Maiti iliyogoma kupumzika kwa amani 😭😭🙏

MAITI ILIYOGOMA KUPUMZIKA KWA AMANI 😭🙏01 Katika maisha yangu nimekumbana na mikasa mingi lakini huu wa kuuwawa kichawi na wakwe zangu kwa kunigeuza msukule huko Gambosh hakika sitokaa nisahau😭 Ilikuwa ni mwaka 2019 ambapo tulikutana na mpenzi wangu Cosmas jijini Dar es Salam. Cos alionyesha hisia zake kwangu na kunitamkia kwamba ananipenda niwe mpenzi wake ikibidi tufunge mpaka ndoa. "Ni kweli Cos, sikatai kwamba unanipenda lakini vijana wengi wa hapa Dar es salam ni waongo sana, akikutaka anakuja kwa unyenyekevu lakini akishapata kile anachokitaka hutamuona tena, mwenzio mpaka leo nawaogopa vijana wa hapa Dar maana nishaumizwa sana. " Nilimuambia Cosmas. "Usiseme hivyo Tunu binadamu hatufanani na tunatofautiana kitabia, sio wote tuna tabia hizo za kuchezea watoto wa watu. Mimi kweli nataka kukuoa naomba unipe nafasi hii dhahabu, sitaki kukukosa Tunu, na nina imani utaenjoy sana kuwa na mimi" Aliniambia Cosmas. "Mh naomba muda nifikirie maana jambo hili halohitaji kufanya maamuzi ya kukurupuka🤔" Nilimwambia lakini moyoni mwangu nilishamkubalia hivyo nilitaka nipate muda kidogo wa kumchunguza kabla sijamjibu kwamba nimemkubalia. Basi siku zilizidi kuyeyuka kama siagi kikaangoni huku Cosmas akiendelea kunihubiria kila kukicha kwamba ananipenda. Alionyesha moyo huo wa kunipenda kwa kunisaidia katika shida ndogondogo na wakati mwingi alikuwa akinibebea vijizawadi kila tunapokuta. Penzi likapamba moto🔥 na kung'ara kama dhahabu inayopitishwa kwenye moto, nilikiwa silali bila kusikia sauti ya Cosmas😒 na ikipita siku sijamtia machoni basi mwenze nakosa raha na kunyong'onyea kama mgonjwa wa homa. Sikuficha upendo wangu kwake niliwaeleza hadi wazazi wangu kuhusu Cosmas, wazazi walinisisitiza nimshawishi Cosmas kwamba kama kweli ananipenda anioe kwani vijana wengi wa mjini wana kasumba akishakujaza upepo tumboni😃 anakukimbia kama vile kakutana na simba msituni😁. Nilipomueleza Cos suala nzima la kufunga ndoa, hakuweka pingamizi, alienda kuonana na wazazi wangu huko Moshi Mkoani kilimanjaro. hatimaye niliosheshwa kwa Cos na tulifanya harusi ndogo tu nyumbani kwetu kutokana na kwamba hatukuwa na uwezo mkubwa kivile. Basi baada ya harusi nilikabidhiwa kwa Cos na ndipo tulipoianza safari ya kuelekea huko Gamboshi wilayani bariadi nyumbani kwako Cosmas. Niling'ang'ania kusindikizwa hata na ndugu zangu wawili lakini mfuko wa mume wangu haukuwa vizuri kutokana na nauli ya kuwapeleka na kuwarudisha, hivyo tulipanga tutakuja kuwachukua siku nyingine mambo yakikaa sawa🥱. Jamani nyie kuolewa hakutawi utumie pupa kwanza unatakiwa uchunguze sehemu unapoenda kuolewa, familia yao ikoje sasa mimi kilichoniponza nilimchunguza Cosmas peke yake na nilipojiridhisha naye niliamua anioe bila kujua huko Gamboshi ninapopelekwa ni makao makuu ya wachawi😳. Basi bwana tulifika Gambosh, nilipokelewa na wakwe zangu pamoja na mawifi kwa chereko, vigelegele na vifijo. lakini jamboa la kwamba lililoanza kunishangaza hapo ukweni kwangu kulikuwa na paka wengi wasio na idadi kama vile wanafuga😳 yani ungefanikiwa kuwaona ni mfano wa mtu mwenye mradi wa kuku. "Mh sasa hawa paka wote ni wa kazi gani" Nilijiuliza na nikataka kuuliza lakini rohoni nikasita kwa uoga. Maisha ya ukweni yalianza, kweli wakwe zangu walikuwa wananipenda, na hatimaye nikabeba ujauzito ambao nilidumu nao kwa miezi tisa, nikiwa huko huko Gambosh. Siku siku nilijifungua mtoto wa kike lakini ajabu 😳kila mmoja alionekana ana huzuni hata mume wangu ambaye alikuwa akifurahia kipindi cha ujauzito wangu, alihuzunika baada ya mimi kijifungua mtoto wa kike. "Mume wangu mbona sielewi kuna nini, naona hali ya sintofahamu mara vikao vya siri bila kushirikishwa kuna nini?" Nilimuuliza Cos mume wangu siku hiyo ya kwanza kujifungua. "Aah we kuwa na amani bwana kwani shida nini" aliniambia Cos, basi nikaufunga mdomo wangu na kukaa kimya. Basi kama ilivyo kawaida mzazi akijifungua lazima achinjiwe kuku anywe supu, na mimi nikawa nasubiri supu hiyo iandaliwe nikiwa chumbani. Sasa bwana sijui ni kitu gani kiliniambia nitoke nje nizunguke nyuma ya nyumba nikakojoe baada kubanwa na mkojo. Nilipotoka nilizunguka nyuma ya nyumba. Hamadi nikashangaa😳 kumkuta kijana mdogo mdogo wa hapo nyumbani akiwa amejifunga kaniki kichwani kama vile kilemba, mkononi mwake alishika kisu kilicholoa damu, nikasogea mpaka kwenye ndoo iliyokuwa mbele yake na kuchungulia ndani ya ndoo. Moyo ulilipuka paaa mithili ya ukuni mkavu huku mshangao ukizidi kunitoka😳 baada ya kuona paka mweusi aliyechinjwa kichwa akiwa ndani ya ndoo nili.......... Jamani acheni nirudi kwanza🏃 maana kila nikikumbuka machozi yananitoka. Ngoja nifute machozi kwanza nije niendeleze au mnasemaje MAITI ILIYOGOMA KUPUMZIKA KWA AMANI 😭🙏02 Nikiwa nimekaa ndani namnyonyesha mtoto wangu mchanga niliyemza, nikabanwa na haja ndogo, basi nikamuweka mtoto pembeni na kutoka nje nikajisaidie. Kusema kweli huko Gambosh ukweni kwangu nilipokuwa njmeolewa hapakuwa na choo, watu walienda kujisaidia vichakani, lakini kwakuwa mimi ilikuwa ni haja ndogo nikazunguka nyuma ya nyumba ili nijisaidie haraka nirudi ndani. Ile nafika nyuma ya nyumba nikashtuka kidogo😳 baada ya kumkuta kijana mdogo wa hapo nyumbani ambaye alikuwa ni shemeji yangu akiwa amejifunga kaniki kichwani huku mkononi mwake akiwa ameshika kisu kilicholoa damu, moja kwa moja nikajua anachinja kuku kwa ajili yangu kwani ndiyo desturi iliyopo vijijini mzazi akijifungua lazima achinjiwe kuku anywe supu😋. Lakini kiherehere changu kikanisogeza mpaka karibu yake, nikachungulia ndani ya ndoo iliyokuwa mbele yake, nilishtuka😳 baada ya kuona paka mweusi akiwa amechinjwa huku kichwa kikiwa kimetenganishwa na kiwiwilili. Nikamuuliza, "shemeji Bashite (jina la kisukuma lenye maana ya mbishi/mtata) sasa mbona unachinja paka badala ya kuku😳, si nimesikia mnachinja kuku?" Nilimuuliza Bashite. "Ah huyu paka ni kwa ajili ya kutengeneza dawa ya viguma kwa watoto kuna watu wametoa oda ndip tunawatengenezea" alijibu shem, Bashite. "Mh lakini sasa mbona umemuweka kwenye ndoo ya maji ya kunywa🤔, yani hukustaili hata kumuweka kwenye ndoo ya chooni?" Nilimuuliza huku nikiwa mkali kidogo kupinga uchafu ule. "Cecy mambo mengine hayakuhusu usiingilie kazi umesikia kwamba hii ndoo haitaoshwa au basi unaongea kwa sauti ili majirani wajue kwamba wewe ni msafi, haya endelea kubweka sio muda utapata tunzo yako ya usafi😏" Alisema Shem Bashite kisha akaitwaa ndoo kwa hasira na kuipeleka jikoni walipokuwa mama mkwe na mawifi zangu kina Kashinje na Kabula. Nikabaki nimeganda kwa mshangao😳 huku nikiwa nimesimama najiuliza maswali kadha wa kashaa kichwani mwangu. "Mh huu si uchafu huu, wasije wakaenda kumchuna ngozi huyo paka wao kwenye sufuria kubwa za kupikia maana hawa kwa uchafu ni kama nzi wa kijani na kinyes ptuuu" Niliongea na kutema mate pembeni kwani niliwajua vizuri wake zangu walikuwa ni wachafu wa kutupwa. Nikawafuata mule jikoni ili nijue wachokifanya, ile naingia jikoni😳 niilishangaa kweli wamemaliza kumchuna yule paka ngozi, na sasa walikuwa wanampasua katikati na kusafisha matumbo huku wakirushia nyama kwenye sufuria iliyoinjikwa jikoni ambayo tulitumia kupikia ugali siku zote. "Heee jamani nini hiki😳" Niliuliza kwa mshangao lakini hakuna aliyejibu, kila mmoja alikuwa bize kuhakikisha supu inaiva, mwingine alitoka nje kupasua kuni na mwingine alikuwa bize kukwangua ngozi ya paka daaah nilisikia hata kutapika walahi🤮 Nilitoka nje na kumuita baba mkwe aone kinachotendeka, niliwaita wote pamoja na mume wangu Cosmas. "Wewe Cecy haya ni mambo ya kimila hupaswi kuyaingilia hata huko kwenu mna mila zenu na sisi hatupaswi kuziingilia lakini maadamu umeolewa katika ukoo huu Mabula ni lazima ufuate mila na itikadi zote zilizopo kwani na wewe ni sehemu ya familia. Sasa ni hivi umezaa mtoto wa kike, tena mangariba waliokusaidia wewe kujifungua wanasema mtoto alizaliwa akiwa ametanguliza matak, huo ni mkosi mkubwa katika familia hata ukoo, tunataka tuutoe mkosi huo kwa kukutengenezea dawa, utakunywa supu ya paka na kula finyango saba zenye dawa ili kutoa mkosi katoka ukoo wetu na ni lazima iwe hivyo" Alisema baba mkwe, jicho lilinitoka kwa mshangao😳 unaweza dhani litadondoka chini kwa jinsi lilivyonitoka. "Hakuna haja ya kushangaa habari ndio hiyo" alisema baba mkwe. "Hata kama ni mila sipo tayari kunywa supu ya paka, wala kula nyama zake. Kama vipi bora niachane na mtoto wenu nirudi kwetu haya siyawezi" Niliongea kwa kung'aka huku nikiwa na hasira sana. "😒alaaa, kumbe wewe kiburi sio. Nadhani tangu ufike hapa Gamboshi hujawahi kuona maajabu ya hapa sasa ndio utajua kwanini hapa paliitwa Gamboshi" alisema baba mkwe kwa kunitisha. "Sitishiki naondoka zangu" Niliongea kwa hasira nikaingia ndani, nikamuweka mtoto wangu mchanga mgongoni, nikashika begi langu la nguo na kutoka nje, niliondoka huku wakwe zangu wakicheka sana. Ajabu kila mwanakikijiji niliyapishana naye njiani na kumsalimia hakuniitikia, basi nikatembea weeee majira hayo yalikuwa ni saa 12 jioni lakini sikufanikiwa kutoka ndani ya kijiji licha ya kutembea umbali mrefu lakini niliona kama narudi nyuma. "Hee sehemu si nimeipita muda si mrefu mbona nipo tena hapa" Nilijiuliza kwani kuna sehemu nilikuwa nazipita lakini nashangaa nazorudia, hapo hofu ikaendelea kutanda . hatimaye usiku ukaingia, ajabu kijiji chote kikabadilia na kuwa chenye maghorofa makubwa kama jiji la new york. "Mh haya mbona maajabu hapa ni wapi sasa maana hata tanzania hakuna mkoa wenye maghorofa kama haya, " Nilijiuliza huku nikiwa nimesimama. Mara nikashtukia😳.......... Je iendeleee ama Isiendeee? nipe maoni yako leo😋 " 😭🙏03 & 04 Jioni ile niliamua kuondoka na mwanangu kwenye kijiji kile cha Gamboshi, ajabu wakwe zangu wala hawakunizuia kama ilivyokawaida mtu unatopotaka kuondoka sehemu kwa kuchukia watu wa sehemu hiyo wapo watakaokubembeleza kwamba ubaki lakini kwao ikuwa tofauti ndio kwanza walikuwa wanacheka. Ajabu sasa kutoka hapo ukweni kwangu mpaka ufike sehemu wanakopaki bondabonda ni mwendo wa dk 20 tu lakini nilijikuta natembea huku nikishangaa sehemu nyingine kama vile nimezipita halafu najikuta nazipita tena yani nilikuwa narudishwa nyuma kichawi , nazunguka kijijini hapo hapo bila kujijua, nilitembea bila kuchoka yani ni kama waliniloga na kunipiga jini mzunguko😁 yani niwe natembea tu bila kufika ninapoenda.Hatimaye usiku ukaingia ikabidi nisimame sehmu na kuanza kutafakari. "🤔 Mh yani toka saa 10 mpaka saa 1 hii bado sijawafikia vijana wa bodaboda ili wanipelekea stendi? wakati ni mwendo wa dakika ishirini tu kwa mwendo kuwafikia, ama kweli hiki kijiji ni wachawi wa kutupwa" Niliwaza wa kutoa sauti. Mara ghafla taa zikawaka kwenye majumba yangu. Kilichonishangaza sasa nyumba nyingi za kile kijiji miaka hiyo zilikuwa ni za nyasi na wachache sana walikuwa na taa za sola, lakini siku hiyo taa ziliwaka kila kona kama vile nipo katikati ya jiji la Newyork usiku wa manane, nilipoangalia zile nyumba za nyasi zilibadilika na kuwa maghorofa makubwa. "Mh ukisikia uchawi ndio huu sasa, yani mchana hiki kijiji kinaonekana bushi sana lakini usiku ni jiji kubwa kiasi hiki dah' Nilibaki ninesimama nakodoa macho tu kwa woga. Hakukua na magari ya nayopita wala watu wanaopita, nilipotazama angani, mara ghafla😳 nikaona wangu wamepanda kwenye ungo mkubwa sana, ungo huu ulikuwa na taa hivyo niliwaona barabara kabisa, nilimuona mama mkwe wangu akiwa ameshika usinga kwenye mkono wake wa kulia na mkono wake wa kushoto alikwa ameshika kibuyu kikubwa kilichozungushiwa shanga za kila rangi. "😒 Nishushe hapo nimchukue abiria wangu" mama mkwe aliongea akiwa angani, alimwambia mzee mmoja ambaye alikuwa amekaa mbele huku akizungusha mikono yake kama vile abazungusha usukani, hapo nikajua mzee yule alikuwa ndiye dereva. Nilitaka kukimbia wakati ungo unashuka uelekeo wa sehemu ile niliyosimama, lakini ajabu😳 miguu iligoma kunyanyuka yani nilikuwa kama nimenasa kwenye matope yenye gundi. Walininyakua kirahisi sana kama mwewe anavyookota kifaranga cha kuku huku mwanangu akilia sana mgongoni, nilipomuangalia mama mkwe kifuani mwake alikuwa na lihirizi likubwa ambalo lilikuwa linahema. "Cecy hapa ndio Gambosh huwezi kututoroka hata iweje na tena sahamu kabisa kuhusu kurudi kwenu, mwanzo hatukutaka kukuonyesha uchawi wetu ila kwa kuwa umechokoza nyuki acha wakuume, kwani ungekubali kunywa supu ya paka na kutafuna japo finyango mbili ungedhurika nini🙄?" Aliongea mama mkwe wakati huo Ungo ulikuwa unakata masafa angani ile balaa. Dereva alikuwa Hodari haswa hata Dereva Mohamed wa bus la Allys Star haoni ndani kwa mikimbio ile😒. Mwenzenu nilikuwa natetemeka tu kwa woga ukichangia na baridi kali lile la angani maana ilikuwa ni alfajiri nadhani kwani hatukuchukua muda tulitua ukweni kwetu. Bado kagiza kale ka saa 11 kalikwepo. Ungo ulitua katikati ya kundi la watu ambao walikuwa wamezunguka tena wakiwa uchi wa mnyama, Nilimuona mume wangu Cosmas naye akiwa ni mmoja wao, baba mkwe, mashemeji pamoja na mawifi wote walikuwa uchi. "😁 Umemrudishaee hapa hawezi kuondoka hivihivi na kwa vile ameshatukasirisha, tutamgeuza msukule na kumuhifadhi kwenye ile nyumba ya msonge kwa wiki moja kisha tutafanya tambiko la kumuua halafu tutaita wanakijiji wazike kawaida kama zinavyozikwa mazishi maiti nyingine. by:Chombezotu.blogspot.com Basi walianza kunisotea matak* yao huku wakiimba nyimbo zao za kichawi na wengine wakilia kama mapaka😳. Makalio yao yalikuwa yanatoa harufu mbaya kama machemba ya choo, nahisi ni kwasababu walikuwa wamezoea kwenda haja vichakani bila kuchamba . Mwisho walinimwagia miungaunga nikaanza kutoa miudenda kama vile tahira, wakamchukua mtoto wangu kisha mimi wakaenda kunifungia kwenye kijumba cha msonge ambacho ndani yake kulikuwa ni giza tu. Basi maisha ya kuishi kama msukule yakaanza rasmi wakawa wakipika viazi maganda ya viazi naletewa ndio chakula changu. Siku ya siku bwana, mara nikashangaa wanaingia na jeneza kwenye kile kijumba cha msonge, ajabu ndani ya Jeneza kuliwa na maiti yangu na mimi nikiwa nimesimama pembeni yani najiona kabisa kwenye jeneza nikiwa nimevalisha sanda na kila kitu. "Hii ni maiti yako na itazikwa kesho, lakini wewe utaendelea kubaki kama msukule, hakuna mtu atakayefanikiwa kukuona ila wewe utakuwa unawaona watu mpaka wanavyokuzika, " alisema mama mkwe wangu, nilijitahidi kulia kwa sauti 😭 lakini machozi yalikuwa hayatoki wala sauti ilikuwa haitoki. Mara mchungaji akaitwa na kuingia ndani ya kile kijumba cha msonge. Ajabu Mchungaji alikuwa hanioni nikiwa nimesimama pembeni ya maiti yangu, hata nililipojaribu kunyoosha mkono nimguse sikuweza kumshika, kweli nilikuwa nineshageuzwa msukule. "Mzee wa kanisa, hii maiti itaagwa kesho lakini harakati za kumuaga marehemu zitaanzia leo kanisani, tutapeleka hili jeneza kanisani kwa ajili ya maombezi ya kumuombea marehemu kwa Mungu amsamehe madhambi yake aliyoyatenda akiwa hai pia ampunguzie adhabu ya kaburi sawa mzee wa kanisa" Mchungaji alimwambia baba mkwe wangu, kwani yeye licha ya kwamba ni mchawi alikuwa na cheo kanisani, mama mkwe pia alikuwa shemasi kanisani, na mawifi walikuwa ni waimba kwanya ila ni wachawi waliobobea kwa macho ya kawaida huwezi kuwadhania. "Mchungaji, sio kwamba tutaingia gharama tukimpeleka kanisani kwanini, tusizike tu hata leoleo tu ili tuendelee na mambo mengine ya kikanisa" baba mkwe alianza kukwepa kistaili huku mama mkwe na mawifi wakisaport. "Kweli kabisa kanisani ni gharama, halafu utawakusanya watu kutwa nzima bila kuwapa chakula? Hizo ni gharama" waliongea mawifi na mashemeji. "Hakuna gharama mbele ya kazi ya bwana, naamini Mungu ataleta chakula watu watakula nawatasaza na mutamuaga mpendwa wetu kwa amani ya bwana, mimi kama mchungaji nitatoa pesa kwenye mfuko wa kanisa kusaidia shughuli hii" alisema Mchungaji, baba mkwe na mama mkwe walionekana kutofurahi kabisa , lakini hawakuwa na jinsi maiti yangu ilipelekwa kanisani na mimi nikishuhudia kwa macho yangu. Huko kanisani sasa😳....... Ama kweli usipoyaona ya Musa utayaona ya firauni , unajua nini kilitokea kanisani. Gonga like na Coment nije haraka sana🔥🔥🔥🔥🔥

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA

Mpya zaidi Nzee zaidi

Ads related

Smartwatchs