❣️
1-----5
ONLY YOU I LOVE 01
Ilikua majira ya sa 12 jioni ambapo Msichana ambae alifahamika kwa jina la clara alikua amekaa chini ya mti uliombele ya nyumba yao akiwa ameshika tama akiwa mwneye huzuni sana ,haijulikani kichwani kwake alikua anawaza nini lakini kwa kumtazama utagundua kua yupo mbali sana kimawazo.
"clara..! clara..!"
clara alishtuka na kumtazama nani anamuita ,alipogeuka akasimama na kuzungumza
"mama kuna nini mbona umenishtua sana..?"
"clara nashangaa umekua mtu wa mawazo sana sijajua chanzo na sababu ya wewe kua na mawazo kiasi hiki"
"aah mama unajua siko sawaa kweli lakini....!"
"basi inatosha sasa sitaki uzungumze kitu ,ila nilitaka kukupatia simu yako ilikua ikiita"
"ah asante sana mama napenda jinsi unavyonipenda na kunijari binti yako"
"usijar mwanangu,ila ukimaliza kuzungumza na simu uje ndani hapo nnje giza lishaanza kuingia"
"sawaa mama"
mama yake clara aliingia ndani na kumwacha clara akitazama simu yake nani alikua anampigia,na baada ya kukagua vizuri alikua namba ngeni ,akawa anajihuliza sana nani atakua anapiga,akaona ajaribu kupiga yeye,simu iliita lakini haikupokelewa,akaachana nayo na kuingia ndani,akamkuta mama yake amemaliza kupika anatazama television, clara alikaa kwenye sofa na kuzungumza
"mama hali hii itakua hivi hadi lini?"
"clara tumekubariana kua maombi ndio nguzo yetu pekee sasa kwanini unaonekan kukata tamaa haraka sana kiasi hiko?"
"sawaa mama nitajitahidi kuvumilia ila nime...."
alitaka kuzungumza lakini mama yake akamwambia
"kwanza ninani ambae alikupigia simu?"
"sijui mama maana imekuja namba ngeni na nilipojaribu kupiga haijapokelewa"
"ooh labda atakua amekosea namba haya sasa kaoge ili uje kula upumzike"
clara aliingia chumbani kwake akajiandaa na kuingia bafuni kwaajiri ya kuoga.
alipomaliza na kurudi chumbani kwake alikaa kitandani kwa muda hadi akapitiwa na usingizi,mama yake alisubiri sana hadi akaona aende kumtazama atakua anafanya nini na kimya cha mda wote huo,alipoingia chumbani, akamkuta tayari clara amelala tena hajitambui kabisa,alimtazama binti na kuvuta shuka na kumfunika vizuri kisha akasema
"najua binti yangu unawaza mambo mengi sana kuhusu kaka yako lakini huna jinsi lazima uvumilie hili ,hata mimi naumia sana sababu sijui atakua na hali gani huko alipo ila najua kua Mungu anaturinda si viumbe vyake sehemu yoyote ile tunapokua hata kijana wangu atamrinda, christian ,mdogo wako anawasiwasi sana na wewe tunakusubiri tena na tunaimani kua utarudi tu baba"
mama clara alizungumza hivyo kwa uchungu sana kisha akavua machozi yake na kum'busu clara na kutoka chumbani kwa mwanae hata yeye hakujiskia kabisa kula chakula akaamua kuingia chumbani kwake kujipumzisha pia.
asubuhi mapema mama clara aliamka na kufanya usafi ndani kote kama ilivyokawaida yake ,sababu ni mama ambaye anayajua vema majukumu yake alikua anapenda sana kujituma kufanya kazi zake mwenyewe tangu alipokua msichana hadi alipopata watoto wake hao hadi wemekua bado hakuacha asili yake ya kufanya kazi tofauti tofauti za nyumbani kwake.
Alipomaliza kufanya usafi akataka kuingia bafuni aweze kuoga na kwenda kwenye biashara zake mara simu ya clara ilianza kuita ikiwa pale seblen mama huyo alisogea kwenye sofa na kuchukua simu hiyo na kumpelekea Clara..
"clara...! amka simu yako hii"
Clara aliamka na kuanza kuongea na simu wakati huo mama yake alitoka chumbani kwake lakini ghafla alisikia kelele chumbani kwa clara kelele ambazo zilimfanya ashtuke pia na kutaka kurudi tena chumbani kwa clara lakini kwa bahati clara mwenyewe alifungua mlango na kumkumbatia mama yake kwa nguvu sana huku akilia mama yake akamuhuliza
"clara unalia nini kuna kitu kibaya kimetokea?"
"mama nafuraha sana uwezi amini yaani simu hii ya asubuhi imenifanya niwe na furaha kupitiliza"
"ni kuhusu christian ama..!?"
baada ya mama yake kumuhuliza hivyo clara aliishiwa pozi na kukaa kwenye sofa kinyonge kisha kuzungumza
True love simulizi 💚💙💜
GREEN HACKER
0
Chapisha Maoni
TOA MAONI YAKO HAPA