simulizi:hatma yangu
mwandishi:mwandishi wa google
SEHEMU YA :01
Kwa majina naitwa Khadija Ally ni mtoto wa tatu na wamwisho katika familia yangu.,nimetokea katika familia duni sana ambayo ilisimamiwa na baba tu🥺mamaangu alifariki 😭pindi tu aliponizaa jambo lililopelekea kuchukiwa zaidi na familia yangu kwa kisingizio kua mimi ni nuksi nilie muua mama yangu 🥺🥹
Baada ya kufariki kwa mama yangu hakuna ndugu yeyote si kwa baba wala mama alie kua tayari kusimamia malezi yangu.,wote hawakunipenda na wengine kuthubutu kuniita mtoto wa laana hivyo hawakutaka niwaharibie maisha yao.
Babaangu mzee Ally pamoja na kakaangu na dadaangu wao ndio waliowajibika katika kunilea licha ya kutokua na uwezo wa kunihudumia..kwa kipindi hiko babaangu aliachishwa kazi shambani kwa kusingiziwa kua laana ya mtoto anae mlea inapelekea mazao yao kuto nawiri vizuri.
Babaangu alionekana ni mtu alie kata tamaa mno.,hii ni kutokana na uzee alio nao na umaskini uliompelekea kutokuweza kuisimamia familia yake.
Kakaangu Mudrik na dadaangu maryam kwa kipindi hiko walikua kidato cha 2 na walilazimika kuachana na masomo kutokana na baba kushindwa kuwatimizia mahitaji yao.
Miaka ilipita hatimae nilifikisha umri wa miaka 7.,
Siku isio sahaulika kwangu ni hii..😭😭
Ilikua ni jumaamosi yenye mvua kali mno, ambapo babaangu alizidiwa na maradhi yake. Kwavile hatukua na uwezo wowote wa fedha tulikimbilia kwa majomba na mashangazi kwakua wao walikua na uwezo wa kifedha,kusudi watusaidie alau elfu moja ya kumnunulia panadoo baba yetu, lakini bahati haikua yetu.kote tulipoenda tuliishia kufukuzwa kama mbwa😭babayetu aliugua mno na hatimae aliiaga dunia😭😭😭
Mimi pamoja na dada tulilia mno 😭😭 tulikosa tumaini la kuishi. Hatukua na mtu yoyote mwengine tuliemtegemea kututetea katika dunia., sio mama wadogo wala mashangazi.,wote hawakutupenda wala kutamani kutuona😞
Tulimzika baba yetu kwa usaidizi wa wana kijiji wachache., hakukua na mtu yoyote wa familia alie jumuika nasisi.
Kilichowashangaza wengi ni baada tu ya kumzika baba,alikuja shangazi pamoja na mumewe na kutuamuru tuondoke katika nyumba yetu🥺kwa madai kua hio haikua ni mali ya babaetu bali ilikua ni urithi wao.,ila walimuachia kwakua babaetu yeye ndo alikua mwenye uwezo duni kwa upa nde wao ndo waliamua kumpatia kama msaada.hivyo kwakua baba hayupo tena basi wao hawana msaada nasisi.,walitutaka tuondoke mda huo huo.
Tulilia mnoo..kaka mudrik aliwaomba sana watuachie japo mwezi mmoja angeweza kujua wapi tutaelekea, lakini hawakukubaliana nasie hata kidogo.
Tuliwaomba na kuwaomba mwishowe wakasema kua wangekua tayari kumchukua dada mariam na kaka mudrik kuwalea,ila sio mimi,mimi ni laana inayotafuna familia yao😭😭kakaangu alikataa kata kata ila dadaangu maryam alikubali kuondoka nao nasisi tukafukuzwa😭
Usiku huo huo tuliondoka na kakaangu tusijue wapi tunaelekea😭 tulifika stendi ya magari tukiwa hatuna hili wale lile😞dunia ilitugeuka😭 kaka alinikumbatia na kuniambia.,dija mdogo wangu nisamehe🥺nakufanya upitie magumu ilhali upo katika umri mdogo😭nisamehe kwa kushindwa kua kaka bora..ila naahidi kukusimamia😭mimi nitakua mzazi wako wa pili baada ya baba kuondoka.wewe ni jukumu langu..nitakutunza na kukusimamia hata kwa kidogo nitakacho kipata😞
Nililia mnoo.,kiukweli nilikua mdogo sana, sikustahiki yote haya, nilimlaumu Mungu kwa kuwachukua wazazi wangu mapema kabla mtoto wao sijaweza kupambana😞
Tulikusanya maboksi na kuyaeka kua ni kitanda Chetu kwa usiku huo,huku tukiwa hatuna matumaini na kesho yetu😞
Itaendelea....
SIMULIZI:❤🩹HATMA YANGU 🫴🏼😚
SEHEMU:03.
Siku zilipita,na kama baba alivyoniambia, nilianza shule ile ile ambayo Naila na Naima walikua wanasoma.,japo ilikua ngumu kwa vile sikuwahi pata fursa hii tangu nilipokua mdogo kabisa., ila nilijitahidi mno na kadri siku zilivyozidi niliweza., huku baba akinitafutia mwalimu wa ziada ambae alikua akinifundisha nyumbani.Nilisoma mpaka nikafikia kidato cha Nne nikiwa miongoni mwa wanafunzi bora shuleni.
Siku moja shule iliandaa ziara ya masomo ambayo ilitakiwa kila mwanafunzi alipie elfu 30. Kiukweli baba hakua na hiana,hakuwahi nibagua, alinipenda kama anavyo wapenda binti zake,ila tatizo lilikua kwa mama😞 yeye hakuwahi kunipenda hata kidogo,licha ya nyumba kua na wafanyakazi ila alinitumikisha zaidi ya hao wafanya kazi.,kila ilipotokea Baba kusafiri kwa ajili ya biashara zake,mama alinitesa sana, hakunipa chakula, hakutaka nilale na watoto wake, hakutamani hata siku moja kuniona naishi maisha ya raha. Hata wakati wa ziara hii baba hakuwepo hivyo alimuagiza mama atulipie mahitaji yetu yote.
Mama aliwalipia wanawe tu wala hakunilipia mimi😞 na hata wanawe walivyouliza kwanini mimi sikulipiwa aliwadanganya kua siku hio nitatakiwa hukudhuria sehemu ambayo ni muhimu kwangu kuliko hio safari😞
Nilijihisi mnyonge sana,nilitamani hata kumwambia baba ila nilimuogopa mama🥹alinitisha na kunambia ikitokea nikamletea matatizo na mumewe hakika angeniua😭
Siku ya ziara ilifika,Naila na Naima walisikitika kwamba sitakua pamoja nao,ila waliniahidi kua watakuja kunisimulia kila kitu watakaporudi, nilikubali japo kiunyonge mno kwakua nilihitaji nami kuongozana nao🥺
Baaya ya wao kuondoka tu mama alinitumikisha kama punda., nilipika nikadeki,nikafua manguo mengii,kila nilipomaliza kazi moja mama alinitafutia nyengine.
Nilichoka sana hio siku😞hadi inafika usiku sikua nimeingiza chochote tumboni mwangu🥹 na hata nilipoelekea jikoni nilikutana na vyombo vilivyonizomea tu,kila nilipofunua kuliniskitikia kwa huruma😞
Nilipomuuliza mama alinijibu kua chakula chote aliwapa mbwa wake na chengine alimwaga😞Nyieeee nililala njaaa🥺yani hata usingizi wangu ulikua watabu.,tumbo lilinilaumu kwa kutokulipa haki yake,nilijikuta tu nikimkumbuka kakaangu Mudrik ambae alinisimamia katika maisha ya shida ila hakuwahi kuninyanyasa😭nilimkumbuka dada maryam nae alietuacha kisa shida tu😭 na kwa miaka yote hio sikua naelewa dadaangu maisha gani aliokua anayaishi japo waliomchukua walikua ni watu wenye uwezo wa juu mno😞niliwaza na kuwaza hatimae usingizi ukanihurumia.,nililala.
Itaendelea..
SIMULIZI:❤🩹HATMA YANGU🫴🏼😚
SEHEMU:04.
Nilikuja kushtuka asubuhi nahii ni kutokana na Naila pamoja na Naima kunisumbua kwa kelele zao wakinitaka niamke. Nilivyoamka tu nikagongana uso na Naila ambae kusudi lake lilikua ni kunivuta ili niamka. Sis!!What's wrong with you anh? Naila aliniuliza baada ya kukutana na sura yangu iliovimba baada ya kulia sana usiku uliopita. Hamna kitu bana, embu sogea bas mnipe habari za safari.,nilimpotezea mada ili asizidi kunihoji juu ya masaibu yaliyonipata😞
Hapo sasa Naima alianza kunipa mkasa mzima juu ya mambo waliyokutana nayo.,nikajikuta tu nafurahi kwa ile namna aliyo itumia kunihadithia japo nilihuzunika kwa kutokuwepo huko.
Naima ni binti mmoja mcheshi sana na asie choka kuongea, huyu tunaweza kumuita mtambo nanusu😂marazote shuleni alikua hakosekani katika kesi mbali mbali..,ikija ya kupigana ni yeye,ikija ya kuto andika ni yeye., ikija ya wanao lala darasani ni yeye😂 Yani Naima alikua ni binti flani ivi mwenye kupenda uhuru wake asie penda kupelekeshwa hata kidogo.
Mara nyingi alithubutu kumkemea mamayake pale alipo ninyanyasa mbele yake.,Kinyume na Naila, yeye alikua ni binti mpole mnoo asie weza tafrani hata kidogo., mara nyingi alimshtakia Naima kila aliemuudhi, na Naima angemalizana nae kwa njia yake mwenyewe😂
Haya bana tuliachana na stori tukaenda kujiandaa kwenda kumpokea baba ambae alikua akirejea nchini siku hio🥰
Baba alirudi,alifurahi kutuona bado wazima,nasi tukafurahi kwa kurejea kwake maana ni takriban miezi minne hakuwepo, tulimmiss mnoo🤗 baba alitupatia kila mmoja zawadi aliomletea na kutuaga kwa ajili ya kwenda kupumzika sasa baada ya machofu ya safari,mama nae aliongozana nae na sebleni tukabaki mimi na kila Naima
Tukimalizia movie tuliokua tukiitizama .
Asubuhi na mapema tukiamkia shuleni.,na zilibaki wiki chache tu kufika mtihani wetu wa taifa (NECTA)., Hivyo kila mwanafunzi alikua busy kujisomea kwa ajili ya kilichotukabili mbeleni.
Siku hio wakati nilipokua nikijisomea library alikuja mwanafunzi mmoja ambae hapo shuleni hakua na mazoea sana na wanafunzi.,yeye aliishi kivyake sana labda ni kutokana na uwezo wa kwao.
Aliniomba kuketi nami kwa lengo la kusolve questions kwa pamoja.,sikua na hiana nilijumuika nae.,na baada ya muda wa shule kuisha tuliagana nami nikafatana na kina Naila kurudi Nyumbani.
Siku zilienda na hatimae tulifanya mitihani yetu salama kabisa, ila siku ya mtihani wa mwisho sasa, wakati tukiwa katika chumba cha Mtihani Neila alianza kutapika mno🥹,alitapika na kutapika jambo lililopelekea kutomaliza mtihani wake💔.,walimu walimchukua na kumpeleka katika hospitali iliokaribu na shule yetu.
Baada ya kumaliza mtihan tuu, tulikimbilia hospital kwalengo la kutambua hali ya Naila..Maskini Naila🥹vipimo vilionesha kua yeye ni mja mzito💔 taarifa hizi zilimshtua kila mmoja,Naila alikua binti mpole na mtiifu mno🥹 tuliwashauri madaktari Warudie tena na tena kumpima tukiamini majibu hayakua sawa..ila waapi🥹majibu yalionesha kua ni yale yale.
Jambo kubwa zaidi lililomsikitisha kila mmoja ni baba😭mzee Mohammed baada ya kupata taarifa za mwanawe hakuvumilia😭 presha ilimpanda na kabla ya kupatiwa huduma yeyote baba nae roho ikaacha mwili😭😭😭 hili ni pigo jengine ambalo sikulitarajia litakua karibu hivi😭Nililia mnooo kiasi ambacho hata ukiambiwa nnae mlilia sina hata undugu nae huamini😭😭 Nililalama kwa uchungu mnoo,nikijiuliza hivi kweli mimi ni mtu mwenye laana,,kila ninapopata nguzo ya kuegemea inanianguka ghafla..nilijiuliza dhambi gani niliotenda niitubie ili Mungu aache kunipokonya wapendwa wangu😭Nililia mnoo maana kila msiba ulinikumbusha msiba wa nyuma😭.
Baada ya kustiriwa kwa mwili wa baba sasa🥹maisha yalinigeukia mimi..mama aliidhihirishia dunia chuki yake juu yangu🥹alinitukana na kunipiga mpaka nikakosa nguvu ya kulia nikaishia kunyamaza tu huku roho ikinyongea mithili ya nyuki anapopoteza mwiba wake.Mama hakutaka tena kuniona nyumbani kwake.,Alinifukuza na hakunipatia kitu chochote,si nguo,simu nilio imiliki ambayo baba alinipatia kama zawadi., mama hakunipa chochote, nililia na kulia nikimuomba anihurumie akaniambia nikaitafute huruma kaburini kwa mamaangu🥹 Nyiee😭
Naima alimzuia mama lakini alimuambia kua angemfukuza nayeye ikiwa atamjibiza🥹sikulitamani hilo kwa Naima.,Nilimuomba abaki kumuangalia Naila.,Nilimuahidi kua nitakua sawa tu.Ivi ushawahi kusema upo sawa kipindi unahitaji kila kitu?? Ushawahi kupitia magumu mpaka ukadhani waliokufa Mungu kawahurumia??
Haya maisha bana🥹hayajawahi kua muaminifu kwa yoyote.,
Niliondoka nyumbani nisijue wapi nitakapo elekea wala hatma ya yote hayo ni nini.
Itaendelea...
SIMULIZI:❤🩹HATMA YANGU 🫴🏼😚
SEHEMU:05
Baada ya mama kunifukuza nyumbani kwake nilipoteza matumaini.,nikaacha kuamini kesho yangu inayomilikiwa na Mungu. Nilitembea kama kifaranga aliekosa umakini wa mamaake🥹niliranda nyumba hadi nyumba nikiomba tu kua wanaweza kunipatia japo kazi itakayonisaidia kuendelea na maisha katika mji huo ulioonekana kutonihurumia.
Niliranda na kuranda bila mafanikio🥹 usiku ulinifikia nikiwa stendi ya magari nisijue niendako wala hatma yake ni nini🥹 nilitafuta sehemu nikakaa na kujiinamia🥹 moyo wangu ni kana kwamba ulikua ukinidhihaki,niliusikia ukisema"maskini khadija., binti mwenye laana,umemuondoa mamaako.,hukuridhika ukamuondoa na babaako,wala hukukomea hapo tu, ukamchukua na mudrik kijana alie jitoa kwa ajili yako, na vipi kwa mzee Mohammed??hata baada ya kukuonesha maana halisi ya mzazi wewe ulimpatia nini??ukamuua khadijaaa😭
Nyie nililia mnoo😭 nilijihisi mkosa sana,nilijiona mtu nisie na shukrani kwa kuwanyea mkono walio amua kunishika🥹Nililia na kulia wala sikuelewa ni wakati gani usingizi uliponihirumia😞
Nilikuja kushtuka na sauti ya kiume iliokua ikiniamsha, dada!dada! Nilishtuka nikaona mvulana ambae mavazi yake yalitosha kunithibitishia kua yeye ni mlinzi katika eneo lile. Aliniamsha na kuniambia kua eneo lile halikua kwa ajili ya kulalia hivyo akaniomba niondoke🥹
Kinyonge kabisa niliinuka na kujikukuta na kuianza upya safari yangu iliokosa muelekeo.Nilizunguka mno kwaajili ya kupata kazi hatimae Mungu akasimama kwa upande huu,baada ya kufika katika nyumba moja ya kifahari na kupokelewa na wenye nyumba hio kama mfanyakazi. Katika nyumba hii nilikutana na familia ya watoto wawili,mmoja wa kiume na mwengine wakike.Pamoja na mama yao ambae alijitambulisha kwangu kama Madam Elizabeth.,nilifahamishwa majukumu ambayo ningetakiwa kuyatimiza kila siku pamoja na sehemu niliotakiwa kulala baada ya kumaliza kazi zangu.,kusema ukweli sehemu niliopatiwa ilikua duni mno..Waweza sema labda awali walikua wakihifadhia mifugo yao humo,hichi kilikua ni chumba kilichokuwepo ndani ya kuta la jumba hilo, sikua na jinsi,mana kwa uwezo wangu nisinge miliki hata kile.
Nilianza kazi vizuri na kwa jitihada ya hali ya juu,mana Madam Eliza alioneoana dhahir kabisa kua ni mmama asiejua maana halisi ya upole, kwake mfanyakazi sio kitu.
Nilifanya kazi usiku na mchana,niliendelea kua mtiifu kwa mwenye nyumba ili tu nisijepoteza kibarua.
Miezi ilipita hatimae matokeo yetu yaliyoka na nilifaulu vizuri tu,ila uwezo wa kurudi skuli sikua nao tena 🥹niliskitika mno,
Nisingekua na kitu cha kunitetea zaidi ya elimu yangu🥹ila ndo hivyo,Ng'ombe wa maskini hazai.
John!John!John!! Aliskima Madam Eliza akimuita mwanae kwa jazba sana,.
John alipofika aliuliza mom,kuna nini hadi upige mazogo hivyo. Madam alimuambia unathubutu kuniuliza eenh!? John umepata wapi ujasiri wa kutoa pesa kiasi chote hicho??, sawa umetoa pesa,unaweza nambia umefanyia nini??
Mom unajua kua jana ilikua ni birthday ya rafiki yangu, so nilitaka ajihisi special, please Mom, usinigombeze.Madam Eliza alionekana kuridhika na maelezo ya mwanae, ila alimuambia tu Next time uwe unanipa taarifa.
John alisema..mom,Million moja tu pia natakiwa kukupa taarifa!,. Nilishtukaa, jamani millioni nzima ni birthday tuu😲 mbona me nikiipata hio nitatajika kama bakhresa kw ntakavofanya biashara!?
Ugomvi wa mama na mtoto uliishia hapo., nikawatengea chakula mezani,baada ya hapo nikaelekea jikoni kusudi nisubiri wamalize nikasafishe meza. Nikiwa nimekaa nimejiinamia sina lile wala hili nikaskia sauti ikiniita Dee! Nilipogeuka nilikutana na sura ya John, nikamwambia samahani..,kuna kitu unahitaji labda?, akanambia ndio.,nikainuka kwa ajili ya kumsikiliza mtoto wa boss.
Aliniambia nnachokihitaji ni mimi kula na wewe now,nilishtukaa mana haikua kawaida yangu,mie nilikua kile ambacho wao wao waliacha, ila Leo nakula kilichopakuliwa., tena na mtoto wa boss, wee kuwezaa😂😂
Sikua na hiana,ukizingatia kwanza nilikua na njaa ndo mamaa nikajikuta nakubali mbio mbio, nikamwambia sawa tunawezaa kukaa hapa basi.John alioneshwa kushangaa sana, akaniuliza kwa mshangao Are you serious Dee?? Nile hapa?? Kwamba nyumba imejaa?
Nilijikuta nikiinamisha kichwa tu maana kwangu sehemu hio ndo ilikua mazoea yangu na ndo mipaka yangu, Madam Eliza alishanikataza kusogea mezani wakati akiwepo na familia yake.Me nilikaa kimya tu John alisema nifuate, nikamfata kwa woga nikizingatia kua kuna mipaka sikutakiwa kuivuka.
Mwendo wake uliishia nyuma ya Nyumba ambapo kulikua na bustani iliopendeza mno, ambayo kwa mandhar yake ilionekana kua na uwezo wa kumhurumia yeyote atakae iendea kwa huzuni.
Tulikaa hapo na John alieshikilia trey iliobeba sahani moja ya chakula na glass mbili za juice ya matunda., tulikula..japo mwanzoni nilionekana kua na hofu kutokana tangia nimefika hapo sikuwahi kuzoeana na John..hio ni kutokana na kazi zake,Sikuelewa kazi halisi aliokua akiifanya ila mda mwingi hakuonekana Nyumbani.
John alitaman kujua historia yangu.,hakujua tu.lau kama angelifaham kua swali lake lilikua ni sawa na kukivalia nguo kidonda cha moto🥹
Nilimhadithia mengi kuhusu mimi,ila sikumuambia kua mimi ni mtoto wa laana🥹niliogopa asije akamwambia mamaake nae akanifanyia kama niliofanyiwa na Bi Maimuna. John alionekana kusikitishwa sana🥹 alinipa pole wakati huo machozi hayakuamua kunihifadhi,yalichofanya ni kuniadhirisha tu🥹 John alisogea karibu yangu na kunipa kumbato la pole, na akaniambia kua ipo siku nitasahau yote hayo,niliitika tu japo niliamini kua hatma yangu ilishachaguliwa tangu siku niliomsababishia kifo mamaangu.
John alikua ni mtoto wa kwanza wa Madam Eliza,kwa kukisia labda kwa wakati huo angefikia miaka 25 ama 26, yeye alikua ni kijana mstaarabu sana,licha ya uhandsome aliobarikiwa,roho yake nzuri ilijitosheleza kumuaminisha yoyote kua yeye ni sehemu salama kabisa😚
Kadri siku zilivyoenda ndivyo ukaribu wangu na John uliongezeka, asingeenda kazini bila ya kunijulia hali, wala asingerudi bila ya kunibebea chochote mkononi.,kidogo kidogo nikajikuta naanza kua huru na maisha.,kidogo kidogo nikaanza kujiona muhimu kwa baadhi ya watu.,
Siku Moja wakati nimelala Niliota ndoto ilionitisha sana..,Niliota mzee Mohammed ananililia,ananiuliza licha ya wema wote alionitendea ndo nimeshindwa hata kuuaga mwili wake, aliniambia hujui kua Naila na Naima wanataman uwepo wako, hujui.. kabla ya kumalizia Niliskia sauti ya Madam Eliza ikiniita kwa jazba Khadijaaaaaaaaa😡
Itaendelea...
Chapisha Maoni
TOA MAONI YAKO HAPA