SITOSAHAU ALICHONIFANYIA 14-17

14__17

SIMULIZI; *SITOSAHAU ALICHONIFANYIA BOSS WANGU* 14

………. ILIPOISHIA……………..

Nilimuuliza ana uwakika gani, akaniambia mimi ninaweza kurudi duniani maana neema yangu bado haijaondelewa bali watu ndio wametaka kuindoa, nilifurahi kusikia vile na hapo nikaadha kufikiria siku nikifika duniani na kukutana tena na familia yangu itakuwa ni siku ya aina gani. ………….. INAENDELEA …………………………

Nilimuahidi yule dada kuwa endapo nitafanikiwa kufika huku duniani nitaifanya hiyo kazi ya kuwaeleza watu siri mzito iliyopo kuhusu maisha ya kule chini, alitabasamu na kuniambia kuwa kuanzia mda ule yupo tayari kuingia kwenye adhamu ambazo anatakiwa kukutana nazo maana moyo wake umelizika kwa kumpata mtu atakae fikisha ule ujumbe huku duniani. Nilimuhurumia maana alikuwa akiongea huku akibubujikwa na machozi na macho yake kuwa myekundu kama mtu aliekuwa amekaa kwenye jiko la kuni kwa mda mrefu. Baada ya hapo nilimuuliza njia gani naweza kuitumia ili nitoke ile sehemu, maana mda uwo nilianza kuikumbuka tena familia yangu baada ya kupewa matumaini ya kuweza kurudi tena duniani, lakini aliniambia bado ni mapema kuniambia njia ya kutoka kule na akuniambia kabla ya siku ya 40 yangu kufika huku duniani natakiwa niwe tayari nimetoka sehemu ile. Baada ya kuniambia vile nilimuuliza zimebaki siku ngapi kufika siku yangu ya 40 akaniambia kama ishirini na siku kadhaa, nikamuuliza tena kwanini amesema kuwa bado ni mapema kujua njia ya kurudi duniani, akaniambia anataka nione mambo mengi ya kutisha yaliyopo kule ili nikija huku niwe na vitu vingi vya kuwaambia kuhusu ile sehemu. Niliumia baada ya kuniambia vile maana sikupenda kabisa niendelee kukaa sehemu ile lakini sikuwa na jinsi ilibidi nikubali kile alichokuwa ameniambia. Mda huo wale wenzetu walikuwa wapo wapo tu awajui hili wala lile kuhusu uwepo wao katika ile sehemu na hata wakati tunaongea hakuna hata mmoja alieonyesha hali ya kusikiliza kile ambacho tulikuwa tunakiongea. Nilimuuliza tena swali lingine kwanini wale wenzangu walikuwa kwenye hali, akanijibu
“ Duniani kila mtu ana bahati yake na MUNGU amekushushia neema yake na hili lilokukuta wewe nahisi amefanya kama pito dogo au kama funzo ambalo anataka na wewe ukawafundishe wenzako na kuwaeleza kuhusu huku, lakini hawa wenzako hiyo neema awajaipata kwahiyo maisha yao yote wataishi kama misukule mpaka pale MUNGU atakapo zichukuwa roho zao “

Aliponiambia vile nilimshukuru sana MUNGU maana niliona amenipa upendeleo wa kipekee, hata kama nilikuwa bado sijatoka kule lakini niliamini yale maneno ya yule dada. Basi baada ya hapo tuliendelea na safari huku nikiwa ninamsimulia chanzo cha mimi kufika katika ile sehemu, alisikitika sana na kuniomba nikifika duniani bosi wangu pamoja na familia yake ndio iwe ya kwanza kuifikishia ujumbe ambao alikuwa amenipatia kuhusu waamini nguvu za giza pamoja na watenda dhambi kwa ujumla. Sasa tukiwa tunaendelea kuongea ghafla nyuma yetu lisikia sauti za watu zikiwa zinalia haraka nikageuka na kutaazama nini kinachowafanya walie hivyo. Niliumia sana baada ya kuona watu kama watano ambao walikuwa wakiburuzwa chini kwenye ile ardhi aliyokomaa kupita maelezo huku wakiwa wanapigwa na mijeredi ya miba miba na yenye kuwaka moto, watu wale walitapakaa damu mwili mzima. Nikamgeukia yule dada na kumuuliza wale watu walikuwa wamefanya nini mpaka wafanyiwe vitendo vile, akanijibu

“ Hao ndio wale ambao wemekuwa wakitafuta njia ya kutoka huku ili warudi duniani yani kutoroka kutokana na kushindwa adhabu zilizopo huku kwahiyo ukikamatwa unakutana na mambo kama yale na vile vidonda vyao ambavyo wamevipata haviponi tena milele na kila mda watakuwa wakipata maumivu makali kutoka kwenye vile vidonda “

Nilimuuliza kwanini vile vidonda havitapona akanijibu “ inakuwa ni adhabu ambayo wanapewa kutokana na kile ambacho wamekifanya pia kila baada ya mda Fulani kwenye vile vidonda watakuwa wakichomwa moto kwa ajili ya kuwaongezea maumivu “.

Nikamuuliza swali lingine “ kutokana na hayo mateso makali wanayokutana nayo awawezi kupoteza maisha “ alinitazama na kunijibu “ Hapana awawezi kufa tena maana tayari walishakufa uko duniani na ndio maana wamekuja huku “ niliwahurumia sana niliposikia vile. Baada ya hapo tuliendelea na safari na mda huo mwili wangu ulianza tena kukosa nguvu kwa ajili ya njaa ambayo nilikuwa nayo, yule dada alinisihi nivumilie maana mda mfupi nitaondokana na zile tabu nilifarijika kusikia vile. lakini nikamuuliza kama ningeweza kutoka na yeye, alitabasamu kisha akaniambia anashukuru kwa kile kitendo cha kumuonea hurama lakini yeye awezi kutoka kule milele na milele. Sasa tukiwa tunaendelea na safari ghafla alinishika mkono na kuniambia niangalie upande wangu wa kulia, niliumia sana baada ya kuona mtu mmoja akichomwa na mikuki yenye moto utazani iliwekwa jikoni kwa mda mrefu sana. ITAENDELEA

SIMULIZI; *SITOSAHAU ALICHONIFANYIA BOSS WANGU* 15

Nilimuuliza kwanini yule mtu anafanyiwa vile akaniambia ni moja ya adhabu ambazo na yeye anaenda kukutana nazo huko kwa mkuu wa giza. Nilimtazama tena yule mtu ambae alikuwa analia huku akiomba msahada kisha nikamtazama tena yule dada huku nikiwa natokwa na machozi na yeye alinitazama na kuniambii nisilie bali nifikiri njia gani nitaitumia katika kuufikisha huu ujumbe kwa wenzangu huku duniani. Sasa nikiwa kwenye hali ya huzuni mara mbele yetu likatokea kundi kubwa la watu ambao walikuwa wamezidi kuchoka na kuchafuka zaidi yetu pia walikuwa wakisukumwa na kupigwa kama ng’ombe anavyokuwa na mchunga wake waendapo machungani { malishoni }. NIkamgeukia tena yule dada na kumuuliza kuhusu kundi lile ndipo akaanza kunielekeza kuhusu wale watu.

“ wale ni misukule ambayo tayari imekamilika kwenda kafanya kazi na pale wanapelekwa tena duniani kwa watu wao ambao wamewahitaji wakawafanyie kazi zao “ niliwatazama tena wale watu na kumuuliza swali lingine “ Sasa huku wanatoka kwa kutumia njia gani “ alinijibu “ wanatumia nguvu za giza kufika huko duniani “ nilitikisa kichwa kuashiria kuelewa kile alicho niambia. Nikiwa naendelea kuwaangalia wale watu na kuwatafakari zaidi, mbele yetu alitokea mtu mrefu sana ambae afanani na mtu yoyote huku duniani na mda wote alikuwa amekasirika kama mtu aliechukizwa na kitu Fulani. kama kawaida nikamgeukia yule dada na kumuuliza kuwa yule nani na mbona yupo kwenye ile hali, akanijibu “ Yule ni mmoja wa masheteani ambae anafanya kazi ya kuwaangalia wachawi duniani, na anauwezo wa kuiangalia dunia kwa mda mmoja na kujua wapi watu wake wapo. na ile hali ya kukasirika inatokana na mawazo ambayo anayo kuhusu siku ya kiama maana na yeye ataandamwa na adhabu kubwa pamoja na moto wa milele “ nilishangaa kusikia vile nikamuuliza swali lingine “ kumbe na wao siku ya mwisho wataingia motoni pamoja na watenda dhambi wote “ akanijibu “ Ndio maana awa ndio wale malaika ambao walimuasi MUNGU

wakatupwa huku chini pamoja na mkuu wao ambae ni shetani “ nilisikitika kusikia vile. Baada ya hapo tukaendelea na safari yetu na tulipofika sehemu Fulani karibu na kufika huko tuendako, yule dada akaniita na kuniambia mda wa kurudi duniani umewadi . kwanza nilishtuka pili nilifurahi na tatu niliogopa nikamuuliza nitawezaje kutoka huku, aliniambia nimuamini MUNGU na kuanzia pale nilipo nianze kuomba kwa imani yangu mpaka pale msahada utakapotokea. Kuanzia hapo nilianza kusali kwa imani yangu huku nikilitaja jina la MUNGU, yule dada alizidi kunisihi nizidi kuomba kwa imani iliyo kuu nitafanikiwa kwa kuwa neema bado ipo juu yangu. ITAENDELEA

SIMULIZI; *SITOSAHAU ALICHONIFANYIA BOSS WANGU* 16 & 17

………….. ILIPOISHIA………………….

Baada ya hapo tukaendelea na safari yetu na tulipofika sehemu Fulani karibu na kufika huko tuendako, yule dada akaniita na kuniambia mda wa kurudi duniani umewadi . kwanza nilishtuka pili nilifurahi na tatu niliogopa nikamuuliza nitawezaje kutoka huku, aliniambia nimuamini MUNGU na kuanzia pale nilipo nianze kuomba kwa imani yangu mpaka pale msahada utakapotokea. Kuanzia hapo nilianza kusali kwa imani yangu huku nikilitaja jina la MUNGU, yule dada alizidi kunisihi nizidi kuomba kwa imani iliyo kuu nitafanikiwa kwa kuwa neema bado ipo juu yangu. ……………. INAENDELEA ……………….. Maneno yake yalinifanya zidi kuomba na kuwa na imani ya kuafnikiwa kile ambacho nilikwa nina kiomba. Nikiwa katikati ya maombi, yule dada alininyamazisha na kuniambia niangalie mbele tuendako, daaa nilitetemeka kupita kiasi maana kile nilichokuwa nimekiona sikuamini haraka nikamgeukia yule dada na kumuuliza swali “ ule moto unatoke wapi na mbona mwingi kiasi kile “ akanijibu “ Petro inaonekana wakati upo duniani ulikuwa hausomi vitabu vya dini, Lile ni ziwa la moto ambalo limetajwa kwenye vitabu vingi sana vya dini na ndio moto ambao utawachoma watenda dhambi wote moja na shetani ikifika siku ya mwisho siku ya hukumu ya wanadamu wote “ niliogopa sana niliposikia vile. tukiwa tunaendelea kuongea yule dada akaniambia niangalie mbele zaidi na nilipofanya hivyo liiiona sehemu moja ambayo ilikuwa ina giza kupindukia na sauti nyingi za watu zilikuwa zikitoka sehemu hiyo, pia mwanga wa radi uliombatana na mingurumo ya kutisha vilikuwa juu ya eneo hilo. kama kawaida yangu nikamgeukia yule dada na kumuuliza kuhusu ile sehemu na yeye akanijibu “ Ile ndio sehemu tuendayo sehemu ya mkuu wa giza sehemu yenye kila aina ya mateso, sehemu ambayo sitamani binadamu wengine waliopo duniani wafike “ nilipoambiwa vile nikageuka tena na kuiangalia ile sehemu. Nikiwa ninatafakari lile eneo, yule dada aliniambie niendelee kumuomba MUNGU maana mda wangu wa kutoka kule umewadia, na mimi bila kuchelewa

nikaanza kusali kwa uchungu huku nikibubujikwa na machozi na kila nilipokuwa nikikumbuka mateso ya sehemu ile nilizidi kulia na kumuomba MUNGU aniepushe na adhabu zilizopo katika ile sehemu. Niliutazama ule umati na kuanza kuwaombea msamaha kwa MUNGU ili wote tupate Neema ya kurudi huku duniani lakini ilishindikana. Sasa nikiwa ninaendela kusali ghafla niliona wale viongozi wasimamizi wa shetani, mkuu wa giza wakinifuata kwa hasira, niliogopa sana lakini yule dada alinisihi nisiogope bali niendelee kuomba msahada kwa MUNGU maana huyo ninae muomba ananguvu kuliko wale. Nilifanya hivyo, na Wale malaika wa baya wa shetani waliponikaribia ghafla mtikisiko mkubwa ukatokea katika ile sehemu, ndipo yule dada akanitazama huku akitabasamu na kuniambia nisisahau kufanya kama alivyoniambia pindi nikifika huku duniani. Sikuelewa kwanini aliniambia vile, kumbe mda wa kukombolewa kwangu

kutoka kwa shetani kule kuzimu ulikuwa umewadia . Baada ya kuniambia vile ghafla alitokea mtu mmoja alievaa nguo nyeupe yenye kung’aa sana na kuniambia nimfuate. Mtu huyo sikufanikiwa kuiona sura yake pia alikuwa anatembea bila kukanyaga ile ardhi naweza kusema alikuwa anapaa japokuwa nilikuwa nikimuona anapiga hatua kama mtu anaekanyaga ardhi, ghafla ikatokea njia ambayo haikuwepo mda wote wakati tupo katika lile eneo. Nilimgeukia yule dada na kumwambia twende wote lakini aliiambia yeye awezi kutufuata hata ile kunyanyua hatua moja kwake haiwezekani, Nilimuhurumia sana kisha nikamtazama yule mtu mwenye kuvaa nguo nyepe ili nimuombe amsaidie yule dada lakini hakunijari wala kuniangalia, lakini yule dada alinimbia nikifika duniani niwatafute ndugu zake na niwaeleze wapi yeye alipo na kwa sababu gani, aliongea kwa sauti kubwa pia akanitajia jina lake na jina la ukoo wake. Lakini kwa bahati mbaya yule dada baada ya kuniambia vile niliwaona wale viongozi malaika wa shetani wakimfuata na kuanza kumpiga na ile mijeredi huku wakimchoma mikuki ya moto katika kila sehemu ya mwili wake. Nililia kwa uchungu sana na kujisemea mwenyewe kimoyo moyo kuwa rahiti wachawi, watu wanao fanya wenzao misukule na watenda dhambi wote wangejua nini wanakuja kukutana nacho baada ya kuingia NDANI YA KABURI sidhani kama wangeifanya ile kazi. Nikiwa kwenye hali ya mawazo kufumba na kufumbua nilijikuta nikiwa kwenye nyumba ya bosi tena kwenye kile chumba ambacho nilikuwa nikifungiwa. Haraka nilitoka kwenye kile chumba lakini baada ya kufika sebuleni nilimkuta bosi akiwa pamoja na familia yake, nilisimama na

kujiuliza nitapitaje sehemu ile bila wao kunio. Nikiwa najiuliza jinsi ya kupita pale nilishikwa mkono na mtu ambae sikumuona na kunipitisha mbele ya ile familia bila mtu yoyote kuniona. Nilipofika nje nilifurahi na nikamshukuru MUNGU kwa upendeleo ambao alinipa wa kunitoa chini ya utawala wa shetani na malaika zake. Baada ya hapo niliondoka pale na kuelekea nyumbani ambako nilikuta umati wa watu ambao walikuwa akipanga kunifanyia 40 yangu siku ya pili yake. Watu baada ya kuniona nimefika nyumbnani wengi walikimbia kwa kuzani ni mzimu wangu ulikuwa umewatokea lakini baadhi walinisogelea na kunichunguza kama kweli ndio mimi au laa, na walipogundua waliwaambia wenzao kuwa ni mimi mwenyewe. Ghafla nilimuona mke wangu akitoka ndani pamoja na wanangu huku wakiwa

wamevaa nguo nyeupe, nilifurahi sana na nililia kama mtoto maana sikuamini kile kilichokuwa kimetokea, nilikumbatiana nao kisha wakanichukuwa na kunipeleka ndani, mda huo nilikuwa nimechoka na nimechafuka kupita kiasi. Baada ya mda kidogo kupita mara ilifika taarifa bosi amelazwa amepatwa na tatizo la mshtuko wa moyo, nilimuomba mke wangu tuelekee huko hospitali ili nikamwambie amuombe MUNGU msamaha kwa kile ambacho alikuwa amekitenda lakini tulichewa maana mda mfupi mbele ikafika taarifa kuwa amefariki dunia. Niliumia sana na nililia kwa uchungu maana nilimuhurumia kutokana na kile anachoenda kukutana nacho kule kwa shetani. watu wengi walinishangaa na kujiuliza kwanini nililia kwa uchungu kiasi kile lakini awakupata jibu mpaka pale ambapo nilieleza ukweli wa mambo yote niliyokutana nayo huko. Wengi walimuhurumia bosi na wengine walisema afadhali kutokana na kile ambacho alikuwa amenifanyia lakini kwa upande wangu sikupenda kimkute kile kilichokuwa kimemkuta. “

Petro baada ya kumaliza kusimulia waandishi wote walibaki vinywa wazi maana hawakutegemea kusikia simulizi ile katika maisha yao. basi baada ya hapo mwandishi mmoja akamuuliza nini malengo yake katika kuufisha ule ujumbe kwa jamii, akajibu

“ Nimepanga nianze kuzunguka Tanzania nzima katika kila sehemu makanisani na misikitini na kila sehemu penye makusanyiko ya watu, nitawaeleza habari hii na wenye kunielewa atanielewa na asietaka kunielewa basi nitaachana nae maana kwa upande wangu nitakuwa sina deni maana nimefikisha ujumbe tayari “

Lile swali ndio lilimaliza yale maojiano dhidi ya waandishi wa habari pamoja na Petro na kuanzia hapo habari zake zikaanza kuenea kwenye vyombo vya habari pamoja na mitandao.KUWA MTU ALIFARIKI AFUFUKA KARIBIA NA SIKU YA 40 YAKE ……………… MWISHOOOO

UMEONAJE SIMULIZI HII NA UMEJIFUNZA NINI?? ACHILIA COMMENT YAKO HAPO CHINI

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA

Mpya zaidi Nzee zaidi

Ads related

Smartwatchs