako,nakupenda Sajda na naahidi kufanya Kila kitu unachokitaka. Utaweza kwenda kutafuta samaki kwenye vumbi,utaweza kuogea sabuni mche mzima na ule ugali kama ulivyonifanyia yaan hapo ndio naweza kuwaza kukusamehe. "Kwamba hautanisamehe ila ndio utawaza kunisamehe,ila wewe mwanamke unanyodo,ila nitese tu maana ni kiherehere changu mwenyewe Cha kukupenda,akasema nikajikuta nacheka. Basi tukaongea sana,nikawa najikuta nasisimka na najisikia vizuri sana kuongea na Tariq ila ndio bado nilikuwa na kaujeuri kananisumbua. Akanambia kesho tutaenda beach na atafanya Kila ninachokitaka,nikakubali Nikijua kuwa anaenda kwenye hizi beach zetu,maana kama tunavyojua coco beach kulivyo na hio siku ilikuwa ni JUMAMOS so nikajua lazima kutakuwa na watu. Kweli tukatoka na ugali wetu nyumban maana nilimpania kweli,yeye akanunua nyama choma. Basi tumefika akavua t shart akabaki kifua wazi. Amejazia sio mchezo,nikajikuta natabasamu Kila ninapomtazama. Na Tariq aliliona Hilo akawa anazidisha manjonjo,mara anikonyeze mara anikiss kwambali,yaan nilikuwa najisikia vizuri,mpaka nikataman nimuachie asiendelee kufanya hizo adhabu. Akaanza kula ugali,yaan ugali upo Huko nyama kule,Akala chap chap mpaka nikawa nashangaa mbona kamaliza mapema hivyo,kumbe mwenzangu mjeda hayo mazoez niliyotaka ayafanye ni kama kupiga push up Kumi tu. Nashangaa sion hata watu,kumbe hio beach hainaga watu Kwa hio nilikuwa mm na Tariq tu, Kamaliza kaanza kuogelea kwenye mchanga baada ya hapo akakataa kata,sabuni akailoweka akajimwagia Kisha akaingia baharin kuogelea. Alipomaliza akatoka akanisogelea mpaka nilipo,akaniangalia Kwa dakika kadhaa na kusema nimeshamaliza Kila kitu haya nambie unataka nn kingine. "Hamna mtu yoyote aliekuona,mbona tuko wenyewe na kwann umeloweka sabun haujaogea kama mm,nikaanza kulalamika. Maisha ni mipango bana,usiponisamehe unayakwako,akasema Kisha akanisogelea zaidi akaanza kujikohoza. "Nasikia baridi sana mke wangu,akasema. "Mm sio mke wako bana niache" ,nikasema. Nikashangaa ananisogelea Kisha akanikumbatia na kuniambia nasikia baridi twende ukanipe kidogo basi. "Nikupe Nini Sasa embu niache. "Wewe nae kama huelewi vile,hivi mfano nikikuoa alafu nikawa nasikia baridi siutakuwa unanipa kidogo we,akasema Tariq. Nikaanza kucheka Kisha nikamwambia ndio nitakupa maembe siunapendag. Alicheka sana Kisha akasema," wewe nae unajitoaga kwenye mstar,Kwan husikiag hata mashoga zako wanawazaga nn wanaume zao bana,yaan kama hivi natetemeka unakuja unanikumbatia Kisha unanambia mume wangu nivue mwenyewe au utanivua wewe,alafu naanza kuringa ringa,unanivua nguo alafu unakuja kujilaza kifuan kwangu mm naanza kuona aibu,utanifanya nn,akasema Tariq. "Nitakubaka,nikasema jaman alicheka Kisha akanikumbatia akanambia nakupenda sana Sajda hope tutaanza upya na tutafungua ukurasa wa penzi letu na hope utanipenda kama ninavyokupenda,akasema na mm wakat wote huo nilikuwa kimya naona zangu aibu tu hapo. NAKUJA SEHEMU YA 13 basi tukatoka pale beach akanipeleka sehemu tukale dinner manaa Giza lilikuwa limeshaingia,ila alikuwa anakula Huku mkono wake Mmoja akiwa amenishika mm. Akala tumemaliza akanishika mkono tukaenda mpaka kwenye gari,akanipeleka mpaka nyumban nikawa namuaga kuwa nataka kuingia ndani,saa ngapi asinivute akaanza kunikiss. Yaan Mwanaume anajua kukiss huyu mpaka nikajikuta nimelegea,na yeye ndio akawa Hana Hali kabisa. "Mwambie mama kuwa unaenda kulala na mm maana Mwenzio sijiwez,yaan nimepambana sana kujizuia ila nashindwa maana mm Nina hisia sna na wewe my love. " Mama hawez kukubali mm nilale nje,so Kwa heri nikasema nikashangaa kanivuta tena akaanza kunikiss upya Kisha akaniachia nikaingia ndani lakin hapo mwili unanichemka balaa. Nikamkuta mama ukumbin nikamsalimia Kisha nikapitiliza chumban,yaan Kwa namna ambavyo nilikuwa najisikia sikutaka kuongea na mtu. Nafika ndani nasikia dirisha linagongwa,kwakuwa nilikuwa nalala pekee yangu nikaenda kufungua,Sasa dirisha langu lilikuwa la alminiaum na hawakuwa wameweka wavu Wala ndondo,nikafungua dirisha,nashangaa nakutana na Tariq. Nimeshindwa mama nakuja kulala na wewe akanambia,nikawa naogopa nikashangaa mwamba ameshaingia ndani,nikakuambia mlangon na kufunga mlango,maana niliogopa sana kama mtu yoyote yule akijua kuwa Kuna Mwanaume ameingia ndani. Nimemaliza tu kufunga mlango akanidaka tukaanza kukiss,nashangaa namuona abdala kichwa wazi katuna balaa,Tariq akaninong'oneza na kusema naomba kidogo tu maana hapa nilipo Sina Hali kabisa,yaan nataman sana kulala na ww usiku kucha mke wangu,akasema Tariq. "Lakin mm sio mke,nikaema ila kabla sijamaliza kusema nikapokelewa na french kiss Moja ya maana nikatulia mwenyewe,yaan tukakiss mpaka mwisho tukajikuta tumezama kuleee kwenye ulimwengu wa huba. Tumemaliza Kwan Tariq anataka kuondoka,yaan ni kama kajisahaulisha kabisa kama kaiba,na hakupaswa kuwa pale kwetu. Ety ananambia kuwa anataka kukutwe ili tufungishwe ndoa ya mkeka maana amechoka kusbiria. "Alafu hayo maswala ya kusema wewe sio mke wangu naomba nisiyasikie tena,maana hujawah kuniita majina mazuri au unahisi sistahili na mm kuitwa majina mazuri. Mm ndio mwenye ruhusa ya kupenda wewe jukum lako ni kuniheshimu tu,akasema Tariq. "Nisisikie tena hizo kauli zako,maana nimependa na nakupenda hayo maswala mengine wewe sema na moyo wako usinaiambie mm Huko,akasema na mm nikawa kimya tu. Basi akakaa pale mpaka adhana ya alfajiri,ety ananambia anataka aende kuoga Kisha akaswali,nikamwambia ataogaje pale maana chumba changu hakukuwa na bafu Kwa maana hio mtu akitaka kuoga ni lazima atoke nje na familia yangu yote itamuona. Tariq hakutaka kuendelea kubishana na mm,akanisogelea na kunikiss Kisha akaondoka zake. Basi kuanzia siku hio penzi likaanza,alikuwa ananipenda sana kiasi kwamba nilikuwa naufell upendo wake kwangu,alikuwa anapambana Sana kutimiza Kila ninachotaka. Kuna muda alikuwa anaenda kambini anakaa hata wiki ila akirudi ananiletea zawad za kutosha na alipambana sana kunipa furaha. .basi tukaanza kupanga siku ya ndoa,akaja nyumban akanitolea mahari akapanga na siku ya ndoa na kiukweli mm sikuwa na kipingamizi Cha aina yoyote Ile. Basi siku zilienda tukaenda kufunga ndoa jeshini,na siku hio kulijaa wanajeshi wa kutosha,tukapanga tuende tukale honeymoon bagamoyo Kwa siku saba Kisha tutaenda kwake,sikuwah hata siku Moja kujua kama ana kwake maana siku zote nilikuwa namuona anaishi Kwa wazaz wake. Usiku basi baada ya ndoa Tariq alikuwa anaonekana kana kwamba anaugwadu sana,akawa kanishika mkono ananikokota chumban. Tumefika mlango wa chumba Cha hotel akanibeba juu juu mpaka kitandani,Kisha akanitupa kitandani na mara baada ya kunitupa kitandani akàaanza ok unifungua gauni Kwa mapozi Huku akiwa ananipapasa mwili,alikuwa anaonekana namna ambavyo alikuwa na hisia Kali sana kwangu. Kamaliza akanibeba mpaka bafuni,yaan tumefika bafuna hatukuweza kuoga hata,yaan kafungulia tu maji akaanza kunilamba mwili mzima kama katoto cha paka. "Mama Nina hisia sana na wewe,mpaka nashindwa kabisa kujizuia mke wangu,yaan hapa nataman hata nisifanye chochote na ww zaidi ya kufanya mapenzi,yaan sio Siri nashindwa kuzizuia hisia zangu nikiwa karibu yako,akasema Tariq na muda wote huo mimi nipo kimya tu. Amemaliza kunilamba tukaingia kwenye burudani yetu Ile,tumemaliza,akaniogesha Kisha akasogea kwenye sikio langu Kisha akanambia, "nataka tena wife. Sikuwa na hata nguvu ya kumpinga maana ameitolea mahar Sasa namnyima ya nn ety. Basi siku hio tulishinda tunapeana burudan na tunaambiana namna tunavyopendana,yaan Tariq alikuwa kana kwamba ameshachanganyikiwa na penzi langu yaan nisije nikajisahau hata bahat mbaya nikaonesha paja yaan ni ata nipamia,nikisema niende kuoga basi yupo nyuma yangu. Basi siku saba ziliisha,Kwa mawazo yangu nikajua ananipeleka Kwa wazaz wake,ila haikuwa hivyo nikashangaa tunaenda masaki kwenye nyumba Moja ya kifahar Ina zinga Moja la geti,Tariq akaingiza gari Kisha akanipa funguo na kusema, "mm ni wako na Kila ninachokimiliki ni Mali yako,nikaribishe nyumban mke wangu. NAKUJA SEHEMU YA 14 Basi bana ilikuwa ni nyumba kubwa sana,yaan sikuamin kama Tariq anaweza akawa anamiliki nyumba kubwa kama Ile,tukaingia ndani na kuwakuta wazaz wa Tariq,Jamila,mama yangu pamoja na binamu yangu warda. Waliandaa tafrija ndogo ambayo ni kama walikuwa wanatukaribisha nyumban,tukala na kisherehekea na Tariq aliashaanda mazingira yetu Mimi na yeye,hivyo watu walivyoondoka akanishika mkono mpaka chumban nikakuta shuka jeupe linamau mekundu na katikati lilikuwa limeandikwan I LOVE U SAJDA,nikatabasamu na kujua hapa mwamba kadhapotea mazima. Tukaingia chumban ambapo alichukua simu yake Kisha akaplay nyumbo ya slowly Ile ya meddy. Akaja akanishika mkono akanisimamisha Kisha akanishika kiuno tukaanza kucheza hapo tupo zero distance,na mm sikuwa najal Wala nn,Kwa sababu kitu kikubwa ni kufurahia penzi letu,nilikuwa nimevaa short dress na Tariq alikuwa ame vaa boksa tu na alikuwa kifua wazi,akawa ananiangalia akiwa ameshalegeza macho. Wewe mtoto hivyo vinguo vyako hivyo,mm nitaenda kazin kweli au ndio nitashinda nakukula tu,akasema. "Ndicho unachowaza hicho,nikamwambia. Lazima niwe nawazi hivyo Kwa sababu nakupenda na ninahisia sana na wewe,yaan ni kwamba najikaza tu usije ukanikimbia ila kiukweli kila ninapokuona najikuta nataka,yaan nataka Kila saa maana nimeitolea mahari hio au umesahau. Hata kama umeitolea mahari ndio utake kuichakaza jaman,nikasema "Haiwez kuchakaa bana maana nakula kistaarabu,twende basi ukanipe tena akasema. "Aweee Mimi sitaki bana,nikaanza kuondoka kuelekea ukumbini,akawa ananifata,nikaanza kujikimbiza akawa ananikimbiza Huku anasema nikikudaka utaichezea wiki nzima yaan hakuna kula Wala kulala. "Utaniua Sasa nikasema . "Siwez kukuuwa bana maana Huku kutaka Kila saa inaonesha ni namna gani nakupenda na namnà Gani Nina hisia na ww,au unataka kunifanya nijizuie kuchukua haki yangu ili nifariki,niache bana,alafu isitoshe mm nafanya mazoezi sana so ni lazima niwe na mzuka Kila wakat wife,hio ndio inaonesha ni namna gani nakupenda na nahisia na wewe,yaan ukiona nimeanza kupunguza ujue na upendo wangu umeanza kupungua au nimeanza kukuona wakawaida sana,akasema Kisha akanishika na kujikuta tunazama kwenye ulimwengu wa huba. Maisha yakawa yanaendelea yaan Tariq alikuwa anapenda sex kuliko kula yaan,ila alikuwa ananipenda sana yaan siku akiwa nyumban hatak niguse chochote kile,yaan kazi zote atazifanya yeye,anakuja kulitea mpaka chai chumban,atanilisha ataniogesha,nikamuuliza Kwann hataki nifanye chochote akawa ananambia anafanya mazoezi kwangu,ili siku tukipata mtoto wa kwanza awe anamuhudumia mwenyewe. Basi alienda nyumban Kwa mama akampa PONGEZI,nakumbuka alimpa pesa na akamuahidi kuwa ni lazima atamfanyia kitu kama shukran ya kunizaa. Kumbe alikuwa anamjengea mama nyumba Kwa Siri,yaan alitaka kukufanyia surprise tu wote,ila hatukujua,na mm nilivyo kidomo Domo nikawa namsimulia binamu yangu raha ambazo nazipata Kwa Tariq kumbe najitengenezea mwenyewe shimo. Yaan nimempata kijana mdogo,ananipenda,anapesa na Yuko tayar kunifanyia Kila ninachokitaka,bahat gani hii. Siku Moja nimekaa na mume wangu mara ikaingia sms kutoka Kwa namba mpya kwenye simu ya mume wangu inasema. "Huyo unaejufanya unampenda hivi unajua Siri zake. Tariq akanionesha Ile message Kisha akasema wanga wameshaanza kazi Yao,mm namblock akanambia. "Usimblock muache tujue lengo lake,nikamjibu "Eheee nambie anasiri gani?,akajibu Ile sms Tariq. "Ameoza Huko nyuma,yaan alikuwa anabadilisha wanaume na analiwa nyuma,sms ikaingia Tariq akacheka Sana Kisha akanionesha Ile sms,kiukweli nilishtuka màana SIKUJUA huyo anaetuma hizo sms anataka nn kwangu.

"Najua kaharibika alafu uzuri mm ndio nimemuharibu,embu acha umbea hivi unajua ananipa nini huyu mwanamke mpaka uanze uchawi wako na nikuambie tu hatuwez kuachana hata mseme Nini maana mm NAMPENDA hata kama angekuwa ni Malaya,Tariq akajibu hivyo ila kiukweli nilijisikia vizuri sana,maana angalau Nina Mwanaume ambae anaweza kinitetea na hapanic Kwa taarifa ambazo hazieleweki. Ila nilishangaa sana maana SIKUJUA ni nani anataka kuniharibia ndoa yangu jaman,maana nilihisi Sina maadui Sasa Kwann amtumie mume wangu sms kama Ile,ungekuwa Mwanaume mwingine mm si ningekuwa nimeshaachika kitambo nikawa najiuliza,Tariq akanisogelea Kisha akanishika mkono na kuniambia, "najua Hawa wanga wanataka kukuwazisha achana nao maana hakuna mtu anauwezo wa kututengenisha,ni dhahiri Kuna watu wanatuonea wivu hivyo wanataka kututengenisha,Sasa tunatakiwa tuwe na mshikamano wa Hali ya juu na ujasiri maana mm sitakaa niisikilize maneno ya watu Kwa sababu nakuamin wewe kuliko mtu yoyote yule kwenye hii Dunia... NAKUJA SEHEM YA 15

Tariq hakutaka kusikia hàbar za MTU yoyote yule KUHUSU Mimi,alinipa kipaumbele Sana Kwenye maisha yake kuliko kitu CHOCHOTE kile,alikuwa hata akipata mshahara wake anauweka MEZAN na anataka mm ndio nipange bajeti,alikuwa ananipenda mpakà nikawa nahisi hakuna MTU anapendwa kuliko Mimi Kwenye hii Dunia,Nilikuwa sipat ujauzito ila Hilo halikuwa tatizo kwake,na mara zote alinipa moyo na kinambia yeye kanipenda Mimi na watoto ni maaliwa,kama mungu atajalia SAWA ila kama hajajalia hawez kuforce mambo MAANA yeye aliapa kuwa na mm maisha yake yote hata nikiwa na mapungufu Gani.. Siku Moja Kuna mjeda mwenzie alikuwa anaoa,akaniambia nijiandae twende wote,basi nikakubali hapo nimejipodoa hatar,Sasa Ile natoka nikashangaa mume wangu kabadilika,akaniambia kapunguze huo urembo huko usoni,MAANA we ni mualikwa na Sio muolewa ji,au unataka bwana harusi abadilishe mawazo akuoe ww alafu mm uniache yatima,Akasema nikajikuta nacheka TU. "Punguza wivu mume wangu jaman,Sasa hutaki nipendeze,Nikasema Akaniangalia Kwa dakika kadhaa Kisha Akasema,"unatakiwa upendeze kwaajili yangu TU,mm siwez kuvumulia kuona MTU anakutolea macho naweza nikaua. "Any way embu twende ukanitikise kidogo na nipime wivu wangu,ila yakinishinda tunarudi NYUMBAN,Akasema nikacheka Kisha tukaanza safar ya kwenda Kwenye HIO sherehe,ila Kila dakika mume wangu alikuwa anananiangalia Kisha anatabasamu TU. "Tumefika Kwenye shughuli akaniambia usishuke Kwenye gari,nikamuuliza kwann akanambia Ety anataka KWENDA kuangalia usalama kwanza,Kwa MAANA natakiwa nilindwe nisije nikaibiwa,nikaanza kucheka TU. Basi akatoka akawa anazunguka zunguka TU,mara akaja Kwenye mlango WA gari akanifungulia mlango,mara tukashangaa taa inamulika pale Kwenye mlango WA gari ,Kisha mc Akasema Kwa sauti kuwa. "Haya Sasa Mr na Mrs Tariq wanaingia karibun Sana,watu wote wakawa wanatuangalia hata wale waliokuwa ndani wakawa wanaotoka nje kutushangaa,sio Siri Nilikuwa naona aibu vibaya Sana yaan.

Kweli bwana Tariq unajua kuchangua,yaan MWANAMKE kama kashushwa vile,MWANAMKE anamwendo WA ngamia,anajicho kama kala kungu,kiuno Sasa dondola sio dondola,akawa anasema mc,Sasa sijui Tariq akawa anaona wivu,saa ngapi asivue koti lake la Situ na kunifunika kichwan Kisha akanishika kana kwamba ananificha,aisee watu walicheka mno ila mm nikaanza kuona aibu MAANA SIKUJUA Tariq anafanya vile Kwa sababu Gani kumbe wivu unamsumbua TU. Akataka nikakae nyuma kabisa ya ukumbi,nikamuuliza kwann,akanambia hataki watu wanikodolee macho na anajuta kutaka kunifanyia surprise MAANA ni kama ananitamgaza watu wanitongoze. "Kwann unasema hivyo mume wangu nikamuuliza Kwa sababu mm nawajua watu wangu ninao Fanya nao KAZI,uhuni pia ni KAZI Yao,so wasije wakaanza kukulaghai ukaniacha,Akasema.

Sio Siri nikajisikia vibaya ila nikamuelewa MAANA alikuwa Kwenye harakat za kulinda penzi lake TU. Basi sisi ni kama sherehe ilikuwa haituhusu Kwa MAANA tulikuwa nyuma huko Hamna hata mwanga,Tariq akawa ananipigia story TU,tukawa tunacheka akawa hataki tujichanganye kabisa. Sasa ikafika Muda WA zawadi akanambia mm nikae pale pale na yeye ataenda kutoa zawad alafu atarudi tuondoke. Nikakubali,kweli akasimama na kuelekea mbele ambapo kulikuwa na maharusi,lakin kitendo Cha yeye kunyanyuka akaja mwababa anakitambi HUYO akaja akakaa pemben yangu,alikuwa ni kama MTU mzima Kwa kumkadiria anaweza kufika miaka 50 na kitu. " Haujambo MREMBo,Akasema mm nikatabasamu TU. "Sio Siri Tariq Anajua kuchagua na ndio maanà anakuficha sana MAANA ungeshaibiwa Akasema mm nikawa natabasamu tu,mara Tariq akarudi aisee alikuwa kavuta mdomo ila alipofika pale akampa heshuma maanà nahisi alikuwa mkuu wake,Kisha akakaa pemben yake akiwa kakunja sura huyo mpaka nikawa namshangaa,nikaona niepushe dhahama na tunyanyuke tuondoke. "Samahan naomba tuondoke,Nikasema "Mbona mapema sana na hata chakula bado,akasema yule baba mwenye kitambi. Sijisikii vizuri tu so acha tuondoke Nikasema Kisha nikaenda kimshika mkono mume wangu,Kisha tukaanza kuondoka. "Yule mpuuzi alikuwa anakuambia nn,akaniuliza Tariq "Alikuwa amekuja kunisalimia tu nikajibu " Ameshaanza kukutolea macho,Mwanaume muhuni yule kama nn,akasema Tariq Kwa sauti ya jazba. "Lakin hakuna baya lolote aliloniambia Zaid ya salamu tu,mbona umekasirika sana nikamuuliza. " Huvijui hivi vizee yaan vina tamaa sana,hapa usikute ameshakutaman,yaan nilitaman nimpasue Sema tu ni mkuu wangu tu yaan sijui kama tutakuja wote tena kwenye hizi shughuli za wajeda maana ni wapuuzi sana na sitokaa niruhusu wakusogelee hata Kwa bahat mbaya maana vimezidi ushenzi,akasema Tariq Kwa jazba ikabidi nimtulize tu Kwa maana namjua alivyokuwa na wivu wa ajabu. Basi akatulia ila akanambia Ety nilitaka atulie zaidi basi niende nikampe utamu ndio unamtulizaga vizuri Ndio vitu unavyoviwaza hivyo ww,haya twende tukaoge alafu nakususia mwili wangu uufanye utakavyo. "Unamaanisha unanisusia kwamba unakuwa gogo na haunipi Yale mauno yako tena,usinisusie bana nataka unipe penzi,akasema tukajikuta tunaanza kucheka. Itaendeleaaaaaaa

"16__17MWISHO" MY KING ❤️❤️❤️

SEHEMU YA 16 Basi tukaoga na mara baada ya kumaliza kuoga tukazama kwenye burudan zetu zile. Siku hio ikapita na mume wangu akanambia kuwa anataka tuanze harakat Sasa za kutafuta mtoto,basi tukaenda hospital na kuambiwa sote hatuna matatizo ni kwamba wakat WA MUNGU haujafika tu,basi maisha yakaendelea,siku Moja nilienda na mume wangu sokon nikakuta mtu anakula ugali na mlenda,yaan nilitaman mpaka nikaenda kumuuliza kaupata akanielekeza ilikuwa ni zile mama ntilie za sokon ziko hovyo hovyo kweli,nikaenda nikaanza kula mpaka mume wangu akaanza kunishangaa maana tumetoka nyumban tukiwa tumeshakula tayar. Nimemaliza kula ugali na mlenda Nikamfata mume wangu na kumuomba anichomee nyama,Wala hakukataa tukaanza kula,yaan nimekula mume wangu ananiangalia Huku akacheka tu. Tumetoka tukarudi nyumban,Yaan sijui n Kwann nilikuwa nasikia njaa,yaan Kila dakika nikawa nawaza kula tu yaan na nilikuwa Kila dakika nasikia njaa,yaan Tariq akawa anacheka tu Kila aliniona. Nilikuwa ni mchapa KAZI mno na Nina appetite ya fundi ujenzi yaan nisione kitu mbele yangu nataka kula tu yaan. Tariq akaanza kuimba,imekatikia imekatikia,nikamuuliza imekatikia nn,akanimbia twende hospital,kweli tukaenda kupima nashangaa mimba imo. Tariq akanibeba juu juu mpaka kwenye gari akawa hataki nifanye kazi yoyote Ile,anasema mimba inatoka,akamwambia mama yangu kuwa nimeshapata mimba,mama yangu akafurahi sana,kumbe na binamu yangu akasikia kuwa Nina ujauzito na taarifa zikaenea mpaka mtaan kuwa Nina ujauzito hapo Nina ujauzito wa miezi miwili tu yaan,tayar Kila mtu Anajua. Tariq ety akataka kuomba likizo anihudumue,nikamwabia aisombe likizo asuburi nikikaribia kujifungua ndio aombe hio likizo... Basi mimba ikawa haimpend Tariq ila Tariq akawa ni muelewa sana maana anajua Heka Heka za mimba na kweli sikuwah kutaka kuwa karibu nae. Siku hio akatumiwa sms kuwa mke wako huyo unaempenda amebeba mimba ambayo sio yako,na anaona aibu kukaa nayo na anataka kuitoa hio mimba,pole Kwa kumuamin mkeo,kama huamin Rudi nyumban utakuta katoa mimba. Kweli nilikuwa nyumban pekee yangu,na kama mnavyojua mimba yangu inapenda chakula Sana,Sasa nimeingia jikon nikakuta juice nikaanza kuifakamia,saa ngapi nisianze kusikia Tumbo linaniuma. Mara namuona Tariq anakuja,akakuta na bleed yaan alipiga kelele Kisha akakaa chini akaanza kulia,nyie alilia hata haangalii kama mm naumwa au laa,alilia sana Kisha akaondoka akaniacha pale chini natokwa na damu japo hazikuwa nyingi nikajikaza nikaenda hospital mwenyewe,nikiwa hospitalin mama yangu akaja,nikaomba simu yangu maana nilishangaa Tariq, katuma sms inasema naomba tupeane nafasi nakupenda sana ila Sina ujasiri wa kukuangalia Sajda,mwenyezi Mungu akuponye,na kama Kuna uwezekano amlinde mwanao.. Nilishangaa Kwann anasema vile kumbe kashapewa gazeti la uongo na akaliamin lakin n lazima aamin ila mm mwenyewe nilishangaa Kwann nablead na wakat Nina ujauzito ila Kwa bahat nzuri mimba haikutika ila nilitakiwa nikae bed rest maana mimba ilikuwa Ina hati hati ya kutoka. Sasa nikalazwa ila kuanzia Niko pale hospital Tariq hakuwah kupatikana Wala kuja kuniona hata Kwa bahat mbaya mpaka nikawa namshangaa amepatwa na nini,na hata nikijaribu kumuulizia Kwa Jamila hata Jamila hakuwa anajua alipo,alinambia tu Yuko kambini,nikaona nitulie tu. Nikakaa hospital Kwa mieizi tisa yote mpaka ikafika siku ambayo nilitakiwa kujifungua,nikajifungua ka baby boy yaan alikuwa copy ya mume wangu Tariq,mama yake akamtuma mtu amuambie kuwa nimejifungua mtoto copy yake,ila Bado siku hio hakuja,alikuja kama baada ya siku mbili na wakat huo nilikuwa kwetu. Alikuwa kakonda sana,yaan alipofika hakutaka hata kuongea na mtu akapitiluza na kumuangalia mtoto,jaman alikuwa amekonda akakaa chini akaanza kulia Kwa uchungu,alilia sana mwisho akatoka nikashangaa ameenda kumkunja binamu yangu akawa anasema nakuuwa Leo. Kwann atake kumpiga binamu yake Sajda usikose kipande kinachofuata. NAKUJA

SEHEMU YA 17

alianza kumuweka vibao mfululizo,jaman alimpiga mpaka mama yangu na mama yake wakaenda kumuamua,akawa hataki anasema nataka kumuona anakufa huyu mwanamke. Amefanya je,ndio akaanza kuonesha sms,yeye ndio alisema kuwa mm Ile mimba haikuwa ya mume wangu ila mume wangu hakuwa anaamin maana alikuwa ananipenda na kuniamin sana Mimi,so hakutaka kabisa kumsikiliza ndipo alipomuambia kama haamin basi arudi nyumban na atanikuta nimetoa mimba,ndio akanikuta na bleed hapo ndipo akaamin kumbe kweli nilikuwa natoa mimba na akawa anaumia sana ndipo akaamua kushinda kambini ila hakuwa sawa kabisa maana hata mazoezi hakuwa anaweza kufanya vizuri Kwa sababu alikuwa anamawazo sana. Na kipindi chote hicho akawa ananiamin binamu yangu,na kina siku hajui hata ilikuwaje akalala na binamu yangu na hapo kumbe binamu yangu alikuwa na ujauzito wa mume wangu,na mume wangu akifanya vile Kwa sababu ya kunikomoa,kama mm nimemsalit basi acha yeye atembee na binamu yangu.

Nilihisi kuchanganyikiwa Kwa kweli,mume wangu akaanza kuomba msamaha,nilimsamehe maana najua namna alivyokuwa ananipenda ila nilitaka kujua Kwann binamu yangu anifanyie vile. Ndio akasema ety nilikuwa naringa sana na akataka kunikomesha maana nilikuwa najifanya kama mm ndio nimeolewa pekee yangu dunian,nilishangaa naringa Kwann maana sijawah kuringa hata Kwa bahat mbaya. Ila nikajua kilichokuwa kinamsumbua ni wivu na husda tu,ni kama alikuwa anayataman maisha yangu na anamtaman mume wangu tu hakuwa na jambo lingine. Basi nikala uzazi mwezi Mmoja na nusu mume wangu akawaalika watu nyumban kwao,akafanya hakika,akamchinjia mtoto wetu na baada ya hio tafrija akataka watu waangalie kitu maana alikiandaa muda mrefu na akawa anataman Kila mtu ajue ni namna gani ananipenda. Kweli tukaingia ndani ilawashwa tv,Tariq akachomeka flash ikaanza kusikika sauti yake akawa anaelezea kuanzia siku ya kwanza ambapo alikutana na mm,ambapo niliemwagia maji machafu mpaka alipoanza kunipenda,mpaka nilivyokuwa namzungusha mpaka aliponioa,na akaaelezea namna ambavyo ananipenda na anajivunia kuwa na mm na akataka binamu yangu aone,na masaa yote alikuwa analia tu.

Baada ya pale tukarudi zetu kwetu na maisha yetu yakaanza kuwa bulbul yaan niseme Nini nisipate jaman,binamu yangu akawa anajaribu kutoa mimba na Kwa bahat mbaya akatoa mimba vibaya ikampelekea kuharibika kizazi na akafariki ila alienda Huko kigoma,mama alienda kumzika maana alikuwa hafai kusafirishwa Kwa namna alivyo haribika. Na maisha yetu yamerudi kama mwanzo Yaan mahaba ya Tariq yamezidi kuliko mwanzo. Ukiwa unafurah na mahusiano yako au ndoa yako jaribu kuifanya Siri. MWISHO

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA

Mpya zaidi Nzee zaidi

Ads related

Smartwatchs