Mubaba wangu

1____5 🌺🌺🌺 *MUBABA WANGU* 🌺🌺🌺 {01} Naitwa Opra.... kwetu nimezaliwa peke angu....nimelelewa na mama pamoja na bibi na babu yangu na familia ya mjomba angu tu ndio walikuwa watu wangu wa karibu......baba yangu simfahamu kabisa....(ila babu yangu ameshafariki kwa sasa)😮‍💨😮‍💨 kuna kipindi ilikuwa likizo ya chuo(nilikuwa mwaka wa kwanza) nikiwa najiandaa kurudi nyumbani mkoani (Tanga) kutokea dar es salaam...... mpenzi wangu anaitwa lameck (tunasoma wote) alinipatia simu....ila haikuwa mpya 🙄 niliamua kuuliza kuwa kaipata wapi...!? Maana Mmmmh! Sitaki matatizo akanambia kuna mwanafunzi mwenzetu pale chuo ndio kamuuzia sababu nauli imepelea,hivyo ameona auze simu yake apate nauli ya kwenda kwao....nikaona sawa😌😌 ukizingatia simu kali balaa😍😍😍mimi nilikuwa n smartphone ya bei chee tu😎😎😎hivyo nikaona nimepanda kidogo🤣🤣🤣nikawa nazo mbili,nikasafiri kurudi nyumbani kwetu Lakini baada ya wiki tu nilishangaa nakuja kukamatwa kuwa nina simu ambayo iliibiwa huko dar nilipotoka😓😓😓nililala rumande 🙆🏻‍♀️🙆🏻‍♀️mama angu alifika kesho yake kwa ajili ya kuniwekea dhamana 🥺🥺lakini ilishindikana wakasema tungoje mwenye simu yake afike kwanza😓😓hivyo nililala rumande siku mbili mpaka huyo anayesemekana kuwa ni simu yake aje Alikuja mbaba mmoja na binti ake....wakatoa maelezo kuhusu ile simu ni ya huyo mwanae,kuwa iliibiwa na wameifuatilia na kuona niko nayo mimi,mm pia niliwapa maelezo nilipoipata nikatoa namba za mpenzi wangu lakini hakupatikana sijui alifanya makusudi...!? Maana rafiki yangu alimpa taarifa jana yake kuwa nimekamatwa sababu ya simu 🙆🏻‍♀️🙆🏻‍♀️🙆🏻‍♀️ nikaona msala ni wangu tu😭😭😭ila yule mbaba akasema; "Binti mimi naona haya mambo hayana haja ya kufika mbali,mimi nachoshukuru ni kwamba simu imepatikana....isiwe kesi kubwa maana hata nawe pia umesema kuwa simu ulipewa tu haufahamu ilitoka wapi,hivyo naona haina haja tena kuendelea kumfuatilia aliyekugea... tutazidi kupoteza muda" "No daddy, inabidi tumpate huyo alomgea kama ametudanganya je na yeye ndio katuibia...!? Tutamuachaje bila adhabu?"yule mwanae alimbishia baba yake "Mercy, naongea mimi baba ako just kaa kimya" "Daddy Kwahiyo unatetea mwizi??? Aaah! Mimi hata sijapenda, yeye si kasema kapewa simu na mpenzi wake huyo mpenzi wake nae atafutwe akamatwe awajibishwe kwa wizi wake na usumbufu waliotusababishia" mtu na mwanae waliendelea kuongea mimi niko kimya tu,yule mzee alionekana amenihurumia na kuona hakuna sababu ya kunifikisha mbali maana simu yao wameshapata,ila mwanae sasa alikuwa hajaridhika🥺🥺eti mpaka wampate aliyenipa simu, wakati mpenzi wangu mwenyewe hakuwepo mkoa huo,nimemuacha dar huko huko.......na aliposikia kuwa mm nimekamatwa alitoweka hewani....kila akipigiwa simu hapatikani 😓😓😓 Baada ya mabishano mabishano pale hatimaye yule mzee aliamua kesi iishe tu na wakaondoka yeye na mwanae na simu nikarudisha kwao🥺🥺🥺mimi na mama yangu tukarudi nyumbani,mama alichukia sana na kuanza kunisema biashara ya kuchukua vitu vya wizi😁😁 sasa mimi sikujua maana mpenzi wangu alinipatia tu ,tena nilimuuliza akanambia amenunua kwa mwenyewe, mama akanambia ipo siku nitachukua simu kumbe mwenyewe kauwawa nitaishia jela😔😔😔halafu kumbe kanipeleka chuo mimi nimejiongezea na majukumu ya kuanza kuhangaika na mahusiano ngoja nipate mimba niishie njiani.....alinisema mpaka basi😓😓🥺 Nilimtafuta mpenzi wangu akawa bado hapatikani, nilimtafuta rafiki angu anaitwa Annet nikamwambia nishaponyeka na hiyo kesi😁😁huyo bae atanizimia simu bure😁😁😁akashukuru tu😍😍😍Baada ya siku tatu nilishangaa kuna polisi amekuja tena nyumbani 😳🙄 nikaona sasa kesi inarudi upya au😔😔😔 Yule polisi Aliniambia kuwa yule mzee amesema nipewe namba zake anataka kujua zaidi kuhusu huyo alonipatia simu🤦🏻‍♀️🤦🏻‍♀️🤦🏻‍♀️nikachukua namba na kumtafuta,cha ajabu akaanza niuliza nitarudi lini dar??? Nilimjibu mpaka likizo iishe bado sana.... akasema basi anataka anitumie simu ingine mpya, maana ile ndo washaninyang'anya Nikamwambia hapana mimi nyingine ya kutumia ninayo😰😰😰ila yule baba alisisitiza kwamba anitumie, nimwambie atume kwenye basi gani ambayo itanifikia kwa uhakika......Mmmmh...! nyieee kutiana majaribuni sindio huku sasa 🤣🤣🤣kwanini anitumie simu jamani🙄niliamua kumshirikisha shoga angu Annet maana nilihisi ni mtego🙆🏻‍♀️🙆🏻‍♀️🙆🏻‍♀️ ITAENDELEA 🌺🌺🌺 *MUBABA WANGU* 🌺🌺🌺 {02} Annet pia aliniambia nisikubali😎isije ikawa tatizo 👐 niliendelea kumkatalia yule baba kuhusu kunitumia simu....ila bhana akawa ananitafuta karibu kila siku 😎😎😎hivi mmehisi nachokihisi..??🤣🤣🤣 Yaani yule mubaba ni kila wakati alikuwa ananitafuta mpaka nikawa naogopa....siku moja akaniambia kuwa anapenda kusikia sauti yangu ndomana ananipigia mara kwa mara😎😎 nikaona huyu mzee mbona hajiheshimu buana😁ila nilijikuta nami namzoea mdogo mdogo😁😁😁akaniambia anaitwa mr Thomas nikamwambia mimi nitakuwa namuita baba tu maana ni analingana na mzazi wangu😁😁😁akaniuliza nasomea nini Nikamjibu Hatimaye likizo iliisha nikajiandaa kurudi chuo mama alinisomea risala ya maana akanitaka huyo mpuuzi wa huko chuo alonipa simu ya wizi niachane naye....nilimjibu kuwa nimemuelewa 😍😍😍nilimiss maisha ya dar😁maana isingekuwa kusoma nisingeenda dar😂😂🙌 nilisafiri kutoka mkoa hadi dar....nilifika salama....mr Thomas akanambia wiki inayofuata atanitafuta tuonane tuongee kwa muda huo amesafiri🌝kwani anataka nini huyu mzee eti..??🌝🌝🌝nilimjibu sawa.....siku niliyofika dar hatukulala yaani na roommates wangu tulikesha kupiga stori za yaliyojiri likizo..... nilitamani nionane na Lameck nitoe nyongo😌kwa matatizo aliyonisababishia😭😭😭na nilimkasirikia maana likizo nzima hakupatikana ng'o which means alibadili line kabisa... wakati sisi sio milima😁😁😁 Lakini cha ajabu tulivyokutana alinipet pet nikasamehe🙄🙄🙆🏻‍♀️bure🤣👐kwani bei gani?😁 akaniuliza habari za kesi.... nilimjibu yameshaisha😎 akanipatia na namba yake mpya na ile ya zaman akairudisha hewan coz aliitoa kwenye simu......Tuliendelea na masomo na hivyo tulikua tumeingia mwaka wa pili.... nikakumbuka mahusia ya mama alichonituma chuo ni kusoma🤣🤣na kwamba niachane na mapenzi.... mapenzi sawa nitaachana nayo ila Lameck ndio siwezi kuachana naye🙈🙈 Baada ya wiki mbili mr Thomas alinitafuta na kuniambia weekend atakuwepo dar, nitakuwa na nafasi tuonane...?? Niliamua kumshirikisha Annet kuhusu mr Thomas🥺 Annet akanambia atakuwa tu ananitaka😳😳😳kama vipi niishe naye tu🙄🙄mimi nikasema Hapana kwakweli naona kama nakosa adabu🤐🤐 si kama baba angu kabisa🙌🙌🙌 "Sikiliza nikwambie rafiki angu,wewe usiogope wala nini....haya ndio maisha ya sasa ebu usichezee bahati mwaya👌👌👌yaani kama ana hela wewe piga au unapenda kuteseka..!? Hapo unakuwa na malengo tu😁😁😁 sio kwamba unampenda au unapenda maisha ya kuteseka Eeeh? Na kupewa simu za wizi? " "Ndio nitembee na yule baba ni kama baba angu jamani...?" "Zubaa diha wewe si umeumbiwa kuteseka..!?" Annet aliendelea kunishawishi Dah...! Mpaka nikajiona kabisa yananiingia🤣🤣🤣nikamuomba basi twende naye siku ya kuonana na yule mzee akasema Hapana niende tu mm mwenyewe siku ya kwanza,ila niwe makini🙆🏻‍♀️ila marafiki jamani mnajua kupoteza wenzenu....unashangaa unapewa ushauri mpaka unaingia kwenye kumi na nane, nilijikuta tu nakubali kwa roho moja kwenda kuonana na Mr Thomas😔😔 madai yangu nikubali wito nikatae maneno🤣🤣🤣 Hiyo siku ilikuwa jumamosi jioni...mr Thomas akanambia atanifuata maeneo ya chuo hivyo nijiandae....mimi tena kwa msaada wa rafiki yangu Annet nilidamshi hatari😍😍alinichagulia code za kuvaa..... alinielekeza mahali alipo hakukuwa mbali na chuo.... nilitoka mdogo mdogo nikafika aliponielekeza nilikuta range nyeusi imepaki🔥🔥🔥ebu kwanza semeni renjiiiiiii🤣🤣🤣 ITAENDELEA 🌺🌺🌺 *MUBABA WANGU* 🌺🌺🌺 {03} Mr Thomas alishuka mule kwenye gari nilimsalimia😎akanifungulia mlango wa gari nikaingia naye pia akaingia na kuondoa gari...mimi hata sikuwa na amani kivile kila muda nilikuwa na nachat na Annet 🙄🙄🙄 namwambia naogopa 😁😁😁 akanambia niache ujinga 🤣🤣🤣wee nisiogope kweli mtu mwenyewe alikuwa haongei anadrive tu🙄mpaka tukafika mahali hivi getini akapiga honi geti likafunguliwa nyumba kali balaa🙄nikahisi ni kwake,alinikaribisha nikashuka nikamsalimia mlinzi nae akanikaribisha.... alinipeleka kwenye bustani kulikuwa kuna viti vinne na meza yake tukakaa pale alikuja mdada na kutusalimia kisha akatwambia atuletee kinywaji 🍷🍷akatuletea juice Mimi nilikuwa naogopa hatari.. yaani Annet ndio aliniforce kwakweli sikutaka kabisa🌝🌝nilikuwa naona ni vitu vya ajabu sana kuweza kuwa na yule mbaba ila Annet akawa ananiambia hizi ni kizazi cha wanaman niache ujinga 🤣🤣🤣 Mr Thomas akaanza kuniambia "Opra karibu sana hapa ni nyumbani kwangu, nimeona nikulete tuweze kuongea vizuri....hivyo jisikie huru kabisa". "Asante sana". "Vipi kuhusu yule kijana uliyesema alikupatia simu nakumbuka ulisema yupo dar hii..!" "Ndio nasoma naye chuo" "Anyway tuachane nae...sababu yeye sio lengo la kukutana hapa....pia kuwa na amani kabisa kuhusu kesi ya simu yameshapita....kuna mengi nataka kuongea na wewe" "Sawa nashukuru sana" "Okay..... najua unasoma chuo pia ulishanielekeza vizuri kuhusu unachosomea....hivyo nilitaka kukwambia kuwa ukazane kusoma ukigraduate vizuri nitakutafutia nafasi ya kazi". "Kweli...!?" Nilishtuka nyieee🙆🏻‍♀️🙆🏻‍♀️🙆🏻‍♀️ ''Yeah... Namaanisha kabisa" "Nashukuru sana,mimi nakuahidi nitajitahidi sana" "Sawa itakuwa vizuri,kitu kingine ni kwamba ilitokea tu nikavutiwa na wewe...japo tulikutana kwenye mazingira mabaya hivyo sikuona sababu niendelee kukuonea mtoto mzuri kama wewe japo nilikuwa nina uwezo wa kufanya kila kitu kwa ajili ya binti yangu afurahi,but sikutaka kuendelea kukusumbua" "Ahsante nashukuru tu kwa moyo wako mzuri babangu" "No mimi sina moyo mzuri,ni kwa sababu tu wewe ni mzuri😍😍 nilijikuta napoa sababu nilikuwa nina hasira binti angu kaibiwa simu na pesa zake hivyo nilikuwa natamani nimkamate huyo mwizi nimtie adabu....but nilipokutana na wewe nilijikuta nasamehe kabisa,sikuwa nashindwa tuendelee kumfuatilia huyo kijana aliyekupa wewe simu but sikutaka kuendelea kukusumbua....kisa wewe nikaona kesi niifutilie mbali" sikumuelewa buana😂😂kisa mimi kisa mimi nini....!?🙄🙄🙄 "Nashukuru tu" "Usijali,pia najua una mtu sindio?" ''Mtu wa nini baba?'' "Namaanisha mpenzi" nilishangaa sana kwanini sasa aniulize hayo huyu baba mm n kama mwanae 😳😳😳 "Nnaye" niliona nijibu tu maana kituo cha polisi nilishasemaga simu ile iliyonipatia kesi ilikuwa nimepewa na mpenzi 😌😌😌 "Oooh...! Anakutimizia mahitaji yako?" Nilibaha nijibu nini....!!! Kumbe kuna kutimiziwa mahitaji Eeeh...!!!🤔🤔🙄 "Ndio ananitimizia" "Kwanini unakaa hosteli" Eeeh mbona jamani huyu mzee ana maswali ya ajabu🌝🌝nilimeza mate kwanza kabla sijamjibu "Sababu kwetu ni mkoa mwingine, hivyo ni lazima nikae tu hosteli" "Lakini kuna wengine hapa dar hawana familia lakini hawakai hosteli,au unapenda kukaa hosteli" "Ndio napenda tu" "No why upende kukaa hostel..!?tafuta mahali mimi nitakupatia pesa ya kupanga.....your so beautiful u deserve better"😍😍😍nikaona ni kweli huyu mzee ananitaka😔😔😔Dah mwenzenu mimi mamangu kanituma kusoma😔😔😔 naogopa haya maswala halafu pia mr Thomas ni kama babangu🥺🥺 sitaweza "Unipangie...!'' "Ndio....Opra let's me be straight nakupenda sana naomba nipatie nafasi nikuonyeshe maana halisi ya mapenzi" ''Unanipenda mm!?🥺mbn mm ni kama mwanao....watu watatuchukuliaje...!? Mm siko tayari"🥺🥺 "Najua ni ngumu...lakini hiyo ndiyo halisi nakupenda na sijaona vema kuacha kukwambia ni uamuzi wako kufanya maamuzi utayoona ni sahihi kwako" Aiseeee mwenzenu niliona ni kitu cha ajabu🥺🥺sana nilimjibu tu haiwezekani kabisa kisha nikamuomba niweze kuondoka maana nimemuacha rafiki angu anaumwa na sasa hivi hajisikii vizuri naomba niende tu nikamuangalie🥺🥺🥺akasema ni sawa ananipeleka ila alinunuliwa zawadi alipokuwa amesafiri hivyo nimsubiri azifuate anipeleke kurudi aliponitoa ITAENDELEA 🌺🌺🌺 *MUBABA WANGU* 🌺🌺🌺 {04} Alielekea ndani na kurudi na mifuko miwili mikubwa.... Akaniambia kuwa naweza angalia tu... Nikamjibu mm mama angu alinikataza nikipewa zawadi kuzifungua hapo hapo🙄mpaka nifike tu nyumbani nitafungua(najifanya nina heshima)😁😁😁 nikamshukuru sana au akasema sawa,tukaanza safari sasa hapo muda wote nawaza hivi naanzaje kuwa na mahusiano na huyu mzee Loooh..! Siwezi nyiee mnawezaje jamani....!!!🙌🙌 Alinifikisha hadi karibu na hosteli nikashuka nikamuaga akanambia nizingatie alichonambia nikamwambia nitatafakari😌😌😌mieee shwaaa hadi ndani kwetu nilikuta Annet kajaa tele anasubiri umbea🌝🌝🌝sasa nimefika tu ndani sms ikaingia muda huo Annet akaja nipokea yaani ana kisebu sebu huyu😁mm nikawa nakazana kusoma sms ilitoka kwa mr Thomas...ilikuwa inasema "OPRA....KAMA HUTOJALI UNAWEZA NIAMBIE UNAHITAJI NINI....I MEAN MAHITAJI YAKO WEWE BINAFSI PIA USISAHAU HILI LA KUMOVE KUTOKA HAPO HOSTELI" Jamani huyu mzee utasema nishamkubali vile anajimilikisha😁😁😁sasa natafakari nijibu nini nakuta Annet kashafungua ile mifuko jamani🙄mfuko wa kwanza kulikuwa na magauni mawili na jumpsuit mbili..... mfuko mwingine ulikuwa na high heels mbili na sneakers mbili🤩🤩🤩kibox kina cheni, bracelet,vikuku na hereni zake🥰🥰🥰sasa nikawa nashindwa kumpa umbea Annet pale ndani maana wengine sio marafiki zake kivile hivyo nikamwambia twende nje tukale ili nipate nafasi ya kumpa umbea🙄🙄 Basi tulienda tukanunua chips na kuanza kupika stori huko huko huku tunakula.... nkamwambia Annet kuhusu yule mzee akanambia nikubali tu niache ujinga,ila niwe na malengo yangu nisijibweteke ukute ana mkewe.... nikamwambia Annet "Tena hilo ndilo naloogopa maana alinipeleka hadi kwake...na wala sijui kuhusu familia yake mm naogopa matatizo" "Inabidi muulize mama, usiache bahati hiyo sahivi wababa ndio wanaweka watu mjini dear....achana na hawa watoto wa elfu mbili... wanajikuta sana, unakuta mtu hakuhudumii bado anakupa stress akuuuu...! mm ndo vinanishindaga hivyo"👋👋👋 "sawa nitamuuliza,ila roho inasita"🙄🙄🙄 "Ebu acha hizo buana"👋🙄 "Sawa mamy....nitasikiliza ushauri wako"🤩🤩🤩 Tulipiga sana story tukarudi hostel nikamtumia sms mr Thomas kumwambia kuwa nashukuru kwa zawadi ni nzuri sana zote zimenikaa vizuri kabisa hata viatu vimenikaa vizuri ni kama aliijua size yangu maana nilijaribu vikanitosha........ akasema nisijali alikadiria tu maana ni mzoefu kununua vitu vya wasichana coz mara nyingi huwa anamnunulia mwanae, nikaona nimuulize hapo hapo "halafu mbona binti yako sikumuona pale nyumbani?" "Aaah..! alitoka tu atarudi kesho" "na vipi kuhusu mkeo maana sikumuona pia" "Mke wangu ameshafariki miaka miwili imepita sasa.... naishi mwenyewe na binti angu" "Pole sana" "Nimeshapoa tayari" "Nikutakie usiku mwema Mr" "Okay kwako pia....jaribu kufikiria yale niliyokueleza" "Sawa nitakupatia jibu" "Itachukua muda gani?" "Almost siku nne"🙈🙈🙈 "Sawa mrembo" Buana buana nikaanza kupata tamaa🤣🤣🤣si niwe nae tu huyu baba buana🙄🙄🙄yaani nimpotezee huyu mubaba kisa Lameck? na Lameck mwenyewe tulianza mahusiano pale chuo sikuwa na uhakika nae kivileee na ndio yeye alikuwa mpenzi wangu wa pili,wa kwanza tuliachanaga kipindi hiko nilikuwa form six alioa mdada mwingine nililia kama nyau🤣🤣🤣sasa napiga mahesabu nisije muumiza Lameck na huyu mzee mmh..! pengine anataka tu kunitumia 😥😥😥 kingine magonjwa mengi😭😭😭hizi tamaa zisije niponza miyeee, mamangu ananitegemea sana😔😔😔roho nyingine inanambia niache ujinga nikubali🤣🤣🤣 Zile zawadi niligawana na Annet,maana kwakweli ni bff wangu tangu form five tulisoma wote,nimemzoea sana na tunasaidianaga mno.....hivyo vile vitu nikampea na yeye...nyieee ushoga kazi😁😁😁 zikapita siku tatu mr Thomas alikuwa kimya 🤔🤔yaani nikasema au hanitaki tena na.mm tamaa ishaanza kunikolea kumkubali tu😂😂😂hapo ilikuwa siku ya jumatano natamani nimtafute🤔🤔🤔nikawa nasita tu😥😥😥 tukawa tumetoka kwenye kipindi na Annet tukapita mahali tupoze koo kwa juice🧃🧃Mr Thomas akawa amenipigia akanambia hii wiki alikuwa bize sana kazini (yeye ni wakili) ndio maana alikuwa kimya kimya na mbona hata mm simkumbuki japo kumsalimia maana amenimiss kuniona niko wapi anijie🙄🙄 nikamwambia niko karibu na chuo niko na best angu tunakunywa juice,akasema basi tumngoje anapitia hapo kutuchukua na huyo best angu....Annet kusikia vile akasema tumngoje na yeye akumuona maana alikuwa hamjui namuhadithiaga tu ITAENDELEAAA 🌺🌺🌺 *MUBABA WANGU* 🌺🌺🌺 {05} Tulikuwa tunaona uvivu hata kurudi hostel kuweka vitu vyetu....tulimngoje hivyo hivyo.... baada ya lisaa limoja ndio alifika tukaondoka nae......hatukwenda mbali sana alipaki gari la kuanza kuongea,nikamtambulisha kwa Annet kuwa ni rafiki yangu kipenzi akasema anashukuru weekend atatufuata atutoe out sisi tukaitikia tu ni sawa..... alinipatia mawigi mawili et mwanae alimuagiza so ameona aninunulie na mm🙈🙈🙈jamani jamani niliyapokea akatushusha pale sisi tukarudi zetu hostel....Annet akasema huyu mzee we mchune tu mama👌👌👌ila mcheck afya usijiaminishe sana,isije ikawa anataka kukukomoa bure mama" "Nimekuelewa mama,ila Lameck sijui itakuwaje " "Hahaha halooo unamuwazia Lameck...!?mdomo koma mieeeee" "Kuna nini kwani?"🙄 "Hamna kitu shoo ngoja ninyamaze ty" "Jamani si uniambie au unipe ushauri nawapanga vipi??" "Sikiliza shoga angu Lameck unamuwazia nae hata sio loyal ujue " "Unataka kumsingizia sababu ya huyu mzee?" "Akuuu ila likizo kuna viwanja nilikutana nae"🙈🙈 "Viwanja gani?"🙄 "Huko maclub ila sikutaka kusema kukuharibia furaha zako" "Sasa mtu kwenda club n kosa Annet?"🙄🙄🙄 "Alikuwa na mtu buana ila nilimuahidi sisemi"🙄🙄🙄 "Annet Annet kuna kiama Annet wewe jizidishie tu dhambi"👌👌 "Wallah vile,hivyo usimtegemee sana" "Kwahiyo ungekaa na hiyo siri mpaka lini??" "Buana tuachane nayo basi " "Sijapenda" "Eeeh...! Wewe jitulize buana Lameck endelea nae na huyu mzee enda nae cha msingi ujitambue tu, hakuna cha peke ako kumbuka....Lameck weee muweke tu kwa hizo siku zijazo uwezi jua labda ndo mumeo" "Haya mama,sasa ole wako uwe umetunga ili nimkubalie huyu mr Thomas " "Huu ni ukweli jamani'' "Poa mama" Tukawa tunarudi hosteli mdogo mdogo,mara tukakutana na Lameck ndio anaelekea kwake,huwa amepanga karibu na chuo akanambia niende naye kwake 🙄mm nikawa nasita maana nilishasikia wivu kwa yale aliyoniambia Annet kuwa aliendaga club na vimwana 😌😌 japo sijui ni kweli au Annet anasingizia🥺🥺 Annet akasupport niende, akachukua na vitu vyangu kwamba anatangulia navyo hostel,mm nikaondoka na Lameck mpaka geto kwake..... tumefika sasa mimi nimekaa nikawa najibu sms ya mr Thomas aliniuliza kuhusu jibu lake nikamwambia nikamjibu weekend tukionana😁😁😁 "Ile gari nyeusi mliyopanda ni ya nani?" Nilishtukia swali kutoka kwa Lameck🙆🏻‍♀️🙆🏻‍♀️ nikashangaa aliona tukipanda gari la mr Thomas 🙄kwani kudanganya shingapi......!!!???😁😁 "Ni ya anko wake Annet alikuja msalimia" "Sio anko wako wewe?" "Hapana"🙄 "Oooh..! Kweli uliniambia kuwa huna ndugu hapa dar....lakini huna uhusiano gani na huyo anko wake Annet? Maana leo sio mara ya kwanza kupanda lile gari...!" "Mimi...!?"🙄🙄 Nilijifanya kushangaa,macho makavu "Hapana sio wewe,mm ni chizi naongea mwenyewe" "Dah babe hayo yanatokea wapi" "Jibu milichokuuliza" "Mm sijawahi kupanda lile gari zaidi ya leo...sasa sielewi haya maswali yako yanatoka wapi..!?" "Basi labda ulipanda lingine,ila siku kadhaa kuna mwanangu amenambia ameshuhudia kwa macho yake unashuka ndani ya gari range.....sasa naomba tu uwe clear mm kupangwa siwezi" "Atakuwa amenifananisha huyo rafiki yako,mm sijawahi hiko kitu.....halafu mbona sio sawa kusikiliza marafiki maana wanaweza kudiriki kusema kitu cha uongo tukaishia kugombana"🙄🙄 "Ooooh...! Sijamsikiliza ndio maana sijakuuliza tangu aniambie,ila nimeona leo nkuulize coz nimeona mnapanda kwenye garia aina hiyo hyo alioniambia rafiki angu nikaunganisha matukio...ila tambua Nakupenda sana sitaki kuona unanizunguka" ''Na mimi nakupenda"🥺🥺🥺 Roho sindio ikaniuma mwenzenu🥺🥺sijui nimpoteze tu mr Thomas nibaki na Lameck tusije kosana🤐🤐🤐ila nikifikiria mr Thomas mtu na pesa zake😁😁😁tamaa ishanijaa hujamuomba zawadi anakupa Lameck hajawahi ninunulia hata pipi iliyo expire zaidi tu ya ile simu iliyonipa kesi.... nachoka miyeeee ITAENDELEA 𝐅𝐔𝐋𝐋 𝐒𝐓𝐎𝐑𝐘 𝟏𝟎𝟎𝟎 𝐖𝐇𝐀𝐓𝐒𝐀𝐏𝐏 Chombezotu.blogspot.com

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA

Mpya zaidi Nzee zaidi

Ads related

Smartwatchs