51 - 55
NILIEMDHANIA KAHABA KUMBE NI BIKRA
SEHEMU YA 51
Upande wa Chini kabisa ndani ya Mashua, kwa nje kabisa alikuwa amesimama mzee mmoja hivi aliekuwa ameshikilia panga lake Refu akiwa anaangalia Chopa iliokuwa hewani , mzee huyu alionekana kutokuwa na wasiwasi kabisa , alikuwa amevalia mavazi ya kitamaduni ya kichina huku akiwa na kipara chake, alikuwa na macho flani hivi ya kutisha kama ana makengeza na mboni za macho hazikuonekana ni rahisi kusema anajicho lisilokuwana kiini cheusi..
Ndani ya mashua hio walionekana vijana wanne hivi wote wakorea waliokuwa wameketi kwenye visturi huku wakinywa kilevi ambacho kilikuwa kikifanana na ulanzi , huku pembeni yake kukiwa na Sanamu Varicana ambalo walikuwa wamelifunika na nguo.
Upande wa kushoto ndani ya mashua hii kulikuwa na maboksi flani ya mbao , kama yale ya kuhifadhia Nyanya wakati wa kuzisafirisha kutoka shambani , chakushangaza ni kwamba maboksi hayo yalikuwa yakitingishika na nikama kulikuwa na mnyama ndani ya maboksi hayo na watu hawa hawakuwa wakijali sana kutingishika kwa maboksi waliendelea kunywa kwa furaha huku wakiongea , lakini muda huohuo ndio walipoanza kusikia mngurumo wa Chopa na wote kwa pamoja walikurupuka na kubeba Bunduki zao na kutoka nje haraka na walimkuta kama kawaida Tzeng akiwa anaingalia ile chopa huku akionekana ni mwenye kukata tamaa , ni kama mtu ambaye alikuwa akisubiria kitu kikubwa Zaidi na hakijatokea. “Master Tzeng”Aliita kijana mmoja wa kikorea huku akimwangalia Monk kwa wasiwasi. “Mtu ninaemsubiria hayupo kwenye hio chopa , naona wale makafir wamenidanganya,imenika tisha moyo , walitaka kunitumia tu kukamilisha mambo yao ,Inasikitisha sana”Aliongea Tzeng.
“Master lakini haujatuambia unaemsubiria kila siku umekuwa wakutuambia kuna mtu unaemsubiria”. “Unafikiri kwa miaka yangu yote niliohudumu kusalia Budha ninaweza kuisaliti huduma yangu kuja kuiba sanamu,Nimewakubalia Dhoruba Nyekundu kuiba hilo sanamu kwasababu wamenihakikishia nitapata nafasi ya kupambana na Hades ,Inasikitisha sana” “Master Hades ni nani?” “Huna haja ya kumjua , kwangu ni mtu ambaye natamani kuupima uwezo wangu wa kimapigano kwa kupambana nae , lakini nimekatishwa tamaa na kutoonekana kwake, nahisi sitoweza kuufamu uwezo wangu wa kimapigano mpaka nakufa inasiikitisha sana”.
Upande wa Chopa kule juu wakati wakiendelea kushangaa chini baharini kama watamuona Roma , Mara walijikuta wakianza kushambuliwa kwa mbele. “Sh**t Ni ni kikosi cha watu wa Dhoruba Nyekundu washafika, Kapteni kuwa makini wasiharibu chombo”. “Pumbavu tulishindwaje kuwagundua wamekaribia? , Boti yao ile” “Sio Boti wewe mpuuzi , ile ni SubMarine(Manuari)”Alion gea Kobota akimrekebisha Mbwa
Mwitu , lakini wakati huohuo lilirushwa kombola na ilibakia kidogo tu ligonge Chopa yao na Rubani alionekana kuwa mtaalamu kweli , kwani aliipindisha Ndege na kugeuza kushoto, mashambulizi yalikuwa makali sana na watu wa Dhoruba Nyekundu walionekana kudhamiria kuidondosha kabisa hio chopa. “Bang .. Bang !!”Ni milio ya risasi iliokuwa ikigonga chopa huku na waliokuwa kwenye ndege wakirusha Risasi. “Hawa wajamaa wanateknolojia kubwa ndio maana ndege yetu imeshindwa kuwanasa kwenye Radar, tusipokuwa makini hii misheni itafeli”Aliongea Rubani msaidizi kwa kijapani. “Sema Pluto naamini ashakufa mpaka sasa , niliwaambia hana lolote yule, na nimeshangaaa kumuhusisha kwenye hii misheni”Aliongea Kibonge huku akimdharau Hades na hio ni kutokana zimepita Zaidi ya dakika tano bila ya kumshuhudia Roma. “Mother***cker!” Rubani alijikuta akitoa tusi mara baada ya kurushiwa Kombora kiasi kwamba Chopa ilianza kutoa mlio wa Alarm lakini ile anataka kulikwepa kwenda kulia , wa kwanza kuruka alikuwa ni kibonge , alionekana kuwa shapu na akafatia Kobota na
Mbwa mwitu na hapohapo ulisikika mlio wa ‘BOOM’ Chopa ilikuwa imelipuka ikiwa na Sunami na Rubani msaidizi Jani , ulikuwa ni mlipuko mkubwa uliosababisha mwanga kutawala kwa sekunde kadhaa mpaka kufifia huku mabaki ya ndege yakidondokea baharini. “Haya yote hayana maana ,Inasikitisha sana”Aliongea Tzeng baada ya kuona mlipuko wa ndege , lakini ile anageuka tu Roma alietoka kwenye maji kama samaki jamii ya Dolphin ,kama mshale huku akijilenga kwa Tzeng , lakini Tzeng alikuwa mwepesi mno kwani aliinama chini kama mti ambao umepindishwa na kichwa kugusa chini huku miguu haijasogea hata kidogo , yaani ni kama mti ulikuwa umechomekwa kwenye shimo na ukapindishwa na Roma akapita na kumvaa kijana aliekuwa akiuliza maswali na akaenda kudondokea baharini . “Amitabha.. Hades”Aliongea Mzee huku akikunja mikono miwili , alionekana kushukuru ujio wa Hades. “Inashangaza kuona Monk kuwa mwizi”Aliongea Roma.
“Kuna Muda inapaswa kuwa hivyo , kama unania ya kutimiza dhumuni kuu kwenye maisha yangu”Aliongea huku wale Wakorea wakiwa wamemzingira na Bunduki zao ila Roma hakuwa ni mwenye kuwajali. Wakati huo huo ile Submarine(Manuari) ilikuwa ishafika usawa wa mashua na walikuwa wakimshuhudia Tzeng na Roma waliokuwa wakiangaliana. “Jason ni Hades , inapaswa kuchukua Sanamu tuondoke wakati akiendelea kupambana na Tzeng” “Jessy tulia kwanza tuone mtanange , tukiona dalili za kushindwa kwa Tzeng tunakimbia , ila waambie vijana waingie kwenye mashua wachukue mzigo ”Aliongea Jason wakati huu chombo chao kikiwa Upande wa Kibonge alionekana kusalimika hukuu akiogelea upande wa ilipokuwa mashua ,aliangalia nyuma na kuwaona wenzake pia wanatapatapa kwenye maji. “Okey!Tzeng nataka nikamuokoe mpenzi wangu,kwasababu umeshindwa kutumikia Budha na kugeukia njia Ovu nikikuua nitakuwa nimefanya jambo la kiimani kwa Mungu wa Budha”Aliongea Roma.
“Bothisativa Sabejatha” Alitamka Tzeng huku akimnsogelea Roma akiwa amenyoosha upanga wake , akilenga tumbo na Roma hakuondoka alipokuwa amesimama na ile Tzeng anafika Roma alisogea kidogo na Upanga ukapita kwenye kwapa , lakini Tzeng alionekana kutumia nguvu isiokuwa ya kawaida , kwani alimsukuma Roma na wote walitumbukia kwenye maji huku wakiwa katika staili kama ya kukumbatina ,Tzeng baada ya kutua kwenye maji mita kadhaa chini kabisa , alimsukuma Roma na kujitoa kwake na kisha akaleta tena pigo huko akizungusha upanga wake kwa spidi kiasi kwamba ulikuwa ukionekana kama sinndano na ile anamfikia Roma kwa nia ya kumchoma Roma aliuzuia na viganja vya mikono kwa kuubana , kitendo ambacho kilimfanya Tzeng
kuuvuta ila Alishindwa na kujikuta akishangaa ni uwezo gani wa nguvu za mikono za Roma, lakini ile anashangaa Roma aliruka sarakasi na miguu ikawa juu na mikono ikiwa chini imeshikilia lile panga na kisha akazunguka kama pia kitendo kilichomfaya Tzeng kukosa mhimili wa kushikilia lile
Panga,Baada ya Tzeng kuona Roma anazunguka na yeye alizunguka vilevile kwa spidi kiasi kwamba Jason ,Jessie ,Kibonge na wenzake kushangazwa na Wimbi lililojitengeneza sehemu ambayo wametumbukia. ****
ATLANTIC OCEAN- ISLAND X PROJECT LADO MONITORING CENRE(PLMC)
Ni ndani ya kisiwa ambacho kilipewa jina la Kisiwa X,kisiwa hiki kilipewa jina hilo kutokana na kwamba kimetolewa kwenye Ramani , yaani ni kisiwa , lakini kwenye Ramani ya dunia hakionekani na ndio maana kikapewa jina la Kisiwa X.ni kisiwa ambacho kipo kwenye bahari ya Antlantic. Ni sehemu ambayo ina ulinzi mkubwa sana kiasi kwamba kama upo habarini kilomita 60 kutoka ndani ya kisiwa hiki utaona Bango kubwa lenye maandishi ya
DON’T GET CLOSER ,ITS DANGEROUS yalioandikwa kwa Rangi nyekundu kuzunguka eneo lote la kisiwa ,ni sehemu ambayo inabaridi kali sana na mkondo mkubwa wa maji na ni mara nyingi kuona meli zinapita karibu na eneo hilo na kama itatokea mtu akifika kwenye eneo hilo ni ngumu sana kutoka hai. Ndani ya eneo hili la kisiwa kuna jengo ambalo kwa juu linaonekana kama kibakuli kilichofunikwa, na jengo hilo lina rangi nyeupe huku pembezoni mwa jengo hili kukiwa na Bendera zinazopepea za mataifa ishirini, ambazo zimepangiliwa kwa umbali sawia kiasi kwamba zilifanya jengo hilo kupendeza. Basi ndani kabisa ya jengo hili ndani ya hiki kisiwa , walionekana watu wanaume na wanawake walio na utofauti wa umri ,yaani kuna wale ambao walionekana kuwa na miaka hamsini na kuna wale ambao walikuwa na miaka Therathini kimakadirio , hapo ndani hapakuonekana mtu ambae yuko chini ya miaka ishirini. Watu hawa wote walikuwa wamevalia tisheti za rangi ya Bluu huku kila mmoja ikiwa na chata la ‘O’ na jicho katikati ambalo limenakishiwa kwa rangi nyekundu, halafu chini ya tisheti hio kuna maneno yanayosomeka Zero`s Organisation.
Ni jengo ambalo kwa ndani lilikuwa limejengwa kitaalamu sana , jengo hili lilikuwa limetenganishwa mara mbili upande wa kulia kuna vyumba ambavyo vimejengewa kwa mfumo wa nusu duara , lakini pia kwa upande mwingine kuna vyumba ambavyo vimejengwa kwa mfumbo wa nusu duara huku katikati pakiachwa wazi huku juu yake kukiwa na paa ambalo lilikuwa likipitisha mwanga na matundu ambavyo yametengenezwa kwa muundo wa nyota. Ukiachana na hili jingo kwa pembeni yaani nje kabisa kulikuwa kumejengewa pia nyumba ambazo zilikuwa kwenye muundo tofauti tofauti ,zilizofanya eneo hili kupendeza sana ukijumlisha na bustani zilizokuwa zimetenezwa kwa muundo wa kuvutia. Sasa ndani ya hili jengo kuna Idara inayofahamika kwa jina la PLMC(PROJECT LADO
MONITORING CENTER), ndani ya hii idara walionekana jumla ya watu kumi na mbili , watano wanawake na saba wanaume wenye umri tofautt tofatui , ndani ya hii idara mbele kabisa kuna ukuta mkubwa ulionjengwa huku ukiwa na skrini kubwa ambayo ilikuwa ikionesha eneo la baharini , lakini ajabu ni kwamba mazingira yanayoonekana ndani ya hili eneo ni yale yale
ambayo Roma na Tzeng wakipigana. “Unafikiri Agent 13 atashinda Carlos?”Aliuliza
mwanamke mmoja wa kizungu makadirio ya miaka hamsini hivi kupanda ambaye alikuwa akila Popcon zake zilizokuwa kwenye kopo bila habari huku akiangalia mpambano kati ya Roma na Tzeng , mwanamama huyu alikuwa amekaa huku pembeni yake kulikuwa na bwana mmoja mweusi kijana, akiwa amekaa pamoja na mwanamama anaekula Popcorn huku nyuma yao wakionekana wenzao ambao wamesimama
wakiwa wanangalia mtanange huo , kwa jisi walivyo makini ni kama walikuwa kwenye ukumbi wa sinema wanaangalia muvi. “Sina mashaka na Agent 13 Dyana, Tzeng ni mtu ambaye ana mafunzo ya juu na ndio maana tukamchagua kupambana na Agent 13 lakini haimaanishi kama anaweza kushinda ni uwekezaji mkubwa na maarifa yaliofanyika kumtengeneza Agent 13 na hatakiwi kushindwa na Tzeng”Aliongea bwana huyu aliefahamika kwa jina la Carlos huku akirudisha umakini wake kwenye pambano. “Sema Agent 13 tokea Agent 17 kufariki ukatili wake umepungua kwa asilimia mia moja ,nadhani mpango wa kumuua Agent 17 ulikuwa bora sana”Aliongea mwanamama huyu lakini bwana Carlos hakujibu.
SEHEMU YA 52
Ilikuwa ni kama kimbunga Jobo kilichokuwa kimejitengeneza ndani ya hili eneo kiasi kwamba ile mashua na Manuari pamoja na wanajeshi wa kikosi cha Dragoni walisukumwa mbali. “Ni nguvu gani hii?”Aliongea Kibonge huku akiendelea kushangaa , kilichowashangaza Zaidi ni kwamba zilipita dakika kumi pasipo ya Roma na Tzeng kuonekana juu ya maji , ikimaanisha kwamba walikuwa wakipigana chini ya maji.
“Mbwa Mwitu kimbia..!”Aliongea Kobota baada ya kuona tukio la kutisha na hio ni mara baada ya eneo wanalopigana Tzeng maji yake kutengeneza barafu kwa spidi kiasi kwamba sehemu waliokuwa wamesima Kobota kuhisi ubaridi wa hali ya juu sana na maji yalikuwa yakigana kuelekea upande wao na kuwafanya waogelee kwenda kusimama mbali.
“What is happening?”Aliuliza Jessie kwa mshangao baada ya duara la Barafu kujitengeneza . “That is Hades Jessie , I told you we have to stay here to enjoy this live show”A;iongea Jason akiwa amekalia ukingo wa Manuari yao ambao ilikuwa imefungua ufuniko kwa juu , licha ya kwamba walikuwa wakisikia barindi kali lakini hawakutaka kuondoka , walitaka waone mpaka mwisho wake. Wakati wakiendelea kuongea Ghafla katikati ya lile barafu paliachia mpasuko wa nguvu kiasi kwamba kurusha vipande vya mabarafu juu na Tzeng Alionekana akichomoka kama mshale lakini wakati huo huo Hades na yeye alitokea , lakini sasa muonekano wa Roma uliwafanya kila mtu kushangaa… “It`s yellow Glows not what I wanted to experience Jessie ,Tzeng is Disapointing”Aliongea Jason na kumfanya Jesie ashangae.
“What do you mean?” “When his eyes emit Yellow glows mean he is using half of his power , I need to see red glows Come on Tzeng” Jesie alizidi kushangaa,huku Jason akionesha kutofurahishwa na uwezo wa Tzeng kwani alitegemea kuona macho ya Roma yakitoa mwanga mwekundu. Roma Macho yake sasa hayakuwa ya kijani tena kama alivyokuwa amezeleka hapa macho yake yalikuwa ya njano huku yakitoa miale flani hivi kama mwanga wa jua lakini usio kuwa mwingi, kiasi kwamba haukuwa ukisambaa , na kutokana na eneo hili kuwa na giza alionekana vyema. “Tzeng huna uwezo wa kunishinda , ikibidi kimbia kabla sijakufanya ukose hewa ya oksijeni”
Aliongea Roma kwa sauti nzito kama Roboti kiasi kwamba watu waliisikia mara mbili kwenye masikio yao kwani ilikuwa na mwangwi, huku Tzeng akionesha wasiwasi wake , ukweli ni kwamba Tzeng aliponea chupuchupi chini ya maji, kwani wakati wakiendelea kupigana Macho ya Roma yalikuwa yakitoa miale ya kijani kiasi kwamba bwana huyu aliogopa kubakia chini ya maji na akataka akimbie , lakini ni kama Roma alijua mawazo yake , kwani alikimbia juu yake na kisha kujikakamua kama mtu ambaye anataka kulazimisha ushuzi na hapohapo na mwili wake ulibadilika Rangi nangi na kuwa kama sanamu ambalo limejengwa kwa barafu huku likimomonyoka kama unga kwa spidi kubwa kiasi kwamba eneo la juu ndio lilianza kutengeneza barafu na hapa ndipo alipoweza kujua kuwa mtu ambae alikuwa akipambana nae hakuwa wa kawaida , yeye katika kusikia kwake kuhusu stori za Hades ni kwamba alikuwa na uwezo wa hali ya juu wa ‘Martial Art’ pamoa na mbinu za kichawi za kichina Lakini hakuwahi kuwaza kama anaweza kugandisha maji.
“Shi*t he is using power to control Density , I can’t Move”Aliwaza Tzeng huku akiwa amejawa na kiwewe. Sasa kile kitendo ch Hades kugandisha maji kwa juu kilimfaya ashindwe kutoka juu na pia Pumzi ilikuwa ikimuishia na aliona akizembea anakufa kizembe na hapo ndipo alipoamua kutumia uchawi wake ambao ulimuongezea nguvu kiasi kwamba alikuwa akisukumwa kutoka chini kwenda juu kwa spidi ya hali ya juu na kuweza kutoboa barafu na upanga wake na kutokezea nje.
“Hapa inabidi nikimbie , huyu sio mtu wa kawaida nitakufa ,Ngoa nikajipange upya nitaomba mpambano tena”.Aliwaza Tzeng wakati akiwa amesimama kwenye barafu iliotengenezwa na Hades huku ikielea juu juu. “Hades tutakutana tena ngoja nikajipange upya”Aliongea Tzeng na palepale aliposimama pakajitengeneza vitu kama majivu na vikapelerushwa na upepo kuelekea magharibi.
Baada ya Tzeng kukimbia Roma mwili wake ulianza kurudi katika hali ya kawaida , lakini sasa nguo zake zote zilikuwa zimechania yaani zilijiachia kama unga na kubakiwa uchi. Jasona baada ya kuona Tzeng kashindwa pambano waliona hapo sio mahala pake kukaa ,kwani wote waliingia kwenye manuari na ikaanza kuzama chini na kukimbia. “Jasona , hatujachukua sanamu”Aliongea Jesie. “Sanamu la nini?” “Kwani tumekuja kufanya nini?” “Jesie acha kuwa na kichwa kigumu , unafikiri tumekuja kuiba sanamu ambalo halina tnamani kwetu” “Kwa hio tumekuja kufanya nini?” “Kurusha pambano live , ndio ilikuwa misheni yetu Jesie”Aliongea Jason . Kibonge hakutaka kabisa hata kumsogelea Roma , kwa matukio ambayo alikuwa ameyashuhudia kwa macho yake ni kama alikuwa kwenye ndoto ,alimwangalia Roma ambaye alikuwa amesimama kwenye
mashua hii akiwa uchi sehemu ambayo alikuwa amesimama Tzeng kabla ya pambano lao.
SEHEMU YA 52 B.
Wale wakorea ambao walikuwa wapo pamoja na Tzeng baada ya kumuona Master wao kakimbia na wao walijirusha majini bila kujiuliza mara mbilimbili , mziki walioushuhudia kutoka kwa Roma waliziambia nafsi zao ni heli kujaribu kufia kwenye maji kuliko kuliko kukutana na adhabu ya shetani aliekuwa mbele yao.. Roma licha ya kwamba eneo hili la baharini kuwa na baridi kali kiasi kwamba kwa mtu wa kawaida ambaye hajazoea baridi anaweza kuzimia , lakini kwa Roma ni kama alikuwa amevaa nguo. Mbwa mwitu alikuwa amesimama nyuma yake , kwenye boti , huku akimwangalia Roma kwa wasiwasi mwingi , kila akifikiria tukio ambalo limetokea dakika chache zilizopita , hakuwa akiamini kama mtu ambae amesimama mbele yake ndio alieweza kufanya yote hayo , zile dharau alizokuwa nazo zilikuwa zishaisha na sasa kilichokuwa kimebaki kwenye akili yake ni woga na hali ya kutokujiamini kila anapomuangalia Roma. “Nilikuwa nikizisikia habari za Hades lakini sikuwa nikijua uwezo wake upo hivi”Aliongea Kobota mara baada ya kumsogelea Mbwa mwitu , muda huu wote wakiwa ndani ya boti hii. “Nimeshaangazwa sana na kilichotokea dakika chache zilizopita Kobota huyu sio mtu”
“Kwani nani kasema ni mtu , wewe hujamsikia kampteni anamwita Mungu wa wafu?” “Nilijua ni jina tu Kobota kama mimi ninavyoitwa Mbwa Mwitu”. Kobota alitabasamu na bila kungea chochote alimgonga gonga begani Mbwa mwitu kama kitendo cha kumfariji na kisha akarudi ndani. Baada ya Roma kusimama muda mrefu akiwa uchi aligeuka na kuanza kutembea na kuingia ndani ya chumba cha boti hii , huku akidhamiria kutafuta nguo kwa ajili ya kujisitiri.
Licha ya kutafuta kwakuchangua maboksi yaliokuwa kwenye hii boti hakuambulia chochote Zaidi ya kuona vitu ambavyo wale wakorea wameviiba,ni vitu ambavyo vilikuwa na thamani kwani kulikuwa na baadhi ya vifaa vya udongo ambavyo alipovichunguza kuna vilivyokuwa ni vya miaka mingi,ikiwemo uwepo wa ‘Porcelain’ ya ‘Song Dynastry’ na makolo kolo mengine Roma baada ya kuona amekosa alirudi na kuungana na Kobota na Mbwa Mwitu waliokuwa wamekaa sehemu ile ile ambayo wale wakorea waikuwa wakinywa na kuongea , lakini kabla hajakaa chini kuna kitu kilimvutia, yalikuwa ni maboksi ya mbao mawili. Aliyasogelea na kuanza kuyasukuma kwa mguu lakini yalikuwa mazito, Kobota na wenzake walikuwa wakimwangalia Roma kwani hata wao waliona hayo maboksi lakini hawakua na habari nayo , ni kama watu ambao walikuwa wamekosa na hamu ya kila kitu kutokana na kuponea chupuchupu kwenye kudunguliwa na ile Chopa na sasa walikuwa wakifikiria kurudi nchi kavu tu. Roma baada ya kuona maboksi haya kuwa mazito , alibeba moja na kuligeuza kwa juu na kisha akafyatua kimlango ambacho kilikuwa kimegongelewa na chuma na hapo ndipo alipojikuta akishangaa , kwani ile anafungua tu boksi ,ulitokea mkono uliokuwa kwenye hali ya ulegevu na hapo ndipo alipojua kuwa ndani ya hayo maboksi kuna watu amba wamefungiwa. Hata Kobota na wenzake walishangazwa na jambo hilo na walisimama na kumsogelea Roma. Walikuwa ni wasichana wawili mmoja Mjapani na mwingine alikuwa ni muafrika kutokana na ngozi yake ,wasichana hawa walionekana kuzimia kutokana na baridi kali na kuelekea mpaka midomo yao kupasuka pasuka na kutengeneza nyufa.
“Wamepoteza fahamu , wanaonekana kuwa hai”Aliongea Roma kwa kijapani na kufanya Kobota na mbwa mwitu waangaliane na kisha kumgeukia Roma kwa mshangao. “Hades tunapaswa kufanya nini kuwaokoa?”Aliuliza Kobota na Roma hakujibu chochote na kuinama huku akimwnaglaia yule mwanadada mwenye rangi ya chocolate ya kiafrika, baada ya kumwangalia kwa dakika aliweka mkono wake kwenye kifua cha yule mwanadada na kisha akafumba macho. Kobota na kibonge walikuwa wakijiuliza Hades anafanya nini , lakini walitulia kuona mwisho wake , lakini ndani ya dakika kadhaa , walihisi joto kiasi na kumkazia macho Hades.
Roma alimuwekea mwanamke yule mweusi kiganja kwenye moyo na kisha akahamia kwenye uso kwa dakika kama tano hivi, na kilichotokea kiliwaacha kobota midomo wazi , kwani ngozi ya yule mwanamke iliokuwa imepauka ilirudi kama kawaida , licha ya kwamba alikuwa bado hajarejewa na fahamu lakini alionekana kuwa na afadhari kuliko alivyokuwa mwanzo. “Hii ni ‘Endless Resolve restoration Energy’ nimejaribu kumuingizia na haitamchukua muda mrefu kurejewa na fahamu”Aliongea Roma. Kobota na Mbwa mwitu waliangaliana kwa mshangao huku wakionekana kutoelewa kile ambacho Roma ameongea na Roma
hakuwajali , alijua hawajaelewa ,alimsogelea na yule mwanadada wa kijapani na kisha akamuwekea kiganja cha mkono kwenye moyo na kisha akahamia kwenye uso na tumboni na ndani ya dakaika tano na yeye mwili wake ulionekana kurejea katika hali ya kawaida. “Niko wapi?”Ilikuwa ni sauti ya msichana aliewekewa mikono na Roma wa kwanza, sasa kilichomshangaza Roma ni kwamba mwanadada huyu alitumia lugha ya Kiswahili kuuliza
Lugha ambayo Kobota na Mbwa mwitu hawakuweza kuielewa
SEHEMU YA 53
Roma aligeuka nyuma na kuanza kumshangaa msichana kwa kitendo cha kuongea lugha ya kiswahili , Msichana huyu alionekana akili yake haikuwa sawa kwa madakika kadhaa ,aliwaangalia wajapani waliokuwa mbele yake na alianza kuwaogopa . Roma ambae hakuwa na nguo hakujali sana kama aliekuwa mbele yake ni mwanamke.
"Unaitwa nani ?" Aliuliza Roma kwa Lugha ya kiswahili na kumfanya msichana huyu amwangalie Roma kuanzia miguuni na kumpandisha taratibu, macho yakatua kwenye kiungo cha Uzazi cha Roma na akatulia hapo , ni kama alikuwa amesahau kama ameulizwa swali. Msichana alionekana kuwa mdogo mdogo kimakadirio umri si zaidi ya miaka ishirini na Tano. "Hey binti unaitwa nani acha kukodolea Mb**o yangu au hujawahi kuona?" Aliongea Roma na lumfanya yule mwanadada aone aibu na kufanya Mbwa mwitu na Kobota wacheke lakini wakati huo huo walijikuta wakigeuza macho mara baada ya kusimia sauti ya kikohozi nyuma ya Roma
Alikuwa ni yule msichana wa kijapani na sasa alionekana kuzinduka huku akionekana akili yake pia haiko sawa kwa jinsi alivyokuwa akiangalia Mazingira ya hapo ndani , alianza kukagua mtu mmoja mmoja ,macho yalipotua kwa msichana mwenzake alionekana kumfahamu kwani alionyesha hali ya wasiwasi kumuondoka , alimgeukia Rpma ambae hakuwa na habari akiwa amekaa kwenye kisturi na kufanya dudu lake lining`inie kwa chini . "Hey!acheni kunikodolea macho , eti wewe binti unaitwa nani na kwanini mlikuwa mmefungiwa kwenye maboksi?". Mwanadada huyu mweusi alionekana kufikiria ni kama alikuwa akikumbuka tukio lakini kabla hajajibu walisikia sauti kwa nje na kuwafanya wote washituke ,Wa kwanza kukurupuka alikuwa ni Kobota na kutoka nje ya chumba na akafuatia Mbwa mwitu. "Hades!"Aliita kobota . "Kuna nini ?"Aliuliza Roma ila Kobota hakujibu alionesha hali ya wasiwasi kwenye macho yake na kumfanya Roma aone kutakuwa na tatizo nje , aliinuka kwenye kiti alichokalia akiwaacha wasichana ambao walikuwa kwenye hali ya wasiwasi. Roma alitoka na kujikuta akishangaa kwani walikuwa wamezingirwa na wanajeshi waliokuwa kwenye ‘SpeedBoat’ za kijeshi ,Roma baada tu ya kuwaangalia alijua ni wanajeshi wa jeshi la maji wa Japani ,alihesabu boti zote na jumla yake zilikuwa nane huku kila boti ikiwa na wanajeshi watatu "Full combat soldiers" ni kama walikuwa kwenye vita. Roma kama kawaida yake ,alionekana kutokuwa na wasiwasi kabisa ,tena hakujali kama alikuwa uchi wa mnyama. "Mko chini ya Ulinzi kwa kosa la kuteka nyara"Aliongea mwanajeshi mmoja ambae sauti yake ilimfanya Roma agundue ni mwanamke. Kobota na Mbwa mwitu mikono ilikuwa juu na wanajeshi hawa licha ya kuwaona Kobota kuwa na sare za Jeshi
,hawakuwaona kama wenzao , ilionekana ni kama hawakua wakiamini mtu. Roma alimwangalia mwanamke mjeda na kisha alimsogelea na kufanya wanajeshi wakoki siraha zao , lakini Roma kama kawaida yake alisogea mpaka aliposimama mwanajeshi kiongozi . "Ukisogea hatua nyingine mbili na kulipua , narudia hatua mbili mbele nakulipua" Mwanajeshi huyu wa kike alionekana kutokuwa na utani hata kidogo , lakini licha ya kua siriasi Roma hakuonekana kuwa na hofu , wanajeshi wengine hawa wa kijapani walikuwa wakishangazwa na ujasiri wa Roma huku pia baadhi yao wakiangalia kiungo cha Roma cha uzazi kilivyokuwa kikubwa . "Paah!!...paaah!!..paa...ba ng..bang..!"
Zilikuwa ni risasi zilizoachiwa mfululizo na wannajeshi hawa mara baada ya kuona Roma hakuwa akitii kwa kile alichokuwa akiambiwa. "Inawezekanaje hiii..!" Aliongea yule mwanadada kwa mshangao na hii ni baada ya risasi zote ambazo zilikuwa zimerushwa kumlenga Roma kutomfikia , yaani ni kama Zilikuwa zikimkwepa kila zikimsogelea na kupita ni kama kuna nguvu ambayo Roma alikuwa akitumia kuzipindisha. Wanajeshi walishikwa naa kiwewe , hakuna aliekuwa akiamini kinachotokea na hawajawahi kukutana na tukio kama hilo , Kobota na Mbwa Mwitu na wenyewe walishangaa mpaka kushusha mikono chini na kusahau kuwa waliambiwa wanyooshe mikono juu , licha ya kwamba walikuwa wameshuhudia tukio la mwanzo la Roma kugandisha maji ya baharini pamoja na macho yake kuwaka taa , lakini hawakujua kama alikuwa na uwezo mwingine . "Bang , bang ... bang ... bang paaa , paa . bang bang ..!!!" Hawa wanajeshi baada ga kuona zoezi la kwanza limefeli waliona warudie tena ni kama walikuwa wakitaka kuthibitisha kile walichohuhudia sekunde chache nyuma lakini hakukuwa na mafanikio risasi zilionekana kukosa nguvu kila zinapomfikia Roma. na upamde wa Roma aliishia kutabasamu na awamu hii hakuwa hata amebadilika macho yaani alikuwa yeye kama Roma aliekuwa katika hali ya uchi. "Tatatata...taatatata.......t aata" Ulikuwa ni mvumo wa chopa ambayo baada ya wanajeshi hawa kuangalia juu waligundua ni ya jeshi la Japani , ilikuwa ni chopa ambayo ilionekana kuwa na wanajeshi waliokuwa wakichungulia chini , baada ya chopa kukaribia usawa ilishushwa kamba na mwannajeshi mmoja alishuka akilenga moja ya boti waliokuwa wale wanajeshi.
"Kapteni mnaweza kuweka siraha chini"Aliongea mwanajeshi huyu na mavazi yake ya gwanda yaliokuwa yamejaa vyeo , alionekana kuwa na cheo kikubwa kwani wannajeshi hawa waionekana kumpa heshima. "Major !!" Aliita mwanamke yule ambaye sasa Roma alimjua kwa cheo cha Kapteni lakini mwanajeshi wa cheo cha Meja alionekana kutotaka maelezo alitoa ishara ya siraha kushushwa chini buku akiamrisha boti isogezwe karibu na Roma na ikasogezwa.
"Hades jina langu ni Major Suzuki ,nitangilize radhi kwa shari ya wanajeshi wetu"Aliongea Afande Suzuki huku akimpa mkono lakini Roma hakuupokea . "Afande Suzuki kabla hatujaendelea unaonaje nikijisitiri, nikipata nguo za mwanajeshi mmoja hapa itafaa sana ,tena ningependelea zenye cheo cheo cha kapteni"
Kwanza kabisa wanajeshi walionekana kishangaa mara baada ya Afande Suzuki kumuita Roma kwa jina la Hades, na hapa waliunganisha na tukio la risasi kutomgusa kabisa Roma na waliamza kujua kuwa mtu ambae walikua wakimshambulia ni mtu ambae alikuwa akisifika sana duniani kwa kila jeshi kwa uwezo wake , walikuwa wanataarifa za Hades kamanda wa jeshi la The Eagles , jeshi ambalo lilipindua serikali ya Wales kwa masaa manne na kumuingiza madarakani Malkia Catherine. Major Suzuki na yeye alikuwa akiusikia uwezo wa Hades licha ya kwamba hajawahi kuona laivu moto wake , lakini alikuwa na taatifa zote zilizokuwa zinamuhusu Hades na hata ujio wake hapo ni kutokana na Oda aliopewa na waluu wake wa kazi.
Meja hakuona haja ya ombi la Hades kulikataa , hasa akikumbuka maagizo aliopewa na wakuu wake wa jeshi kutomuudhi Hades , Aligeuka na kumwangalia Kapteni na kumpa ishara avue nguo . Kapteni alionyesha hasira yake ya wazi kabisa , hakuwa tayari kudhalilika mbele ya kikosi chake , licha ya kwamba alikuwa akijua mtu aliekuwa mbele yake ni Hades au Mfalme Pluto hakuwa tayari kuvua nguo kwani kwake ilikuwa ni udhalilishaji wa hali ya juu na ukizingatia yeye ni mwanamke
“Afande Suzuki naona hauna nguvu jeshini kiasi cha Kapteni kutotii amri yako , mimi hapa ni muhamga na siwezi kutoa msamaha kirahisi angalia zote hizi ni risasi ambazo zimelengwa kwangu kwa
ajili ya kinidhuru ,mimi adhabu yangu katika maisha yangu haijawahi kuwa fofauti na kifo lakini kwa mara ya kwanza leo najisiki kutoa aina nyingine ya msamaha" Kwa jinsj Roma alivyokua akiongea utadhani hayupo
siriasi , ila ukweli ni kwamba alikuwa siriasi sana na alikuwa akimaanisha, na hata Meja Suzuki alikuwa akielewa kuwa hakuna neno lolote lishawahi kumtoka Pluto likawa la utani hasa ukilinganisba na hali ilivyo. "Kapteni nakuamrisha kama mkuu wako vua nguo umpatie Hades" "Meja kwanini nivue nguo wakati sina kosa , sisi kumshambulia Hades ni kutokana alikaidi, hakuna kosa lolote nimefanya na siwezi kudhalilika kwa kuvua nguo mbele ya kikosi change" Jibu lilionekana kimkasirisha sana Meja Suzuki , kilichomkasiriaha Meja sio kwasababu ya kwamba Kapteni alikuwa akionewa au hakua na makosa kilichomkasiriaha ni kwamba Kapteni hakutii amri kutoka kwa mkuu wake kicheo. Meja aliangalia Maafande wote waliokuwa wapo ndani ya hili eneo , na muda ulikuwa umeenda sana na uzuri tu ni kwamba kulikuwa na Mwezi, Aliwapa amri wanajeshi waliokuwa wamesimama na Kapteni wamvue nguo,
"Mtu asije akanigusa natoa Amri" Aliongea Kapteni lakini wanajeshi wlikuwa wakitii oda kutoka kwa Meja zaidi, licha ya kwamba aliekuwa mbele yao ni mkuu wa kikosi chao , wao walikuwa wakitii Amri kutoka kwa mwenye cheo kikubwa na hio ndio ilivyo kwa majeshi yote duniani . Kapteni alipigwa Roba na wanajeshi wake huku akianza kufurukuta kiasi cha kufanya boti iyumbe , lakini wanajeshi walionekana kumzidi nguvu na walianza kumsaula gwanda zote na akabakia na Singlend pamoja na Bukta . “Hahaha... kumbe shida yote hio ya ukaidi,kumbe ulikuwa ukiogopa bukta lako limetoboka kwa kuchakaa" Wanajeshi wenzake walicheka ,ikiwemo na Kobota na Mbwa Mwitu ,Ni kweli Bukta ya kitambaa aliokuwa amevaa mwanajeshi huyi wa kike ilikuwa imesagika nyuma kwa kuacha matobo mawili upande wa ta*ko la kulia na kushoto na ilionesha ilikuwa imevaliwa muda mrefu sana , hakika Kapteni alikuwa amedhalilika sana usiku huo na katika maisba yake , alitamani kutoa chozi lakini alijikaza kijeshi .
Roma alijikuta akiridhika na hali hio na hapa aliona kisasi chake ashakilipiza , hakutaka kubaki na deni , kwani kitendo cha kushambuliwa na wanajeshi wa Japani ambao kwanza kabisa ndio waliosababisha kuwepo hapo usiku huo kwenye baridi, halafu hao hao wamshambulie lwa dhamira ya kumuua alikasirika ila hakutaka kuonyesha. Roma alivaa nguo za Kapteni , licha ya kwamba zilimbana kutokana na kwamba Kapteni alikuwa na mwili mwembamba kuliko wake, ila alilazimisba hivyo hivyo . "Sasa Meja tunaweza kuendelea , kwanini kapteni kanivamia na kumishambulia ili hali jeshi lenu ndio mmenipatia misheni hii ya kuja hapa , kwanini muanze kuniita
mtekaji?"
"Sir Pluto kwanza tunaomba radhi , mpaka sasa Kapteni Kisu Mvunjiko yupo chini ya ulinzi kwa kukiuka sheria za Jeshi" Kobota na mwenzake walijikuta wakianza kushamgaa huku wakijawa na hofu hawakuelewa alichokuwa akimaanisha Meja Suzuki "Meja Suzuki hebu toa maelezo ya kueleweka" "Hades Kisu mvunjiko kafanya uasi kwenye jeshi letu na mpaka sasa yupo chini ya ulinzi , katusaliti kwa kula njama na Korea Kaskazini Kwa kumteka mtoto wa waziri mkuu na kutaka kumsafirisha" "Na vipi kuhusu Sanamu ambalo alisema lilibiwa na lenyewe likuwa ni mpango wa Korea kaskazini ?" "Hades mpaka sasa hatujapata maelezo ya kutosha kutoka kwa Kapteni mvunjiko kwani yupo anahojiwa chini ya ulinzi mkali wa Jeshi , kilichokutokea wewe ni sehemu ya mipango ambayo mpaka sasa hatuna taarifa kamili , lakini Sanamu ambalo amesema limeibiwa ni feki Sanamu Varicana lipo kwenye jengo la Makumbusho mpaka sasa" "Shi**"t huyo ni wa kuua tu " Aliongea Roma huku akionesha hasira waziwazi .
"Vipi kuhusu Dorisi yuko salama ?" "Huna haja ya kuwa na wasiwasi Pluto Dorisi yuko sala..."Kabla hajamaliza kuongea walionekana wale wasichana wakitoka nje na sasa walionekana kuwa na nguvu . "Miss Shirani !" Aliita kapteni huku akimwangalia yule mwanadada wa Kijapani , na Shirani alionekana kutoa machozi . "Bro Suzuki" Aliita kwa kijapani na mwanadada alimsogelea Suzuki na wakashikana mikono huku akitoa machozi . "Pole sana , kwa yalio watokea wewe na Sophia , Shukrani kwa uwepo wa Pluto mmesalimika kabla ya kupelekwa Korea Kaskazini , mheshimiwa amekuwa na wasiwasi sana juu ya usalama wako".
Shirani alimgeukia Roma na kumuangalia na Roma baada ya kukutanisha macho na Shirani alimkonyeza huku akitabasamu na muda huo pia Sophia aliwasogelea mpaka kwenye ukingo wa boti hio . "Sophia Balozi Ramadhani baba yako ana wasiwasi sana , mama yako yupo hospitalini kwa mshitiko , pole sana" Aliongea kwa kingereza na akamgeukia Roma "Sir Pluto nitakuelezea mlolongo mzima wa matukio lakini kwasasa inabidi kurudi nchi kavu "Aliongea Meja na Roma , Sophia na Shirani walipandiahwa kwenye chopa na kuondoka huku wakimuacha Kapteni akiwa na hasira kali baada ya kudhalilishwa na Hades ITAENDELEA
SEHEMU YA 54
Kutoka Osaka mpaka ilipokuwa kambi iliokuwa ikifahamika kwa jina la Hastiti hapakuwa mbali na chopa ilitumia dakika kumi na tano tu kua angani. Muda wote ambao Sophie na Shira kuwa angani , walikuwa wakimshangaa Roma ,hawakuwa wakielewa kwanini mtu aliekuwa uchi mbele yao dakika kadhaa nyuma alionekana kuheshimika sana mbele ya Meja Suzuki , lakini pia hawakuwa wakielewa kwanini Meja Suzuki alikuwa akimwita mwanaume aliekuwa mbele yao Hades, walikuwa na maswali mengi yaliokuwa yamewajaa kwenye vichwa vyao , kwao Roma alikuwa
akionekana kawaida sana kwenye macho yao na kitu pekee ambacho hakikua cha kawaida kuhusu Roma ni ukubwa wa dudu lake tu, lakini pia hawakuwa wakiamini kama Roma ndio aliowaokoa,Laiti wangeshuhudia mziki alioufanya Roma wakati wakiwa kwenye maboksi wasingekuwa na maswali ya aina hio.
Licha ya Sophie kuwa katika hali mbaya kimavazi , urembo wake haukua umejificha , alionekana kuwa mrembo kweli kiasi kwamba hata kwa Dorisi hakuwa akimfikia , na kwa kumwangalia tu Sophia ni dhahiri kwamba utagundua mmoja ya mzazi wa Sophie ni mwarabu kutokana na nywele zake. “Kanaonekana kuwa karembo , kwanini muda ule sikuwa nimekaangalia vizuri”Aliwaza Roma wakati wakiwa wanakaribia ilipo kambi ya Hastiti nje kidogo na jiji hili la Osaka.
Chopa ilitua kwa ustadi katika uwanja mdogo wa Hastiti , licha ya uwanja huu kuonekana mdogoi lakini ulikuwa ukitosha kabisa kwa ndege kubwa kutua , ilikuwa yapata saa nane za usiku lakini ndani ya eneo hili ni kama mchana kutokana na taa aina ya ‘Spotlight’ zilizokuwa zimefungwa kwa kuzungushwa eneo zima la kambi kumulika. Kitendo cha Roma kukanyaga Ardhini tu , alimuona mwanamke akimkimbilia , alikuwa ni Dorisi, aliekuwa kwenye mavazi yake yale yale , licha ya kwamba Roma alikuwa amemuacha akiwa amechomwa sindano ya sumu na Kisu Mvunjiko , lakini hapa alionekana kuwa katika hali ya uzima wa afya.
Roma alijikuta akitabasamu mara baada ya kumuona mrembo Dorisi ,Mrembo huyu alionekana alikuwa na wasiwasi kweli , walikumbatiana na kufanya watu waliokuwa eneo hili wawaangalie kwa macho ya tofauti , huku Shira na Sophia wakiwa ni wenye kushangazwa na uzuri wa Dorisi , licha ya kwamba Sophia alikuwa mzuri lakini alikiri Dorisi alikuwa mzuri. “Wanaonekana wanapendana sana”Aliwaza Sophie. “Bebii Dorisi naona umepona”Aliongea Roma huku akiwa na tabasamu kama kawaida yake.
“Nilikuwa na wasiwasi sana , roho ilitaka kunitoka , nilikuwa nikiwaza kama jambo baya likikutokea nitamwambia nini Edna, na mimi nitaishi vipi” Aliongea Dorisi na kumfanya Roma amkumbuke mke wake Edna , kwani tokea afike Japani hawakuwa ni wenye kuwasiliana hata kwa ujumbe wa meseji , hawakupigiana simu kujuliana hali wanandoa hawa wa mkataba. Roma alijikuta akijisikia vibaya , licha ya kwamba yeye hakuwa amempigia mke wake simu lakini aliona Edna alipaswa kumpigia yeye , kwani Edna alikuwa na taarifa zote za kile kilichokuwa kikiendelea Japani.
“Hakuna jambo linaweza kunipata Dorisi , hupaswi kuwa na wasiwasi mimi hakuna kiumbe kinachoweza kunidhuru kwenye hii dunia”Aliongea Roma na kumfanya Dorisi atabasamu , kwa namna ambavyo Roma alikuwa akiongea usingedhania kama ni yule aliekuwa akifanya mambo ya kutisha masaa kadhaa nyuma , huyu alikuwa Roma wa kawaida ambaye mtu yoyote angemuangalia asingeyumbishwa na uwepo wake, kwani alikuwa wa kawaida sana.
“Dadii..” Aliita Sophine mara baada ya kumuona baba yake aliekuwa akiingia ndani ya sehemu hii ya uwanja wa ndege na akamkimbilia na wakakumbatiana huku Sophie akianza kulia kwa kwikwi . “My Daughter ,I am so Sorry I Could’nt Protect you”Aliongea mzee huyu huku akionekana kujutia kwa kuruhusu tukio la kutekwa kwa mtoto wake , aliona yeye ndio msababishi kwani hakuwa makini na usalama na mtoto wake. Balozi Ramadhani Shabani alikuwa ni Balozi wa Tanzania nchini Japani , alikuwa ni mwanaume ambaye ukimwangalia tu utajua alikuwa na umri usiokuwa ukipungua miaka arobaini hivi , alikuwa ni mwanaume mweusi tii jambo ambalo lilimshangaza Roma , inakuwaje Baba yake Sophia kuwa mweusi sana halafu Sophia kuwa mzuri kiasi hiko , kwani Rangi ya Sophia na ya baba yake havikuwa vikiendana ila Roma alijiambia moyoni huenda Mama yake Sophia ni mweupe , hivyo hakutaka sana kujisumbua na mawazo hayo kwanza ni maswala ambayo hayakuwa yakimhusu.
“Hades naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa kumuokoa mwanangu , sijui ni zawadi gani nikupatie , kwani kama Sophia angepelekwa Korea Kaskazini sijui ningemuangalia vipi mke wangu” Roma alimwangalia mzee huyu na kwa maneno yake tu alijua huyu mzee watakuwa ni wale wanaoendeshwa na wake zao , wale wanaume wanaopenda kupitiliza ,kiasi kwamba hata wakosee wao mara nyingi ndio wanapiga magoti kuomba msamaha. “Mzee kama unanishukuru kwa kumuokoa mwanao unaonaje,ukiwa mkwe wangu kabisa” Aliongea Roma na kumfanya Sophia aone aibu na hapohapo akili yake ikakumbuka dudu ya Roma .
“Kuhusu hilo Hades nitalifikiria”. “Karibu sana Hades , kwenye kambi yetu , na ninafuraha ya kukutana na wewe , naitwa kanali Sotoko”Aliongea bwana mmoja kijana, baada ya kuwasogelea Roma ,Dorisi na Balozi waliokuwa wakisalimiana. “Ooh!Kanali nafurahi kukufahamu pia na ni vyema umekuja kunipokea , kabla ya mambo mengine kuendelea Kanali nina njaa sio ya kawaida , unaonaje ukitoa amri nifanyiwe mpango wa chakula , kabla hamjanipeleka kuonana na Kapteni Kisu Mvunjiko” Kanali alitabasamu na kuwapa ishara vijana wake waliokuwa mita kadhaa kutoka alipo yeye na kisha wakaondoka na walionekana walienda kuandaa chakula kama alivyokuwa ameongea Roma , kwani Roma alikuwa akiongea na Afande Sotoko kwa lugha ya kijapani.
Baada ya kama nusu saa kupita ,Roma alikuwa ameshikilia bakuli lake la Tambi. Huku pembeni yake akiwa amesimama mpishi aliekuwa na hotpoti kubwa ambalo lilionekana dakika chache zilizopita lilikuwa limejaa. Mpishi huyu muda wote aliikuwa ni mwenye kutoa macho ya mshangao kutoka na uwezo wa Roma kula , hakuamini kama hotipoti zima la tambi ambalo amekuwa akizoea kuwekea watu watano lilikuwa linaisha.
Roma baada ya kumaliza bakuli la nne alimwambia mpishi amalizie tambi zilizokuwa kwenye hotpoti , na mpishi alifanya kama alivyoagizwa na baada ya Roma kukabidhiwa bakuli lake , alimwangalia Kanali Sotoko aliekuwa ameketi pembeni kwenye masofa alionekana na yeye ni mwenyekushangazwa na uwezo wa Roma kula chakula kingi halafu anaonekana kawaida , alijiuliza bwana huyu ni mtu au ngombe , ila hakutaka kuonesha kama alikuwa akimfikiria vibaya Hades , kwani alikuwa amepewa maelekezo kutoka uongozi wa juu kumpa heshima.
“Kanali nadhani ni muda wa kunipeleka kwa Kapteni Kisu Mvunjiko nina machache ya kumuuliza”. “Sir pluto vijana washaandaa utaratibu tayari nasubiria umalizie” “Nitaenda nakula taratibu Kanali tunaweza kuelekea maana sitaki kupoteza muda , kesho nina safari ya kurudi Tanzania nimemmisi mke wangu”
Aliongea Roma na kumfanya Kanali ashangae , ndio alishangaa kwasababu muda mfupi uliopita Roma alikuwa amekumbatia na kuonyeshana mapenzi kama yote na Dorisi , inakuwaje sasa
anamwambia amemmisi mke wake , ila hakutaka kuongea chochote , walinyanyuka na kuelekea nje huku Roma akiwa na Bakuli lake akitembea huku anakula , jambo ambalo liliwafanya wanajeshi waliokuwa kwenye Korido hizi za kambi kumshangaa Roma kwa tabia yake , mshangao wao kwa Roma ni kama heshima..
Wanajeshi waliokuwa na vyeo mbalimbali walikuwa wamejipanga kwa mstari kumuangalia Hades wakati akipita , walikuwa na taarifa zote za ujio wa Hades ndani ya kambi yao na wakaona hio ndio nafasi yao ya kumuona mtu ambaye ana umaarufu mkubwa sana duniani ndani ya majeshi yote , Pluto , Mrithi wa kiti cha mfalme wa Kuzimu na mmiliki wa pete ya Hades. Ni ndani ya gereza ndani ya kambi hii , Mlango ulifunguliwa na mwanajeshi aliekuwa akihusika na ulinzi na kumruhusu Roma na Kanali Sotoko waingie ,
Kapteni Kisu mvunjiko alionekana katika hali ya majeraha mengi mno , alionekana alikuwa amepitia mateso makali sana ndani ya saa chache zilizopita na hata Roma alipoingia hapo ndani , licha ya kwamba alikuwa ni mwenye kuonyesha wasiwasi baada ya kutambua mtu aliekuwa mbele yake alikuwa ni Hades, lakini hakuweza hata kunyanyuka wala kusogea mahali alipokuwa amekaa. Roma alikaa kwenye kiti kilichokuwa hapo ndani na kuendelea kula Tambi zake bila habari na ndani ya dakika kama tano hivi alikuwa amemaliza na sasa aligeuza shingo yake na kumwangalia Kapteni Kisu Mvunjiko. “Okey! Kapteni kisu tusipoteze muda , sitaki kuondoka kwenye hili taifa na nikaacha deni nyuma , utaniambia kila kitu na nikishamaliza nisikufiche nitakuua”
“Hades niombe Radhi kwa kuingilia lakini huyu ni mtuhumiwa wetu na mpaka sasa yupo chini ya Jeshi tunakuruhusu kumuhoji lakini sio kumuua”. “Afande kama mnamjali sana Kapteni Kisu hapa mimi sina shida , ila mimi bila ya kuua ndani ya taifa hili siondoki , sitaki kudaiwa na sitaki kumdai mtu , mimi nchi yenu nawadai kifo cha Kapteni kisu , ila kama kwenu Kapteni kisu ni muhimu nitafutieni mwanajeshi yoyote hapa kambini nimuue na deni langu litakuwa limeisha” Afande Sotoko alijikuta akitoa jasho .
“Hades sio kwamba tunaumuhimu sana na Kapteni Kisu , ila tokea tulipoanza kumuhoji hakuna ukweli wowote ambao ameongea mpaka sasa” “Sasa kama shida ni hio kwanini uwe na wasiwasi , nitamfanya atapike kila kitu hapa kama unachukua kalamu na karatasi andaa kabisa na nikimaliza nitamuua”
Kanali Sotoko aliona hakuwa na maamuzi ya mwisho juu ya swala hilo , aliona kwanza awasiliane na wakuu wake na alifanya hivyo kwa kutoka nje , huku Roma akibakia na Kapteni kisu Mvunjiko. “Kapteni kisu usiwe na wasiwasi nitahakikisha kifo chako kutokuwa cha maumivu kama utaniambia mwenyewe kila kitu na usije ukafikiria kunidanganya maana nina mbinu nyingi za kujua ukweli sawa”Aliongea Roma huku akimgusagusa nywele Kapteni Kisu kama mtoto ambaye anabembelezwa alale . Kapteni kisu alimwangalia Roma kwa wasiwasi mkubwa sana, lakini licha ya kuwa na woga alijiambia katika nafsi yake hatoongea ukweli wowote na yupo radhi kufa. Baada ya dakika tatu Afande Sotoko alirudi. “Nipe ripoti Afande mnaniruhusu nimuue au mtanipatia mwanajeshi yoyote cheo cha kapteni nitulize kiu yangu na tumalizane nirudi zangu kwa mke wangu?”Aliuliza Roma. “Hades Mkuu wa majeshi kakupa nafasi ya kufanya kile unachotaka kufanya ilimradi Kapteni kusu mvunjiko atapike siri zote”.Roma alitabasamu. “Okey! Kapteni kisu nadhani ushasikia mwenywe kutoka kwa
Kapteni , sasa hivi mimi ni kama Mungu kwako , ninaweza kukuweka hai na ninaweza pia kuruhusu kifo chako , lakini pia ninaweza kukupa kifo cha maumivu lakini pia ninaweza kukupatia kifo kisichokuwa na maumivu katika chaguzi unatakiwa kuchagua vitu viwili tu kifo cha maumivu au kifo ambacho sio cha maumivu” “Naomba uniue tu siwezi kuongea chochote”. “Nina asilimia mia moja wewe ni shushu kutoka Korea Kaskazinina huenda wewe ni sehemu ya jeshi lao na sifa ya kipuuzi ambayo wanaaminishwa dunia ni kwamba , wanajeshi wa Korea Kaskazini mnajua kuvumilia mateso ya aina yoyote, hio sifa kwangu ni ya kipuuzi na nikwambie tu huwezi kuvumilia mateso ambayo nitakupatia”Aliongea Roma na Kisu mvunjiko licha ya maneno hayo hakuonekana kuyumba kwa aina yoyote ile alijiambia kwenye nafsi yake hizo Zote ni tambo za Hades na haongei chochote.
SEHEMU YA 55
YOKOTA AIR BASEJAPAN Ni ndani ya makao makuu ya jeshi la anga la Marekani nchini Japani , ndani ya ukumbi mkubwa uliozoeleka kwa kufanyia mikutano , alionekana mkuu wa majeshi wa Japani na maafisa wakuu wa jeshi la Japani na wa Marekani wakiwa wamezunguka meza kubwa, na kwa namna ambavyo wamekaa walionekana kuwa na kikao ambacho kinaendelea. Mbele kabisa ya meza kulikuwa na Skrini kubwa ambayo ilikuwa ikionyesha chumba cha mahojiano moja kwa moja kutoka Hastiti , huku pembeni akiwa amesimama mzungu mmoja ambae ameshikilia
Tablet(kishikwambi) yake , huku maafisa hawa wakiwa wanamuangalia bwana huyu ambaye amevalia nguo za kawaida tofauti na watu wote waliokuwa ndani ya chumba. “Naitwa Meja Stanlaus Homer , nipo hapa kwa ajili ya kutoa maelekezo ya kile kinachoendelea katika chumba cha mahojiano kutoka kambi ya Hastiti, mahojiano ambayo yatakwenda kufanywa na Hades , hii ni fursa kwetu hapa kujua aina ya mateso ambayo Hades hutumia pale anapomhoji adui , nitaelezea kwa kila kitu kitakacho kuwa kinaendelea”
Aliongea Meja Stanlaus huku akionekana kujiamini, alionekana alikuwa ameshiba taarifa ambazo zinamhusu Hades, na baada ya kutoa utambulisho huo mfupi aliruhusu sauti ya Hades kusikika ndani ya chumba hiki huku maafisa hawa wakiangalia kile kinachoendelea. “Kapteni kisu , unajua kwanini naitwa King Of hell?”Kapteni Kisu hakuongea chochote. “Ni kwasababu kila kiumbe kinachokufa kinakuwa chini ya utawala wangu, na kwasababu mimi ni Mungu wa kuzimu vilevile ninaweza nikakataa baadhi ya raia , hivyo hata wewe hapa ninaweza nikakuua kwenye huu ulimwengu unaoonekana kwa mateso makali na nikakukataa kwenye ulimwengu wa kuzimu … kwa hio utakuwa unakufa na kufufuka , ni rahisi kukuambia
nitakutesa mpaka ufe halafu na kufufua tena nakutesa unakufa nakufufua tena”Aliongea Roma na kufanya maafisa wa jeshi watabasamu kwa biti hilo. “Kwa hio Kapteni nieleze ukweli wote nikupe kifo cha kistaarabu ujistukie tu upo kuzimu , au nikupe kifo cha maumivu ambacho nitahakikisha ukiwa kuzimu bado unahisi maumivu” “Niue siwezi kuongea chochote” Aliongea Kapteni kisu mvunjiko na Roma akatabasamu na kisha akamsogelea na
kumuingizia vidole viwili masikioni na kuanza kumminya kwa nguvu , na kadiri ambavyo Roma alikuwa akimminya ndivyo kapteni alivyoanza kutoa kilio , alionekana kuhisi maumivu makali sana kiasi kwamba alitoa ukulele , lakini bwana huyu bado hakuonyesha kuongea na Roma pia hakuonyesha kuacha na alijikuta akizimia kwa maumivu na Roma akamuwekea viganja mashavuni kwa sekunde kumi na akashituka tena na maafisa wa jeshi wakamgeukia Stanlausi , walionekana walikuwa wakitaka maelezo. “Hiyo inaitwa ‘Endless Energy Restoration’ ni nguvu inayopatikana kati ya mbingu na ardhi kwa kufanya ‘Meditation’ na hii nguvu Hades aliipatia wakati akiwa kwenye mafunzo ya ‘Martial Art’ kwenye Shaolini Tempo za kichina , ni Hades pekee ambae ameweza kufikia mzunguko wa juu wa kufyonza nguvu hii inayozalishwa kati ya mbingu na ardhi na hili ndio jambo ambalo linamfanya Hades kuwa tishio kwa ‘Master’ wote wa mafunzo ya kimapigano wa matempo ya kichina,na mpaka sasa hakuna
‘Master’ yoyote kutoka China anaeweza kupigana na Hades kwa nguvu za kichawi na ‘Martial Art’”Aliongea na kuwafanya washangae na kuendelea anachokifanya Hades. Licha ya mateso makali ambayo Kapteni Kisu alikuwa akifanyiwa na Roma hakuwa tayari kuongea na hili lilimshangaza Roma mwenyewe na mpaka akajiuliza kuna sababu gani ya mtu huyu kuwa na moyo mgumu kiasi cha kuvumilia mateso yake , lakini licha ya ugumu huo wa Kapteni Kisu hakukubali kushindwa. “Ngoja kwanza nimpeleke kuzimu , akikutana na wafu ataongea tu” Aliwaza Roma na kisha akamuwekea vidole kwa mara nyingine na hapa ndipo Kapteni Kisu alivyoanza kutetema , alionekana akiwa akishindana na kifo na uhai , lakini licha ya
mateso hayo hakuwa tayari kuongea , alitamani kufa, na zilichukua sekunde therathinni tu , alinyooosha miguu na kukakamaa na alionekana amekufa , na hili swala liliwafanya maafisa hawa wa jeshi kutoa macho kwa mshangao. “Sh**t sisi ni wapumbavu tumeacha amemuua , haya sasa tumekosa taarifa muhimu sana kwa jeshi letu,tutakuwa jeshi la kwanza duniani kwa kuwa wapuuzi” “ Brigedia Shomboto kaa chini tuliza mshono Alah!”Aliongea Mkuu wa majeshi kwa hasira na alionekana hakupendezwa na uropokaji wa Brigedia Shomboto. Roma baada ya kutulia dakika mbili aliona hizo zinatosha sana kwa Kisu Mvunjiko kuiona kuzimu , alimuwekea viganja tena na baada ya dakika tano ,Kapteni kisu mvunjiko alishituka tena , huku akionekana ni mtu ambaye kama alikuwa akikimbizwa ndotoni , kwani alikuwa akihema mno. “Hehe…. Kapteni nadhani umepaona palivyo?” ‘Naomba usiniue tafadhari nipo tayari kuongea”. Roma alitabasamu nakuona Zoezi lake limefanikiwa
Maafisa wa jeshi wakamgeukia Meja Stanlausi , walionekana kutaka maelezo ya kile kilichotokea.
“Hapo Hades amempeleka katika falme yake ambayo haionekani kwa macho(realm) na anachokifanya ni kumuingizia nguvu ya kimiujiza mtu na kufanya viungo vyote vya mwili kupoteza mawasiliano na mtu kuonekana kama amekufa lakini akili ya mtu ikiendelea kufanya kazi , unaweza ukashangaa ni kwanini hili linawezekana, ila jibu ni kwamba Hades ana nguvu nyingine aliopata kutoka kwa mfalme Pluto , nguvu hio inaitwa ‘Divinity of light’ hii ni nguvu ambayo inampa uwezo wa kumfanya mtu akili yake kufanya kazi wakati akiwa amekufa, sasa baada ya Hades kuua mawasiliano ya viungo vyote vya mwili ,sasa Hades kwa kutumia ‘Divinity of Light’ anaweza kuifanya akili yako kuwa katika falme yake(realm) na kwa jinsi nilivyoona kwa Kapteni kisu ni dhahiri Hades alimpeleka sehemu zinazotisha katika falme yake”Aliongea na kuwafanya maafisa hawa kushangaa na kujiuliza Hades katoa wapi mambo yote hayo.
“Ongea kwanza kapteni , umekuwa mtu wa kwanza kuvumilia mateso yangu kwa muda mrefu mpaka nikakupelea kutalii kuzimu na kurudi”. Kapteni Kisu alionyesha uwoga wa hali ya juu kiasi kwamba aliwafanya maafisa hawa wa jeshi waangaliane ,unachotakiwa kuelewa hapa ni kwamba wakuu hawa wajeshi walikuwa Tokyo Okinawa na Hades alikuwa Honshu –Osaka
Hastiti Military base. “Naipenda sana nchi yangu ya Japani, lakini licha ya kuipenda hii nchi nampenda Zaidi mtoto wangu , yote nimefanya kwa ajili ya kumuokoa mtoto wangu”Aliongea Kisu kwa hali ya huzuni huku akianza kububujikwa na machozi.
“Mtoto wangu wa kike kashikiliwa nchini Korea Kaskazini na nimefanya yote ili kumuokoa asije akanyongwa” Hapa ndani maafisa wote walishangaa ,Kapteni Kisu alionekana kuwa kwenye maumivu mengi , aliangalia juu dalini. “Kihoi mwanangu naomba unisamehe baba yako , najua nitakaposema haya yote ndio mwisho wako na wangu …..”
Aliongea kwa masikitiko makubwa na Mkuu wa jeshi pale alitoa maagizo kwa taarifa za kihoi kutafutwa haraka, na muunganiko wa kimajukumu wa jeshi hili ulionekana kuwa vizuri kweli sio kama Tanzania unakuta kutafuta taarifa mtandao uko ‘slow’, kwani ilichukua dakika mbili tu taarifa za Kihoi zilianza kuonekana kwenye Tv hilo la hapo ndani ya chumba cha mikutano , huku Skrini ikigawanywa mara mbili , sehemu ya kulia ni video inayomuonyesha Roma na Kapteni kisu kwenye chumba cha Mahojiano na upande wa pili ni taarifa za Kihoi .
Alikuwa ni msichana mdogo sana mrembo aliekuwa kwenye gauni jeupe, alionekana kuwa na mchanganyiko wa mataifa mawili, yaani Korea na Japani na hii ilimfanya mtoto huyo kuwa mzuri na mabwana hawa walishangazwa na muonekano wa huyo Binti katika picha , kwa maelezo yaliokuwa kwenye Skrini yalisomeka kuwa Kihoiu mama yake ni Raia wa Korea Kaskazini. “Kwa hio Kapteni ilikuwaje mtoto wako akafika Korea Kaskazini?”Aliuliza Roma “Mama yake ni raia wa Korea Kaskazini , mwanzoni wakati nakutana na mama yake Kihoi ni nchini Korea Kusini nilipokuwa kwenye misheni maalumu ya kijeshi , na misheni yangu ilinifanya kuonana na Mama yake Kihoi mara kwa mara kutokana na kwamba alikuwa akiuza Bar na uhusiano wetu ndipo ulipoanzia ,tulikula bata sana ndani ya jiji la
Seoul mpaka misheni ilipoisha na mimi kurudi hapa nchini ,baada ya miaka mitatu ya kupotezana na mama yake Kihoi ndipo siku moja alinitafuta na kunieleza juu ya uwepo wa mtoto wangu jijini Seoul na akanipatia ‘Anuani namba , nilijaribu kumuuliza yeye yuko wapi , hakujibu na kukata simu na hapo ndipo nilipofanya safari ya kwenda Seoul kumfatilia mtoto wangu , lakini licha ya kufika sehemu husika kama Anuani ilivyoonesha
Anuani ambayo alinipatia mama yake Kihoi, sikuweza kumpata nilitumia majirani kuweza kumtafuta , lakini kila aliekuwa akinipa taarifa hazikuwa ni za kueleweka baada ya kutafuta sana nilishindwa kumpata Kihoi na kukata tamaa na ndipo niliporejea nchini , lakini ajabu ni kwamba nilikaa siku tatu tu nikatafutwa na mtu aliejitambulisha kwa jina la Kim Deshen kutoka
Korea Kaskazini na kunieleza mama yake Kihoi alikuwa ni ‘Spy’ nchini Korea Kusini na wamegundua kuwa amezaa mtoto akiwa kazini jambo ambalo ni kinyume na sheria na ili kutoa mfano kwa wengine mama yake Kihoi ashanyongwa , huku Kim akiniambia kuwa taarifa nzuri ni kwamba washamrudisha Kihoi na kama anataka asinyongwe kama mama yake inabidi nifanye kile wanachonieleza na hapo ndipo nilipokuwa ‘Spy’
rasmi ndani ya jeshi langu la taifa langu ninalolipenda”Alisimulia Kapteni kisu mkasa wake. “Okey Kapteni Kisu , stori yako inaonekana kusikitisha sana ila mimi hayo hayanihusu , kifo bado kipo palepale ila kutokana na Kihoi hana hatia ngoja nikusaidie juu ya hilo”Aliongea Roma na kisha akamgeukia Kanali. “Nahitaji kuongea na mkuu wa Majeshi wa Kotea Kaskazini sasa hivi nadhani jeshi lina namna ya kuwasiliana nae”
Aliongea Roma akiwa siriasi na Kanali alishangaa na kumuona Roma kama Mwehu , lakini palepale Mkuu wa majeshi alitoa amri ya Mkuu wa majeshi wa Korea Kaskazini atafutwe na aunganishwe na Hades, kilikuwa kitendo cha dakika kadhaa tu simu iliunganishwa na makao makuu ya jeshi la Korea Kaskazini Baada ya simu kupokelewa simu ya Kanali ilitoa mlio na akapokea “Mpe Hades simu”Na Kanali alimpatia Hades. “Mnaonekana kufatilia ninachofanya hapa ndani mbwa nyie mnaoniangalia”Aliongea Hades na kisha akaweka simu sikioni. “Oi! Mjeda ni mimi Hades” Aliongea Roma na kuwafanya maafisa hawa watoe macho na kujiuliza inakuwaje Roma anaongea na Mkuu wa majeshi wa Korea kaskazini kama mshikaji wake maana mkuu wa majeshi wa Korea kaskazini alikuwa akisifika kwa Roho mbaya ndani ya Korea Kaskazini yote. “Haha.. !Pacha ni wewe nasikia umeoa…?”.
Roma alionekana kuongea na mkuu wa Majeshi kama mshikaji wake , walioneakna wawili hao kuwa na stori yao iliopelekea kufahamiana. “Okey! Hades hatutaki kukukasirisha , licha ya kwamba dunia inatuona kama watu wenye roho mbaya lakini sisi tunashukrani kwa kile ulichotufanyia na kwa mtu yoyote ambaye anafanya wema juu ya nchi yetu, kinachotutofautisha sisi na wao ni mtazamo wa kisheria tu hakuna mengine , lakini pia nia yetu ya kujitegemea wametufanya kuwa maadui ,Kihoi ataachwa hai , lakini naamini Hades unajua cha kufanya juu ya taifa letu”. “Tuko pamoja , swala hili nataka liishe kidemokrasia Zaidi”
“Hakuna shida Hades,Japani hatuna ugomvi nao , ni marafiki wetu wa siri , ila kwenye urafiki kuna kukoseana na kusameheana naamini nitaongea na mkuu wa majeshi na tutayajenga” Na hapo simu ilikatwa na kile Hades alichoongea na mkuu wa majeshi wa Korea Kaskazini walisikia maafisa hawa kila kitu. Kapteni aliongea kila kitu na katika mazungumzo yake , alisema Watu wa Dhorua nyekundu walimtishia kumfichua kama shushu kwa jeshi na hapo ndipo walipompa maelekezo ya kutengeneza misheni feki kwa ajili ya kumpeleka Roma kwenda kupambana na Tzeng. Kuhusu kutekwa kwa Sophia na Shirani , alisema ni swala ambalo hakuwa akilitambua na hakuhusika nalo na haikueleweka kwanini walikuwa kwenye hio boti na alionekana kuongea ukweli na Roma akamwamini na swali likabaki ni kwanini Hirashia na Sophie wakatekwa , kwani wanadada hao wote wawili hawakuwa na jambo kubwa ambalo lingekuwa linahitajika kwa Korea Kaskazini , kwani Hirashia alikuwa ni mwimbaji wa nyimbo za kitamaduni za Japani na Sophie na yeye alikuwa ni msaanii pia wa nyimo za kileo, lakini pia licha ya hivyo jeshi la Korea Kaskazini walionesha kutokuhusika na jambo hilo.
Kapteni kisu Mvunjiko alihukumiwa na Hades kwa kukiuka sheria namba moja ya Hades ya kutumia watu wake wakaribu kumpata na kwa mtu yoyote anaevunja sharia kwa Hades hakuwa na huruma kwa watu hao na adhabu yake kubwa ni kifo.
****** Ni siku nyingine kabisa Roma akiwa na Dorisi , walionekana kuwa ndani ya ndege kubwa ya kifahari ‘Private’ ambayo ilikua ikiwarudisha Tanzania na Ndege hii ilikuwa imetolewa na Serikali ya Japani kwa ajili ya kuwarudisha kutokana na mchango wa Hades kumuokoa mtoto wa waziri mkuu Shirani. Roma licha ya kwamba mke wake hakuwa amemtafurta tokea aingie Japani na sasa anarudi , katika moyo wake alikuwa amemkumbuka mno , licha ya kwamba alikaa siku tatu japani , lakini kwake ilikuwa kama ni Mwezi , alitamani sana kumuona Edna hakuelewa kwanini amemmisi hivyo. Safari ilikuwa ni kama ndoto kwa Dorisi , hakika hakuwahi kuwaza atakuja kutumia ndege kubwa ya kifahari kama hio kwenye maisha yake , alitamani safari isiishe aenendelee kubaki na Roma. Mwanadada huyu alionekana kuwa na huzuni , kwani alijua Roma anarudi kwenye mikono ya mke wake na sasa kuonana kwao kutakuwa ni kazini na nafasi za kuchepuka za Roma na ni hapo mpaka amkumbuke. “Wapendwa wetu mnapaswa kufunga mikanda , tunakaribia kutua kwenye uwanja wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam”Roma alimwangalia mwanamke huyu mrembo wa kijapani na kisha akafunga mkanda pamoja na Dorisi. Ni muda wa asubuhi ambao Roma na Dorisi walitoka nje kabisa ya jengo la wageni la uwanja huu, kwa muonekano wa Roma ni kama alikuwa akitokea Bukoba, ila Dorisi alikuwa amependeza mno na Begi lake la kuvuta kiasi kwamba alikuwa kivutio kwa watu waliokuwa eneo hili.
Roma moyo wake uliikuta ukipiga Paah! Baada ya kumuona Edna aliekuwa amependeza mno akiwa anawapungia mkono huku akiwa na miwani ya jua…
NAIMANI UMEJIFUNZA MAMBO MENGI KUHUSU HII SIMULIZI AMBAYO UMEANZA NAYO MWANZO WA SEASON 1 & 2 UNAWEZA UKATUMA UJUMBE HAPO CHINI KUHUSIANA NA ULICHO JIFUNZE AU UMEIONAJE SIMULIZI HII
Chapisha Maoni
TOA MAONI YAKO HAPA