mwandishi:romantic voice
Chombezotu.blogspot.com
1~~~~~5
THE WRONG NUMBER 1
kuna muda kwenye maisha tunakuwa na haraka Sana ya mambo na Hali ya kuwa Mungu ndio mpangaji wa hatma yetu.
Ngoja niwape Kisa changu ili tuone namna wakat wa Mungu ulivyokuwa wakat sahihi.
Siku Moja nilikuwa nimetoka kazin, na siku hio ilikuwa ni siku mbaya sana kwangu, maana mchana wa siku hio nilimfumania mpenzi wangu akiwa anamkiss mfanyakazi mwenzetu, maana sote tulikuwa tunafanya kazi sehemu Moja, nilikuwa kwenye maumivu makali, maana nilikuwa nampenda na kumuamin sana huyo mwanaume, na kwanamna ambavyo alikuwa ananihandle ungeweza ukadhan hakuna mwanaume kama YEYE Dunian.
Niliumia sana na kutaman kupiga kelele ili kila mtu ajue maumivu yangu, alunipigia simu mara kadhaa ila sikupokea maana nilijua kuwa anataka kuniongipiea so sikutaka kabisa kuzungumza nae.
Majira ya kama saa nne usiku iliingia sms ila hata sikujiangaisha kujifungua maana nilihisi atakuwa ni morson maana ndio lilikuwa jina la mpenzi wangu.
Baada ya kama dakika tano simu yangu ikaanza kuita ila wakat huu niliangalia ni nani anapiga maana ilikuwa ni namba ngeni, niliisogelea simu yangu na kulipokea ili nijue anaepiga ni nani.
Ilikuwa sauti ya kiume tamu ambayo ilipenya kwenye masikio yangu na kwenda kuutukisa moyo wangu,
"Hellow, ulisikika upande wa pili mara baada ya kupokea simu.
"Hellow na mm nikajibu.
"Oww samahan kwa kukusumbua najua haunifahamu ila naomba unisaidie jambo, akasema huyo mwanaume.
"Bila shaka, karibu nakusikiliza,nikasema.
"Samahan mrembo nimekosea kutuma pesa kimakosa ikaja kwako, kama hautajal naomba unirudishie maana ni pesa ya muhimu sana kwangu kwa wakat huu, akasema huyo kijana na wakat huo huo nikaingia upande wa sms na kuangalia kama ni kweli kuna hio pesa anayosema, na kweli nikakuta kama laki sita.
"Nimeiona naomba namba ya muamala nikutumie pesa yako, nikasema na yule kaka wakat huo huo akanitumia namba na jina na baada ya dakika chache nikamtumia pesa yake.
Mara baada ya kutuma pesa akapiga simu wakat huo huo na kuanza kunishkuru.
"Asante sana mrembo, sijaamin kama kuna watu kama wewe kwenye Dunia yetu ya Leo, nimejikuta nataman kukufahamu zaidi, akasema yule mwanaume.
"Naitwa Zinath, nikasema.
"Owww unajina zuri mm naitwa Fahad, akajibu yule mwanaume na mm kwa sauti ya unyonge nikajibu kuwa "nashkuru kukufahamu Fahad.
"Mbona kama unaongea kinyonge sana, upo sawa kweli mamaa, akasema Fahad.
Nikajikuta naanza kulia maana hata SIKUJUA natakiwa kujibu nn, akawa kimya ananisikiliza ninavyolia, na kiukweli kitendo Cha mm kulia na kukawa na mtu wa kunisikiliza kulinipa faraja sana.
"Lia TU mamaa mm nipo kwaajili yako, akasema Fahad na ndio nikazidi kulia, jaman nililia kwa takriban nusu saa, Kisha nikanyamaza na mara baada ya kunyamaza Fahad akakohoa kidogo Kisha akasema "nisawa kulia zinath maana muda mwingine ili tujisikie vzr ni lazima kutoa chozi so naamin angalau kidogo umekuwa sawa,sio Siri maneno yake yalinifanya nijisikia vzr sana na kujikuta namshukuru TU maana sio Siri nilikuwa nasikia aman sana ya moyo kwa maneno yake.
"Unaishi wapi? Fahad akaniuliza
"Nipo Arusha huku majengo, nikajibu.
"Owww mm nipo dar es salaam lakin mwisho wa mwezi naweza kuja huko, naomba usikatae kuonana na mm, akasema na kiukweli nikajikuta nakubali haraka haraka kama kachizi vile😃😃😃.
"Ila sio utani unasauti tamu, akasema Fahad na mm nikajikuta natabasamu na kuona aibu na wakat hata mtu mwenyewe hayopo hapo.
.
"ACHA utan bana siwez kukufikia wewe na mm nikasema....
"Mm Sina sauti tamu kama Yako, huon kama nashindwa kukata simu Toka nimekasikia kasauti chako Cha kichokozi, akasema Fahad na mm nikatabasamu Kisha nikajiambia na mm nianze kumpamba sasa.
"Yaan mwenzio nilikuwa na majonzi ila niliposikia hio gentralman voice Yako nikajikuta hasira zote zimeyeyuka, seriously una gentralman voice Fahad, nikasema.
"Owww wow, kweli, hivi nikisema nikupende nitakuwa na makosa kweli, maana maneno yako mm hoi huku, akasema Fahad na mm nikawa najichekea TU nikiwa najua ni utani tu na kuna uwezekano nisionane na Fahad au nikimuona asinivutie, kwanza nimetoka kufumania so nilikuwa natakiwa kuushukilia moyo wangu uache kiherehere😃😃
"Owww kunipenda ni wewe TU na moyo wako, ila kwangu ruksa kama una hela TU, siunajua sisi WAnawake na pesa ni ndg, nikasema.
Jaman Fahad alicheka Kisha akanambia "muda umeenda, shemeji asije akaanza kushangaa unaongea na nani, na mm kwa kujisahau sijambo, ila tatizo sio mm tatizo ni sauti Yako, yaan mpaka nahisi nikikata simu nitakuwa nimefanya makosa makubwa sana, akasema Fahad.
"Mm nasomea usister bana, kwa hio, michezo ya kikubwa siijuagi, nikasema jaman Fahad alicheka sana Kisha akasema "akat unaonekana kabisa ni fundi, any way usiku mwema mamaa maana mm natakiwa nipumzike sasa ili kesho nisije kuchelewa kazin, akasema Fahad na mm nikatabasamu Kisha akakata simu.
Yaan nilijikuta nakumbatia simu na kusahau kama nimetoka kufumania siku hio, yaan siku hio nimelala na tabasamu kubwa kwa mtu ambae hata simjui ila mapenzi ni upuuzi sana.
NAKUJA
WRONG NUMBER (Mr romantic voice) 2.
Basi usiku wangu wote ulikuwa ni WA furaha maana nilikuwa navuta taswira kama nipo na Fahad vile, yaan mwanaume hata simjui ila namuimagine TU.
Basi asubuh nikaamka na kuanza kujiandaa kwenda kazin ila wakat najiandaa mara simu yangu ikaanza kuita kuangalia ni Fahad, na niliemsave Fahad na kaalama Cha kopa nyekundu maana aliutetemesha moyo wangu ghafla ghafla TU.
"Hellow mrembo umeamka je, ukasikika upande wa pili baada ya mm kupokea simu
Yaan sauti yake TU mm hoi taaban jaman, nikajikuta naanza kutabasamu kabla ya kumjibu chochote kile.
Nikajikohoza kidogo nikijiandaa kubana sauti na mm ili nisiwe nyuma na kujibu "Salama.
"Owww wow uko Salama kweli na kasauti Kako akasema Fahad nikajikuta natabasamu.
"Sijambo Mr romantic voice nikajibu akacheka Kisha akanambia "ila wewe mchokozi, any way hakikisha Leo hakuna mtu atakae sababisha ulie, akasema Fahad.
"Nitajitahidi na wewe kuwa makin, nikasema
"Wewe nijali TU ila nikiangaza kukupenda usinilaumu, akasema Fahad nikajikuta natabasamu Kisha nikajibu "lazima nikulaumu sasa kwann unipende.
"Kwa sababu you are so adorable, akasema nikacheka Kisha nikamwambia mm nachelewa kazin bana tutaongea baadae.
Akapunguza sauti na kuongea kwa sauti ya chini akasema "take care,Kisha akakata simu.
Nyie nilihisi kuvurugwa na hicho kisauti chake yaan unaweza ukadhan ni mwanaume anakaribia kufika namna ambavyo kinasisimua,nikajikuta natabasamu.
Nimefika kazin yaan Sina habar na Morrison Wala kimada wake, wakat naingia nikapishana na huyo dada nikamsalimia Kisha nikaendelea na mambo yangu, hapo YEYE anajishuku balaa na Wala sikumzingatia, yaan nilikuwa nawaza TU ile sauti jaman jaman, au Fahad ni mchawi nn maana naona kama ameniloga ghafla sana.
Kuna muda wa mapunziko kidogo pale kazin Morrison akanifata akawa anataka kuongea na mm.
"Shida Yako, nikamuuliza
"Naomba tuongee akasema morson
"Nakusikiliza, nikamjibu
"Mambo hayako kama ulivyofikiria zinath, yule bint alikuwa ananilazimisha na sikuwa nataka, akasema Morrison na mm nikawa namuangalia TU anavyonidanganya, anasema kalazimishwa na wakat nilikuwa naona kabisa namna ambavyo alikuwa anatoa ushirikiano, sikutaka kukimbizana nae nikamwambia TU mm na wewe basi.
Ni kama hakuamin masikio yake, maana alitegemea bado nitamlilia, kwa kweli nimechoka kulia kwa sababu ya mtoto wa mtu, maana nimelia sana kwaajili yake na kila siku nimekuwa ni mtu wa kumuomba msamaha hata kama makosa ni yake, ila safar hii kagonga mwamba, kwa kweli sikutaka kurudi nyuma na nikawa nataka kumtumia Fahad kama mtu wa kunisaidia kulipiza kisasi kwa maana sikuwa na mpango wa kuwa na mahusiano serious maana niliona kama mapenzi ni ujinga, maana huyu Morrison nimekaa nae kwenye mahusiano kwa takriban miaka mitatu na akaniahid kuwa atabadilisha dini kwaajili yangu ila haikuwa hivyo na siku zote amekuwa kama tapeli kwangu, kwa maana hakuna jambo hata Moja ambalo alilisema na akalitekeleza.
Morson alihisi kama namtania, alijua labda nitamlilia kama nilivyokuwa nalia Lia.
Nikawa hata simsemeshi Wala simnunii ila sikutaka kabisa mazoea nae, akaanza kunifuatilia ili ajue kama Nina mahusiano mengine.
Siku Moja Fahad alinipigia, alikuwa anataka nimshauri kuhusu nguo ambayo ataivaa Siku hio, yaan ilikuwa ghafla sana kwa Fahad maana alinipa sehemu kubwa ya maisha yake, kwamaana alikuwa ananishirukisha kwa kila anachokifanya, mpaka nikawa nashangaa, maana mm nilitaka kumtumia TU kwaajili ya kumuumiza marson na Sio kuwa nae, maana kwanza simjui so siwez kumuamin haraka kiasi hicho.
Sasa wakat naongea nae nikamuona morson anapita nikaongea kwa sauti kuwa "hakikisha unavaa shart jeupe na suruali ya dark blue maana hizo nguo zinakupendezaga sana mume wangu, nikasema.
"What embu rudia ulichosema zinath, akasema Fahad na wakat huo morson akasimama Kisha akageuka upande ambao nilikuwepo Kisha akawa ananifata huku kakunja sura, nikaanza kuogopa sasa.
Unafikiri ni Kwann Fahad ameshtuka na kwann morson anamfata zinath.
USIKOSE KIPANDE KINACHOFUATA
WRONG NUMBER (Mr romantic voice) 3
Morson aliponikaribia nikakata simu kwa uoga maana namjua akiwa na hasira, "kwa hio umeshapata na mume kabisa, kwa hio uliniacha kwa sababu ya mwanaume wako, akasema morson kwa sauti ya ukali.
"Unajua morson unanichukuliaga kama mnyonge sana yaan, unanichukuliaga kama bwege lako ambalo unaweza kulifanya utakavyo, ni hivi Mimi Nina mahusiano yangu na nampenda mwanaume wangu so achana na mm, nikasema Kisha nikaondoka zangu.
Nafika ofisin nashangaa Fahad ananipigia simu, nikapokea Kisha akanambia "ulikuwa na nani wakat ule?.
"Wakat upi Fahad, nikamjibu
"Wakat ambao nilikuwa nakuomba unichagulie nguo ya kuvaa, mbona kama ulikuwa unaongea kama unataka kumrusha mtu roho, kuna mwanaume anakusumbua hapo kazin, akasema Fahad.
Nikakata kimya kwa sekunde kadhaa Kisha nikamwambia hakuna mtu anaenisumbua maana sikuwah kumsimulia kuhusu morson so sikuona busara kuingiza Hilo jambo hapo.
"Zinath unakumbuka ulivyoniita mume wangu, au ulisema TU, akasema Fahad.
"Oww Fahad ni kwamba huniamin, au hujapenda nilivyokuita mume wangu ety, kama hujapenda nambie na sitorudia, nikashangaa kama anapatwa na kigugumizi Cha ghafla Kisha akanambia "sijasema kama nimechukia mamaa,ila naona kama umepania kunivuruga, akasema Fahad namm nikatabasamu Kisha nikasema "nikuvuruge kwa nn honey.
"Owww zinath ACHA basi, au umepania kunifanya niache kufanya kazi niwe nakufikiria TU, ila ni ghafla sana maana hakuwah kuonesha kama unanipenda hata siku Moja na hata nilipokuwa natupia tupia maneno ya kichokozi ulikuwa unayakwepa, "naomba usinitanie zinath na unambie ukweli, ni kweli umemaanisha ulichokisema? Akauliza Fahad.
Nikawa kimya kwa sekunde kadhaa nikashangaa Fahad anasema kuwa "it ok, Hauna haja ya kuniambia kwenye simu, Kwan this week nakuja Arusha nataka uniite mume wako ukiwa unanitazama uson, akasema Fahad.
Kiukweli nilijisikia vibaya maana mm sikuwa na lengo la kumpenda hivyo anavyodhan ingawa sauti yake inanivurugaga, ila nilikuwa nataman sana ajue ukweli kuwa mm sipo kama anavyonifikiria kabisa.
"Zinath take care kwaajili yangu, akasema kwa ile sauti yake ya kuninong'oneza ni kama alishagundua kuwa akiongeaga sauti flan anakuwa ananivuruga kabisa yaan.
"Sawa Fahad na wewe jichunge, nikasema kwa sauti ya chini.
"ACHA basi, kwann lakin unanifanyia hivi mamaa, akauliza Fahad.
"Nimefanya nini tena jaman, nikasema.
"Next time ukitaja jina langu hakikisha upo kwenye kifua changu au niwe na kukiss, maana the way you call my name (namna unavyotaja jina langu) unanivuruga sana, akasema Fahad.
"Alafu muda ule nilisikia kama sauti ya ndevu, usikute una mwanaume alafu unakuja kuniroga na mm, akasema Fahad.
Nilicheka sana Kisha nikamuuliza "hio sauti ya ndevu ndio ikoje, alafu mm Sina mwanaume ila naogopa, nikasema.
" Aaa usiogope bn nitaweka kichwa TU, akasema Fahad.
Jaman nilicheka sana maana sikutegemea kama atasema vile, basi tutaongea maneno mawili matatu Kisha tukaagana, hapo kamoyo kangu kakisikiaga sauti ya fahad kanatulia kweli ila ndio hivyo najiambia kila wakat kuwa siko tayar kupenda.
Sasa nimekata simu ya Fahad hapo nacheka Cheka kama nimepewa offer ya abaya la idd🤣🤣🤣, naangalia mlangon nashangaa namuona morson ananikata jicho la chuki, ila sikujal, nikajifanya kama sijamuona na kuendelea na majukum yangu mengine.
Nikashangaa anaingia ofisin kwangu Kisha akashika meza akawa ananiangalia kwa chuki, Kisha akasema "nitakutoa lunch, akasema morson kwa hasira.
"Kwan lazima bro, embu achana na mm, na naomba uondoke ofisin kwangu maana Nina kazi nyingi za kufanya, nikasema
"Mimi ni mwanaume na bado hatujaachana so bado KAULI yangu ni amri kwako, akasema morson.
Nikabana pua Kisha nikasema "Mimi ni mwanaume na bado hatujaachana so bado KAULI yangu ni amri kwako, hivi wewe unakichaa, nahisi kama akili zako haziko sawa, ndio wewe ni mwanaume sijakataa maana unapumbu mbili zimening'inia, lakin Hauna mamlaka ya kunipangia Cha kufanya maana mm na wewe ukurasa wetu umeshafungwa na siwez kuwa na wewe tena, hata iweje, nikasema na morson akataka kunipiga kibao nikakidaka Kisha nikasema "Mimi Sio zinath wa zaman, yaan ukisubutu kunigusa jua jela itakuhusu maana najua kabisa unakijua kichaa changu, nikasema na morson akasunya Kisha akaondoka zake.
Alipokuwa anaondoka nikamzomea maana nilimuona kama fungu la kukosa tu, maana Hana jipya tena.
Basi weekend ya wiki hio Fahad alikuja, akataka nikampikee, jaman ni super handsome mpaka nikajikuta natabasamu mara baada ya kumuona, nikajikuta nasahau kuushikilia moyo wangu kama ninavyojiambiaga maana najikutaga mwamba na kujiambia kuwa nataka kuwachezea wanaume, na wakat najiambia sikuwah kumuona Fahad live, maana badala ya kuwachezea wanaume nitajikuta nachezewa Mimi.
NAKUJA
: WRONG NUMBER 4.
(Mr romantic voice)
Basi akaniomba nimpeleke sehemu ya maana kwa haraka haraka nikawaza Naura spring, sikuwa na uhakika na huduma zake maana sijawah kuingia ila Fahad alikuwa anaonekana kama mwanaume wa kwenda, yaan alikuwa anaonekana kama mtu flan hivi superstar, mpaka nikawa najikuta sijiamin nikitembea nae, maana watu walikuwa wanatushangaa sana, nikawa najiona kama kahouse girl TU mbele ya Fahad, Fahad akataka
kutembea na mm akiwa kanishika mikono nikamzuia, akaniangalia nikajikuta natabasamu TU.
Tumefika tukaagiza chakula, muda wote Fahad ananiangalia hapo moyo wangu unaruka danadana balaa, yaan nilikuwa najiona napotelea penzin, ila nikajiambia kuwa nijishkilie maana mwanaume mwenyewe ndio kwanza tunaona alafu najikuta navurugwa kiasi hichi, naelekea kupotea sasa nikawaza.
"Hivi Unajua kwamba wewe ni mrembo, akasema Fahad na mm nikatabasamu TU maana SIKUJUA hata natakiwa kufanya nn.
"Your eyes, your lips na hako kapua chako sasa kama kamebandikwa, akasema Fahad na kuniacha speechless.
"Kuna muda nataman nataman ningekuwa hicho chakula unachokula ili nionje ladha ya mate Yako, akasema Fahad
Hivi mnamuelewa huyu, yaan kama hamumuelewi hata mm simuelewi, nikaanza kujiambia kuwa huyu atakuwa ni Malaya huyu, na kwa muonekano pamoja na sauti yake nikajiambia kuwa lazima atakuwa ni wale wanaume wanaochezea wanaume so natakiwa kujishkilia nisije nikalia Bure.
Nikakaza macho Kisha nikamuangalia,"ACHA basi hizo, mbona unaningalia kama unataka kunimeza, akasema nikajikuta nacheka maana nilitaka kumuwekea wambuzi ili nisizame mazima maana nilikuwa najiona kabisa kuwa napotelea kwa Fahad.
"Ila siulinambia kuwa hata nikikupenda hakuna tatizo sasa Mimi naku.... Akawa anasema Fahad ila kabla hajamaliza KUONGEA nikadakia Kisha nikasema "naomba unisaidie, samahan maana mm nilikuwa nakutumia TU, nikasema na Fahad akatoa macho maana alidhan kuwa nitapagawa na u handsome wake, nikweli nilipagawa ila niliamua kuishikilia nafsi yangu, kwa maana bado natakiwa kumuangamiza morson.
Nikaona Fahad kanywea sana Kisha akaniangalia kwa unyonge mpaka nikajisikia vibaya Kisha akasema, "your my friend na nipo hapa KUKUSAIDIA.
"Unakumbuka ile siku ya kwanza ambayo nilikuwa naongea na wewe, nikasema.
"Ndio nakumbuka siku ambayo nilikosea namba, akasema Fahad.
" Ndio hio hio, sasa kuna wakat tukawa tunaongea Nikaanza kulia, nilikumbuka tukio nilioliona mchana wake, samahan Fahad ila nilimshuhudia mwanaume wangu akifanya romance na mfanyakazi mwenzetu, nilihisi kuvurugwa, na Sio Siri namshuru Mungu kwa kukuleta siku ile na kukufanya ukosee namba, maana nilikuwa nafikiria kufanya jambo baya sana ila angalau ukanituliza, naomba unisaidie Fahad kumuumiza huyu mjinga maana alichonifanyia ni zaidi ya unyama, nimemfumania sana ila sasa ni wakat wangu wa kumuumiza na YEYE, anatakiwa kujuta, anatakiwa kulia kuliko alivyoniliza, anatakiwa kuniona Nina furaha na Nina mwanaume Bora kuliko YEYE, naomba nisaidie Fahad,nikawa nasema huku nalia.
Fahad alinisogelea Kisha akanikumbatia, yaan namna ambavyo alikuwa ananukia na kifua kilivyotanuka nikajikuta Hadi nasinzia.
"Usijal zinath nipo kwaajili yako, embu nambie umepanga nn kwa sasa, akasema.
"Naomba twende photoshoot tukapige picha nikasema.
"Oww sawa twende, siunajua ombi lako kwangu amri, akasema Fahad nikajikuta nacheka.
Basi tukaenda photoshoot, hayo mapozi yake sasa ni kama alikuwa anataka kunichanganya TU hakuwa na kingine.
Yaan mara aniangalie kama ananitaman, mara anikiss shavuni, mara anibebe, mara anishike kiuno, nikiuliza ananambia kuwa ni lazima huyo mjinga aamin kuwa sisi ni wapenzi so nisimzuie, yaan alivyokuwa anasema ni kama nilikuwa na ubavu wa kumzuia, kwa maana kila alichokuwa anakifanya kilikuwa kinanipa Raha sana.
Tumemaliza kupiga picha akanishika mikono Kisha akanambia , "anaishi wapi huyo mjinga au mida kama ile atakuwa wapi, nikamjibu kuwa anapenda kwenda sehemu Moja imetulia sana, mara nyingi akiwa Hana kazi anapendaga kwenda huko.
"Subir Kwan si una namba yake, akasema Fahad Kisha nikaitikia kwa kutikisa kichwa kwa ishara ya kukubali.
Embu nipe simu Yako, akasema na mm nikampa akanambia nitaje namba, nikataja, nikashangaa kabadilika ghafla alafu akajikohoza na kusema "inaonekana bado unampenda kwa maana haujabadilisha hata jina ulilomsave maana bado naona umemsave my darling, akasema Fahad kana kwamba hakupendezwa kukuta sijabadili jina la morson...
"Nilikuwa kama nimechanganyikiwa ila simpendi na sitakaa nimpende hata siku Moja ya maisha yangu, nikasema na Fahad akatabasamu Kisha akasema hakuna shida.
Akaanza kumtafuta morson kwa Google map, na location ikawa inaonesha kuwa yuko ccm mkoa, akaniuliza kama napafahamu, nikamjibu ndio napafahamu maana YEYE hakuwa mwenyeji sana wa mkoa wa Arusha.
Basi tukaanza kushuka taratibu kuelekea huko maana hatukua mbali sana na Hilo eneo.
Akaomba nimuoneshe picha nikamuonesha na mara baada ya kumuonesha akasema sawa twende.
Basi tukaenda mpaka kwenye ile bustan pale ccm mkoa, akawa anaangaza angaza, mara Fahad akamuona morson ila mm sikumuona, akanishika mkono Kisha akanipokea pochi, na baada ya hapo akataka tupite sehemu ambayo alikuwa morson na nimuegemee began.
Mm Ni nani nisikubali jaman, nikakubali haraka haraka Kisha nikamuegemea kama alivyosema Kisha tukawa tunatembea na mm muda wote sikuwa nimemuona morson kumbe Fahad anatarget yake.
Nikashangaa mtu katokea nyuma yetu akamkwida Fahad.
Fahad hata hakuwa na wasiwasi, akageuka kwa mapozi Kisha akamuangalia yule aliemkwida na kusema "una shida Gani wewe,mbona unanivamia unanijua? Akauliza Fahad.
"Wewe ni nani mpaka umshike MWANAMKE wangu, Unajua huyo unaekumbatiana nae ni nani kwangu,ni mke wangu, akasema morson na Fahad akanigeukia kwa mshtuko Kisha akasema "Kwan wewe ni mke wa mtu, owww zinath kwann hukunambia, akasema Fahad.
"Hapana bby mbona mm simjui huyu, ety kaka unanijua mm, naomba usiniharibie kwa mume wangu mtarajiwa, mm sijawah kuolewa ila nakaribia kuolewa so naomba usivunje uaminifu wangu kwa mume wangu kipenzi, nikasema Kisha nikaubusu mkono wa Fahad.
Morson akawa mwekundu na hivi alikuwa mweupe, Kisha akasema ni lazima nikufundishe ADABU na kuondoka zake ila Hilo halikumtisha Fahad na badala yake akanishika mkono na kuniambia nataman ingekuwa kweli.
Basi siku hio ikapita na usiku ilikuwa ni siku ya kupost picha zangu mm na fahad.
Yaan nikachagua zile ambazo zilikuwa na mapozi konki ndio nikazipost.
Saa hio hio morson akanipigia, sikupokea.
Simu ilivyokata akapiga Fahad, nikapokea haraka haraka maana sikutaka kabisa KUONGEA na morson.
"Embu nambie huyo mjinga amekupigia, akauliza Fahad.
"Ndio nikajibu Kisha Fahad akaCheka na tukaanza kupiga zetu story, yaan Fahad ni zaidi ya comedian maana anavituko sana.
Hapo morson kapiga simu karibu mara 30 na mara Zote akipiga anakuta natumika, basi nikaongea na Fahad kwa takriban masaa mawili Kisha akaniomba alale na kukata simu.
Alipokata simu TU nikashangaa sms kutoka kwa morson ikaingia inasema "wewe Malaya ongea na simu mpaka asubuh na Wala huniumize na ukimaliza KUONGEA nenda ukat*mbe*e.
NAKUJA
WRONG NUMBER 5.
nikawa namuona morson kama fungu la kukosa TU, sasa ananitukania nn na wakat anawanawake wake.
Basi nikampiga block maana sikutaka kuona sms zake za kupuuzi tena maana niliona kama nitaendelea kuhifadhi namba yake, basi kuna siku atanikera sana Nije kujuta Bure.
Kumbe Fahad alikuwa anamfatilia morson bana, siku Moja nikapigiwa simu na namba ngeni, nikapokea mikashangaa anaambiwa kuwa rafiki yake kaanguka na naombwa nifike eneo la tukio, sio Siri nilipanic na kuanza kujiandaa kama mwenda wazimu, ila kabla sinatoka simu yangu iliita na aliekuwa anapiga alikuwa ni Fahad.
" Upo wapi? Akaniuliza
"Nipo nyumban ila najiandaa kutoka kwa maana nimepugiwa simu kuwa kuna rafiki yangu yuko kwenye matatizo, nikasema.
"Naomba unisikilize kwa makin ninayokuambia, akasema Fahad.
"Ingia ndani na ulock milango Yako yote, na kingeni usopokee simu ya namba ngeni yoyote ile na mm NAKUJA sasa hivi, Fahad alisema na SIKUJUA kwann alikuwa anasema vile, kuna muda nikawa najikuta Nina hofu sana ila kuna muda mwingine nikawa najiambia nitulie maana huenda kuna jsmbo ambalo Fahad ameshaliona so sipaswi kuwa na papara.
Mara simu yangu ikaanza kuita na nilipoangalia ilikuwa ni namba ngeni, sikupokea, mara mlango ukaanza kugongwa na nilipoenda kuchungulia nikakutana na Fahad, basi nolamfumgulia mlango na akaingia ndani mkuku mkuku.
"Naomba ujiandae maana tunaondoka Fahad akasema na sikuwa namuelewa kabisa kuwa kamaanisha Nini, ila Fahad alinikazania mpaka ikabidi tuondoke, na muda huo huo tukaenda kupanda basi na ilikuwa ni usiku, Yale mabasi ya usiku na kesho yake tukafika dar.
"Kwann umetaka niondoke kwenye mkoa ambao nimeuzoea na pia vipi kuhusu kazi, nikamuuliza Fahad akanambia kuwa tutaongea nisiwe na mashaka na kuhusu kazi ameshanitafutia so nisiwe na wasiwasi.
Basi akanipeleka kwenye nyumba Moja ambayo ilikuwa ni room mbili kwa maana ya chumba na sebule pamoja na choo, akanambia nitakaa hapo Kisha YEYE akaondoka zake.
Kesho yake asubuh akanipigia simu na kuniambia anaenda kazin lakin akitoka atakuja, akanitumia elfu 20 akanambia nitakula, basi na mm sikuwa na neno nikatulia zangu TU.
Sasa kwenye majira ya kama saa tano asubuh nikasikia simu yangu inaita, nilipoenda kuangalia ilikuwa ni namba mpya, nikawa najiuliza kama nipokee au nisipokee maana morson nilishamblock huenda ameamua kutumia namba nyingine...
Nikaona nipokee TU, na kweli alikuwa ni morson.
"Wewe Malaya upo wapi, akauliza mara baada ya mm kupokea simu
"Niko huku kwenye madanguro najiuza, nikajibu na morson akaachia msonyo huo😃😃
"Hivi unajikutaga nani wewe.akasema morson
"Najikuta keki na ice cream mbili, unataka nn wewe boya la nchi kavu, nikasema.
"Nitakuzingua ujue, mm sio sawa na huyo Malaya mwenzio unajua, embu nambie upo wapi kabla sijafanya kitu kibaya, akasema morson
"Nipo kwenye ile nyumba ambayo wewe ulianza kunifundishia umalaya nafanya mazoezi, nikasema akasunya tena Kisha akasema " nikikupata utajua mm ni nani, akasema Kisha akakata simu..
Alivyokata TU nikampigia Fahad na kumueleza kila kitu akanambia hakuna tatizo ila kikubwa nisimzingatie.
Basi jion kama saa kumi na Moja Fahad alikuja, nilihisi alikuwa amechoka sana so nikamuandalia chakula Akala na mara baada ya kuimaliza kula akaniangalia kwa dakika kadhaa Kisha akasema "embu imagine mm ndio mumeo saa hio, narudi nyumban unanipikia alafu naoga alafu nakula nikimaliza nakula tena, huon kama ni Raha sana, akasema.
"ACHA maskhara Yako bana, ehee nambie ulichotaka kuniambia Jana, nikasema na akatoa simu..
Kulikuwa kuna voice note nyingi sana na ilikuwa ni sauti ya Morrison.
"Moja ilisema kuwa morson anataka aniteke Kisha wajanibake ili waone kama nitaendelea kuringa, tena Mmoja ya watu awe muathirika ili wanikomeshe, nilihisi kuchoka.
Maana SIKUJUA nimemfanyia nn morson kibaya hivyo mpaka atake kunifanyia hayo yote...
Fahad akawa ananifariji pale, mwisho akanambia kuwa amenitafutia kazi na kesho yake natakiwa kuanza, kiukweli sikutegemea nikajikuta naenda kumkumbatia, sasa wakat nataka kujitoa nikashangaa amening'ang'ania, ikabidi na mm nitulie woi, mwanaume mwenye muhandsome hivi alafu nijifanye najitoa kwenye mwili wake haraka haraka nataka nn mie, nikawaza.
Basi tukakumbatiana pale mpaka Fahad akarudhika mwisho akanambia kuwa nimsindikize aondoke na mm nikatii, basi nikajiandaa pale Kisha tukatoka nikawa namsindikiza Fahad.
Basi tumefika sehemu kulikuwa kuna kama kauchochoro, saa ngapi Fahad asinishike mkono, sio Siri nilishtuka nikataka kuutoa mkono wake, akawa kaning'ang'ania Kisha akaniangalia na kusema "Nakupenda zinath.
Sio Siri nilijisikia vzr ila tatizo Fahad ni handsome sana mpaka muda miwngine nahisi kama sio hadhi yangu, maana morson wakawaida TU na amenisaliti vipi kwa huyu kijana handsome si ndio nitafumania kila siku, nikawaza nikajikuta nimeropoka kuwa " Nakupenda zaidi Fahad rafiki yangu, Fahad aliniangalia Kisha akaanza kucheka, yaan alicheka sana mpaka nikabaki namshangaa.
FULL. comment apo
The wrong number
GREEN HACKER
0
Chapisha Maoni
TOA MAONI YAKO HAPA