NILIEMDHANIA KAHABA KUMBE NI BIKRA season 2 (31-34)

KARIBU SEASON 2

31 - 34 SEASON TWO

NILIEMDHANIA KAHABA KUMBE NI BIKRA

SEHEMU YA 31

Ilikuwa ni Jumapili tulivu , kwa wale wakristo waliokuwa wakienda kanisani walikuwa wakienda na kwa wale ambao walikuwa ni wa dini nyingine walikuwa na pilipilika za mambo mengine za Maisha yao. Roma kama kawaida yake aliamka asubuhi asubuhi na kwenda kufanya mazoezi ya hapa na pale ili kuweka mwili wake katika hali nzuri , kwa upande wa Bi wema alikuwa bize na kuandaa kifungua kinywa kwa siku hio na kwa upande wa Edna alikuwa bize na kusoma kama ilivyokuwa kawaida yake , aliamini matatizo yake yote yanaweza kutatuliwa na kusoma na ndio maana aliamini katika kusoma sana.

Alijitahidi kusoma kwa muda , lakini akili yake haikuwa ni yenye kutulia , alionekana kuna jambo lilikuwa likimuumiza kichwa kwani alikosa utulivu , baada ya kuona haelewi kile alichokuwa anakisoma alisogelea tarakishi yake ya mapakato na kuingia kwenye mtandao wa Google na kuanza kutafuta taarifa zinazohusiana na macho ya mtu kubadilika Rangi , lakini kila majibu yaliokuwa yamekuja yalionekana kutokumridhisha kabisa na kukosa jibu alilokuwa analitaka. “Au nimuulize mimi mwenywe kwanini macho yake yanabadilika Rangi?” Aliwaza mrembo huyu huku akiwa amevalia kigauni chake kilichoufanya mwili wake mnene kiasi kupendeza.

“Ila naamini siku moja ataniambia mwenyewe kwanini yuko vile , sitakiwi kumuuliza”Alijiibu mwanamke huyu huku akiona hayupo kwenye nafasi ya kumuuliza mume wake Roma kwanini macho yake yanabadilika rangi anapokuwa na hasira kali. Saa mbili kamili za asubuhi Edna alishuka chini kwa ajili ya kupata kifungua kinywa baada ya kuitwa na Bi Wema , Roma alikuwa tayari yupo mezani , na alikuwa anamsubiria mke wake waanze , baada ya Edna kuketi wanafamilia hawa watatu ndani ya jumba hili kubwa la kifahari walianza kupata kifungua kinywa chao ambacho kwa familia za Maisha ya chini wangedhania moja kwa moja aina hio ya chukula ni kwa ajili ya sherehe.
“Miss unaonaje ukienda na Mr Roma leo kituoni?”Aliongea Bi Wema na kupendekeza . “Bi Wema kituo gani?”Aliuliza Roma “Kuna kituo cha kulelea yatima kipo Mkoa wa pwani Bagamoyo Kiwangwa, Ni kituo ambacho kampuni inakifadhili na imekuwa utamaduni kila jumapili Miss Edna kwenda huko kuwatembelea Watoto hao na kuwapelekea baadhi ya mahitaji muhimu”Roma alishangaa. Edna alimwangalia Roma , hakuwa akipinga swala hilo la kwenda nae , kwanza kabisa mrembo huyu alipanga kujiweka kidogo karibu na Roma ili kuweza kujua ni kwanini macho yake yanabadilika Rangi , aliamini kama watakuwa marafiki Roma anaweza kumfungukia. “Bi Wema kama mke wangu anapenda kuongozana na mimi nipo tayari , isitoshe leo sina pakwenda na sijazoea kukaa ndani”Aliongea Roma. “Roma itakuwa vizuri kama tutaenda wote , unisaidie kwenye kubeba mizigo ya kwenda nayo”Aliongea Edna na Roma aliitikia kwa kichwa.

Baada ya nusu saa Roma alikuwa ashajiandaa kwa ajili ya kuianza safari ya kuelekea Bagamoyo , alikuwa sebuleni akimsubiria Edna ambaye kama ilivyokuwa tabia ya wanawake kujiandaa muda mrefu Edna alichukua lisaa mpaka kuonekana akiwa anashuka.

Roma siku zote alikuwa akijivunia hata kuitwa mume wa Edna , kwani mwanamke huyu hata avae nini , alikuwa akipendeza sana na kuvutia,Edna alikuwa amevaa leo Suruali ya jeans rangi ya Bluu iliomfanya umbo lake kuonekana vyema, na kishati flani kitambaa mtelezo mikono mirefu , na akakikunJa hadi kwenye kiwiko cha mikono , chini akiwa amevalia viatu vyeupe kama Raba Rangi ya pink.

Edna alimpa Roma ufunguo na Roma alitangulia mpaka sehemu ya kuegeshea magari na kubonyeza Rimoti na Pickup aina ya Cadillac Escalade EX ili Tweak na kuwasha taa ,Roma alitabasamu na ufahari wa hii gari , aliitoa na kuleta mpaka katikati na Edna aliingia.

Bi Wema aliekuwa juu ya Gorofa alikuwa akitabasamu kwa furaha baada ya kuona Edna na Roma wakitoka , alijiambia ni mwenye akili sana kushauri waende pamoja. “Kuanzia sasa misheni yangu ni kuhakikisha wanafanya mambo kwa pamoja , hii itawaongezea kuwa karibu” Aliwaza Bi Wema huku akijiona jasusi mbobezi likija swala la mapenzi.

Safari ya wanandoa hawa iliishia Mliman City , Watu waliokuwa ndani ya eneo hili waliwaangalia kwa macho ya tofauti kabisa huku kila mtu akiwa na mawazo yake ,Edna alikuwa amevalia miwani ambayo ilimfanya apendeze lakini yeye hakuvaa kwa ajili ya kupendeza , alikuwa amevaa kwa ajili ya kufanya watu wasimtambue.

Roma alievalia jeans lake Rangi nyeusi na koti la Ugolo alijongea upande upande na mke wake , huku akijisikia fahari namna ambavyo wanaume wa eneo hili walivyokuwa wanamwangalia kwa macho ya wivu.
Walinunua mahitaji mengi ndani maduka ya vyakula , baadhi ya nguo , taulo za kike na makolo koloo mengi sana ambayo yalikwa ni sehemu ya mahitaji ya Watoto , walichukua na baadhi ya zawadi kwa Watoto hao ikiwemo biskuti pipi na vitu vingine.

Baada ya kumaliza kufanya manunuzi , Roma kusaidiana na baadhi wafanya kazi walipakia huku Edna akiwa bize kulipia. Wakati Roma akiwa bize kupandisha vitu , mara alisikia sauti iliokuwa ikimuita nyuma yake , sauti ya kike ambayo alikuwa akifahamu vyema, alikuwa ni mrembo Doris ambaye alikuwa akiegesha gari yake , akiwa yupo peke yake aliependeza kama kawaida.

“Doris !”Aliongea Roma kwa kushangaa baada ya kumuona mrembo huyu mbele yake.. wakati Doris anamwangalia Roma kwa mshangao mara alikuja Edna na kwenda kusimama karibu na Roma. “Edna!”Macho yalimtoka Doris , hakuelewa ni kwanini wawili hao wako pamoja . “Vipi Doris umekuja kufanya Shopping?”Aliuliza Edna wa kwanza baada ya kuona Dorisi yupo kwenye mshangao pasipo kuongea neno. “Ndio Edna , lakini kwanini upo na Roma?” “Nisamehe Dorisi rafiki yangu , nadhani unakumbuka nilikuambia nina mume?” “Usiniambie Edna huyu ndio mumeo na siku zote huniambii?”. “Ndio Dorisi huyu ni mke wangu,Tunaelekea Bagamoyo na muda unaenda tutaongea Zaidi”Aliongea Roma akikata mazungumzo hayo , hakutaka waendeleee kusimama ndani ya eneo hilo la maegeisho ya magari

“Nitakupigia simu Doris , tutaongea”Aliongea Edna na Roma alimshika bega Edna na kumsukumizia ndani na kufunga mlango na kisha akazunguka upande wa dereva na kuingia ndani na kuliwasha huku wakimwangalia Doris aliekuwa amesimama akiangalia gari yao ikitokomea.

“F**ck you Roma , siku zote unanichora tu kumbe mkeo ni Edna , halafu kwanini Edna

hajaniambia”Alijiongelesh a mwenyewe na kusahau kuwa baadhi ya watu walikuwa wakimshangaa , alifuta machozi kwa mkono ambayo yalikuwa yashaanza kujitengeneza ndani ya mboni za macho yake na kufungua mlango wa gari na kuingia na kisha akatoa gari ndani ya eneo hilo , alionekana kughairi , alichokuwa amefata hapo.

“Doris atakuwa amekasirika”Alianzisha maongezi Edna wakati wakipita Lugalo. “Kwanini unasema hivyo?”

“Doris ni Rafiki yangu wa muda mrefu na niseme ni Zaidi ya Rafiki yangu , tumekuwa pamoja kwa muda mrefu kidogo , nilimwambia nimeolewa na kumuhaidi nitakutambulisha kwake lakini sikufanya hivyo na leo ametuona pamoja , kama marafiki atakasirika na kujisikia vibaya”. “Mke wangu usiwe ni mwenye wasiwasi , Doris ni Rafiki yako na wewe ulikuwa pia na sababu za kutonitambulisha kwake mapema , hivyo atakuelewa , isitoshe hatuna muda mrefu tokea tumesajili ndoa yetu”.Edna aliitikia kwa kichwa. “Kila jumapili unakujaga huku kutembelea kituo?”Aliuliza Roma kwa makusudi a ya kubadilisha stori. “Ndio , imekuwa utamaduni , kila jumapili lazima nitembelee , napenda Watoto na najisikia faraja ninapokuwa nao karibu”. “Mke wangu nilijua wewe ni kauzu kila sekta , kumbe una upande wako mwingine ambao sikuwa nikiufahamu”. “Mimi sio kauzu ila napenda kuwa siriasi kwenye maeneo yanayonitaka kuwa hivyo , sipo kama wewe kila eneo haupo siriasi”. “Kwa hio mke wangu wewe unataka niwe vipi?”Edna hakujibu aliendelea kukaza macho barabarani na Roma hakutaka kuongea Zaidi.

Ni masaa machache tu walikuwa washafika ndani ya kituo hiki , kilikuwa ni kituo kikubwa sana, kilikuwa na majengo makubwa kama chuo , jambo ambalo lilimshangaza Roma. “Mke wangu hiki kituo ni kikubwa ni shirika gani limejenga hiki kituo?” “Sio shirika ni mke wa raisi wa Kenya ndio amejenga hapa Tanzania”Roma alishangaa ,yaani mke wa raisi atoke Kenya kwao ambako kuna Watoto wengi waliozagaa mtaani aje ajenge Tanzania , alishangazwa na jambo hilo. “Kwanini ajenge Tanzania sio Kwao Kenya?”
“Hata Kenya kajenga vituo vingi tu na sio Kenya wala Tanzania ,Uganda , Rwanda na Kongo kajenga vituo vinavyofanana hivi hivi, ni mwanamke ambaye ana moyo mzuri sana na anasifika sana ndani ya Afrika kwa kuisadia jamii. Roma alitingisha kichwa baada ya kupewa jibu hilo na mke wake , aliona huyo mwanamama anapaswa kupewa tuzo kwa msaada mkubwa ambao anaufanya kwa jamii zenye uhitaji.

Kitendo cha kumaliza kuegesha Gari Tu ni kama Watoto waliokuwa ndani ya hili eneo walikuwa wakimsubiria Edna kwani kundi lote lilimkimbilia na kumzingira huku wakionyesha furaha yake na Edna na yeye hakuwa nyuma , alionekana kufurahi kweli uwepo wa Watoto na kwa mara ya kwanza Roma anamshuhudia Edna akiwa na furaha sana.

“Sikujua mke wangu kumbe mzuri hivi akicheka , halafu anaonekana kuwa na moyo mzuri sana , kanaigiza tu kuwa siriasi”Aliwaza Roma huku Watoto hao wakiwa hawana habari nae. “Edna karibu” Aliongea mwanamama mmoja hivi mnene mwili wa kibonge mwenye umri si chini ya hamsini hivi alikuwa wa maji ya kunde. “Asante Mama Issa

”Alijibu Edna aliekuwa akiwaangalia Watoto hawa , lakini kwa upande wa yule mama alimwangalia Roma na hapa ndipo Edna aliekuwa amemshau Roma akainuka. “Mama Issa Watoto wamenifanya nisahau kukutambulisha , huyu ni mume wangu anaitwa Roma Ramoni” Mama huyu macho yalimtoka kwa mshangao huku Roma akiwa ni mwenye kutabasamu , alijiuliza huyu mwanaume ana nini mpaka kupata nafasi katika maisha ya Edna.

“Sikujua.. kumbe umepata mume Edna .. jamanii.. karibu baba mimi naitwa Tabea Singano ni mkuu wa hiki kituo”Aliongea mama huyu huku akionyesha furaha yake waziwazi , alionekana pia ni mtu ambaye alitamani siku moja Edna kumtambulisha mume wake kwake. “Nashukuru sana kukufahamu Mama”. “Karibu sana , unabahati sana kumpata Edna katika Maisha yako , umchunge sana”Aliongea mwanamama huyu huku Edna hata hakuwa akiwasikia , kwani alikuwa bize na Watoto aliokuwa akiwabeba mmoja mmoja juu.

Walishusha mizigo kwa kusaidiana na wafanya kazi wa hapa ndani , na Roma pia alisaidia katika kazi hio na baada ya zoezi hilo dogo kuisha Edna na Roma walichukua zawaidi walizokuwa wamekuja nazo na kuanza kuzigawa kwa Watoto hao . Roma alimkubali sana aliejenga hiki kituo kutokana na wingi wa Watoto hao , kilikuwa mpaka na shule kubwa ya msingi mpaka sekondari , ni kituo ambacho kilionesha kujitosheleza sana kwa kila kitu.

Mama Issa alimchukua Roma na kuanza kumtembeza ndani ya kituo hichi , kwa kumuonesha baadhi ya huduma ambazo wanatoa kwa Watoto hawa ya kimalezi , mama huyu alionekana kuwa mkarimu sana. “Edna ni msichana wa kipekee sana ,nimemuona akikua kwanzia alivyokuwa mdogo”Roma alishanga “Mlikuwa maishi majirani?”.aliuliza Roma na mwanamama huyu alitabasamu.

“Hapana , wakati wa utoto wake alikuwa akija na bibi yake hapa mara kwa mara kucheza na Watoto na naweza kusema Muda wake wa utoto mwingi alicheza na Watoto ambao walikuwa kwenye hiki kituo”Aliongea mama huyu na kumfanya Roma ashangae , na wakati huu walikuwa wakiingia ndani ya mejengo ya ofisi hizi za kituo hiki kilichokuwa kinafahamika kwa jina la

Son and Daughter Orphanage(SDO).. Roma baada ya kuingia

ndani ya hii ofisi kubwa ya mama Issa alijikuta akishangaa picha iliokuwa juu ya ukuta ,ilikuwa ni picha ya mwanamama mmoja maji ya kunde aliekuwa kwenye pozi la kutabasamu, kichwa chake kilianza kuuma na kupiga kama Radi na picha picha za matukio zikianza kupita .. macho yake yalianza kubadilika palepale na kuwa ya kijani.

SEHEMU YA 32

Roma alishindwa kuvumilia , alikuwa akishindana na hali iliokuwa ikiendelea kwenye mwili wake , alifumba macho yake haraka sana , ili Mama Issa asimuone akibadilika na kisha akageuka, Uzuri ni kwamba mwanamama huyu alikuwa amempa mgongo Roma na hakuwa akijua kilichokuwa kikiendelea kwenye kichwa chake.

Roma alikimbilia nje , lakini ile anatoka kwenye ofisi alijikuta akikumbana na Edna ambaye aliona hali yake ya macho Alitaka kumwepa lakini Edna hakufanya hivyo , alimshika mkono. “Roma Calm

Down”Aliongea Edna na Roma ni kama ameshituka kwani macho yake yaligeuka na kurudi katika hali yake ya kawaida na kumwangalia Edna. “Am Sorry Edna”. “Sorry ya nini?” “Sijui …”Kabla Roma hajaibu walishitushwa na sauti ya Bi Tabea. “Nilishangaa umeenda wapi kumbe umemfata mkeo”Aliongea Bi Tabea na Edna alitabasamu.

“Edna niseme tu hongera sana kwa kupata mume , Roma anaonekana kuwa kijana mzuri naamini mama yako na bibi yako watakuwa na furaha na wanaweza kupumzika kwa amani maana wewe..” “Mama Issa Maana nini…”aliongea huku akicheka.

“Umekuwa mgumu sana , nakumbuka yule nani yule .. ee Elvice alikuwa akitoka jeshini lazima aje hapa kulalamika..”Mama huyu alijikuta akiishia njiani kuongea na kujiona ameropoka ila kwa Roma alikuwa amesikia kila kitu na akajiuliza kuna historia gani kati ya Elvice na Edna ambayo hakuwa akiijua , ila hakutaka kuuliza.

Saa moja kamili za jioni ndio muda ambao wawili hawa walitoka ndani ya kituo hiki kurudi nyumbani , Edna alionekana kuchoka kweli kutokana na kucheza na Watoto , kwa upande wa Roma yeye hakuwa amechoka , kwanza hakucheza kabisa na Watoto kwani sio mtu wakupenda sana kama ilivyokuwa kwa Edna.

Alimwangalia mke wake aliekuwa amesinzia pembeni na kujikuta moyo wake ukiwa wa moto , alitamani Maisha yake yawe kama hivyo kila siku ,awe anapendana na mke wake , watembee hapa na pale kurefresh mind, alitamani kufurahi na kuendeleza Maisha ya ukawaida , lakini Roma Maisha ya aina hio yalikuwa kwake ni ndoto. “Hapana lazima nifanye juu chini nina kamilisha yote yalionileta Tanzania , nikishachimba swala hili kwa undani na kujua kwanini nilikuwa kwenye kile kisiwa cha mateso mimi na Seventeen na kuifahamu familia yangu nadhani nitatulia na mke wangu, Edna licha ya kwamba hatujaoana kimapenzi , lakini sidhani kama itakuja siku

nitakuacha hata pale mkataba utakapoisha”Roma aliwaza mawazo hayo mchanganyiko huku akizidi kukanyaga pedeli kuelekea jijini Dar es salaam. Wakati akiendelea kuendesha gari alikumbuka kauli ya Bi Issa kumuuliza hali ya kimaendeleao ya Nasra , alijiuliza kwanini mwanamama yule kauliza juu ya maendeleo ya Nasra ila alikosa majibu kwa wakati mmoja , alijiambia kuwa atafahamu kadri atakavyokuwa karibu na Nasra. ****

Doris alijikuta ni mwenye hasira sana , baada ya kujua kuwa Edna na Roma ni mume na mke , alikasirika sana , lakini na kuumizwa kwa wakati mmoja. Alianza kukumbuka tukio ambalo Roma alimuomba hela ya nauli wakati akiwa anarudi nyumbani na kumpatia , alikumbuka usiku wao waliotumia na kufanya mapenzi na mwanadada huyu alizidi kutokwa na machozi ,alihisi moyo wake ulikuwa ukimuuma sana kiasi cha kwamba mwenyewe alishindwa kuelewa kwamba moyo wake ulikuwa ukimuuma

kutokana na kwamba Edna na Roma walimficha na kumuona mjinga siku zote , au ni kwasababu alijua kuwa Roma mke wake ni Edna mwanamke mrembo na kilichokuwa kikimliza ni wivu wa kimapenzi. Alisimama kukodolea maji ya baharini muda huu wa jioni huku machozi yakiwa yanamtoka , lakini kila alipokuwa akiangalia baadhi ya wapenzi waliokwa ndani ya fukwe hii ya Coco walivyokuwa wakifurahi na kuonyesheana mapenzi , aliijikuta akizidi kutoa machozi.

“Ninaonekana kutokuwa na bahati katika Maisha yangu , Edna nifanye nini mimi nahisi kumpenda sana mumeo , najiona kabisa siwezi kumuacha hata kidogo , kwanini iwe wewe rafiki yangu”Aliwaza mwanadada huyu na kuwazua huku akionekana ni mwenye kukosa jibu , alionekana alikuwa akishindana na hisia zake. Doris licha ya kwamba alikuwa sio mwenye kuonyesha waziwazi mapenzi yake kwa Roma alikuwa ashampenda tokea siku ya kwanza wanaonana ,Roma alivyomuomba kiasi cha

pesa , tokea siku ile alikuwa alikuwa ni mwenye kumkumbuka Roma , hakujua ni kwanini alikuwa akimkiumbuka mwanaume huyo , lakini picha yake haikuwa ni yenye kutoka kwenye kichwa chake.

Siku ambayo anamuona Roma kwa mara nyingine ndani ya kampuni yake , akija kufanya usaili , alijiambia kabisa ni Mungu ndie aliekuwa amewakutanisha kwa mara nyingine na hivyo hapaswi kuzarau kile Mungu alichompatia na ndio maana siku ile ile aliona atumie nafasi ile kumtambulisha Roma kwa mwanaume mzee aliekuwa akimsumbua , mwanaume aliekuwa akimfahamu kama Mr Kijembe . Hakujali kabisa katika

moyo wake kwamba Roma ameoa , alichokuwa akiamini ni Kwamba Roma alikuwa amepangiwa kuwa nae katika Maisha yao yote na mke aliemua ni makosa ambayo Roma alikuwa amefanya , hayo ndio yalikuwa mawazo ya mwanadada huyu mrembo , aliamini mke wa Roma sio mtu sahihi kwa Roma na yeye ndio alikuwa sahihi , kwani matukio yao ya kukutana ni kama Mungu aliwakutanisha. Hata pale alipopata taarifa ya Roma kulala na mwanamke Neema Luwazo Mwanamke ambaye alikuwa akimjua sana tu, kwa kuwa na mahusiano na Raisi mstaafu , alijiambia kuwa ni mihemko tu ya Roma ya kukosa mtu sahihi wa kumtuliza na kama atampata basi Roma angetulia kwake na kuachana na mambo ya wanawake , kwani angempa kile kitu ambacho anakitafuta nje , kitu ambacho aliamini ni kwamba alikuwa akikikosa kwa mke wake.

Siku ya Jumapili ndio siku ambayo alipanga kutimiza jambo lake la kuanza kuweka ukaribu na Roma , aliamini anapaswa kufanikisha swala la yeye kuwa karibu kabla ya kwenda safari ya kikazi Japani , alitaka katika safari hio waitumie kama sehemu yao ya matembezi kama wapenzi , na ili kukamilisha swala hilo anachotakiwa kufanya ni kuhakikisha Roma anakuwa karibu yake anamzoea na hatimae kumpenda.

Baada ya kuwaza hayo , hatua ya kwanza aliofikiria ni kwenda kutafuta zawadi yoyote ambayo aliamini itamfurahisha Roma na eneo pekee alipoona panafaa kupata zawadi hio kwa siko hio ya jumapili ni Mlimani City. Nwanadada huyu

alijiandaa , alichukua kadi yake ya benki aina ya ‘Black Card’ kadi ambayo ilikuwa ikimruhusu kutoa kiasi chochote kile cha pesa na kuiweka katika mkoba wake , na kisha akachukua ufunguo wa gari yake na kutoka ndani ya jumba hili la kifahari alilokuwa akiishi mwenywe na wafanya kazi.,Jumba ambalo alikuwa amenunuliwa kama zawaidi na baba yake . Lakini baada ya kufanya safari yake na kufika Mlimani anajikuta akishuhudia kitu ambacho moyo wake haukutarajia kukiona , alimuona mwanamke ambaye aliamini sio sahihi kwa Roma akiwa ni Edna , Rafiki yake kipenzi , bosi wake kazini, moyo wake ulipigwa na ganzi. “Doris!!”Ilikuwa ni sauti ya mwanaume iliosikika nyuma yake na kumfanya mwanadada huyu ageuke
ni nani anamuita , lakini ile anageika alikutana na uso wa Abu. “Abu vipi , kwanini uko hapa ?”Aliuliza Doris kwa namna ya kushangaa. “Nimekuja kupunga upepo kama wengine Doris , wewe vipi , kwanini uko hapa?”. “Namini nipo kwa ajili ya kupunga upepo “Abu alijikuta akitabasamu . “Doris najua unaonekana kuwa katika hali ya mawazo , lakini nimekuwa nikisubiria sana jibu lako”

Doris alishangaa na kuanza kuvuta pumzi kwa nguvu na kumgeukia Abuu…. Ni jibu gani ?? SEHEMU YA 33

2010 -KIGALI STATE HOUSE

Ni mwaka 2010 muda wa saa tano za Asubuhi mheshimiwa Jeremy alionekana ndani ya ofisi yake akifanya kazi kama kawaida, katika kuwatumikia wananchi wa Rwanda, lakini siku hii kwa mheshimiwa huyu hali yake ilionekana kuwa sio ya kawaida , kwani alionekana kuwa ni mwenye wasiwasi sana kuliko siku zote hali ambayo ilimfanya kukosa utulivu , kila saa alionekana kuangalia saa ya ukutani kama mtu ambae alikuwa na jambo ambalo alikuwa akilisubiria.Ilivyofika saa sita na nusu aliingia Linda mlinzi wa karibu wa Mheshimiwa Jeremy. “Mheshimiwa Ashafika”Aliongea Linda na kumfanya mheshimiwa Jeremy avute pumzi . “Mruhusu aingie”Aliongea mheshimiwa na kisha akatoka kwenye meza yake na kwenda kwenye masofa na hapo hapo mlango ulifunguliwa na aliingia mwanaume mmoja wa kizungu alievalia shati la Blue bahari na suruali ya kadeti , muonekano wa huyu jamaa ni kama vile hakuwa akiingia kuonana na mheshimiwa , kwani alivaa kikawaida sana kama muhuni flani hivi. “Welcome Mr Viladkov”Aliongea mheshimiwa kwa kingereza.

“Asante sana mheshimiwa”Aliongea na kisha alitoa karamu nyeusi flani hivi pana kidogo lakini ya kawaida , kama zile za rangi na kisha alianza kuifungua kama mtu ambae anatoa ule mrija wa wino, na akatoa kifaa Fulani hivi kama kile kichwa cha kuchomekea kwenye Earphone lakini hiki kwa juu mwisho kina kitu kama kigoroli. “Hili ndio faili mheshimiwa”Aliongea na kisha alimpatia Jeremy kile kidude na mheshimiwa alishangaa m inakuwaje kadude kama hako kawe ndio faili ambalo alikuwa akilisubiria kwa hamu.

‘”Usishangae mheshimiwa Hata Urusi sasa imeendelea kwenye teknolojia , na hio ni mbinu yetu mpya kuficha taarifa wakati wa kuzisafirisha” ’Mheshimiwa Jeremy hapa alishangaa na akachukua Tablet iliokuwa kwenye meza yake na kuchomeka kale kadude na baada ya tablet ile kusoma kama Earphone ilisoma kama memori , alishangaa na Viladkov akatabasamu. “Ni taarifa nyeti sana hio , na serikali ya Urusi imelipa kiasi kikubwa kuinunua kwa mtu aliekuwa akiuza”Aliongea bwana huyu na mheshimiwa Jeremy aliifungua na ajabu ni kwamba alikutana na picha.

“Mbona ni picha sio kama faili nilivyokuwa nikitegemea?” “Angalia kwanza hizo picha mheshimiwa kwa umakini na uniambie umegundua nini?” Alianza kuangalia hizo picha kwa kuzizoom na katika picha hizo kulionekana meli kubwa ya mizigo ikiwa inashusha mavyuma , lakini baada ya mheshimiwa kuangalia kwa ukaribu Zaidi aligundua ni bawa la Ndege.

“Linaonekana kama bawa la Ndege” “Angalia na hio nyingine” Aliangalia na pia yenyewe ilionekana kama baadhi ya vipandevvipande vya mabaki ya ndege. “Hio meli inamilikiwa na kampuni Neptune , kampuni ambayo ni sehemu ya kampuni kubwa ya kuzalisha ndege ya kimarekani inayofahamika kwa jina la Ngebo Aeronautical”Mheshimiwa alionekana kushangaa , lakini pia alizidi kuongeza umakini. “Hizo picha zilipigwa Tarehe saba March 1998”Aliongea na mheshimiwa huyu alishangaa sana. “Unataka kumaanisha kwamba ni siku moja kabla ya ndege ya Malaysia kupotea?” “Ndio kutoka sehemu ambayo meli hio ilipo na sehemu ambavyo ndege ya shirika M ilipotea ni umbali wa kilomita ishirini tu , kwa maana hio hayo ni mahesabu ambayo yamepigwa kabisa na hio meli ilitupa mabaki hayo unayoyaona kwenye hizo picha eneo hilo”Mheshimiwa Raisi alijikuta akitetemeka maana anacho ambiwa

hapo ni taarifa nzito sana , tena nzito kweli kweli. “Mheshimiwa hii ni siri ninayokupatia ambayo ni siri kubwa ndani ya taifa la Urusi na ni kama Asset kwetu , hivyo taarifa hii inapaswa kuwa siri , mheshimiwa Raisi Viladmn karuhusu upatiwe taarifa hio ili kwa ajili ya kushawishi mataifa ya Afrika kuingia kwenye Mpango TASAC”Mheshimiwa alishangaa Zaidi.

:Mheshimiwa chomoa hio flash na uichomeke tena” aliongea Viladkov na mheshimiwa alichomoa na kuichomeka tena na ikasoma tena kama memori , aligusa ten ana zile picha zikawa zimefutika ils sasa kulionekana faili lililokuwa kwa mfumo wa ‘Xml’ , mheshimiwa alilifungua na kuanza kusoma na hapa ndipo aliposhangaa. “Hio ni barua ya wito iliotumwa kwa mashirika ya kijasusi makubwa yote duniani na katika hio barua inaonesha kulikuwa na makubaliano ambayo yalikuwa yanatakiwa

kufanyika juu ya mpango ambao ulipewa jina la LADO ambapo sisi tulishindwa kung`amua kirefu cha neno hilo , na shirika letu pekee ndiio halikutuma muwakilishi kwenda kuhudhuria kikao hiko ambacho kilifanyikia nchini Italy”Mheshimiwa jasho lilimtoka maana kadiri anavyoambiwa ndio anavyoona siri hii kuzidi kuwa nzito na kuhofia Maisha yake.

“Kwa hio unamaanisha kwamba LADO na kupotea kwa ndege ya shirika la M ni swala ambalo lina muunganiko na limeratibiwa kwa makubaliano ya mashirika makubwa ya kijasusi duniani?” Aliuliza na jamaa alitingisha kichwa kukubaliana nae.

“Kwanini mmeamua kunipa hii taarifa?” “Mpango TASAC ni mpango ambao unahusisha serikali ya Urusi kurudisha umoja wa Kisoviet , lakini hili ili liweze kufanikiwa , tunahitaji sapoti kutoka Afrika , tunahitaji udhaifu kutoka kwa mataifa makubwa ambao utatusaidia pale itakapobidi serikali yetu kuingia vitani , mataifa haya hayatoi msaada , lakini nyie wa mataifa ya Afrika mnapaswa kutuunga mkono kwa kukaa kimya.” “Na ili swala hili lifanikiwe unapaswa kuhakikisha asiliamia sabini ya mataifa ya Afrika yanakuwa kwenye huu mpango TASAC na mheshimiwa Raisi wa Urusi amekuchagua wewe kutokana na uzoefu wako katika uongozi, ukifanikisha mpango huu basi serikali ya Urusi itafanya juu chini kubaini ni nini kipo ndani ya operesheni iliopewa jina la LADO”.
“Natakiwa kukubali swala hili hapa hapa?” “Hapana mheshimiwa , swala hili lina umuhimu sana kwa nchi yetu na mheshimiwa Raisi atakupigia simu na mimi nipo hapa kwa ajili ya kukueleza haya , kwani tunajua kuwa wewe ni mmoja ya wahanga wa AJali ya ndege na unataka kulipiza kisasi , lakini kutokana na ukubwa wa tukio lenyewe na udogo wa taifa lako, hautoweza kupata hio nafasi ya kuujua ukweli”Aliongea bwana huyu na heshimiwa Jeremy alikubali kuwa kiongozi wa juu wa mpango TASAC. ****

“Sauron habari za muda huu?” “Salama kabisa mfalme Pluto, habari za Tanzania?” “Hapa ni kwema kabisa Sauron , nimekupigia kupata ripori ya yale tilioongea jana” “Mfalme Pluto , nimeshayakamilisha yote na nimepanga vijana kumi wenye uwezo wa hali ya juu kwa ajili ya kuja nchini Tanzania, lakini kuna jambo moja nimeona nitoe pendekezo” “Edelea kuongea Sauron nakusikiliza” “Nimeona makomandoo hawa wakiingia nchini kama watalii hawatapata kibali cha muda mrefu cha kukaa hapo Tanzania , hivyo nimejaribu kuwasiliana na balozi ya Sweeden nchini Tanzania na kuwaomba watufanyie mpango wa kuwaingiza wanajeshi wetu kama wafanya kazi wao”Roma Alitabasamu. “Sauron wewe unakili sana , hili sikulifikiria , ni kweli watapaswa kukaa nchini muda mrefu kidogo kwani pia nataka wamlinde mke wangu”Sauron alishangaa. “Mfalme Pluto usiniambie umepata mke?” “Ndio Sauron , sio muda mrefu sana nimefanikiwa kupata mke” “Hongera sana mfalme Pluto , ila kwa hatua hio sidhani kama utarudi huku kisiwani” “Yanayotokea kesho hatuyajui Sauonoi hivyo siwezi kuongea lolote juu ya hili”. “Ni kweli Mheshimiwa Pluto , ila nitatamani kumuona malkia wetu”Roma alitabasamu “Utamuona Sauron nitakuja nae siku moja , Sauron kuna jipya lolote kutoka The Zeros?” “Mfalme Pluto vijana bado wanaendelea kufuatilia na naamini muda si mrefu watatupatia taarifa “ “Sawa Sauron , nadhani tutawasiliana baada ya vijana kufika Tanzania”Baada ya hapo waliagana na Roma akakata simu .

Muda huu Roma anawasiliana na Sauron ilikuwa ni saa moja kwenda saa mbili hivi , hivyo baada ya kumaliza tu aliitwa na Bi wema kwa ajili ya chakula cha usiku. Baada ya kufika tu chini na Edna alikuwa akishuka alievalia kigauni kilichokuwa kikipeperuka kiasi kwamba kilimfanya Roma aliekuwa chini ya ngazi aone mapaja ya malaini ya Edna na alijikuta hisia za mapenzi zikimuandama. “Kukaa na mwanamke kama Edna halafu hupati kitumbua chake ni swala ambalo nina uhakika madaktari wataniambia ni sumu kwa Afya yangu , nikimaliza hapa nduki kwa Rose nikapunguze kichupa”Aliwaza Roma huku akivuta kiti na kuketi. Edna na yeye alijikuta akitabasamu baada ya kumuona Roma leo hajatoka kabakia nyumbani , kwani mara nyingi hakuwa akipenda sana Roma a tabia yake ya kutoka na kurudi asubuhi yeye kama mke aliona sio vizuri.
Wanafamilia hawa walikula wakashiba na baada ya hapo Edna aliungana na Bi wema kusafisha vyombo , lakini wakati Edna akiwa bize na vyombo upande wa jikoni Roma alimchungulia kwenye mlango. “Bebi ndio natoka hivyo , hapa hadi kesho”Aliongea Roma na Edna ambaye alikuwa ameweka mikono yake kwenye Sink alijikuta akikunja ngumi kwenye maji na kung`ata meno , kwani kila ambacho kilikuwa kikimfurahisha dakika chache nyuma kimegeuka ndivyo sivyo,Edna aliishia kutingisha kichwa na

Roma hakujali aliondoka. “Yaani huyu mwanaume hatulii nyumbani”Aliongea Edna kwasauti pasipo kujua nyuma yake kasimama jasusi mbobezi wa mapenzi Bi Wema. “Miss ulifikiri sasa atafanyaje , mmeoana lakini hamlali chumba kimoja , yule ni mwanaume na wanaume tendo la nndoa ni kama hitaji lao la msingi hawezi kukaa na mtoto mrembo kama wewe halafu akuangalie kama picha ya ukutani”Edna alifikiria kidogo.

“Bi Wema nitafanyaje , bado sina hisia nae na wewe unaelewa tumeoana kimkataba”. “Naelewa ndio , lakini miss angalau jaribu kuufungua moyo kwa Roma , huenda ukampenda na mkawa Mume na mke kimapenzi sio kimkataba”Edna alitingisha kichwa kuelewa Baada ya kufika chumbani kwake alionekana kuwaza maneno ya Bi Wema na kuona kidogo yana maana. “Au nijaribu kumpa?”Aliwaza Edna akimaanisha ajaribu kumpa Roma kitumbua.

SEHEMU YA 34

Ni jumatatu asubuhi iliokuwa imekucha na makucha yake , wengi huwa hawaipendi hii siku kutokana na mambo mengi ambayo huwa yanatokea wikiend , sio wanafunzi , sio waajiriwa kila mtu anasababu yake ya kutokuipenda hii siku , lakini kwa mwanadada Edna alikuwa na motisha , kwake jumatatu

aliichukulia kama safari ya wiki ya kimafanikio.

Mwanadada huyu alikuwa na jambo kubwa sana mbeleni ambalo alikuwa akilipanga kulifanikisha , dili ambalo kama likienda kama alivyokuwa amepanga , lingezidi kumfanya kuwa mwanamke Tajiri Zaidi , lakIni pia kampuni yake ingezidi kuchanja mbuga na kufahamika duniani kote na ndio maana hakutana ‘glitches’ za aina yoyote katika mkataba anaokwenda kusaini na kampuni ya Yamakuza , kampuni kubwa ndani ya taifa la Japani. Kwake uwekezaji huo ndio mkubwa Zaidi kuwahi kuutekeleza tokea aichukue kampuni hio kutoka kwenye mikono ya mama yake na kama dili hilo pia litafanikiwa ndio dili ambalo litaifanya kampuni yake kuwa na mafanikio makubwa ndani ya mwaka huo.
Asubuhi ya leo alikuwa ameketi kwenye kiti akipata ;Breakfast’ , huku Roma akiwa mbele yake , upande wa kushoto kwake kulikuwa na Bi Wema ambaye muda wote alikuwa akimwangalia Roma kwa tabasamu akiwa ni mwenye kufurahishwa na uwezo wa kula wa Roma. “Siku zote nyumba ikiwa na mwanaume inaonekana kuwa hai”Aliwaza mwanamama huyu Mzungu wa Roho. Upande wa Edna , macho yake yalikuwa kwa Roma , aliwaza Roma ni mwanaume wa aina gani , kwanza amerudi asubuhi hio akitoka kwa wanawake wake , lakini alionesha kutokuwa na hatia hata kidogo , ndio ndoa yao ni ya mkataba lakini angalau aonyeshe ile heshima ambayo ambayo ipo ndani ya neno ‘Ndoa’ lakini kwa Roma hakuwa ni mwenye kujali.

Edna aliendelea kutafakari , kwanini Roma yupo kama alivyo Roma , kwanini hakuwa siriasi na Maisha , haoneshi kuwa na mipango ya kimaisha ya baadae , yeye anafikiria kufanya mageuzi katika biashara lakini mume wake wa mkataba yeye anafurahia chakula na wanawake pasipo mpango wowote alikuwa akishangaa na kujiuliza maswali lakini alikosa majibu.

“Mke wangu , itoshe kusema najivunia sana kuwa mumeo ,maana hii ‘breakfast’ ni nzito , wakati nabeba mizigo kwenye soko la Mbagala kuna siku nilikuwa nashindia mihogo”Aliongea Roma na kisha alibeba bakuli iliokuwa na mchuzi na kupeleka mchuzi wote tumboni.

“Roma unaonaje kwanzia sasa ukiwa siriasi na kazi?”Aliongea Edna aliekuwa akimwangalia ,Roma kabla ya kujibu alichukua yai la kuchemsha na kuligonga mezani na kisha akaanza kulibandua na kisha akalipeleka mdomoni lote , akavuta kikombe cha chai na kushushia.. “Aargh … mke wangu umeng`ang`ania na mimi kuwa siriasi na Maisha , lakini mimi najiona niko siriasi”.

“Uko siriasi kivipi Roma , kila siku naletewa ripoti ya wewe kucheza magemu tu kazini na kwenda kula , huo usiriasi unaozungumzia ni upi, haya ukirudi nyumbani badala ya kukaa kutulia na kuwaza siku ya kesho ,ila wewe unawaza wanawake na unaenda huko unalala na unarudi asubuhi kweli Roma”Edna leo hii asubuhi alionekana kuwa na nongwa sana , kiasi ambacho kilimfanya Roma kushangaa nini kimempata mke wake mpaka kuanza kulalamika.

“Mke wangu wewe piga kazi , mimi nitaishi kama mtoto wa Tajiri , nitafute mapesa mengi ya nini wakati hizi hatutazimaliza …Bebi Edna labda tukipata mtoto na nikiitwa baba naweza kuishi kama baba”.

Edna hakutaka kuongea maana aliona kuongea na Roma hakuna heri yoyote , alichukua mkoba wake na kumuaga Bi Wema na kisha akatoka. “Sijui ninamfanya nini angalau awe siriasi na Maisha?”Aliwaza Edna wakati akiwasha gari yake .

Roma alifika kazini kama kawaida , na kuingia kwenye jengo hili ambalo kwake kila siku sehemu hii ilizidi kumvutia kutokana na harufu nzuri za pafumu za warembo. “Romaa..”Ilikuwa ni sauti iliomwita Roma akiwa anaingia kwenye Lift na mwanadada aliekuwa akimwita alikuwa ni Benadetha. Benadetha kwenye macho ya Roma alikuwa mrembo sana ambaye alitamani pia angalau apate wasaa mzuri wa kumjua nje na ndani , hayo ndio yalikuwa mawazo yake , lakini mwanadada huyu alionekana kuwa bize sana na kazi , muda mwingi hakuwa akipenda sana kupiga Stori kama ilivyokuwa marafiki zake. “Niambie mrembo, za wikiend?” “Nzuri vipi wewe?” “Njema kabisa”Alijibu Roma wakati wakiwa wamesimama wakisubiria Lift ifunguke waingie , lakini mara nyuma yao wakasimama wanaume wawili na wanaume hawa hawakuwa wengine bali alikuwa ni Abu na Elvice .

Elvice baada ya kumuona Roma alijikuta akikumbuka tukio ambalo alifanyiwa na Roma na alijikuta hofu ikianza kumjaa,Benadetha alisalimiana na Abu pamoja na Elvice , ila Roma alionyesha hali ya kutofurahia uwepo wa mabwana hawa. “Mmekuja kufanya nini hapa?”Aliuliza Roma pasipo kusalimia , huku Benadetha yeye akitangulia akiwaacha Abu na Elvice wanamwangalia. “Mr Roma nadhani uwepo wetu hapa haukuhusu , kwanza nasikia una nafasi ndogo sana kwenye hii kampuni kwanini tuongee na wewe juu ya swala lililotuleta hapa?”Aliongea Abu kwa kejeli na Roma kwanza alitabasamu.

“Ni kweli sipaswi kujua nini kimekuleta hapa , lakini naamini unakumbuka onyo nililokupa mara ya mwisho , hivyo kuwa makini”Aliongea Roma na muda huo huo Lift ilifunguka na Roma aliingia huku Abu na Elvice wakiwa wamesimama wakiangalia Lift hio inajifunga taratibu na Roma akamwangalia Elvice na kumkonyeza. “Hawa mafala wote wamekuja kufanya nini hapa?”Alijiuliza Roma wakati akiingia ndani ya ofisi aliokuwa akifanyia kazi na aliiendeea meza yake , huku akisalimiana na baadhi ya wafanya kazi wenzake ambao walikuwa bize , isipokuwa tu Recho pekee ambaye hakuonekana kwenye meza yake na alijiuliza ni kwannini mwanadada huyo hakuwa amefika kazini , lakini alipotezea.

“Hapa nicheze EuroTrack simulator nipoteze poteze muda , hii kazi siipendi , sema ndio hivyo kuna warembo wanaonipa motisha lakini pia nataka kumridhisha mke wangu”Aliwaza Roma na kuwasha gemu na kuanza kucheza , lakini bado akili yae ilionekana kutofarahia gemu hilo , ni kama moyo wake haukuwa na amani , baada ya kuona hafurahii aliinuka kwenye meza yake na kutoka nje ya ofisi, huku wafanyakazi wenzake wakimshangaa , aliingia moja kwa moja kwenye Lift na kwenda juu. “ Miss Airport nahitaji kuonana na CEO”Aliongea Roma mara baada ya kumfikia Monica

mwanamke ambaye alikuwa sekretari wa Edna , kwa Roma mwanadada huyu alimuona kama mbaya kuliko wanawake wote wa hii kampuni , kwanza kabisa alimuona kuwa na kifua ambacho hakikuwa na manyonyo na kilikuwa Flati kama vile barabara za Airport.

Kwa huyu Monica na yeye hakuwa akipendezwa kabisa na Roma , alionekana kutompenda kwenye hii kampuni na alitamanni awe na uwezo amfukuze , lakini licha ya kutokumpenda hakuwa akijua kuwa Roma ni mume wa Boss wake. “Yupo ila ana wageni huwezi kuingia”Aliongea Miss Airport .

“Miss Airport haujui kujibu maswali , darasani ulikuwa unapata ngapi mimi nimeuliza swali moja ila wewe umajibu mawili”Aliongea Roma na kuuendea mlango wa CEO na kuufungua na kuzama ndani na Monica alipandwa na Jazba na kumfuata Roma.

Roma baada ya kuingia alikutana na Sura tano , ya kwanza ilikuwa nni ya Mke wake ambaye yuko ‘Composed’ kama ilivyokuwa kawaida yake ya kujiamini akiwa amekunja nne na suti yake ya rangi nyeupe , wa pili alikuwa ni Nadia mwanasheria Mpya wa kampuni na Roma hakumtaraia ndani hapo na watatu alikuwa ni Doris ambaye alikuwa amependeza kama kawaida , lakini alikuwa na uso wa usiriasi, wawili wa mwisho ni wanaume ambao Roma hakuwa akiwapenda hasa wakiwa karibu na mke wake yaani Abubakari Hamadi na Elvice Temba. Kwanza wote watano walijikuta wakimwangalia Roma ambaye aliingia bila hodi na muda huo huo na Monica aliingia. “Boss nisamehe nimejaribu kumzuia lakini hakunielewa”Aliongea Monica kwa wasiwasi mno , aliogopa kumkasirisha bosi wake.

“Unaweza kwenda kuendelea na kazi Monica”Aliongea Edna ambaye alionekana kuwa kawaida , lakini alikasirishwa na kitendo cha Roma kuingia hapo ndani moyoni kwani alikuwa na kikao muhimu sana na wageni wake, baada ya Monicca kutoka Roma alijongea mpaka upande wa kiti anachokaa mke wake na kisha akaketi huku akizunguka zunguka , hakuwa na wasiwasi hata kidogo, Abuu alikuwa na hasira alitamani afanye shambulizi palepale kwa Roma , kwani alikuwa akimchukia sana bwana huyo , lakini hakuwa na ujasiri wa kupambana na Roma ana kwa ana , alijua sio saizi yake , kwa upande wa Elvice na yeye alikuwa hampendi kabisa Roma , hasa akikumbuka bwana huyo ni mume wa Edna

alijikuta akitaka kuonyesha uwezo wake wa kimapigano aliokuwa ameupata akiwa jeshini , lakini alivyokumbuka namna ambavyo Roma macho yake yalibadilika na kutaka kunyongwa na mkono mmoja aliogopa na kuona atulize mshono Upande wa Doris na Nadia haikuelewaka walikuwa na mawazo gani ila walimwangalia Roma kwa macho ambayo yalikuwa na maswali mengi , upande wa Edna alikuwa akimwangalia kila mmoja aliekuwa hapa muonekano wake , na kisha akamgeukia Roma.

`TELEGRAM` harkingteach `YOUTUBE` harkingteach

, Endelea na kikao chako sijaja kukuvuruga”Aliongea Roma na kisha aligeuza kiti chake na kuangalia upande wa nje kwa kutumia Dirisha akiangalia upande wa bandari hii ya

Dar es salaam ilivyokuwa bize. Edna hakuwa na chakumfanya Roma , kwanza angeonekana sio mke bora kama angemfukuza , lakini pia lilikuwa ni jukumu lake kumlindia heshima Roma kama mume wake , walikuwa wameoana kwa mkataba lakini alikuwa akiheshimu sheria za ndoa , hivyo aliwasihi wenzake

waendelee na kikao. “Tunaweza kuendelea , Roma ni mume wangu hivyo hakuna kinachoharibika akiwepo hapa , labda kama kuna mwenye shida na uwepo wake”Aliongea Edna na kuwaangalia wenzake na Nadia ndio aliekuwa wa kwanza kutingisha kichwa chake kuonyesha anakubaliana na Edna , na wengine wote wakaonyesha sura za kwamba hakuna tatizo , ila ukweli kila mmoja hapo ndani hakufurahishwa na kauli ya Edna , kila mtu aliona kauli hio kama Risasi iliozama moja kwa moja moyoni na kutibua chemba za moyo.

Kikao kiliendelea na Roma aligeuka na kuanza kutumia Computer ya mke wake , kama kawaida alikutana na gemu la nyoka na kuanza kucheza huku akila Karanga zilizokuwa kwenye kibakuli.

“Kutokana na ukubwa wa uwekezaji huu naamini viongozi wote wa juu tunapaswa kwenda Japan kusaini huu mkataba na hayo pia ni mapendekezo ya Viongozi wa Yamakuza”Aliongea Abubakari. “Kuna ulazima wa CEO wote kusafiri mpaka Japan ?”Aliuliza Edna. “Ndio Edna” Maagizo niliopewa na Yamakuza ni kwamba CEO Abubakari na wewe lazima muwepo , hili ni dili kubwa sana ambalo kampuni ya Yamakuza inafanya kwa mara ya kwanza na kampuni za Afrika ,tusilichukulie kwa wepesi”Aliongea Elvice na alionekana yupo hapo ofisini kuwakilisha kampuni ya Yamakuza.

“Kuna ulazima gani wa mke wangu kwenda?”Aliuliza Roma kwa sauti na alionekana kukerwa sana na Elvice kwani aliona hakukuwa na sababu ya Edna kwenda kama tu anataka kuwakilishwa na mtu mwingine. “Mr Roma hili ni swala ambalo linahusu uongozi wa juu wa kampuni , hivyo unatakiwa ukae kimpya mabosi wako tukiongea”Aliongea Abubakari na Roma kwanza alitabasamu. “Kwanza nikurekebishe , unaonekana hauko profesheno na kazi yako , mimi sio boss wako , pili sioni haja ya Edna kwenda kama anataka kuwakilishwa na mtu kutoka kwenye kampuni , sioni utofauti mtu mwingine akienda , kwani mazungumzo ya kibiashara yashafanyika kupitia mkataba na kule ni kitendo cha kutia sahihi , kuna tatizo gani hapo , au shida tu uende na mke wangu”

Abu na Elvice walionekana kukasirishwa sana na Roma , ni kweli hakukuwa na shida ya Edna kwenda ila Elvice alitaka atumie nafasi ya kwenda Japan na Edna ili akajiweke karibu na angalie namna ya kumpata mrembo huyo, na mpango wa Elvice na wa Abuu hakukuwa na

utofauti na kila mtu aliona hio ndio nafasi ya kuongeza ukaribu na Edna , lakini waliona mipango yao Roma anaingilia , kwanini wafurahi. “Alichongea Roma ni sahihi , hakuna haja ya CEO kwenda kama anataka kutuma mwakilishi naweza kwenda mimi au Doris na hata Nasra ambaye ni mhasibu mkuu wa kampuni”Aliongea Nadia na Roma alikumbuka kwanini Nasra hakuwa kwenye kikao hicho kwani na yeye pia swala hili la mkataba lilikuwa likimhusu.

“Swala hili sio nani kwenda , swala ni kwamba kampuni ya Yamakuza wamotoia ombi hilo kama Sharti”Aliongea Elvice na alimfanya Roma akasirike Zaidi , jambo ambalo kwa Nadia na Doris hawakulipenda , kwani Roma alikuwa akionyesha wivu waziwazi. “Mimi Roma Ramoni .. Edna ni mke wangu licha ya kwamba ni kiongozi mkubwa wa kampuni hii lakini pia lazima apate baraka zote kutoka kwangu hilo ni la kwanza , la pili naomba nimuulize mke wangu ..” huku akimwangalia Edna “Mke wangu kwenye huo mkataba kuna kipengele chochote ambacho kinakulazimisha wewe kwenda Japan??”Edna alitingisha kichwa kama hakuna na Roma alitabasamu. “Sasa nasema hivi nisikie mtu anaongea tena kuhusu Mke wangu kwenda kusaini huo mkataba uone ..”

Aliongea Roma na kurudi kwenye kiti na kuendelea kucheza gemu baada ya kutoa biti ambalo lilimkasirisha kila mmoja Abu na Elvice walikasirishwa na kitendo cha Roma kuharibu mipango yao na Doris na Nadia walionekana kuwa na wivu wa Roma kumlinda Edna , walitamani nafasi hio iwe ya kwao. Elvice na Abuu japo ya kukasirika walipiga kimya , hakutaka tena kuongea swala hilo, kwani waliogopa. “Okey kwa upande wangu ataniwakilisha Doris pamoja na Mume wangu”Aliongea Edna na kufanya hali ya hewa ibadilike.

SEHEMUYA 35

Roma alishangazwa na mke wake kumpendekeza kwenda Japani na Doris kwa ajili ya kusaini mkataba huo , lakini sio kwake tu alieshanga , kila mmoa hapo ndani alishangaa isipokuwa Dorisi. “Naona mmeshangaa , lakini nimemchagua mume wangu kuniwakilisha kwakua anafahamu vizuri kuzungumza kijapani , itakuwa msaada mkubwa kwa Doris pia”Aliongea Edna na na alionekana maamuzi yake ni ya mwisho na hakukuwa na wakupinga , ila Roma bado alikuwa akiwaza kwanini mke wake anafanya hayo pasipo kumuambia kwanza kama anataka kwenda

Japani au la. Kikao kiliisha na Edna aliwaambia waondoke kwani alikuwa na mazungumzo na mume wake na hakukuna aliekuwa akipinga wote walikuwa ndani ya ofisi ya mwenye kampuni na pia Edna na Roma ni mume na mke hivyo ni haki yao kuongea hata kama hawapendi. “Mke wangu kuna ulazima mimi wa kwenda Japani ,Doris anaweza kufanya vizuri tu kwani anajua kingereza”.
“Mimi ndio bosi wako na nishafanya maamuzi hivyo, Kwanza inuka kwenye kiti changu”Aliongea na Roma hakuleta ubishi alinyanyuka. “Lakini hata kama, kwanini haukuniambia mapema , tokea nyumbani , jana tumeshinda wote hausemi”Edna alinyamaza hakujua aseme nini , ukweli Edna alitaka kumwambia Roma jana yake usiku lakini Roma aliondoka kwenda kwa mahawala wake hivyo alikosa nafasi. “Kama hutaki kwenda nitaenda mimi mwenyewe” Roma alijikuta akianza kufkiria , aliwaza kama Edna akienda wale mamluki lazima wangetumia nafasi hio kuweka mazoea na mke

wake , lakini pia aliamini huenda Edna hakutaka kwenda kutokana na kuwakwepa Abu na Elvice , aliona huenda ni maamuzi sahihi mke wake ameyafanya. “Okey mke wangu nitaenda kukuwakilisha vyema na kuhakikisha dili lako linafanikiwa”.Edna alitingisha kichwa. Na Roma aliona asiendeleea kukaa hapo ndani na aliusogelea mlango kwa ajili ya kutoka. “Roma..! “Aliita Edna na kumfanya Roma ageuke amwangalie “Nini mke wangu?”. “Najua siku tuliosaini mkataba haukuusoma licha ya kwamba nilikuambia uusome”

“Ndio , lakini mkataba unaingiaje hapa Edna?”Edna alifikiria kidogo kwa kukaa kimya na kumwangalia Roma . “Basi unaweza kwenda tutaonana nyumbani”Aliongea na Roma alitingisha kichwa na kisha akatoka. “Ningemwambia mkataba wetu unakipengele cha kutoingiliana kwenye maswala ya kikazi huenda angekasirika nadhani nimefanya jambo zuri kutoongea , ningezidi kujiweka mbali na yeye na ushauri wa Bi Wema pia ni wa maana lakini pia nataka kujua kwanini macho yake yanabadilika”Aliwaza Edna.

“Miss Airport kazi njema” Aliongea Roma huku akimpita Monica ambaye aliishia kubenua midomo, hakupendezwa na Roma lakini pia alijiuliza kwanini anamwita “Miss Aiport’ . Roma baada ya kutoka moja kwa moja alienda kwenye ofisi ya Doris, alitaka kwenda kumpetipeti mwanamke huyo kwani alijua alikuwa na hasira nae , kwani macho yake wakati wakiwa ndani ya ofisi yalikuwa yakionyesha kabisa , hali iliokuwa ikiendelea kwenye kichwa cha mrembo huyo .

Aliingia na kumkuta akiwa bize kama kawaida akiwa na miwani ya kuzuia mwanga wa Bluu wakati wa kutumia tarakishi,licha ya kumuona Roma ameingia lakini hakutaka kumuongelesha Roma , bado alikuwa na chuki nae. “Bebi Doris , acha kujifanya haujaniona”. “Roma niko bize kwasasa naomba kama hauna jambo la maana usinisumbue”Roma alitabasamu na kisha akasogea mpaka kwenye kiti cha Doris na kukigeuza na kikazunguka na wakaangaliana.

“Roma nimekuambia nina kazi naomba utoke ofisini kwangu , jaribu kuwa muele..” Kabla hajamaliza Roma alikuwa ashanasisha mdomo wake kwa Dorisi na kumfanya mwanamke huyu atoe macho na kuanza kumsukuma Roma , lakini alishindwa kwani Roma alikuwa amembana haswa , na alishitukia mkono umetua kwenye suruali yake, kwenye kitumbua chake na alihisi shoti ikisambaa mwili mzima na Roma aliendelea kufokonyoa.

Dakika mbili mbele Doris hisia zilimzidia na alishindwa kujizuia , akili ilikuwa inamwambia unachofanya sio sahihi na hapo ni ofisini lakini mwili haukuwa tayari kuacha na Roma alitumia udhaifu huo haswa kwani aliongeza mashambulizi na kuendelea kufokonyoa.

Dakika tano mbele Doris alimvua surali Roma mwenyewe na kutoa Mchi wa Roma , huku akisimama kabisa na waliendelea kunyonyana midomo , hakuna aliewaza kabisa hapo ni ofisini , akili zao zilikuwa mbali kabisa , baada ya Roma kuona jaribio lake limefanikia alifyatua suruali ya Doris na kuishusha akikusanya na nguo ya ndani kwa wakati mmoja na Dorisi alielewa somo kwani alishikilia kiti na kubinuka kimbuzi mbuzi na Roma akauzamisha mpini na kilichosikika hapo ni miguno ya kuzidiwa kutoka kwa Dorisi.

“Romaa..Arrgh..”

Doris hakuamini kama amefanya uzinzi kwenye ofisi yake , siku zote alikuwa ni mwenye kujiambia kwamba hata iweje hawezi kupanajisi sehemu yake anayofanyia kazi , lakini siku hii ya leoalikuwa amefanya kile alichokuwa hataki kitokee. “Naomba utoke niendelee na kazi”Aliongea Doris huku akimwangalia Roma. “Seme bebi cha ofisini ni kitamu balaa”. “Roma naomba utoke”Alitumia kauli ya kibabe na Roma hakuwa na ubishi alitoka zake na kurudi kwenye ofisi yake anayofanyia kazi kuendelea na kucheza gemu. Ile anakaa na kutulia tu simu yake ilianza kuita na alipoangalia anaepiga alikuwa ni Najma , alijikuta akijilaumu kwa wakati mmoja kumsahau Najma kwani tokea amuache hospitalini hakuwa amemtafuta hata kidogo.

Alipokea na Najma alionekana kumlalamikia Roma kwamba kamdanganya , kwani alimuahidi kwamba atarudi na Roma nae hakuwa nyuma alimpa habari za kiuongo uongo na mwanadada huyo alikubari japo kishingo upande.
Ki ufupi ndani ya moyo wa Roma alikuwa akimpenda Najma lakini alikuwa mzito sana kuuanzisha mahusiano nae , hakujua ni kwanini lakini aliona kukaa mbali na Najma ni heri Zaidi kuwa nae na ndio maana hakuaka sana kuonekana mbele ya Najma. ****

Ilikuwa ni muda wa usiku saa nne hivi kwenda saa tano , ndani ya jiji la Mwanza ,alionekana mwanamke ambaye alikuwa akikimbia huku akiwa ameshikilia tumbo kwa mkono mmoja , huku mkono mwingine ukimsaidia kumpa sapoti ya kutembea katikati ya chochoro zilizokuwa ndani ya eneo la Mabatini. Mwanamke huyu alionekana kupitia maumivu mengi , kwani damu nyingi zilikuwa zimeganda kwenye nguo zake hasa upande wa tumbon na kwenye kifua , alikuwa amevalia suruali ya jeans rangi nyeusi na viatu vikubwa kama Mabuti vyeusi , huku akiwa na blazia ya rangi nyeupe ambayo ilimfanya damu iliokuwa imemtoka na kusambaa na kuonekana vyema. Watu waliokuwa kwenye hili eneo walionekana kumshangaa mwanamke , licha ya kwamba alionekana kutaka msaada kutoka kwao kutokana na hali yake ila hakukuwa na mtu mwenye ujasili wa kumsaidia na pia kwa mwanamke hakuonekana kuwa tayari kuomba msaada kwa watu waliokuwa ndani ya hili eneo ,ni kama mtu ambaye hakutaka kumbebesha mtu mzigo juu ya mazira yake.

Baada ya mwanamke kutembea kwa umbali mrefu , akikaribia kutoka ndani ya sehemu hii iliokuwa ikifahamika kwa jina la Mabatini kuingia mtaa mwingine upande wa kushoto , alijikuta akidondoka pembeni ya bababara , sehemu ambayo ilikuwa na nyasi ndefu kidogo zilizomfanya kumzibia kwa mbele asipate kuonekana kwa wale wanaopita , lakini sehemu hii pia kulikuwa na mti mkubwa ambao ulifanya hili eneo liwe na kivuli kilichofanya giza kuwa kubwa kuliko maeneo mengine .

“Atakuwa ameelekea wapi?” Aliuliza kijana mmoja kati ya watatu walikuwa barabarani mita kadhaa kutoka alipodondokea Mwanamke , walionekana walikuwa wakimfafuta , wanaume hawa walikuwa wameshikilia siraha mkononi na walionekana walikuwa wakimtafuta mwnamke kwa ajili ya kumfanyia shari. “Ngalu ana jeraha la risasi , hawezi kwenda mbali maana amepoteza damu nyingi “Aliongea lakini moja ya wale wanaume aliona majani yaliokuwa upande wake yakitingishika , huku akiwa ameona kivuli cha mtu lakini ni kama hakuwa na uhakika.

“Oya pale” Aliongea na wenzake wote wakageuza macho kuangalia na hawakutaka tu kuangalia kwa umbali , walianza kusogea ndani ya eneo hilo , ili kuhakiki kile wanachodhania. Walijongea kwa tahadhari kubwa sana , lakini kabla hata hawajaafika ile sehemu , mmoja aliangalia chini na kuona kitu . “Oya Kishoka angalia hiki”Aliongea bwana huyu mfupi kuliko wenzake wote huku akiwa ameshikilia kitambaa aina ya Bandama , walianza kukikagua. “Ndio ni damu hii , hayuko mbali “ waliongea huku wakianza kutawanyika , kwani waliona mtu ambaye walikuwa wakimtafuta alikuwa maeneo hayo . Upande mwingine , wakati vijana hawa wakiendelea kutafuta , Mwanamke alikuwa mita kadhaa kutoka walipokuwa wamesimama na alionekana kuvumilia kutoa kelele kwani maumivu yalikuwa makali , ni kweli alikuwa amedondosha kitambaa alichokuwa akitumia kuzuia sehemu ya jeraha la risasi na kufanya kidonda kizidi kuvuja damu huku maumivu yakiwa ya hali ya juu.

“Hatimae nimekupata” Aliongea bwana huyu aliekuwa anaitwa Kishoka na kuwaita wenzake , Mwanamke hakutaraia kukamatwa mapema hivyo licha ya kuvumilia sana maumivu alitamani kuongea neno , ila nguvu zilimuishia kabisa. “Oya kishoka mpige risasi tuondoke” “Unaonaje tukimpeleka kwa boss kwanza akafanya maamuzi, huenda akawa na maamuzi mengine kuliko aliotoa mwanzo” “Kishoka boss alituambia tukimkamata tumpige risasi , tumpeleke wa nini sasa mtu mwenyewe anakaribia kufa , wewe mmalizie , kama unashindwa lete nifanye mimi” “Okey Ngalu wewe mmalize” Aliongea na kisha akampatia siraha alioshika mkononi kijana mnene kidogo alieenda hewani ambaye alikuwa akifahamika kwa jina la Ngalu na alionekana kutokuwa muoga na kuwa katili kuliko wenzake , alinyoosha bastora kwa ajili ya kumpiga mwanamke aliekuwa chini akiwaangalia kwa tabu , Mwanamke alionekana kuwa nusu mfu hakuweza kujitetea hata kwa kuongea.

Mwanamke , alionekana kukata tamaa kabisa , alianza kuona picha picha wakati akiwa mtoto akicheza na mama yake huku akiwa na furaha sana , alianza kuona kumbukiumbu nzuri ambazo kwake zilionekana kuwa ndio nyakati aliopokuwa na furaha sana katika Maisha yake alipokuwa na mama yake ,alijikuta akilazimisha tabasamu hakutaka kufa akiwa na sononeko moyoni , tabasamu la mwanamke huyu liliashiria hali ya kufuta yote na yupo tayari kupokea kile ambacho Mungu amemuamulia. “Nisamehe mama , sijafanikiwa kulipiza kisasi”

Aliwaza mwanadada huyu na kisha akafumba macho kusubiria saa yake ya mwisho , aliendelea kufumba macho kwa takribani dakika mbili , lakini bado alijiona mzima , alifungua macho huku akiwa anadhania labda wanaume hao wameghairi kumuua kama ambavyo wametumwa na bosi wao , lakini ile anafungua macho anakutana na sura nyingine kabisa , licha ya kwamba macho yake yalikuwa na ukungu , lakini aliweza kutambua kuwa mtu aliekuwa mbele yake alikuwa ni mwanaume ambaye hakuwahi kumuona mahali kutokana na mavazi yake, aliangalia pembeni na kushangaa Zaidi baada ya kuona wale watu waliokuwa wakitaka kumuua dakika chache nyuma wanatapatapa huku miili yao ikishindana na kifo , lakini licha ya mapambano hayo ya kimwili ,kifo kilionekana kuwa na nguvu Zaidi na wakatulia tuli. Mwanaume yule alichuchumaa na kisha alishika mkono wa mwanamke na kisha akatoa mkono aliouweka katika jeraha lake , na kitendo cha kutoa tu mkono damu zilianza kutoka mfululizo. “Inaonekana umeumia sana , inashangaza mwanamke kama wewe kuwa na uwezo mkubwa wa kuvumilia maumivu” Aliongea mwanaume huyu huku mwanamke akiendelea kumwangalia kwa mshangao ,alishindwa kuongea lolote kutokana na hali yake ya kimwili kukosa nguvu hata ya kutamka neno , alichofanya ni kumwangalia tu pasipo kusema lolote. Yule mwanamke nguvu zilizidi kumuishia na alijikuta macho yakijifumba yenyewe pasipo yeye kuyaruhusu na mpaka hapo hakuelewa nini kiliendelea. Baada ya kufumba macho muda mrefu huku akishindwa kuelewa nini kiliendela , hatimae aliweza kuyafumbua , aliangaza eneo alilokuwepo na kujiona yupo ndani ya chumba chenye harufu nzuri , sehemu ambayo hakuwa akiijua kabisa. Wakati akiendelea kuangalia mandhari ya hili eneo , huku akijihisi kuwa na nguvu kuliko alivyokuwa mwanzo , alizidi kushangaa , chumba kilikuwa kizuri lakini alikuwa pake yake na hakujua ni kwa namna gani alifika mahali hapo , alinyanyuka na kukaa kitako huku akianza kukumbuka matukio yaliomtokea na picha mbalimbali zilianza kumtokea , alikumbuka alivyokuwa akipambana na mpaka kupigwa na Risasi tumboni, namna ambavyo alikuwa akikimbia huku akivuja damu na kusikia maumivu makali na watu walioagizwa kummaliza wakiwa nyuma yake wanamfukuzia , alikumbuka yote hayo lakini mwisho kabisa alikumbuka alipokuwa amekamatwa tena na wanaume ambao walikuwa wanataka kummaliza na akafumba macho kwa mara ya mwisho kusubiria kifo chake , aliendelea kukumbuka alipofungua macho yake na kumuona mwnaume ambaye hakuwa akimtambua na baada ya hapo hakuelewa ni nini kiliendelea .
Baada ya mwanamke kukumbuka hayo , alijikuta akijiangalia tumboni na kujiona akiwa msafi huku akiwa na mavazi mengine kabisa , alitoa blazia ya rangi ya pink aliokuwa amevalia na kuangalia eneo la tumboni , lakini kilichomshangaza huyu mwanamke ni kwamba sehemu yake ya tumbo ilikuwa ikifanana na sehemu nyingine za mwili , kwa maana kwamba hakukuwa na jeraha la aina yoyote. “Imekuwaje? Ni swali la kwanza la mwanamke huyu kujiuliza , kwani alikuwa akikumbuka kabisa kuwa alikuwa na jeraha tumboni. “Au nimepona , inamaana nimelala muda mrefu kiasi kwamba hata jeraha langu limepona na kutokuacha kovu?”Aliendelea kujiuliza maswali kedekede yaliokosa majibu. “Hapana hata kama nimepona , lazima kuwe na alama au kovu siwezi kupona haraka sana kwa namna hii”Aliendelea kujiuliza mwanamke maswali meengi , lakini yasio kuwa na majibu , wakati akiendelea kuwaza mara mlango ulifunguliwa na akaingia mwanamke mwingine.

“Habari yako dada, umeamka?” “Hapa ni wapi na nimelala kwa miezi mingapi?” Mwanadada yule alievalia sketi ya rangi ya bluu na tisheti ambayo kwa kumwangalia mara mmoja tu ungejua ni muhudumu wa hoteli. “Upo Iringa dada , hapa ni Camp Nine Motel , umeletwa jana na mwanaume alietambulisha kwa jina la Roa Ramoni” “Roma Ramoni , jana???!!!”Mwanamke alishangaa yaani kama ni kweli aliletwa jana , inamaana ni jana yake alipigwa risasi na kuokolewa lakini pia ni jana yake ameletwa hapa Moteli na mtu anaefahamika kwa jina la Roma Ramoni akiwa na jeraha tumboni. “Dada leo ni tarhe ngapi na ni siku gani?”Mwanadada muhudumu alishangaa. “Leo ni Jumanne na ni tarehe ishirini mwezi wa kumi mwaka 2021”Alizidi kushagaa Zaidi na Zaidi , aliinua tena blazia aliokuwa amevaa na kuangalia sehemu ambayo anakumbuka kabisa amepigwa risasi lakini bado ni vilevile. “Dada hebu kwanza naomba unieleze , wakati naletwa hapa nilikuwaje kuwaje yaani sikuwa nimeumia?”Mwanadada muhudumu bado aliendelea kushangaa , kwanini mteja wake ana maswali mengi , kwani alichokuwa akikumbuka kwenye akili yake ni kwamba mwanaume aliemleta alimuachia tu maagizo kwamba mtu wake anapaswa kupewa huduma kwa uangalizi mpaka pale atakapo amka lakini hakuwa na shida yoyote Zaidi ya kuwa usingizini.

“Uliletwa kama ulivyo tofauti ni kwamba ulikuwa tu umelala , mbona maswali mengi dada kwani aliekuleta sio mpenzi wako?” Mwanamke bado alishangaa maswali ya mhudumu na kuzidi kuchanganyikiwa Zaidi , alitaka kuthitbitisha kile ambacho anawaza , hakuamini kwamba yupo ndotoni na kupigwa kwake risasi kulikuwa ni ndoto. “Jana nimeletwa hapa saa ngapi ?”Aliuliza mwanamke na mhudumu akafikiria kuonekana alikuwa akikumbuka.

“Umeletwa hapa kati ya saa tano na nusu hivi”Mshangao mwingine ulimpata mwanamke . “Kama nililetwa saa tano na nusu na nilikuwa Mwanza wakati napigwa risasi amenisafirisha vipi mpaka kunileta Iringa ndani ya nusu saa” mwanamke aliwaza .

“Dada mini nina wateja wengine wa kuwahudumia , hizi ni pesa ambazo mpenzi wako kakuachia kaniambia ni kukabidhi baada ya kuamka , alisema zitakusadia katika matumizi”Aliongea mwanadada yule huku akitoa kibunda cha pesa zilizokuwa kwenye mfumo wa Euro na kumkabidhi mwanamke na mwanamke

alizidi kushangaa maradufu. Baada ya mhudumu kutoka , mwanamke alijiramba kofi moja zito ili aamke katika ndoto , lakini haikuwa ndoto , bado alihisi maumivu na kujiona kinachotendeka kwa wakati huo ni uhalisia. “Rose amka kwenye usingizi , Rose unaota amka” Mwanamke alijiambia kwa kujiita jina lake , ili aamke katika ndoto , lakini bado mwanamke hakua akiota kila kitu kilikuwa ni uhalisia na mwanamke katika kichwa chake likabaki jina la Roma Ramoni . Naam mwanamke ndio Rose wa Club B ilikuwaje inaendelea Kiliendelea nini baada ya hapo .. tunaendelea…

GUSA HAPA KUENDELEA NA SIMULIZI

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA

Mpya zaidi Nzee zaidi

Ads related

Smartwatchs