NILIEMDHANIA KAHABA KUMBE NI BIKRA 56-60

SEHEMU YA 56 -60 MWISHO WA SEASON TWO

NILIEMDHANIA KAHABA KUMBE NI BIKRA

SEHEMU YA 56 YA SIMULIZI HII

Edna aliekuwa amesimama akiwapungia mkono Dorisi na Roma , alikuwa na hisia ambazo hakuweza kuzielewa mwenyewe , kwani siku kadhaa alionekana kumkumbuka sana Roma na kutamani arudi haraka , licha ya kwamba hakuwa amempigia simu, lakini alitaka kufanya hivyo mara kibao , kila alipokuwa akitaka kupiga aliishia kughaili hakujua ni kwanini

kuna nguvu mbili zilizokuwa zikishindana ndani ya moyo wake na kutokana na nguvu ya kutotaka kumpigia Roma kuwa kubwa aliishia kutokumpigia, lakini licha ya hivyo alikuwa akimkumbuka sana na sio yeye tu hata kwa Bi wema walitokea kumkumbuka sana Roma na waliweza kujua umuhimu wake ndani ya nyumba. “Kwanini akiwa mbali namkumbuka sana na kutamani kumuona , ila akiwa karibu yangu sipendi kumuona tena”Ni mawazo aliokuwa nayo Edna mara baada ya Roma na Dorisi kuwafikia. “Bebi unaonekana kunimisi mumeo sana , naamini siku nzima tutaitumia kuonesheana mapemzi”

Aliongea Roma huku akiweka tabasamu usoni baada kukumbatiana na Edna alifanya hivyo tu kwasababu Dorisi alikuwa mbele yao ,Edna hakutaka ijulikane kama ndoa yake na Roma ni ya Mkataba na hakuna mapenzi katikati yao , aliona kama ikijulikana Dorisi na wanawake wa Roma wanaweza wakamchukua Roma na ndoa kufa kabla ya muda aliopanga kuachana na Roma . “Niilikumisi sana”Aliongea Edna kwa aibu za kike , kwake ndio mara ya kwanza kumwambia mwanaume amemmisi. “Nimekumisi pia mke wangu”Aliongea Roma lakini Edna aliishia kutabasamu tu na Edna alimgeukia sasa Dorisi. “Dorisi karibuni tena nyumbani na hongereni kwa kufanikisha jambo kubwa kwa kampuni , lakini pia niwape pole kwa kila kitu kilichotokea”.
“Asante Sana , Shukrani ziende pia kwa Roma kwani ndio alifanya kazi yote kwa asilimia kubwa na kama isingekuwa kwa yeye sijui nini kingetokea kwa kampuni”Aliongea Dorisi mbele ya Roma na Edna licha ya kwamba alikuwa akichemka ndani kwa ndani kwa wivu lakini hakutaka kuficha kile anachojiskia,Roma alimwangalia Dorisi na kisha akamkonyeza na akamgeukia mke wake. “Mke wangu ni zawadi gani umeniandalia kwa mchango wangu kwa kampuni?”. “Nimekuandalia chakula”Aliongea Edna na kumfanya Dorisi na Roma washangae . “Hehe..Bebi nadhani kitakuwa kitamu kuliko cha siku ile”Aliongea Roma na Edna hakufurahia neno hilo ni kama alioua Roma alikuwa akimkejeli. Wakati wakiwa wamesimama wanaongea , mara uliingia msafara wa gari za Raisi Senga ndani ya uwanja huo na kuwafanya Roma ,Dorisi na Edna wasogee pembeni. “Simamisha gari”Aliongea mheshimiwa Senga na mlinzi wa pembemi alishikilia sikio namna ya kuwasiliana. “Gari ya mheshimiwa inasimama , narudia gari ya mheshimiwa inasimama na itifaki za kiusalama kwa mheshimiwa zichukukuliwe” Aliongea afisa usalama huyu na hapohapo gari zilisimama na watu waliokuwa ndani ya hili eneo walikaa pembeni . Baada ya mheshimiwa kushuka , aliwasogelea Edna ,Roma na Dorisi waliokuwa wamesimama upande wa kushoto. Na wao baada ya kuona kwamba gari ya mheshimiwa ilisimama kwa ajili ya wao, Edna ndio aliekuwa wa kwanza kumsogelea mheshimiwa huku walinzi na wao wakimtangulia mheshimiwa, afisa usalama hawa walionekana kuwa makini na kazi yao. “Morning! Mr President” “Morning Edna nimefurahi kuwaona kabla sijaelekea safairi yangu , nadhani kukutana kwenu ni Baraka kwa safari ninayoendeea”Edna alitabasamu. “Asante sana mheshimiwa kwa kuona kukutana kwetu ni Baraka , na nakuombea mafanikiio” “Asante sana Edna”Huku aiwageukia Roma na Dorisi waliokuwa nyuma ya Edna. “Morning Mr President”Alisalimia Dorisi kwa Heshima. “Morning Dorisi”aliongea
Meshimiwa na kumfanya Dorisi atabasamu na kujisikia vizuri kwa kuitwa kwa jina lake , kwani hakujua kama mheshimiwa alikuwa akimfahamu lakini alishangaa mheshimiwa kamfahamu vipi. “Mr Roma , nasikia wewe na Dorisi mmekuwa na mchango mkubwa sana kwa Vexto kwa kufanikisha dili nono , niwape hongera sana , mafanikio ya Vexto ni maendeleao ya taifa kwa ujumla , asanteni kwa mara nyingine” “Mheshimiwa huna haja kunishukuru, mimi sjiafanya kwa ajili ya taifa , nimefanya kumfurahisha mke wangu tu ili azidi kunipenda hayo mengine ni ya ziada”

Aliongea Roma na kumfanya mheshimiwa atabasamu ila Edna alikunja sura alitamani amfinye Roma palepale maana aliona anaongea upuuzi, na hata kwa Dorisi aliona kauli ya Roma haikuwa na maana ila hakutaka kuonesha hali yoyote ya kutokufurahia. “Mheshimiwa nikutakie safari ya mafanikio kwa ajili ya taifa letu”. “Asante sana Edna” Mheshmiwa Senga aliwaacha Edna na yeye akaendelea na safari yake. “Kabwe nipe ripoti”Aliongea Mheshimiwa mara baada ya kuingia kwenye ndege hii kubwa ya shirika la ATCL. “Mheshimiwa hii ndio ripoti iliotoka kwa balozi Ramadhani Japani”Aliongea Kabwe huku akimpatia mheshimiwa Senga Kishikwambi na mheshimiwa alianza kuangalia taarifa hio ambayo ilimfanya macho yake kuwa makubwa kwa kuoneysha mashangao. kwenye Tablet ilikuwa ikionyesha picha mbalimbali za Roma akiwa Kambi ya jeshi Hastiti , lakini kulikuwa na picha ambazo Roma alipiga na mheshimiwa Waziri mkuu wa Japani.

“Kila taarifa ya Roma inayonifikia kila siku inakuwa sio ya kawaida , inanishangaza sana sina taarifa zote zinazomuhusu , hili swala linaniumizakichwa sana Kabwe , hebu jitahidi kuwasiliana na watu wakubwa ndani ya Marekani tuweze kupata mwanga kuhusu huyu mtu” “Sawa mheshimiwa nitalifanyia kazi” “Vipi kuna taarifa yoyote ya Dorisi kuwasiliana na baba yake?”. “Mpaka sasa hakuna mawasiliano yoyote ya Dorisi kuwasiliana na baba yake mheshimiwa , lakini tumegundua kitu ambacho hakipo sawa”. “Nieleze, hayo mambo ambayo hayapo sawa ndio nayataka”. “Mheshimiwa Dorisi anatumia ‘Black Card’ kufanyia malipo” “Hebu elezea vizuri ni kipi hakipo kawaida kabwe” Kabwe alivuta pumzi na kuona kweli maelezo hayo hayakuwa yanatosha , kwani mheshimiwa Senga licha ya kuwa Raisi wa wananchi wa Tanzania , ila Elimu yake ilikuwa ni ya kufoji vyeti na siri hio waliokuwa wakiijua ndani ya Taifa la Tanzania ni watu wachache sana. Ndio mheshimiwa Senga aliishia kidato cha sita tu na akarudi nyumbani kwao Songea na kuanza kuuza viazi vya kuaanga, na kwa wananchi wa Songea ukweli ni kwaba hawakua na taarifa za kutosha kuhusu raisi Senga , kwani Senga baada ya kuuza uza Chipsi huko Matalawe Songea baada ya kumaliza kidato cha sita Songea boys, aliondoka na kwenda kusiko julikana na siku ambayo anarudi tena Songea alikuwa na ukwasi mkubwa wa Pesa huku akiwa ameoa mwanamke aliekuwa akifahamika kwa jina la Blandina na mpaka kupata mtoto wao wa kwanza walikuwa wakiishi Songea na hata kampuni ya usafirishaji wa mizigo ilianzia hapo hapo Songea na ndio kampuni ambayo ilimpa utajiri wa haraka kwa kipindi hicho kwani alikuwa akipokea tenda nyingi sana kutokana na umiliki wa magari makubwa aina ya Scania., Baada ya mheshimiwa Senga kujiunga ndani ya siasa , watu walishangaa Senga kuwa mhitimu kutoka chuo kikuu katika masomo ya ‘political’ kutoka chuo kikuu cha Syndey Australia kwa ngazi ya Degree(Shahada) na Masters(uzaamili) na vyeti vyake vilikuwa ni halali kabisa.

“Mheshimiwa Black Card ni aina ya kadi ambazo zinatolewa kwa mwaliko maalumu na Benk ya Uswis hapa nchini kupitia tawi la Botswana ,Kwa inavyojulikana duniani kote benki hazijaweka vigezo maalumu vya mtu kupatiwa Black Card, na akaunti ya kibenki kukidhi vigezo hivyo ni kuwa na kiwango cha matumizi ya pesa yasiopungua bilioni mbili za kitanzania”Aliongea Kabwe. “Kwa hio Kabwe unamaanisha kwamba ni ngumu sana kwa Dorisi kumiliki akaunti hio? ,ijapokua nahisi muunganiko wa Dorisi na The Don hapa nchini , lakini nashindwa kupata uthibitisho Kabwe , ila nina uhakika wa asiliamia mia moja Dorisi ni mtoto wa The Doni” “Hilo linawezekana kwa Dorisi mheshimiwa” “Kwa hio mmejaribu kufuatilia mmiliki wa Akaunti ya Dorisi?” “Ndio mheshimiwa tumejaribu , lakini kutokana na sheria kali za kibenki za Swiss Bank, wamekataa kutupatia taarifa”.
“Endeleeni kumfuatilia kwa karibu sana , nilikuwa nina mpango wa kumuweka karibu kama mchepuko wangu , lakini naona ni hatari Zaidi kwangu , kwani The Doni anaweza kunishitukia mipango yangu mapema na Senior kanishauri juu ya hili na mimi pia nimeona ni jambo jema , na pia hata kama ningefanya hivyo yule mpuuzi anaonekana kumchanganya Dorisi na mapenzi yake feki”aliongea mheshimiwa. “Sawa mheshimiwa , lakini kwanini tusijaribu kumuuliza Senior kama anaweza kutupatia taarifa zinazomuhusu Roma , yule anakonekeshini kuliko wewe”Aliongea Kabwe.

“Senior amekuwa mgumu sana kunieleza juu ya Taarifa zinazomuhusu Roma na mara nyingi amekuwa wa kuniambia nihakikishe sifanyi jambo lolote kuwa katika upande mbaya na Roma”Kabwe alionekana kumuelewa mheshimiwa na maongezi yao yaliishia pale ndege ilipoanza kupaa mheshimiwa Senga alikuwa akielekea nchini Kenya kwa ziara yake ya siku moja. “Roma jifunze kuwa na majibu mazuri basi unapoongea , hasa na watu wakubwa duniani , nakuambia hivyo sio kama nimekasirika , lakini itakusaidia sana pale ambapo utahitaji msaada mbao unahiraji Koneksheni , hivyo ndio dunia inavyoenda” “Mke wangu , wewe usiwe na wasiwasi , na isitoshe sijamjibu vibaya mheshimiwa , nikweli nafanya haya yote kwa ajili yako , wanasiasa siku zote wana maneno matamu matamu kukuvutia lakini kwangu ni tofauti”. “Lakini hio ndio maana ya siasa , unafikiri mwanasisasa anatakiwa kuongeaje?” “Mke wangu , najua tumeoana , lakini hujawahi kujua nini napenda na kipi sipendi” “Kwa hio wewe unapenda nini na kipi hupendi?” “Hehe.. mke nitajibu nusu ya swali lako , mpaka nijue umenipikia nini?” “Haya jibu” “Kwenye mambo ambayo sipendi moja wapo ni wanasiasa ..mwanasiasa siku zote ni mtu muongo na mimi nachukia uongo” “Unachukia uongo , je wewe husemi uongo?” “Mimi siwezi kusema uongo ,pasipo na sababu , nitadanganya kwa muda tu lakini nitaishia kwenye kusema , ukweli na nafanya hivyo kama mtu ambae anapaswa kuujua ukweli hatoweza kunielewa hata nikimwambia hivyo , au pale ninapoona hawezi kuhimili ukweli , lakini nitaishia kumwambia ukweli mwisho wa siku” “Hebu nniambie mpaka sasa tokea tusajili ndoa yetu ambayo hata mwezi haujaisha , je kwenye kipindi cha muda wote tumekuwa mume na mke kihalali ni wanawake wangapi umelala nao?”Aliuliza Edna na wakati huu walikuwa wakikaribia kuingia ndani ya nyuumba yao wanayoishi Kigamboni. ITAENDELEA. SEHEMU YA 57 Roma alitabasamu na aliona kabisa amejiingiza kwenye mtego wa Edna , na kujilaumu kwa kutokuwa makini na maneno yake , lakini alijiwazia kuwa sheria yake kubwa ni kuongea ukweli pale inapobidi kufanya hivyo. “Nimelala na Dorisi ,Nasra , Rose na Neema Luwazo”Aliongea na kumfanya Edna akunje sura , kitendo cha Roma kujibu swali lake bila hatia kilimuuzi sana na alitamani agonge geti na gari “Bebi wife umeridhika na jibu?” “Ndio”Aliibu Edna na kisha hakutaka maoangezi tena , baada ya kuingiza gari ndani ya uzio , alichukua mkoba wake na kuingia ndani na hakuhangaika hata kuegesha gari. “Bi Wema nimerudi”Roma alimsalimia Bi Wema kwa tabasamu. “Karibu sana Mr Roma nyumbani kwako” “Asante sana Bi Wema nimemisi chakula chako sana”Bi Wema alitabasamu.

“Karibu Mezani Mkeo leo aliamka mapema kukuandalia chai nzito na sasa ipo mezani”aliongea Bi Wema huku akiwa ni mwenye kutabasamu , lakini kwa Roma alishangaa kidogo , alijua Edna alikuwa akitiania alivyosema amemuandalia chakula. Roma alijongea mezani huku akiwa na hamu ya kujua ni kipi Edna awamu hiia amepika. “Bi Wema kaandaa Edna hizi tambi?”Aliuliza roma baada ya kula kidogo , alishangazwa na tambi hizo kuwa nzuri licha ya kwamba hazikuwa tamu kwa kiwango cha juu lakini zilikuwa tamu. “Ndio Miss amekuwa akijifunza kupita tokea uondoke na amesema amepata rafiki anaemfundissha kupika”
Roma alijikuta akizidi kushangaa , alijiuliza ni rafiki gani huyo Edna mke wake amempata , kwani kwa namna ambavyo mke wake alikuwa kauzu, ilikuwa ni ngumu sana kuwa na marafiki kwani hata Dorisi ambaye alikuwa ni rafiki yake walionekana kama sio marafiki. “Bi Wema ni rafiki gani Edna kampata?” “Mimi sifahamu lakini ninachofahamu ni kwamba huyo rafiki yake ni mwalimu mpya ndani ya shule ya kituo cha kulelea yatima”. Roma alitingisha kichwa hakutaka kuuliza sana maswali , lakini alikuwa na shauku ni rafiki Gani Edna kaweza kumpata ndani ya muda mfupi aliosafiri kuelekea Japai , alishangaa. ***** Upande mwingine ndani ya makao makuu ya kampuni ya JR alioneakna Abuu akiwa ameketi kwenye kiti chake huku sura yake ikiwa katika hali ya wasiwasi sana na jambo ambalo lilimfanya bwana huyu kuwa na wasiwasi ni kutokana na Hisa za kampuni yao zinavyoendelea kushuka , kutokana na kushindwa kusaini mkataba wa Dili la Yamakuza, akiwa amekalia anaangaia tarakishi yake iliokuwa ikimuonesha chati ya Candlestick . Mlango wa ofisi yake ulifunguliwa na alionekana Isack Makamu wa raisi wa Makapuni haya ya JR, huku mkononi akiwa ameshikilia karatasi. “Kuna nini Isaack?” “Abu kuna swala hapa ambalo sio la kawaida” “Unamaanisha nini?”Aliuliza na Isack alimpatia Abu karatasi aliokuwa ameshikilia. “Kama unavyona kwenye hio orodha ni baadhi ya watu ambao wamenuunua Hisa zetu baada ya kushuka kwa Thamani , lakini kuna mtu anaejiita Athena anaonekana kununua kiasi kikubwa sana cha hisa na hii ni hatari kwa kampuni , kwani mpaka sasa mtu huyu ana asilimia Zaidi ya therahini za umiliki wa kampuni”Abu macho yalimtoka , aliangalia na ni kweli kuna mtu kanunua hisa zao kwa kiwango kikubwa sana Zaidi ya bilioni mia mbili. “Kana hisa zikiendelea kushuka Thamani kwa muda wa wiki , anaweza kununua Zaidi”Aliongea Abu. “Ndio , inatakiwa kuwa na mpango wa kutatua hili tatizo zisishuke thamani Zaidi ya hapa” “Huyu mtu unafikiri a anampango gani wa kununua hisa zote hizi?”Aliuliza Abuu “Kuns mawili hapo huenda anataka kuwa na sehemu kubwa ya umiliki wa Kampuni , pili labda ni mtu ambaye ana matarajio chanya ya hisa za kampuni yetu kupanda thamanni baadae ,hivyo anatafuta faida” “Okey Isack , lakini lazima tuwe makini na pesa yote hii ambayo imeingia kwenye Kampuni yetu , jaribu kutafura namna ya kuwasiliana na huyu mtu , ili tuweze kujua nia yake”

“Sawa boss” Baada ya Abuu kuongea na Isack ,aliingia marasta . “Vipi Seif anaendeleaje Jose?” “Anaendelea vizuri , bado yupo hospitalini anaendelea kuongezea Glucose na virtubisho mbalimbali ili mwili kupata nguvu” “Okey Kazi nzuri” “Lakini Boss hujaniambia , kwanini tunamtibu kizee kama yule?, sio kawaida yako” “Jose wewe fanya kama ninavyoelekeza na acha maswali megni sawa” “Sawa Bosi, Halafi Roma asharudi nchini leo asubuhi , kapokelewa na mke wake uwanja wa ndege na waliongea na Raisi”.Abu alitafakari kwa muda. “Okey , waambie vijana waendelee kumfatilia kwa kila kitu anachokifanya na nataka taarifa zote zinazomuhusu” “Sawa bosi” Baada ya Marasta kutoka , aliingia Elvice ndani ya ofisi hii na kumfanya Abu atabasamu na kumkaribisha. “Halafu Elvice haujaniambia kwanini mpango wa kumteka Edna ulishindwa kwa mara nyingine wakati nikiwa Japani , nilisahau hata kukuuliza maana niikuuwa nimechanganyikiwa. “Nilituma vijana wangu kama kawaida , kutoka jeshini , lakini jambo la kushagnaza ni kwamba mpaka sasa sijui walipo , kwani mara ya mwisho niliwasiliana nao wakiwa nje ya nyumba ya Edna”Abuu alishangaa. “Kwahio unamaanisah kwamba wamekukimbia au imekuwaje , sijaelewa mpaka hapo”. “Sio wamekimbia , nilijaribu kufatilia kupitia polisi na majibu nilioyapata ni kwamba waliingia kabisa na kuwadhibiti walinzi wa Edna , lakini kwa maelezo ya polisi waliofika kwenye tukio ,Edna alieleza kuwa walidhibitiwa na Wazungu na kisha wakawabeba na kuondoka nao” “Mh! , hii inaweza ikawa shida kwa upande wetu Elvice kama watakutaja?” “Hawawezi , ni vijana kutoka jeshini ninao waamini sana na nina uhakika hawawezi kuniuza nimewatumia katika kazi nyingi”Abuu alitikia kwa kichwa kuonesha kuwa amekubali jibu hilo. “Mpango wetu ni wikiend hii?” “Ndio bado siku mbili tu kumuondosha yule shetani , japo bado nina wasiwasi?” “Hupasi kuwa na wasiwasi , licha ya kwamba ulisema alibadillika kama shetani , lakini naamini Roma ni mwanadamu na hawezi kupona na risasi ya moyo” “Naunga mkono hoja , cha msingi ni kuhakikisha tunamwandalia mazingira seif mazuri ya kufana kazi” “Hilo muhimu” *****

Ni Kaskazini mashariki ya Kiimwa kimwe na Kaskazini Mashariki ya Kirawe katikati ya haya maeneo ndipo ilipo Ikulu ya Wananchi wa Kenya , makazi ya mtawala wa Kenya aliemadarakani ndugu Kamau Kamau. Ndani ya jengo hili ndani ya chumba wanachotumia kulala wanandoa, yaani mheshimiwa Kamau Kamau na mke wake Maina aliemaarufu kama ‘First lady’. Alionekana mheshimiwa Kamau Kamau kwenye kioo kikubwa huku akiwa anaweka suti yake sawa huku nyuma yake akiwa amejilaza mke wake Maina. “Blandina , utamuepuka mpaka lini Senga , jambo hili linanikasirisha mara kwa mara, na kumuepuka kwako kunanifanya nione bado una hisia nae” “Kamau hayo ni mawazo yako , ni miaka mingapi mpaka sasa tuwepamoja?” “Miaka ishirini na tano ya ndoa yetu” “Sasa nimeishi kwa miaka yote hio na wewe , kwanini bado hujiamini kama nakupenda?” “Sio sijiamini Blandina , lakini huyu ni kiongozi na inapaswa tumpokee kwa pamoja, nataka ujiamini mbele ya Senga”.
“Sio kama sijiamini mbele ya Senga , lakini wewe ndio umenifanya kuwa hivi , miaka ile nilivyokuambiaa tumuambie Senga ukweli wote ukataka tumfiche huku ukinilazimisha kuishi kwa sura bandia , unafikiri napenda eh”Alianza kulia. “Am sorry Blandina , yote nimefanya kwa ajili yako na mapenzi yetu , sikutaka Senga ayaingilie” “You are Selfish Kamau , its always you as you , kwanini unaijali sana nafsi yako kuliko yangu Kamau , ni mapenzi ya aina gani hayo unayo juu yangu ,nimekuwa wakuishi kwa mateso miaka na miaka Kamau, lakini mpaka sasa hats mtoto wa kutoka kwenye tumbo langu sina….”Aliongea na kulia mno mwanamke huyu.

“Nisamehe sana Blandina ,, najua umeishi na mimi miaka na miaka na umekuwa ni mwenye kunifariji , huku ukiacha kuziishi ndoto zako , ni mapenzi makubwa sana ambayo umenipatia , Blandina naahidi baada ya mimi kustaafu I will make evertihing up for you mpenzi , nakupenda sana na nitaendelea kukupenda naomba usinikatie tamaa mapema hivi mke wangu sawa mama” Kamau alionekana kumbembeleza mwanamama huyu ambaye ana majina mawili , yaani lile la Maina , ambalo lilikuwa likifahamika na watu wengi kama mke wa raisi , lakini pia alikuwa akifahamika kama Blandina , jina ambalo ni watu wachache sana waliokuwa wakilifahamu, na pia ni watu wachache ambao walikuwa wakijua kuwa Maina waliekuwa wakimjua ni feki. Baada ya kubembelezana muda mrefu ,Maina kinyonge alikubali kujiandaa kwa ajli ya kuelekea uwanja wa ndege kumpokea Raisi senga, ambaye atakuwa hapo nchini kwa ziara ya siku moja. Ni ndani ya nusu saa wanandoa hawa na baadhi ya viongozi wajuu walikuwa ndani ya uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyata kusubiria ujio wa Raisi senga. Ilichukua takribani dakika kumi kwa ndege ya ATCL kutua na kusimama kabisa na pia kutoka kwa mheshimiwa Senga. Maina alijikuta akigonganisha macho na Senga na Senga na yeye alimwangalia Maina huku kwenye kichwa cha Maina mambo mfululizo yakipita , haikueleweka mwanamke huyu alikuwa akifikiria nini kwa wakati mmoja .

SEHEMU YA 58 YA SIMULIZI

Mheshimiwa Senga baada tu ya kushuka kwenye Ndege alianza kusalimiana na mwenyeji wake Raisi Kamau ,aliekuwa ameambata na mke wake Maina . Muda wote Maina alikuwa akimwangalia Senga , mwanamama huyu alionekana kuwa na majuto makuu , alionesha hali ya kujutia kwa kitendo cha kujivika sura bandia ili mradi asifahamike uwepo wake duniani kwa Senga.

Senga nae licha ya kwamba alikuwa akisalimiana na viongozi mbalimbali wa juu wa taifa hili la Kenya , lakini akili yale ilikuwa kwa Maina ,Senga alikuwa akijihisi kitu cha ajabu kila anapokutana na mke wa raisi mwenzake , hakujua ni kwanini anapata hisia ambazo ni kama amezisahau katika maisha yake . "Karibu sana Kenya Mheshimiwa Senga" "Asante sama Komredi , kila ninapokuja ndani ya taifa hili hua natoka na kitu kipya ni kama kuna nguvu ya Kimungu iliopo ndani ya hili taifa, nakiri Kenya imebarikiwa sana" "Hahaha.. ni kweli ,Senga hata mimi mara ya mwisho kuja Tanzania niseme nilijisikia Amani na natamani baada ya kuachia madaraka nihamie Kwenye nchi yako" Aliongea Kamau na kwa namna ambavyo alikuwa akionekana kuongea usingemdhania kuwa alikuwa akificha mengi moyoni . Waswahili wanasema Moyo wa mtu ni kichaka, na hili ndio lililokuwa likijidhihirisha mbele ya Maraisi hawa wa nchi jirani. Baada ya salamu na mapokezi ya aina yake ya Raisi Senga hatimae walianza mazungumzo yao baada ya kuingia ndani ya Ikulu. "Senga umekuwa sio wa kuambatana na mkeo mara kwa mara unapofika Kenya Au Damasi anakataa kuja Kenya , nimemkumbuka sana " "Kamau yule mwanamke acha tu ni mvivu kupindukia na hapendi sana kuonekana hadharani na hio imekuwa tabia yake tokea namuoa". "Ndio nakumbuka sana ,Sema tumetoka mbali sana Senga, ile mitihani tuliopitia kipindi kile katika kutafuta maisha ilikuwa ni ya aina yake , nakumbuka kila hali ilivyokuwa mbaya kwako na kujihisi kukata tamaa, Blandina ndio aliekuwa akikutia nguvu na neno moja la Blandina kwako la faraja ,ulionekana kuwa mpya na kupambana zaidi".

"Umenikumbusha mbali sana yaani, kama sio Blandina kufariki kwenye ile ajali pamoja na mwanangu Denisi huenda maisha yangu yangekuwa ya tofauti sana"Aliongea huku akiwa ni mwenye Huzuni na muda huo hio aliingia Maina. Maina alionesha hali ya kutojiamini kabisa mbele ya raisi Senga , alikuwa ni mwenye kukwepesha macho kila mara wanapoangaliana. "Maina niseme sana Asante kwa kujenga kile kituo kule Bagamoyo , hakika kimesaidia sana jamii ya wenye uhitaji , kimekuwa tumaimi kwa watoto ambao walipoteza wazazi wao wakiwa wadogo". Asante sana Senga , moyo wangi unafarijika pale ninapo ona watoto wakiwa na furaha na kuishi katika mazingira salama" "Ni kweli mchango wako kwa jamii za Afrika ni mkubwa sana na unapaswa kupewa tuzo"Maina alitabasamu namuda wote Kamau alikuwa akiwaangalia wawili hao walivyokuwa wakiongea ni kama alikuwa akitafuta jambo flani kupitia kukutana kwao. Kwa namna ambavyo Senga alikuwa akiongea na raisi Kamau mabwana hawa walionekana kuwa na stori yao ambayo bado watu hawakua wakiifahamu, kwani kwa namna ambavyo waliweza kukumbushiana mambo yaliowatokea miaka ya nyuma , ilionekana walifahamiana kabla hata ya kufanikiwa

,haikueleweka mara moja ilikuwaje mpaka wote wakawa maraisi. "Sijajua kwanini najisikia wa tofauti kila ninapokutana na Maina".Aliwaza Senga huku akiwa ameshilia picha ilioonekana kuchakaa , picha ambayo ameitoa kwenye mfuko wa koti lake ,ni picha ambayo ilikuwa ikimuonesha mwanamke mrembo , licha ya kwamba picha hio ilikuwa imechakaa , lakini mwanamke aliekuwa kwenye pivha hio alikuwa akionekana vyema kwa urembo wake. *** Roma baada ya kumaliza kunywa chai ilioandaliwa na mke wake Edna , aliingia chumbani kwake na ndani ya madakika kadhaa alionekana kubadilisha nguo na sasa alikuwa amependeza huku mkononi akiwa ameshikilia ufunguo wa gari yake .
“Bi Wema mimi natoka kidogo nitarudi jioni”Aliongea Roma na Bi Wema akaitikia. Wakati Roma anatoka Edna kama kawaida yake alikuwa juu ya Balconi akimwangalia Roma ambaye alikuwa akielekea uelekeo wa yalipokuwa yakiegeshwa magari. “Zishaamka , yaani sijawahi pata ona mwanaume Malaya hivi , kama wanaume wote wako hivi , bora hata mimi niliolewa kwa mkataba, katumia zaidi ya siku tatu zote kuwa na Dorisi lakini saivi pale ni kwenda kutafuta mwanamke mwingine”Aliwaza Edna huku akiangalia Gari ya Roma inayotokomea nje . “Nimemmisi Rose , japo ni asubuhi ngoja nikaonanane nae”Aliwaza Roma huku akikanyaga pedeli kuchanja mbuga kuelekea Mbagala. Dakika chache mbele kama nusu saa hivi , Roma alikuwa akiingiza gari ndani ya Club B. Aliegesha gari yake na moja kwa moja aliingia kwenye Bar hii ambayo wakati wa mchana ni wateja wachache sana wanaokuwepo hapo.
“Mr Roma karibu sana”Aliongea Zonga mara baada ya kumuona Roma akiingia hapo ndani , lakini Roma kuna kitu alikiona kwenye macho ya Zonga , aliona hali ya wasiwasi. “Rose yuko wapi na mbona leo naona hali ni kama nisivyoizoea?” “Ndio Roma na bora hata umekuja , kwani Boss yupo kwenye hali mbaya” “Nini kimempata Rose?” aliongea Roma kwa kushangaa huku akianza kupiga hatua kuelekea ilipo ofisi ya Rose. “Boss yupo nyumbani kwake kajeruhiwa na risasi ya tumbo”Aliongea Zonga na kumfanya Roma ashangae na kuwa na wasiwasi pia , aligeuza na kutoka nje na kisha akaingia kwenye gari na kuipeleka mpaka ilipo nyumba ya mwanadada Rose. Baada ya kuingia hapa ndani ,aliona kweli Rose alikuwa kwenye shida , kwani kulikuwa kimya mno , kiasi ambacho ungedhania kuwa wenyeji wamehama. “Rose!”Aliita Roma mara baada ya kuingia kwenye sebule hii kubwa na kumkuta Rose ambaye amejilaza kwenye sofa huku akionekana kupauka kweli , ule uzuri wake ulikuwa umefifia na huyu alikuwa ni Roze anaeumwa. “Huby!”Aliitikia Rose kwa sauti dhaifu na kumfanya Roma amuonee huruma mchepuko wake. Roma baada ya kumsogelea , hakutaka kuongea sana alivuta juu blazia aliokuwa amevalia Rose na kuangalia jeraha la Risasi , na hapo Roma alijikuta akikumbuka siku alioingia Tanzania kwa mara ya kwanza ,alianza kukutana na Rose akiwa kwenye hali mbaya , hali ambayo ilikuwa ikifanana na hii anaiona sasa , kwani sehemu aliojeruhiwa Rose ni hio hio. “Kwanini hujaenda hospitalini?” “Ni jeraha la risasi , sikutaka kwenda hospitalini ingeleta shida kwa upande wangu na pia maadui zangu wangenimaliza kabla hata sijapona” “Unamaanisha nini, mbona unaongea kama upo kwenye Vita?”Aliuliza Roma na Rose alionekana kusikia maumivu makali akongea na alijikuta akikohoa na Roma alilitambua hilo , na alichokifanya ni kumuwekea Rose mkono kwenye shavu la kulia na kushoto na palepale Rose alifumba macho , ni kama amepewa sindano ya ganzi. Roma baada ya kuona Rose kalala , alienda mpaka jikoni na kisha akachukua kisu na kurudi nacho sebuleni, baada ya kukaa alifyonza kidole chake na kisha akamuweka Rose kwa kumlaza chali na kisha akafunua blazia na kutoa bendeji iliokuwa imeloana na damu nyingi. Roma alichukua kisu na kuchana kiganja chake kwa kutumia kisu na damu zilianza kumtoka na hapohapo akasogeza mkono wake usawa wa jeraha la Rose na damu ile kuingia kwenye jeraha. Ilikuwa ni kama kidonda cha Rose kilikuwa kikiungua kwa moto kwani ile sehemu ya jeraha kadiri Roma alivyokuwa akiruhusu damu kuingia , mvuke flani hivi mfano wa moshi ulianza kutoka , Roma alikata kiganja kingine na akaweka tena na mvuke ulizidi kuongezeka na ndani ya dakika tano alikuwa ashamaliza na sasa jeraha la Rose lilianza kuvutana na lilionekana kufunga taratibu na kadri dakika zilivyokuwa zikisogea ndipo jeraha lilipozidi kujifunga na ndani ya dakika kumi tu , ile sehemu iliokuwa na jeraha ilifanana na sehemu nyingine za mwili.

“Bebi Rose sasa hivi damu yako sio ya kawaida , umekuwa mtu wa kwanza kuhimili damu yangu yenye maambukizi ya kirusi kwa Zaidi ya mara mbili” . Aliongea Roma huku akiwmangalia Rose aliekuwa amelala bila ya fahamu. “Roma!!”Aliita Zonga aliesimama mlangoni , akimwangalia kwa hali ya wasiwasi , haikueleweka alisimama hapo kwa muda again.

NINI KITAENDELEA

SEHEMU YA 59

Zonga haikueleweka amefika mlangoni hapo saa ngapi ,Roma alimwangalia na kumuona akiwa na wasiwasi. “Kuna nini Zonga , mbona unaonekana kuwa na wasiwasi?”. “Baba yake Rose , kafika na kundi lake la Fupa Faru” “Roma hakuwa akimuelewa Zonga anamaanisha nini kwani hakuwahi kusikia kuhusu Fupa Faru”

“Fupa Faru ndio watu gani?” “Ni kundi analomiliki baba yake Rose”Aliongea Zonga na hapo ni kama Roma alipata mwanga,alimwangalia Rose kwa dakika na kisha akaangalia kidonda na kuona kashapona , alimuwekea tena mkono na Rose akashituka. Zonga aliekuwa amesimama mita kadhaa kutoka alipokaa Roma na

Rose alijikuta akishangazwa na namna bosi wake alivyoamka akiwa na hali ya utofauti. “Hubby!”Aliita Rose huku akijishangaa kutokuhisi maumivu yoyote na Roma alimwangalia huku akiwa na tabasamu. Rose alianza kujikagua jeraha lake na kitendo hiko kilimfanya Zonga amsogelee na kumwangalia. “Boss!”Aliita Zonga kwa mshangao , kwani ni kama alikuwa ndotoni , hakuamini kile alichokuwa akikiona kwa macho yake. “Inawezekana vipi hii , Boss si ulikuwa na jeraha tumboni la Risasi , limeenda wapi?” Rose alikuwa kama Zonga tu , licha ya kwamba jambo hilo lilikuwa ni mara ya pili kutokea kwake , lakini bado hakuwa akijua lilifanyikaje. Upande wa Roma ile sehemu ambayo alijikata ni kama haikuwa na alama yoyote ile , ilikuwa imejifunga kabisa na hakukuwa na dalili ya kuchanwa Zaidi ya ushahidi wa kisu kilichokuwa kwenye meza ya kioo. Roma aliwaangalia wawili hawa walivyokuwa wakishangaaa na kuwa na maswali mengi katika vichwa vyao. “Bebi umenifanyia nini nikapona haraka?” “Rose usiulize maswali mengi maana hata nikikueleza hautaelewa , wewe chukulia tu ni kama Mungu kakufanyia miujiza”Aliongea Roma na kumfanya Zonga azidi kushangaa. “Boss ! Baba yako kafika na kundi lake la Fupa Faru”Aliongea Zonga baada ya akili yake kufanya kazi na kukumbuka kuwa aliacha watu Bar. Rose alimwangalia Zonga akageuza macho kwa mpenzi wake Roma na Roma akatabasamu.

“Zonga nakuja muda si mrefu nenda kawahudumie na angalia vijana wetu wasilete shida ikatokea vurugu”Aliongea Rose na Zonga alisogea tena kumkagua bosi wake , ni kama bado hakuwa akiamini alichokuwa ameona. “Bosi , unauhakika hausikii maumivu yoyote?”Aliuliza Zonga na Rose alimwangalia Roma na kisha akamtingishia kivhwa Zonga kwamba hna aina yoyote ya maumivu , licha ya sehemu hio kuwasha pekee.Zonga alitingisha kichwa na kisha alitoka. “Nakumbuka hii ni mara ya pili Roma kuniponya kimiujiza , miezi ile niliishi kwa mawazo sana kwa kukufikiria , umewezaje kuniokoa na pia ukaniponya kwa wakati mmoja”Aliongea Rose huku akianza kutokwa na machozi , alionekana alikuwa akikumbuka kipindi kile Cha nyuma baada ya kuokolewa na Roma Ramoni. “Usiwaze sana Rose kuhusu yaliopita , chukulia yote yaliotokea ni miujiza na usiulize maswali mengi”Aliongea Roma akiwa siriasi na alizidi kumfanya Rose atoe machozi. Ndani ya moyo wa Rose alikuwa akifikiria vitu vingi , lakini kubwa Zaidi alikuwa akiwaza , kwanini mwanaume aliekuwa akimpenda, aliekaa mbele yake kumfanyia mambo makubwa kama hayo , kwani alikumbuka kama sio yeye angekuwa ashauliwa na watu wa baba yake. “Rose Acha kulia”aliongea Roma baada ya Rose kumkumbatia ghafla. “Nimeacha hubby , ni kwamba sijui namna ya kukushukuru Roma , umenipa uhai Zaidi ya mara mbili , sijui nini nifanye kwa ajili yako”.

“Bebi Rose , wewe usifikirie cha kunifanyia , unachopaswa kufanya ni kunipenda na mimi nitahakikisha na kulinda na lolote baya lisikufikie , ukitaka niue kwa ajili yako wewe sema nani unataka afe na sababu ya kifo chake na mimi nitamtanguliza mbele za haki” Rose alijikuta moyo wake ukipata joto ambalo sio la kawaida , ni kama ameongezewa kikombe kingine cha damu kwenye chemba ya moyo wa kulia,alimuona Roma kama mwanaume ambaye anampenda kwa mapenzi ya dhati kabisa na alishindwa kuelewa inakuwaje Roma akampenda namna hio halafu akaoa mwanamke mwingine , lakini hakutaka kuuliza , yeye alijiambia katika maisha yake atashukuru kwa nafasi ambayo atakuwa nayo ndani ya maisha ya Roma na hatofanya jambo lolote kumkasirisha. “Rose Fupa Faru ndio kundi gani , sijawahi kulisikia?”Roma baada ya kuuliza swali hilo Alimfanya Rose kuwa mnyonge. “Uliponiokoa kipindi kile , watu waliokuwa wakitaka kuniua ni hawa Fupa Faru”Roma alishangaa. “Kwa hio unamaanisha Baba yako ndio aliekuwa anahusika na kujeruhiwa kwako siku ile na yeye ndio kaagiza watu kukuua?”

“Ndio mpenzi na hata jana yake ndio hao hao walioniwinda , wakati nilipokuwa Mtwara nikipokea mzigo wangu wa Madawa kutoka Columbia kupitia bandari ya Mtwara” Roma alijikuta akipandwa na hasira , yaani ile hamu ya kuua mtu ilianza kuutekenya mwili wake , alijiambia hao watu wote wanahitaji kutangulizwa , kwanini wamdhuru mpenzi wake , lakini pia alimuonea Rose huruma kwa wakati mmoja , hakuelewa ni kwanini baba yake Rose alikuwa akimuwinda mtoto wake hivyo. “Rose naamini kuna jambo kubwa ambalo lipo kati yako na baba yako , na nitahitaji kulifahamu , lakini sio sasa unapaswa

kwenda kuonana nao wanataka nini na nitakuwa na wewe na wakileta jambo lolote la kijinga nitamuua mbele ya macho yako na hutoweza kunuzuia , Mimi Roma Ramoni nasema hivi kwenye maisha yangu sitokuja kuruhusu mwanamke wangu anaguswa na mtu yoyote yule , labda niwe mfu, hivyo bebi Dorisi jipige kifuani , upo na mwanajeshi hapa” Aliongea Roma akiwa siriasi jambo ambalo lilimfanya kuhisi utamu usioelezeka kwenye mwili wake na kuhisi vishoti vikiushitua mwili wake na kupandwa na hisia , alitamani amvue Roma nguo naanze kuimba na maiki. Rose aliingia chumbani kwa ajili ya kuoga na kujiandaa kwenda Club B ili kukutana na kundi la Fupa Faru ,Roma yeye alitangulia , alitaka kwenda kukutana na huyo anaejiita baba yake Rose. Roma baada ya kuingia ndani ya Bar ya Club B alikutana na Zogo la watu waliokuwa wamekaa kwenye meza huku wakiwa na chupa za bia kila mmoja , kwa kila meza ilikuwa na watu watatu watatu.

Watu waliokuwa hapo ndani wote walikuwa wapo kwenye mavazi ya suti , na ilionekana kwa kundi hilo la Fupa Faru , suti zilikuwa ndio sare zao. Kwa namna ambavyo walikuwa wakionekana ni dhahiri kwamba walikuwa wapo tayari kwa kuanzisha vurugu muda wowote. Baada ya Roma kuingia , watu hawa walimwangalia kwa macho ya kujiuliza maswali , walionekana walikuwa wakimjua vema Roma. “Boss , haka ndio kajamaa kanakomnyandua Rose”aliongea bwana mmoja aliekuwa amekaa meza moja na bwana mmoja ambae alikuwa amevalia jeans na koti la suti ya Bluu na ni yeye pekee ambaye alikuwa amevalia mavazi tofauti, nadhani ni kwa ajili ya kuonyesha kwamba yeye ndio aliyekuwa kiongozi wa kundi hilo. Mzee huyu alinyanyua macho yake na kumgeukia Roma , alimkagua kutoka chini mpaka juu na kujiuliza ili kuwaje mwanae Rose kuwa na mwanaume wa kawaida namna hio. “Bosi anaonekana kuwa wa kawaida sana , hata mimi namfaa Rose Zaidi kuliko yeye”Aliongea huyu bwana aliekuwa na mwanya uliosababishwa na kuong`olewa jino na Roma alimsikia kejeli zake zote, lakini hakutaka kufanya nae fujo , alimuacha aongee atakavyo.

“Oya wewe Mse***ge unaweza kweli hata kumridhisha Rose wewe?”Jamaa baada ya kuona Roma kamuacha na kejeli zake , alinyanyuka na kumsogelea Roma kibabe m kiasi cha kumfanya Roma ageuze pembeni uso wake , kwani alikuwa ananuka mdomo isivyo kawaida. Unajua ndani ya hili eneo sio kwamba waliokuwa wamekaa ndani ya Bar ni Kundi la Faru Tembo pekee , watu wa Tembo waliokuwa wakimilikiwa na Rose pia walikuwepo upande wa kulia kwa mbele na walikuwa wakisikilizia tu wenzao waliamshe na wao waalianzishe . Utofauti wa kundi la Tembo na hawa wa Fupa Faru ni umri , kundi la Rose lilikuwa lina vijana wengi , ambao muda wowote walikuwa tayari kumlinda bosi wao na kudni la Faru ambalo linamilikiwa na baba yake Rose lilikuwa na wazee

wengi , hili inaonesha ni kutokana na kwamba mzee huyu alianzisha miaka mingi kundi lake. Hasara kubwa ambayo ipo kwa kundi la Rose ni kwamba vijana wake walikuwa hawana uzoefu mkubwa na kazi na kundi la baba yake walikuwa na uzoefu mkubwa wa kazi.
Baada ya dakika kadhaa kupita hatimae Rose aliingia hapa ndani na kufanya watu wote wa Fupa Faru washangazwe na uzima wa Afya wa Rose , kwani walikumbuka kabisa Rose walikuwa wamemjeruhi pakubwa na walitegeea kumkuta katika hali ya kufa. “Bosi anaonekana mzima , unafikiri mpango wetu utafanikiwa?”aliuliza Pengo akimwangalia bosi wake ambaye licha ya kuvuta sigara , alionekana kuwa katika mashangao , kwani anavyomuona Rose ni tofauti na vijana wake. “Umekuja kufanya nini hapa Situ”aliongea Rose akiwa katika hali ya kuwa siriasi kiasi kwamba usingedhani wawili hao ni kitu na baba yake , na Rose alimwita mzee huyu kwa majina yake. “Rose mimi na wewe ni adui kwenye upande wa biashara zetu , kwasababu ulinisaliti miaka ya nyuma , lakini tukitoka kwenye biashara , wewe ni mwanangu , na pale unapopatwa na matatizo napaswa kuja kukutembelea”Aliongea na kumfanya Roma amuone mzee ni mnafiki sana. “Sina haja ya kusikiliza unafiki wako Situ , huwezi kuja kuniona wakati uliagiza vijana wako wanidhuru, na kuchukua mzigo wangu nilioulipia gharama nyingi, unataka kunizorotesha ili uchukue nafasi yangu ndani ya ukanda wa pwani , hilo halitoweza kutokea” Hapo ndipo Roma alielewa kwanini Rose alikuwa akionekana kama alikuwa kwenye vita baada ya kumkuta kule nyumbani kwake. “Sina budi kufanya hivyo Rose , licha ya wewe ni mwanangu wa kike lakini katika biashara zangu wewe ni adui , kwasasa nimetoka Mwanza nataka niweke makazi yangu ya kibiashara hapa ,nilikupa pendekezo ya wewe kuwa chini yangu lakini ukakataa” “Situ jimbo langu la Kisarawe na Kibiti ulilolichukua huku ukiua raia wengi nasema nitalipiza kisasi na nitachukua jimbo langu na biashara itaendelea kama kawaida”. “Kama unauwezo huo jaribu Rose , ila leo sijaja kwa ajili ya mazungumzo ya biashara nimekuja hapa na taarifa nzuri sana mimi kama baba yako”. “Jakuna neno ambalo ushawahi kuongea likawa taarifa nzuri kwangu Situ”

“Rose wewe ni mwanangu na nusu ya damu yako ni ya kwangu na hilo huwezi kulikataa na kwakua una damu yangu ndio maana nipo hapa , taarifa niliokuja nayo ni kwamba nimekutafutia mchumba , achana na hiki Kibwengo hapa kinakupotezea muda na kukuzeesha tu” Aliongea Situ ambaye ni baba yake Rose kiongozi wa kundi la Fupa Faru na kumfanya Rose aone baba yake kachanganyikiwa. “Haahahaha…Hahahaa… Situ nafikiri unazeeka vibaya , unaongea upuuzi Situ , na hiko unachokisemea hakitakuja kutokea”Mzee alitabasamu kwanza na kisha akavuta sigara yake na kutoa moshi kidogo na kisha akamwangalia mwanae. “Sikia Rose najua unaongea tu kwasababu hujamuona mwanaume ambaye nataka awe mume wako , sikulazimishi kuolewa nae , ila wiki ijayo uje Kisarawe tutafanya sherehe ya kusherehekea ushindi wa kupata jimbo la kisarawe na siku hio Mumeo mtarajiwa atakuwepo na nipo hapa kwa ajili ya kukupatia taarifa hizo , hakikisha unakuja siku ni jumamosi wiki ijayo saa mbili usiku ,ndani ya jumba lako la kifahari ambalo sasa ni mali yangu”Aliongea Situ na kisha akamgeukia Roma. “Dogo tafuta wa saizi yako , pambana utoe harufu ya jasho , huna uwezo wa kuwa na Rose”Aliongea Situ huku akimpiga piga Roma vikofi mashavuni na siku hii haikueleweka Roma alikuwa akifikiria nini wala kakutwa na nini , kwani alikuwa mpole mno na alimwangalia Situ mpaka akitokomea kwenye mlango na kundi lake ambalo wote walichekeshwa sana na maneno ya bosi wao yalioelekezwa kwa Roma.

“Hubby Am Sory”Aliongea Rose huku akimkumbatia Roma kwa Mbele , Rose alikuwa Romantic mno na kwa namna ambayo alikuwa amemkumbatia Roma kwa kuweka mikono shingoni iliwafanya wa vijana wake wa kazi waamwangalie Roma. “Huyu fala anakojolea pazuri, mimi kwa uzuri wa bosi nadhani nikiingiza tu nilazima zinitoke”Aliongea bwana mmoja hivi alienyoa kiduku na kufanya wenzake wacheke. “Utaenda kwenye hio sherehe yao?”Aliuliza Roma. “Ndio bebi lazima niende nina mpango wa kurudisha jimbo langu la kibiashara siku hio, kuna mpango nishauandaa tayari”Aliongea Rose. “Tutaenda wote”Aliongea Roma na kumfanya Rose atabasamu na akambusu Roma kwenye lipsi na kufanya hali ya iwe mbaya kwa vijana wake. “Bosi unadhani atakuja?”Aliuliza Pengo mara baada ya kuingia kwenye gari na bosi wake Situ.
“Kwa ninavyomjua Rose lazima aje na lazima atakuwa na mpango wa kurudisha Jimbo lake , nataka siku hio iwe ndio mwisho wa maisha yake , nimemkosa kosa sana awamu hii sitaki ujinga kabisa , wasiliana na Hassani kabisa kusiwe na udhuru wowote kwa vijana wake”Aliongea Situ na alionekana alikuwa na mpango wa kumdhuru Rose kwa kushirikiana na kundi la Black Mamba. SEHEMU YA 60 Roma Na Dorisi walipewa mapumziko ya siku mbili kabla ya kurejea kazini , hivyo Roma muda wote alibakia nyumbani , kiufupi hakukua na jambo kubwa sana ambalo lilikuwa limetokea ndani ya siku nzima. Edna alionekana kuwa bize sana tokea Roma
arudi nchini , Roma mwenyewe alishangazwa na ubize wa nke wake, Edna alikuwa akirudi usiku sana kwani alikuwa akifanya kazi Overtime,Kwa Roma hakutaka sana kumuuliza nini kinaendela kwenye kampuni mpaka mke wake kuwa bize kiasi hicho.

Siku ya ijumaa nzima Roma hakuwa ameonana na Edna , kwani ile anaamka mwanadada huyu alikuwa tayari ashaenda kazini. Roma jambbo hili lilikuwa likimshangaza sana , hakuelewa Edna ni mwanamke wa aina gani , kwani alikuwa na pesa nyingi lakini alikuwa akifanya kazi Zaidi ya wale waliokuwa hawana hela na pia wafanyakazi wake yaani yeye ndio kama ameajiriwa. Edna na Bi wema ni kama walikuwa wamesahau tikio la wao kuvamiwa , kwani Roma hakuwa na taarifa nalo , hakuwa akijua kama kuna watu ambao walikuja kuingia ndani ya nyumba yake, kwani hata jeshi lake hawakumpatia taarifa na Roma hakuwa ameenda kuwatembelea, alijiambia katika nafsi yake ngoja awape muda kidogo wa kufanya uchunguzi , ili akienda kuchukua ripoti iwe imeshiba.

Naam ni siku ya jumamosi,Roma aliamka vizuri na kujinyoosha na kisha alishuka kuelekea kwenye chumba cha mazoezi na ile anafika sebuleni , alikuta Bi Wema kama kawaida yake alikuwa ashaamka na sasa alikuwa akifanya usafi, na Roma alimsalimia. “Bi Wema Edna jana alirudi?”Aliuliza Roma maana alienda kulala mapema kabla ya Edna kurudi. “Miss jana hajarudi , alinipa taarifa kama atalala ofisini”Alijibu Roma na kushangaa. “Bi Wema hii ya kulala ofisini imeanza juzi au ni mazoea?”. “Ndio kuna siku hakuwa akirudi kabisa , na hii ni kama kuna jambo kubwa linaendelea ndani ya kampuni” Alijibu Bi wema na Roma hakutaka kuongea Zaidi , licha ya kushangazwa na ufanyaji kazi wa

Edna , hakujua k mke wake alikuwa akihitati kiasi gani cha pesa mpaka kuridhika , kwani kwa Roma ilikuwa ni jana tu aliweza kupata kuona taarifa ya Edna utajiri wake kuongezeka kwa dola bilioni moja kutokana na hisa za kampuni kupanda . “Ilimradi wanajeshi wangu wapo makini na usalama wake , haina shida, ngoja afanye kazi”Alijiwazia Roma baada ya kuingia kwenye chumba cha mazoezi. Baada ya kufanya mazoezi kwa madakika , alitoka na akaenda kuoga, kujiandaa kwa ajili ya kifungua kinywa na alitumia dakika chache tu alishuka na kukaa ,na leo hii alikuwa peke yake, kwani Bi Wema na yeye alitoa sababu za kutokunyuwa chai asubuhi hio na Roma hakujali sana , aliendelea kunywa zake chai taratibu, lakini chai ya hio ilionekana sio tamu kwake na mwenyewe alijishangaa kwanini leo hajisikii kunywa chai.

Wakati Roma anaendelea kunywa chai taratibu huku akiwa ni mwenye kukosa hamu , mara Bi Wema aliekuwa ameshikilia mfuko alionekana kushuka kutoka juu na alionekana alikuwa akitoka kwenye chumba cha Edna. “Bi Wema mbona unaonekana kama unasafari?”Aliuliza Roma huku akimwangalia “Nampelekea Miss chai, na baadhi ya nguo za kubadilisha,Jumamosi hakuna utaratibu wa wafanyakazi kufika kazini mpaka jumatatu”Aliongea Bi Wema na Roma alikuwa akielewa kuwa wafanyakazi wa Vexto Jumamosi walikuwa hawalazimishiwi kufika kazini na ni mara chache sana kukuta Kantini ya kampuni kuwa na wapishi siku za jumamosi.

“Bi Wema ngoja nimpelekee mimi , kwanza sina hamu ya kunywa chai leo”.Aliongea Roma na Bi Wema alitabasamu. “Angejua nilikuwa nilikuja kumpa ampelekee asingeniomba maana ningemlazimisha”Aliwaza Bi Wema na alionekana alikuwa na mpango wake kichwani. “Itakuwa vyema ukipeleka ndio”Aliongea Bi Wema na kisha aliandaa vitu ambavyo Roma antakiwa kwenda navyo, na ndani ya dakika kumi Roma alikuwa tayari kwa safari ya kuelekea kazini kwa mke wake huku Jasusi wa mapenzi akiwa ni mwenye kufarijika baada ya kumuona Roma akitoka na gari. “Hivi ndio inatakiwa iwe”Aliwaza Bi Wema na kisha alirudi ndani kuendelea na majukumu yake ya kazi.
“Dakika chache mbele, Roma aliingiza gari yake sehemu ya maegesho , siku hii kweli aliona ni tofauti kwani magari yalikuwa machache mno,lakini kuna jambo moja lilimfurahisha Roma ni baada ya kuona Gari ya Chiara iliokuwa imepaki na Chiara alimuona Roma wakati anatoka na Roma alitabasamu na kutingisha kichwa kama ishara ya salamu. “Wanajitahidi sana kumlinda Edna , nitamwambia Sauroni awaongeze mshahara”Aliwaza Roma wakati akiingia kwenye Lift.

Kampuni leo ilikuw imetulia kimya sana , ni wafanyakazi wachache sana ambao walionekana kuhudhuria siku ya leo. Lift ilimchukua Roma mpaka Floor ya ofisi za wafanyakazi wa juu wa kampuni. “Leo Miss Airport anaoneakana na yeye hajaja kazini”Aliwaza Roma huku akiwa na mfuko wake. Roma hakujisumbua kugonga , alisukuma mlango na ulionekana kuwa wazi na akazama ndani , lakini alijikuta akishangaa na hii ni mara baada ya kumkuta Edna aliekuwa amejifunika na khanga , kwenye sofa akiwa amelala , Roma alishangazwa na jambbo hili na kuwaza kama mtu amechoka kwanini harudi nyumbani kulala. Alisogea mpaka kwenye meza ya mke wake na kisha akaweka ule mfuko, na kugeuka na kutembea mpaka kwenye masofa na kumwangalia Edna alivyokuwa amelala. “Mke wangu anaonekana mrembo Zaidi wakati akiwa amelala”Aliwaza Roma huku akivuta Khanga aliojifunika Edna na kumuweka vizuri kwani ilikuwa imeacha mwili na kuburuzika kwenye marumaru.

Roma hakutaka kumuamsha Edna , aliona ngoja amuache kwanza apumzike , na yeye alienda kukaa kwenye kiti cha mke wake. Lakini Edna alionekana kuwa macho , kwani Roma ile anakaa kwenye kiti cha mzunguko cha mke wake ,Edna alifumbua macho na kumuangalia Roma na kisha akaendelea kulala. Roma wakati anafungua tarakishi ya mke wake kwa ajili ya kucheza gemu , kuna karatasi juu ya faili ambalo lilikuwa pembenni , mbalo lilimvutia, alilichukua na kuanza kusoma. Ilikuwa ni karatasi ambayo ilikuwa na majina ya kampuni za kitanzania ambazo zimezungushiwa kwa Wino , lakini sio zote, moja ya kampuni ambayo ilikuwa imezungushiwa kwa wino ilikuwa ni JR , alishangazwa na karatasi hio na kushindwa kuelewa ilikuwa ikihusu nini , hakutaka kujisumbua sana kama ilivyo kawaida yake, hakupenda kufikiria fikiria.

Edna ilionekana wakati alipokuwa peke yake alikuwa akikosa usingizi kutokana na wasiwasi , kwani kitendo cha Roma kuingia hapo ni kama ameruhusiwa , alilala muda mrefu mno kiasi kwamba hata Roma alijikuta akipitiwa na usingizi baada ya kuchoka kucheza gemu.
Mpaka inafika saa tisa na nusu bado hakuwa ameshituka,Roma alimwangalia Edna na kuishia kutabasamu , ukweli ni kwamba Roma aliona alikuwa na safari ndefu sana ya kumfahamu mke wake. “Anaonekana hakulala usiku mzima, sijui ni kipi kinachomfanya kuwa bize kiasi cha kutolala” Aliwaza Roma na muda huohuo Edna alishituka huku akionekana ni kama alikuwa amekurupushwa.

“Wife unaonekana ulikuwa umechoka sana”Aliongea Roma huku akianza kuachama , kwani alihisi njaa. “Saa ngapi?”Aliuliza Edna. “Saa Tisa”Edna alijikuta akitoa macho hakujua kuwa amelala muda wote huo , alijishngaa kwani ilikuwa ni mara yake ya kwanza kulala ofisini Zaidi ya masaa sita. “Nimepitiliza”Aliongea Edna huku akimwangalia Roma na macho yaliokuwa na usingizi bado.
“Ndio umelala sana mke wangu, yaani huwa nakushangaa Edna kwanini unafanya kazi kama huna hela”aliongea Roma lakini Edna hakutaka kumsikiliza alinyanyuka na kisha akazama kwenye mlango upande wa kulia , ulikuwa mlango wa maliwato kwani ofisi ya Edna ilikuwa imeunganishwa na choo na bafu kwa ndani.

Baada ya dakika kumi hivi kupita Edna alitoka huku akiweka nywele zake vizuri,ile chai ambayo Roma ameleta haikuwa na maana tena kwani muda ulikuwa umeenda na ilishapoa , Roma aliona jambo la maana hapo ni kutoka na Edna kwenda kupata chakula cha mchana. “Wife nina njaa twende tukale kabla ya kwenda nyumbani”Aliongea Roma na nikama Roma alishitua njaa, na Edna alikumbuka hakuwa ameweka chochote tumboni tokea jana usiku, alimwangalia Roma na kisha akatingisha kichwa kukubali. “Leo saa mbili nadhani hujasahau Roma”Aliongea Edna baada ya kuingia barabarani.

“Nishasahau mke wangu unaonaje ukinikumbusha”Aliongea Roma na ni kweli alikuwa ashasahau. “Kusanyiko la wafanyabiashara ni leo , tukitoka kula unipeleke nikatafute nguo ya kuvaa maana nimesahau kuandaa”Aliongea “Usijali mke wangu , nitaenda kukuchagulia mimi mwenywe , nguo
itakayokupendeza , nataka usiku wa leo uonekane kama malkia kwa kupendeza , na hivyo ulivyomzuri mke wangu”Edna aliishia kutabasamu na kuangalia mbele. Roma hakuwa akijua wapi asimamishe kwa ajili ya wao kupata chakula cha mchana , aliendesha taratibu , huku akiangaza macho kulia na kushoto na baada ya dakika kumi aliona sehemu ambayo ilikuwa ni nzuri kwa wao kukaa kwa ajili ya kula.

Ulikuwa ni mgahawa uliokuwa ndani ya posta , uliokuwa ukifahamika kwa jina la Rachel Dishes , ni mgahawa maarufu sana na ulikuwa umepakana na Mgahawa wa vyakula vya kichina. Edna alipenda piam azingira ya mgahawa huo na waliangalia sehemu ambayo inawafaa kwa wao kukaa , sehemu hii ilikuwa na watu , licha ya kwamba sio wengi sana , maana muda ulikuwa umeenda.
Leo ndio ilikuwa mara ya kwanza kwa Roma kutoka na mke wake kwa ajili ya chakula tokea wafunge ndoa yao. “Bebi unajua leo ndio siku yetu ya kwanza kutoka pamoja kama hivi kupata chakula”Aliongea Roma na Edna alimwangalia na kisha hakuongea chochote huku akiangalia chakula cha kuagiza kwenye kitabu cha orodha.
Baada ya dakika kama kumi na tano waliwekewa chakula chao na kuanza kula ,Roma alimwangalia Edna na wakakutanisha macho na Roma akatabasamu na kuendelea kula. “Natamani maisha yangu yangekuwa hivi , ila naona kama nina safari ndefu”Aliwaza Roma. ****

Naam ni muda wa Saa mbili kamili za jioni ndani ya hoteli iliokuwa pembezoni mwa ufukwe wa Kunduchi , hoteli iliokuwa ikimilikiwa na Maple Group , hoteli ambayo ilikuwa maarufu sana ambayo ilikuwa ikifahamika kwa jina la Apple hoteli. Hoteli hii ilikuwa imepakana na majengo mawili yaliokuwa yakifanana na yote yalikuwa yakimilikiwa na kampuni ya Maple , jengo la kulia lilikuwani la Apartment na jengo la kushoto kwake ndio ilikuwa hoteli hii nzuri ya kimataifa.
Hapa ndani ya hii hoteli ndio mahali ambapo kusanyiko la wafanyabiashara lilikuwa likifanyika na sasa ni muda wa saa mbili kamili za usiku gari za kifahari zilionekana kuingia ndani ya eneo hili kwa kupishana na kuegeshwa katika eneo maalumu, Ni saa mbili kamili dakika kumi na tano,Gari ya kifahari aina ya Roly Royce iliingia hapa ndani na kwenda kusimama katika eneo la maegesho na baada ya gari hii kusimama, alishuka dereva ambaye alikuwa ni Roma Ramoni na kuzunguka upande wa pili na kufungua mlango na hapa ndipo alipoonekana mwanamke Mrembo sana akiingia na mwanamke huyu hakuwa mwingine bali ni Edna

Upande kulia wa jengo hili alionekana Seif Ramadhani mwanajeshi kutoka jeshi la Irani aliezamia nchini Tanzania kwa sababu ambazo hazikuwa zikifahamika , bwana huyu alionekana akiwa ndani ya jengo hili huku akiweka bunduki yake vizuri aina ya Assault Sniper Riffle Koflo 64 iliotengenezwa nchini Urusi. Bwana seif alionekana kujiamini mno , baada ya kuweka standi ya kusapoti bunduki lake , aliweka jicho kwenye Lensi ya bunduki hii na na kuvuta pumzi kwa ishara ya ahueni.

“Target is clear in Position 12 O Clock”Alionekana alikuwa akiongea na mtu na kumwambia kuwa tageti yake inaonekana. “Fanya haraka na kisha utoweke sehemu ya tukio”Ilisikika sauti ya upande wa pili.
Baada ya Seif kuruhusiwa , alimlenga vizuri , huku mtu aliekuwa akionekana kwenye lensi yake alikuwa ni mrembo Edna , bwana huyu alivuta pumzi nyingi na kuzizuia na kisha akazilekeza kifuani na palepale akavuta Triga na Risasi ikachomoka kuelekea ndani ya ukumbi uliokuwa ukifanyia kusanyiko. NAAAAAAM

SEASON THREE NILIEMDHANIA KAHABA KUMBE NI BIKRA

GUSA HAPA KUENDELEA KUSOMA SEASON THREE SASA

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA

Mpya zaidi Nzee zaidi

Ads related

Smartwatchs