Uwongo wa mapenzi❤๐Ÿ’˜

TRUE AND FALSE STORY ❤️๐Ÿ’˜ *LIES OF LOVE (UWONGO WA MAPENZI)*๐Ÿ’” *SEHEMU YA 01----05* Chombezotu.blogspot.com Mpyaaaaaaa๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ *(Stori hii itakuwa na Vipande 60, Unaweza kulipia ili niendelee kukufowadia Vipande Vitano kila Siku au Unaweza kusubiri FULL tarehe 22 mwezi huu, maelezo yapo chini kabisa ya Stori๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡)* ***** "Grrrrrrhhh! grrrrrhhh!" simu ya mkononi ya Anorld iliita akaishika tu na kuitazama bila kupokea kisha akairudisha mezani na kuiacha vile vile iendelee kuita na muda huo huo aliingia rafiki na muwekezaji mwenzake aitwae Henry katika kampuni yao ya A.H BROTHERS, inayohusika na uagizaji na uuzaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi kama magari, vyombo vya kielektroniki, samani za majumbani (furniture) na bidhaa nyingine nyingi, ambayo inamilikiwa na wote wawili. Chombezotu.blogspot.com Anorld na Henry siyo ndugu wa tumbo moja ila ni marafiki walioshibana, marafiki wa miaka mingi tangu walipokutana wakati wanasoma elimu ya sekondari, wakaingia elimu ya juu ya kidato cha tano na cha sita pamoja na hawakuishia hapo, wakaingia mpaka elimu ya chuo kikuu pamoja na mpaka wanamaliza shahada zao katika masomo ya udaktari walikuwa wote pamoja, huwezi kumtaja Henry bila Anorld na vile vile huwezi kumtaja Anorld bila Henry. Baada ya kumaliza masomo yao ya udaktari na kutokana na uchache wa ajira na wingi wa vijana wasomi wanaomaliza vyuo vikuu hapa nchini, Anorld na Henry walijikuta wakiishia kuzunguka na bahasha zao mtaani kutafuta ajira mpaka Anorld alipopata wazo la kuanzisha biashara ya kuagiza vitu vidogo vidogo kutoka nje ya nchi na Henry ambae kwao maisha yalikuwa siyo mabaya sana, baba yake akiwa anafanya kazi ofisi ya mkuu wa mkoa wakati huo akaona isiwe tabu, akaunga mkono wazo la rafikiye kwa kutoa mtaji ambao aliupata kwa njia ya kumdanganya baba yake. Si kwamba nafasi ya ajira kwa Henry haikupatikana, ilipatikana mara kadhaa kutokana na nafasi aliyonayo baba yake lakini aliikataa kwa sababu ya rafiki yake yaani Arnold ambae wameshibana na walikuwa pamoja katika kila hatua kwenye masomo yao na asingependa kufanikiwa yeye bila mwenzake huyo, alikubali kuzikataa nafasi alizounganishwa na baba yake kwenye hospitali kubwa hapa nchini na taasisi za afya na kuungana na Anorld kutafuta ajira pamoja hata kama ni za kawaida kwenye vituo vya kawaida, na hata wazo la biashara lilipotoka kwa rafiki yake huyo ambae wazazi wake walikuwa masikini na alisoma kwa ufadhili wa shirika la kanisa, alilipokea na kuliongezea nyama kwa kuweka mtaji mdogo alioupata kwa baba yake kwa njia ya udanganyifu. Wema wa Henry kwa Anorld haukuwa wa hivi hivi tu yaani usio na sababu, ulikuwa na sababu yenye mashiko, yaani ulikuwa na chanzo. Wakati wote ambao wawili hao walikuwa shuleni tangu kidato cha kwanza mpaka elimu ya chuo kikuu, Anorld ndiye aliyekuwa na akili nyingi darasani, akishika nafasi za juu katika mitihani na wakati huo Henry akiwa kilaza tu ambae nafasi zake ni za mwishoni mwishoni kabisa jambo ambalo halikumfurahisha Anorld, akaamua kujifunga kibwebwe kuhakikisha hatua zote za kitaaluma anazopanda kiwango basi anamshika mkono rafiki yake huyo ama kwa kumfundisha asichoelewa au kwa kumsaidia majibu kwa njia yoyote ile wakati wa mitihani na kuna wakati aliwahi kumfanyia mtihani kwa siri na kwa bahati mbaya ilijulikana wakiwa kidato cha nne, mtihani wa robo muhula, jambo lililomfanya Anorld kusimamishwa masomo kwa muda na kurudishwa nyumbani (suspension) kwa mwezi zaidi ya mmoja mpaka aliposamehewa kutokana na uwezo wake mkubwa darasani ambao ulikuwa unaipa shule sifa katika mitihani ya kiwilaya na kimkoa. "Cheki kaka hizi ishu hapa, nadhani tuanze kuchukua na hizi bidhaa kutoka Dubai, watu wameanza kuziulizia sana siku hizi" Henry alimwonyesha mshirika mwenzake huyo wa biashara. "Oooh ni sawa" Anorld aliitikia lakini akishindwa kuonyesha ushirikiano kwa mwenzake ambae alimtazama kwanza na kisha akaitazama simu iliyokuwa inaita mezani bila kupokelewa. "Mbona unaonekana kama haupo hapa na simu yako inaita wala hupokei, kuna nini kimekusibu kaka, hebu pokea, shemeji anapiga" aliichuku

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA

Mpya zaidi Nzee zaidi

Ads related

Smartwatchs