46 - 50 NILIEMDHANIA KAHABA KUMBE NI BIKRA
SEHEMU YA 46 YA SIMULIZI HII
Tikayi kwenye Maisha yake hakuwahi kuwaza kama anaweza kukutana na mtu anaebadilika kama ilivyokuwa kwa Roma , alijiambia katika akili yake kwamba katika siku zote alikuwa amefanya makosa na kumgusa mtu ambae hakupaswa kuguswa basi ni bwana aliekuwa mbele yake, aliamini ana asilimia ndogo sana za kutoka hapo ndani akiwa salama , akili yake ilikuwa ikifanya kazi kama mashine , alimwangalia Roma ambaye awamu hii alikuwa anaonekana kawaida na nikama alikuwa haamini kama mtu aliekuwa mbele yake dakika kadhaa zilizopita alikuwa kiumbe cha kutisha kilichojaa ukatili.
“Utachukua asilimia sitini za faida ndani ya mkataba wa kibiashara tutakaofanya”Aliropoka Tikayi na kumfanya Dorisi ashangae , kwani katika mkataba huo wa kibiashara walikuwa wakichukua asilimia therathini tu na JR asilimia ishirini huku Yamakuza wakichukua asilimia hamsini, hivyo Dorisi kusikia hivyo moyo waka ulipiga kite na kuona dili hilo litakuwa nono kama tu wangelikubali
“Unadhani ninaweza kukuacha hai kwa asilimia sitini?”Aliongea Roma kwa sauti ya kawaida na Tikayi akamwangalia Roma kwa wasiwasi. “Asilimia hizo ni nyingi sana ndani ya kampuni yenu kutokana na uthamani wa Material” “Umefanya makosa mangapi , isije ukawa unapendekeza asilimia sitini lakini hata makosa yako huyajui”
Tikayi alinyanyuka na kupiga magoti , huku akianza kufikiria ni makosa mangapi alikuwa amefanya na kisha akamwangalia Dorisi aliekuwa akimwangalia kwa wasiwasi na Tikayi ni kama alikuwa akitaka kuomba msaada kwa Dorisi. “Nimefanya makosa matatu” “Yataje niyasikie” “Kwanza kabisa nilipanga kuwaua wewe na Dorisi kule nyumbani , pili nikataka kukuaa hapa ndani ,tatu….”Alianza kujikuna kichwa akifikiria ni kosa gani tena ambalo alikuwa amelifanya , lakini hakuelewa alikumbuka katika makosa yote alitaka tu kumuua Roma. “Umenikosea halafu hukumbuki makosa yako , sasa nasema hivi mimi Roma Ramoni siwezi kukuacha hai leo na nakupa dakika moja tu unishawishi nisikuue na kama unajiona huwezi kunishawishi niambie niivunje shingo mapema tu nisipoteze muda wangu, mimi kuua kwangu ni jambo jepesi sana” Aliongea Roma huku akionekana kuwa siriasi na Tikayi alijikuta akikumbuka macho ya Roma dakika kadhaa zilizopita na mwili wake ukahisi ubaridi wa hali ya juu sana wa woga. Dorisi alishindwa kuongea chochote , alitamani kumwambia Roma
wakubaliane na asilimia Sitini alizotaja Tikayi lakini alishindwa kuongea , hakuelewa kwasababu gani, lakini alikosa hali ya kujiamini kuongea na Roma. “Bado Sekunde kumi”aliongea Roma huku akiendelea kumuangalia na Tikai hakujua ni namna gani anaweza kumshawishi Roma asimue. “Tatuuu ….mbiliii ….” “Kosa lingine tulitaka kuwasainisha mkataba feki”Aliongea Tikayi kwa kukurupuka na kumfanya Roma atabasamu na Dorisi macho yalimtoka , hakuelewa alichozungumza Tikayi kina ukweli ndani yake. “Wewe na nani mlitaka kutusainisha mkataba feki, nataka maelezo yalionyooka la sivyo nitakunyonga hapahapa na Japani yote hii hakuna atakae kuwa na uwezo wa kunigusa”Roma alionyesha hasira zake waziwazi na kumfanya Tikayi kuanza kuogopa. “Black Mamba kupitia muwakilishi wao Abubakar”Dorisi alizidi kushangaa na hakuelewa
Black
Mamba ni mtu gani , lakini kwa Roma alikuwa ashasikia sana hili kundi na pia alikumnbuka Karimu ndio aliekuwa kiongozi wa kundi hilo na baada ya kusikia maneno haya kutoka kwa Tikayi alijua Black Mamba walikuwa wakitafuta namna ya kulipiza kisasi kupitia kampuni ya mke wake , alijikuta akikasirika na kujilaumu kwanini alimuachia Abu akimbiena hakumua , lakini alijiambia katika nafsi yake atamkamata tu na kifo kitamuhusu. “Kwa hio unamaanisha swala lote la Mkataba kati ya Yamakuza na kampuni yetu , yote yalikuwa ni uongo na hakukupaswa kuwa na mazungumzo ya aina yoyote yale ya kibiashara baina yetu?”Aliuliza Dorisi na hio ni baada ya Roma kumueleza kinachoendelea kwa kutafsiri maneno ya Tikayi.
“Kuhusu Material Mapya ni biashara ya kweli , lakini kuhusu material hayo kusambazwa na kampuni ya Vexto hakuna kitu kama hiko, kampuni ambazo tulichagua kufanya nayo kazi kwa Tanzania ni Maple Group na JR Group na mkataba halisi ulipangwa kusainiwa siku tatu mbele baada ya kusaini na nyie mkataba feki a kuhakikisha mmetupa kiasi cha pesa ambacho kipo kwenye mkataba” Aliongea Tikayi na kumfanya Dorisi kushangaa mno , lakini sio kushangaa tu aliogopa kwa wakati mmoja , kwani kama angesaini huo mkataba na kisha wakaruhusu kiasi kikubwa cha pesa kikatoka kwenye kampuni na baada ya hapo wakagundua kuwa mkataba ulikuwa ni feki huenda Vexto Grupu ingefilisika rasmi,Dorisi alimwangalia Roma na kuzidi kushangaa na aliamini hata kama angekuja Edna mwenyewe Japani huenda asingegundua jambo hilo. “Sasa Bwana Tikayi nyie na hawa Black Mamba mna uhusiano gani na kwanini mkubaliane nao kwa ajili ya kusaini
mkataba feki na kampuni yetu , ilihali swala hili huenda lingewaletea matatizo mbeleni?” Tikayi alifikiria kidogo na kisha akakaa chini kabisa kwani alionekana kuchoka kwa kutumia magoti na hakujali uchafu uliokuwa chini na kisha akamwangalia Roma kwa wasiwasi ,Tikayi hakuwa na namna , aliona bila ya kusema ukweli asingeweza kutoka kwenye mikono ya Roma.
“Black Mamba ndio wasambazaji wakubwa wa madawa yetu ya kulevya kwa Afrika Mashariki yote kwa Zaidi ya miaka kumi , lakini miaka mitatu nyuma kulitokea tatizo baada ya raisi mpya kuchukua madaraka”
“Tatizo gani?”
“Njia ambayo tulikuwa tukitumia kuingiza madawa ya kulevya ndani ya Tanzania Raisi Senga aliigundua na kuizuia , lakini pia sharia zake mpya na ukaguzi mkali bandarini na njia zote za usafirishaji tulishindwa kupata Njia salama ya kupitisha madawa na kwa Afrika mashariki soko kubwa la madawa lipo Tanzania , hivyo uongozi wa senga ulifanya mapato ya biashara kushuka kwa kiasi kikubwa san ana hapo ndipo tulipokuja na wazo la kutengeneza njia mbdala ya kuingiza madawa Tanzania”. “Hio njia yenu inahusiana vipi na kampuni ya Vexto?” “Vexto ndio kampuni pekee ambayo imepewa mkataba wa kudumu wa kuingiza mafuta ya petroli Tanzania kutoka India na huo mkataba unaifanya Vexto kuwa na nguvu ndani ya taifa la Tanzania”Aliongea Tikayi na kumfanya Roma ashangae kwani hilo hakuwa akilifahamu na alimgeukia Dorisi na Dorisi alitingisha kichwa kuashiria ni kweli. “Saa kama ndio wanamkataba wa kudumu wa kuingiza Mafuta inahusiana vipi na madawa yenu ya kulevya?” “Njia salama ya kusafirisha madawa ya kulevya duniani kwasasa ni kwa njia ya Shehena ya Mafuta”Dorisi alishangaa lakini Roma hakushangaa. “Kwa hio mlitaka muitumie Vexto kuingiza madawa Tanzania kupitia shehena ya Mafuta wanayoingiza?”Alitingisha kichwa kuashiria ni kweli. “Black Mamba mkuu wake ndani ya Tanzania ni nani?” “Mkuu wa Black Mamba Tanzania simfahamu ila ninachojua ni kwamba anafahamika kwa jina la The Doni , ila muwakilishi wake mkuu ambaye mara nyingi ndie anaemuakilisha katika mazungumzo ya kibiashara ni Abubakari Juma” Roma alijikuta akishangaa na kuwaza huyu The Doni ni nani , kwanini kila mtu hakuwa akimjua na ana nguvu gani ndani ya taifa la Tanzania , ila alijiambia atayajua yote hayo taratibu huku akijipiza moyonni akimpata lazima amvunje shingo. “Baada ya kutusainisha mkataba feki ni kipi kingefuara baada ya hapo?” “Mpango uliokuwepo ni kwamba kama mkataba huo ungesainiwa na ikajulikana kwamba ni feki ,Edna angekosa vigezo vya kuwa CEO , lakini wakati huo huo kampuni ingefirisika na JR Group ingeinunua kampuni ya Vexto na JR ni sehemu ya Black Mamba na mpango ungekuwa umefanikiwa kirahisi” Dorisi alijikuta akivuta pumzi , hakuwa akijua kuwa kampuni ya Vexto ilikuwa ikikodolewa macho kwa namna hio na wafanya biashara wa madawa ya kulevya , sasa alianza kuhisi ile michakato yote ya Abu kutaka kumuoa Edna ni kwasababu ya hilo swala la uingizaji wa Madawa nchini , hakika alishangaa na kuona siku hio amejua mengi lakini pia alishukuru moyoni kwamba swala hilo la kusaini mkataba feki halikuwa limefanikiwa, maana kila alipokuwa akikumbuka nguvu na juhudi za Rafiki yake Edna kuifikisha Vexto ilipofikia aliogopa na aliona huenda Edna angechukua maamuzi magumu hata ya kujinyonga. “Mpaka hapo bwana Tikayi umenishawishi japo bado kidogo sana , nadhani mpaka sasa unafahamu kuwa mimi na Dorisi ndio tunajua kuwa wewe ndio umemuaa Tikayeshi ndugu yako , lakini pia mpaka sasa unajua fika kwamba ulitaka kutuua , lakini pia mlitaka kutusainisha mkataba feki , Sasa wewe mwenyewe hebu kaa chini tena fikiria unadhani utanipatia kitu gani cha thamani nikusamehe?”Aliongea Roma na kumfanya Tikayi afikirie,
“Kwakua biashara ya Material mapya ni halali nitaiota JR Group kwenye mkataba na kuiingiza Vexto , lakini katika mkataba huu Vexto mtapata asilimia sitinni na Tano ya faida yote ya mauzo kwa bara la Afrika nadhani hilo sio dili baya kwa kampuni ya Vexto” Dorisi macho yalimtoka , alitamani aseme ndio hapo hapo lakini alikumbuka dakika chache nyuma kuwa kama sio Roma wangesainishwa mkataba feki bila wao kujua. Akaona atulie na Roma amalize kila kitu. Basi Roma alikubaliana na Tikayi kwa kusainishana mkataba mpya kati ya Maple Group na Vexto Group huku kampuni ya JR ikitolewa kwenye mkataba huo. Roma kama kawaida yake alimpiga mkwara wa kutosha Tikayi kwa kumtishia kama tu angefanya ujinga mwingine wa kufanya janjajanja ya kumzunguka , basi angeimaliza familia nzima ya Yamamoto na kuchukua na kampuni yao na Tikayi kutokana na mziki wa Roma aliokuwa ameushuhudia kwa macho yake , alijikuta akiapia kwa majina yote hatokuja kumuuzi Roma tena na atafanya kama ambavyo wamekubaliana. Siku iliofuata Roma na Dorisi hawakulala ndani ya Twillight villa kutokana na mambo yaliotokea kati ya Tikayi na Roma , lakini pia familia hio ilikuwa kwenye maombolezo ya msiba wa Tikayeshi ambaye alikuwa ameuliwa na mdogo wake Tikayeshi na kuhusu Tikayi kumuua kaka yake lilimalizwa kifamilia na hakukuwa na taarifa yoyote iliotolewa Zaidi ya kutangaza kuwa ni ajali ambayo ilitokea na kumuua Tikayeshi. Dorisi aliwasiliana na Edna na kumpa taarifa ya kile kilichokuwa kimetokea na Edna alifurahishwa sana na taarifa hio huku akiahidi zawadi kwa wawili hao watakaporudi nchini. Mkataba ulikuwa ukisainiwa siku mbili mbele lakini kabla ya kusainishana mkataba huo viongozi wa Maple Group walitakiwa kufika nchini Japani kwa ajili ya
mazungumzo hayo ya kibiashara lakini pia kukagua miundo mbinu ya kiwanda ambacho kitakuwa kikitumika kutengenezea material hayo mapya. Ni saa Moja za jioni ndani ya uwanja wa Kansai Tikayi alikuwa eneo la mapokezi la kufikia wageni akimsubiria mgeni atakaeiwakilisha Maple Group katika kusainishana mkataba mpya. Baada ya kusubiria kwa takribani nusu saa akiwa na walinzi wake , hatimae eneo la kutokea wageni alionekana mwanamke mrembo akiwa anatoka huku akiwa amependeza sana , mwanamke huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni Naibu waziri wa Sanaa , mheshimiwa Neema Luwazo.
SEHEMU YA 47 YA SIMULIZI HII
Neema Luwazo waziri wa Sanaa kutoka Tanzania alionekana kufurahia ukaribisho kutoka kwa Tikayi kwani muda wote alionekana kuwa na uso uliokuwa umepambwa na tabasamu.
“Licha ya kwamba swala hili la kibiashara lilikuwa ghafla kwangu baada ya kuvuta tarehe nyuma , lakini nafurahi sana kufanya kazi na kampuni yenu”Aliongea Neema baada ya kuingia kwenye gari ile ile iliowapokea Dorisi na Roma Caddillac Limuosine “Hata sisi pia kama kampuni tunafuraha kubwa sana kufanya kazi na Maple grupu , karibu tena Japani kwa mara nyingine” “Nashurkuru sana , sio mara yangu ya kwanza kufika Japani lakini ni mara yangu ya kwanza kufika hapa Osaka , unaonekana kuwa mji mzuri sana , nimezoea kufika Tokyo mara kwa mara katika safari zangu zote za kibiashara” “Ndio Osaka ni mji mzuri sana na una utulivu wa hali ya juu”Alijibu Tikayi kwa kingereza safi na safari iliishia katikati ya mji huu kwenye hoteli iliokuwa ikifahamika kwa jina la W Osaka Luxury one ni moja ya hoteli nzuri sana na ya bei ghali ndani ya jiji hili la Osaka usiku mmoja tu ni milioni nne za kitanzania. “Wow! Its so amaizing hereTikayi”Aliongea Neema huku akifurahishwa na mandhari mazuri yaliokuwa ndani ya hili eneo na alishindwa kuzuia furaha yake na Tikayi alitabasamu na kumuongoza ndani.
Ni Siku nyingine ndani ya makao makuu ya kampuni ya Yamakuza kwenye ukumbi mkubwa wa mikutano , walionekana viongozi wa juu kabisa wa kampuni wakiwa wameizunguka meza , lakini pia kwenye meza hio alionekana mwanadada Neema luwazo alievalia vazi lake la suti akiwa ameketi kwenye nafasi yake , huku pembeni yake kukiwa na viti viwili ambavyo vilikuwa wazi ni kama watu ambao walitarajiwa kukaa kwenye viti hivyo ni kama walichelewa , kwani watu wote walikuwa washawasili akiwemo Tikayi ambaye siku hio ndio alieonekana kuongoza mazungumzo yote yaliokuwa yakihusu mkataba wa biashara kati ya kampuni ya Yamakuza Corporationi`s na kampuni mbili kutoka Afrika yaani Maple group ambayo ilikuwa ikiwakilishwa na Neema ambaye ndie alikuwa mmiliki na mwenyekiti wa kampuni hio , lakini pia Dorisi na Roma ambao ndio walikuwa wawakilishi wa kampuni ya Vexto International.
Dakika chache mbele mlango wa chumba hiki cha mikutano ulifunguliwa na akaingia mrembo Dorisi akiwa ameambatana na Roma Ramoni , wawakilisi wa kampuni ya Vexto. Kila mmoja macho yalikuwa kwa wawili hao na kwa jinsi walivyokuwa wamependeza ni kama vile walichelewa makusudi ili kujionyesha , viongozi hawa wajuu walikuwa wanawaangalia Dorisi na Roma kwa namna ya macho ya kitathimini , upande mwingine mwanamama Neema Luwazo jicho lilikuwa limemtoka mara baada ya kumuona mtu ambaye hakuwa amemtarajia kumuona , tena kwenye nchi ya mbali kama hii ya Japani. “How This possible?” Alijiwazia huku akiendelea kumuangalia Roma ambaye kama kawaida yake , alikuwa akijiamini mno kiasi kwamba hata watu walijiuliza ni ninni kinamfanya kujiamini kwa namna hio , kwani kwa Roma watu waliokuwa mbele yake ni kama alikuwa akiwafahamu wote. Dorisi akiwa nyuma Roma alitangulia na kuelekea upande ambao ndio nafasi zao zilikuwa zimeandaliwa , wakati wote huu Roma hakuwa amemuona Neema bado mpaka pale
alipofikia kiti ndipo alipomuona mwanamke ambaye kwa kumuangalia tu kumbukumbu zake zilimrudisha ndani ya taifa la Tanzania kwenye hoteli ya New Afrika akiwa amemkunja kisawasawa lakini sio kwa Roma tu aliemuona Neema hata pia kwa Dorisi alimtambua mara tu baada ya kumuona na alionyesha waziwazi kutofurahia uwepo wa mwanamama huyo hapa ndani. “Mrembo ni wewe?” Aliongea Roma mara baada ya kumfikia huku akivuta kiti kwa ajili ya kuketi , lakini Neema alishindwa kuongea chocote kwani muda wote alikuwa akimwangalia Roma kwa mshangao mpaka pale Tikayii alipoanza kuongea na kufungua kikao hiko. Tikayi alionekana kujiamini sana , lakini kila alipokuwa akikutanisha macho na Roma alijikuta akikosa utulivu na hali hio Roma na Dorisi waliishuhudia na Roma alimkonyeza Tikayi na akatabasamu na kuendeleza kikao. Baada ya utangulizi wa ajenda za kikao hiko kuhusu mkataba wa kibiashara juu ya uzalishaji wa material mapya ambayo kama kampuni walikuwa wakiamini yanakwenda kuweka historia kimauzo , ilifikia wakati ambao sasa watafiti wa kampuni ya Yamakuza ambao ndio waliokuwa wakihusika kwa asilimia miamoja na gunduzi ya material hayo , walitakiwa kutoa
‘representation’ kwa ufupi.
Na Tikayi alichukua nafasi hio kumkaribisha kiongozi wa juu wa utafiti kuingia ndani ya chumba hiko cha mkutanao kwa ajili ya jambo lililokusudiwa na baada ya kutoa ukaribisho mlango ulifunguliwa na akaingia kijana mmoja wa kijapani mrefu mwembaba aliekuwa na nywele ndefu lakini zilizokuwa na staili flani hivi kama wigi, alikuwa ni kijana wa makadirio ya umri kati ya miaka si chini ya ishirini na Tano ,bwana huyu alijitambulisha kwa jina la Mori Satoshi. “Kabla sijaanza kutoa taarifa juu ya Project hii ambayo imenichukua miaka mingi kufanya utafiti na majaribio mpaka kuikamilisha naomba kwa heshima kubwa nimtambulishe mwalimu wangu ambaye alikuwa na mimi bega kwa bega katika masomo yangu ndani ya
chuo kikuu cha Oxford Dr Clark Stephanie” Aliongea Mori na hapohapo mlango ukafunguliwa na akaingia mwanadada ambaye alimfanya Roma atoe macho. Alikuwa ni mwanamke mzungu mrembo sana wa kuvutia mno kwa muonekano wake , mwenye muonekano ambao ukiangalia utagundua kuwa alikuwa na umri mdogo sana na hii ilifanya watu wengi hapa ndani kushangazwa na mtu ambaye anaitwa Profesa n ani mwalimu wa Mori kuwa ndio huyo mwanamke.
Profesa Clark alijikuta macho yakimtoka mara baada ya kukutanisha macho na Roma ni kama mtu ambaye hakutegemea kumuona mtu huyo hapo ndani na mshangao wake ulifanya watu hapa ndani kuangalia upande ambao macho ya Profesa clark yalikuwa yameelekea na wote wakagundua kuwa Profesa alikuwa akimwangalia Roma na huku Roma baada ya kuona macho ya Profesa yanamwangalia aliinua mkono na kumpungia huku akiachia tabasamu pana usoni na hapa ndipo watu walizidi kushangaa ,sio Dorisi na Neema waliokuwa wamekaa karibu na Roma ,lakini pia Mori mwenyewe aliemleta profesa wake hapo ndani alikuwa kwenye mshangao na pia Tikayi alikuwa kwenye mshangao.
Baada ya hali hio ya mshituko kupita Profesa Clark alianza kuitambulisha. “I am renowned Professor Clark Stephanie, it has been an honor for me to attend this session which involves the success of my student Mori in his research which has led to development of new materials, Despite having a tight schedule, it's a pleasure for me to be able to listen to what Mori prepared, but I'm also happy to meet each of you”. “Mimi ni Profesa maarufu ninaefahamika kwa jina la Profesa Clark Stephanie , ni heshima kwangu kupata nafasi ya kuwa moja ya wahudhuriaji wa kikao hiki ambacho kinahusisha taarifa ya mafanikio ya Utafiti wa mwanafunzi wangu Mori , ambao umepelekea kupatikana kwa Material mapya, licha ya kuwa na ratiba iliobanana ni furaha kwangu kusikiliza kile Mori alichoandaa na pia nimefurahi kukutana na kila mmoja hapa ndani” Aliongea kwa kujiamini kabisa , huku akionyesha ile hali flani ya mtu kujiamini anapokuwa na mafanikio makubwa.
Kila mmoja alivutiwa na sauti ya mrembo huyu na kutamamani waendele kusikiliza. “Huyu ndio Princess wa Wales ,Mtoto wa malkia Catherine Steohanie” Walinong`onezana mabwana wawili kwa lugha ya kijapani wakati huo Profesa Clark akienda kukaa sehemu ambayo iliandaliwa,lakini mwanadada huyu mrembo macho yake yote yakiwa kwa Roma, ambaye alionekana kuanza kuchoka kukaa hapo ndani. Ukweli utofauti kati ya Edna Clark likija swala la uzuri kama utawalinganisha Profesa Clark na Edna wameachana kidogo sana , na kitakachombeba Edna Zaidi ni umbo.
Basi kikao kiliendelea kwa takribani saa moja na nusu jambo ambalo kwa Roma ni kama hakuwa akielewa kile kinachoendelea na kujiamulia kulala zake kwa kujiinamisha kwenye kiti huku akibenua kichwa juu na kufanya koo lake lionekane na hata pale alipokuwa akimeza mate Neema na Dorisi waliokuwa wamekaa pembeni yake walikuwa wakiona misuli ikipishana. Waandishi walikuwepo ndani ya jengo hili refu la kampunni ya Yamakuza na kila kilichokuwa kikiendelea kilikuwa kikinakiliwa kwa ajili ya matangazo na hio ni moja ya mbinu ya kufanya kampuni ambazo zipo katika mfumo wa ‘Trading’ Hisa zao kupanda. **** Edna leo hii alikuwa ndani ya kampuni yake ndani ya ofisi yake huku macho yote yakiwa kwenye chati ya ‘Candlestick’ ya soko la hisa ambayo ilikuwa ikishuka na kupanda . Katika tarakishi yake alikuwa amegawanya sehemu mbili.
Sehemu ya kwanza kulikuwa na chati iliokuwa ikionesha graph ya kampuni ya JR Group na upande wa pili ilikuwa ikionesha chati ya kampuni yake. Utofauti wa hizi graph ni kwamba kuna ambayo ilikuwa ikishuka na kuna ambayo ilikuwa ikipanda , graph ambayo ilikuwa na mstari wa kushuka ni ya kampuni ya JR na hii iliashiria hisa za kampuni hio zikishuka thamanni tena kwa spidi kubwa lakini upande mwingine hisa za kampuni ya Vexto zikipanda thamani kwa siku hio , hali zote mbili zilionekana kumfurahisha sana Edna na alichukua simu yake iliokuwa kwenye meza na kutafuta namba ilioandikwa kwa jina la ATHENA na kisha akapiga. “I think with the ongoing situation you know what to do Amiri?” “Yes! Madam”. “Okay!, look at the Dow Jones Line for today when it get to the lowest point where we intended to, initiate the plan”. “Angalia Mstari wa Dow jones kwa siku ya leo ukifikia point ambayo ndio tumekusudia , Anzisha mpango wetu” “Rest Assured Madam , leave everything to us” “Kaa kwa kutulia Madam , tuachie kila kitu sisi” Sauti ya mwanaume ilisikika upande wa pili , mwanaume ambaye Edna alimtamka kwa jina la Amiri. Baada ya Mrembo huyu ambaye alikuwa akionekana kiprofesheno Zaidi baada ya kuongea na simu yake aliendelea kukodolea macho tarakishi yake na kutabasamu lakini muda huo huo mlango ulifunguliwa na akaingia mrembo Nasra akiwa amependeza kama kawaida huku mkononi akiwa ameshikilia kishikwambi(Tablet). “Boss Taarifa ya kampuni yetu kutoka japani ipo mtandaoni” Aliongea Nasra huku akimpatia Tablet alioshika mkononi na Edna aliichukua na kuangalia picha mbalimbali zikimuonesha Roma na Dorisi wakipeana mikono na wafanyakazi wa kampuni ya Yamakuza. Edna alishindwa kuzuia tabasamu lake mara baada ya kumuona mume wake kwenye picha hio huku moyo wake ukipata kajimsisimko flani hivi ambako mwenyewe ameshindwa kukatafsiri kwani kalisafiri kuwanzia kichwani na kwenda kuishia katikati ya mapaja. “Boss nadhani huu ndio mkataba ambao kampuni imeufanikisha tokea kuanzishwa kwake , shukrani ziende kwa Roma na Dorisi walioweza kupata asilimia kubwa za gawio la Faida”Aliongea Nasra huku akimwangalia Edna. “Hakika Nasra lakini haya yote ni juhudi za kila mfanyakazi wa Vexto nitahakikisha tunaendelea kusaini mikataba mikubwa zaidi na kuipanua hii kampuni duniani kote”.Nasra alitabasamu na kisha akasema: “Nadhani muda si mrefu Forbes watakutoa kwenye nafasi yako ya mwanamke tajiri duniani uliopo na kukupandisha juu Zaidi , kutokana na mauzo ya hisa ya leo yanavyopanda,natamani Madam Rahel angekuwepo hai Edna”Aliongea Nasra huku machozi yakianza kutoka, machozi ya huzuni. “Ni kweli Nasra , unaonekana kummiss sana Mama eti eh?” “Huwezi amini Edna kwenye siku mbili hizi nilikuwa nikimuota kwenye ndoto , nammissi kila siku , wema wake alionitendea kwenye Maisha yangu umemfanya kuwa mtu muhimu sana kwenye Maisha yangu” Edna alitabasamu na kutoka kwenye meza yake na kisha akamsogelea Nasra na kumkumbatia huku na yeye akitoa machozi na walionekana kufarijiana.
Upande mwingine hapa ndani ya jii la Dar kwa upande wa Masaki alionekana mzee Alex akiwa kwenye Runinga huku akiwa na mtoto wake wa kike aliekua ameshikiria simu yake ya I phone akichati huku akiwa si mwenye kuzingatia kile alichokuwa akiangalia baba yake sebuleni hapo kwani alionekana kuwa bize , lakini Ghafla mzee huyu alirusha rimoti kwa nguvu na kuipigiza kwenye Tv iliokuwa ikionesha channel ya Bloomberg , huku taarifa mbalimbali zikiendelea ikiwemo ya kampuni ya Vexto international kusaini mkataba mnono na kampuni ya Yamakuza , lakini pia wakati taarifa hio ikiwa nzuri ,pia kulikuwa na taarifa mbaya ya Kampuni ya JR kutolewa katika mkataba huo na ilionekana jambo hili ndio ambalo lilimkasirisha sana mzee Alex.
“Dadiii…!”Aliita mrembo huyu kwa sauti yake nyororo huku akimwangalia baba yake aliekuwa akipandisha ngazi lakini mzee alimpotezea , mrembo huyu ambaye alikuwa akifahamika kwa jina la Queen alionekana kushangazwa na kitendo ambacho baba yake amekifanya na alijikuta akigeuza macho yake kuangalia kwenye TV hio kubwa ya teknolojia ya OLED na kuona taarifa ambayo ilimkasirisha baba yake na alijikuta akitoa kicheko kwa nguvu. “Masikini Abuu… sijui awamu hii baba atamfanya nini?”
Aliongea mwanadada huyu kwa kufurahi huku akiendelea kuchatika kwa mapozi mara akae uchi mara ajibinue na simu yake hio kubwa na hakuoneskana kuguswa na chochote kilichokuwa kikiendelea kwenye kampuni ya baba yake. Baada ya mzee Alex kuingia kwenye Ofisi yake ndani ya jumba hilo alivuta mtoto wa meza na kisha akatoa Bastora na kuchukua funguo na kushuka chini na kumfanya Queen azidi kushangaa baada ya kumuona baba yake na siraha … alishindwa kuongea chochote mpaka pale baba yake alipotokomea nje na kusikilizia mngurumo wa sauti uliokuwa ukifubaa kwenye masikio yake.. “Hahahahaha…”Lilikuwa ni cheko la kishambenga la Queen. Nini kitendelea ….. usichoke.
SEHEMU YA 48 YA SIMULIZI HII
Baada ya mtiririko wa matukio ndani ya kampuni ya Yamakuza kuisha , hatimae wageni walikuwa wakiagana kila mtu kurejea kwenye majukumu yake na wale ambao walikuwa ni wageni kuondoka na kuendelea na majukumu yao. “Tunaweza kuongea Private Pluto?”Lilikuwa ni ombi kutoka kwa Profesa Clark kwenda kwa Roma na Roma alitabasamu. “Sawa Clark hata mimi ninatamani kuongea na wewe baada ya muda mrefu kutoonana , tuelekeee juu kabisa ya jengo hili nadhani ni sehemu inayofaa” Aliongea Roma huku akiongoza njia na wakati huu Dorisi walikuwa bize na kuagana na baadhi ya watu lakini alimuona Roma na Profesa Clark wakiingia kwenye lift na alishangaa , lakini sio yeye tu pia Neema Luwazo ambaye bado hakuongea neno lolote na Roma aliliona tukio hilo , lakini pia Mori aliekuwa akiongea na Tikayi wote kwa pamoja walimuona Profesa Clark na Roma wakifuatishana na kuingia kweye lift na kila mmoja akabaki na swali hao wawili wamefahamiana lini , kwani muonekano wa Roma ulikuwa wa kawaida sana kiasi kwamba hakuwa tishio lolote kwa jamiii , yaani alionekana kama mkulima alieziotea pesa jana yake na leo kaja kuichanganya kutoa ushamba na matajiri ambao pesa ilikuwa kama marashi kwao na kiasi kwamba hata harufu zao zilikuwa zikitoa marashi ya kidola dola na ki Euro , Euro. “Nilipata taarifa kwa mwanafunzu wangu Ashley umepata mke pluto”Aliongea Profesa Clark aliekuwa nyuma ya Roma wakiwa juu kabisa ya gorofa hili la kampuni ya Yamakuza , kiasi kwamba walikuwa wakiliona jiji lote la Osaka , ni sehemu ambayo ilikuwa ikivuma upepo na kufanya nywele za mwanadada Clark kupepea na kumfunika uso na kwa mapozi alikuwa akizitoa usoni na kuzidi kumfanya kuwa mrembo. Roma aliekuwa amefika mwishoni kabisa wa floor ya ufuniko wa gorofa hii alitabasamu kidogo pasipo kugeuka. “Ndio Clark , nadhani unataarifa kama anafanana kwa kila kitu na Seventeen”. Profesa Clark ambaye alionekana kutofurahishwa na tarifa hio alivuta pumzi na kuzitoa nywele zake ndefu zilizojaaa usoni na kisha kuangalia mgongo wa Roma kwa dakika na hapohapo alifanya maamuzi na kwenda kumkutambia Roma kwa nyuma na kupitisha mikono kwa mbele huku wote wakiangalia upande wa baharini ndani ya jiji hili la Osaka na upepo ukiwa unawapuliza. “Niliishi kwa mateso sana ulivyoondoka Pluto kwenye macho yangu , kila siku nilikuwa mwenye kukuwazia”Aliongea mwanadada huyu huku machozi yakimtoka na kuloanisha suti ya Roma. “Pole sana Clark , lakini ulinipa baraka zote wakati wa kuondoka na tuliagana , kwanini uwe katika hali ya mateso , maamuzi nilioyafanya kipindi kile ndio maamuzi ambayo nitayafanya pia kwa Zaidi ya mara elfu moja,Clark nimeshaachana na kuwa mashine ya kufanyia matajiri kazi kama mtumwa”
Aliongea Roma na hapa kama ungemuona usingedhania ni yule ambaye muda wote alikuwa akionekana kutokuwa siriasi , hapa alionekana Roma ambaye alikuwa na uchungu mkubwa lakini aliekuwa akidhirisha kile anachokiongea kwa muonekano wake wa sura. “Ndio najua, najua uliopoondoka nilikupa baraka zote , lakini moyo wangu haukukubaliana na wewe kuniacha , niliteseka na kuwaza kila siku kuhusu ugonjwa wako kukurudia tena , kwani dawa ambazo nilikupatia zilikuwa ni za kuutuliza tu , uliondoka katikati ya matibabu na katikati ya utafiti wangu wa
kukutafutia dawa, ni kwanini nisiwe na mawazo ilihali umekuwa mtu wa muhimu kwangu mimi na mama yangu Pluto!?” “Kwanza ni tukiachana na hayo ,Catherine anaendeleaje?” Aliongea Roma na wakati huu akiwa washaachiana na walikuwa wote wamesimama upande upande kuangaia upande wa baharini. “Unamkumbuka? ,yeye yupo ni mwenye kutamani kila siku kukutana na wewe kwa mara nyingine , kila siku amekuwa wakunilalamikia kukuhusu kurudi Tanzania”Roma alitabasamu . “Naamini siku moja tutakutana , mpe salamu zangu Clark,sidhani kama tunayo mengi ya sisi kuongea Clark mimi ni yule yule na maamuzi yangu , imekuwa jambo jema kukutana na wewe daktari wangu , umezidi kuwa mrembo” Aliongea Roma na kumfanya mwanadada huyu atabasamu lakini pia kuhudhunika kwa wakati mmoja. “Mimi siku zote nitakuwa mwenye kuwa upande wako kwa kila maamuzi utakayo yafanya Pluto”Roma alitabasamu na kumgusa shavu kwa namna ya kuliminya “Okey! Clark nadhani ni muda wangu sasa wa kurudi chini , Dorisi mfanyakazi mwenzangu atakuwa ananisubiri , kwasasa nafahimika kwa jina jipya la Roma unaweza kuniita hivyo tukionana kwa mara nyingine , kwaheri Clark msalimie malkia Catherine” Aliongea Roma na kisha akageuka kuondoka . “Wait..!!” Aliongea clark na kumsogelea kwa mara nyingine Roma na kisha alitoa Pentorch(Kalamu za mwanga wanatumia sana madaktari) iliokuwa kwenye koti lake la suti ya rangi ya bluu na kumsogelea Roma kwa mbele. “Naomba angalau nione macho yako”Aliongea na Roma aliitikia kwa kichwa na kisha mwanadada huyu alimmulika kisha akabonyeza maratatu ile pentorch kwa kila jicho. “Hii ni teknolojia mpya ya kuscan Nevu(nerve) ambayo nimeitengeneza , inaweza kunisaidia kujua kwa sasa hali ya ugonwa wako nitaenda kuzichambua picha nilizozipiga hapa” Aliongea na kisha aliingiza mkono kwenye mfuko wa koti na kutoa mkebe mwingine na kumpatia Roma.
“Humo ndani kuna dawa mpya ambazo nimefanikiwa kuzitengeneza , kama utahisi tatizo lako kukurudia jaribu kumeza , tukikutana kwa mara nyingine nitakupima na kujua kama zinafanya kazi kwa ufanisi” “Asante sana Clark kwa kunijali , unaonekana ulikuwa ukitembea na dawa zangu muda wote kwenye koti lako kwa kuamini tunaweza kukutana”Roma alionekana kuguswa na matendo ya mrembo huyu. “I just Could `nt help my Self Pluto , this is how I relieve my worries , I told my self we will meet again even by chance and here we are”(Sikuweza kujisadia mwenyewe Pluto , hii ndio ilikuwa namna nilivyokuwa nikipunguza wasiwasi wangu , nilikuwa nikijiambia ninaweza kukutana na wewe kwa bahati mbaya na leo imetokea) “Clark you are good woman whom I had ever know in my life and every act of your kindness has a lot of meaning to me ,Thank you So much and goodbye”(Clark umekuwa mwanamke mwema kwangu sana ambaye nimewahi kukutana nae kwenye Maisha yangu na kila tendo la kikarimu unalofanya linamaana kubwa sana kwangu ,
Asante sana na kwaheri) Aliongea Roma na kisha akaondoka na kumuacha mwanadada huyu akiangalia kivuli chake kinachotokomea kwenye macho yake na alijikuta akipeleka mkono kwenye macho yake na kufuta machozi ambayo hakujua yameanza kumtoka , huzuni aliokuwa nayo huyu mwanadada ni kama vile hatomuona tena Roma , haikueleweka ni hisia gani za huyu mwanadada anazo juu ya Roma. ***** Mzee Alex alionekana kuwa ni mwenye hasira sana , alikuwa akitweta huku akitoa jasho , hakuamini dili kama hilo kampuni yake imeshindwa kulipata , hakuelewa ni kitu gani abuu anakifanya huko Japani mpaka kukosa dili kubwa kama hilo , aliapia kwa majina yote ya ukoo wake Abuu akirudi lazima amtandike risasi. Alimfikiria Abuu kama toto jinga ambalo halikupaswa kupewa nafasi kubwa katika uongozi wa kampuni , kiasi cha kwamba aliamini huenda angempa mtoto wake mkubwa wa kike nafasi hio huenda angeleta mabadiliko makubwa. “Abubakari ni mjinga sana , kashindwaje kusaini mkataba mnono kama ule na kumuachia Edna , anajua ni kiasi gani gepu ambalo lipo kwasasa baada ya kampuni yetu kukosa hilo dili na Edna kulipata ,, sh**t huyu mtoto nikimuacha hai labda sio mimi Alex , labda asirudi na anabahati hata kazima simu ningemtukana mpaka matusi ambayo hayajavumbuliwa bado” Alijiongelesha maneno yasio na mpangilio kwa sauti huku akigonga stering ya gari wakati likiendelea kuwa katika mwendo, na wakati huu alikuwa akipita Kongowe na kuchanja mbuga na ndani ya madakika kadhaa tu alikuwa ashafika sehemu aliokusudia na kukata kushoto na Range yake kuingia kwenye barabara iliokuwa na rami lakini iliokuwa imependezeshwa na miti midogo ya miarobaini iliopandwa kwa mstari pembezoni mwa barabara na kufanya eneo hili lipendeze. Baada ya kutembea umbali wa mita chache tu alikutana na kizuizi cha geti na kusimammisha gari na alitoka askari aliekuwa ameshikilia SMG na baada ya kumuona ni mzee Alex alitingisha kichwa chake kwa heshima na kumruhusu. Naam hapa ndio anapoishi mheshimiwa mstaafu Kigombola , sehemu ambayo ilikuwa ikifahamika kwa jina la Village G , ni sehemu ambayo ilijaa ufahari kuanzia mazingira mpaka nyumba. Mheshimiwa huyu alionekana alipenda muundo wa jengo la ikulu ya Dar kwani , hapa ndani palikuwa pakifanana san ana ni kama injinia aliejenga hapa ndani alikopi tu muundo na kujenga ,hivyo hii sehemu ni sahihi kusema ni kopi ya ikulu, mheshimiwa kigombola alionekana kupenda ‘vibe’ la ikulu. Baada ya Mzee alex kuegesha gari alitoka moja kwa moja , huku siraha yake ikiwa kiunoni bila ya kuonekana. Baada ya kuingia kwenye sebule kubwa iliokuwa ndani ya jengo hili , sebule maalumu kwa ajili ya maongezi ya mheshimiwa Kigombola na wageni wake ,Mzee Alex alijikuta akishangaa watu waliokuwa hapo ndani na ghafla tu akachomoa Bastora yake na kuikoki. “Baba….Babababa .. naomba unisamehe .. babba najua nimeboronga.. lakini naomba unisameh…aaa”Alikuwa ni Abuu aliekurupuka mara baada ya kumuona baba yake mlezi, haikueleweka alikuwa amefika saa ngapi nchini na hapo ndani. Kila mtu alishangazwa na kitendo cha mzee Alex kutoa siraha , waliokuwa hapa ndani walikuwa ni Abu , Mheshimiwa Kigombola ,Elvice Temba , mzee Temba mwenyewe ambaye alikuwa ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma , alikuwepo pia Meya wa jiji la Dodoma mzee Abubakari Juma lakini pia kiongozi mkuu wa kundi la Black Mamba . “Alex hebu punguza jazba… weka siraha chini tupo hapa kwa ajili ya kujenga sio kubomoa , acha kuonesha udhaifu mbele ya kila mtu” Aliongea mheshimiwa Kigombola kwa hasira na muda ule ule tu Aliingia kwa kitaalamu kabisa mlinzi wa Kigombola wa kike na kubetua siraha na ikadodokea mikononi kwake na kumpiga Roba Alex. “Scorpion , unaweza kumuachia” Aliongea Kigombola na Scorpion aliekuwa amempiga Roba mzee Alex alimuachia , lakini ni kama Alex alifunguliwa kwani alimkimbilia Abu na kuanza kumpiga mangumi na Abu ambaye alikuwa amepiga magoti alijikuta akidondoka chini , lakini mzee Alex hakuacha aliandelea kusindilia mateke , ngumi , Scorpion alitaka kuingilia lakini Mzee kigombola alimpa ishara asifanye chochote.
Abuu alipigika na mpaka damu zikaanza kumtoka ndipo mzee Alex alipomuachia huku Abuu akilia kama mtoto. “Mzee Alex kama hasira zako zimepungua unaweza ukaketi tukaongea tuyajenge sasa , sio muda wa malumbano sasa , mwenyewe sijapenda yalitokea huko Japani , lakini hata kama ni wewe usingeweza kumdhibiti Roma.” Aliongea Kigombola na mzee Alex alionekana kupoa kidogo na muda huo huo aliingia mhudumu na kumpa glasi ya maji na akayanywa yote kwa pupa na kisha akasogelea sofa na kukaa. Ilionesha Abu alikuwa ashahadithia kila kitu kilichotokea huko Japani mpaka kujikojolea kwake na sasa Kigombola alikuwa akimpasha habari kwa ufupi ya kile walichoambiwa na Abu. “Niseme tu hata mimi naelewa Roma sio mtu wa kawaida , nimejaribu hata mimi kufukunyua kupata taarifa zinazomuhusu Roma lakini sikufanikiwa , badala ya kupata taarifa inayoonesha , alikuwa akiishi nchini Marekani kabla ya kuja hapa Tanzania na inasemekana nchini Marekani alikuwa akilelewa na moja ya matajiri wakubwa , jimbo la Michigani , Tajiri mmoja anefahamika kwa jina la Robert Eglon”Aliongea Kigombola.
“Hata kama sio wa kawaida , tunashindwaje kumuua mtu mmoja watu wote sisi na nguvu yote tulionayo , tunaachaje mtu mmoja aharibu kila kitu tulichokijenga kwa miaka”Aliongea Mzee Alex na Mstaafu kama kawaida yake aliachia tabasamu. “Alex kwenye vita ili uwe na uhakika wa kushinda mbinu ya kwanza ni kujua adui yako anauwezo wa namna gani , huwezi kwenda kichwa kichwa utashindwa , na sisi kusema Roma sio wa kawaida ni swala la kuutambua uwezo wake , lakini haimaanishi tumeshindwa”
Aliongea na kisha alimimina maji kwenye glasi na kunywa kidogo na akageuka na kuwaangalia kila mmoja hata Abuu ambaye alikuwa akimwangalia baba yake kwa woga. “Mpango mzima wa Yamakuza mpaka sasa tuseme umefeli kwa asilimia mia moja na tumezidiwa akili , lakini haimaanishi kwamba tumeshindwa , Roma ni kama nzi kwetu na cha kufanya ni kuitega na viganja viwili na kisha kuimaliza”
Kila mmmoja alimwangalia mzee wa mipango bwana mstaafu kwa kumtaka endelea kuongea Zaidi. “Najua wote mnaelewa The Doni alikuwa ni mtu ambaye siku zote ni mwenye kutaka upatikanaji wa ‘Safe Root’ katika biashara zetu na niwaambie tu , hilo swala lazima lifanikiwe na hakuna njia nyingine ,Vexto ni kama zao la mkulima aliepanda mbegu njiani na hakuna budi kwa wapita njia kukanyaga na kutengeneza njia”
“Kwa hio mhesimiwa nini kifanyike?” “Nadhani kila kitu kipo kwenye mipango Bakari , kwani mpango B wenu mliopanga ulikuwaje?” “Mpango B ilikuwa ni kumua Roma na Edna siku ya kusanyiko la wafanyabiashara” “Nadhani tuendelee na mpango huo huo cha kufanya tu ni kwamba mpango huu tunatakiwa kuongezea nguvu ili uwe na asilimia kubwa za mafanikio” Kila mmoja alishangaa lakini
mheshimiwa alitabasamu na kisha akamgeukia mlinzi wake. “Mwambie aingie” Mlango ulifunguliwa na hapohapo akaingia bwana ambaye aliwafanya kila mtu kugeuza macho na kushangaa. Make kwa kutulia nitaleta muendelezo saa nne kamili usiku , kama huwezi kusubiria lala utaukuta asubuhi………….SINGANO JR
SEHEMU YA 49 YA SIMULIZI HII
Chapisha Maoni
TOA MAONI YAKO HAPA