Mapito ya hidaya

MAPITO YA HIDAYA 1____5 Hidaya ni binti wa miaka 12 aliyeishi na Bibi yake bi mboza mkoa wa tanga wilaya ya muheza. Waliishi maisha ya shida Sana. Mama yake hidaya alifariki hidaya alipokuwa na umri wa mwaka mmoja. Hakumfahamu baba yake na alitamani Sana kumfahamu akamuuliza Bibi yake " Bibi hivi baba yangu atakuja kuzichukua lini? " Mjukuu wangu habari za baba yako Mimi hata sizijui Kwanza hata nikikutana nae leo hii sijui Kama nitamjua. " Kwanini Bibi? " Baba yako nilimuona Mara moja to alivyo mleta mama yako alipokuwa na ujauzito wako baada ya hapo cjamuona mpaka leo. " Inamaana baba hanifahamu? " Ndio mjukuu wangu. Hidaya alikuwa na huzuni. " Usihuzunike mjukuu wangu ipo siku baba yako atakutafuta tu. Maisha yao yalizidi kuwa magumu kila kukicha afazali ya Jana. Walifanya vibarua kwenye mashamba ya watu ili wapate helakidogo wa chakula. " Bibi maisha haya mpaka lini ujue Mimi siyapendi . " Mmh! Tutafanyaje hidaya ndio tulivyopangiwa. " Kila siku sisi ndio tumepangiwa hivi tunafanya kazi ngumu malipo kidogo. " Sasa tutafanyaje . " Bibi nataka niende mjini nikatafute kazi tubadilishe haya maisha. " Hidaya sikubaliani na wewe kabisa ukiondoka unaniacha na Nani? Wewe ndio mwenzangu hidaya . Hidaya aliwaza aliondoka atamuachaje Bibi yake na yeye ndio anamsaidia kazi ndogondogo za pale nyumbani " Sawa Bibi twende tukalale muda umeenda. Hidaya na rafiki yake Amina walikuwa wanaenda mtoni kuchota maji. " Amina Mimi natakaniende mjini nikatafute kazi. " Yani Kama vile upo kichwani kwangu unaonaje tukiondoka wote twende dar kwa mjomba angu? " Mimi sija wahi kufika mjini . " Mimi napafahamu ni kuzuri watu wanavaa wanapendeza mjini Kuna kila kitu. Hidaya alifurahi kusikia vile akajua akienda mjini shida zake zitaisha. " Lakini Mimi Sina hela ya nauli " Usijali kuhusu kusafiri wewe jiandae keshokutwa asubuhi tuondoke. Hidaya anywea " Nini sasa mbona haufurahi Tena. " Amina Bibi yangu hataki niondoke nitafanyaje? " Acha ujinga si tunatoroka. "Hapo sawa. Wakacheka wakagonga, wakachota maji yakajitwisha na kurudi nyumbani. Walipo fika nyumbani hidaya akatoa nguo zake chafu akawa anafua huku anaumba kwa furaha. Bi mboza alikuwa anatoka shamba alishusha jembe lake chini akawa anamuangalia mjukuu wake anavyoimba kwa furaha " Unanini shoga yangu mbona unafuraha ? " Bibi sio kila siku tunakuwa na huzuni hata Kama hatunakitu inabidi tufurahi. Bi mboza alicheka " Hahahaha kweli kabisa mjukuu wangu. Bi mboza alikaa kimvulini akamuomba hidaya ampe maji ya kunywa. Hidaya alimpelekea Bibi yake maji akarudisha. Kesho yake mida ya jioni Amina alimfuata hidaya nyumbani kwao. " Hidaya kesho ndio safari jitahidi kuamka mapema tukutane barabarani " Mimi nitaamka mapema Sana wewe ndio usichelewe. " Sawa Mimi naondoka bi mboza asije akatushitukia. Usiku hidaya hakupata usingizi aliwaza safari. Kila wakati alikuwa akichungulia nje kuanga Lia Kama kumekucha . Kulipo Anza kukicha alienda kalibu na alipo lala Bibi yake akamuwekea karatasi akabeba mfuko wa nguo zake akafungua mlango taratibu akatoka nje na kuufunga mlango taratibu Bibi yake asiamke. " Kwaheli Bibi najua nimekukosea Sana naomba unisamehe naenda kutafuta maisha angalau na wewe Bibi yangu ule na kuvaa vizuri. Aliongea hidaya huku machizi yanamtoka. MAPITO YA HIDAYA 2 Amina na hidaya walipata lifti kwenye fuso lililokuwa linasafirisha machungwa kwenda dar. Hidaya alikuwa muoga " Amina tukidaiwa nauli Mimi Sina hela. " Huyu ni rafiki yake Kaka angu nimemwambia tunaenda dar kwa mjomba hatatudai hela usiogope . Aliongea Amina kwa kunong'o a. Safari iliendelea walipofika kibaha dereva aliwaambia " Simnapafahamu kwa mjomba enu? Amina akadakia " Ndio,ndio napafahamu. " Sasa sisi tunashusha mzigo hapa chukueni nauli twendeni nikawapandishe gari . Aliwaza elfu kumi Kisha akaongozananao akawapandisha gari. Yule dereva akauliza " mkifika dar mnafahamu mnakoenda? Amina alijibu " Ndio ni tabata kwa mjomba. " Sawa kuweni makini. Waliagana na yule dereva. Walipofika stendi walianza kushangaa hidaya alimshangaa watu na majengo. Amina hakujua wapi aelekee. " Hidaya mbona wakati nakuja hakukuwa hivi " Kumekuwaje? " Kunanichanganya " Sasa tutafanyaje? Walizunguka hawakujua wapi wataelekea na Giza lilianza kuingia. " Amina nimechoka njaa inauma usiku unaingia tutalala wapi? " Mimi sielewi hidaya tukae hapahapa Kwanza tutajualakufanya. " Naogopa sisi ni wageni huku. " Usiogope tutampata tu mjombaangu. Usiku unaingia wakajibanza kwenye vibaraza vya nyumba za watu wakalala. Walishitushwa na sauti ya mama mmoja " Nyie mabinti amkeni. Wakaamka wallikuwa wamechoka Sana. Wakajinyoosha " Shikamoo! Marahaba. Mnafanyanini hapa? " Tulilala. " Nani kawaruhusu mlale hapa? Amina na hidaya waliangaliana hawakujibu kitu " Nyumbani kwenu ni wapi? " Muheza . " Sasa Mimi sitaki machikolaa muondoke na msirudie Tena kulala hapa. Hidaya na Amina walinyanyuka wakawa wanazurura mitaani. Bi mboza alosikitika Sana hidaya alivyoondoka " Jamani huyu mtoto kwanini kaamua kufanya hivi kaenda dar kwanani? Sijui anakula Nini ,analala wapi. Aaah hidaya wangu rudi nyumbani. Amina na hidaya walianza kuzoea maisha ya mtaani waliomba ilipofika jioni walienda kulala kwenye jumba bovu. Siku moja wakiwa wamelala walivamiwa na kibaka hidaya akafanikiwa kukimbia lakini alimfikiria Amina aliekuwa anapiga kelele akawa anarudi akakutanana Amina anatoka mbio hidaya nae akaanza kukimbia na yule kibaka alikuwa ana wakimbiza kila mtu alikimbia sehemu yake. Amina na hidaya wakapotezana. Hidaya hakuwa na hamu ya ule mji alitamani arudi nyumbani kwao lakini alikosa hata nauli ya kumrudisha kwao. hidaya alipata kazi hotelini ya kuosha viombo na kusambaza chakula jioni alilipwa helayake. Siku moja tajiri yake alimuuliza hivi hidaya unakaa wapi? Hidaya aliminya vidole na kuangaliachini machozi yakiwa yanamtoka " Mbona unalia sasa hidaya? " Dada Sina sehemu ya kuishi naishi mitaani. " Basi usilie kwanini sikuzote husemi? Basi kuanzia Leo utaishi na Mimi. " Asante dada. Dada yake hidaya( Monika) aliishi mwenyewe lakini Mara mojamoja mpenzi wake alikuwa anamtembelea. Baada ya kufungasha kazi Monica aliongozana na hidaya mpaka kwake." Karibu hidaya hapa ndio ninapokaa na wewe utakaa hapa mpaka mambo yako yatakapokaa sawa. " Sawa dada nashukuru mungu akubaliki. Amina alifanikiwa kupata kazi ya ndani. MAPITO YA HIDAYA 3 Baada ya miezi mitatu hidaya alianza kupendeza alinawiri wanaume wakaanza kumkodolea macho. " Hidaya mdogo wangu mbona unakuwa mshamba tumia uzuri wako. " Maneno gani unaniambia dada " Wewe sio wakuishi maisha haya wenzako wanatumia uzuri Kama wako kufanikisha mambo yao nakushangaa wewe unaerizika na elfu tano tano ninazokulipa. " Lakini dada zinanitosha. " Hakuna mtu anaetosheka na hela usijidanganye na ipo siku nitakutimua kwangu ndio utajua hiyo hela ninayokupa inatosha au haitoshi". Hidaya alikuwa na mawazo Siku moja hidaya alikuwa hajiskii vizuri hakwenda kazini. " Hidaya nitatuma mtu akuletee chakula usihangaike. " Sawa dada. Monica alijiandaa akaenda kazini . Ilipofika mida ya saanane Kuna kijana alishuka kwenye pikipiki akaenda kugonga kwa hidaya. Hidaya akafungua mlango." Nimeagizwa na Monica nimekuletea chakula. Hidaya alipokea " Asante. Lakini yule kijana hakuondoka alisukuma mlango akaingiaakaingia ndani. Hidaya alimshangaa." Mbona umesimama njoo. Hidaya aliingia akaweka chakula pemben akawa anamuangalia yule kijana " Mbona unaniangalia kula chakula chako Tena ule ushibe. Hidaya alichukua vijiko akaweka na chakula yule kijana alichukua kijiko akachota chakula akala " Mmmh chakula kitamu . Kula mrembo . Hidaya alimkazia jicho yule kijana akachota chakula na kumsogelea hidaya ili amlishe hidaya alikisukuma kill kijiko akataka kunyanyuka yule kijana akamsukuma hidaya akaanguka wakaanza purukushani hidaya alipigakelele yule kijana akamxiba mdomo. Hidaya akakosa msaada yule kijana akambaka. Alivyomaliza alivaanguo zake. " Pole hidaya hela yako ipo kwa Monica na nitarudi Tena mchumba. Hidaya alilia Sana alisikia maumivu makali alinyanyua akaenda bafuni kuoga. Monika aliporudi alimpongeza " Hongera mdogo wangu hapoumekuwa sasa na haya ndio maisha shika hii hela " Dada kwanini unenifanyia haya wewe ndio sababu ya Mimi kubakwa. Aliongea huku analia. " Acha kujiliza shika hela. Monica alimtupia hidaya . Hidaya aliendelea kufanya kazi lakini Monica alizidi kumkuwadia kwa wanaume. Tabia ya Monica haikumpendeza Ilikuwa usiku Monica alirudi alimkuta amelala. " Wewe hidaya hebu amka uko. Hidaya aliamka akakaa. " Unamatatizo gani ? Nilikwambia uende wapi. " Dada Mimi siwezi ukahaba. " Ahha umekuwa jeuri sasa Kama huwezi siwezi kuendelea kukubembeleza uondoke kwangu. MAPITO YA HIDAYA 4 Kulipokucha hidaya alifungasha mizigo yake akaondoka alipofika sehemu akahesabu hella alizokuwanazo. " Mmh laki tatu nitaigawaje? Nahitaji chumba Cha kukaa, kula na hata ikiwezekana nipate mtaji hata wa maandazi. Alijisemea hidaya. Wakati anahangaika akakutanana na Kaka mmoja " Vipi dada? " Safi. " Unaelekea wapi ? Nimekuona muda unazunguka na mzigo wako. Hidaya alimkunjia sura alionekana kuboreka na maswali ya yule Kaka. " Naitwa James unaitwa Nani? " Jina langu halitakusaidia chochote. " Huwezi jua pengine naweza kutoa msaada. Hidaya alimuangalia kwa zarau akaamua kuondoka na kumuacha James alimuangalia. Hidaya alienda kwa mama ntilie akaagiza wali na maharage alikula kwakufakamia alikuwa na njaa sana. Aliwaza kwa siku hiyo atapata wapi sehemu ya kulala wakati akiendelea kuwaza alishituliwa na mtu aliemgusa begani alipogeuka alikuwa ni James. Hidaya alishusha pumzi " Hivi kwanini unanifuatafuata? James alitabasamu Kisha akakaa. " Unatakakujua kwanini ninakufuata? Hidaya hakumjibu akamimina maji kwenye grass akanywa alipogeuka jicho akamkuta James bado anamuangalia . " Inaonekana unamatatizo. " Sina matatizo na mbona unanikosesha amani unachotaka kwangu ni Nini? " Punguza hasira sisi ni watu wazima naimani tutaelewana tu. " Unajua kichwa changu kinamambo mengi Sana nahitaji kutulia niyatafakari unavyonisumbua unanipotezea muda Kaka. " Nimekuelewa nahisi utakuwa umepotea au haunasehemu ya kwenda. Hidaya akakaa kimnya huku akiwa anatafakari huyu mtu pengine anania ya kunisaidia . " Kama Nina shida hiyo utanisaidiaje? James alitabasamu " Naweza kukusaidia. Hata sehemu ya kukaanitakupatia. " Nitakuamini vipi mtu sikujui " Naomba uniamini. " Sio rahisi kukuamini ikiwa Leo ndio siku ya Kwanza kuonana na wewe siwezi kujitoa sadaka. " Hahahaha! Sikia tutaenda mpaka kwa mwenyekiti wa mtaa hapo pia hauniamini? " Hapo sawa kidogo naamini. Walikubaliana James akabeba begi wakaongozana na hidaya mpaka ofisi ya mwenyekiti. James akamueleza mwenyekiti amepata mgeni mwenyekiti akamuondoa wasiwasi hidaya " Usijali binti huyu ni kijana wetu na anafaamika Sana hapa mtaani. Hidaya na James walivyomaliza a na mwenyekiti walionfoka wakaenda nyumbani kwa james. Walipofika James akafungua mlango " Karibu hapa ndipo ninapoishi. Hidaya akaingia ndani akaenda kukaa kwenye Kochi aliangaza kila Kona ya chumba " Kuwa huru utakaa hapa mpaka mambo yako yatakapokaa sawa. Ilipofika usiku James alienda kununua chips akamletea hidaya " Kula chakula upumzike. Hidaya alinawa mikono akaanza kula lakini kichwani mwake alijiliza " Sasa chumba chenyewe kimoja tutalalaje? Wakati yupo kwenye dimbwi la mawazo James akamshitua " Unawaza Nini? " Siwazi kitu nimeshiba " Mbona sasa haujalala? " Nitakula kesho. James alihisi Kuna kitu hidaya anaogopa. " Haya kitanda kilepale unaweza kwenda kulala MAPITO YA HIDAYA 5 Na wewe utalala wapi! Hidaya aliuliza " Usiogope Mimi popote nalala hata chini. Hidaya hakuwa na imani na wanaume aliogopa usiku asije kufanyiwa vitu vibaya na James. James Kuna kipindi alikuwa anafuatilia kwenye tv kilipoisha alichukua shuka na kujilaza kwenye Kochi. Hidaya hakuwa na usingizi kula wakati alishituka na kumchungulia James. Mida ya saa kumi na moja alfajir hidaya aliamka na kukaa kitandani . " Huyu James anamaana gani kunileta kwake ikiwa anachumba kimoja? Mungu wangu nitaweza kweli haya maisha? Hapana nitaondoka tu yasije yakanikuta mengine.hidaya alijiliza maswali na pasipo kupata jibu. James aliamka akasimama na kujinyoosha . " Vipi hidaya mbona umekaa si ulale mapema yote hii. " Usingizi umekata. James alitabasamu " Najua unaogopa, Mimi ni mtu powa Sana kuwa na amani. James alichukua mswaki na taulo lake akaenda bafuni kuoga alivyomaliza alijiandaa akamuachia hidaya elfu tano " Natoka naenda kwenye shuhuri zangu shika hii hela utaenda kununua chochote kwaajili ya kula. Hidaya akaipokea. Hidaya akatoka akawa anaenda chooni akakutanana na wanawake wa pangaji wenzake na James kila mmoja alikuwa na kazi yake wengine waliosha viombo, wengine walikuwa wanafua aliwasalimia akaingia chooni. Mpangaji mmoja akaguma " Mmmh! " Mama Steve utasutwa kinachokugunisha Nini. " Naguna huyu dada kujakujiingiza kwa firauni binti mdogo mrembo. " Ya ngoswe muachie ngoswe . Walivyosikia mlango was chooni una funguliwa walinyamaza kimnya. Siku zilivyosogea James alionyesha hisia za mapenzi kwa hidaya . hidaya akakubali na na James wakaishi Kama mke na mume mapenzi yalikuwa motomoto hidaya alipendeza alichotaka alipewa ila alipewa masharti na mume wake. " Hidaya mke wangu unajua nakupenda mpaka sijielew nimekuwa mjinga sababu ya penzi lako. Hidaya aliona aibu " Acha kunilewesha na sifa nisizostahili. " Sikuongopei mama nakupenda. " Nakupenda pia. Hidaya akambusu James " Wait! Asante! Hidaya wewe ni make wangu sikufichi kinamambo ambaya Mimi sipendi ufanye. " Mambo gani? " Sipendi ukae vibarazani na hawa wanawake pia sitapenda nikukute umesimama na mwanaume yoyote. " Huo wivu sasa mume wangu. " Nikweli ugonjwa wangu mkubwa nihicho Nina wivu haswa. " Sawa baba mwenye nyumba. Ilikuwa mida ya saa saba mama Steve alienda kumgongea hidaya. " Hidaya love anaumwa na hapa tupo Mimi na wewe naomba unisaidie tumpeleke hospital. Aliongea huku anahema " Ina maana anaumwa na uchungu? " Ndio. Hidaya alichukua kitenge akajifunga akafunga mlangowake na kwenda kumchukua love wapaita taxi wakampeleka hospital. Mida ya saakumi na mbili jioni hidaya na mama Steve walipokuwa wanarudi walimkuta James amesimama mlangoni huku akiwa amefura kwa hasira. Mama Steve bila kuongea chochote alienda kifungua mlango wake akaingia .James hakuongea na hidaya alimnyang'anya funguo akafungua mlango akaingia ndani. Hidaya nae akaingia. " Mume wangu samahani sikukuaga tulimpeleka dada wa chumba hicho hospital alikuwa anaumwa uchungu. " Wewe ni Kama Nani kwake? Na ni likwambiaje? " Lakini sisi ni majirani tunatakiwa tusaidiane nikijitenga nitakapopata tatizo nitasaidiwa na Nani? James aliamka kwenye Kochi na kumsukumiza ukutani Kisha akambana. " Kwahiyo sikuile wakati naongea na wewe ulikuwa unaniona punguwani Sia akili au vipi? "Sio hivyo. Alijibu hidaya huku anatetemeka. " Hidaya usiujalibu uvumilivu wangu. Aliongea kwa hasira na kumuachia. Hidaya alitetemeka na machozi yalikuwa yanatililika mashavuni mwake. Maisha yalizidi kuwa magumu kwa hidaya kwaajili ya kufungiwa na akifanyakosa kidogo alipigwa . Majirani zake walimuona huruma " Mnajua huyu dada anapata tabu Sana Mimi namuonea huruma. Aliongea moja was jirani zake " Unajitoa ufahamu inamaana James umemsahau? Huyu Kaka habadiliki wanawake kila siku anakimbiwa na wanawake. Hidaya aliwasikia kwa dirishani walivyotoka . " Mungu wangu nimejidumbukiza kwenye shimo gani? Laiti ningejua ningeenda kwa Bibi yangu. Aliongea hidaya huku analia.

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA

Mpya zaidi Nzee zaidi

Ads related

Smartwatchs