SITOSAHAU ALICHONIFANYIA BOSS WANGU* 01 -02

01__02

SIMULIZI; *SITOSAHAU ALICHONIFANYIA BOSS WANGU* 01

“ Sitasahau jambo hili maishani mwangu “ maneno ambayo alitamka petro huku akiwa amezungukwa na kundi la watu. Mama moja baada ya kusikia vile akaanza kuuliza maswali
“ kwanini unasema hivyo, pia tunaomba utuambie nini kilitokea mpaka ukafikia kwenye ile hali “

petro baada ya kuulizwa vile, akainamia chini huku akitikisa kichwa chake mwishoe akakubali kuwaambia nini kilimkuta, na ndipo kila mmoja mle ndani akachukuwa mepeni na karatasi na kukaa vizuri kwa ajili ya kumsikiliza na kuandika vitu muhimu ambavyo ataviongea. “ ilikuwa siku ya jumamosi nilikuwa nimekaa pamoja na familia yangu tukiongea mambo mbalimbali kuhusu maisha yetu, siku hiyo sikuwa na ratiba yoyote kazini, kutokana na magari ya ofisi kuwa na kazi nyingine ambazo walikuwa wanafanya madereva wenzangu ambao tuliajiriwa pamoja hapo kazini.

Ile siku niliifurahia sana maana nilikuwa sipati mda wa kukaa na mke wangu pamoja na familia yangu nikafurahi nao kama ambavyo ilikuwa siku hiyo. Mke wangu na wanangu pia walifurahi maana na wao walikuwa wakitamani sana siku nipate nafasi na nikae nao siku mzima tukiwa tunafurahi kwa pamoja. Raiti ningejua nini kilikuwa kinakuja mbele yangu, nahisi ile siku nisingekuwa na furaha kubwa kiasi kile, pia hata watoto wangu na mke wangu na wao wasingefurahi vile “

Petro aliposema vile, kijana mmoja akamuuliza swali linguine “ kwanini unasema hivyo “ Petro akujibu lile swali maana alijua kuwa wale waandishi wa habari walikuwa wanataka kujua nini kiliendelea, kwahiyo akaendelea kusimulia nini kiliendelea .

“ Ile siku baada ya kufika majira ya saa nne au saa tano asubuhi nikikiwa naongea na kufurahi na familia yangu, mara simu yangu ikaanza kuita na nilipoangalia nikagundua kuwa bosi ndie alikuwa anapiga maana namba yake ilitokea kwenye kioo cha simu yangu. Kama binadamu tungekuwa na uwezo wa kugundua kitu cha mbele nina uhakika ile simu nisingeipokea maana ndio ilisababisha mimi kuonekana mfu na wakati sio mfu “
Baada ya kesema vile akachukua kikombe cha maji ambacho kilikuwa karibu yake na kuanza kunywa maji, alipomaliza akaendelea kuongea huku watu wote wakimsikiliza kwa umakini mkubwa.

“ Nilipoona simu yangu inaita na kugundua ni bosi, haraka nikapokea na kuanza kuongea nae huku nikiwa najiuliza nini anataka kuniambia. Nilichukizwa sana na maneno yake baada ya kuniomba niende ofisi nikachukue gari ili nimpeleke kwenye kikao ambacho kilikuwa nje kidogo na hapa mjini, na hata mke wangu baada ya kumpa ile taarifa alichukia pia. Nilijitahidi kumdanganya bosi ili ahailishe kunichukuwa mimi na aende na mwenzangu mwingine lakini alikataa katakata, na kuniambia anapenda sana akipanda gari huku dereva nikiwa mimi. Niliumia sana lakini sikuwa na jinsi na kubidi nikubari kufanya kile ambacho yeye alikuwa anahitaji nikifanye japokuwa kwa shingo upande..........
ITAENDELEA chombezotu.blogspot.com

SIMULIZI; *SITASAHAU ALICHONIFANYIA BOSS WANGU* 02

Baada yapo nilienda ndani pamoja na mke wangu na kuanza kujiaanda na nilipomaliaza nilimuaga na kubwambia ukweli wa moyoni mwa kuwa ninaenda kufanya anavyotaka Bosi ila sipo ridhaa, lakini yeye alinibembeleza na kunisihi nifanye hivyo japokuwa na yeye hakupende ile dharula lakini kwa ajili ya kulinda kazi yangu aliniomba nifanye hivyo.

Aliponiambia vile nikamkumbatia na kumpusu shavuni huku mapigo yangu ya moyo yakienda mbio kama mtu ambae anaogopa kitu Fulani au anafanya kitu ambacho hakutegemea kufanya. Baada ya kuagana na mke wangu nikawaita wanangu na kuwaaga pia na kuwaahidi nitarudi usiku na kama itashindikana basi nitarudi siku ya pili yake asubuhi, na kuwaahidi kuwaletea zawadi nyingi kama ambavyo nilikuwa ninafanya nikienda safari yoyote nje ya mji wetu. Niliondoka na kuwaacha wote wakiwa wamehuzunika sana, rahiti ningejua zile nyuso zao za huzuni zilikuwa zikiashilia nini, sidhani kama ningesikiliza ule wito wa bosi wangu. “

Petro baada ya kusema vile akanyamaza kidogo kwa ajili ya kumeza mate na kupunguza presha ambayo alikuwa nayo mda ule. Akiwa kwenye hizo harakati mwandishi mwingine akamuuliza swali lingile ambalo lilipelekea aendelee kusimulia kilichoendelea baada ya kutoka pale nyumbani kwake. “ Baada ya kutoka nyumbani kwako nini kiliendelea “ bila kuchelewa Petro akajibu na kuendelea kusimulia.

“ Baada ya kutoka nyumbani nikaenda moja ka moja mpaka ofisi na kumkuta Bosi akiwa ananisuburia, nikamuomba msamaha kwa kuchelewa lakini yeye alifurahi tu na hakuonyesha hali yoyote ya kuchukia zaidi na yeye kuniomba msamaha kwa kuaribu ratiba zangu. Kuanzia hapo tulianza safari yetu tukiwa watu wanne kwenye gari la ofisi aina ya TOYOTA LAND CRUISER. Tukiwa njiani tuliongea mambo mengi na tulichekesha pia, na kati yetu hakuna mtu hata mmoja ambae alionyesha hali ya tofauti na kupelekea kuichukia ile safari. Kusema kweli baadae nilijikuta nikiifurahia ile safari na ile huzuni ikatoweka kabisa, na ndipo ule usimi

usemae JAMBO USILOLIJUA NIA KAMA USIKUWA WA GIZA ukatimia kwangu, maana niliifurahia safari ambayo ilikuwa mbaya kwangu. Tulisafiri kwa mda wa masaa mawili na kufanikiwa kufika huko eneo la tukio, ambalo tulikutana na wenzetu wengi ambao wametoka sehemu zingine na kuja kwenye hiko kikao. Baada ya dakika kadhaa kupita kikao kikaanza na wale wenzangu wawili pamoja na Bosi wakaingia kwenye ukumbi wa mkutano kwa ajili ya kuiwakilisha ofisi yetu “

Petro baada ya kusema vile, akaa kimya kwa sekunde kadhaa huku akiwa anatizama juu ya paa ya nyumba na kufanya wale waandishi wamshangae, alipomaliza kufanya hivyo akashusha kichwa chake huku akisikitika na kuendelea kusimulia nini kiliendelea.
ITAENDELEA chombezotu.blogspot.com

GUSA HAPA KUENDELEA KUSOMA

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA

Mpya zaidi Nzee zaidi

Ads related

Smartwatchs