Doctor merry (mtumishi wa kuzimu)

chombezotu.blogspot.com 🍅*1-----------4* Hadithi: DOCTOR MERY (Mtumishi wa Kuzimu) Sehemu 1 Saa sita na nusu usiku, zilisikika kelele za mama mjamzito akishushwa kutoka kwenye gari, Mumewe akimtia moyo na kumpa maneno ya faraja, lakini maneno hayo hayakuweza kumpunguzia uchungu aliokuwa akiusikia. Aliendelea kulalamika akisema "mume wangu nakufa, tumbo linanikata kata, sijui kama naweza kuiona kesho, ohooo!!!, mwenzenu tumbo langu mie" mumewe alidondosha machozi kwa kumuhurumia alitamani ule uchungu uhamie kwake "Najua ni kiasi gani mke wangu unaumia, Kama uliweza kuvumilia, manyanyaso, kashifa, dharau, kutukanwa na ndugu zangu kisa huzai, pia uliweza kuvumilia wakati tunahangaika kwenda mahospitalini, kwa waganga wa kienyeji ili kupata tiba ya tatizo la kutokuzaa kwako, hatimae baada ya miaka 20 mungu amesikia kilio chetu, tunaenda kuitwa baba na mama, usilie mpenzi onesha furaha" hayo yalikuwa maneno ya Mume kumtia Moyo mkewe, Muda huo walishafika mapokezi ,nesi alimpokea kwa maneno ya kejeli "mtoto wa kike jikaze bwana, unalia lia unafikiri hapa kwa mama yako, ndio ujue mwanzo wa utamu mwishoe uchungu" Mmewe alimgeukia nesi akimuomba apunguze ukali wa maneno kwa mkewe, "we unanifundisha kazi??, unataka nimbembeleze amekuwa mtoto mdogo??, ajikaze analegea utadhani ni mimba ya kwanza." " Ndio nesi katika maisha yetu ya ndoa hatukubahatika kupata mtoto, hii ni mimba ya kwanza kwa mke wangu" baada ya maneno ya Baba Yule nesi kidogo upole ukamshika na kuuliza "kweli umri wote huu hamna mtoto??? " "ndio hivyo nesi " "mmmhh mkubwa, haya nisaidie kumnyanyua tumpeleke kwa daktari". Dr Mery akiwa ofisini kwake mlango ulifunguliwa akaingizwa yule mama mjamzito, chupa ya uzazi ilishapasuka na alianza kutiririsha damu, Dr aliamuru apelekwe chumba cha kujifungulia haraka, alipopelekwa njia ya kutokea mtoto ikawa ndogo. Mumewe alikua nje akifurahia muda mchache ujao ataitwa baba "Tumehangaika sana hospitalini, kienyeji mke wangu aweze kuzaa, kweli nimeamini mvumilivu hula mbivu" alikuwa anajiongelesha pekee yake pale Nje, ila gafla akaona kitanda kikitolewa kwa kasi akauliza kwa hamaki "nesi nini tena?" " mkeo ameshindwa kujifungua kwa njia ya kawaida hivyo tunampeleka chumba cha upasuaji" "upasuaji tena??" wala hakujibiwa nae alichofanya ni kufuata kwa nyuma. Dr Mery ndiye alieongoza upasuaji walifanikiwa kukitoa kichanga salama, lakini gafla Pete aliyovaa Dr Mery ilitoa mwanga hiyo iliashiria kuna Ujumbe anatakiwa kuupokea, aliipeleka Pete hiyo sikioni akasikia sauti ikimwambia "Tunakiitaji hicho kichanga huku kuzimu" baada ya happ sauti ikakata, alimshona mzazi na kumwamuru nesi ampeleke wodini wakati yeye akiendelea kushughulika na kile kichanga. Mume wa yule mama alisimama baada ya kuona mlango wa chumba cha upasuaji ukifunguliwa,alimuona mkewe akiwa bado hajitambui, nesi alitabasamu akimpa hongera kwa kumpa hongera ya kupata mtoto wa kiume, Baba wa watu aliruka ruka kwa furaha akimbusu mkewe mfululizo ambae alikua anapelekwa wodini, huku nyuma Dr Mery alikatazama kale kachanga ambako kanatakiwa kapelekwe kuzimu, kalikuwa katoto kazuri kavulana kenye afya njema, aliinamisha uso wake chini akachukua vidole vyake viwili na kubana pua ya kale katoto, maskini kalishindwa kupumua kakakata roho, Nesi baada ya kumfikisha mgonjwa wodini alimwambia mme wa yule mama kuwa "ngoja sasa nikakuletee jembe lako" akimaanisha mtoto wa kiume, halafu umwangalie mkeo maana akizinduka hapo atataka akae si unajua ana mshono. Nesi alizipiga hatua kuelekea chumba cha upasuaji ,alipofika hakusikia kelele za mtoto kulia alimuona katulia, ikabidi amuulize Dr "haka katoto vipi mbona nashindwa kukaelewa??" Dr Mery alimjibu huyo mtoto si rizki, "Dr mbona nashindwa kukuelewa si rizki kivipi??" "unashindwa kunielewa nini ina maana maiti huijui?" "Haaaa!! Dr hapana mtoto ametoka akiwa na afya njema hana tatizo eti amekufa,!!!!??" Dr mery akamwambia "we unamuona mzima huyo?," "imekuwaje akafa Dr," "mi siyo mungu nenda kamwite mzazi wa hii maiti apewe taarifa ya kifo cha mtoto wake" Nesi aliyejulikana kwa jina la Nesi Tina akiwa mwenye mawazo akishangazwa na kifo cha ghafla cha yule kichanga, pia anawaza atakavyowaambia wazazi wale waliokuwa na shauku kubwa ya kupata mtoto baada ya kuhangaika takribani miaka ishirini, kule wodini mzazi alizinduka kutoka usingizini cha kwanza aliomba apewe mtoto wake. Mambo Ndo Hayo Je wazazi watakubaliana na kifo Cha mtoto wao!? Ndo kwanza tupo mwanzo wa Hadithi. Itaendelea......... Hadithi: DOCTOR MERY (Mtumishi wa Kuzimu) Sehemu 2 Nesi Tina alitembea kuelekea wodini walipo wazazi wa yule mtoto aliefariki. kichwani alikua na maswali mengi juu ya kile kifo, pili ni jinsi ya kufikisha taarifa kwa wahusika waliokuwa na shauku ya kupata mtoto baada ya kuhangaika kwa muda mrefu. Upande wa Huku wodini Mama kichanga baada ya kurejewa na fahamu alimgeukia mmewe akimuomba ampe mtoto aliejifungua, "Pole mke wangu kwa misuko suko ulioipata Mungu ametujalia mtoto wa kiume" kwa sauti dhaifu mke wake alitabasamu "huyo atakuwa baba yangu" " aah atakuwa baba yangu mimi" Yalikua ni majibizano ya utani Kati ya wawili wale, nesi alifika akijitahidi kuficha huzuni yake, mume akauliza "yuko wapi mtoto??" "samahani naomba unifate" "wapi tena??" mkewe akamwambia "nenda bwana kaniletee mwanangu" alinyanyuka na kumfuata nesi hadi kalibu na theatre, walipofika mlangoni walisimama nesi alimuuliza "katika maisha ni kitu gani ambacho huwezi kuja kusahau?" "kiukweli tulivyohangaika kupata mtoto sitakuja sahau" akamuuliza tena "unapendelea nini katika maisha??" "mbona maswali yamekuwa mengi naomba unikabidhi mwanangu nimpeleke kwa mama yake" "ooh unajuwa wewe ni mwanaume, ninaamin nyie huwa ni watu jasiri kuliko sisi!" "unamaanisha nin Nesi??" "sina maana mbaya sana ila katika maisha kuna vitu huwa vinatokea halafu tunashindwa kuamini" "Yeah ni kweli nesi" "OK naomba uniamini kwa hili nitakalo kueleza" jamaa uso ulibadilika wasiwasi ukaanza kumshika "nesi kuna nini nashindwa kukuelewa??" "no hupaswi kushituka Kwa sababu wewe siyo wa kwanza kutokewa, mtoto wako hatunae tena, amefariki dunia" alikaa kimya sekunde kadhaa akasema "usinitanie nesi mtoto wangu hawezi kufa mapema hivyo" "siyo utani na hatuwezi kuleta masikhara kwenye maisha ya mtu, mwanzo nilikuambia wewe ni mwanaume (always men are courageous (siku zote wanaume ni majasiri) ndio maana nimekuleta huku kukuambia siyo pale kalibu na mkeo" Machozi yalimdondoka furaha aliyokuwa akiitegemea haipo tena, alishajua sasa amekuwa baba baada ya kuhangaika kwa muda wa miaka mingi,alifikiria mkewe atamuelewaje 'aliendelea kutiririsha machozi ya uchungu. Nesi alimshika mkono akimwambia 'crying doesn't solution, poured water can't be fatched '( kulia si ufumbuzi wa tatizo, maji yakishamwagika hayazoleki) naomba twende ukaone mwili wa mwanao hata mimi inaniuma sana bado siamini mtoto alikuwa na afya njema" aliingia akautazama mwili wa mwanae akawa anamtingisha akimwambia "niite baba, niite baba mwanangu, katika maisha yangu sijabahatika kuitwa oooh!! Leo nilijua sasa naitwa, umeondoka kabla ya kuniita, please my baby call me father (tafadhali mtoto wangu niite baba) aah kweli fungu la kukosa ni la kukosa tu why me God (kwa nini mimi Mungu)" Nesi Tina machozi ya huruma yakamtoka alienda kumtoa pale akimpa maneno ya faraja "acha kumsumbua hakusikii huyo, mungu atakupa mwingine". Dr Mery aliingia akaanza kumfokea nesi Tina "we muda wote mmekaa tu hapa unamwachia huyu anapiga makelele utafikiri hajawahi kufiwa, hebu mtoe hapa, peleka mwili mochwari halafu uje ofisini upitie ripoti ya kifo cha huyu mtoto" "Dr mbona huna huruma jamani??," "daktari hatakiwi kuwa na huruma fanya kama nilivyokuagiza haraka,." Baba wa watu aliingia wodini akiendelea kulia, nesi anamwomba asilie ajikaze ili mkewe asielewe kitu kwa kuwa bado anakidonda kibichi utazidi kumuumiza, maneno yake hayakusaidia kitu aliendelea kulia, mkewe alishtuka baada ya kumuona mmewe kwenye hali ile kwa utu uzima aliokuwa nao alishajua Nini kimeendelea, nae akaanza kulia, akamuuliza mumewe "yuko wapi mtoto wangu?" Je watafanya nini Hawa wazazi Ambao mtoto wao amekufa katika mazingira ya utatanishi!?? Itaendelea.......... Hadithi: DOCTOR MERY (Mtumishi wa Kuzimu) Sehemu 3 ,,,,alipokuwa akiingia wodini alitiririsha machozi huku nesi akimsihi asilie kwani kulia kwake kutafanya mkewe aliekuwepo kitandani kujua nini kimetokea, Nesi alimsihi " please stop crying "( nyamaza usilie). Haikusaidia kitu kwa uchungu aliokuwa nao, mkewe aliona ile hali ya mumewe 'alimuuliza kwa uchungu "yuko wapi mtoto wangu" maskini Baba wa watu alishindwa kuongea alishika nguzo ya kitanda na kukiegemea akilia kwa kwikwi, mkewe alimgeukia nesi " "nesi nini kimetokea kwa mme wangu, kuna kitu hakiko sawa kwake, niambie nini kinaendelea?"Nesi alimtizama akamwambia "hakuna kitu mpendwa" aliuma mdomo na kumtizama kwa jicho Kali mapigo ya moyo wake yakianza kupiga kwa kasi "naomba usinieleze neno tofauti kuhusu mtoto wangu, nimehangaika muda mrefu kutafuta mtoto miaka na miaka, naomba mniletee mwanangu nimnyonyeshe" mmewe akiendelea kububujika machozi alimgeukia akamwambia "mke wangu sisi ni fungu la kukosa" "unamaanisha nini mume wangu mbona nashindwa kuwaelewa? nilikuagiza umfate mtoto ajabu unarudi mikono mitupu uku ukilia" alimpa jibu moja tu kuwa 'mtoto wetu ameaga dunia ' kwa mshtuko na hali ya mshangao aliuliza kama hakusikia kitu "unasemaaaah!!!!!!!!",jibu lilikua ni lile lile,alipigiza kichwa kwenye mto na kuichomoa dripu iliyokuwa mkononi kwa ghafla akajitupa chini sakafuni, palepale nae akatulia hakuweza kutikisika tena. "Nesi msaidie mke wangu please mbona unamtazama tu" nesi aliondoka kuelekea chumba cha daktari. Baba yule alimwinua mkewe uku akimtingisha na kumwita jina lake, hakupata jibu lolote zaidi ya kuona damu zikitiririka kutoka pale alipofanyiwa upasuaji wa kumtoa mtoto wao ambae sasa ni marehemu kabla ya hata kunyonya ziwa la mama yake. Dokta Mery alifika na kuamuru anyanyuliwe awekwe kitandani, alimpima mapigo ya moyo 'alitikisa kichwa na kusema mbona ameshafariki huyu. Kaka wa watu alizidi kuchanganyikiwa na kumwambia "dokta hapana, mke wangu hawezi kufa ghafla hivi, huyu atakuwa amelala tu ngoja nimuamshe umpe dawa". Dokta mery alikunja uso wake kidogo akamuuliza kwa ukali "we una elimu kunizidi mimi??, halafu we kaka msumbufu sana ujawai kufiwa au??, mfyuuuuuuu" aliongea Kwa Kufoka akamsonya na kuondoka pale. Ikumbukwe Dk mery ndie aliemuua mtoto wa huyo kaka, katika siku ambayo ilikua ngumu kwa huyu Baba na sidhani Kama ataweza kuisahau basi ni siku hii,uchungu aliokuwa akiusikia ni kama amechomwa na mkuki moyoni,aliongea maneno mengi sana na kumchukia yule dokta ambae amesababisha vifo vya watu wake wawili muhimu. Dokta Mery akiwa ofisini kwake aliingia mgonjwa Kama utaratibu ulivyo kwa watu wanapokwenda hospital kupata huduma, "Ehee! nakusikiliza mzee una shida gani?" " "Aaahh dokta sijisikii vizuri nimeamka naona kichwa kinanigonga kweli ndio nimeamua nipitie hapa nipate matibabu kidogo nielekee kazini" "ok iyo hali imekuanza lini??" "Ni Leo dokta baada ya kuamka" "sawa ngoja nikuandikie dawa ukatumie" wakati dokta mery akijiandaa kumwandikia dawa, Pete yake ya kidoleni ilitoa mwanga Tena, na ni yeye tu anaeweza kuuona, ule mwanga ni ishara kuwa kuna jambo anataka kuambiwa kutoka kuzimu ,aliinuka kwenye kiti chake akimuomba radhi "samahani mzee nisubiri Kama dakika tano hivi nakuja" wala hakwenda mbali aliishia kwenye kordo akaisogeza ile Pete sikioni akaisikiliza sekunde kadhaa ndipo akarudi ndani akiwa mchangamfu kweli "Vipi baba nimekuchelewesha??" "hapana mama si unajua na nyie kazi zenu hamtulii sehem moja" dokta mery alimjibu "kweli kabisa mzee wangu, halafu nilisahau kukuuliza jina ili niandike kwenye hili daftari lako la matibabu sijui unaitwa nani?!?" "mimi jina langu ni Sixbert Henry" "mzee unajua nyie mnapenda sana kunywa mavidonge ndio maana huwa hamponi haraka," Mzee sixbert akamjibu "hivyo ndio vinapatikana kwa urahisi na bei nafuu". Dokta Mery alijichekesha na kusema "kuna dawa nataka nikupatie hiyo dawa ukiitumia hutakuja kuumwa tena kichwa maisha yako yote," Mzee wa watu akauliza dawa gani hiyo, akaambiwa ipo ila si ya kidonge ni ya sindano,, "ee!!! mama na umri wangu huu unichome sindano" "ndio hivyo mzee umekuja hospital upate tiba au?" "(ndio) " "basi fata ushauri wa daktari sawa" mzee wa watu ile hali ya kuchomwa sindano ilimshangaza kidogo ila kwa kuwa yupo na daktari hakuwa na jinsi, laiti angejua asingekubali kuchomwa, alijitayarisha vizuri, dokta Mery alichukua kichupa kidogo cha dawa na bomba la sindano akaivuta dawa kwenye sindano kisha akamchoma kwenye paja baada ya kumaliza akamuuliza "unajisikiaje mzee" "kawaida" "ulikuwa unaogopa bure tu mzee wangu sasa tatizo la kichwa hutalisikia tena" ghafla mzee akaanza kulalamika kuwa mwili wake unakosa nguvu "jikaze tu baba hiyo dawa ina nguvu sana" mwisho nguvu zilimwiishia kabisa akadondoka chini. Kwa haraka dokta Merry alifunguwa mlango na kuita "nesi nesi nesiii,, Leta kitanda kuna mgonjwa kazidiwa umpeleke wodini" Nesi alipofika alishangaa "haa!! Dokta mbona huyu mzee alinipita akiwa mzima tena tumesalimiana nae imekuwaje azidiwe hivi!?" Dokta Mery alimjibu kwa ukali akimwambia "sijakuita uje uniulize maswali ya kipumbavu angekuwa haumwi angepanga foleni ya kuniona? Hebu Fanya haraka umpeleke wodini" Je ipi hatima ya Doctor huyu ambaye anaonekana amekuwa tishio la maisha ya Watu!?? Itaendelea.......... Hadithi: DOCTOR MERY (Mtumishi wa Kuzimu) Sehemu 4 Dokta Mery alimwambia usiniulize maswali ya kipumbavu,kama mtu alikua haumwi foleni aliyopanga ya kuniona ilikuwa ya nini. Nesi Tina alitaka kusema kitu lakini jicho Kali alilokutana nalo kutoka kwa Dokta Mery ilibidi anywee 'alisikia sauti Kali akiamuliwa ambebe mgonjwa haraka Sana ampeleke wodini kwa matibabu zaidi "unashangaa nini sasa?? hebu sukuma kitanda umtoe kuna watu wengi wanasubiri Huduma yangu wako nje" Mzee sixbert akiwa katika hali ya kutojielewa baada ya kuchomwa sindano asiyoielewa, alipelekwa wodini ambako haikuchukua sekunde aliaga dunia huku Nesi Tina akishuhudia, kwa haraka alitoka mbio kurudi kwa Dokta Mery akitetwa kwa mshutuko, aliulizwa we vipi??, "aaah dokta yule mgonjwa, a, a, a," dokta Mery akibetua midomo yake "aa nini si useme mbona unababaika babaika," Nesi Tina akamwambia nilipomfikisha tu wodini amekata roho,,, "khaa sasa hilo ndio likutoe mbio kwani mtu kukata roho ni jambo la ajabu??" "siyo hivyo dokta tatizo kifo chake kimenishtua yaani nimesalimiana nae akiwa na tabasamu tele, muda huu amekuwa marehemu dah amekufa kirahisi kweli." Dokta Mery alimtupia swali la dhihaka akisema "haa kumbe kuna kifo kirahisi na kigumu hebu nieleze hao wanaokufa kigumu inakuwaje eti??, ebu acha utoto wewe nenda kampekue uchukue na simu yake uwajulishe ndugu zake wamfanyie taratibu za kuuchukua huu mwili," Mke wa mzee Sixbert aliiona simu yake ikiita alipoichukua aliona namba ya mmewe "mm huyu nae sijui anataka kuniambia nini, basi ukiona hivyo kapewa panadol anywe anaogopa ngoja nimsikilize,, "Haloo baba carolin" upande wa pili alisikia sauti ngeni ya kike ikimwambia samahan hapa ni hospital tunakuomba ufike hali ya mme wako imebadilika, simu ikakatwa. Mama Carolin alihisi kuchanganyikiwa hadi Caro alitambua kwamba mama yake hayuko sawa, alimuuliza "mama kuna nini kwani mbona kama umechanganyikiwa" "mwanangu nimepigiwa simu kutoka hospitali eti baba yako amezidiwa" "amezidiwaaa!!??" "ee ndio hivyo ngoja nimpigie simu baba yako mdogo twende nae, we kaa hapa nyumbani.". Walifika pale Hospitali mtu na shemeji yake hadi mapokezi, baada ya kujitambulisha waliambiwa wasubiri. Mdogo wake na mzee Sixbert alimuuliza shemeji yake mama Caro, "kwani shemeji kaka alikua anaumwa sana au??" "wala mi aliniambia tu kuwa hajisikii vizuri hivyo kabla ya kwenda kazini atapitia hospital." Mbele yao alisimama Nesi akawaambia "samahanini nyie ndio ndugu zake na sixbert???," wote kwa pamoja wakamjibu ndio sisi, "ok we kaka naomba unifate kwanza, anty nisubiri hapohapo". Mke wa mzee sixbert machale yakaanza kumcheza, mdogo wake na mzee sixbert alijulikana kwa jina la Josephat aliingia kwenye chumba cha daktari kilichotumiwa na Dokta Mery,, alikaribishwa "karibu Josephat" alishtuka kusikia jina lake likitajwa na Dokta ambae hamfahamu wala hakuwahi kumuona,. "usishtuke Josephat vp umekuja kufatilia hali ya kaka yako??" "ndio dokta" "sawa a, aa, kaka yako alifika hapa asubuhi akilalamika kichwa kinamuuma wakati nikitaka kumfanyia vipimo alizidiwa, nikaamuru apelekwe wodini kwa msaada zaidi", alitulia kidogo dokta Mery kisha akaendelea "unajua sisi madaktari kazi yetu ni kutibia na si kuponya, mponyaji ni Mungu tu yeye ndie huamua hatma ya maisha yetu , tumejitahid kumtibia kaka yako ila Mungu hajapenda kumponya hivyo hatunae tena duniani." Josephati alitingisha kichwa kuashiria kwamba hakukubaliana kwa kile alichoelezwa na dokta Mery. Aliitwa Nesi Tina na kuambiwa ampeleke Josephat mochwari akashuhudie mwili wa ndugu yake. Mzee Sixbert alizinduka na kujikuta amesimama pembeni ulipokuwa umelala mwili wake, alishindwa kutambua nini kimemtokea akiangalia huku na kule anaona maiti zimetapakaa ukiwepo na mwili wake, hakuweza kunyanyua mguu wala kutikisa kidole zaidi ya kuchezesha macho na kuzunguusha kichwa akijiuliza mbona huyu alielala hapa ni mimi imekuwaje. kidogo mlango ulifunguliwa akamuona mdogo wake Joseph akiingia na Nesi, pia aliweza kumkumbuka yule Nesi waliposalimiana nae wakati anakwenda kumuona Dokta Mery, baada ya kufika pale Jose aliukagua mwili wa kaka yake uliokuwa umelazwa chini, machozi yalimdondoka kwa kumpoteza kaka yake ambae ndie alikuwa nguzo kwenye familia yao. Sasa mzee Sixbert akaelewa nini kinaendelea alitaka kumgusa mdogo wake kumwambia kuwa yeye ni mzima wala hajafa alishindwa kufanya hivyo, yeye aliwaona ila wao hawakumuona alibaki akimtazama tu mdogo wake jinsi alivyokuwa akiutingisha mwili unaofanana kabisa na yeye, alitamani kusema akashindwa, mwisho alishuhudia mdogo wake na nesi wakiondoka. Josephati ilibidi ajikaze kiume hadi pale alipomuacha shemeji yake kufika tu mama Caro alisimama na kumtupia maswali mfululizo "shemeji mbona umechelewa hebu niambie hali ya mme wangu?" Ndo kwanza mambo yanaanza Je ndugu wa Mzee Sixbert watakubali kufiwa kizembe!? Ipi hatima ya Doctor Mery!?? Itaendelea....... Full 1000

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA

Mpya zaidi Nzee zaidi

Ads related

Smartwatchs