🥺🥺🥺🥺🥺NANI AMENIPA MIMBA?🥺🥺🥺🥺
( SEHEMU YA 01 )
😒💔🔥
Kwa majina naitwa Witness Kijeba, ni mtoto pekee wa mzee Kijeba na bi Kijeba. Mimi ni mwanachuo wa Diploma mwaka wa pili, umri wangu ni miaka 21 na kimuonekano mimi ni mrefu wastani, mwembamba wastani, mweusi mwenye sura ya kawaida ila nimebarikiwa shepu yenye kalio pana. Historia yangu ya mahusiano ni kwamba tangu niachane na mwanaume aliyenitoa bikra sikujihusisha na mwanaume mwingine yeyote, na mipango yangu mikubwa ilikuwa ni kujihusisha tena muda wa kuolewa; nilipanga kuguswa na mwanaume ambaye atanioa tu, lakini kabla sijaolewa nilikutwa na mkasa ambao leo hii nataka niwasimulie, twende pamoja!
*****
Ilikuwa ni saa sita za usiku, ndani ya nyumba nilibaki mimi peke yangu; wazazi wangu ambao nilikuwa naishi nao walisafiri walielekea kijijini kusalimia ndugu zetu. Usiku huo nikiwa nimelala kwa mbali nilisikia kama kuna mtu anagonga mlango; Kwanza niliogopa kwa sababu sikujua ni nani anagonga mlango usiku kama huo, pili niliogopa kwa sababu ndani ya nyumba nilibaki mimi pekeyangu, na tatu niliogopa kwa sababu mimi ni mwoga sana. Moyo wangu ulienda kasi, pumzi zangu zilisikika kwa nguvu, kiukweli nilipata hofu kubwa, niliwaza nikafungue mlango au nisiende? Hata hivyo nilihisi labda ni mtu anayenifahamu, labda ni majirani au wazazi wangu wamerudi kijijini; Taratibu nilijifunua shuka kisha nilipiga hatua nilielekea sebuleni, niliwasha taa kisha nilielekea mlangoni, nilifungua mlango; ajabu ni kwamba sikuona mtu yeyote, hapo sasa nilizidi kupagawa, plesha ilipanda na kushuka, kijasho kinene kilinidondoka.
Nilijipa ujasiri nilisimama pale pale mlangoni, nilisubiri labda nitamuona mtu aliyekuwa anagonga mlango, nilisubiri sana lakini sikumuona mtu yeyote. Ubaya wa nyumba yetu ni kwamba haikuzungushwa fensi wala haikuwa na geti, ilikuwa ni nyumba kama nyumba. Baada ya kujithibitishia kuwa hakukuwa na mtu yeyote nilifunga mlango kisha nilirudi ndani, sikuzima taa ya sebuleni; niliacha iwake hivyohivyo, nilielekea chumbani kwangu nililala. Sio kwamba nililala usingizi, nilijilaza tu lakini akili na fikra zangu zilikuwa mlangoni, masikio yangu yalikuwa makini kusikiliza kama kuna mtu atagonga mlango lakini sikusikia. Hapo sasa nilijifariji nikiamini labda ni upepo tu ndio ulisukuma mlango. Baada ya kujihakikishia usalama nilitulia nikitafuta usingizi, ilinichukua muda mrefu hadi nilipolala fofofo, sikujua kilichoendelea duniani, ilikuwa ni mimi na raha zangu za usingizi.
comments tu na tuma nyingine apa🥱🥱🥱
Nani amenipa mimba?
GREEN HACKER
0
Chapisha Maoni
TOA MAONI YAKO HAPA