( USIKU WA HARUSI YANGU) Chombezotu.blogspot.com SEHEMU
YA................... 01 " Nimekuelewa mama, sawa mama, nawezaje kukataa jambo
jema kama hilo? Namaanisha nimekubali moja kwa moja." Ni sauti ya binti mmoja
mrefu wa mnene kiasi, nikisema mnene kiasi namaanisha ana shepu la kihaya.
Mnayajua mashepua ya kihaya nyie. Ndo huyu binti aliekua katupa mgongo akiongea
na simu alikuwa na shepu hilo, mshepu namba nane, huku nywele zake nyeusi
zikining'inia kwenye mabega yake, alikuwa kavaa gauni la kijani kibichi
lililombana kiasi kwamba tuliweza kuiona shepu yake vyema. Miguu yake minene na
mzuri yenye utege wa kulegeza nyonga iling'aa kwa rangi nzuri ya chocolate,
ukimwangalia hivyo tu unakubali mwenyewe kwamba dada yule ni dada wa kishuaa
dada wa kitajiri. " maisara bado unaongea na simu" alitokea binti mmoja
aliejulikana kwa jina la Zawadi, akiwa kavaa miwani wa mikanda mieusi mipana na
mviringo. Alimfanya Maisara ageuke na tuweze kuujua uso wake vyema ni jinsi gani
alikuwa mzuri sana bi dada huyo. Aliachia tabasamu pana kwenye uso wake huku
akimwangalia rafiki yake aliebaki na uso wa mashaka. " una wazimu wewe?'' Zawadi
alimwambia kwa sababu hakujua kinachompa sababu ya kucheka huyo mwenda wazimu
wake ni kitu gani?. Maisara alimtazama tena zawadi tabasamu la furaha likizidi
kumuangazia, haraka sana alimrukia na kumkumbatia huku akiongea kwa sauti. Yaani
ni kama alipiga mikelele. " Thabit kanichumbia, kanitolea posa hadi mahari
tayari zawadi nahisi furaha nahisu furaha mimi, atokee mtu auone moyo wangu
unavyotabasamu " zawadi alihisi furaha zaidi baada ya kusikia hilo. "
Unamaanisha unachosema?" " ndio zawadi " " we kweli" alimtoa wenye kumbatio lake
akaanza kumbia huku akishangiria " jamani hatimae imekuwa kweli, siamini
limetia, hatimae limetimia weuweee" shangwe alilokuwa nalo zawadi lilimfanya
maisara aone aibu, kwani yeye ndo alikuwa kachumbiwa lakini rafiki yake
alishangiria zaidi kuliko yeye. " zawadi ni mwenda wazimu, ahahahahaa" alijikea
hapo kisha akijitazama mara mbili mbili jinsi alivyo kisha akaikumbuka siku ya
kwanza anakutana na Thabiti huyo mwanaume aliemchumbia. Walikuwa hostel yeye
pamoja na rafiki yake zawadi wakijiandaa kutoka, siku hiyo ilikuwa siku ya
ijumaa na walipanga kwenda kulala kwa rafiki yao anaeishi nje ya chuo. Mlango wa
chumba chao ulisukumwa kwa kasi ya kawaida na msichana kibinge na mrefu mweupee,
akaingia ndani moja kwa moja. " yaani bado tu. Nimeenda kwa white mpaka nimerudi
hamjamaliza kujiandaa?" Sophie ambae ni rafiki yao wa karibu sana. " tumemaliza
si unaona mwenyewe, wanafunzi wa first sijui mpoje?" Aliongea zawadi maisara
akamgeukia na kumjibu. " shida sio first year shida ni wavaa miwani, ahahahaa"
maisara alicheka huku wawili hao wakimwangalia kwa hasira ya kutaniana. "
masikio popo wewe" zawadi alitukana. " ndo maana una komwe" Sophie nae alitia
neno. " komwe linatenganisha nywele na nyusi nyie vipi?, tuondokeni mbuzi nyie"
aliwaambua na kuweka begi lake mgongoni kisha wakafunga chumba chao cha hostel
wakaongoza njia hadi sokoni. Sokoni walinunua mahitaji kadhaa ya usiku huo kisha
wakaondoka kuelekea nyumbani kwa Sophie. " Sophie aliwahi kuchukua funguo na
kufunngua mlango wa chumba chake wawili hao yeye akiwa nyuma yao walitangukia
kuingia ndani. Walitupa mabegi yao hovyo na kujitupia kitandani. " hamjaja
kulala hapa mbuzi nyie" Sophie aliwaambia. " sasa tufanye nini? Kwanza
assignment ya madam kimei mlikusanya" alihoji maisara " ndio ulidhani tutaacha,
bahati yako mimi ndo group admin kina faraja waliweka mgomo kabisa usisainiwe"
zawadi alimwambia maisara alietia sura ya aibu maana hakuhudhuria muda huo kwa
sababu alikuwa kalala tu hostel. " lakini si bahati mbaya kwani naonekana kuwa
mzembee?" Alihoji huku akitegemea jibu kali kutoka kwa rafiki zake wawili. "
bora ukae kimya" zawadi alisema na hapo maisara alipitisha kidole chake mdomoni
ishara kaufunga zipu mdomo wake. Marafiki hao wa tatu walianza na ratiba zao
zilizowakutanisha hapo kwa pamoja, hatimae maisara aliingia jikoni kupika
chakula kitamu. Kisha wakatoka kutembea tembea wakiusogeza mda ufike. Majira ya
usiku walirudi wakala na kulala zao, walikuwa wasichana fulani hivi wasio na
mambo mengi, li ufupi walijitambua kitabia na walikuwa marafiki walioshibana
sana. Wasio na walijaliana katika kila aina ya dhiki na hakuna ambae alitamani
kuona mwenzie akikosa furaha. Majira ya asubuhi zawadi aliamka akijinyoisha
nyoosha kisha akachukua ndoo akaweka maji ya kumtosha kisha akael3kea bafuni
kuoga. Wakati huo maisara alikuwa tayari katoa vyombo nje anaosha, Sophie yeye
alibaki kitandani kalala. " ndo maana anazidi kuwa mnene, we mtu gani analala
masaa yote hayo na aridhiki?" Aliongea zawadi akizidi kwenda bafuni. Katika
nyumba hiyo kulikuwa na vyumba vingi sana kama chumba cha Sophie, na bahati ni
kwamba nyumba hiyo walipanga wanafunzi wa chuo zaidi hakukuwa na watu tifauti na
wanafunzi, walikuwa mchanganyiko wasichana kwa wavulana. Kwa sababunilikuwa
asubuhi sana basi mmoja mmoja alifungua chumba chake na kupiga mswaki, wengine
wangeenda kuoga huku wengine wangeingia bafuni kwa haja zao ndogo kisha warudi
kulala. Wakati maisara anaosha vyombo kwenye sink la kupigia mswaki kulikuwa na
vijana wawili wakipiga mswaki, mmoja wao alikuwa mrefu mwenye mwili wa mvuto
rangi yake nyeusi ilikuwa na mng'ao wa kifahari alivutia kwa hakika. Huku kando
yake alisimama kijana mwenzie mwenye makamu kama yake umri miaka 27 hivi, huyu
yeye alikuwa na rangi nyeupe kiasi. kwa pamoja walikuwa wakipiga mswaki huku
hadithi kadhaa zikiendelea. " mpira wa jana haukuwa na mvuto kama ilivyo
zoeleka, hivi chama ndo wa kushindwa kutupa heshima ule mda, yaani walikosa goal
kizembe " alizungumza kijana mwenye rangi nyeupe alitambulika kwa jina la
Richard. " unadhani ni rahisi kama unavyoporoja Richard, mpira so mwepesi kiasi
hicho" kijana mrefu mweusi alimjibu Richard. Wakati huo aligeuz shingo yake
kutazqma bombani, ndipo alipoweza kuuona uso mzuri wa maisara aliekuwa akiinuka
baada ya kuosha vyombo vyote. " ni kweli usemalo Thabit, lakini kwa sasa simba
inatuangusha, kuna muda natamani hadi kuhama timu, tutafakari basi tuhamie Uto
ee!" Richard alimtania Thabit huku akingoja jibu kali kutoka kwa Thabit lakini
Thabit alikuwa kimya. Ilibidi ageuke kusudi aone kinachomfanya Thabit awe kimya
bila kuongea. Ndipo alipoweza kuona wasichana wawili wakipeana nafasi ya kuingia
ndani ya chumba cha msichana aliemtambua kwa jina la Sophie maana hakuwa
kazoeana nae. "Zawadi na Maisara, yupi unaemtazama kwa makini?" Ilibidi amhoji
Thabit kwa sababu aligeuja jumla bila kulegeza macho, na alionekana kuvutiwa
zaidi na mtu mmoja wapo kati ya hao. Kwa akili za Richard alidhani moja kwa moja
Thabit itakuwa kadata na makalio yaliyofichwa ndani ya khanga ya mtoto wa kike
zawadi alikuwa katokea bafuani kuoga. Maana yeye ni mwanaume alafu ashuhidie
vitu kama hivyo asubuhi asubuhi. " jamaa, naona umeelewa chumbo iliyonona kwenye
khanga iliyoloa eee, kumbe umo mshikaji wangu" Richard muongeaji sana alimtania
Thabit. " haiwezi kuwa, nimempenda na so kumtamani, msicha aliekuwa akiosha
vyombo hapo awali huyo ndo kanivutia sana" yalikuwa maneno ya Thabit kumuelekea
Richard ambae aliangua tabasamu na kumjibu. " ni kweli umempenda Maisara?" "
anaitwa maisara, ana jina zuri sana, kweli kabisa nimempenda na sio kumtamani"
maneno ya Thabit yalimfanya Richard afikirie kuhusu kupenda, mmhh! Alikunja
mdomk wake baada ya kuona hiyo itakuwa haraka sana bila shaka, hapana hataki
hivyo, yeye bado muda wake kumkabidhi mtoto wa mtu moyo, huo ni muda wa yeye
kula ujana. " nisaidie kunikutanisha nae" hiyo ilikuwa kauli ya Thabit
kumuelekea Richard aliehisi kuchanganyikiwa. " sawa, mie tena" alijibu na kumpa
Thabit tabasamu pana. Unahisi nini kitafata?????? Usikose kufatilia..........
sijawahi kuwaacha wenyewe sweetheart
Simulizi: MAISARA ( USIKU WA HARUSI YANGU) MTUNZI: KIM SWAN SIMULIZI
HOUSE........... SEHEMU YA.................. 03 Hatimae wawili hao walikaa
katika viti viwili vilivyokuwa vimejitenga na watu wengine kabisaa, yaani
walionekana kuwa VIP kabisaa wawili hao Maisara alijawa na aibu kana kwamba
hakuwa Maisara yule aliekuwa kazoeleka na Thabit kwenye simu, Thabit hakuondoa
macho yake kwa kumtazama msichana huyo.mrembo aliekuwa kavaa gauni la rangi ya
maziwa huku nywele zakiwa zikiwa katika muundo wa kufungwa nyuma kwa kifundo
kilichofanya nyingine nining'inie. Uso wake wa mviringo ulifanya aonekane wa
thamani zaidi. " kuwa huru Maisara " aliongea Thabit na hapo maisara akakaza
shingo yake kana kwamba alitii amri ya kijeshi. " unataka niwe Normal, utaomba
msaada kwa maneno ya mdomoni kwangu" Thabit alitabasamu, ni kweli kabisa
alitamani iwe hivyo. " maneno yako yananipa faraja zaidi mimi, najikuta
nakupenda tu kwa kusikia maneno yako" Maisara alihisi aibu wakati huo wahudjmu
wawili waliwasili pale kwa unyenyekevu, waliuliza kitu gani ambacho wawili hao
watatumia katika huo mtoko. " leta kila kilichoandaliwa hapa" aliongea Thabit
Maisara akamtolea macho yake makubwa, Thabit akamuuliza. " nini?" " una sifa,
kwani we muhaya" Thabit alihisi kucheka kwani kafanya nini hadi aonekane kuwa
mtu wa misifa? Alafu alimuita ye muhaya? " ndio mi muhaya, alafu muhaya wa
bukoba haswaa" " ahaaa! Ndo maana, usijari tumbo langu lipo free kwa kila kitu
yaani mpaka hapo kaa kwa kusubiri uone mtoto wa kike ntavyokushangaza" "
ahahahaa, unishangaze kwa kipi?" " ntakula kila kilicholetwa" Maisara alijibu
kwa Thabit ilionekana kama Masihara lakini huo ndo ukweli alimaanisha kabisa
atakula kila kitu. " kwani we unapendelea kufanya kitu gani katika maisha,
nijibu japo najua unasomea sheria" " nasoma kwa sababu wanataka nisome, hata
sikuwa nimechagua kitu gani nisomee ila baba tayari alifanya maamuzi nisomee
sheria, kwani nani alisema anataka kuwa hakimu kama yeye?" Thabiti alimtazama
kisha akajibu. " sa ntafanya nini? Sina jinsi, kikubwa nisome kwa bidii nifaulu
sana na niuaminishe ulimwengu kwamba nilisoma kufaulu labda mi genius, hapana
isipokua nazingatia maokoto yangu ya baadae, baba yangu ni hakimu, kaka yangu ni
Hakimu pia ahahhaa, imekaaa kwa kuchekesha, lakini hiyo inanipa uhakika kabisa
kwamba mimi ntapata kazi mapema mara baada tu ya kumaliza masomo yangu, najua
unajua tayari connection inanilenga mimi" aliongea Maisara na kufanya Thabit
acheke zaidi, ni kama aliposema ajiachie basi alfungulia bomba mvua kwa kasi ya
ajabu. " yaani sijui niseme nini? Hapa nilipo nina ndoto nyingi sana, bila shaka
natamani kutimiza zote, ntafungua duka la nguo za watoto, duka la urembo na kila
kinachohusiana pia, subiri muda ufike nifaulu, alafu zaidi mimi napenda sana
mziki, ntafungua darasa la mziki kwa ajiri ya watoto na watu wazima ili kukuza
vipaji kwa wanaopenda ku dance" aliongea kana kwamba alikuwa na uwezo wakati
huo. " mmhh! Una ndoto nyingi sana kipenzi, na zote unazifanya lini?" Thabit
aliuliza " nikipata pesa" alijibu huku akiweka uso kwa makini. Thabit hakuweza
tena kuzuia kicheko chake yaani tayari alikuwa na ndoto nyingi hivyo na alisema
akipata pesa. Ahahahaa!. Wakati huo huo kila kitu kililetwa na hapo maisara
alipagawa maana meza ziliandaliwa nyingi mpaka akabaki mdomo wazi. Kwani yeye
aliesema atakula kila kilicholetwa alihisi ni nini? Au alikuwa amesema kwa
bahati mbaya labda ulimi ulitereza? " hapana sitaweza kula hata theluthi, nipo
kwenye mfungo mkali" " hapana lazima utimize ulicho ahidi, huwezi kuvunja" "
sijaahidi kitu chochote mimi, zaidi ya kusema ntakula na sio ahadi usipende
kusingizia watu Mungu hapendi" Thabit alihisi kumuonea huruma, haya sawa, sawa
sawa, nimekuelewa mpenzi utakula kulingana na uwezo wako. Aliongea Thabit na
maisara akachagua meza moja iliyokuwa imeandali vyakula mbali mbali, kwanza
kabisa akalipima tumbo lake kisha akasema. " kwa hapa nahisi nusu nzima
ntamaliza" hapo Thabit alimsogelea na kiti chake baada ya kuangaliana wakaanza
kula kwa pamoja, " mwenyewe naona. Hivyo nusu itayosalia basi ntakula mimi hapa"
kwa maneno hayo walianza kula bila kuchelewesha muda. Maisara alieahidi kula
kitu hakumaliza hata robo ya chakula tayari alihisi kushiba na kumuacha Thabit
akiendelea. Wakati huo huo simu yake iliingia ujumbe. [ mpenzi, mmesha agiza
chakula wewe na huyo sweetheart wako, au bado unabung'aa macho unamuonea aibu]
aiiii! Maisara alihisi aibu kwani alimuonaje? Aliona atapooza nini? Ngoja kwanza
ajibu. [ tangu lini nikapooza mbele zake mtu? Umechundwa zawadi? Najiishi mimi
sifeki mambo kwa mtu. Thabit mwenyewe yupo charming sana, nikiongea anacheka
kama nini?] [ waooh waooohh waooh! Hadi nimependa hakikisha unamkamata huyo
mwanaume mpaka anatangaza ndoa, nipo tayari kukusindikiza mpaka katika chumba
chake usiku wenu wa kwanza] [ sitaki makando kando siku yenyewe] alijibu kana
kwamba tayari aliambiwa ana pendwa? Sema alihisi uhakika ndani yake kwamba
ataambiwa neno nakupenda. Hatimae walimaliza kula wawili hao na kwa pamoja
wakakaa kwa utulivu kando la bwawa la kuvulia samaki. Muda wote huo maisara
alikuwa akijitahidi kuvua samaki kwa uweredi ili asije kosa maana waliekeana dau
kwa kila anaepata basi anaomba chochote kwa mwenzie. Bahati mbaya iliyoje kwa
maisara maana Thabiti alikuwa tayari kapata mara tatu ilhali yeye akiwa amekosa
kabisa. " aaaaahh! Sa ndo nini?" Alilalamika hapo na Thabit alimcheka kisha
akamuuliza " umekata tamaa?" " hayo matumizi mabaya ya dhambi" " hee! Kuna
dhambi nzuri" " ndio, sasa dhambi ya kukata tamaa nayo niifanye kweli hapana?
Ntapambana" alijitahidi kutupia nyavu mwisho akabahatisha kumuinua samaki toka
ndani ya maji akiwa bado kanasa kwenye ndoano, bila kujua alifaa amuweke nchi
kavu kwanza ndo ashangirie ye kwa wenge lake alijikuta akishangiria kwa kumpata
tu. " tulia utampoteza" aliongea Thabit lakini alichelewa tayari maana samaki
alikuwa tayari kajinasua kwenye ndoano na amemuacha maisara. " ana roho mbaya
hanipi hata nafasi ya kumshangiria" aliongea Maisara na kumuacha hoi Thabit,
bila shaka ni kosa lake?. " sawa jaribu tena" maisara hakufa moyo aliamua
kujaribu tena kikubwa ampate huyo samaki au samaki yeyote yule. Kwenye ndoano,
mara hii alikuwa makini zaidi mpaka pale alipobahatisha kumpata huyo samaki wa
kwanza kwa upande wake, Thabit alimpongeza na yeye akafurahia. " bado wa ngapi?"
Thabit alimhoji baada ya kuona katimiza wawili tayari. " bado watatu nipate
mkono" " sawa" Thabit hakuweza kumpinga zaidi ya kumpapu azidi kupambana, na
wakati huo aliitazama saa yake na kugundua ilikuwa tayari ni saa sita za usiku.
Mtoto wa kike wala hakujua kama muda umesonga. Mungu mkubwa maisara alibahatika
kuvua samaki wa tano na hapo Thabit alimhoji. " umekuwa na ujuzi zaidi, vizuri
sana, hutoendelea ili uridhike?" " hapana, nilisema tano acha iwe tano
nimeridhika, nimepata watano wa tano for the first time, i hit it i kill it, i
made it" aliongea kwa shangwe na kujikuta tayari kamrukia Thabit na kumkumbatia
kwa nguvu na shangwe la kufanikiwa. " you kill me too" ( umeniua pia) aliongea
Thabit na kufanya masikio ya maisara yapate utulivu, hivi kweli alikuwa akiongea
na nani wakati huo? Alikuwa akiongea na Thabit ambae alijikaza haswaa kwenye
mwili wake alihisi aibu alianza kujitoa pole pole huku macho yake mazuri na ya
mviringo yakikosa ujasiri wa kumtazama Thabit. Unahisi nini kitafuata........??
Usikose kufatilia mkasa huu mtamuu... njoo uimalize kwa 1000 tuuuu [06/12,
17:31] +255 693 292 583: Simulizi: MAISARA ( USIKU WA HARUSI YANGU) MTUNZI: KIM
SWAN TEAM: SIMULIZI HOUSE........... SEHEMU YA.................. 04
Ilipoishia............... " you kill me too" ( umeniua pia) aliongea Thabit na
kufanya masikio ya maisara yapate utulivu, hivi kweli alikuwa akiongea na nani
wakati huo? Alikuwa akiongea na Thabit ambae alijikaza haswaa kwenye mwili wake
alihisi aibu alianza kujitoa pole pole huku macho yake mazuri na ya mviringo
yakikosa ujasiri wa kumtazama Thabit. Songa nayo............ " usinionee aibu
maana kila niongeacho hapa na maanisha " alisema Thabit na maisara akazidi
kusogea kando na kujituliza haswaa. " Maisara , natamani sasa kuusema ukweli
uliopo ndani ya moyo wangu kuanzia hivi sasa, sina mbio zaidi ya kutangaza
kilichousibu moyo wangu tangu siku ya kwanza nakuona wewe hapo. Nakumiss zaidi
unapokuwa mbali ama unapochelewa kujibu kila aina ya text nayo kutumia. Natamani
uelewe kila angle ya neno nalo tamka toka ndani ya kinywa changu. Elewa maneno
yangu ya thamani Maisara " Maisara alihisi aibu, hatimae wasaa aliokuwa
akiungoja kwa hamu ulimfikia.na alijikuta useless asie na kauli yoyote ile mbele
yake, ni kama aliambiwa tulia usitikise hata unyayo kusudi usikie maneno yake. "
mara zote napoteza control kila ninapokuona, au unapokuwa mbele yangu. Natamani
kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja huku nikijua sio sawa kwa sababu bado
haujawa kamili kama mpenzi au mwanamke wangu nae muwazia. Maisara naomba
uukabidhi moyo wako msafi na usio na hatia upande wangu mimi" " mimi mimi hapa
sii sijui mimi hapa naomba kwanza nikae " maisara alihisi kama miguu itamuuma
maana alihisi kutetemeka. Thabiti alimkamata kwa sababu alijua na kufahamu zaidi
maisara ana aibu sana. " maisara " alimuita akiwa kaushika mkono wake mzuri na
laini kusudi amzuie kupiga hatua, kwa ustawi na ustaarabu tayari Thabit
alijikuta kaangukia goti lake moja na kumuomba akubaliwe ombi lake. Maisara
alihisi aibu na kuangalia kila kona na pande za maeneo hayo ya bwawa la samaki
huenda labda angeona mtu. Hapana jamani haikufaa mtu yeyote yule kuwaona. "
Maisara, kama kukutongoza wewe hapo kunanipa faraja ya karne namna hii, nauona
moyo wangu ukipata mlipuko wa bomu kwa kuwa kando yako, najiuliza ni vipi
nitajiona mawinguni iwapo utakubali na kuwa tayari kuwa nami kando yangu, maisha
yetu yatakuwa ya furaha zaidi kwa kuwa na wewe tu , kubali kunifanya wa kwako
maisara, sio tu kwamba nakupenda uwe.mpenzi wangu bali nakupa ahadi ya kweli
kwamba utakuwa mke wangu, nitaishi nawe daima " Thabit alitulia kidogo kisha
akazungumza moja kwa moja. " Nakupenda Maisara " neno hilo moja la Nakupenda
kutoka kwa Thabit lilizunguka karibu mara nane ndani ya akili na kichwa cha
maisara. Maisara alizidisha aibu na kuomba apate nafasi kidogo atulie maana
alihisi kupagawa kwa maneno yake tu. " Thabit naomba kwenda washroom, tafadhali
" alimuaga Thabit hakuweza kupingana nae. Alielewa hali yake ya uwoga na mwisho
akamwambia. " sina haja ya kupata jibu lako leo, bali nakupa wakati wako ujipe
muda wa kutosha kunipenda na kuniamini " Maisara aliitikia hilo na kuondoka
haraka sana kuelekea washroom. Akiwa washroom alihisi faraja, yaani alikuwa
anatamani kupaa alijihisi kama angeweza angeachiwa dunia kwa muda tu ajipepee
kwa furaha aliyokuwa nayo. Alifumba macho kwa aibu the way alivyokuwa akihisi.
Kwani nini kilimkuta jamani loo! Yote hayo kwa sababu tu ya kutamkiwa maneno ya
kupendwa tu. Loo! Baada ya kujichangamsha huko washroom hatimae alipunguza aibu
kwa kila neno la ujasiri alilojipa kisha akatembea moja kwa moja mpaka
alipomuacha Thabit. Thabit alimshika mkono wake na kwa pamoja waliongozana mpaka
kwenye gari. Hawakuwa na haja ya kusubiri hapo kwani muda ulikuwa umeenda sana.
Kwenye gari maisara alikuwa kimya kwa aibu sana kiasi kwamba Thabit alihisi kuwa
bored. " niwashe mziki?" Thabit alimhoji maisara " ndio washa" maisara alikubali
kwa sauti ya pekee ambayo ilimfanya Thabit achanganyikiwe, kumbe kuna muda
alikuwa na sauti ya utulivu sana. Alitabasamu na kuwasha mziki ambao ulianza
kumpa hamasa ya kuusikiliza zaidi. Wakati huo gari ilikuwa imeenda sana kiasi
kwamba alikaribia hadi kufika hostel. ♧ Just a smile and rain is gone♧ ♧can
hardly believe it yeah ♧ ♧ There's an angel standing next to me ♧ ♧ Reaching for
my heart ❤ ♧ ♧ just a smile and there's a no way back♧ ♧ can hardly believe it,
yeah♧ ♧ But there's an angel calling me♧ ♧ Reaching for my heart ❤ ♧ ♧ i know
that I'll be okay now ♧ ♧ This time it's really ♧ ♧ I lay my love on you, it's
all i wanna do, every time i breathe, I feel brand new♧ ♧ you open up my heart ❤
♧ ♧ show me all you'll have♧ ♧ and walk right through ♧ ♧as i lay my love on
you♧ Hatimae kwa wakati huo ambao ndo gari iliwasili katika hostel maisara
alikuwa kazama katika hisia za wimbo mtamu ambao alihisi kabisa Thabit aliuweka
kwa ajiri yake ama kwa sababu yake mwenyewe. Alihisi faraja baada ya kufunguliwa
mlango na Thabit, akampa.nafasi ya kutembea huku wimbo ule ule ukiendelea. Wimbo
ulimaanisha. ♧ Tabasamu tu na mvua imeisha, ni ngumu sana kuamini, kweli,, kuna
malaika kasimama kando yangu, kuufikia moyo wangu,, Kwa tabasamu tu, sina njia
ya kurudi nyuma, ni ngumu kuamini, kweli, lakini kuna malaika ananiita,,
kuufikia moyo wangu♧ ♧lakini najua ntakuwa poa sasa, muda huu ni ya ukweli♧ ♧
nayaweka mapenzi yangu kwako, ndo nachopenda kufanya, muda wote naopumua,
najihisi kuwa mpya,, umeufungua moyo wangu, nionyeshe kila utakacho, na upite
ndani yake. Kama nilivyolaza mapenzi yangu kwako♧ Maisara alitabasamu baada ya
kuangaliana na Thabit kisha akakosa neno. " ufike salama sawa" Thabit
alimsemehsa. " mmhh! Sawa nawe ufike salama, uendeshe kwa makini barabarani "
maisara hatimae aliongea sauti ndefu baada ya dakika nyingi kukatika. Thabit
alitabasamu na kumkumbatia kiasi huyo msichana mrembo aliekuwa kasimama mbele
yake. " kwa heri, Nakupenda sana" alimwambia kisha akambusu kidogo kwenye paji
la uso wake. Maisara alitembea taratibu akiwaza kila kilichojiri siku hiyo,
aiii! Ilikuwa super alitamani muda urudi nyuma aambiwe maneno yale aliyoambiwa
na Thabit. Aliingia ndani baada ya kukuta tayari wambea wawili ambao ni Zawadi
na Sophie washamfungulia mlango huku wakisubiri kujua kilichojiri. Maisara
alipagawa kiasi cha kushindwa kuona uwepo wao. Unahisi nini kitafuata........??
Usikose kufatilia mkasa huu mtamuu... PATA OFAA YA LEO TUU....... Simulizi:
MAISARA ( USIKU WA HARUSI YANGU) Chombezotu.blogspot.com SEHEMU
YA.................. 05 Ilipoishia............... Aliingia ndani baada ya kukuta
tayari wambea wawili ambao ni Zawadi na Sophie washamfungulia mlango huku
wakisubiri kujua kilichojiri. Maisara alipagawa kiasi cha kushindwa kuona uwepo
wao. Songa nayo.................. " tuelezee basi nini kilijiri?" Zawadi
alishindwa kuvumilia ilibidi amshtue huyo mwanamke amsimulie kwa nini alikuwa na
furaha kubwa kiasi hicho. " jamani wewe Maisara tusimlie sisi" Walianza kurejea
maneno hayo mpaka Maisara akahisi kuwakatia tamaa kwa nini hawakumpa muda wa
kumuwaza Thabit wake. " twambie wenzio tuna arosto ya kujua kila kitu sema basi"
" eeehh! Nasema bhana nyie vipi?" Aliwapigia kelele wakawa kimya kisha akaongea
taratibu. " ki ufupi, ameniambia ukweli nilioufata siku ya leo, lakini mimi
nimeshindwa kumpa jibu nililoandaa kwa ajiri yake tangu mwanzo" " weeeehh!"
Zawadi alikaa karibu zaidi akihisi labda itakuwa ngumu sana kumsikia Maisara,
Maisara alianza kuhadithia kila kitu mpaka akarejeshwa hapo nyumbani, Zawadi
alijikuta kashika tama akimuonea raha rafiki yake jamani huyu msichana mrembo
kapata bahati kiasi gani? Alijawa hisia kiasi kwamba uso.wake uliwaka kwa hisia
na kuwa mwekundu kama nyanya. Hakuchelewa kumrukia na kumkumbatia. " nakuombea
awe mtu muelewa na mzuri zaidi milele jamani, I feel proud of youu sweetheart"
Sophie pia aliungana na kumbatio la wawili hao huku wakimuombea asiwe muoga
wakati mwingine aseme tu anampenda pia huyo mwamba. Maisara alikubaliana nao
wenzake. Siku hiyo ilipita na siku zikasonga huku Maisara akizidi kuwa karibu na
Thabit, hatimae Thabit alimaliza masomo yake kwani hakuwa akisoma tu bali
alikuwa akisoma kwa sababu zake mwenyewe binafsi, kama ni kuhitimu alihitimu
tayari hapo awali. Maisara alikuwa mwaka wa pili siku ambayo aliweza kumkubalia
Thabit na kuthibitisha moyo wake kumpenda moja kwa moja. Siku hiyo ilikuwa siku
ambayo wanafunzi waliomaliza pamoja na Thabit wakifanya mahafali ya graduation,
lakini kwake yeye Thabit hakuwa tayari kufanya mahafali, hivyo alichukua cheti
chake tu na kuondoka zake bila hata kupiga picha. " sasa kwa nini hajafanya
mahafali, nilitegemea atakuja na siku hii special kwake niifanye iwe special
zaidi lakini ameishia kuondoka bila hata kusema chochote " alilalamika Maisara
kwa sababu alimuandalia surprise pendwa Thabit na alipanga kuudhihirisha moyo
wake siku hiyo. " ni sawa kama mambo yameenda tofauti na ulivyopanga lakini sasa
nii unaweza kumpatia surprise hii kwa muda wa pekee yenu, kwa nini usimwambie
mkutane mahali ili umpe zawadi ulioandaa kwa juhudi kubwa" Zawadi alimwambia
Maisara akabaki hana usemi alinuna tu. Akiwa kavimbisha mashavu yake simu yake
iliita " My heartbeat" jina lilisomeka namna hiyo kwenye kioo cha simu yake. "
amepiga pokea" Sophie alimpa simu haraka.sana Maisara alipokea pia. " halo"
alianza kwa kuongea " samahani sweet, nimeondoka kimya bila kukutaarifu mpenzi
wangu" " sawa tu" " samahani, naomba nijipe muda kwanzia saa hii jioni mpaka
kesho asubuhi kwa ajili yako, iwapo kuna chochote ulitamani kuongea na mimi au
ulitaka nipatia ni muda wako sasa" " nilitaka kuongea na wewe zaidi, sina zawadi
zaidi ya maneno tu" maisara aliongea. " nayatamani hayo hayo ya thamani "
alisema Thabit na wakati huo huo maisara hakuchelewa kumpa maelekezo wapi
wakutane. Na ndo hiyo siku ambayo alifanikiwa kukiri maneno matatu muhimu ya
kiingereza mbele ya upeo wa uso wake. Alimpatia box dogo la zawadi kabla ya yote
kisha akamuomba afungue. Thabit alifungua na kukutana na karatasi nyeupe kabisa
isiyo na maneno yoyote yale. Aliutazama uso wa Maisara akatamani kuuliza mbona
karatasi tupu? " ondoa hiyo" maisara alimwambia kwa ishara na hapo Thabit
aliondoa na kukutana na karatasi nyekundu ikiwa imeandikwa kwa wino pendwa wa
rangi nyeupe. " I" ilisomeka herufi hiyo kwa wino uliokorea na kwa harufi kubwa.
Kisha alitoa karatasi hiyo na kukutana na karatsi nyeusi iliyokolezwa na maneno
meupe. " need your permission" alisoma karatasi hiyo pia kisha akatoa na
kuendelea kufunua karatasi zaidi karatasi iliyofata ilisomeka kwa maneno meupe
pia " to confess my feelings " hapo Thabit aliweza kuachia tabasamu lake baada
ya kuona ndani ya box hilo dogo hakuna tena karatasi zaidi. " I need your
permission, to confess my feelings" ( nahitaji ruhusa yako kukiri hisia zangu)
alisoma kwa pamoja Thabit. " ndio namaanisha Thabit " alizungumza Maisara kisha
akasogea karibu yake sana alimkumbatia Thabit bila aibu japo ndani kabisa ya
moyo wake alihisi kulia na kutamani kujificha. " Thabit " aliita jina lake kisha
akamwambia. " Muda umefanya nielewe, kukuchagua wewe ni chaguo bora zaidi la
maamuzi niliyowahi kuyafanya hapo awali katika maisha yangu. "Najua imekuwa
ngumu kuelewa moyo wangu unataka nini lakini umekuwa mwepesi zaidi kuzielewa
hisia zangu, ni ukweli uliowazi kwamba nakupenda zaidi wewe, ni ukweli sitaficha
tena hisia hizi zisizoeleweka Thabit, Nakupenda sana hivi sasa" Thabit alihisi
raha sana, ni vile tu Maisara hakuwa na ruhusa ya kuuvamia moyo.wa Thabit ili
ajue kuna kipi ndani yake kweli Thabit alihisi ushindi usiopingwa ndani yake,
hatimae sasa alikuwa na ruhusa ya kufanya maamuzi mengi juu yake japo hakuwa na
haki ya kumfanya mke wake. Lakini angalau alikuwa na nafasi ya kuibusu kwa muda
mrefu midomo yake mizuri sana. " ndio Thabit, Nakupenda na natamaninuwe wa
kwangu, sijui ni vipi uliweza kunipenda mimi lakini kujari na kusumbua kwako
hapo awali kulifanya nikupende zaidi" Thabit alimshika chini ya mashavu yake na
mikono yake miwili kisha akambusu midomk hake mitamu, Maisara alitulia japo
ilikuwa kwa kushtukiza lakini ilikuwa kana kwamba alijiandaa kwa hiyo busu. "
Nakupenda zaidi maisara " aliongea Thabit na kumfanya Maisara ajae raha na
gabasamu kwenye uso wake. Usiku huo walipata muda wa kuongea mambo mengi sana na
zaidi wakipanga mustakabali wao vipi uende. Thabit alimwambia kama ilivyo yeye
kampa jibu katika siku yake hiyo ya graduation basi na yeye pia atamshangaza
sana katika siku yake ya graduation, kitu pekee anachofaa kufanya ni kusoma kwa
bidii na kuhakikisha hafanyi makosa katika maisha haya ya chuoni, anafaa kusoma
kwa bidii ili kusudi hapo baadae aweze kutimiza ndoto zake alizomuahidi hapo
awali. " bila shaka nitafanya hivyo Thabit nitafanya kila kitu kwa ajiri ya
future yetu" alimpa ahadi ya kusoma kwa bidii na kutimiza kila kitu kwa bidii.
Na hapo ndo muda ambao Thabit alimwambia atamsapoti.kwa kila jema lake. Unahisi
nini kitafuata........?? Usikose kufatilia mkasa huu mtamuu...
Usiku wa harusi yangu
GREEN HACKER
0
Tags
Simulizi za sauti
Chapisha Maoni
TOA MAONI YAKO HAPA