17 - 20
NILIEMDHANIA KAHABA KUMBE NI BIKRA
.
SEHEMU YA KUMI NA
SABA
.
Kwa jinsi Roma alivyokuwa anaendesha gari , kila mtu alishangazwa na uwezo huo , Roma alikuwa akikwepa magari kama chizi kitendo ambacho wengi
walidhania ni kama Muvi , dakika chache mbele alikuwa akiingia Mbagala , Roma aliendesha ndani ya mtaa huu uliokuwa na baadhi ya viwanda na kampuni za usafirishaji , lakini ile
anakaribia nyumba anayoishi Najma , Alimuona Juma akiwa nje , alisimamisha Gari na kushuka haraka haraka.
“Niambie nini kimetokea?”Aliongea Roma huku akiona baadhi ya watu wakiwasogelea na walionekana kujua nini kimetokea.
“Kuna majambazi ambayo siyafahamu , yamekuja na kunitishia na bunduki na kisha wakamkamata Najma na kuondoka nae , huku wakiniachia maagizo kuwa nikitaka kumpata dada yangu akiwa mzima , niwasiliane na wewe na uende sehemu watakayo niambia”
“Sasa wamekuambia ni sehemu gani?”.
“Hawajaniambia wamesema watapiga simu ndani ya lisaa limoja”Aliongea Juma aliekuwa na wasiwasi huku wapangaji wakiwa wamewazunguka , kuna waliokuwa wakimwangalia Roma kwa wasiwasi ili kuona kama atakuwa na njia ya kumuokoa Najma , ila kuna wale waliokuwa wakishangaa mabadiliko ya Roma.
Baaada ya lisaa ni kweli simu ya Juma iliita na alipokea haraka haraka huku akiweka Loudspeaker na hata Roma kusikia.
“Dogo nadhani ushamwambia muhusika?” “Ndio yuko hapa”
“Mpatie simu”Ilisikika sauti na Roma aliinyakua kutoka kwenye mikono ya Juma na kuweka silence huku akiiingia kwenye Gari yake na kufunga mlango.
“Ongea”.
“Roma hakikisha unakuja mahali ambapo tunakuambia kwa sasa na uje peke yako , ukifanya ujinga wa aina yoyote kama kutaarifu polisi Najma atakufa kifo cha kikatili sana”Ilisikika sauti hio.
“Nipe simu kwanza niongee na Najma siwezi kuja kabla sijasikia sauti yake mimi sio mjinga kiasi hiko”Aliongea Roma na dakika chache sauti ilisikika kwenye masikio yake.
“Najma uko salama?”
“Roma usije watakuua , wana siraha usifanye wanach..”Alipokonywa simu.
“Sikia Roma eneo ni Vikindu , hakikisha unakuja peke yako”Ilisikika sauti na kumfanya Roma akasirike na hio ni baada ya simu ile kukatwa na Roma hakujiuliza sana alitoa gari eneo hilo kwa spidi kiasi cha kufanya watu watumbue macho.
Roma alikuwa na hasira mno , kwanza kilichomkasirisha ni kwamba watu hao wamemuambia kwenda Vikindu lakini hawakuwa wameeleza Vikindu sehemu gani.
Roma baada ya kuingia ndani ya barabara ya Kongowe , alizidi kuendesha gari hio kwa spidi na ilikuwa na spidi kweli kwani zilikuwa zile gari za gharama ya hali ya juu , alikuwa akiyapita magari kama mwehu kiasi kilichofanya kuwanyanyua polisi wa barabarani.
“Shi**t huyu mpuuzi ni nani huyu anaendesha gari kwa spidi hivi kama hii
nchi ya baba yake?”Alionekana mwanamke trafiki akiwa amekasirika mara baada ya kuisimamisha gari ya Roma lakini ilimpita bila ya kusimama na kumuachia upepo tu. “Huyu hanijui vizuri ngoja nitamkamata tu”Aliongea mwanadada huyu mrembo huku wenzake wakiwa ni wenye kushangazwa na spidi ya gari iliowapita ndani ya eneo hili la Kongowe.
“Mage unaenda wapi?”
“Namfukuzia yule mshenzi, wasiliana na Trafiki wa mbele yetu uwape taarifa juu ya hio gari waizuie “Aliongea mrembo huyu mwenye kalio kubwa huku akikimbilia Pikipiki yake kubwa ya kijapani Kawasaki Ninja H2/R hii ni moja ya pikipiku ya kifahari sana na ni chache sana Tanzania , inaupiga mwingi sana hii pikipiki kwenye spidi , ina Zaidi ya 322bhp na imeingia kwenye kumi bora ya pikipiki zenye spidi sana duniani , thamani yake sio chini ya milioni 100 za kitanzania. .
Haikueleweka ni kivipi mtembo huyu Trafiki anaimiliki vipi kwani ni ya bei kubwa mno. “Unafikiri ataifikia ile gari?”Aliuliza Trafiki wa kiume mweupe.
“Hio pikipiki ina upiga mwingi sana hio anaweza kuifikia ila inategemea na uwezo wake wa kuendesha”Aliongea
Trafiki maji ya kunde.
Ni dakika chache tu Roma alikuwa ashafika Vikindu na kusimamisha gari huku akijiuliza ni uelekeo gani aelekee, alikuwa akiangalia daladala zilizokuwa zikiingia ndani ya stendi , lakini ile anajiuliza simu yake ilianza kuita tena.
Simama kwenye bango
kubwa la Tigo hapo Stendi na kuna mtu atakufuata hapo”Roma aliangalia mahali sahihi pakuweka gari yake na kulisimamisha na kisha alishuka na kwenda kusimama chini ya Bango kubwa la Tigo.
“Hey! Brazaaa mambo ni vipi , kuna wana wameniambia nije nikuchukue nadhani wewe ndio Roma”Roma aliitikia kwa kichwa huku akimwangalia huyu kijana ambaye anaonekana kuharibiwa na madawa ya kulevya.
Baada ya dakika chache za kukata kona hatimae walivuka kiwanda kimoja amacho Roma hakukitambua kilikuwa cha nini , walipita upande wa kushoto na kusimama kwenye geti kubwa jeusi na mlango ukafunguliwa na Roma akaingia na hapa ndipo alipojua eneo hili ni la kuhifadhia nondo , kwani zilikuwa nyingi upande wa kulia , ni kama ghala.
Alitembea kwa kuongozwa na kijana huyo huku akiangalia baadhi ya mabaunsa waliokuwa wameshikilia bunduki za SMG wakilinda eneo hili kitendo ambacho kilimshangaza Roma , inakuwaje nhi yenye
Amani kama hii kuna watu wanamiliki Siraha kiholela ila hakutaka kujisumbua maaana sio kazi yake, aliingia ndani na hapa ndipo alipomshuhudia
Najma aliekuwa amefungwa kwenye nguzo, na kitambaa mdomoni , alionekana kuchoka kweli kweli alikuwa akitoa jasho kiasi kwamba baadhi ya Sehemu za Hijabu yake zimeloana.
Roma alimuonea huruma mrembo huyo kwa mateso aliokuwa akipitia , aligeuza macho na kuangalia
mabaunsa haya Zaidi ya matano yakiwa na bastora na kisha aligeuka upande mwingine akimuangalia jamaa ambae alionekana kuwa ndio bosi kwani yeye hakushika siraha yoyote na alikuwa amekaa kwenye kiti na sigara yake mkononi.
“Roma unaonekana sana kumjali huyu mrembo,
cheupe dawa mpaka
ukajileta mwenyewe”Aliongea
jamaa hili huku likionekana kutafuna bablishi. “Nishafika mfungulieni Najma aondoke , ili tuongee shida yenu na mimi”Aliongea Roma kwa hasira.
“Acha upuuzi wewe , yaani unaniona mimi joka la kibisa , nimlete mrembo kama huyu ndani ya hili eneo halafu nimuache bila hata ya
kumuonja”Aliongea
Jambazi huyu huku akimshia kidevu Najma na
kumuangalia kisha akaanza kumnusa usoni na shingoni.
“Kananukia vizuri na vijdomo vyake vidogo nadhani hata ka ‘K’ kake ni kadogo”Aliongea huyu jambazi mkuu na kumfanya Roma azidi kupandwa na hasira , ila hakutaka kufanya jambo lolote la kijinga kwani alihofia usalama wa Najma kwani watu hawa walikuwa wengi na wote walikuwa na siraha,Najma muda wote alikuwa mwenye kutokwa na machozi , alishindwa kuongea ila alionekana kumhurumia Roma kwani walikuwa wamemziba na matambala.
“Mfungeni kwanza , nataka nimfanye demu wake mbele yake”Aliamrisha na Roma alifungwa na yeye kwenye nguzo .
“Unajua kwanini nina shida na wewe fala?”.
“Wewe ndio umeniita hapa , naona unaanza kuuliza maswali ya kipuuzi”Aliongea Roma lakini alijikuta akianza kupigwa ngumi za Tumbo nyingi za haraka haraka na kisha akamaliziwa na Teke, kiasi cha kukohoa na kutema damu.
“Ulifanya kosa kubwa sana kulala na Rose,Mwanamke ambaye nimemhangaikia tokea anaingia ndani ya hili jiji , na wewe na hako kamashine kako ukajiona kidume, sasa leo nitahakikisha namto**mba huyu demu mbele yako , halafu nitahakikisha hautoki na hiko kibolo chako hapa ndani”Aliongea bwana huyu huku akionekana hakuwa ni mwenye utani kabisa.
“Hahaha .. sasa kama umemhangaikia ulishindwa nini kumpata , acha kuudhihirisha ubwege wako kwangu bwana , wewe ni fala tu”Aliongea Roma kwa hasira na kumfanya bwana huyo awaambie vijana wake wamsulubu Roma , kitendo ambacho kwa Najma kilimuumiza mno kwani ni kama alikuwa akipigwa yeye.
Roma alitema damu kwa mara nyingine na bwana huyu aliridhshwa na kipondo hiko na sasa kazi iliokuwa inafuata ni kukamilisha jambo lake kwa Najma.
“Ukimgusa huyo mwanamke nakuhakikisha nitakufanya kitu ambacho hutokisahau katika maisha yako”Aliongea Roma, kwani licha ya kupewa kichapo cha uhakika lakini alionekana kama hajapigwa vile.
“Ila lile jambazi kuu halikujali sana alimfungua Najma na kisha alimshika mkono kwa nguvu na akaanza kumvuta upande mwingine uliokuwa na maboksi.
“Kitendo kile kilimuuzi sana Roma kiasi kwamba mboni za macho yake zilianza kubadilika na kuwa za kijani na hata wale majambazi wengine walishuhudia hilo.
“Boss!”Aliita jambazi mmoja aliekuwa karibu na Roma , lakini kabla hajajibiwa alijikuta akiwa hewani na hakujua ni kwa namna gani , alipigwa na hapa Roma alikuwa amekata Kamba zote zilizokuwa zimemfunga . “Mpige Risasi mbona mnamuangalia”Aliongea yule Jambazi kuu , lakini katika hali ambayo hata yeye hakujua imetokea vipi , aliskia sauti ‘Shwaa..
Shwaaa tiii …Aiii, Shwaa… Aiii..’ na mabodigai wote walikuwa chini huku wakiugulia maumivu.
Jambazi kuu alishangazwa na uwezo huo wa Roma na kuanza kutetemeka kwa woga , lakini sio yeye hata Najma alishangaa .
Wakati Jambazi hili kuu likiwa linashangaa , lilijikuta limefikiwa na Roma na kishikwa shingoni na kuning`inizwa hewani kwa mkono mmoja kitendo ambacho Najma ni kama alikuwa akiangalia Muvi za kihindi zile zenye uongo mwingi , yaani unakuta steringi kabeba gari na mkono mmoja. “Sipendagi kutishiwa kwenye maisha yangu , pili Onyo mara moja ukirudia ni kifo, tatu sipendi watu wanaotumia watu wangu wa karibu kupambana na mimi Sababu hizo tatu zinanipa uhalali wa kukuondoa duniani maana wewe ni takataka”Ilikuwa sauti nzito kama ya Roboti. “Najma Fumba macho mpaka nikwambie fumbua ”Aliongea Roma kwa sauti nzito na Najma alifumba kweli na ndani ya dakika mbili alimwambia fumbua na hapo ndipo Najma alipopigwa na mshangao , kwani majambazi yote manne yalikuwa yamelala chini huku yakiwa yamefunikwa na maboksi kwenye uso huku Roma akilipapasa lile jambazi kuu , lakini hakuambulia cha maana Zaidi ya pakiti ya sigara za SM na kuzichukua na kuweka mfukoni.
“Hawa wote ni maiti , ndugu zao watakuja kuchukua miili na sijui kama wanasafirisha au wanazika hapa hapa”Aliongea Roma bila wasiwasi na kumsogelea Najma ili amshike mkono , lakini Najma alirudi nyuma kwani alikuwa ni mwenye kutetemeka mno na alimuogopa Roma , hakumuona kama yule
Roma aliekuwa akimjua na kumpenda ila huyu ni
Roma mwinginekabisa mkatili na muuaji.
“Nifuate nyuma kama unaiogopa”Aliongea Roma na kuanza kupiga hatua na
Najma japo alikuwa akimuogopa Roma ila alimkimbilia kwani aliogopa kukaa na maiti na isitoshe ilikuwa ni usiku.
Roma baada ya kukatiza kona ya chumba hiki alimwambia Asubiri kwa dakika chache lakini
Najma hakusubiri , aitoka na kuangalia nje na hapo ndipo aliposhuhudia kwani alimuona Roma akitembea kama upepo flani hivi ulioambatana na kivuli cha mtu , na alichoweza kusikia ni ‘Crak shwaa..Aiii, Crak .. Shwaa ..Aii Crak.. Aiii Crak Crack;’.
Majambazi yote yalikuwa chini Roma akiwa ashayavunja shingo , yaani ni kitendo cha dakika moja tu , Roma ashamaliza kazi na aligeuka nyuma na kumuona Najma na kumuita kwa ishara ila Najma alizidi kumuogopa Roma.
“Najma nisamehe sana kwa kufanya mambo haya mbele yako , ila sikuwa na jinsi , sahau kabisa kilichotokea leo na nitahakikisha hakuna mtu anaekugusa tena”Aliongea Roma ila Najma hakujibu kitu aliishia kutoa machozi tu na kutangulia mbele.
Roma na yeye hakutaka kumuongelesha , alijuwa mwanake huyo atakuwa kwenye mshituko mkubwa sana , hivyo aliona muda pekee ndio utakao weza kumuweka sawa.
Baada ya kutembea kwa dakika kadhaa hatimae , walifika barabarani, alimuona kijana ambaye alikuja kumchukua akiendelea na upiga debe na Roma hakumjali sana , lakini ile anakaribia gari lake , aliona matrafiki wawili watatu wameegamia gari yake wawili wakiwa wanawake na mwingine akiwa ni mwanaume.
Na wakati huu macho yake yalikuwa yasharudi kwenye hali yake ya kawaida , na alikuwa Roma ambaye Najma alikuwa amemzoea , sio yule muaaji wa kutisha.
“Jamani habari zenu “Alisalimia Roma kama kawaida yake huku akitabasamu na Mage polisi aliekuwa akimfukuzia , aligeuza macho yake na kumwangalia Roma juu hadi chini, kwa muonekano wa Roma hakuonesha kuweza kumiliki ndinga kama hio na ndio maana baada ya kumuangalia kwa sekunde aligeuka na kuendelea kupiga stori na trafiki mwenzake wa kike huku akimuacha trafiki wa kiume akidili na Roma.
“Jamani mmesimama kwenye gari yangu nataka nikampumzishe huyu mrembo si , mnaona jinsi alivyochoka na pia giza kali hili”Hapo ndipo Mage aligeuka tena na kumwangalia Roma.
“Wewe ndio mwenye hii gari?”
“Ndio mrembo”
“Uko chini ya ulinzi kwanzia sasa , kwa kukiuka sheria za barabarani lakini pia kwa kuidharau serikali”.Aliongea Mage huku akiweka uso wa usiriasi.
“Mrembo nilikuwa na dharula ndio maana”
“Mpuuzi sana wewe , hata kama unadharula gani hii nchi sio ya baba yako kuendesha gari kama kichaa , unataka kusababisha ajali na usiku huu na mipombe yako”Aliongea Mage kwa hasira.
Roma aliona hana cha kujitetea , alimwangalia Najma alivyokuwa amechoka na kumuonea huruma.
“Utaenda na sisi mpaka polisi , usituletee shida kisa unaendesha gari la kuazima, Edwin endesha gari yake mpaka kituoni”Aliongea Mage na kumuamrisha trafiki wa kiume achukue funguo kwa Roma.Trafiki yule
alitabasamu meno yote nje
.
“Leo naenda kuonja kuendesha huu mchuma , Mungu anipe nini mimi nikimfikisha kituoni hata nikifa nitakuwa na Amani”Alijiwazia huyu trafiki kichwani mwake baada ya kupokea ufunguo Najma , Roma waliingia kwenye gari na safari ya kuelekea kituoni ikaanza
SEHEMU YA KUMI NA
NANE
Unaambiwa hakuna Trafiki aliekuwa akiwasumbua watu waliokuwa wakipita barabara ya Kongowe kama Mage, huyu Trafiki waendesha daladala na boda boda walikuwa wamembadilisha jina na kumuita ‘Mnaaa’, Mage alikuwa mzuri mno lakini hakuwa akifanania na usiriasi wake akiwa eneo lake la kazi , aliwanyoosha watu kisawasawa.
Mage anamiezi miwili tu tokea aanze kufanya kazi hii ya utrafiki na kilichomfanya kuwa trafiki ni adhabu aliokuwa amepewa , kwani Mage alikuwa ni Koplo polisi ndani ya kituo cha Osterbay jijini Dar es salaam , lakini kutokana na kumpiga mtuhumiwa mpaka kuzimia wakati akifanya nae mahojiano ndio kilichomfanya kupewa adhabu ya kufanya kazi kama Trafiki na kutolewa katika cheo chake.
Mwanzoni mkuu wa polisi alitaka amfukuze Mage lakini alishindwa kutokana na nguvu iliokuwa nyuma ya mrembo huyu , kwani inasemekana baba yake ni mtu mkubwa sana ndani ya ulingo wa siasa. “Jina nani?” “Roma Ramoni”
“Umri?”
“Miaka 24”
“Kabila”
“Mhehe”
“Uraia wako” Roma kimya
.
“Jinsia yako?”
“Mwanamke”Jamaa yule wa kipolisi alimwangalia Roma kwa hasira na kisha kuendelea kuandika na baada ya dakika chache aliingia kwenye kijiofisi hiki afande mwingine.
“ Afande Dulla ,Mage amesema atadili mwenyewe na mtuhumiwa”Jamaa alionekana kukasirishwa sana jambo hili , kwani kwanza baada ya afande Dulla kuona gari kali ya Roma V8 aliamini huo ni mchongo Mungu amempatia usiku huo na aliona akiacha mchongo huo upite atakuwa fala.
“Huyu Mage ni mnoko sana tokea apangwe ukanda huu hakuna Amani na michongo imepungua”Aliongea Afande Dulla huku akitoka kwa hasira nje,hakuwa na cha kumfanya Mage kwani alikuwa akizijua tetesi kwamba Mage sio mtu wa kuwa nae adui.
Najma alikuwa asharudi nyumbani kwani hakuwa akihusika baada ya kutoa maelezo yake , aliekuwa amebaki kituoni alikuwa ni Roma , lakini jambo ambalo lililomkasirisha Roma ni kwamba Mage alichelewa sana , yaani alifika kituoni baada ya saa moja na Nusu.
“Kwanza huna leseni , pili nilivyokusimamisha ukajifanya mjuaji na kunipita , tatu spidi ya gari yako kwenye barabara hii yenye magari mengi ni kinyume na sheria , mpaka hapo una makossa matatu”Aliongea Mage , lakini wakati huu Roma alikuwa anamwangalia tu mrembo huyu huku akitafakari inakuwaje pisi kama hii ni Trafiki.
“Inakuwaje mrembo kama wewe ukawa polisi ,halafu unaonekana umeanza mzunguko wako wa mwezi jana”.Mage alizidi kukasirika.
“Huyu fala kajuaje nipo kwenye Period na nimeanza jana?” “Wewe Nguruwe unadhani upo mtaani hapa, au kwasababu unaendesha V8 unataka kujiona upo kwenu hapa?”
“Hehe…Inaonekana nimepatia”Aliongea Roma na ilikuwa kitendo cha dakika tu alisikilizia maumivu kwenye mguu wake maana Mage alirusha buti yake yenye kisigino kirefu na kutua kwenye mguu wa Roma kiasi cha kumfanya Roma ainame huku akisikilizia maumivu.
Baada ya kupishana kwa muda hatimae Mage alimpa adhabu ya Roma
kulipa faini milioni moja kwa makossa yake yote matatu.
*****
Ni usiku muda wa saa saba Edna hakuwa amelala, haikueleweka kwanini alikuwa hajalala , ila alionekana ameshikilia kitabu cha kingereza kilichokuwa na Title ‘HOW TO THINK POSITIVE akiwa anasoma , ni dakika chache pekee alizosoma alisikia simu yake ikiianza kuita mfululizo kiasi cha kuichukua haraka haraka ila alipoangalia jina ni ‘Mbakaji’Alikuta akiendelea kuangalia ikiendelea kuita. Ilikatika na ikaita mara ya pili na hapa hakuwa na jinsi na kuipokea kisha akaweka sikioni.
“Unataka nini?”
“Bebi ,Usiniambie ulikuwa umelala mumeo sijarudi” “Sema shida yako nina usingizi mimi?”.
“Kuna polisi mrembo hapa anataka kuongea na wewe”Aliongea Roma . “Hellow! habari za Kiza kinene, nadhani huyu mlevi ni mumeo , basi hapa ni kituo cha polisi Chalambe tunamshikiria mumeo kwa kukiuka
sheria za barabarani na kuidharau Mamlaka na atatoka iwapo atalipa kiasi cha milioni moja za kitanzania kama faini”.
“Sawa”Aliongea Edna na kukata simu.
Baada ya kukata simu ile alionekna ni mwenye kukasirishwa na jambo hilo , ila alifikiria kwa dakika na kuona ni jukumu lake kutatua matatizo ya ndoa , kwani licha ya wawili hao kutokuoana kwa mapenzi , ila walikuwa ni wanandoa kihalali na walikuwa na wajibu wa kusaidiana.
Edna alitafuta jina kwenye simu na kisha alipiga , japo muda ulikuwa umeenda sana , lakini simu hio iliopokelewa.
“Nataka aachiwe kwa sasa nadhani unakumbuka nilikusaidia kupandishwa cheo , sasa hivi ni usiku sana sitaki aendelee kuwa kituoni”Sentensi ya mwisho Edna alioongea na kisha akakata simu.
Upande wa huku Mbagala chalambe ,Mage alionekana kuwa ndani ya maliwato huku akiwa ameshusha jezi yake ya kitrafiki huku mkononi akiwa ameshikilia pedi , Alitoa ile aliokuwa amejifunga na kisha akachukua ile nyingine mpya na kuiweka vizuri na kisha akajivalisha vyema nguo yake ya ndani na kupandisha jezi yake hio nyeupe na akanawa mikono na kutupia ile pedi iliotumika kwenye dustibin.
“Hivi huyu choko kajuaje mimi niko kwenye
period”Alijiongelesha huku akijigeuza geuza kwenye kioo kuangalia kama ana alama yoyote ya damu inayomuonesha yuko kwenye Period, alijikagua kwenye mpododo wake ambao ni ugonjwa wa wanaume wengi lakini hakuona kitu. “Au hapa mbele pametuna sana ,Mh! Lakini panaonekana kawaida”Baada ya kumaliza alichukua mkoba wake na kutoka kwenye maliwato.
“Mage kuna simu yako kutoka kwa mkuu”Aliongea Edwin na Mage alipokea .
“Mkuu haiwezekani huyu ni muhalifu na sheria inapaswa kuchukua mkondo wake , kwanini tumuachie”
“Mage nakuambia muachie sasa hivi , huyo mtu uliemshikiria ana koneksheni na wenye nchi, sitaki kuhatarisha kibarua changu ninasomesha bado , muachie haraka , halafu acha ubishi mkuu wako wa kazi akikuambia achia , wewe achia ,nikikuambia jamba jikakamue jamba hio ndio maana ya mwanajeshi kutii amri Ala”Huku simu ikikatwa na Mage alitoa sonyo.
“Edwin mrudishie yule choko vitu vyake aondoke”Edwin alishangaa ila hakuwa na cha kuongea Zaidi ya kufanya hivyo.
“Hey!Mrembo usicheze na wenye nchi”Aliongea Roma ilimradi tu kumkasirisha Mage aliesimama karibu na barabara.
“Siku nyingine nikikukamata nakuapia lazima uozee jela”.
“Hehehe..Sawa bibie , ila naona ushabadilisha”
“Nishabadilisha nini?”Aliongea Mage kwa mshangao na Roma hakujibu aliingia kwenye gari lake na kuondoka kwa spidi huku Edwin akiliangalia gari kwa matamanio .
“Huyu choko ukute mchawi huyu kajuaje nimebadilisha pedi huyu”Alijiwazia Mage huku akijionea aibu , alikiri katika maisha yake ya kibabe kama mwanamke ashawahi kukutana na watu wengi ila hakuwahi kuyumbishwa kama alivyoyumbishwa usiku huo,alikasirika maradufu na alijiapiza siku atakayo mkamata Roma hata kama ana koneksheni atamtia kwanza ukilema na mengine yataendelea.
.
Ilikuwa ni asubuhi saa kumi na moja Roma alikuwa akikata kiuno huku mwanadada Rose
akitoa miguno ya kimahaba ya kila aina ,
mwanadada huyu mrembo alikuwa mwekundu kama nyanya , kwani alikuwa anakunjwa , aligeuzwa geuzwa kama andazi linalokaangwa huku likirukaruka , alikuwa akibonyezwa bonyezwa kama embe huku ametoa ulimi kama anakata moto ni Zaidi ya dakika sabini zimepita Roma hajafunga goli hata moja huku yeye akipoteza hesabu ya idadi ya magoli aliokuwa ametupia.
.
“Roma tupumzike kwanza , kuna waka moto”.
“Tulia bebi namalizia chenga ya mwisho nitupie wavuni kama
Mayele”Aliongea Roma na ndani ya dakika kumi alikuwa ametupia wavuni na kujitupa pembeni ya Rose.
“Bebi sidhani kama kuna mwanaume anajua kuto**mba kama wewe?”. “Rose mpenzi usiniambie unawaza kufanya utafiti na ushapata idea”.
“Hahah.. yaani wewe , mimi nimeongea tu”Roma alitabasamu huku akimfinya Rose mashavu na muda huu wote wakiwa uchi.
“Halafu bebi ulitokea wapi jana , mbona ilikuwa usiku sana”.
“Halafu umenikumbusha , hebu kalete kwanza kiberiti nina sigara zangu kwenye suruali”Aliongea Roma na Rose alinyanyuka bila ya nguo na kwenda kuchukua
kiberiti , alikuja nacho na kisha alipekua mfuko wa suruali ya Roma na kisha alitoa pakiti ya sigara na kuchomoa moja na kisha akampatia na kisha akawasha moto na kuunguza sigara ile na akaweka kiberiti pembeni na kurudi kwenye kitanda hiki kikubwa , huku Rose akiwa ameshikilia sahani flani ya udongo ,Roma alikuwa akivuta kidogo anaweka majivu kwenye ile sahani.
.
Ungemuona kitendo anachofanya Rose ungedhania ni wanawake wanaotumika kuwafurahisha wafalme kwenye majumba yao(maids) , hakuwa yule Rose ambae anaongoza kundi la Tembo na kuogopwa na walio chini yake.
.
“Kuna mpuuzi jana amemteka Najma , na kunitishia Amani huku akijinadi kwamba wewe ni wake na mimi nilikosea sana kulala na wewe”Rose alishangaa lakini pia aliwaza ni mtu gani mwenye uwezo wa kufanya jambo hilo na hapo hapo jibu alilipata.
“Unataka kuniambia Karimu ndio aliefanya hivyo?”
“Sitaki hata kumjua jina ni mpuuzi mmoja hivi mwenye nywele za kisomali”Huku akitoa moshi wa sigara na kufanya chumba kijae harufu ila Rose hakujali. “Ni karimu bebi huyo , unakumbuka ile siku zile bia za ofa kwenye bethidei yangu , basi yeye ndioe alielipia gharama zote”Roma alielewa.
“Kwa hio ilikuwaje mpenzi?”
“Jibu unalo Rose”Alitoa macho. “Unamaanisha..” “Ndio nimemuua na vifaranga vyake vyote nadhani ndugu zake watakuwa wanaomboleza kwasasa kama wamepata taarifa”.
“Ila mpenzi ikijulikana wewe ndio umemuua
.
inaweza ikakuletea shida , baba yake Karim ni meya , lakini pia ni mmiliki wa kundi la Black Mamba ni kundi kubwa sana kuliko la kwangu na linajihusisha na mambo mengi , kama kuuza viungo vya binadamu nje ya nchi , usafirishaji wa meno ya Tembo , Madawa na mengine mengi ambayo si halali katika ulimwengu unaonekana, na huyo Karimu ndio mkuu wa kundi hilo ila maagizo yote anapokea kwa baba yake , lakini pia inasemekana, baba yake Larim na The Doni wanaukaribu ambao unahisiwa kuwa ni undugu”Aliongea Rose kwa kirefu na kumshangaza Roma.
.
“The Doni?” Alishangaa
Roma
.
SEHEMU YA KUMI NA
TISA.
.
Tembo ni kikundi ambacho kilikuwa kikijihusisha na mambo mengi ndani ya ulimwengu usioonekana,moja ya kazi kubwa ilikuwa ni
Smuggling(kuingiza bidhaa mbalimbali kimagendo),Kuuza ngada,na kusafirisha meno ya tembo lakini pia kundi hili kama yalivyokuwa makundi mengine , lilikuwa likitumiwa na viongozi wa juu wa kisiasa na wafanya biashara katika kazi haramu , kama kuua , kuteka na mengineo yanayofanana na hayo.
Katika ulimwengu usioonekana mambo ambayo mengi si ya
kihalali kwa kipimio cha haki na sheria katika ulimwengu unaonekana mambo hayo yote ni halali.
Katika ulimwengu usionekana kanuni kubwa ni ‘survive for fittest’yaani ndani ya ulimwengu huo unaishi kutokana na uwezo na nguvu zako za kumtawala mwingine , sasa basi baina ya hizi pande zote mbili , mara nyingi zinaenda
.
sambamba , unaweza usielewe ila viongozi wakubwa duniani pamoja na wafanya biashara wanaelewa sana umuhimu wa huu ulimwengu usionekana.
.
Hivyo wafanyabiashara na wanasiasa siku zote wanahakikisha kuna uwiano sahihi kati ya hizi pande zote mbili, sasa kwa hapa bongo pia kuna sehemu ya ulimwengu huu usioonekana na raia wake tunaishi nao.
.
Ushawahi kukutana na mtu hana kazi maalumu mjini , ila yeye anavaa anakula na kutanua maisha kuliko wewe ambaye unahangaika kila siku , basi jua huyo mtu huenda anacheo kikubwa katika ulimwengu huo usionekana , unaweza kuupa majina utakayo , unaweza kuita ulimwengu wa kiza , ila wazungu wanapenda kuita ‘Underworld’ yaani the world of
.
criminals(ulimwengu wa wahalifu) sasa usishangae sana ukaona mwanasiasa anatoka hadharani na anakemea matendo mabaya yanayofanyika ndani ya ulimwengu wa kiza lakini yeye akawa ni moja ya wahusika wa wahalifu hao, hii ndio sababu inayofanya ulimwengu huu kuja kudumu milele na inaweza ikafikia siku ule uwiano ukavunjika na ulimwengu huu ukawa na nguvu na hapa ndipo utaona mambo mengi ya kihalifu yakifanyika katika dunia,wewe ishi ila kuna mambo mengi yanafanyika eneo unaloishi na ni ya kutisha na usifahamu, na hautofahamu kwakuwa wewe upo kwenye unaishi kwa kutazama uhalisia unaonekana lakini yapo mengi yanayofanyika nyuma ya huo uhalisia. Unaouona.
Sasa kundi la Tembo , Black Mamba ndio makundi makubwa yaliokuwa yakifanya kazi ndani ya jiji hili la Dar Es Salaam , yapo makundi mengi ila hayo ndio yenye nguvu huku mmiliki wa kundi la Tembo akiwa ni Rose na mmiliki wa Black
Mamba akiwa ni Marehemu Karimu.
“Huyu The Don ni nani haswa Rose?”Aliuliza
Roma
“Hata mimi si mtambui , ila ndio mwenye nguvu kubwa sana hapa nchini , hafamiki kwa jina ila inasemakana ni mwanasiasa mkubwa na mfanyabiashara na mimi kabla ya kuweka makazi yangu hapa Dar nilipitia hatua za kuomba ruhusa kwa The Don”Aliongea
Rose.
“Hebu niambie kwanza uliwezaje kuweka kundi lako hapa Dar?”
“Ni stori ndefu Roma ila ukweli ni kwamba ,damu nyingi zilimwagika mpaka kupata koloni hili na baadae kuingia mkataba na Black Mamba”aliongea Rose na Roma alielewa anachomaanisha na hakutaka maelezo mengi kwani muda umeenda , Rose alienda kuandaa chai na Roma alijiandaa vizuri na kunywa chai , na baada ya k ushiba , alitoka na kuingia kwenye gari yake. “Hapa niende moja kwa moja kazini”Aliwaza Roma wakati akipita maeneo ya Rangi tatu sokoni.
*****
Juma alishangaa sana kumuona Najma baada ya kumfungulia Geti , bwana huyu alionekana kuwa na wasiwasi sana wakati wote ambao Najma alikuwa ameshikiliwa. “Najma uko salama?”Aliuliza Juma , lakini Najma hakuongea kitu Zaidi ya kupita na kuingia chumbani kwake na kujirusha kitandanni huku akianza kulia kwa kwikwi , akiwa amejikunyata.
Jjuma yeye hakuweza kuingia kwenye chumba cha dada yake hivyo aliona jambo pekee ni kutulia , lakini kwa hali aliomuona nayo Najma aliamini kabisa kuna jambo ambalo limemkuta Roma.
“kwa hali aliokuwa nayo Najma lazima Roma hatupo nae tena Duniani na mpango wangu utakuwa umeenda kama nilivyokuwa nimepanga”Aliwaza Juma huku akionekana kutabasamu na kujiona mshindi.
“Ila yale maneno ya
Mganga yatakuwa ya
uongo yale”Alifikiia Juma maneno alioambiwa siku kadhaa zilizopita na mganga huko Chanika.
Ilikuwa hivi baada ya siku ile Roma kuondoka , swala lile lilimuuma sana Juma , yaani sio kidogo na kilichomuuma yeye lilikuwa ni swala la mafanikio ya Roma , katika maisha yake ashajiwekea kuwa Roma siku zote atakuwa masikini na yeye atakuwa tajiri , lakini mabadiliko yaliotokea ghafla yalimsononesha mno na alikuwa hana Amani hata kidogo katika moyo wake na ndio maana baada ya siku mili zilivyopita alienda kwa mganga chanika.
Mganga Maluweluwe alikuwa akisifika sana upande huu wa Chanika kwa tiba zake zake za kuaminika , watu wengi walienda kwake kwa ajili ya kutatua matatizo yao , sio viongozi wa kisiasa sio wafanya biashara walikuwa wakienda kwa Maluweluwe kwa ajili ya kutatua shida zao.
Sasa na Juma aliaminni swala lake linaweza kutatuliwa na mganga huyu na ndio maana alifunga safari kutoka Rangi tatu na kwenda kwa Maluweluwe . Ilikuwa asubuhi Juma alifika mtaa huu wa
Maluweluwe na kwenda moja kwa moja kwa mganga , Mganga huyu alikuwa yuko vyema sana kiuchumi, kwani katika eneo hilo nyumba yake ndio ilikuwa kubwa tena ya Ghorofa mbili kwenda juu huku ikiwa imezungushiwa ukuta mkubwa, na
mafanikio ya Maluweluwe ni kutokana na tiba yake hio ya kienyeji ambayo alikuwa akiwafanyia watu.
Juma alikaribishwa pale na wasaidizi wa Maluweluwe , huku akishangaa baadhi ya magari yaliokuwa hapo ndani ya watu waliokuja kufata Tiba , hali hio ilimfanya Juma moyo wake unyong`onyee na kujiona ni mwanaume mwenye
laana , kwani ukilinganisha na watu waliokuwa wapo hapo ndani na yeye , alijiona yeye pekee ndie ambae alikuwa masikini, sasa cha kushangaza Zaidi ni kwamba alikuwa hapo ndani kwa ajili ya kumroga mwenzake ili afanane nae.
Baada ya foleni hii kuisha hatimae Juma ilikuwa zamu yake , Maluweluwe alikuwa Profesheno
kwenye kazi yake , kwani alikuwa na mhasibu kabisa na ukishalipia kwa mhasibu unaingia kwenye chumba ambacho juu kabisa kuna kibao kimeandikwa ‘Chumba cha
Daktari’.
Ukweli licha ya Juma kumsikia sana sifa za Maluweluwe hakuwahi kumuona , lakini leo hii ndio amemuona na katika akili yake alikuwa akidhania kuwa anaenda kukutana na mzee mwenye mvi , ila Maluweluwe alikuwa kijana ambae kwa haraka haraka
ungemkadiria umri wake kuwa miaka therethini kwenda juu.
“Karibu kijana”Aliongea mganga huyu ambae hakuwa na utofauti sana kimuonekano wa kimavazi na mitindo kama wale waganga unaowaona kwenye Bongo muvi , au kama wewe ushawahi kwenda kwa mganga basi utakuwa unajua muonekano wa Maluweluwe.
Basi kama kawaida ya waganga alianza mbwembwe za hapa na pale , na kupandisha mashetai ya kimchongo na kisha alimruhusu Juma kueleza shida yake kwa kina.
“Kuna rafiki yangu juzi juzi hapa kapata mke tajiri , jambo ambalo halijanifurahisha , kwani maisha yake yamebadilika sana, hivyo nimekuja umfanyizie aachwe na azidi kuwa masikini”.Mganga huyu alimwangalia Juma na ujasiri wake na kisha alianza kupandisha mashetani.
“Leta jinaaaa… Leta jinaaaa”Aliongea mganga huyu kwa sauti nzito na kumfanya Juma moyo wake utabasamu kuona yes hapa kafika mahali penyewe maana sio kwa mashetani hayo.
“Anaitwa Roma,, yes Roma Ramoni anaitwa”.Mganga baada
ya kufanya mbwembwe zake pale aliita jini lake la utambuzi ili kumpa taarifa zinazomuhsu Roma na ndani ya dakika chache mganga huyu alionekana kutoa jasho.
“Kijana mtu unaetaka kumroga hashikiki ,,,, nasema haogekii , harogekii”
“Unamaanisha nini Maluweluwe?” “Majini yamekataa kujihusisha na mtu huyo unaweza kuondoka” “Maluweluwe nishalipia hela yangu , nataka tiba”Juma alijifanya haelewe na kumkazia mganga.
.
“Tiba sahihi kijana ni kukaa mbali na Roma , ni Zaidi ya mchawi na simuwezi na majini yamekataa kutoa tiba” HIvyo ndivyo ilivyokuwa huko kwa mganga na maneno hayo yalikuwa yakimfikirisha Juma kwa siku nzima mpaka pale alipokuja kupata jambo jipya.
.
Juma siku ya pili yake akiwa kazini baada ya kutoka kwa mganga , alifuatwa na bwana mmoja hivi mwenye kijitambi cha pesa, na ni baada ya bwana huyu kuulizia ulizia ndani ya soko hili la Mbagala na ndipo
alipokuja kumpata Juma aliekuwa bize kuhamisha magunia ya yeboyebo kwenda kuyahifadhi na muda huo ulikuwa jioni saa moja.
“Sikia nitakulipa mara mbili ya hela unayopata kwa kusukuma hayo magunia”Aliongea bwana huyu ili aweze kupata nafasi ya kuongea na Juma , na kutokana na ofa hio Juma hakukataa na kukubali na kuingia kwenye Gari ya Verosa nyeusi na bwana huyu mwenye kitambi na gari hii ilikuja kusimamishwa mtaa wa Zakiem kwenye mgahawa mmoja hivi pembeni ya barabara inayoenda Kijichi.
“Naitwa Ahmedi ni Meneja mauzo kampuni ya Tigo mkoa huu na nimekuomba kuongea na wewe juu ya mdogo wako Najma”Juma
alishangaa ila alitaka bwana huyo aendelee kuongea.
“Sikia Juma nimetokea kumpenda sana Najma na nipo tayari hata kumuoa , lakini dada yako nimejaribu kila mbinu kumpata ila amekuwa mgumu na hio ndio sababu inayonifanya tuwe na haya maongezi , nataka unisaidie kumpata Najma maana kaniambia ana mtu anampenda , lakini anaonekana kunidanganya”.Juma kwanza alishangaaa , lakini alitabasamu moyoni kwa wakati mmoja, kwa bwana kama huyu mwenye pesa zake kumpenda dada yake , Juma mtu aliekuwa mbele yake sio mtu pekee anaempenda dada yake ila aliona fursa Adhimu sana.
.
“Bro nimekuelewa sana , pia nimefurahishwa na nia yako ya kutaka kumuoa
Najma”Jamaa alitabasamu.
“Sasa unanisaidiaje kumpata Najma au ni kweli ana mtu kama alivyosema?”
“Ndio kuna jamaa mmoja hivi anampenda , ila mimi naamini sio upendo ila ni ujinga wa dada yangu tu kwani hajawahi kuingia kwenye mapenzi”Jamaa alitoa tabasamu la ushindi. “Huyo mtu ni nani na anafanya kazi gani?”
“Huyo jamaa, alikuwa ni mbeba mizigo kama mimi anaitwa Roma , lakini kwa sasa ameoa na haishi maeneo haya..Broo tusiongee mengi mimi nimekukubali bro na
Najma ni wako”Aliongea Abuu , lakini wakati wanaendelea kupiga Stori mara aliingia jamaa flani ambae alikuwa na nywele za kisomali hakuwa mweusi na pia hakuwa mweupe sana.
“Karim umejuaje niko hapa?”Aliongea bwana huyu Ahmed akimchangamkia Karim na walionekana walikuwa wakifahamiana.
“Kuna mtu nia miadi nae maeneo haya , ila naona tumekutana”Aliongea huku Juma akimwangalia Karim maana alikuwa akimjua vyema na hakuna ambae hakuwa akimjua Karim ndani ya meneo hayo ya mbagala maana alikuwa akimiliki biashara nyingi.
“Huyu ni kaka yake Najma”Aliongea Ahmedi na Karimu alimwangalia Juma na kisha akatingisha kichwa na wakati huo huo alifika bwana mmoja hivi alievalia kibishoo na kusogea meza waliokuwa wamekaa Juma .
“Vipi Zonga ni taarifa gani unayo , ambayo umesema ni muhimu”Aliongea Karim mara baada ya Zonga kufika .
“Bro huyo jamaa ndio anatoka na Rose”Aliongea Zonga huku akimkabidhi
Karim picha , ambayo Juma baada ya kuiona tu aliitambua maana alikuwa amekaa karibu na Karim. “Huyu Fala anaitwa nani na anakazi gani hapa mjini?”.
.
“Hana mishe yoyote ya kueleweka ila kwasasa anamke”Aliongea Zonga.
Ahmedi na Juma waliendelea na mazungumzo yao huku wakiacha kumfatilia Karim, lakini wakati wakiendelea kuongea simu ya Ahmedi iliita na baada ya kuona jina la mpigaji alijikuta akikunja sura yake na kunyanyuka na kutoa waleti yake na kumpa Juma nyekundu tatu huku akimpa simu ndogo aandike namba zake za simu.
“Sasa sikia Juma tutawasiliana , Karim ninadharula ngoja kuna mishe niwahi nitakutafuta mida basi”
“Okey poa”Alijibu Karim huku akiendelea kumsikiliza Zonga na Juma alinyanyuka na kutoka nje ya Mgahawa huo na zilipita dakika chache tu Zonga alitoka na kuondoka na baadae kidogo akatoka Karim na kuiendea gari yake.
.
“Broo”Karim aligeuka na kuangalia mtu anaemwita na alimwona ni kaka yake Najma.
“Vipi?”Aliuliza karim maana hakutaka stori sana maana alimuona Juma wakawaida sana kuongea nae , na bwana huyu alikuwa akijisikia mno na alikuwa akichagua wakuongea nae.
“Namjua huyo Roma , jamaa aliekuonyesha picha na najua namna ya kumpata”Aliongea juma haraka haraka na hapa karim alimwangalia Juma na kuvutiwa na mongezi.
“Ingia kwenye gari”Juma aliingia.
“Unamjua vipi Roma?”
Juma alianza kueleza namna alivyokuja kumjua Roma sikuyakwanza na mpaka Roma alivyopata mke .
.
“Sasa ni namna gani ya kumpata Roma?”.
“Roma anampenda sana Najma Sana , hivyo kama tutamtumia dada yangu itakuwa rahisi”Karimu aliona wazo zuri kwani alikumbuka maneno ya Zonga kuwa Roma alikuwa akimnyandua Rose mwanamke anaempenda
.
na kumhangaikia kila siku , ila huyo fala anaeitwa Roma anakula bila ya kufanya juhudi yoyote moyo wake uliuma na aliapia kwenye moyo wake kumpoteza Roma Duniani na kubaki na Rose wake lakini alikuwa hajui namna ya kumpata Roma, sasa baada ya Juma kujieleza aliona yes ,
.
mpango wake unakwenda kukamilika kirahisi. “Sasa sikia tutamteka Najma baada ya kumteka tutampigia Roma aje kumuokoa Najma maana umesema anampenda na una uhakika atakuja na hapo tutamkamata Roma”. “Yes huo ndio mpango wangu bro”Karim alimuona Juma ni asset kumtumia kwenye mpango wake na siku moja mbele mpango ulikamilishwa ,Majambazi yalikuja ndani ya nyumba ya Juma na kumbeba Najma , huku Juma akiahidiwa kuwa
.
Najma atakuwa salama , mpango huo Ahmed hakujua , Juma alitaka kupiga ndege wawili kwa jiwe moja , yaani kwanza Najma ashuhudie Roma akifa mbele yake , pili baada ya Roma kufa itakuwa rahisi kumshawishi Najma kuolewa na Ahmedi na yeye atakuwa na shemeji mwenye pesa na ukali wa maisha utapungua na aliwaza kabisa angemuomba shemeji yake mtaji aanzishe biashara.
.
Sasa baada ya mpango wenyewe kutekelezwa na Najma kupelekwa Vikindu na Karimu kwa mara ya kwanza kukutana na Najma mwanamke ambaye alikuwa akisikia taarifa zake kwa Ahmed , Karim alishangazwa na uzuri wa Najma kiasi kwamba pepo la ngono lilimvaa hapo na alipanga lazima alalale na Najma baada ya kutekeleza nia yake ya kumuua Roma , hakutaka kujali ahadi yake na Juma kwani alimuona kama kapuku tu , lakini pia hakutaka kmfikiria Ahmedi
kwanza alijua uyo mwanamke hampendi hivyo hakuwa na hasara kufanya yeye.
SEHEMU YA ISHIRINI
Ni saa mbili kamili za Asubuhi ndani ya hoteli moja maarufu ndani ya makao makuu ya nchi mjini Dodoma ,ndani ya chumba kikubwa cha hadhi ya juu ndani ya hoteli hii , anaonekana mzee mmoja mweupe mwenye nywele nyingi kichwani , lakini zilizokuwa na mvi ,Mzee huyu kwa makadirio ya umri hakuwa chini ya miaka Hamsini.
Mzee huyu alikuwa amesimama huku nyuma yake kwenye kitanda alionekana mrembo mmoja maarufu nchini akiwa amelala , akiwa hana habari na kinachoendelea kwa mgoni wake.
Mzee huyu alikuwa ameshikilia simu , lakini simu ilionekana nzito kwake , kwani alikuwa ni
mwenye kutetemeka sana,Mzee huyu wakati akiendelea kuangalia simu yake , mara simu yake ilipata uhai na kuanza kuita na mzee huyu kinyonge sana aliipokea.
“Nini kimetokea Hassani , inakuwaje mwanangu
akauwawa kikatili namna
hii”
.
“Mzee hata sisi tumeshindwa kuelewa na swala hili tunaendelea kulichunguza kwanini limetokea ghafla hivi” “Naomba hili lifanyike haraka Hassani , inaniuma sana kumpoteza Karim mrithi wangu”
“Sawa Mzee , swala hili lazima tutalichimba kujua undani wake nakuhakikishia lazima
tulipize kwa aliemfanyia unyama huu Karim”Ilisikika sauti hio na mzee huyu alikata simu , huku akisogelea sofa lililokuwa pembeni kwa kujikokota huku akiwa amejishika kifua chake , mzee huyu alionekanna kuwa katika maumivu ya kumpoteza kijana wake.
Alichukua mvinyo uliokuwa kwenye chupa na kumimina kwenye glass na kunywa kwa pupa na kisha akarudisha glasi kwenye meza.
“Naapia kwa mbingu na Arfhi uliehusika na kifo cha mwanangu nitakusaka mahali popote na nitahakikisha na kukata kiungo kimoja kimoja mpaka kifo chako”.Aliongea mzee huyu huku akiegamia kwenye sofa na kufumba macho kwa sekunde lakini alikuja kushituliwa na simu ilioanza kuita mfululizo , baada ya kuangalia nani anampiga aliona ni mke wake na hapa ni kama mzee huyu alizinduka kwani haraka sana alikimbilia nguo zake na kuvaa.
“Sijui mke wangu ataipokeaje hii taarifa”Aliwaza mzee huyu huku akiangalia simu ambayo ilikuwa ikiita kwa mara ya pili , lakini hakupokea Zaidi ya kutoka ndani ya chumba hiko.
.
Naam huyu ni meya wa mji wa jiji hili la Dodoma afahamikae kwa jina la Bakari Juma lakini pia anafahika kama “The man behind the Power’ndani ya kundi la The Black Mamba. ****
Juma aliamka asubuhi na mapema sana kama
kawaida yake , ili awahi kwenye kazi yake ya ubeba mizigo , siku hii bwana huyu alionekana kuwa na furaha sana , kwani kila akikumbuka tukio la jana moyo wake ulikuwa mweupe.
.
Baada ya kujiandaa alimuaga Najma na kuianza safari ya kuelekea kazini ndani ya mdakika
kadhaa tu alikuwa ashafika na kupata dili la haraka na kulishughulikia. Muda wa saa mbili ndani ya soko hili kulikuwa kumechangamka sana na kama ujuavyo Mbagala kwa kuwa na watu wengi ,Juma akiwa anapiga hadhithi na wenzake ndipo alipoanza kusikia habari ambazo hakuwa amezitarajia.
“Oy wadau inasemekana Karim amekufa jana kwa kuuliwa”Aliongea Yusuph na kumfanya Juma ashangae na kuona huenda Yusuph amechanganya majina kati ya Karim na Roma. “Wee..! kweli acha utani
,ilikuwaje?”
.
“Mwamba nasikia kagusa pasipo gusika na hivyo kuingia kingi”
“Oy yusuph ni kweli Karim kafariki?”
“Habari ni za kweli kabisa , japo kwa sasa ni za chinichini ia , mwili wa Karim upo Muhimbili ninavyoongea hapa na hakufa peke yake”Kwa muonekano wa Yusuph wa uongeaji wake Juma aliamini bwana huyu hakuwa akidanganya kwani alikuwa akimwamini sana , lakini bado kwenye kichwa chake alikuwa na maswali ni kwa namna gani Karim amekufa na sio Roma , au watu wameona vibaya hayo ndio yaliokuwa mawazo yake.
Juma aliendelea kuchapa kazi mpaka muda wa saa tano na hapo ndipo aliposikia simu yake inaita na kuitoa mfukoni na namba ilikuwa mpya.
“Juma!!, Najma hali yake mbaya rudi umuone mdogo wako”Juma mara
baada ya kusikia sauti hii aliitambua vyema kama moja ya wanawake waliokuwa ni wapangajii katika nyumba yao na Juma hakutaka kubaki ndani ya hili soko kkwani aliondoka haraka na kurudi nyumbani.
Ni kweli mara baada ya kuingia ndani ya chumba cha Najma alimuona dada yake alivyokuwa akitoa jasho jingi , huku hali yake ikiwa mbaya , ule weupe aliokuwa nao Najma ulikuwa umebadilika na kuwa mwekundu , huku mwanadada huyu akitetemeka.
Juma hali ile ilimuogopesha na maamuzi alioyafanya haraka haraka ni kumchukua Najma na kuita bajaji kwa ajili ya kuelekea hosputalini akishirikiana na mpangaji aliempigia simu.
Ndani ya madakika kadhaa tu walikuwa washafika ndani ya hospitali ya Zakhiem na kupokelewa , huku Najma akiingizwa kwenye chumba cha daktari pamoja na Juma.
Juma alitoa maelekezo ya haraka haraka huku akiingiza maeneno mengi yasio na ukweli na kisha dokta huyo aliandika vipimo na Najma akatolewa na kuingizwa wodini .
Zilikuwa ni dakika kadhaa tu za Juma baada ya kutoa maelezo kwa dokta na kumuacha mpangaji aendelee kumwangalia Najma kutokana na yeye kutoruhusiwa kuingia wodi za wanawake , alitoka nje kabisa ya geti na wakati anatoka tu ni kama alikuwa akisubiriwa kwani , vijana wawili waliovalia mavazi ya kawaida walimsogelea. “Oy Broo wewe ndio
Juma?”
“Yes ni mimi”.
“Kuna inshu Fulani tunataka kukuuliza , ila hapa si salama tuna gari yetu upande wa pili itakuwa vyema kama tutaenda wote”Juma alifikiria kwa muda huku akiwangaalia vijana hawa na kuona hawakuwa na hatari yoyote kwake na aliona ni vyema kuongozana nao.
Gari walikuwa wameipaki upande wa kushoto mbele kabisa na ukumbi maarufu jijini Dar es salaam unaofahamika kama Dar Live , vijana wale waliisogelea gari nyeupe aina ya Toyota Corola na kisha mmoja aliingia wa kwanza na kisha akafatia juma na yule mwingine akaingia mbele.
Kitendo cha juma kuingia tu kwenye gari alishituka akiwekewa kitambaa kwenye pua zake na mtu ambaye ilionesha ni Dhahiri kabisa alikuwa ndani ya gari hili kabla ya Juma kuingia.
Baada ya ukio lile lililofanyika bila ya mtu yoyote kuona kinachoendelea hatimae gari ile ilitolewa kwa spidi kueekea upande wa kariakoo na ikawa Juma katekwa kiulaini.
****
Roma kama kawaida alifika kazini huku kwenye akili yake akiwa na mawazo ya kwenda kupoteza poteza muda
kwa kucheza magemu ili arudi zake nyumbani kula na kwenda kiwanja cha bata.
“Hiii kazi nafanya kumridhisha tu Edna , ila kutokana na ugonjwa wangu sipaswi kufanya kazi ambayo inanifikirisha
, lazima nijichunge”Alijiongelesha Roma wakati akiingia ndani ya ofisi yake ya kazi.
Na siku hii haikueleweka , ila Wafanya kazi walionekana kuwa bize kweli na kazi na hata Roma alishangaa kwani hata Recho ambaye alikuwa akipenda kuongea sana , alionekana kuwa bize na Zaidi ya salamu hakukuwa na Zaidi ya maongezi, ila Roma hakujali sana yeye aliendelea zake na kucheza gemu.
Muda wa chakula ulivyowadia ndio alikuwa mtu wa kwanza kuinuka kwa ajili ya kuelekea kula kitendo kilichowafanya wawafanya kazi wenzake wamwangalie , ila hakujali , kwani Roma sifa yake kubwa ni kwamba jamaa huyu mshipa wa Aibu ni kama umekatwa.
Roma baada ya kujiona ameshiba , alimkumbuka Doris sana na alitamani amuombe mchezo baadae , ila alikumbuka kuwa alikuwa amenuniwa tokea tukio la yeye kulala na waziri Neema Luwazo , hivyo hakutaka kujihangaisha kwake , aliona kama Neema atarudi kwake basi wataendelea na kama
hatorudi hana haja ya kwenda kuomba msamaha na kubembeleza.
Roma baada ya kushiba alichuku maji yake ya Kilimanjaro makubwa na kisha alitoka sehemu hii ya kantini lakini ile anakata kulia ili kuingia upande ambao zipo Lift alikuja kukutana na Edna njiani akiwa na Doris , walionekana walikuwa
ndio wanaelekea kula ,Doris hakuongea na Roma na hivyohivyo hata kwa Edna , alimpita Roma kama hamjui , ila kwa Roma hakujali licha ya kujisikia vibaya moyoni.
Ilikuwa ni muda wa saa kumi za jioni Roma akiwa ndani ya sehemu ya kuegeeshea magari , akilisogelea gari lake V8 , mara gari aina ya BMW M4 ya pink ilikuja kupaki pembeni yake kiasi kwamba ilitaka kumgonga.
Roma wakati akishangaa , kioo cha gari hio kilishushwa na kumuona mwanamke mrembo na huyu hakuwa mwingine bali aalikuwa ni Nasra.
“Roma naomba
unisindikize mahali?”Ilisikika sauti ya mrembo huyu na Roma alimwangalia huyu mwanadada na kisha aliitikia kwa kichwa na kuingia kwenye gari ya huyu mrembo na kisha ikatolewa ndani ya jengo hili kwa spidi.
Gari hii haikwenda mbali sana , kwani ilikuja kusimama nyuma ya hospitali ya Aghakhani
,Baada ya gari hii
kusimama mwanadada Nasra alishuka kwa maringo na Roma nae alishuka na mwanadada huyu alielekea upande wa Beach, chini kidogo sehemu ambao ilikuwa na miti.
“Nasra yuko wapi?”Ilikuwa ni sauti ya Roma akimwangalia mwanadada aliekuwa mbele yake , swali hilo ni kama lilikuwa la kijinga kwani mtu aliekuwa mbele ya Roma alikuwa ni Nasra , lakini sio kweli kwani baada ya Roma kuuliza swali hilo mara mwanadada yule alibadilika sura na kuwa mtu mwingine kabisa ,Alibadilika kama Jini.
.
Alikuwa ni mwadada wa kijapani mrefu saizi ya kati. Mwenye mwili mwembamba na ungejiuliza ni kwa namna gani mwanadada huyu aliweza kuchukua muonekano wa Nasra mfanyakazi wa kampuni ila huo wote ni uchawi wa kijapani.
“Yamata sect ! Naona wajapani mmezidi kuimarika kwenye mbinu yenu ya kichawi ya kuiba uhusika wa mtu”Aliongea Roma kwa lugha ya kijapani.
“Tunazo mbinu nyingi za kichawi Hades , ambazo ni mpya na
hauzitambui”.Roma
alitabasamu na kumwangalia mwanamke huyu wa kijapani akimwita Hades.
“Jina lako ni nani kabla sijakuua”Aliongea Roma. “Jina langu ni Tanya na nipo hapa Tanzania kwa aili ya kuchukua jiwe la
.
Kimungu(Godstone)”Rom a alitabasamu na hapo hapo akakumbuka kiboksi alichokuwa amekificha kule nyumbani kwenye chumba cha mazoezi , alikumbuka pia siku ambayo alisachiwa kule nyumbani kwa Juma alikokuwa amepanga , aliweza pia kukumbuka siku ambayo anaenda ikulu na Edna kuna gari iliokuwa ikiwafatilia nyuma.
.
“Inaonekana mpo hapa nchini kwa muda mrefu kidogo kuliko nilivyowadhania”. “Umepatia tupo hapa nchini kwa Zaidi ya mwezi sasa na , tumekuwa tukikufatilia kwa kila unachokifanya kila siku , lakini Master anahitaji jiwe la kimungu mapema na hataki tena tukiongeza hata siku moja hapa nchini , hivyo leo
utaniambia ni wapi jiwe
hilo lilipo”
.
“Sijui mnacho kiongelea kwani sina jiwe hilo na hata kama ningekuwa nalo nisingewapatia” “Unajidanganya Hades, Nasra yupo mikononi mwetu na kama unataka aishi huna budi kutupatia kile tunachotaka”
.
Aliongea Tanya mwanadada huyu wa kijapani akimwita Roma Hades , yaani Mungu wa wafu au Mungu wa wahalifu na jina hili linatoka katika historia ya Ugiriki ya kale.
.
Roma alimwangalia Tanya na kuona huyu mwanadada hakuwa akitania hata kidogo , lakini licha ya hivyo hakuwa tayari kutoa Jiwe alililokuwa nalo kwani alihofia nguvu ya jiwe hilo endapo likitua kwenye mikono ya watu ambaoo sio sahihi dunia inaweza ikawa sio salama na hata mtu aliemkabidhi jiwe hilo alikuwa na maana kubwa kani aliamini kwamba Roma ndio mtu pekee ambaye ana uwezo wa
.
kulilinda lisiwafikie wahalifu..
Roma hasira zilianza kuonekana kwenye macho yake , na kiini cha macho yake kikaanza kubadilika rangi na kuwa cha kijani , tena kijanni kilichokolea kiasi kwamba kilianza kumuogepesa mwanadada huyu wa kijapani.
“Hades ukifanya ujinga Nasra atakufa , yupo kwenye mikono yetu na sipo hapa kwa ajili ya kupigana”
.
“Mpaka kunileta mahali hapa ni Dhahiri upo kwa ajili ya kupigana na hata haupo hapa kwa ajili ya kupigana umevunja sharia kuu mbili nilizoweka , sipendi kutishiwa na pili sipendi mtu anaetumia watu wengine kunipata”Baada ya kusema hapo Roma kama upepo alitoweka sehemu aliokuwa amesimama na kumsogelea Tanya ,lakini ile anafika ile sehemu Tanya alipotea ghafla na hapa Roma alitabasamu.
.
“Kajinga sana haka kademu , kanaona kwa vijimtego vyake vya kichawi kanaweza kunizidi hakuna mchawi aliewahi kunizidi”Aliwaza Roma na kisha alifumba macho huku masikio yakiwa juu juu kama popo na hapa alionekana alikuwa akipambana kwa hisia kwani , sekunde chache tu alikuwa ashahama aliposimama na kwa spidi ya ajabu alirusha ngumi na kilichosikika ni: “Aiii...”.Na hapa mwanamke yule alijitokeza kwa mara nyingine.
.
“Leo nakuua hapahapa”Aliongea Roma huku akianza kupeleka mashambulio kwa kasi , yaani kwa namna wawili hawa walivyokuwa wanapigana kama
.
ungekuwepo eneo la tukio ungehisi upepo tu ambao sio kawaida.
Tanya aliruka hewani huku akija upande aliosimama Roma kwa
spidi ya hali ya juu , na ile anamkaribia karibu alirusha kisu ambacho alimlenga nacho kwenye koo la shingo , lakini tendo hilo Roma aliliona na
.
alichofanya ni kuruka juu na kisha akazuia kile kisu kwa mkono kiasi kwamba kikaenda kutua kwenye mchanga wa baharini , baada ya kutua Roma kwa spidi ya hali ya juu alikichukua na kumrushia Tanya , lakini mwanadada huyu alionekana mwepesi balaa kwani alijibiringisha hewani mara mbili na kupotea , lakini kwa upande wa Roma ni kama vile alitegemea kitendo hicho kwani ile Tanya anapotea alisogea upade wa kushoto na kurusha ngumi nzito na mguno wa kike wa maumivu ulisikika na Tanya alikuwa chini , ngumi ile ilionekana kumtaiti vyema , Roma hakuishia hapo tu
.
alimsogelea na kumshika koo.
“Niambie Nasra yuko wapi kabla sijakuvunja shingo”Aliongea Roma kwa sauti kama ya Roboti , sauti ambayo ilimuogopesha Tanya lakini kabla Tanya hajavunjwa shingo mara gari nyingine ilifika na wakashuka watu wawili kwa haraka sana na kusogelea uande aliokuwepo Roma.,wote walikuwa wanaume pia wakiwa wajapani.
“Naona wenzako wamefika na hii inanirahisishia kazi , nitawaua wote hapa hapa”Aliongea Roma huku akijiandaa kumvunja shingo Tanya .
“Hades Acha usimuue tupo tayari kukupatia Nasra”Aliongea mwanaume yule wa
kijapani kwa lugha ile ile ya kijapani na Roma alimwangalia na kisha kuwajibu kwa kijapani.
“Siwezi kuwaamini”.
“Nasra yupo kwenye gari , unaweza kumchukua
Tanya mpaka kwenye Gari na ukithibitisha kwa kumuona Nasra tunaomba umuachie”
.
“Nikora niko tayari kufa , ila hakikisheni tunapata jiwe na mumpelekee
Master”
“Hapana Tanya Master alitupa maagizo ya kukulinda kwa namna yoyote ile”Aliongea huyu jamaa ambaye Tanya alimwita kwa jina la
Nikora.
Roma aliona afanye kama walivyokuwa wanataka na alimchukua Tanya kama mateka na kwenda nae
kwenye gari , na akafungua mlango na kumuona Nasra akiwa hajitambui huku akiwa hana nguo hata moja.
.
Baada ya kujiridhisha , Roma alimpiga Tanya ngumi na mwanadada huyu alitoa ukulele na baada ya kuridhika Roma alimsukuma kwa nguvu na kwenda kutua kwenye mchanga wa Beach na kitendo hiki kuna baadhi ya watu waliokiona ,ila walikuwa bize na mambo yao.
.
Roma alitoa gari ya Nasra na kwenda kuisimamisha kwenye duka moja la nguo ,alinunua nguo za kike na kurudi nazo kwenye gari na kulitoa kurudi kwenye kampuni ,
.
baada ya kuingiza gari sehemu ya maegesho alimshika kwa kumuwekea Nasra kiganja cha mkono kwenye kifua na akashituka.
.
Nasra alijishangaa akiwa uchi pembeni ya Roma , alimwangalia Roma huku akionekana ni mwenyekuchanganyikiwa na kitu cha kwanza kuziba ni sehemu zake za siri , lakini Roma wala hakujali alikuwa ametabasamu tu akimwangalia mwanadada huyu anavyoona aibu.
INAENDELEA GUSA BUTTON APA CHINI KUENDELEA MBELE
.
ENDELEA KUSOMA
```
Chapisha Maoni
TOA MAONI YAKO HAPA