SEASON THREE
61 - 65
NILIEMDHANIA KAHABA KUMBE NI BIKRA
SEHEMU YA 61
Masaa machache nyuma.
Roma na Edna baada ya kumaliza kupata chakula ambacho walikiita chakula cha mchana kutokana na kuchelewa kwao kupata chakula hicho ,Roma alimchukua Edna mpaka My World Fashion Mall , kwa ajili ya kuchagua vazi la kuvaa kwenye kusanyiko la wafanyabiashara ambalo lilikuwa likitegemewa kufanyika usiku wa siku hio.
Ilikuwa ni wikiend na ndani ya eneo hili lilikuwa na watu wengi mno ambao walikuwa wakifanya ‘Shopping’ , kuna waliokuwa na wapenzi wao , kuna waliokuwa na marafiki zao jinsia moja , lakini pia kuna waliokuwa peke yao wakijinunulia nguo. Kama kawaida baada ya Roma na Edna kuingia ndani ya eneo hili , walikodolewa macho na watu wengi , huku macho yote yakielekezwa kwa Edna ambaye licha ya kwamba hakuwa amepaka kitu chochote kwenye uso wake , lakini alionekana mrembo Zaidi kuliko mwanamke yoyote aliekuwa hapo ndani.
“Baby hivi unajifahamu kama ni mzuri sana , angalia wanaume wanavyokuangalia kwa kukutamani”Aliongea Roma kwa kumtania Edna wakati wakipanda kwenye ‘ Elevetor’ za jengo hili . “Nishazoea, acha waniangalie”Aliongea Edna huku akionyesha kutojali kwa namna ya watu walivyokuwa wakimkodolea macho.
“Karibu Madam”Aliongea moja ya mfanyakazi ,ambaye leo alikuwa ni wa tofauti na wa siku kadhaa zilizopita ambapo Edna alifika hapo akiwa na Roma. “Kuna nguo ipi ingizo jipya ambayo unaamini itanikaa vizuri Tusi?”Aliuliza Edna huku Roma akimwangalia mwanadada huyu ambaye alikuwa mzuri wa haja, aliekuwa akifahamika kwa jina la Tusi. “Kuna aina mbili kutoka Ufaransa kampuni ya Luis Vuiton na nyingine ni kutoka Norf Italy”Aliongea mwanadada huyu na Edna akajikuta akijawa na shauku ya kuona nguo hizo . “Edna karibu!”Aliongea mwanamama mmoja ambaye aliwasogelea , alikuwa ni mnene wa wastani mrefu kiasi , alikuwa ni wale wanawake wanaojipenda , kwani licha ya kuonekana kuwa na wa umri mkubwa lakini bado uzuri wake haujapotea.. “Mama T!”Aliita Edna kwamshangao , ni kama hakuwa amemtegemea mwanamama huyo ndani ya hili eneo ,huku mwanamama huyu akimkodolea macho Roma , alikuwa akijiuliza hiuyu ni mlinzi mpya wa Edna , maana kwa muonekano wa Roma hakuonyesha kama mtu wa ukaribu na Edna. “Roma huyu ni Mrs Augustin ni mmiliki wa haya maduka,alikuwa jirani yetu Osterbay , tumezoea kumuita Mama T ,Mama T huyu ni Roma ni mume wangu”Aliongea Edna na kumfanya Mama T ashangae kwa kutoa macho na kisha akampa mkono Roma aliekuwa kwenye tabasamu namna ambavyo Edna alikuwa akimtambulisha. “Ooh! Edna jamanii mbona hujanipa taarifa kama umeolewa?”Aliongea mwanamama huyu huku akishanga.
“Mama T ndoa yetu haina hata muda mrefu na tumeona tu bila hata ya kufanya sherehe”Aliongea Edna na kumfanya mama huyu kuonekana kuelewa.
“Hongereni sana Edna , Hongera Mr Roma kwa kupata mke kama Edna”Aliongea mama huyu na alionekana alikuwa akitoa pongezi zake kwa dhati kabisa. “Asante sana na pia nafurahi kukufahamu Mama T , ila bado sijaelewa kwanini unaitwa mama T?” “T maana yake ni kirefu cha Twin, mama T ana watoto mapacha”Aliongea na hapa Roma alionekana kuelewa na kuona maelezo hayo yanajitosheleza lakini pia ni sahihi. “Edna kwasaabu leo ndio nimejua umeolewa , nataka nikupe Zawadi , nilishawahi kumwambia Rahel siku utakayo olewa lazima nikupe zawadi”Aliongea Mama T na kisha akamshika mkono Edna huku wakienda upande wa kulia kwenye duka kubwa ambalo lilikuwa limesheheni mavazi ya kike na hata Roma alifuatisha nyuma. Roma aliona mwanamaa huyu alikuwa na pesa nyingi , kwani hili duka halikuwa la kawaida , japo kwenye jengo hili kulikuwa na maduka menginye ya nguo makubwa tu, ila la Mama T lilionekana kuwa kubwa Zaidi. “Nina nguo mpya Edna , kwa uzuri wako kama utaivaa lazima ikupendeze na naamini utanisaidia kuitangaza leo usiku kwenye kusanyiko”Aliongea Mama huku Edna akikaa kwenye Sofa na mama huyu akienda upande wa ‘Store’ , alionekana hakuwa kabisa ameiweka kwenye nguo ambazo zinauzwa. Baada ya kuitoa Edna alishangazwa mno na aina hio ya gauni lililokuwa la maua maua , kabla hata ya kulijaribu alikuwa ashalipenda tayari na hata kwa Roma pia alipendezwa na aina hio ya Gauni,na Edna alienda kujaribisha. Roma alijikuta akiridhika na namna ambavyo mke wake alikuwa amependeza , Edna alionekana kama malaika mbele ya macho ya Roma , ni kama hakuwa akiamini kama ana mke mzuri kama huyo. Mama T na yeye aliliridhishwa na vazi hilo kwa kiasi cha juu sana kwa namna ambavyo lilikuwa limekaa kwenywe mwili wa Edna , lilikuwa ni gauni jekundu lilikuwa na aina flani ya vimaua aina ya Rose`s vilivyokuwa vimeshonwa kimpangilio kwenye shingo , huku mbele ya kifua likiaacha uwazi kidogo wa mfumo wa V. “Edna ungekuwa msanini hakika nadhani kila kampuni ingekutaka kuwa balozi wao kutangaza biashara ya mavazi”Aliongea Mama T . **** “Diego Unamkumbuka Alfshar Bahman?”Aliuliza Bram aliekuwa akichezesha vidole vyake kwenye Tarakishi yake huku akitafuna bublish. “Nishamsahau nikumbushe”Aliongea Diego kiongozi wa kundi la The Eagles. “Unasahau sana Diego ,utamsahau vipi Afshar?,kumbuka tukio lililotokea miaka kumi na moja iliopita Dallas , siku ya Christimas?”Aliongea Bram na kumfanya Deigo kuonekana kukumbuka. “Yes ! akili ilikuwa mbali , unamaansiha yule Gaidi aliye ua raia wa Kimarekani Zaidi ya ishirinni na tano kwenye mkesha wa sikukuu ya Christmas? Na akatoweka baada ya tukio lile na mpaka leo FBI wanamtafuta?” “Ndio huyo huyo” “Kwanini umetaja jina lake?”
“Notification yake imeletwa kutumia ‘Facial Recognition System’ na satilaiti ya Crogo”.Diego alishangaa kwani mtu ambaye alikuwa akitafutwa miaka na miaka na kundi la FBI kwa tukio la kutisha lilofanyika miaka kumi na moja nyuma siku ya sikukuu ya Christmas na kutoweka kusiko julikana baada ya tukio bila kuacha alama yoyote ya uwepo wake. Ukiwauliza Raia wa Marekani ea Dallas juu ya mtu anaeitwa Afshar Bahman hakuna ambae atashindwa kumfahamu , kutokana na maumivu aliyoyasababisba kwa familia pamoja na Taifa la Marekani. Tukio la Afshar Bahman linakuja miaka kumi na moja nyuma baada ya Afshar Bahman ambae alikuwa akitumia jina feki la Mahmood kumiminia waumini wa kanisa la The Forgiven chini Marekani na kuua raia 25 papo kwa papo na kujeruhi washirika kumi na moja huku kumi ya Raia kati ya ishirini na tano wakiwa ni watoto , tukio ambalo lilitokea miaka kumi na moja katika usiku wa mkesha wa sikukuu ya Christmasi saa saba kasoro ,baada ya waumini hao kuanza kutawanyika kuelekea majumbani baada ya ibada hio kuisha.
Kwa maelezo ya awali ya FBI baada ya tukio hilo la kutisha la kihistoria Mtuhumiwa huuyo ambae alikuwa akijiita Mahmood , alikuwa akitumia jina feki na jina lake halisi lilikuwa ni Afshar Bahman ,lakini taarifa ya kushangaza iliotolewa na idara hio ya usalama ya FBI ilisema Afshar Bahman baada ya kukamilisha tukio hilo alitoweka kwenye mazingira ya kutatanisha, jambo ambalo kwa zaidi ya muongo mmoja FBI walikuwa wakijiuliza bwana huyo alitoweka vipi pasipo kukamatika wala kuacha kivuli nyuma, swala hili liliwaumiza sana vichwa na kuanzia siku hio ya tukio Afshar Bahman akaingia lwenye jarada la watu wanaotafutwa zaidi na FBI(Most Wanted).
"Unamaanisha satilaiti yetu imeweza kumnasa Afshar ?"Aliuliza Diego huku akionesha hali ya mchecheto kwani aliamini kama swala hilo litakuwa la kweli basi litakuwa ni swala la mafanikio kwa kundi la The Eagles. "Ndio amekmatwa na Rada na anaonekana kuwa hapa Tanzania , angalia hiii alama nyekundu ni eneo ambalo anaonekana kuwepo" Aliongea Bram.
"Sehemu hio ni wapi?”Aliuliza Diego na Bram alizoom na jina likasomeka Kunduchi. na wote waliangaliana. "Hebu badilisha kwenda ‘Satelite View’ tuone eneo husika"Aliongea kwa haraka na Bram alifanya hivyo. "Apple Apartment!"Aliongea Bram ,na ungeshangaa uwezo wa satelite kwani waliweza kusoma mpaka maandishi ya jengo refu la Apple Apartment ambalo linamilikiwa na Maple Group na muda huu haya yakiendelea ilikuwa ni Saa mbili za usiku kama dakika nane hivi. Diego naamini kuna tukio linaenda kutokea ndani ya hili eneo na nadhani unakumbuka kunaa kisanyiko la wafanyabiashara wakubwa ndani ya hoteli ya Apple" Aliongea Bram na kumfanya Diego ashangae. “Wasiliana na Chiara na John haraka tujue nia yake na wape maelekezo ya kutosha , ngoja niende na vijana na tuta ‘secure perimeter’ kabla hajatoroka,wape msisitizo tuunamtaka akiwa haoi"Aliongea Diego na kutoka hapo haraka huku Bram akifanya mawasiliano na Chiara na John. ***** Suti ambayo Edna alimchagulia Roma ilikuwa imemkaa vizuri sana Roma , licha ya kwamba Roma alikuwa na mwonekano wa kawaida hata avae kitu cha thamani kubwa, lakini usiku huu alikuwa amependeza mno. Roma na Edna walikuwa ni kama kusanyiko hilo lilikuwa la kwao , kwani kwa namna ambavyo walikuwa wakionekana ndani ya eneo hili la kuingilia ndani ya hoteli, waliwafanya watu watu kuwa midomo wazi , Madam T alionekana kufaulu katika zoezi zima la kumpamba Edna na vazi alilochagua. “Roma usije ukaniangusha , hakikisha unaongea vizuri na wafanyabiashara , hii ni sehemu yako kwa kujenga kesho yako kupitia koneksheni” Aliongea Edna aliekuwa ameshikilia mkono wa Roma huku wakiingia kwenye Lift kwenda Floor ya kumi na Sita ambayo ndio kulikuwa na ukumbi maalumu kwa ajili ya kusanyiko la wafanyabiashara. "My wife usiwe na wasiwasi leo kwa jinsi ulivyopndeza nitahakikisha sikukasirishi usiku huu"Aliongea Roma na kumfanya Edna atabasamu na ndani ya dakika chache tu walikuwa nje ya mlango wa kuingilia ndani ya Ukumbi huu mkubwa unaotumiwakwa ajili ya hafla mbalimbali. Eneo la ndani ya ukumbi lilikuwa limepambwa likapambika ,kwa namna ambavyo sehemu jii ilionekana ni dhahiri ilikuwa ikiwakilisha watu ambao walikuwa na pesa. Wahudumu waliokuwa na vinywaji walipita huku na huko kuhakikisha wafanyabiashara hawa wanaumwagilia moyo vyema , lakini pia siku hii kulikuwa kumealikwa mpishi mkubwa sana Duniani kwa ajili ya kuandaa chakula kitamu kwa Wafanyabiashara hawa.
Wafanyabiashar wengi walikuwa washafika na ni wahcache sana ambao bado hawakuwa wamefika na walikuwa wakitarajiwa kufika , moja ya watu maarufun waliokuwa hapo ndani kwenye ukumbi alikuwa ni Neema luwazo huyu alikuwa ni Naibu waziri wa Sanaa na almaarufu kama Pisi ya mheshimiwa Kigombola , alikuwepo pia Abubakari Hamadi CEO , alikuwepo pia Meya wa jiji la Dodoma ndugu Bakari Juma , alikuwepo Mzee Alex mmiliki wa makampuni ya JR , Alikuwepo pia Balozi wa Tanzania nchini Japani , hao ni moja ya watu maarufu waliokuqepo ndani ya eneo hili lililopendeza na kuwakawaka taa nzuri za mapambo. Abubakari kama kawaida yake leo hii alionekana kupendeza mno ,suti aliokuwa amevaa ilikuwa imemkaa vyema ,ukijumlisha na muonekano wake wa Kihandsome ulichangia kupendeza kwake , wakati huu alionekana kushikilia glass ya wine huku akiongea na wafanyabiashara wakubwa ndani ya taifa la Tanzania na muda wote alionekana kuachia cheko la kibiashara,cheko la pesa. Neema Luwazo na yeye hakuwa nyuma katika kupendeza usiku huu , alionekana kama malaika , alikuwa amevaa akapendeza na kwa namna mwanamama huyu alivyokua akiongea na wafanyabiashara ungeona uzoefu uliokuwa ndani yake kwani muda wote alionekana kutabasamu na kutawala maongezi,alionekana kutumia fursa hiyo vyema kujijengea Koneksheni,ndio biashara ni koneksheni na hili linafahamika duniani kote , usipokuwa na koneksheni kwenye biashara huwezi kufanikiwa kirahisi lakini sio kwenye biashara tu , mambo mengi yanahitai Koneksheni . Tajiri namba moja Tanzania Mohamed Azizi pia na yeye alikuwepo na bwama huyu alionekana kama kivutio kwa wafanyabiashara wengi , kwani kila mtu alionekana kutumia fursa yake vyema kuongea nae . Ndani ya madakika kadhaa kupita hatimae hali ya hewa ilibadilika baada ya mrembo tajiri ndani ha Taifa la Tanzania kutokezea kwenye mlango wa kukngilia akiwa ameambatana na mtu ambae kwa wafanya biashara hawa walikuwa na hamu ya kumuona yaani mume wa tajiri mrembo Edna CEO . Neema Luwazo alijikuta akipagawa na moyo wake kupiga kite mara baada ya kumuona Roma kwa mara ya tatu ,.Mwanaume ambae alikuwa akimuota kila siku akifanya nae mapenzi, hata muda mwingine kujimalizia mwenyewe , mwanaume ambaye alifanya amnyime kitumbua mheshimiwa Kigombola ,kilichomfanya mwanamama huyu kushangaa zaidi ni Mwanaume huyo kushikana mikono kimahaba na mtu ambae hakuwa akimtegemea yaani Edna Adebayo CEO,Malkia ndani yaulimwengu wa biashara, kwanini asipagawe . “Madam Nasra kutana na mume wangu Roma , Roma huyu ni Naibu waziri Neema na mmiliki wa kampuni ya Maple group nadhani mlikutana nchini Japan” Edna alimtambulisha Neema kinafiki licha ya kwamba alikuwa akijua Roma na mwanamke huyo walikuwa na historia lakini hakutaka kuonyesha analifahamu hivyo kwani kwake ingekuwa udhaifu na alitumia nafasi hio kumuonesha Neema yeye ni mchepuko tu na yeye ameshikilia mpini , na kwa Roma aliona acheze ngoma alioanzisha mkewe kwani na yeye alifuata . “Mr Roma hii ni mara yetu pili kukutana , nilidhani ni mfanyakazi pekee wa Vexto kumbe ni mume wa mrembo na Tajiri Edna” “Ndio ndugu Waziri ! ,mimi ni mume wa huyu mrembo mzuri kuliko wanawake wote ndani ya hii dunia"Aliongea Roma na kumfanya Edna ajisikie utamu , lakini pia kumfanya Neema kuumia ndani kwa ndani na aliona ni kama Roma alikuwa akimfanyia makusudi mbele ya mkewe.
SEHEMU YA 62
Muda wote wakati Edna anaongea na Neema , watu wote hapa ndani macho yalikuwa kwa Edna na Roma , ni kama walikuwa kivutio usiku huu wa leo, na kwanini wasimwangalie sasa , kwani asilimia kubwa ya wanaume waliokuwa hapo ndani walishawahi kumtongoza Edna na kukataliwa , lakini jamaa wa kawaida sana asie Handsome kampata mrembo kama Edna , kwao ilikuwa ni pigo na aliekuwa akipumulia mashine ni Abuu,maana yeye ndie aliekuwa na juhudi lakini wapi. Edna baada ya kusalimiana na Neema walihamia kwa wafanyabiashara wengine wakubwa wakubwa , na ni kama Edna alikuwa akichagua yupi wa kusalimiana nae na yupi wa kumuacha na hii ni kawaida sana , kwani Edna alikuwa matawi ya juu na pia asingeweza kusalimiana na kila mfanyabiashara kwani walikuwa wengi. .
“Edna sio pesa tu zilizoongezeka ila na wewe pia umezidi kuwa mrembo"Aliongea Tajiri Azizi na Edna alitabasamu . “Asante Sann Mr Azizi , Kutana na Roma Ramoni mume wangu” “Mr Roma nilikuwa nikisikia Edna kapata mume ,kumbe ndio wewe , Hongera sana kijana umekuwa kati ya vijana waliobahatika kupata mwanamke mrembo ndani ya taifa hili"
"Mr Azizi acha kumbania mke wangu , utapungukiwa nini ukitoa sifa zote , wewe sema dunia nzima ,halafu ongezea ,mbeba mizigo wa kwanza kupata mwanamke mrembo halafu tajiri"Aliongea Roma na kumfanya Mr Azizi acheke kama ilivyo kawaida yake ya kucheka na kufanya wafanya mbiashara wengine wawaangalie Baada ya kutoka kwa Azizi walihamia kwa Mr Alex tajiri wa JR , Alex muda wote alikuwa akimtathimini Roma ni kama hakuwa akiamini maneno ya sifa aliokuwa akiambiwa , alimuona Roma kama kijana wak awaida sana na kujiuliza inakuwaje akawa anaogopwa na watu.
“Leo lazima utoe machozi wewe baada ya kumuona Edna akifa mbele yako”Aluwaza Alex huku akipokea mikono na Roma na wakaangaliana machoni ni kama walikuwa wakiwasiliana na Roma aligundua chuki kutoka kwa bwana huyu. Baada ya kutoka kwa Alex walihamia kwa Abu ambae alikuwa akichemka muda wote kwa wivu , kwani alitamani nafasi ya Roma iwe yake na sio kutamani tu, aliona Roma amemuibia nafasi yake, Roms leo hii alionekannaa kufanya vyema sana mbele ya Edna na Edna alishukuru katika hilo kaani Roma hakuongea sana zaidi ya kupeana mikono. “Muda si mrefu Edna utatoa machozi huyu kinyago ukimuona anakufan mbele yako”Aluwaza Abuu .
Na kwa namna ilivyonekana hapa ndani Abu alikuwa na mawazo tofauti na baba yake , kwani mzee Alex alikuwa akiwaza Kifo cha Edna na Abu alikuwa akiwaza kifo cha Roma ,kila mtu alikuwa na kipaumbele chake kati ya baba mlezi na mwana . Neema Luwazo alikosa utulivu kabisa licha ya kwamba alikuwa akisalimiana na kundi lingine la wafanyabiashara , lakini akili yake ilikuwa kwa Roma , ni kama hakuwa akiamini kama mwanaume aliekuwa akimpenda, mke wake alikuwa ni Edna malkia wa biashara , alijiknta ile nafasi aliokuwa nayo ya ushindi ya kumpata Roma imeshika kwa asilimia kubwa sana na sasa alikuwa na silimia mbili tu za kumpata ,mpango wake wa kuwa mchepuki Grade A aliona umekutana na kikwazo , aliona hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa .
“Kwa Edna kanizidi kila kitu ,pesa na urembo ,kanipiga gepu pia kwenye umri ,mimi nina miaka mingi Edna bado mdogo hii ni changamoto kwangu ya kumpata Roma”Aliwaza Neema huku akisalimiana na baadhi ya wafanyabiashara .
Sasa ndani ya dakika chache aliingia mtu ambaye alifanya Roma atoe macho, huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni Mama T ambae hakuwa peke yake na hili jambo lilimfanya Roma kushangaa zaidi , Mama T alikuwa ameambatana na mapacha wake, yaani Mage na Magdalena wadada hawa kwa namna walivyopemdeza katika vazi la aina moja ,na wao pia walikuwa kivutio kwa wafanyabiashara. Mage ndie aliekuwa wa kwanza kumuona Roma lakini pia wakati huo macho yake yalishangaa zaidi kumuona Edna akiwa na Roma . “Magdaelana yule si Edna!?” Aliongea Mage huku akishangaa lakini wakati huo huo ni kama na Edna aliwaona kwani aliwasogelea kutoka alipokuwa amesimama na walikumbatiana , Edna na Mage walionekana kufahamiana jambo ambalo lilimuacha Roma mdomo wazi. "Edna jamani ... ni siku nyingi hatujaonana kama hatuishi wote ndani ya nchi moja "Aliongea Mage huku akimwangalia usoni . "Mambo ni mengi tokea nihame Osterbay, ni kama nilikuwa nje ya nchi kwa ubize... Magdaelana umerudi lini?"Aliuliza Edna na kumshitua Magdaelana ambae macho yake muda wote yalikuwa kwa Roma.
Kwa Magdalena hakua kama dada yake aliekuwa akimshangaa Roma kwanini yupo na Edna ,alichokuwa akishangaa ni wasiwasi wake wa kimaswali juu ya mtu anaeitwa Pluto kuwa mwanaume huyu ambae kwake ni mwanaume wa Kawaida sana na hakuwa akionesha upluto wowote kama alivyokuwa akisikia habari zake , aliona Afande Maeda huenda kamfananisha. “Jamani huyu ni mume wangu anaitwa Roma Ramoni, Roma hawa ni marafiki zangu wa utotoni tumekuwa pamoja , majirani zetu”
Mage alianza kukumbuka siku ya kwanza alipokutana na Roma Vikindu mpaka kumpeleka kituo cha polisi Chalambe , alikumbuka akiongea na mwanamke kwenye simu ambaye kwa Roma alimtambulisha kwake kama mke wake. “Kwanini sikuweza kuifahamu sauti ya Edna siku ile , ndi maana Mkuu alipaniki na kuniambia nimuachie “
Aliwaza Mage na pia akaanza kukumbuka tukio la Nadia Alfonso na hapa alizidi kuunganisha matukio na kuona kweli huyu mwanaume licha ya kwamba alikuwa akionekana wa kawaida , lakini hakuwa kawaida kama alivyokuwa anamdhania. Roma aliwaangalia wanawake wakufanana waliokuwa mbele yake , na kisha akatabasamu na kuwapa mkono. “Nafurahi kufahamina na ninyi japo sio mara ya kwanza , kwa Afande Mage na Afande Magdalena”Aliongea Roma na kumfanya Edna ashangae.
“Kumbe mashawahi kuonana?”Aliongea Edna kwa mshangao na Mage alitabasamu na kutingisha kichwa , lakini wakati wanaendelae kuaongesa mara alikuja Balozi wa Japani.
“Mr Roma , Miss Edna!”aliita mzee huyu na kumfanya Edna amwanagalie ,aliekuwa akiongea na Mage akitaka kujua namna ambavyo waliweza kukutana na mume wake “Its been a while Edna since we last met, limekua jambo jema mara yetu ya pili kukutana umeshaolewa”Aliongea Balozi na Edna akaachia tabasamu lake ambalo lilizidi kuudhihirisha uzuri wake.lakini Roma akaingilia. “Balozi tunaonana tena”. “Ndio Mr Roma na moja ya sababu kubwa ya kufika hapa Tanzania ni kwa ajili ya kuonana na wewe” Aliongea Balozi na kumfanya Roma ashangae na hata Edna , hakujua ni vipi Roma alikuwa akifahamiana nipi na Balozi , lakini alijisikia faraja kuona mume wake alikuwa akifahamina na baadhi ya watu wakubwa , aliona ni hatua nzuri , hakutaka kufikiria sana ni kwa namna gani wawili hao waliweza kufahamiana.
“Miss Edna naamini haitakuuzi nikimchukua mume kwa dakika kadhaa nina mazungumzo nae”Aliongea na Edna alitingisha kichwa kukubali huku Edna na Mage wakisogea mpaka ndani kabisa upande ambao ulikuwa ukiangaliana na jengo la Apple Apartment.
“Hades najua sio jambo jema kuongellea hapa , ila sina muda mwingi hapa Tazania , kesho inanibidi kurudi Japani” “Haina haja ya kuzungukazukuka Balozi , nenda moja kwa moja kwenye swala lako”Aliongea Roma na bwana huyu alivuta pumzi kidogo na kuzitoa.
“Nimefikiria lile swala la wewe kuwa mkwe wangu , niseme kwamba nimeridhia kiroho safi , na sababu kubwa ni Sopha anasumbua sana , anasema anataka kuwa mke wako , na mimi pia baada ya kufikiria swala hili nimeona sio jambo baya , Hades sijui historia yako ya nyuma , lakini nasikia watu wanakutia Mfalme Pluto hii ni sifa tosha ya wewe kutomkataa Sophia”Roma alijikuta akishangaa , nikama alishindwa kumuelewa mzee huyu , kwani siku ile maneno aliongea kwake yalikuwa ni utani iweje kachukulia siriasi.
“Balozi sina mpango wa kuoa tena nishakuwa na mke tayari”
“Hades naelewa unachomaanisha ,sikuambii umuache mkeo, nachokuambia umuoe Sophia awe mke wako mdogo , wewe ndio mtu pekee ambae unaweza kumlinda Sophia , nimekua nikijiambia kwenye maisha yangu mwanaume ambaye Sophia atakuja kuolewa nae lazima awe na nguvu za kumlinda na wewe umejitokeza na pia Sophia anakupenda kiasi cha kunitishia Amani , anasema usipo muoa wewe haolewi na mimi mpaka sasa nashangaa umemfanya nini Sophia Hades mpaka kupenda kwa muda mfupi kiasi hicho”Roma aliona sasa hapa kinachoendelea ni jaribu, hakuelewa .
“Sophia atakuja kuishi hapa Tanzania Hades naamini utampa ulinzi wa kutosha m na pia kadri ukakavyokua nae karibu naamini lazima utampenda,Sophia ni mrembo na pia anakili nyingi”
Aliongea Balozi na kisha akageuka ni kama hakutaka kusikiliza jibu kutoka kwa Roma , lakini sasa wakati Balozi anageuka Roma macho yake yalitua kwa Chiara aliekuwa akiingia hapo ndani akihema , na kumfanya Roma kumwangalia Edna na ni kama macho yake yalikuwa na X-Ray kwani aliweza kuona Risasi inayotoka kwenye Bunduki upande wa pili , ilikuwa ni kitendo cha haraka sana kilichofanyika , kwani Roma alipokuwa amesimama alihama kama jini , na ile anaibuka , alikuwa amemkinga Edna na mgongo wake na palepale Risasi mbili zikatua kwenye mgongo wa Roma na hali ya hewa ikabadilika , huku dirisa likiwa na tobo la Risasi
Magdalena alikuwa ametoa macho ya mshangao , kwani jambo ambalo lilitokea alilishuhudia , kwani yeye pekee ndie aliekuwa akimwangalia Roma muda wote .
Roma alijikuta akimtemea Damu Edna , hali ya hewa ilibadilika ghafla , kila mtu alishindwa kuelewa kile ambacho kimetokea , watu walianza kuhaha , kwa tukio hilo , lilikuwa ni swala ambalo liliacha mshituko kwa kila mtu..
Upande wa pili chmba alichokuwa Seif , baada ya kuona mtu aliempiga risasi ni Roma alitoa tusi , lakini aliona sio mbaya pia, alikumbuka kuwa Abu tageti yake ni Roma na Mheshimiwa Kigombola na Mzee Alex tageti yao ilikuwa ni Edna.
“Not Bad” Aliwaza
Baada ya kumaliza tu alianza kukusanya bunduki lake kwa ajili ya kuondoka eneo la tukio , lakini ni kama alichelewa kwani muda huo huo aliingai John na Bastora yake mkononi na haikueleweka aliitoa wapi kwani Tanzania hawakuja na Siraha.
“Mikono juu Afshar Bahman! Jambo lolote la kijinga nakupasu”Aliamrisha John na kumshitua Seif ambaye alikuwa bize na kufunga bunduki lake, lakini bwana huyu hakugeuka , akili yake ilifanya kazi haraka , alikumbuka mkataba na mabosi wake haukuwa ukimtaka kukamatwa baada ya tukioo na kama itatokea amekaamatwa basi ahakikishe anajiua, lakini kubwa Zaidi lililomshangaza ni mzungu ambaye alimwita kwa jina lake halisi. “FBI how did the found me?”Aliwaza
Kilikuwa ni kitendo cha haraka sana Seif alichokifanya , alijirusha nje kwenye gorofa hio ya floor Zaidi ya ishirini , ni kitendo ambacho John hakuwa amekitegemea. “Sh***T!”Alitamka tusi na kisha akakimbilia Dirishani na kuangalia chini , lakini ajabu ni kwamba chini Seif hakuonekana , alizidi kuangalia kwa umakini , lakini Seif hakuonekana , lilikuwa jambo la kushangaza. “Diego he is Disappered , our Target disappeared again just like eleven year ago with FBI” “What.. how!”Ilikuwa sauti ya upande wa pili ya Diego” “I just can1t comprehend , I need to confirm the situation , Back up is needed” “Okey we are coming , we will secure the perimeter , he is not going to Escape again”Aliongea Diego kwenye simu huku John akikimbilia chini kwa kutumia ngazi.
SEHEMU YA 63
John alikimbia mpaka chini kwenye bustani za jengo hili na kuhakikisha, lakini hakukuua na dalili zozote za Afshar kuonekana , jambo hili lilimshangaza sana. “How this possible!?”Alijiuliza huku akiwa sio mwenye kuamini kama Afshar kapotea , aliamini lazima atakuwa katika mazingira hayohayo.
Upande wa ndani ya ukumbi hali ilikuwa mbaya , lile kusanyiko lilikuwa limeharibika ,Chiara alikuwa fasta sana , baada ya kuona Edna Analia pasipo kufanya lolote alimsogelea. “Madam tunapaswa kumpeleka hospitalini”Aliongea Chiara kwa kingereza na kumfanya Edna aliekuwa haoni vizuri kwa machozi amwangalie na akili yake kuanza kufanya kazi, alikuwa akilia huku akitaja jina la Roma , alijua mwanaume aliekuwa chini alikuwa amepigwa risasi kwa ajili ya kumlinda yeye. Watu walio majasiri walizunguka na wale waliokuwa na waoga kama makunguru walianza kutawanyika,Chiara alimbeba Roma na kumuweka begeani , licha ya kuwa mwanadada lakini alidhihrisha uwanajeshi wake.
Tukio la mzungu kumbeba Roma na kumtoa liliwaacha Mzee Alex pamoja na Abuu kwenye maswali mengi, na ni kama Abuu sasa akili yake ilikuwa ikija na kupotea ,alianza kukumbuka maneno ya Elvice juu ya wanajeshi wake aliowaagiza kuingia kwenye nyumba ya Edna kumteka kudhibitiwa na wazungu. “Unafikiri atapona?”Aliuliza Mzee alex aliekuwa nyuma ya Abuu na kumfanya bwana huyu ageuke kwa mshituko. “Hata kama yupo hai , tunaenda kummalizia hukohuko”Aliongea abuu alieawa na Faraja moyoni. “Ila bado kuna jambo sijaelewa hapa , huenda yale maneno naanza kuyaamini , huyu bwana sio wa kawaida , unajua alikuwa mbali na Edna lakini nilishangaa yeye ndio amepigwa na Risasi sio Edna”Aliongea Mzee Alex huku akimwangalia Abu ni kama alikuwa akitafuta sapoti kwa maneno aliyoyasema. “Ulikuwa huamini baba , lakini naamini saivi umeanza kuelewa mkasa niliopitia , ila hata hivyo yashaisha haya Roma huu ndio mwisho wake na Edna anaenda kuwa wangu”Aliongea na Mzee alex alitabasamu na kumpigapiga Begani na kuondoka na fimbo yake ya kutembelea.
Magdalena na Mage walikuwa ndio wa kwanza kutoka nje ya jengo ukumbi huku wakionesha dhamira ya kumkamata Sniper , na wao walifika mpaka kwenye bustani na kumkuta John ambaye alikuwa bize kuhangaika kutafuta.
Chiara baada ya kumfikisha Roma kwenye Gari na nyuma nyuma akiwa Edna pamoja na Neema ambao wote walionekana kuwa na wasiwasi , huku aliekuwa kweye wasiwasi Zaidi alikuwa ni Edna, Chiara alimuweka Roma kwenye siti ya Gari.
“Chiara hapa panatosha , utakaa karibu na Edna nakuja kumchukua”Aliongea Roma aliekuwa amenyanyuka na kumfanya Edna atumbue macho na haikuwa kwa Edna tu hata kwa Neema. “Roma!”Aliita Edna ambaye alikuwa akifuta kamasi na machozi kwa wakati mmoja na sasa ni kama alipata ahueni , ila bado hakuwa akiamini kama aliekuwa mbele yake ni Roma
“Hehe…My wife nani kakuambia nakufa kizembe hivyo mumeo , nilikuwa nikisikia unavyolia , unaonekana unanipenda sana,siwezi kufa nani atakulinda”Aliongea Roma huku akijishika eneo la Bega ambalo damu zilianza kupungua kutoka na kisha akavua koti la suti na kuliweka kwenye gari na hapo shati alilokuwa amevaa lililonekana kuwa na damu ambazo zimesambaa kiasi.
Lakini Edna alionekana kutoridhika , alijua Roma alikuwa na maumivu na anajikaza ,licha ya kwamba yeye na Neema wote walikuwa kwenye mshangao wa kuamka kwa ghafla kwa Roma.
“Mke wangu utabaki na Chiara atakupa Ulinzi hapa mpaka nitakaporudi , ngoja nikamkamate alieataka kukuzuru na utaamua tumpe kifo cha aina gani”
Aliongea Roma na kisha kuanza kupiga hatua , huku watu wakimshangaa kumuona Roma kaamka, hawakuelewa nini kimetokea kwani mtu ambaye walidhania kuwa mfu anaonekana kuwa hai tena.
“Mahesabu yangu yalienda kama nilivyotaka , nigekosea kidogo tu huenda ingenipata kwenye uti wa mgongo”Aliwaza Roma akikatisha upande wa kulia kuelekea lilipo jengo la Apartment.
“Your Majest!”Aliita John na kufanya Magdalenda na Mage wageuke kumwangalia Roma aliekuwa akitembea kama hakijatokea kitu na hapa ndipo macho ya Mage yalimtoka. “John imekuwaje?” “Ni Afshar Bahman Sir”Aliongea John na kumfanya Roma ashangae. “Afshar Bahman?, yule gadi wa miaka kumi na moja nyuma?”Aliuliza Roma na kumfanya John atingishe kichwa kwa ishara ya ndio. “Sasa yuko wapi?” “Kapotea Ghafla baada ya kujirusha kutoka ‘floor’ ile ya ishirini”aliongea na Roma akaangalia juu na kisha akatabasamu ni kama mtu ambaye ameona kitu.
“Endelea kutoa ulinzi hapa nakuja” Aliongea Roma kisha akwapita Mage na Magdalena waliokuwa wakimshangaa na Roma aliwakonyeza lakini kitu na pacha wake walishindwa kuongea , waliishia kuangalia Shati la Roma lilivyokuwa limechafuka kwa damu.
Roma baada ya kuingia kwenye jengo hili ambalo ni kama halikuwa na wapangaji , ila walikuwepo na wamejifungia katika vyumba vyao , alipandisha na lift mpaka Floor ya kumi na kisha akatoka na kutembea mpaka ‘Apartment’ namba kumi na moja iliokuwa na mlango upande wa kushoto kwake na kisha akasimama. *****
Upande wa ndani ya ‘Apartment’ namba kumi na moja alionekana jamaa mmoja ambaye alikuwa upande wa jikoni , akiwa bize na maswala ya upishi, alikuwa ni mwanaume mzungu aliekuwa na nywele fupi , ukimwangalia kimakadiro si chini ya miaka therathini,alikuwa amevaa suruali ya Truch Suit , pamoja na Tishen ya kata mikono yenye picha ya Mike Tyson.
Alichukua vttunguu ambavyo alikuwa amevikata harakaharaka na kisha akaweka mafuta kwenye kikaangio baada tu ya kumaliza alipasua mayai manne na kuweka kwenye kikaangio hiko na kuweka mayai. “Chwaaa…. Chwaa,,,,”
Ulikuwa ni mlio wa mkaango , huyu bwana wa kizungu alionekana kuwa vyema sana katika swala la upishi , kwani alivyokuwa akizungusha yai muundo wa chapatti iliokuwa kwenye kikaangio ungesema ‘Yes’ huyu ndio mzungu anaejua kupika.
Baada ya bwana huyu kuona pishi lake lipo tayari , aliweka kwenye sahani na kisha akazima gesi na kutoka hadi eneo la Sebuleni.
Ajabu ni kwamba eneo la Sebuleni alikuwepo Seif, akiwa amefungwa na mabendeji kwenye miguu na mikononi pia na kwenye tumbo lake alikuwa amezungushiwa Pazia ambalo lilikuwa limefungwa kwenye mguu wa sofa kwa chini, Seif alikuwa mzima na alimwangalia mzungu aliekuwa mbele yake na katika akili yake alijua mtu huyu lazima atakuwa ni FBI tu maana ndio watu aliokuwa wakimtafuta.
Bwana huyu wakizungu alionekana kutomjali Seif , aliwasha Tv na Rimoti na kisha akaweka sahani yake kwenye meza ya kioo na kuendelea kula mayai yake ya kukaanga.
Lakini muda huohuo mlango uligongwa na kisha alitabasamu na kumwangalia Afshar. “Ulietaka kumuua yupo mlangoni”Aliongea kwa kingereza na kumfanya Afshar atoe macho na bwana huyu alitabasamu na kisha akasogelea mlango. “Hahahaha.. Hades! Naona umewahi kuliko nilivyotarajia”Aliongwa bwana huyu kwa kingereza na kumfanya Roma atabasamu.
“Nilijua tu Mpishi wa kimataifa upo Bongo ,uwepo wako niliunusa wakati naingia na Gari ndani ya haya maeneo”
Aliongea Roma na alionekana kumfahamu sana bwana huyu aliemwita mpishi wa kimataifa na wakati huo Afshar aliefungwa na mabendeji akitoa macho kama kabanwa na mlango.
“How this possible?”Aliwaza kwenye akili yake maana alikuwa akikumbuka kabisa alimpiga Roma risasi za mgongoni , alijiuliza inawezekanaje aonekane kama hajajeruhiwa , maana Afshar alimuona Roma akiwa mzima , licha ya ushahidi wa damu tu katika shati yake.,
“Poseidon , siui unafanya nini Tanzania , lakini nimekuja kuchukua mtu wangu alietaka kumuua mke wangu”Aliongea Roma na kumfanya Poseidon arudi kukaa kwenye Sofa na kisha akala kidogo , upande wa Roma licha ya kumuona bwana huyu aliemwita Poseidon hakuonesha kubadilika , yaani hakuwa na furaha sana , alikuwa kawaida tu kama vile mtu huyo alikuwa akionana nae mara kwa mara.
“Hades nimefulia sana , sina hata hela ya kula, kuna mshikaji kanipa tu hifadhi kwenye hii ‘Apartment’ kupitia AirBnB, unaonaje ukinilipa kama malipo ya kumuokoa mtu wako alietaka kujiua”Aliongea mwanaume ambaye sasa tunamfahamu kwa jina la Poseidon na namna alivyokuwa akiongea alionyesha kweli hana hela , lakini pia ungeshagaa mzungu huyu kukosa hela maana katika jamii nyingi za kiafrika ni mara nyingi sana kwa mzungu kukosa hela , japo wanafulia.
“Poseidon sijakuomba unisaidie kumuokoa , kwasababu nitamuua , ni vilevile tu kwanini nikupatie pesa, pambana na shida zako , mimi mwenywe nalishwa na mke wangu, hela natoa wapi,halafu huyu fala hapa anataka kumuua”. Afshar ambaye alikuwa akiwaelewa Hades na Poseidon , sasa alikuwa amepata mwanga namna ambavyo aliokolewa, kwani wakati anajirusha alihisi nguvu isio ya kawaida ikimvuta kupitia usawa wa dirisha na aliposhituka tu yupo ndani ya hiki chumba.
“They are God`s”Aliwaza Seif kwa mshangao akimaanisha watu waliokuwa mbele yake ni
Miungu baada ya kusikia jina la Pseidon na Hades , Seif alionekna kuwa na baadhi ya taarifa zinazohusu Miungu watu .”Hawa ndio tuliokuwa tukiwasikia jeshini , kumbe ilikuwa kweli , nilikuwa nikidhani ni hadithi za kufikirika “Aliendelea kuwaza huku akizidi kuogopa na kujiona kaingia cha kike.
“Hades acha zako ,unajifanya kama hunijui, ukiwa ndani ya nchi yako, hatujaonana muda mrefu Tokea tusaini The God`s treaty ulitakiwa sasa unikaribishe kwa shangwe,inakuwaje wewe pekee ndio huoneshi kunimisi”Aliongea Poseidon akionekana ni mwenye kulalamika “Kwanza unafanya nini Tanzania , si nilisikia upo China wewe umefungua mgahawa?”Aliuliza Roma ***
Upande mwingine Abu na mzee Alex walitoka mpaka nje chini kabisa ya maegesho , wakwanza kutoka alikuwa ni mzee Alex ambaye alionekana kuwa na furaha sana usiku huu kwa kufanikisha jambo ambalo lilikuwa likiwaumiza vichwa muda mrefu na sasa aliona kilichobaki ni kuhakikisha anapata kampuni ya Edna.
Lakini sasa alijikuta akishangaa mara baada ya kumuona mzungu ,Edna pamoja na Neema Luwazo waliokuwa wamesimama kwenye magari , wakati akijiuliza nini kinaendela alisogelewa na kijana wake na kisha akamwambia jambo kwa sauti ya chini na kumfanya mzee huyu aanze kupumua kwa kasi,, sijui alikuwa ameambiwa nini.,lakini aligeuza na kurudi ndani kwa spidi na fimbo yake ya kutembelea.
Edna na Neema Luwazo walijikuta wakimshangaa mzee huyu , kwani alionekna kama alikuwa amechanganyikiwa. Baada ya dakika chache tu Abu alietangulizana na Mzee Alex walionekana kurudi kwa spidi. “Hehe.. wife mtu wetu tumemkamata”.Aliongea Roma aliekuwa amemuweka Begani Seif akiwa kwenye mabendeji , akiwa mzima ,Seif aliishia kumwangalia Abuu. Huku Abu akijiona kama akili yake haifanyi kazi vizuri.
SEHEMU YA 64
Mzee Alex pamoja na wafanya biashara wengine waliokuwepo eneo la maegesho , walikuwa kwenye mshangao mkubwa sana , ni kama macho yao yaliku yakiwadanganya kwa kile walichokuwa wakikiona mbele yao , mtu ambaye dakika chache nyuma walimshuhudia kupigwa risasi alikuwa amembeba Seif begani , kwanini wasishangae.
“Jamani si tumeshudia akipigwa risasi huyu, au haikumpata?”Aliuliza mwanamama mmoja mnene aliekuwa ameshikilia simu yake kubwa ya I phone akiongea na mwanaume aliekuwa pembeni yake.
“Ni yeye si unaona shati limechafuka kwa damu , lakini inanishangaza kuona ni mzima”Alijibu mzee huyu. Abuu alishindwa hata kuongea neno lolote Zaidi ya kumwangalia Roma anaemwingiza Seif kwenye gari , lakini muda huo huo Diego akiwa ameambatana na wazungu sita , wanajeshi wa Kikosi cha The Eagles waliingia ndani ya hili eneo na kumsogelea Roma.
“Sire!” Aliita Diego kwa mshangao mara baada ya kumuona Afshar kwenye gari.
“Diego nadhani mnataarifa za huyu muuaji?”
“Ndio Sir”
“Basi nadhani mnajua cha kufanya , mchukueni mpaka kambini , nitakuja kumhoji mimi mwenyewe .nikishamfikisha mke wangu nyumbani”
Aliongea na Diego alionekana kuelewa na haraka sana alimpa ishara Chiara na John kuondoka na Seif , huku na wao wakianza kuondoka eneo la hoteli hii , hawakutaka kukutwa na polisi ambao walikuwa njiani kufika eneo la tukio kwa kuchelewa.
Kila kilichokuwa kimetokea dakika kadhaa nyuma kilionekana kuwa kama muvi kwa macho ya watu wengi,waliokuwa wameshuhudia tukio hili kwanzia mwanzo mpaka mwisho. Baada ya Roma kutoa maagizo , alimshika Edna mkono ambaye muda wote alikuwa akimwangalia Mume wake kama kiumbe ambacho ndio kwanza anakutana nacho leo kwa mara ya kwanza. Edna alikuwa ni kama haelewi kile kinachoendelea na alimuona Roma kama mgeni kwenye macho yake , licha ya kwamba mrembo huyu alikuwa akijua Roma hakuwa wa kawaida , lakini hakudhania kama atakuwa ni Zaidi ya ule ukawaida aliokuwa akiujua,kwani kila siku alikuwa akishangazwa na jambo jipya kuhusu Roma. Neema Luwazo na yeye alikuwa kwenye mshangao , alikuwa haelewi, kinachoendelea , licha ya kwamba tukio lote lilitokea kwenye majengo yake ya kampuni , lakini ni kama alikosa nguvu ya kutoa maagizo , kwani muda wote alikuwa ni mwenye kunyamaza na kuangalia kile kinachoendelea , mwanamama huyu alikuwa kwenye mshangao mkubwa.
“Abu tunatakiwa kufanya nini kwenye hali kama hii?””Aliuliza Mzee Alex aliekuwa ni kama haamini kinachoendelea na kwa mara ya kwanza kwenye maisha yake , alikosa maamuzi ya hapokwa hapo , na ni mara ya kwanza pia kumuuliza kijana wake ni jambo gani linatakiwa kufanyika kwa wakati huo , lakini kwa Abuu alikuwa ni kama baba yake tu , kwani wote hawakujua ni hatua gani za kufuatwa kwa wakati huo. “Baba hii ni hatari wakimhoji Seif na kututaja kama wahusika wa mpango mzima”Aliongea Abu na hapa ni kama alikuwa ameshituka.
“Mpigie Kigombola”Aliamrisha Mzee Alex huku akisogelea gari yake na kijana wake alimfungulia mlango , huku Abuu akiangalia Roll Royce ,gari alilopanda Edna na Roma likitokomea kwenye macho yake.
“Fu****ck!”Abuu alijikuta akigongagonga kioo cha gari yake kwa hasira , huku baadhi ya watu wakimshangaa , lakini sasa wakati hayo yanaendelea Azizi Mohamed alikuwa ndani ya maeneo hayo , na haikueleweka alikuwa wapi , kwani ndio kwanza alikuwa akitokeza kwenye mlango wa kutokea ndani ya jengo hili la Hoteli.
“Kuna nini kimetokea?”Aliuliza tajiri Azizi na kijana wake alievalia suti alimweleza kwa sauti ya chini na Mzee huyu aliachia cheko , lililofanya baadhi ya watu wamwangalie , lakini kama ilivyokuwa sifa yake , hakujali , alitembea kulisogelea gari yake na kuingia.
“Hii habari itamfurahisha Rafiki yangu Jeremy.. hahahaha”Huyu mzee Tajiri alionekana kufurahishwa sana na tukio hilo.
“Bosi!”Aliuliza Dereva baada ya kumuona bossi wake anacheka pasipo kuelewa ni nini kimchekeshacho. “Hahahahaha ..Nipeleke nyumbani Sadiki nikalale mie”Aliongea mzee huyu na kisha Sadiki alitoa gari hio ya kifahari aina ya Range na kutoka nje ya hoteli hio. Upande mwingine Mage na Magdalena walishuhudia tukio lote la Roma kutoka akiwa na Seif,Kwa Magdalena kwake ilikuwa ni afadhari kwani alikuwa mwanaeshi , ila kwa pacha mwenzake Mage hali ilikuwa mbaya.
“Magdalena mbona ni kama sielewi kinachoendelea , naielezeaje hii hali?”Aliongea Mage mwanadada huyu ,masikini alionekana kuchanganyikiwa kwa wakati mmoja , hakuwa akielewa tukio zima lilivyotokea na mpaka kuisha. “Usiumize kichwa sana Mage, Mume wa Edna sio wa kawaida”.
“Unamaanisha nini Magdalena?, sio wa kawaida kivipi?, mbona unaonekana kuna jambo unalijua unanificha” “Siwezi kukuambia lolote Mage, ila jua sio mtu wa kawaida ,nimemsikia siku moja akisema wewe ni moja ya Askari wanaomchukia kwenye taifa hii , ila Mage nikwambie tu jitahidi kukaa nae mbali”Aliongea Magdalena wakati wakiwa kwenye Gari na kuzidi kumchanganya sana Mage.
“Mtu sio wa kawaida halafu nikae nae mbali , mimi ndio Mage , lazima nijue kila kitu , nitaanza kumfatilia kimya kimya” Aliwaza Mage , hakutaka kumuuliza sana dada yake maana alijua tabia yake ya kutotaka kuongea mara kwa mara hasa maswala ambayo yalikuwa yakihusu kazi yake.
Edna alionekana kuegamia kiti cha gari , huku akionekana kuwa na mawazo mengi kwa wakati mmoja , hakutaka kuongea chochote na Roma na hata Roma mwenyewe hakuwa akielewa mke wake alikuwa akifikiria nini na ndio maana hakutaka kumuuliza , aliendesha gari kimya kimta kuelekea nyumbani.
“Anaonekana kuwa na mshituko na najua ana maswali mengi , lakini siwezi kuanza mimi kumueleza , ila siku akitaka kujua historia yangu ya maisha yangu ya nyuma nitamueleza kila kitu”Aliwaza Roma wakati akiingia daraja la Kigamboni.
Edna aliekuwa ameegamia kwenye kiti alikuwa pia akiwaza kama alichokuwa akiwaza Roma. “Sio kama nilivyomfikiria ,Anaonekana kuwa na historia kubwa sana kwenye maisha yake , lakini sitomuuliza mpaka atakaponiambia mwenyewe”Aliwaza Edna katika kichwa chake.
Wanandoa hawa walionekana kuwa na mawazo yanayotofautiana , Roma alikuwa akiwaza kumuambia Edna kila kitu kama tu ataamua kumuuliza,lakini wakati huo Edna anawaza pia kutomuuliza Roma chochote kuhusu maisha yake ya nyuma mpaka atakapomuambia mwenyewe. Muda mchache mbele walifika nyumbani na Roma aliekuwa na shati lililokuwa na damu alitoka , huku Edna akiwa wa kwanza , alibeba mkoba wake mrembo huyu na kisha akakimbilia ndani na kumfanya Roma asimame amwangalie Edna, alishindwa kuelewa ni nini Edna anawaza kwa wakati huo.
“Mr Roma nini kimekukuta?”Aliuliza Bi wema kwa wasiwasi mkubwa baada ya kumuona Roma mgongo wake kutapakaa damu.
“Bi Wema kuna tatizo limetokea ila nitakueleza vizuri kesho , kuna mahali nataka kwenda , kuwa karibu na Edna anaonekana kuwa kwenye hali ambayo sio nzuri”Aliongea Roma na kisha akapanda mpaka chumbani kwake na kisha akaanza kuvua nguo.
Ndani ya dakika chache tu alikuwa ashamaliza na kusogelea kioo na kujiangalia kiupandeupande kwenye bega lake , lakini ajabu mgongo wa Roma ulikuwa na Tatuu kubwa tatu , bega la kulia na kushoto kulikuwa na tatuu mbili halafu chini ya mgongo usawa wa tumbo pia kulikuwa na tatuu. Tatuu ya kwanza sehemu ambayo ndio risasi ilipita kulikuwa na tatu ya chata ya Zero’s Organisation, upande wa kulia kulikuwa na chata la The Eagles’s , upande wa chini usawa tumbo kulikuwa na chata kubwa ya Pete ambayo katikati ilikuwa na maneno ya kigiriki ‘AIDES’.
Jeraha la Roma lilonekan kuziba pamoja na risasi yake ndani ,Baada ya kujiangalia kwa muda alibadilisha mavazi yake na kuchukua ufunguo wa gari yake ya Aud na kisha akatoka. “Bi Wema naweza kuchelewa kurudi”Aliongea Roma na kumfanya Bi Wema amshangae na kujiuliza huyu mwanaume anaenda wapi na usiku huo kwani ilikuwa ni saa nne na inaenda kwenye saa tano. **** Upande wa village G,aliingia Scorpion na kumsogelea mheshimiwa Kigombola aliekuwa akiangalia runinga huku akisinzia sinzia. “Kuna nini?”
“Mishenii imefeli”Aliongea Scorpion na kumfanya mheshimiwa Kigombola ashangae , lakini wakati huohuo simu yake iliokuwa kwenye meza ya kioo ilianza kuita kwa kucheza cheza na Mheshimiwa aliangalia na kisha akaichukua na alijikuta macho yakimtoka , kwan jina lililokuwa likisomeka kwa kwenye kioo ililikuwa ni la ‘First Black’.
“Kigombola habari za usiku?”Sauti ya First Black iliokuwa kwenye utulivi kama kawaida ilisikika upande wa pili na kwa Kigombola hata ile hali ya kuwa na usingizi ilikuwa imemuishia. “Salama kabisa Rafiki yangu , nimeshangazwa na simu ya usiku usiku”. “Ndio Kigombola simu hii ya usiku ni ya jambo muhimu sana”Aliongea na kumfanya Kigombola kushangaa.
“Nakusilikiza Mheshimiwa”.Kigombola alibadili jina kutoka rafiki yangu na kumuita Mheshimiwa na hii ilikuwa ni kawaida yake , kama hakukua na swala muhimu walikuwa wakiitana marafiki na kama kuna swala muhimu kikazi Zaidi alikuwa akimwiita The First Black Mheshimiwa, walikuwa wakiongea kwa kutumia lugha ya kingereza.
“Nadhani unakumbuka vifo vya raia wa Marekani vilivyotokea miaka kumi na moja nyuma”. “Nakumbuka mheshimiwa ,tena nnilikuwa moja ya watu waliotuma salamu za pole” “Ni vyema kama unakumbuka Kigombola , swala ni hili, mtu aliehusika kwenye tukio lile ni
Afshar Bahman na leo FBI wapepata kujua yupo Tanzania , na kwa maelezo ya haraka haraka Afshar Bahman anashikiliwa na kikosi cha The Eagles ,Afshar Bahman kupotea kwake baada ya tukio lile hakukuwa kwa bahati mbaya na sitaki FBI wapate ukweli wowote kutoka kwa Afshar maana ni swala ambalo linaweza kuibua mgongano wa kisiasa ndani ya taifa langu” “Mheshimiwa unataka nifanye nini?”
“Vijana wangu wapo njiani kuja Tanzania na watafika muda mfupi nchini Tanzania nataka uwaandalie mazingira ya kufanya kazi yao kwa ufanisi,nafikiri una nguvu kubwa serikalini , hivyo swala hili naomba liendee vizuri kusiwe na aina yoyote ya ‘Loopholes’,Narudia swala hili lazima lifanikiwe kwa namna yoyote ile ,Kigombola miseme tu kwa swala hili la Afshar unahusika moja kwa moja maana wewe ndio umemtoa Afshar kwenye mwanga baada ya kujificha ndani ya Tanzania kwa muda mrefu” “Unamaanisha nini mheshimiwa , kwanini nahusika na swala hili?” “Mtu aliekuja kwako na kujitambulisha kwa jina la Seif ni Afshar Bahman ninaemzungumzia na wanaintelijensia wangu wamenipatia hayo maelezo kwamba umempatia kazi ambayo imefeli na kupelekea kukamatwa na kikosi cha The Eagles , sitaki kuongea mengi juu ya kikosi cha The Eagles , lakini naamini swala nililokuambia litafanikiwa kwa asilimia mia moja”
Mzee Kigombola alijikuta akikunja ngumi kwa hasira na kujitukana , hakuelewa ni kwanini hakumjua Seif kama moja ya watu waliohusika na vifo vya watu Zaidi ya ishirini na tano nyuma. “Nilitakiwa kujua kwanini Seif alizamia Tanzania , hili swala lake kuanzia mwanzo lilikuwa na maswali mengi ambayo yalihitaji majibu,I was being emotion na hili swala la Edna , hii yote ni kutokana na The Don kunipa presha ya kutatua njia ya ‘Safe Root’.
SEHEMU YA 65
Chapisha Maoni
TOA MAONI YAKO HAPA