03__05
SIMULIZI;*SITOSAHAU ALICHONIFANYIA BOSS WANGU* 03
“ Baada ya kuona vile, taratibu nikaondoka lile eneo la mkutano na kuanza kuzunguka huku na kule na lile gari la ofisi. Nilipofika maeneo Fulani ambayo sikujua ni sehemu gani, pembeni ya barabara niliona mabibi wawili wakinitizama huku wakitikisa vichwa vyao huku wakiwa wanatokwa na machozi. Nilijiuliza kwanini wale watu walikuwa kwenye ile hali lakini sikupata jibu na kuamua kupuhuzia jambo lile. Baada ya kwenda mbele zaidi, nilimuona mtoto mmoja wa kike akiwa amekaa upanda ule ule ambao wale mabibi walikuwa wamekaa, pia na yeye nilimuona akitokwa na machozi ila nilishangazwa kidogo nilipoona akisimamisha gari langu, haraka nikasimama na kushuka kwa ajili ya kwenda kumsikiliza nini alikuwa anahitaji, maana mda huo alikuwa amesimama katikati ya barabara. Lakini cha ajabu baada ya kushuka kwenye gari tu ghafla Yule mtoto alitoweka kwa mazingira ya kutatanisha, maana sikuona wapi alikuwa ameenda. Nilipoona vile nikarudi ndani ya gari huku mapigo yangu ya moyo yakienda mbio kutokana na kile ambacho nilikuwa nimekiona. Haraka niligeuza gari na kuanza kurudi kule ambako nilikuwa ninatoka na nilipofika pale ambapo mabibi walikuwa wamekaa, pia niliwakuta lakini walikaa upande mwingine tofauti na mara ya kwanza, wakiendelea kusikitikia huku wakibubujikwa na majozi. Kutokan na kile kilichonikuta sikuhitaji kusimama tena maana nilihisi ile sehemu kuzungukwa na nguvu za giza. Baada ya kuwapita wale mabibi nikaendelea na safari hatimae nikafika kwenye eneo ambalo kikao kilikuwa kinafanyika. Nilitafakari na kujiuliza maswali mengi kuhusu vile ambavyo niliviona lakini sikupata jibu zaidi ya kichwa changu kupata moto na kuanza kuuma. Nilikaa kwenye gari kwa mda kama wa masaa mawili kwa bahati mzuri nikapitiwa na usingizi mzito ambao ulipelekea kuota ndoto mbaya, na kufanya nizidi kuamini katika lile eneo wetu wake ni wachawi sana. Nilipoota ile hiyo ndoto nilishtuka kutoka usingizini maana hata sikutamani tena kulala nilihisi ile ndoto ingejirudia “
Petro baada ya kusema vile akanyaamaza kupisha wale waandishi kuuliza swali lolote, lakini hakuna ambae aliuliza kwahiyo akaendelea kusimulia.
“ Nikiwa nimekaa kwenye gari na kutafakari lile eneo, niliwaona wenzangu wakitoka kwenye ukumbi na kuja ambapo nilikuwa nimepaki gari na kuniambia tutafute sehemu kwa ajili ya kupata chakula cha mcahana maana mda huo ilikuwa ya pata majira ya saa tisa au saa kumi kasoro. Baada ya kuambiwa vile nikawasha gari na kuondoka zetu na mda mchache mbele tukafanikiwa kupata sehemu ya kula chakula, lakini mda wote huo nilikuwa sijawaambia wenzangu vitu ambavyo nilikutana navyo nilipoenda kuzunguka. Basi tulikula na baada ya kumaliza tukapumzika kama nusu saa na kuanza safari ya kuludi nyumbani, mda huo ilikuwa yapata majira ya saa kumi na moja jioni. Tulipotoka pale tukapitia sheri kutia mafuta na kuianza safari rasmi ya kuludi nyumba. Mda huo wote mawazo yangu yalikuwa yakimuwaza mke wangu pamoja na watoto wangu, na kikubwa ambacho nilikuwa ninawaza ni zawadi gani mzuri ya kuwachukulia. Ilipofika majira ya saa moja na nusu usiku tulifika sehemu moja ambayo hapo kuna wafanya biashara wa kila aina kwa ajili ya wasafiri na hapo ndipo nikakusanya vitu vingi sana kwa ajili ya kuifurahisha familia yangu. Kama ningejua kitu ambacho kinakuja mbele yangu, sidhani kama vile vitu ningenunua lakini kwa kuwa nilifumbwa kujua kitu cha mbele basi nilifanya hivyo. Majira ya saa mbili kamili usiku tuliondoka eneo lile na kuendelea na safari yetu, huku wote wanne tukiwa na furaha tele kutokana na vile vitu ambavyo tulikuwa tumenunua kwa ajili ya familia zetu. Baada ya kutembea kwa umbali mrefu kidogo kutoka kwenye lile eneo, ghafla kichwa kikaanza kuniuma tena kwa nguvu, na macho yangu yakaanza kupungua uwezo wa kuona. Nilipoona vile nikasimamisha gari pembeni kidogo ya barabara na kuwaeleza wenzangu hali ambayo ilikuwa imenipata ghafla, na kuomba mmoja wapo anisaidie kuendesha gari kwa ajili ya usalama wetu, lakini nilishangaa kuona wote wakilazimisha mimi kuendelea kuendesha lile gari. Nilijitahidi kuwaomba nisifanye hivyo lakini wao hawakukubali, na kwa kuwa walikuwa wakubwa kikazi ilinibidi niendelee kuendesha lakini mda huo hali yangu ilizidi kuwa mbaya zaidi. Zilipita dakika kadhaa huku ile hali ikiendelea kunisumbua, na baada ya kusogea mbele kidogo macho yangu yalishindwa kabisa kuona. Baada ya kufikia hiyo hatua ya kuto kuona kabisa ghafla nikaanza kusikia sauti za wenzangu zikigumia kuomba msahada, jambo ambalo liliniogopesha sana maana nilikuwa sijui nini kinaendelea. Baada ya kupita sekunde kadhaa ghafla nilianza kujigong gonga huku na kule ndani ya lile gari, na hapo ndipo nikagundua kuwa tulikuwa tumepata ajari, na mda mchache baadae nahisi nikapoteza fahamu maana sikuelewa nini kiliendelea pale. Baada ya kupita mda Fulani nilihisi kumwagiwa maji usoni ghafla nikashtuka na cha ajabu zaidi mda huo maumivu ya kichwa yalikata kabisa pia macho yangu yalikuwa yanaona vizuri sana, mda huo nilikuwa nimelazwa pembeni kidogo na sehemu ambayo gari lilikuwa nimepinduka. Nilitazama huku na kule nikawaona wale wenzangu watatu wakiwa wamesimama pembeni yangu huku bosi akiwa ameshika kibakuri chenye maji ndani yake.
ITAENDELEA
SIMULIZI;*SITOSAHAU ALICHONIFANYIA BOSS WANGU* 04
……… ILIPOISHIA ………….
Baada ya kupita mda Fulani nilihisi kumwagiwa maji usoni ghafla nikashtuka na cha ajabu zaidi mda huo maumivu ya kichwa yalikata kabisa pia macho yangu yalikuwa yanaona vizuri sana, mda huo nilikuwa nimelazwa pembeni kidogo na sehemu ambayo gari lilikuwa nimepinduka. Nilitazama huku na kule nikawaona wale wenzangu watatu wakiwa wamesimama pembeni yangu huku bosi akiwa ameshika kibakuri chenye maji ndani yake.
……….. INAENDELEA ……………………
Wenzangu baada ya kuona nimeamka, Bosi alinipa mkono na kuniinua pale ambapo nilikuwa nimelala, maana mda huo watu walianza kujaa kwenye eneo la tukio. Sasa tukiwa tumesogea pembeni watu walitufuata na kuanza kuuliza maswali juu ya kile kilichotokea, lakini haoawakuonyesha hali yoyote ya kunijari, na kupelekea kujiuliza kwamba awanioni au laa. Nikiwa kwenye hali ya mawazo, sehemu ambayo lile gari lilianguka nilisikia sauti za watu zikisema kuna mmoja bado yupo ndani amebanwa vibaya sana. Nilishtuka sana niliposikia vile na kujiuliza huyo mwingine alibanwa humo ni nani, maana wote wanne tulikuwa tumesimama sehemu moja na hakuna hata mtu ambae alibaki kwenye gari. Wale watu baada ya kusema vile, vijana kadhaa walisogea kwenye gari na kuanza harakati za kumtoa mtu ambae yupo kwenye hilo gari, nilitamani niende kuwasaidia ili nimuone mtu mwenyewe lakini bosi alinizua na kuambia nitulize akili yangu kwanza, nilikubari lakini roho yangu iliumia sana. Baada ya kupita dakika kadhaa tuliona wale vijana wakitoka kwenye lile gari huku wakiwa wamembeba mtu juu ambae alionekana kuvunjwa na damu mwili mzima, nilishangaa sana kuona vile na kujawa na shahuku ya kutaka kumuona huyo mtu ambae alikuwa amebaki kwenye lile gari. Daaa sikuamini macho yangu baada ya wale vijana kusogea karibu na mimi, maana mtu ambae walikuwa wamembema nilikuwa ni mimi mwenyewe. Nilipoona vile haraka nilimgeukia bosi na kumuuliza kama ameona kile ambacho mimi nimekiona, lakini hakunijali ndipo nikachukua ahamuzi wa kuwaita wale vijana ili wasimame na nimuangalie vizuri Yule mtu, lakini na wao awakunijali na wala hawakuonyesha hali ya kunisikia tu. Nikiwa kwenye hali ya kuangaika kutaka kujua kuhusu lile swala nilimuona mwenzetu mmoja analia huku akilitaja jina langu, lakini bosi pamoja na mwenzetu mwingine wao hawakuonyesha hali yoyote ya kujari jambo lile. Nilimtazama Yule mwenzangu na kujiuliza kwamba anioni au laa lakini sikupata jibu, ndipo nikachukua uamuzi wa kumfuata ili nimuulize nini kinamliza. Nilipomsogelea na kumgusa hakugeuga na wala hakuonyesha ishara ya kuisi kuguswa na kitu chochote bali aliendelea kulia huku akilitaja jina langu. Kuanzia hapo kichwa changu kikaanza kupata moto na kujiuliza maswali mengi ambayo yalikuwa hayana majibu. Baada ya kuona vile, nikarudi tena kwa Bosi na kumuuliza nini kinaendelea lakini yeye aliniambia neno moja tu TULIA, hakuendelea kuongea neno linguine zaidi. Baada ya kuniambiwa vile nilitoka na kuelekea sehemu ambayo wale vijana walimpeleka Yule mtu , lakini wakati naelekea huko kila mtu ambae nilikuwa napishana nae hakuonyesha hali yoyote ya kuniona, na mda mwingine nilikukwa nikimgusa mtu au kumgonga ili nione kama
angeniona lakini sikufanikiwa. Kuanzia hapo nilihisi kuchanganyikiwa kutokana na lile ambalo lilikuwa limetokea, niliona kama ndoto. Nilipofika sehemu ambayo Yule mtu amelazwa, nilijikuta nikitokwa na machozi maana lile jambo lilikuwa linatisha. Nilijaribu kupenyapenya na hatimae nikafika mpaka mwili wangu mwingine ulipo na kuanza kuukaguwa huku mwili wangu ukiwa unatetemeka kama mtu ambae amemwagiwa maji ya baridi sana. Lakini wakati nafanya hivyo nilishangazwa na kitu kimoja maana kila nilipokuwa nikiugusa ule mwili nilisihi kama ninagusa kitu kigumu mithili ya mti mbichi ambao umeviligiwa kwenye kitu Fulani. Nilitamani niwaulize watu kama na wao wameona ile hali, lakini nilishindwa maana hakuna mtu ambae alikuwa ananiona, jambo ambalo liliniumiza sana. Baada ya saa kama moja kupita gari la polisi likawasiri kwenye lile eneo na kuanza kufanya kazi yao ya uchunguzi wa awali. Kwanza waliutazama ule mwili na kuufunika na kitambaa ambacho walikuja nacho kisha wakaenda sehemu ambayo Bosi pamoja na wale wanzangu walikuwa wamekaa na kuanza kuwauliza maswali. Nilipoona vile, haraka nikasogea na kuanza kusikiliza nini wale polisi wanauliza. Nilishangaa sana baada ya kusikia polisi mmoja akimwambia Bosi amtajie jina la marehemu na bila wasiwasi akataja jina langu, nilitamani kugumia lakini nilijikuta nikiishiwa nguvu ya kufanya hivyo. Ndipo nikasogea mpaka pale ambapo yeye yupo na kuanza kumuomba awaambie ukweli kuwa mimi sijafariki, lakini yeye alinitizama na kutabasamu kisha akaendelea kuongea na wale mapolisi. Niliumia sana na mwishoe nikakata tama na kukaa chini huku nikiwa nalia kwa uchungu, nilimkumbuka mke wangu pia niliwakumbuka sana watoto wangu na mwisho nikajiuliza mwenyewe kitu gani kimetokea kwangu. Nikiwa kwenye hali ya huzuni, gari la wagonjwa lilifika na kuuchukua ule mwili na kuupeleka hospitali kuu ya mko, ila Bosi pamoja na wale wenzangu waliambiwa wapande kwenye gari la polisi kwa ajili ya kwenda kutoa maelezo kituoni. Baada ya wale wenzangu wawili kupanda kwenye gari, Bosi akanifuata sehemu ambayo nilikuwa nimekaa na kunishika mkono na kwenda kupanda gari pamoja nae. Mara kwa mara nilijiuliza kwanini watu wengine hawanioni lakini Bosi alikuwa ananiona lakini sikupata jibu lolote kichwani kwangu.
ITAENDELEA
SIMULIZI;*SITOSAHAU ALICHONIFANYIA BOSS WANGU* 05
Basi baada ya hapo tulichukuliwa mpaka kwenye kituo cha polisi na ndipo Bosi akaanza kutoa maelezo kuhusu ile ajali jinsi ilivyotokea. Nilishanga kusikia bosi akisema chanzo cha ajari ni uzembe wangu kutokana na kuendesha gari kwa wendo kasi huku nikiwa nimelewa, nilijitahidi kupinga maneno yale lakini kwa bahati mbaya hakuna ambae alinisikia zaidi ya bosi, kwa dharau akanigeukia na kuanza kunicheka,niliumia sana. Alipomaliza kutoa maelezo tulichukuliwa na kupelekwa hospitali kuuangalia mwili wa mtu ambae amefanana na mimi kila kitu, lakini baada ya kufika huko nilishtuka nilipoona ule mwili ni mti ambao umevesha nguo shat pamoja na suruali. Jambo lile nahisi wenzangu hawakuliona maana niliwaona wakisikitika na kusema kuwa nimeumia vibaya sana, nilijitahiti kuwaita
na kuwagusa ili wagundue yule wanae muangalia sio mimi lakini ilishindikana, kwa hasira niligumia na kujipigapiga kichwani huku majozi pamoja na kamasi vikitapakaa usoni kwangu kutokana na kulia kwa mda mrefu. Mda mfupi mbele kwa mbali nje ya jingo la mochwali nilisikia sauti ya mwanamke ikiita mume wangu mume wangu, nilijiuliza ni mwanamke gani ambae analia lakini baada ya kuingia ndani sikuamini macho yangu, maana alikuwa mke wangu ambae ameambatana na baadhi ya rafiki zake na rafiki zangu pia. Nilipowaona haraka nikawasogelea na kuanza kumuita mke wangu huku nikimtikisa kwa nguvu, lakini na yeye hakuonesha hali ya kuhisi kitu chochote zaidi ya kung’ang’ania kuukumbatia ule mwili ambao ulikuwa upo kwenye jokofu la kuifadhia mahiti. Baada ya kuangaika mda mrefu bila mafanikio yoyote nikamuacha mke wangu kisha nikaenda kukaa chini huku
nikiendelea kulia na kusikitika kutokana na kile ambacho kimenikuta. Zilipita dakika kadhaa na hatimae watu wote tukatotlewa mule ndani na kama kawaida bosi akasogea ambapo nilikuwa nimekaa kisha akanishika mkono na kutoka na mimi nje nikiwa nimeongozana na mke wangu. Tulipofika nje hapo uchungu ulizidi kupita kiasi baada ya kuona watoto wangu wakilia kwa uchungu huku wakiita baba baba, nilitamani niende kuwanyamazisha lakini nilishindwa fanya hivyo, ndipo nikamtazama Bosi na kumuuliza
kwanini umenifanyia vile lakini hakujibu kitu zaidi ya kutabasamu na kuendelea kunivuta na kunipeleka ndani ya gari lingine la ofisi. Kabla sijapanda kwenye gari nilimsikia mke wangu akigumia kama mtu aliepandisha mashetani haraka nikageuka na kuona karibia watu wanne wamemshika mke wangu na kumsaidia kutembea, kwa hasira nikamuita kwa jina lake, ghafla akasimama na kuangalia sehemu ambyo mimi nilikuwepo huku akiwa kama mtu aliesikia kitu Fulani. Mapigo ya moyo wangu yakaanza kwenda mbio
na kujiuliza itakuwa amenisikia au lakini sikupata jibu na kuamua kumuita tena kama ambavyo nilifanya mara ya kwanza lakini mda huo hakugeuka. Nikiwa naingia kwenye gari nilitazama wanangu ambao walikuwa wameshikwa na rafiki yangu wa karibu sana huku wote wakiwa kwenye hali ya majonzi yasio na kifani. Basi baada ya hapo watu wakaludi nyumbani na mipango ya mazishi yakaanza kufanyika. Siku ya pili majira ya saa kumi jioni ule mwili ulizikwa huku mimi mwenyewe nikiwa nashuhudia lakini sikuwa na kitu cha kufanya kwa mda ule baada ya kugundua kuwa nguvu za giza zipo juu yangu.
ITAENDELEA
GUSA HAPA KUENDELEA KUSOMA
Chapisha Maoni
TOA MAONI YAKO HAPA