SITOSAHAU ALICHONIFANYIA 06-13

06___13

SIMULIZI; *SITOSAHAU ALICHONIFANYIA BOSS WANGU* 06

………. ILIPOISHIA ……………

Nikiwa naingia kwenye gari nilitazama wanangu ambao walikuwa wameshikwa na rafiki yangu wa karibu sana huku wote wakiwa kwenye hali ya majonzi yasio na kifani. Basi baada ya hapo watu wakaludi nyumbani na mipango ya mazishi yakaanza kufanyika. Siku ya pili majira ya saa kumi jioni ule mwili ulizikwa huku mimi mwenyewe nikiwa nashuhudia lakini sikuwa na kitu cha kufanya kwa mda ule baada ya kugundua kuwa nguvu za giza zipo juu yangu.

………… INAENDELEA ……………………….

Kila nilipokuwa nikimtazama bosi , mda wote nilikuwa nikimuona akitaasamu kuonyesha kufurahishwa na kile kitendo. Baada ya hapo mazishi yaliendelea na yalipoisha watu wote tukarudi nyumbani, huko ndiko nilikutana na ndugu zangu na marafiki zangu wengi sana ambao wengi wao ulimepita mda mrefu sana bila kuonana nao. Nilipoona vile nikaa chini huku nikiwa nimeweka mikono yangu kichwani nikilitafakari lile tukio. Nikiwa kwenye hali ya huzuni bosi alinifuata na kuniambia niwaage wale watu wote kwa mara ya mwisho maana sitawaona tena baada ya kutoka pale nyumbani. Kwa hasira nilitamani kumrukia lakini nilishindwa maana mwili wangu ulikuwa umechoka kutokana na njaa ambayo nilikuwa nayo pamoja na guvu za giza ambazo zilikuwa zimenigandamiza. Mambo yaliendelea na hatimae mda wa bosi kurudi nyumbani kwake ukawaidi ndipo akanifuata na kuniambia niiangalie familia yangu kwa mara ya mwisho maana sitaiona tena maishani mwangu, mda huo mke wangu pamoja na wanangu walikuwa wamekaa pamoja huku mke wangu akiwa amevimba macho kutokana na kulia kwa mda mrefu. Niliwatazama kisha nikasikitika huku nikibubujikwa na machozi, ndipo bosi akanishika mkona na kuondoka na mimi mpaka nyumbani kwake ambako huko niliikuta familia yake ikiwa na furaha tele. Niliumia sana baada ya kuona vile na kuanza kuikumbuka familia yangu na kukumbuka kipindi ambacho nilikuwa ninakaa nao pamoja na kufurahi nao kama jinsi nilivyoona kwenye ile familia ya bosi. Basi nilikaa kwenye ile nyumba kwa mda wa siku tatu huku nikiwa ninakula mabaki ya vyakula ambavyo walikuwa wanaacha watoto wa bosi, kusema kweli niliishi maisha ya shida sana ile sehemu mpaka sitamani hata kukumbuka yale mambo. “

Petro baada ya kusema vile akanyamaza na kuwaachia nafasi waandishi ili wamuulize swali lolote kuhusu kile ambacho tayari alikuwa amekiongea. Mwandishi mmoja wa kike akamuuliza swali “ umesema baada ya kutoka nyumbani kwenu akakupeleka nyumbani kwake na ukaishi huko siku tatu, sasa je mke wake alikuwa anafahamu kitu chochote kuhusu uwepo wako mule ndani au mume wake alikuwa anafanya siri “ mwandishi baada ya kunyamaza, petro akajibu “ Hapana wala hakuwa anafanya siri maana mke wake alikuwa anajua kila kitu na yeye ndie ambae alikuwa akiniletea hayo mabaki ya chakula cha watoto wao “ Petro alipojibu vile waandishi wote walisikitika. Basi baada ya hapo wakamuomba aendelee kusimulia nini kiliendelea baada ya kukaa siku tatu kwenye nyumba ya bosi wake. ITAENDELEA

SIMULIZI; *SITOSAHAU ALICHONIFANYIA BOSS WANGU* 07

"ilipofika siku ya tatu majira ya saa mbili usiku bosi pamoja na mke wake wakanichukua na kunipeleka mpaka kwenye kaburi langu kisha wakanizungusha mara tatu na baada ya hapo wakanilaza juu yake na kuniwagia maji nyenye rangi nyekundu. Tukio lile lilichukua kama dakika 30 au 20 hivi kisha wakanichukuwa tena na kunirudisha kwenye nyumba yao, mda huo nilikuwa nikinuka kama maji machafu kutokana na maji ambayo walikuwa wamenimwagia. Tulipofika kwao walinipeleka kwenye chumba ambacho nilikuwa ninakaa kishwa wakanifungia mlango, wao wakaenda zao kulala. Siku hiyo nililia sana na kujiuliza baya gani ambalo nilikuwa nimemfanyia bosi na kupelekea yeye kunifanyia unyama ule, nilisikitika sana, niikumbuka familia yangu pamoja na ndugu zangu maana wengi wao walikuwa wananitegemea mimi katika kuendesha maisha yao, nilizidi kulia nilipokumbuka jambo hilo. Ile siku ilipopita na kuja siku ya nne bosi akanichukua na kunipeleka sehemu moja msituni ambako huko sikuweza kusikia sauti za binadamu wala wanyama ambao nimewazoea kama ngombe, mbuzi au mbwa na kadharika bali nilikuwa nikisikia sauti za wanyama wakali kama simba na wengineo. Nilijiuliza ni wapi bosi ananipeleka lakini sikupata jibu na nilipojitahidi kufikilia zaidi ili nigundue nia yake, nilihisi labda alikuwa anaenda kunitupa katika huo msitu mkubwa wakutisha na iwe mwisho wangu huko. Nilipofikiria vile kimoyo moyo nikasema lolote na liwe, maana nilikuwa tayari nimesha jishukuru kuwa mimi ni mtu wa kifo na sina msahada tena. Basi tuliendelea na safari na tulipofika katikati ya huo msitu tulikutana na kibanda kimoja cha manyasi ambacho kilikuwa kidogo kama kijumba cha kucheza watoto michezo yao ya madangi. Tulipofika hapo bosi akasimamisha gari kisha akanishusha tukaenda kuingia kwenye hiko kibanda, ambapo tulikuta na Mzee mmoja ambae alikuwa amevaa nguo zilizo tengenezwa na magome ya miti. Huyo mzee baada ya kumuona bosi alimpokea kwa shangwe kubwa mpaka nikajiuliza wanauhusiano gani wawili wale, baada ya hapo wakaanza kusalimiana na mda huo mimi nilikuwa nikiwatazama. Walipomaliza ndipo bosi akaanza kuongea mambo ambayo yalinishangaza sana. BOSI: mzee wangu kijana ambae uliniambia nimtafute kwa ajili ya kukamilisha yale mambo yangu ndio huyu hapa nimemleta. Yule mzee baada ya kuambiwa vile akanyanyuka sehemu ambayo alikuwa amekaa na kunifuata nilipokuwa nimekaa, nilimtazama na alipofika kwangu akatoa kisu ambacho kilikuwa kiunoni kwake na kunitoboa kidogo mkononi na kuanza kuinyonya damu yangu. Nilipata maumivu makali sana ambayo tangu nizaliwe sikuwai kupata maumivu makali kiasi kile japokuwa kitendo ambacho alikuwa amenifanyia kilikuwa akiwiani na maumivu ambayo nilikuwa nimeyapata, nilishangaa. Alipomaliza kufanya hivyo alitikisa kichwa chake na kurudi sehemu ambayo alikuwa amekaa kisha akachukua kikombe chenye maji na kuanza kuyanywa hayo maji, Alipomaliza ndipo akaanza kuongea na bosi. MZEE: Kijana unajua kuchagua nakupa hongera maana sikutegemea kama ungemleta mtu kama huyu ambae damu yake bado mbichi inauwezo wa kufanya kitu chochote na ukafanikiwa maana inachemka. Yule mzee baada ya kusema vile bosi alicheka sana na kuanza kuongea. BOSI: hahaha Na mimi nilijua tu lazima unisifie maana huyu mtu tangu tupo kazini niliiona nyota yake iking’aa kuliko za watu wote pale na ndio maana nikaona bora nimchukue yeye nilihisi atafaa zaidi kuliko mtu mwingine yoyote.

MZEE: Uliwaza jambo zuri sana.

Walipomaliza maongezi yao, Yule mzee akanisogelea tena na kuanza kunimwagia unga mwili mzima huku akiwa anaimba nyimbo za kilugha, mda huo bosi alikuwa akitazama kile anachofanya Yule mzee huku akipiga makofi sawa sawa na nyimbo ambazo alikuwa akiziimba. Walipomaliza kufanya vile, ghafla nilianza kuona kizunguzungu na mwili wangu kuishiwa nguvu kabisa nilijitahidi nisianguke lakini ilishindikana, nilianguka na kupoteza fahamu. ITAENDELEA SIMULIZI; *SITOSAHAU ALICHONIFANYIA BOSS WANGU* 08

……….. ILIPOISHIA………………. Walipomaliza maongezi yao, Yule mzee akanisogelea tena na kuanza kunimwagia unga mwili mzima huku akiwa anaimba nyimbo za kilugha, mda huo bosi alikuwa akitazama kile anachofanya Yule mzee huku akipiga makofi sawa sawa na nyimbo ambazo alikuwa akiziimba. Walipomaliza kufanya vile, ghafla nilianza kuona kizunguzungu na mwili wangu kuishiwa nguvu kabisa nilijitahidi nisianguke lakini ilishindikana, nilianguka na kupoteza fahamu. ………………… INAENDELE ………………………….

Baada ya hapo sikuelewa nini kiliendelea maana nilipokuja kushtuka ilikuwa ni usiku wa manane tena nikiwa peke yangu kwenye kile kibanda. Nilitazama huku na kule kuwatafuta wawili wale lakini sikuwaona na kuanza kujiuliza kuwa wameenda wapi, nikiwa natafakari lile jambo nilishikwa na njaa ya ghafla ambayo ilifanya nizidi kuangaza macho yangu huku na kule nje ya kile kibanda ili nimuone bosi au Yule mzee na nimwambie shida yangu japokuwa nilijua sio watu wazuri kwangu lakini sikuwa na jinsi. Zilipita dakika kadhaa na hatimae bosi pamoja na Yule mzee wakawasili kwenye kile kibanda huku wakiwa wamebeba mizizi ya miti. Kabla hawajaongea kitu chochote nilimuita bosi na kumwambia nina njaa, alicheka sana na kupeana mkono na mzee kisha akaenda sehemu Fulani ambapo kulikuwa na mtungi na kuchota unga kwenye bakuli kisha akaniletea huku akiniambia kuwa ndio chakula changu cha siku ile. Nilihuzunika sana lakini siku na jinsi maana njaa ilikuwa imenishika kupita kiasi. Taratibu nikaanza kula ule unga ilimradi tumboni muwe na kitu cha kunitia nguvu, ilipomaliza kula Yule mzee akamgeukia bosi na kumwambia kazi yao tayari imekamilika, taarifa ambayo ilimfurahisha sana bosi. Baada ya hapo ndipo Yule mzee akaanza kumpa maelezo bosi nini amatakiwa kufanya juu yangu.

MZEE: Mwanangu mpaka hapo kwa upande wangu nimebakiwa na kazi moja tu ya kumzimisha huyu mtu ila kazi zingine zilizobaki zinahitajika zifanyiwe na wewe mwenyewe na ninaaomba unisikilize kwa makini. Kuanzia sasa hivi huyu mtu atakuwa ni nusu mfu na hali hiyo atakuwa nayo mpaka pale wewe utakapomaliza kuifanya kazi ambayo nitakuambia uende ukaifanye ukifika usiku wa kesho. Kesho majira ya saa sita usiku nenda kwenye lile kaburi kisha lifukue mpaka maeneo ya kiunoni kwako alafu mfukie huyu na uondoke, hapo utakuwa umemaliza kazi yako na mambo yako yatakuwa yanaenda vizuri ila ikifika siku ya 40 yeke huko kwao, siku inayofuatia wewe unatakiwa uje huku kumchukua mtu wako akiwa tayari yupo kikazi zaidi.

Nilishtuka na kuogopa sana na kuanza kumtazama bosi ambae kwa mda huo yeye alikuwa akifurahia kile ambacho alikuwa anaambiwa, nilitamani nikimbie lakini mwili wangu ulikuwa hauna nguvu ya kufanya hivyo. Basi baada ya hapo Yule mzee akachukua unga Fulani mweusi na kunipulizia kisha nikadondoka chini na kuanzia hapo sikujua nini kiliendelea. “

Petro baada ya kusema vile kama kawaida akanyamaza na kuwaachia wale waandishi nafasi ya kumuuliza maswali lakini kwa mda huo hakuna hata mmoja ambae alikuwa na swali zaidi ya wote kuwa na shahuku ya kutaka kujua nini kiliendelea, kwahiyo Petro akaendelea kusimulia.

” Nikiwa kwenye ile hali kwa mda ambao sikuufahamu, nilishtuliwa na sauti za watu ambazo nilizisikia zikigumia kuashia kupata maumivu makali sana. Niliposhtuka nikataza pande zote nne za dunia ili nitambue pale nilipo ni wapi lakini sikubahatika kupafahamu, lakini ni sehemu moja ambayo ilikuwa inatisha na kulikuwa na makundi ya watu wengi sana ambao walikuwa wamezohofika, na wengine mda wote walikuwa wakitokwa na mate kama watoto wadogo. Nilipoona vile nikaitazama ardhi yake ilikuwa ni kame iliyokomaa mithili ya zege nikagundua kuwa kwa mda mrefu sana eneo lile halijawai kupita maji, baada ya hapo nikainua macho yangu na kutazama anga la sehemu ile ambako huko nilikutana na giza nene na kupelekea kushindwa kuona hata nyota moja wala mwezi. Kwa ishara ile niligundua kuwa ile sehemu itakuwa halijawai kutokea jua. Sasa nikiwa naendelea kulitafakari lile eneo mara alikuja mtu ambae alikuwa ameshika mjeledi mkoni mwake na kutuchukua mimi pamoja na wenzangu ambao nilikuwa nipo nao kwa mda ule. Taratibu tukaanza safari ya kuelekea sehemu ambayo sikufahamu ni wapi tulikuwa tunapelekwa lakini njiani tulikutana na watu wengi wengi sana ambao kila mmoja alikuwa yupo busy na mambo yake, lakini walikuwa kwenye hali ya tofauti kabisa. Nilitamani kuwauliza wenzangu nini kinaendelea na pale tulipo ni wapi lakini kila niliemtaza ili niongee nae hakunijari bali alionekana kuwa na mawzo mengi kichwani mwake. ITAENDELEA SIMULIZI; *SITOSAHAU ALICHONIFANYIA BOSS WANGU* 09

Nilipoona vile taratibu nikaanza kufanya uchunguzi mimi mwenye ili nijue pale tulipo ni wapi, ila kusema kweli ile sehemu ilikuwa inatisha na sio mzuri binadamu kutamani kwenda kuishi huko, maana kuna joto kali kupita kiasi pia eneo lote limeandamwa na moshi, pia kila sehemu kumezungukwa na majabari ya mawe na visima vya moto ambavyo vipo kila baada ya hatua kadhaa. Tuliendelea na safari huku kila mmoja akiwa kivyake, mara kwa mara mtu ambae alikuwa ametusimamia nilimuona akiniangalia kama mtu aliehisi kitu Fulani, niliogopa lakini nikakaza moyo na kuendelea na chunguzi wangu. Njiani tulikutana na vitu vingi na vyakutisha pamoja na vilio vya watu visivyokuwa na kikomo, niliogopa sana lakini wenzangu sikuwaona kama walikuwa na hali ambayo mimi nilikuwa nayo. Baada ya kutembea kwa umbali mrefu kidogo tulifika sehemu ambayo Yule mtu alituamuru tusimame, tulipofanya hivyo akamuita mwanzake ambae tulimkuta katika hilo eneo na kuanza kuongea nae kwa ishara kama mabubu. Sikutaka kulijadiri lile lakini nilianza kuzunguka zunguka katika lile kundi huku nikiongea peke yangu ili nione nani atanijibu, lakini sikufanikiwa. Mda huo mikuu yangu ilikuwa inauma kutokana na kutembea kwa mda mrefu pia njaa ilikuwa imeanza kunishika. Wawili wale baada ya kumaliza kuongea, msimamizi wa kwanza akaondoka na kutuacha kwa Yule mwenzake, ambae mda mfupi mbele tukaendelea na safari tukiwa chini yake “

Petro baada ya kusema vile kama kawaida akanyamaza kupisha maswali na ndipo mwandishi mwingine wa kiume akamuuliza “ unaweza kutuambia huyo mtu wa pili kuwaongoza alikuwa kwenye hali gani, ya kutisha au ya kawaida “ Petro akajibu “ kwanza kabla ya yote naomba mlijue hili, huko hakuna mtu mzuri hata mmoja kila mtu yupo kama jini au shetani kuanzia sura zao mpaka roho ni wabaya. Huyo mtu wa pili alikuwa ni mweusi mara mbili ya mkaa alikuwa akionekana macho tu, pia meno yake yalikuwa kama chuma ambacho kimeshika kutu na alikuwa anakucha ndefu ambazo sijawai kuziona kwa binadamu wowote hapa dunia, na sidhani kama kuna ambae ataweza kufuga kucha na kufikia urefu ule. “ mwandishi akaauliza tena swali lingine “ umesema baada ya kupoteza fahamu kule msituni haukushtuka tena mpaka ulipofika huko na ulipoamka ulijikuta ukiwa kwenye kundi la watu, sasa unaweza kutuambia hao wenzako ambao ulikuwa nao walikuwa kwenye hali gani “ Petro bila kuchelewa akajubu “ wenzangu ambao nilikuwa nao hapo na kuwa msafara mmoja katika kuelekea sehemu ambayo hatuifahamu, wao walikuwa tofauti na wale wengine ambao tulikuwa tumewakuta huko, sisi sote tulikuwa na muonekano wa kibinadamu ila mimi nilitofautiana nao kitu kimoja tu nilikuwa najitambua ila wao walikuwa kama mabumbuwazi au wamepigwa na butwaa “ wale waandishi baada ya kulidhika na yale majibu wakamruhusu aendelee kusimulia nini kiliendelea, Petro akaaendelea. ITAENDELEA 10__13 SIMULIZI; *SITOSAHAU ALICHONIFANYIA BOSS WANGU* 10

………….. ILIPOISHIA……………….

Petro bila kuchelewa akajubu “ wenzangu ambao nilikuwa nao hapo na kuwa msafara mmoja katika kuelekea sehemu ambayo hatuifahamu, wao walikuwa tofauti na wale wengine ambao tulikuwa tumewakuta huko, sisi sote tulikuwa na muonekano wa kibinadamu ila mimi nilitofautiana nao kitu kimoja tu nilikuwa najitambua ila wao walikuwa kama mabumbuwazi au wamepigwa na butwaa “ wale waandishi baada ya kulidhika na yale majibu wakamruhusu aendelee kusimulia nini kiliendelea, Petro akaaendelea.

…………… INAENDELEA …………………..

“ tukiwa chini ya Yule mtu tulitembea kwa umbali kidogo kisha tukakutana na kundi lingine la watu ambao wengi wao walikuwa wamechoka na wamelegea kama mtu ambae amekaa mda mrefu bila kula huku akifanya kazi ngumu. Tukaamuliwa kuchanganyika na wale watu, mda huo sikujua ni saa ngapi maana niliona mda kama hautembei katika eneo lile kutokana na ile hali kutobadilika hata kidogo, pia njaa ilizidi kunichukuwa na taratibu nikaanza kupoteza nguvu. Tuliendela kutembea na kufika katika mji mmoja ambao sikujua unaitwaje, nilijaribu kuvuta taswira ya eneo lile labda nitapafahamu lakini sikufanikiwa. Huo mji ulikuwa kimya na giza nene likiwa juu yake , pia eneo hilo kulikuwa na ndege wengi wa ajabu sana sana bundi, naweza kusema walikuwa walinzi wa eneo lile kutokana na kuwa makini kutuangalia. Kama kawaida nilipofka huko nikaanza kuzunguka baadhi ya maeneo ya mji ule huku nikifuatwa na baadhi ya bundi, sikuwajari bali niliendelea na safari yangu ya kuzunguka katika ule mji mdogo. Wakati naendelea kuzunguka huku nikiwashangaa wale ndege, nilikutana na dada mmoja ambae nilimuona yuko tofauti kidogo na wale wenzetu wengine, nilihisi anajifahamu tofauti na wale wengine, bila uwoga nilimfuata na kuanza kumuongelesha lakini alitikisa kichwa chake na kuanza kuongea kwa ishara kama bubu. Nilisikitika sana maana niliona nimefikilia kitu ambacho kipo tofauti, ndipo nikachukua uamuzi wa kuachana nae na kurudi walipokuwa wenzangu maana hapakuwa mbali. Nilipofika huko mara alikuja Yule mtu akietusimamia akiwa ameongozana na wenzake wanne huku wameshika mandoo mikononi mwao, nilifurahi baada ya kuona vile, nilijua tumeletewa maji ya kunywa maana kiu nayo ilikuwa imenishika. Walipofika tulipo sisi wakaweka yale mandoo chini kisha wakaondoka zao, mda huo karibia wenzangu wote wakasimama sikujua kwanini wamefanya vile. Sasa kile kitendo cha wale wasimamizi kutugeuzia visogo, nilisukumwa na kundi la watu ambalo lilikuwa likikimbilia katika yale mandoo, nilijiuliza ni nini kile ambacho kimeletwa mpaka watu hawa wawe hivi, pia nikajiuliza tena je kwa uwingi wa watu hawa kitu kile kitatosha kwa wote. Nikiwa kwenye hali ya mawazo watu wakaanza kutoka kwenye lile eneo ambalo liliwekwa yale mandoo na kila ambae alikuwa akitoka eneo lile alitapakaa unga mwilini mwake, nikiwa kwenye hali ya mshangao nilijiuliza mwenyewe wale watu kukimbia kote na kusukumana walikuwa wakikimbilia ule unga, nilisikitika sana. Sasa wakati naendelea kuwashanga, ghafla niliguswa begani nilishtuka kupita kiasi maana sikutegemea kutokea jambo lile. Haraka nikageuka ili nimuone huyo alienigusa ndipo nikakutana uso kwa uso na Yule dada huku akiwa anatabasamu kama mtu ambae hayupo kwenye matatizo. Nilishangaa kumuona akiwa kwenye ile hali lakini nilishindwa kumuuliza maana nilijua awezi kuongea kutokana na kile ambacho alinionyesha mara ya kwanza. Nilikaa kimya huku nikimtazama na kusubiria nini anataka kufanya, lakini nilishtuka baada ya kusikia akiniambia neno NIFUATE. Moyo wangu ulilipuka maana sikutegemea kabisa kitu kile, haraka nikamfuata na ndipo tukaenda kukaa katikati ya kundi la watu jambo ambalo alikunipendeza, kwasababu nilitamani niongee nae mambo mengi lakini kwa siri. Akaniuliza ninaitwa nani nikamtajia jina langu, pia na mimi nikamuuliza yeye anaitwa nani lakini hakutaka kunitajia jina lake. Hilo sikujari sana bali nilimuuliza pale tulipo ni wapi akanijinbu “ hapa tulipo ni sehemu ya mkuu wa giza, mkuu wa wachawi wote, shetani “ Baada ya kunijibu vile nilishika kichwa changu na kutazama huku na kule kisha nikamuuliza swali lingingi kuhusu lile eneo wapi lilipo kwa huku duniani, akanijibu “ Petro hili eneo wala halipo duniani bali lipo chini ya dunia sehemu ambayo watenda dhambi wote watatupwa siku ya kiama yani siku ya dunia kufika mwisho wake na kukutana na moto mkali kuliko yote duniani “. ITAENDELEA

SIMULIZI; *SITOSAHAU ALICHONIFANYIA BOSS WANGU* 11

Aliponiambia vile mapigo ya moyo wangu yakaanza kwenda mbia kutokana na yale niliyoambiwa, pia nikajiuliza nitakuwa tayari nimekufa au laa, nilikaa kimya kidogo kisha nikamuuliza swali lingine kuhusu uwepo wake yeye maeneo yale, lakini aliniju kwa mkato “ Kuhusu mimi kuwepo huku ni stori ndefu kidogo na kama itanipendeza nitakusimulia kwa ufupi “ aliponiambia vile nikatikisa kichwa changu kuashiria kukubali kile alichoniambia, lakini na yeye alishangaa uwepo wangu katika ile sehemu na kuniuliza nimefika vipi kule, nilimueleza kwa ufupi lakini hakuniamini na kuniambia sehemu kama ile siwezi kwenda mtu hai kama nilivyokuwa mimi. Alipomaliza kuniambia vile na mimi nikamuuliza swali lingine kama yeye alikuwa tayari amekufa au laa, lakini hakunijibu na kuniambia siku ikimpendeza ataniambia ila alinisihi nisikae mbali na yeye popote tuendapo. Kabla hatujamaliza kuonge nilimuuliza swali la mwisho, kwanini mda ule alinijibu kwa ishara kama mtu asijua kuongea, akanijibu “ nilifanya vile watu wa eneo hili wasijue kama mimi nipo tofauti na wengine “ nilimuuliza hao watu wangejuaje na wakati tulikuwa wawili tu eneo lile, akanijibu “ wala hatukuwa wawili, wale ndege aina ya bundi ambao ulikuwa unawaona wakikufuata ni malaika wa shetani ambao wanafanya kazi ya kulinda hili eneo na kuchunguza nani yupo hapa bila kupitia umauti “ aliponiambia vile nikamuuliza tena jinsi gani hao malaika wanamgundua mtu ambae ajapia umauti, akanijibu “ Wanagundua kama hivi nilivyo mimi na wewe yani kujitambua, tofauti na mtu alieonja umauti uwa kama taila maana uja huku bila akili yoyote “. Nilisikitika sana nilipoambiwa vile, kisha nikautazama umati wa watu ambao ulikuwa eneo lile, nikamgeukia tena na kumuuliza swali lingine kuhusu umati wa watu waliopo kule kuwa wote ni watenda dhambi, akaniji “ hapana “ ghafla akanyamaza kuongea na kuanza kunielekeza kwa vitendo kama alivyofanya mara ya kwanza. Nilipomuuliza kwanini anafanya vile, akanionyesha ishara nigeuke nyuma na nilipofanya hivyo niliwaona wale wasimamizi wakiwa karibu yetu. Nilinyamaza na kuendelea kufanya mambo mengine huku roho yangu kwa mbali ikiwa imepata faraja kutokana na kumpata mtu ambae anafahamu mambo mengi kuhusu sehemu ile. Baada ya hapo wale watu wakatukusanya wote pamoja na kuendelea na safari yetu ya kuelekea kusiko julikana. Tukiwa njiani Yule dada alinisogerea na kuniuliza swali “ Tangu ufike huku una mda gani “ nahisi kama masaa mawili au matatu nilimjibu, akatikisa kichwa cheke kuashiria kukubali kile ambacho nilimwambia na kuniambia kitu ambacho kilinishangaza sana “ Kwahiyo una siku tano tangu utoke duniani “. Nilimuuliza kwanini amesema vile ndipo akaanza kunielekeza jinsi masaa ya kule yanavyopishana sana na huku duniani “ Huku kunatofautina sana na duniani sana sana kwenye swala la mda, saa moja la huku sawa sawa na siku mbili kule duniani “ nilibaki mdomo wazi. Tuliendelea na safari na hatimae tukafika sehemu nyingine ambayo tulikutana na mji kama ule wa kwanza lakini huo ulizidi ukubwa kidogo, pia kulikuwa na watu wanaishi hapo tofauti na ule wa kwanza. Tulipofika Yule dada akanifuata na kuniambia kuwa niwe makini sana kwenye ule mji na nisiwe mtu wa kuchunguza chunguza vitu kama nilivyofanya kwenye mji wa kwanza, nilimuuliza kwanini akaniambia ule ni mji wanaishi viumbe wabaya wasio na huruma hata kidogo. Nilimuuliza yeye aliwajuaje lakini hakuniambia zaidi ya kutabasamu na kuniambia mda ukifika ataniambia kila kitu kuhusu eneo lile na uwepo wake yeye kule.

ITAENDELEA

SIMULIZI; *SITOSAHAU ALICHONIFANYIA BOSS WANGU* 12 & 13

……………… ILIPOISHIA……………….

Tuliendelea na safari na hatimae tukafika sehemu nyingine ambayo tulikutana na mji kama ule wa kwanza lakini huo ulizidi ukubwa kidogo, pia kulikuwa na watu wanaishi hapo tofauti na ule wa kwanza. Tulipofika Yule dada akanifuata na kuniambia kuwa niwe makini sana kwenye ule mji na nisiwe mtu wa kuchunguza chunguza vitu kama nilivyofanya kwenye mji wa kwanza, nilimuuliza kwanini akaniambia ule ni mji wanaishi viumbe wabaya wasio na huruma hata kidogo. Nilimuuliza yeye aliwajuaje lakini hakuniambia zaidi ya kutabasamu na kuniambia mda ukifika ataniambia kila kitu kuhusu eneo lile na uwepo wake yeye kule. …………….. INAENDELEA ……………………..

Sasa tukiwa tumepumzishwa hapo, kama kawaida wale wasimamizi wakaenda kuchukuwa mandoo ya unga na kuleta tulipo sisi, mda huo sikutaka kujiweka nyuma haraka nikakimbia na kuanza kula ule unga huku nikiwa nasukumwa na kukanyagwa na wenzangu ambao na wao walikuwa wakiitaji kula. Mda huo yule dada alikuwa amesimama pembeni akiwa ananitazama kile ninachokifanya. Nilipomaliza kula na kuona angalau tumboni kuna kitu nikarudi tena kwake huku nikiwa nimechafuka unga mdomoni na baadhi ya sehemu katika mwili wangu. Yule dada akaniuliza “ ulikuwa na njaa sana “ nikaitikia akanitazama kwa mda kisha akaongea tena “ unatamani uishi huku mpa mwisho wa uhai wako “ hapana sitamani nilimjibu “ kama hautamani basi unatakiwa kuvumilia baadhi ya vitu ukiwa huku maana wewe ni tofauti na hawa wenzako na kama utaendelea kula ule unga maisha yako yatakuwa huku milele, ila jua unanafasi ya kurudi duniani endapo utaweza kuyashinda majiribu ya huku “ nilijiuliza ni majaribu gani lakini sikupata jibu na yeye akuendelea kuongea, nilitamani nimuulize maswali lakini hakuonyesha hali yoyote ya kunijari. Lakini mda wote nilikuwa nikitafakari lile neno ambalo aliniambia kuwa nina nafasi ya kurudi tena duniani. Baada ya kupumzika kwa mda kidogo wale wasimamizi walikuja na kutuambia tuendelee na safari yetu ndipo yule mwenzangu akaniambia kitu kimoja ambacho kiliniogopesha sana “ tangu tuanze kutembea mpaka sasa tumetumia masaa kama saba na kwa duniani zimepita siku kama kumi naa, huko tunakoelekea sasa ni mbali sana tunaweza kutumia hata masaa kumi na tano au kumi na sita sawa sawa na siku 35 au hata 40 duniani. Hii safari haitakuwa na mapumziko tena mpaka tunafika huko tuendako mikononi mwa kuu wa giza na kutufanyia kile atakacho sawa sawa na tulivyo pangiwa “ nikamuuliza swali “ je hatuwezi kukimbia ili tusifike huko “ akanitazama na kunijubu “ kwa upande wako wewe inawezekana lakini kwangu mimi sio rahisi hata nifanye nini “ nilihitaji kujua kwanini kwa upande wangu mimi inawezekana lakini kwake yeye haiwezekani ndipo akaanza kuniambia na kunipa stori yake kwa ufupi.

“ kwanza kabisa wakati nipo duniani nilikuwa mchawi na nimetoa roho za watu wengi sana wasio na hatia, niligeuza binadamu wenzangu kuwa vifaa vya kufanyia kazi, lakini kuna siku nilifanya makosa nilishindwa kumuua mama yangu mzazi ndipo nikapewa adhabu ya kuja huku. Ila kwa kule duniani nilipoteza maisha kabisa kama wengi wao hapa na ndio maana siwezi kutoka huku kwa hizo sababu kuu mbili. Lakini wewe unauwezo wa kutoka kwa sababu sio mfu kama tulivyo sisi umeletwa huku kwa nguvu za kiza giza ambazo ni rahisi sana kuzishinda “

Baada ya kuniambia vile ghafla tulisikia kelele za mtu akigumia kwa uchungu niliogopa na kuanza kutetemeka nikamuuliza yule dada huyo mtu analia kwa sababu gani , kanijibu “ Yupo kwenye adhabu ambazo na mimi naenda kukutana nazo nikifika huko “ nilimuuliza kwanini aseme yeye tu na sio watu wote akanijibu.

“ hapa wengi wenu mmeletwa huku kwa ajili ya kubadilishwa kutoka kwenye hali ya ubinadamu na kufanywa misukule na ndio maana vyakula vyenu ni unga. Ila kwa mtu kama mimi au huyo ambae umesikia sauti yake akilia tumeletwa huku kwa ajili ya kupata adhabu ya mateso makali kutokana na kufanya mambo tofauti na tulivyotakiwa kufanya au kupinga amri ya mkuu wa giza “ Baada ya kuniambia hivyo nilimuhurumia sana maana machozi yalianza kumlenga machoni mwake ndipo nikamuuliza swali lingine “ Kwahiyo hayo mateso mwisho wake lini “ akanijibu “ Baada ya kufika huko tunapewa mateso mpaka siku ya mwisho wa dunia yani kiama na hapo ndipo tutaenda kukutana na adhabu kubwa kuliko hizi kutoka kwa MUNGU zikiambatana na moto mkali kuliko huu unaouona huku “

Nilimuhurumia sana maana aliongea kama mtu ambae yupo kwenye majuto makubwa pia na mwenyewe alikili kwa mdomo wake “ Najuta na kujirahumu kwanini nilikuwa mchawi, kwanini nilikubali kuwa chini ya mkuu wa giza, kwanini nilifanya vitendo vya kumchukiza MUUMBA. Natamani nipewe angalau mda mchache ili nirudi duniani na niwaambie ndugu, jamaa na marafiki ambao wapo chini ya shetani, waachane nae maana huku sio kuzuri hata kidogo na ukipata bahati mbaya kuja huku kama nilivyokuja mimi utajutia maisha yako yote na kutamani kama usingezaliwa “

Maneno yake yaliuchoma sana moyo wangu maana alinisihi kama nikibahatika kurudi huku duniani niwaambie watu juu ya swala hili na waachane kabisa na swala la uchawi pamoja na mambo yote yenye kumchukiza MUNGU maana mwisho wa hayo yote ni kuzimu ambako watakutana na mateso makali mara kumi uangukiwe na ghorofa au ukanyagwe na treni kuliko adhabu utakazo kutana nazo huko. Baada ya kuniambia vile nikamuuliza swali lingine kuwa ana mda gani tangu afike eneo lile akanijibu “ nina mda mrefu kidogo na kama sio kukimbia kimbia kabla sijafika kwenye adhabu wala usingenikuta maana wenzangu ambao nilifika nao huku ndio hao unao wasikia huko wakigumia “

Nilimuuliza kwanini alikuwa anakimbia na akanijibu “ NIlikuwa ninatafuta njia ya kurudi tena duniani ili nifikishe huu ujumbe kwa ndugu zangu na wao waufikishe kwa watu wengine lakini mara zote imekuwa ikishindikana kwa sababu neema ya kuendelea kuishi duniani kwa upande wangu tayari imeondolewa lakini kwa kuwa nimekutana na wewe najua tayari ujumbe utakuwa umefika duniani “
Nilimuuliza ana uwakika gani, akaniambia mimi ninaweza kurudi duniani maana neema yangu bado haijaondelewa bali watu ndio wametaka kuindoa, nilifurahi kusikia vile na hapo nikaadha kufikiria siku nikifika duniani na kukutana tena na familia yangu itakuwa ni siku ya aina gani.
ITAENDELEA GUSA HAPA KUENDELEA KUSOMA

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA

Mpya zaidi Nzee zaidi

Ads related

Smartwatchs