Ndoa yangu

welcome katika Simulizizaonline.blogspot.com naimani muwazima wa afya emoji ( 1———3 ) ❤️🔥 NDOA YANGU EPISODE -01 Baada ya kufuta meza ya chakula na kuosha vyombo, nilienda chumbani, sikujisumbua kusema usiku mwema kwa Antony ambae alikuwa sebuleni akiangalia fainali ya ligi ya mpira wa kikapu (NBA) kati ya Golden Warriors na Cleveland Cavaliers. Nikijua lazima atakuja chumbani si muda mrefu, hivyo nlitaka akifika tu afikiri mimi nimeshalala muda mrefu. Haraka haraka nikaingia bafuni na kuoga kabla sijapanda kitandani. Nikahakikisha navaa suruali ndefu ili kusiwe na namna yeyote ya yeye ku-'access' mwili wangu. Baada ya saa moja nikamsikia akipanda juu ya kitanda na kugeukia upande mwingine, kidogo nikashusha pumzi nliyoibana kwa muda mrefu. Nikafurahi kwa kuwa niliweza kukwepa kufanya tendo la ndoa usiku ule. Asubuhi ile nilijua lazima tutakuwa na ugomvi tena, nikamuomba Mungu kimya kimya aniepushe na ugomvi. Mara nikahisi mikono yake ikinipapasa papasa mwili wangu. Nikawa sina shaka kabisa nini kinachohitajika na ni kipi kitatokea. Nikafungua macho yangu na kutizama saa iliyopo ukutani. Ilikuwa saa kumi na mbili kasoro robo asubuhi. Nikageuka na kuondoa mikono yake na kujaribu kuamka lakini akanivuta nisiamke. Kama mara tatu kila nikitaka kuamka ananivuta nibaki kitandani. Mwishowe akasema; "Baby leo unayo sababu gani ya kuninyima haki yangu ya ndoa? Ni wiki mbili sasa for Christ sake. Unafikiri mimi nitakuwa na furaha kivipi kama unaninyima haki yangu ya ndoa?" Akasema hayo huku akionekana ameghafirika mno!! "Unataka kuniambia furaha yako ni kufanya mapenzi tu? Kwa hiyo bado hujanielewa mwenzako? Nafanya hivi kwa ajili yetu. Kwa ajili ya ndoa yetu na kwa ajili ya kesho yetu. Nilikwambia kabla sijaanza hivi kwamba haya yatakuja kutokea na tukakubaliana hutafanya hivyo na sasa hivi umenigeuka nionekane nina hatia. Seriously mimi unanichanganya!!" Nikamweleza hayo huku nami nikiwa nimekasirika! Victoria, mimi sipingi wewe kufunga na kuomba. Nampenda Mungu pia na ninaenda kanisani lakini hauwezi ukategemea mimi nikae siku 100 bila haki yangu ya ndoa eti kwa vile upo kwenye maombi ya kufunga, hiyo haipo!!" Tony aliongea. Nilikasirika mno baada ya kunieleza hayo, "seriously Tony? Unanitania? Hauwezi kujizuia? Hii inaonesha ni jinsi gani mume wangu umeanguka kiimani. Sio wewe uliyekuwa ukifunga na kuomba na mimi kila mara kabla hatujaoana? Kwahiyo kipindi kile ulikua ukijifanyisha tu! Sio sisi tuliokaa kwenye uchumba miaka miwili bila ya kufanya ngono? Kwaio inamaanisha ulikua unanisaliti? Nini? Unawezaje kusema hayo? Umechanganyikiwa ee? Unaweza vipi kufananisha kipindi kile na sasa hivi? Kipindi kile nilikuwa single sasa hivo nimeoa. Kuna maana gani ya mimi kuoa kama siwezi kupata haki yangu ya ndoa? "Ahaa kwaio mimi ni sex machine? Ulinioa kwa sababu ya sex?" Nilimuuliza. "Unajua nini, siwezi kupoteza muda wangu katika maongezi na wewe yasiyo na tija. Ninakuonya mara ya mwisho. Sitaki kusikia mambo yako ya kufunga na you will learn to respect me katika hii nyumba. Kama huu ndio upuuzi mnaofundishana huko kanisani, nitakuzuia kwenda tena shabàash" "You wont dare Tony, usijaribu nakwambia. Kama ningeambiwa kuchagua wewe na Mungu wangu, wewe ungepoteza. Mungu kwanza wewe unafuata. Huyo shetani anaejaribu kukutumia..hatanikamata na mimi" "Try me Vicky, nijaribu uone Vicky" akaongea huku akielekea bafuni na kufunga mlango. Nikatoka chumbani na kuelekea jikoni nikiwa nimeumia mno moyoni. Nikiwa ninaandaa kifungua kinywa nilikuwa nimejawa na huzuni mno, sikuelewa kwanini Tony alikuwa na hasira juu ya uhusiano wangu na Mungu. Sikutarajia kama mambo kama haya yangetokea ndani ya miezi 6 tu ya ndoa yetu. Anafahamu fika ni jinsi gani ninavyompenda Mungu na ni kiasi gani uhusiano na Mungu una maana kwangu lakini hakuwa akinielewa. Na tuliongea haya wakati wa uchumba na alikuwa akiniambia ni kwa namna gani ananipenda kutokana na nilivyojitoa kumpenda Mungu.Tumejaribu kutafuta mtoto kwa kwa miezi mitano sasa, na hakuna lolote lililotokea. Na ninafahamu fika inanibidi nikazane kumuomba Mungu kabla hiyo miezi mitano bila ya ujauzito isije kuwa miaka 15 bila ya mtoto. Na nikamwambia kabisa nataka kujiunga na maombi ya kufunga ya siku 100. Mwanzoni alikubali kujiunga na mimi kwenye maombi ila baada ya siku tatu akaacha. Sikuhisi amenitenga mimi niliendelea mwenyewe, sikufikiri kama atakuwa mchungu kwangu katika jambo jema kama hili. Baada ya kumaliza kuandaa kifungua kinywa ikiwa ni kama nusu saa tokea tuzozane alitoka chumbani akiwa ameshavaa vizuri suti iliyompendeza na akapitiliza moja kwa moja nje huju akinipita bila kunisemesha lolote. Nikamkimbilia na kumshika mkono, kabla hajaingia kwenye gari yake. " Haujala kifungua kinywa nilichokuandalia" Nikamwambia.. "Nitolee upuuzi wako hapa, kifungua kinywa my foot!! Sitaki chakula chako sasa na mpaka utakapojifunza kuniheshimu kama mume wako na kichwa cha nyumba na pale utakapoona kipi ni cha muhimu kwako" akasema hayo huku akiingia ndani ya gari na kufunga mlango kwa nguvu, akawasha gari na kuondoka haraka, nikasimama pale huku nimepigwa na butwaa. Tumekuwa na kutoelewana juu ya tendo la ndoa wiki ya pili sasa ila sijawahi kumuona Tony akiwa amekasirika kama leo hii. Nilijua kabisa nipo kwenye jaribio kubwa sana la ndoa yangu, nilitakiwa kuomba sana juu ya mume wangu...labda sikujua ni nini natakiwa kufanya kama mke! kwa kweli nilichoka.......... ITAENDELEA... NDOA YANGU EPISODE (2) Baada ya Tony kuondoka, niliazimia hili jambo nilifikishe kwa Mungu wangu kupitia maombi. Niliingia ndani na kuanza kusali. Nilisali kwa takribani masaa mawili nikimlilia Mungu juu ya ndoa yangu. . "Baba nilinde juu ya ndoa yangu, ondoa kila aina ya ushetani unaomnyemelea mume wangu. Mithali 21:1 inasema, "Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa BWANA; Kama mifereji ya maji huugeuza popote aendapo." . Oh Mungu wangu geuza moyo wa mume wangu Tony asipende Sex mpaka siku hizi 100 za kufunga ziishe..Amen. Baada ya sala ya muda mrefu nikajihisi kupata moyo upya na nikapata namna ya kufanya. . Nilikuwa sina sababu yeyote tena ya kuweza kumshawishi Tony asifanye mapenzi na mimi, hivyo nilitakiwa nitumie busara tu kuzuia kwa kufanya mambo ambayo yatamfanya Tony asitamani kufanya tendo la ndoa na mimi. . Hivyo nikaamua nisioge siku nzima. Nilifahamu fika ni jinsi gani Tony alivyokua akipenda kuniona nikiwa naoga na kuwa msafi nikinukia muda wote. . Alirudi nyumbani mishale ya saa moja jioni, nilihakikisha chakula cha usiku nimeshakiandaa. Nilijua tu lazima malumbano yataanza tena. Na kwa kweli sikukosea maana baada tu ya kuingia ndani akaanza; . "Madam, umeshaweka mambo yako sawa?" "Mambo gani Tony?" Njoo ule chakula nilichokuandalia" "Ulifikiri ninakutania? Unafikiri kwa kutokuoga kwako kutasaidia kunibadilisha maamuzi yangu? Au unafikiri mimi ni mpumbavu nisijue kwamba kutokuoga kwako leo ni trick ya kujaribu kunizuia nisishiriki na wewe sex?" . Kwa kweli nilipata mshtuko na kigugumizi nisijue niongee nini baada ya yeye kugundua plan yangu ilikua ni nini. "Tony please naomba unielewe. Natakiwa nijikite kwa Mungu." Nikaanza kumuomba Tony. . . "Vicky, get it straight, mimi sikulazimishi usifunge. Kuna ubaya gani kama tukishiriki tendo kati ya saa kumi na mbili jioni unapofungua funga yako mpaka saa sita usiku unapoanza funga yako tena? Hicho ndicho ninachokuomba Vicky mke wangu." . "Samahani Tony, siamini kama hivyo ndio vizuri zaid. Natakiwa niwe msafi bila kushiriki tendo siku zote 100. Kushiriki tendo katikati ya hizo siku nitajisikia si msafi." Nikamuelezea hayo Tony. . "Upi si usafi katika tendo la ndoa kati ya mume na mke waliohalalishwa? Tunaruhusiwa kabisa!!" . "Nisikilize Tony, unatakiwa uwe mvumilivu. Nimebakiwa na siku 85 tu baada ya hapo tutafanya mpaka mwenyewe uchoke" . "Ngoja nikwambie kitu Vicky, hii ni mara ya mwisho kwangu kuongelea hili suala. Kama umeshindwa namna ya ku-balance ndoa yako na kufunga, basi utakua huna tena hiyo ndoa baada ya kumaliza hizo siku zako 100 za kufunga_ . "Nini unamaanisha Tony? Mungu aingilie kati kuzuia hayo maneno mabaya ya mkosi yatokayo kinywani mwako." . Tony akaniacha nimesimama pale na akaelekea chumbani. Nikapata mshangao baadae usiku pale Tony alipoanza kuhamishia vitu vyake chumba cha kulala wageni. Nilitaka niende nikamuombe asifanye vile lakini baadae nikaamua ni bora akae huko kwa hizo siku 85 zilizobaki. . Labda huu ulikua mpango wa Mungu kunitafutia ufumbuzi. Nikamshukuru Mungu kwa kunipa ile njia ya kukaa chumba tofauti na Tony na hivyo kutosumbuliwa tena juu ya tendo la ndoa. . . Siku ya 60 ya kufunga na kuomba, nikazidi kuchangangikiwa. Furaha na amani ya kufunga na kuomba ikapotea. Tony na mimi tukawa kama wageni ndani ya nyumba. . Hakula chakula nilichompikia kwa takribani wiki 6 sasa, nikajawa na hofu na uoga. Akawa ameanza kurudi nyumbani kwa kuchelewa na tukawa hatuongei tena. Kila nilipojaribu kumuongelesha aliniambia nifunge mdomo wangu hataki kunisikia. . Wote tulikuwa tukienda kazini na kurudi nyumbani lakini kila mtu alielekea chumbani kwake. Nilikuwa sijui hata nianzie wapi. Nilifahamu fika hakuna jambo baya nililolifanya, nilichokua nafanya ni chema kwa ajili ya ndoa yetu na nikashangaa kwanini Tony halioni hilo. . . Siku moja jioni nikiwa nimetangulia kufika nyumbani mida ya saa moja usiku nilipata text toka kwa Tony iliyoniumiza sana, text hiyo ilisema "Usinisubiri mimi, sitarudi nyumbani leo" Sikuamini macho yangu, na haraka haraka nikamjibu text iliyosema "Uko wapi? Kwanini hutarudi nyumbani?" . je umependa simulizi hii na una taka mwendelezo tutumie messege apa kwa heriiiiiiiii . Jibu lake lilinifanya nilie kilio kikubwa na uchungu mwingi.....oh ndoa yangu, masikini mimi kumbe sikujua!!!!... ITAENDELEA...

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA

Mpya zaidi Nzee zaidi

Ads related

Smartwatchs