NILIEMDHANIA KAHABA KUMBE NI BIKRA

.

25 - 28

.

NILIEMDHANIA KAHABA KUMBE NI BIKRA

.

SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO.

.

Mage kwanza kabisa alishangazwa na urembo wa Najma kiasi kwamba alijiulizaje huyu Jambazi akapata pisi kama hio kwenye Maisha yake , lakini hakukuwa na majibu sahihi yaliopatikanan katika halmashari ya kichwa chake.

.

“Najma usilie tena .. kaka yako alipatwa na matatizo na kwasasa yupo kalazwa anapatiwa matibabu , mimi naenda na hawa polisi kuna jambo la kuweka sawa , hakikisha kaka yako anapatiwa matibabu sawa?”Aliongea Roma kama mwanaume na mwanadada huyu aliekuwa ametokewa na machozi kutingisha kichwa kwa kukubaliana nae , lakini licha ya kumuuelewa alionekana hakuwa tayari kumuachia Roma. “Eti kuna jambo la kuweka sawa .. yaani huna aibu unamuongopea mwanamke mrembo kama huuyu hahaha.. wewe mwambie unaenda jela na atafute bwana mwingine”aliongea Mage kwa kebehi na kumfanya Nama amwangalie mwanadada huyo kwa hasira. “Wewe dada wa kitrafiki , mimi namjua Roma sio Jambazi na hayo maneno yote unayoongea hayakai kwenye Maisha ya

.

Roma”Aliongea Najma na kumfanya Roma amwangalie mwanamke huyu na kutabasamu.

.

“Hilo litajulikana mrembo eh na Ushahidi tulionao , hakuna mengi ya kuzungumza na nitahakikisha hili Jambazi halirudi mtaani kuwarubuni Watoto wakike kama wewe , Mrembo wewe ni mhanga huyu jamaa kakubuhu hivyo shukuru ninamtoa kwenye Maisha yako , nakwambia utanishukuru baadae”

.

Aliongea Mage na baada ya kumaliza tu Difenda ya polisi iliingia hapo ndani na Mage aliwaamrisha polisi wengine waendeshe gari ya Roma na Mage akapanda kwenye pikipiki yake huku wakimwacha Najma anaetokwa na machozi.

.

“Najma nitarudi baadae sawa , usiwe na wasiwasi . hakikisha kaka yako anapatiwa matibabu”aliongea Roma na kufanya watu waliokuwa eneo hili la hospitali washangazwe na Roma maana maneno yake yalikuwa na nguvu sana kwenye mioyo ya watu hawa.

.

Ni baada ya lisaa limoja tokea Roma aingizwe ndani ya kituo kikubwa cha polisi wilaya ya Temeke alionekana mwanamke mmoa mrembo sana maarufu sana hapa nchini akiingia akiwa ameshikilia mkoba wake , huyu mwanadada alikuwa mrembo sio kawaida , ila licha ya urembo wake wote hakuwa akimfikia mrembo Edna.

.

Mwanadada huyu hakuwa mwingine bali alifahamika kwa jina la Nadia Alfonso , lakini nchini na duniani wengi walikuwa wakimuita kwa jina la ‘Goddes of law’ umaarufu wa jina hili mwanamke huyu

.

hakupewa tu , ila yote hayo ni kutokana na heshima aliojijengea katika ulingo wa kutafsiri sheria, usomi wa mwanadada huyu pamoja

.

na kipaji chake kilichangia pakubwa heshima aliokuwa nayo . Nsdia Alfonso ni mwanasheria aliemaliza masomo yake ndani ya chou kikuu cha Harvard kuanzia digrii yake ya kwanza mpaka ngazi ya juu yabisa ya PhD , unaweza ukajiuliza inakuwaje mwanamke mdogo kama huyu kuwa na mafanikio makubwa kama hayo , lakini yote hayo ni kutokana na juhudi binafsi za mwanadada huyu tokea alipkuwa mdogo , lakini pia ukijumlisha na uwezo mkubwa wa akili Mungu aliombariki nao.

.

Umaarufu wake unakuja mara baada ya kusimamia kesi ya Raisi mstaafu wa Korea kusini , kesi ambayo ilikuwa ni gumzo sana duniani , kesi ambayo ilikuwa ikimtuhumu raisi huyo kwa ufisadi , lakini kwa uwezo mkubwa wa Nadia raisi huyo alipata haki yake na Dunia ikatambua kuwa raisi huyo sio kama walivyomdhania kwani alisafisha jina lake , lakini kufanikiwa huko kunazua gumzo baada ya Raisi huyo kutoa hotuba ya shukrani mbele ya waandishi wa habari na kumshukuru Nadia Alfonso kama mwanasheria mkuu alisimama kidete katika kufanikisha kwake kupata haki yake kisheria , lakini pia kusafishika kwa kile alichokiita kusingiziwa kesi ya ufisadi , kwanzia siku hio ndipo jina la Nadia liliposambaa duniani ,umahiri wake uliotukuka aliounesha katika kesi hio , kwanzia kukusanya Ushahidi ulimpa heshima kubwa sana., umaarufu ulimfanya mwanadada huyu kutafutwa na watu wengi maarufu duniani

.

kwa ajili ya kusimamia kesi zao hayo ni machache kuhusu Nadia A.k.a Goddes of Law. Polisi waliokuwa wakimjua mwanadada huyu ambaye alikuwa akipewa heshima kubwa na Taifa kwakuwa mtanzania wa kwanza kung`ara katika fani ya sheria , walihaha , walikuwa wakijiuliza imekuwaje mwanasheria huyu akaja kwenye kituo chao , na si hao tu , hata

.

Mage aliekuwa yupo kituoni hapo kuhakikisha Roma hachomoki alishangazwa sana. Kwanza kabisa Nadia kwake alikuwa ni Role Model , kwani katika Maisha yake Mage alikuwa akipenda sana sheria na alipigania sana ndoto yake hio kuja kuwa mwanasheria huku nguvu kubwa ya kimsukumo ikitoka kwa Nadia ambaye watu wengi katika sheria walimuita ‘Chain Breaker’ yaani mkata minyororo au kwa tafsiri ya haraka haraka yaa maana hi ni kwamba mtu ambaye ameshinda vizuizi vyote yeye kama mwanamke na kuudhihirishia ulimwengu kama mshindi , sasa wewe jaribu kuwaza mtu ambaye ulimhudusu kwenye Maisha yako yote akatokea mbele yako ghafla tu , basi hio ndio namna ambavyo Mage alishituka na hakuwa akiamini kwamba mtu aliekuwa mbele yake alikuwa ni ‘Goddes of law’ mwanamke aliekuwa akimpenda na kumpenda Zaidi ya neno lenyewe.

.

Mage machozi yalianza kumtoka , alikumbuka miaka kadhaa nyuma alivyokuwa akipambania kusoma sheria , lakini kutokanana na kile alichokiita mweyewe uwezo wake mdogo kiakili alikuwa akifeli kila mara na kumpelekea kukata tamaa na kuachana na sheria na kujiunga na jeshi la polisi huku akiamini kwamba polisi na wanasheria wanafanana kwa vitu vingi ,aliamini licha ya kufeli kuwa mwanasheria kuwa polisi sio mbali sana na ndoto zake. Mkuu wa kituo cha polisi ndio wa kwanza kutoka kwa ajili ya kuonana na Nadia ili kumpa heshima zote kubwa , kwani mwanadada huyo hakuwa mdogo kabisa ndani ya

.

taifa hili, lakini licha ya hivyo polisi wengine wote walijipanga mstari kwa ajili ya kutoa heshima kwa Goddes of law. “Karibu sana mheshimiwa ,, Ini furaha kwangu kufamiana na mrembo kama wewe na mtu mkubwa sana duniani karibu kituoni kwetu”. “Asante sana , lakini sijaja hapa kimatembezi nipo hapa kama mwanasheria na nina mteja wangu hapa”Aliongea Nadia kwa sauti yake tamu na kuwafanya polisi wote washangae , anachozungumza Nadia , kwanza hapo polisi hakukuwa na mtuhumiwa mwenye hadhi ya juu kama anavyoongea mwanadada huyu , kwani hakuwa na taarifa ya mtu wa hadhi alieshikiliwa na kituo chake Zaidi ya vikapuku tu waliowafunga.

.

“Mheshimiwa Labda umekosea , hapa hatuna mtu tuliemshikilia ambaye ni wa hadhi kuhudumiwa na wewe kisheria” “Kwangu kila mtu anaehitaji sheria anapaswa kuhudumiwa na mimi na sijawahi kubagua watu kutokana na nafasi zao katika jamii”Baada ya kuongea hivyo alimpita mkuu huyu wa kituo .

.

“Pumbavu nimeongea ujinga”Aliwaza mkuu huyu wakituo huku akifatisha nyuma na waliingia kwenye ofisi ya kuonana na wageni. “Nipo hapa kwa ajili ya mteja wangu anaefahamika kwa jina la Roma Ramoni”Aliongea na kumfanya Mheshimiwa ashituke na kujiuliza Roma ni nani mpaka mtu mkubwa duniani kama huyu aje kumtoa.

.

“Mheshimiwa mtu unayemzungumzia ni jambazi ambalo tulikuwa tukilitafuta kwa muda mrefu sana na leo tumemkamata hatuwezi kumuachia kirahisi” Aliongea Mkuu wa kituo na hakuwa tayari kumuachia Roma kizembe hivyo , kwani alishuhudia yale maburungutu ya pesa na alikuwa ashayapigia plani kabisa wa kulipa deni ambalo alikuwa akidaiwa na anaemdai kumkalia kooni , lakini pia alikuwa akipanga kulipa kodi ya nyumba anayoishi maana hakuwa akiishi kwenye nyumba za polisi maaruufu kama kota , lakini pia alikuwa akisumbuliwa na mchepuko wake juu ya hela ya mtaji na alikuwa amenyimwa kitumbua na mchepuko huyo kwa muda wa mwezi mmoja , pia mke wake alikuwa akidaiwa vikoba sasa kwa matatizo hayo yote aliona kwa pesa hizo zilizofika kwenye ofisi yake , aliona ni Mungu ndio kaleta fursa , sasa hakuwa mzembe kiasi hicho licha ya kwamba mtu aliekuwa mbele yake alikuwa mkubwa tu katika sheria, tamaa ya pesa ikisukumwa na matatizo aliokuwa nayo aliona asimamie msimambo wake

.

“Nishatangulia kusema sipo hapa kaa mtu maarufu , ila nimekuja kwa ajili ya mteja wangu na nina Ushahidi wa kutosha ambao unamfanya mteja wangu kutokuwa na makosa” Aliongea mwanadada huyu kwa upole na kujiamnini kisha akatoa Ushahidi wake na kwa namna ambavyo mwanadada huyu alielezea na kuoonyesha uhahidi Mkuu wa kituo alijisemea moyoni yes hapa kakutana na profesheno mwenyewe.

.

“Naomba kwanza kuonana na mteja wangu”Aliongea Nadia na mkuu wa kituo hakuwa na sababu ya kumzuia . Huku upande wa nje Mage alikuwa kwenye mshangao mara baada ya kusikia kuwa Mrembo Nadia amekuja kwa ajili ya Roma , alishangaa sana sana , inakuwaje choko kama Roma kuja kupata huduma ya kisheria kutoka kwa mwanasheria nguli duniani na hapo hapo swali la Roma ni nani lilianza kuibuka kwenye kichwa chake.

.

“Pluto!” Aliita Nadia na kumfanya Roma anyanyuie uso wake na kuangalia sauti tamu inayomwita kwa jina ambalo hajalisikia muda mrefu.

.

“Haha.. Nadia unafanya nini hapa?”Roma alishangaa sana na alionekana alikuwa akimfahamu vyema Nadia na mrembo huyu aliachia tabasamu ambalo ungekuwa mwanaume rijali kama Roma ungekuwa hoi. “Za siku nyingi The Great Pluto nimefurahi sana kukuona tena , hujui tu nilivyokuwa nikitamani kupata nafasi ya sisi kuonana tena tokea tulivyo achana nchini

.

Korea Kusini” “Nadia hayo mambo tuache kuyaongelea sasa hivi , nataka uniambie unafanya nini hapa”Aliongea Roma kwa usiriasi na mwanadada huyu alimwangalia na kuonekana kama hajafurahia , kwani alitamani kumuona Roma akiwa kwenye mshangao na furaha ya wao kukutana tena baada ya miaka mingi. “Nipo hapa kama mwanasheria mpya wa kampuni unayofanyia kazi, na nipo kukutoa”Aliongea mwanadada huyu na kumfanya Roma ashangae.

.

“Okey! Basi fanya hima nitoke hapa maana nina njaa sio poa”Aliongea Roma huku akijigusa tumbo , yaani kwa Roma alionekana hakuwa akimchukulia kabisa Nadia kama mtu mkubwa vile tofauti na wengi walivyokuwa wakimchukulia , kwani Nadia alikuwa akipewa heshima ya jiuu mpaka na maraisi wa Afrika , lakini kwa Roma alimuona Nadia kama wa kawaida.

.

“Tayari mpaka sasa upo huru”Aliongea Nadia na mlango ulifunguliwa na akaingia mkuu wa kituo akiwa ni mwenye kutoa jasho jingi usoni. “Mheshimiwa mteja wako yupo huru”Aliongea mkuu huyu huku akionekana ni mwenye kuhema , sijui nini kimemtokea maana ujasiri aliokuwa nao umeisha wote.

.

“Daah ! Afadhali maana sio kwa njaa hii ,Nadia uko vizuri sana kwenye kazi yako”Aliongea Roma huku akiamka wa kwanza na kutangulia mlangoni akimuacha Nadia aliekuwa akimwangalia mwanaume huyo kwa hali ya hudhuni inaonekana alitarajia kitu kikubwa Zaidi kutoka kwa Roma.

.

“Niletewe begi langu lenye pesa niondoke nina njaa ”Aliongea Roma huku akimwangalia Mage aliekuwa akimwangalia bwana huyu pasipo kummaliza na alionekana ni mwenye maswali mengi sana katika kichwa chake.

.

“Boss begi lako hili hapa”Aliongea Afande mmoja kwa heshima na kumpatia Roma begi lake na Roma alilibeba lakini akasita. “Huu uzito ni tofauti , kuna kiasi cha pesa kimepungua”Aliongea Roma na kuwafanya mapolisi hawa wote waangaliane kama kondoo. “Rudisheni pesa zote zilizokuwa humu ndani , najua kiasi kamili cha hizi pesa , mkigoma nitakaa hapa nakuhesabu zote na hakuna mtu kuondoka nikihakikisha hela ni pungufu nitawasachi wote” “Rudisheni pesa , acheni kuvunja sheria la sivyo swala hili sitoliacha lipite hivi hivi”Aliongea Nadia baada ya kumuona Roma anaongea na Polisi wote walitoa jasho akiwemo mkuu wa kituo.

.

“Huyu jamaa mahela yote hayo kajuaje nimepunguza vibunda viwili”Aliwaza mkuu wa kituo huku akikumbuka vibunda alivyoficha ofisini kwake,wakati akiendelea kutoa jasho simu yake iliingia ujumbe na kufungua na kuangalia meseji ilitoka kwa jina la ‘Mke Wangu’

.

“BABA LEAH MWENYE NYUMBA ANAKUSUBIRI NA ANASEMA HAONDOKI MPAKA UTOE PESA YAKE , HALAFU GESI IMEISHA

.

MPAKA SASA HATUJUI TUNAPIKA NA NINI” ilikuwa ni meseji kutoka kwa mke wake iliandikwa kwa herufi kubwa kabisa kuonesha msisitizo , mzee huyu jasho lilizidi .

.

“Hapana sitoi zile pesa nitakuwa mjinga wa karne” Uasiri uliongezeka. “Narudia nataka pesa zangu zote ili niondoke”Aliongea Roma akianza kuwangalia polisi mmoja mmoja na baada ya macho yake kutua kwa mkuu wa kituo , aliona jambo na kumsogelea. “Nataka pesa zangu” Aliongea Roma huku akiwa amemkaribia mkuu wa kituo karibu kabisa. “Sijachukua pesa mimi , siwezi kuiba , mimi ni mkuu wa kituo na nachukia wezi” Aliongea kwa kujiamini na muda huo huo Simu yake iliingia ujumbe mwingine na aliinua simu yake na kuangalia ujumbe huo ulitoka kwa jina la “Fundi cherehani’

.

“ WEWE MWANAUME VIPI MBONA HUTUMI HIO HELA , AU ULIKUWA UNAJIGAMBA BURE UMEPATA PESA NYINGI LEO , KAMA HUNA HELA USEME UACHE KUNISUMBUA MIMI KUNA WANAUME WENZIO WANAWEZA KUNIHUDUMIA , NITUMIE HIO HELA NIKANUNUE WIGI”

.

Baada ya mkuu huyu wa kituo kuona meseji hio alikunja ngumi na kusema liwalo na liwe pesa sitoi. Roma baada ya kuona mkuu wa kituo anakataa , alimsukuma na kisha alimpita na kuingia kwenye ofisi yake , baada ya kuingia tu , alivuta mtoto wa Meza na kuibuka na mabuda mawili ya pesa na kutoka.

.

“Mimi siibiwi kizembe ohoo..”Aliongea huku mkuu wa kituo akimtukana moyoni na kuona mkeka umechanika. “Hawa ndio majambazi ambao unatakiwa kuwakamata kama unajali sana sheria , sio raia wema kama sisi mrembo eh” Aliongea Roma wakati akiwa amemsogelea Mage karibu kabisa na Mage hakuwa na la kuongea kwani wakati huo alionekana kuwa kwenye mawazo mengi sana kwa wakati mmoja. Roma baada ya kutoka alifanya mawasiliano na Nasr ana kumuuliza yuko wapi na mwanadada huyo alimjibu bado yupo ofisni , Roma alishangaa kwani muda ulikuwa umeenda sana , lakini alijua huenda mwanadada huyo kabanwa na majukumu mengi Zaidi. Ndani ya masaa machache Roma alikuwa ashafika ndani ya kampuni

.

, haikueleweka waliachana vipi na mrembo Nadia ila Roma alikuwa ni aina flani ya wanaume ambao hawakujali sana baadhi ya mambo na ilionekana anahistoria kubwa san ana mwanadada huyo. ******

.

MASAA MACHACHE NYUMA Kitendo cha Roma kufanikisha kazi ya kurudisha feza kutoka PANZ Security kilimfurahisha sana Edna, na kwa mara ya kwanza alijihisi kweli ana mume. “Nitampikia chakula leo ,ananidharau sana sijui kupika ananiona sistahili kuwa mke ”Aliwaza mrembo huyu wakati akiwa ndani ya ofisi yake “Bosi Miss Nadia amefika?” ilikuwa ni sauti ya Monica akitoa taarifa kwa bosi wake. “Okey mruhusu aingie” “Wow! You are beutifull Edna as the rumors” “Asante sana Nadia , na wewe pia umrembo” Wawili hawa walikaribishana na kuanza mazungumzo ya kibiashara. “Nimekubali ombi la kuwa mwanasheria wa Kampuni yako”Edna alishangaa maana haikuwa kazi rahisi kumfanya mwanasheria mkubwa duniani kuwa mwanasheria wa kampuni change kama Vexto maana

.

Nadia alikuwa akifanya kazi na makampuni makubwa kama Sumsung

.

“Nashukuru sana Nadia kwa kuchagua kufanya kazi na kampuni yangu na niseme tu nitahakikisha unafurahia kufanya kazi na sisi”. Nadia alitabasamu huku akihusudu urembo aliokuwa nao Edna , alikiri kuwa hakuwa akiingia kwa urembo wa mwanadada huyo hata kidogo. Basi wawili hawa walikutana kwa ajili ya kusaini mkataba wa Nadia kusimamia kampuni ya Edna kisheria yaani VExto. Wakati wakiagana mara simu ya CEO Edna iliita na alipoangalia jina aliona ni ‘Mbakaji’ na bahati mbaya ni kwamba simu ilikuwa mezani hivyo Nadia aliona jia hilo na kujiuta akishangaa.

.

“Hello!” “Bebi nimekamatwa tena na polisi”Ilikuwa ni sauti ya Roma na Edna alishangaa. “Ilikuwaje “ “Nina kesi ya utakatishaji fedha , nimedharau sharia za nchi”Aliongea Roma na Edna hakuongea chochote . “Bebi mbona huongei , usiniambie mapenzi siku hizi yamepungua kiasi cha kutaka mumeo nikae jela”Edna alimwangalia Nadia. “Natuma mwanasheria aje kukutoa” Baada ya kukata simu Edna alivuta pumzi. “Nitaenda mimi” Aliongea mwanadada Nadia. Nadna alishangaa “Lakini..” “Usiwe na wasiwasi , najua unachofikiria lakini nitaenda mimi iweke kama kazi yangu ya kwanza kwa kampuni”Baada ya kuongea maneno hayo Nadia alichukua mkoba wake na kushuka hadi kwenye maegesho ya gari na kuingia . “Evans nipe taarifa?” Aliongea mwanadada huyu na kupewa taarifa na mtu anaefahamika kwa jina la Evans. “Okey ! nikusanyie ushahidi wote na tukutane” “Sawa madam” ilisikika sauti upande wa pili wa simu . Baada ya smu hio kukatwa mwanadada huyu alifatufa jina lingine na kupiga . “ Ndio boss nishasaini mkataba, anaonekana kufurahia sana kwa mimi kufanya kazi ndani ya kamupini” “Hongera sana Nadia ni mwanzo mzuri nadhani ni wakati sasa wa kuendelea mipango yetu” ilisikika sauti nyingine kwenye simu , sauti nzito.

.

SURA YA ISHIRINI NA SITA A

.

Muda wa saa kumi na nusu Edna alifika nyumbani huku mwanadada huyu akionekana siku ya leo kuwa na furaha kuliko siku zote jambo ambalo Bi wema aliligundua , lakini hakuuliza Zaidi , kwake huyu mwanamke alitamani sana kumuona Edna akifurahi ndio iliokuwa ndoto yake kubwwa sana , alikuwa akiumizwa sana na tabia ya Edna muda wote kufanya kazi kiasi kwamba kwake hakuwa na siku ya kupumzika , Edna hakuwa kama wafanya biashara wengine ambao walikuwa wakipenda kula bata kila ifikapo wikiendi , Edna yeye alikuwa ni aina flani ya wanawake ambao alikuwa akirudi nyumbani ni kusomana kulala. Ndani ya chumba cha Edna kulikuwa na mavitabu mengi sana na karibia vitabu vyote hivyo alikuwa amevisoma , kwa mtu wa kawaida unaweza kushangazwa na swala hilo lakini kwa Edna lilikuwa swala la kawaida sana , ndio Maisha yake ambayo alikuwa amezoea , kwake kusoma vitabu ndio ilikuwa starehe yake kuliko kujichanganya na marafiki.

.

Edna alikuwa ni mtu wa kutabasamu mara chache sana , muda wote alikuwa yupo siriasi kiasi ambacho kilifanya hata wafanya kazi wenzake wamuogope kumsogelea, lakini leo hii mwanadada huyu anaonekana kutabasamu mbele ya Bi Wema , mwanamama huyu aliekula chumvi nyingi alitamani kujua ni kipi kinamfanya mwanae huyu wa kambo kutabasamu , ila hautaka kuuliza. “Bi Wema leo niachie jiko nitapika mimi” aliongea Edna na kumfanya Bi wema kutumbua macho

.

lakini Edna hakujali sana , alikaa kwenye sofa huku mkononi akiwa ameshikilia kitabu cha mapishi. “Sawa Miss , lakini haujawahi kuingia jikoni utapika nini?” “Bi Wema hio ni siri , wewe utaona wakati wa kupakua”Bi Wema alijikuta akitabasamu na katika akili yake alikuwa ashajua kilichokuwa kikiendelea kwa Edna , aliamini kuna jambo ambalo lilikuwa limetokea kazini na kusababisha mabadiliko hayo . Saa moja kamili za jioni Edna alikuwa bize na mapishi huku Bi Wema akiendelea kuangalia tamthilia, muda nao ulisonga lakini Roma bado hakuwa amerudi.

.

“Bi Wema Roma hajarudi bado?”Aliuliza mwanadada huyu aliekuwa amevalia Apron na kumfanya apendeze sana , kiasi kwamba wewe ndio ungekuwa mume wa Edna na ungemuana jinsi alivyovalia Apron ni hakika ungenenepa kabla hata ya kula chakula. “Hajarudi bado na hajatoa hata taarifa kama atachelewa kurudi”Aliongea Bi Wema na kumfanya Edna kuonyesha hali ya kuhuzunika. “Ukute na hangaika hapa yupo na mwanamke”Aliwaza Edna huku akirudi jikoni kuendelea na upishi akitegemea Roma atarudi.

.

Muda wa saa tatu na nusu alionekana Bi Wema akiwa ndani ya chumba cha maliwato akitapika huku akisukutua maji. “Nimewahi kula chakula kibaya ila hiki cha leo ni kiboko , Chakula kama mavi ya mtoto mchanga khaa.. Edna ananitia aibu jamani”Aliongea Bi Wema huku akisukutua . “Nimekula kumridhisha tu ilia aone na yeye mwanamke , ila kile sio chakula”. Wakati Bi Wema akiendelea kutapika huko ,Edna alikuwa amekaa kwenye sofa akimsubiria mwamba Roma arudi huku Mabakuli ya chakula akiwa ameyapangilia kwenye Meza , na kwa jinsi yalivyopangwa moja kwa moja utaamini kuwa kuna bonge la pishi limefunikwa. Upande Nasra alionekana akiwa nyumbani kwake jikoni akiwa bize na mapishi , alionekana kuwa mtaalamu kweli , kwani kwa namna ambavyo alikuwa akikata kitunguuu Ungejiambia mwenyewe ndio hapa yupo mwanamke. Bebi Nasra unajua sana kupika” Aliongea Roma huku akiwa amejipumzisha na pensi la kike na haraka haraka ukimwangalia lazima ugundue hilo pensi ni la Nasra maana lilikuwa na Marinda Marinda chepete , ila Roma hakuwa na habari huyu bwana , yaani hakuwa na aibu hata kidogo. Baada ya kula na kushiba , hakukuwa na kilichoendelea zaidi ya kuingia kwenye mtanange . “Bebi hii Staili inaitwaje?”Aliuliza Nasra huku akionekana kukosa pumzi maana alikuwa amelemewa na utamu. “Mh! Mimi hata sijui ila umekaa kipopo popo ,, itakuwa ndio Popo kanyea Mbingu”Aliongea Roma huku akiongeza spidi.

.

Muda wa saa kumi na mbili za Asubuhi Roma aliingiza gari yake nyumbani bila wasiwasi kabisa na baada ya kuliegesha aliingia ndani na kumkuta Bi Wema. Bi wema kama kawaida , alikuwa mzungu wa Roho maana alimpokea Roma na kuitikia salamu kama hakujatokea kitu ila kiukweli moyoni alikuwa na huzuniko , kwani kwa mara ya kwanza anamuona Edna akiingia jikoni jambo ambalo kwake aliliona kama hatua ya kwanza ya Edna kuwa kama mwanamke

.

aliekamilika , lakini Roma hakuonekana nyumbani , aliona kitendo hicho kimemnyong`onyesha Edna juhudi zake , kwani Edna kwa mara ya kwanza alimsubiria Roma kwa muda mrefu jambo ambalo sio kawaida. “Roma jana ulikuwa wapi , hukutoa taarifa Miss alipika na akakusubiri lakini hukutokea”Aliongea Bi wema wakati Roma akianza kupandisha ngazi kuelekea chumbani kwake , lakini baada ya kusikia maneno hayo alijikuta akisimama na kushangaa. “Bi Wema unamaanisha Edna jana kaingia jikoni kupika?”

.

“Ndio chakula bado kipo mezani”Aliongea Bi Wema na Roma hakuendela kwenda juu ,, alirudi chini na kwenda meza ya kulia chakula na kufunua mabakuli yaliopikwa. “Bi Wema nitakula kama kiporo na chai”Aliongea Roma na kupanda ngazi kuelekea chumbani kwake na baada ya muda alishuka kwa aili ya Chai na Edna alikuwa amejaa mezani akinywa chai oamoja na Bi Wema.

.

“Wife hebu tuone leo ulichopika”Aliongea Roma na kisha alifunua mabakuli hayo huku Edna licha ya kwamba hakuwa akimwangalia Roma usoni lakini akili yake ilikuwa ni kusbiria nini ataongea Roma baada ya kula chakula chake.

.

Roma alipakuwa chakula na kisha alichota mtori hhuo na kupeleka kinywani na kula. “Nilijua mtori kumbe ni tambi Looh! Hapa nina jipu sio mke”Roma aliwaza moyomi na kisha akachota kijiko kingine na kula , wakati huo Bi Wema alikuwa amekunja sura utadhani chakula kilikuwa kikiingia Tumboni kwake.

.

Roma alimwangalia Edna huku mrembo huyu akijifanyisha kunywa chai , lakini alikuwa akisubiri Roma atamke neno.

.

“Wife umejitahidi sana leo, ukiendelea hivi utakuwa mpishi mzuri”Aliongea Roma na kuendelea kula bila ya wasiwasi huku nia yake ni kutokumkatisha tamaa Edna na Bi wema alifurahishwa na maneno ya Roma na kule kukasirika kwa kutokurudi nyumbani kulipotea , lakini bado kuna kitu kilimshangaza , kwa jinsi chakula hiko kilivyokuwa na chumvi , alijiuliza Roma amewezaje kula.

.

“Okey ! ngoja nijipe adhabu ya kumaliza hiki chakula maana sio kwa huu utopolo”Aliwaza Roma , ila kwa Edna moyo wake ulitabasamu , licha ya kwamba hakuwa akionyesha usoni lakini alifurahia sifa hizo kutoka kwa Roma. Roma baada ya kumaliza kunywa chai ya asubuhi alipandisha chumbani kwake kwa ajili ya kupumzika , siku hii ya leo aliona akae kidogo nyumbani , kwani tokea afike ndani ya familia hii hakuwahi kukaa nyumbani kwa muda mrefu , muda mwingi alikuwa misele ya hapa na pale. Wakati akiwa amejilaza kwenye kitanda alijikuta akiachia tabasamu . “Edna mambo yake ni kama ya Seventeen nakiri kwa asilimia kubwa wanafanana”Aliwaza Roma huku akiwa ni mwenye tabasamu. **** 1998- KIGALI RWANDA March 8 Ilikuwa ni ndani ya ofisi ya mheshimiwa Jeremy Paul (JP),walionekana watu wanne wakiwa wameketi ndani ya ofisi hii na ilionekana kuna kikao kilichokuwa kikiendelea kati ya mheshimiwa Jeremy na wanaume watatu kukamilisha idadi ya wanaume wane ndani ya ofisi hii. Wanaiume watatu walikuwa ni watu maarufu sana waliokuwa wakifahamika ndani ya jiji la Kigali na moja ya sifa kubwa ambayo ilikuwa ikiwafanya watu hawa kufahamika ni kutokana na michango yao katika taifa hili dogo.

.

Mtu wa kwanza aliekuwa amekaa upande wa kushoto wa mheshimiwa Jrtrmy alifahamika kwa jina la Uwimana ,huyu alikuwa ni mfanya biashara mkubwa sana ndani ya taifa hili la Rwanda na alikuwa akimiliki visima vingi vya Mafuta , pamoja na kampuni kubwa ya usafirishaji , Mwingine alikuwa ni Jean , Wengi ndani ya taifa hili wanapenda kumuita kwa jina la Profesa J , huyu nae licha ya kuwa mfanya biashara lakini pia alikuwa ni mkuu wa chuo kikuu cha Rwanda,Mtu wa tatu hakuwa akifahamika sana ndani ya taifa la Rwanda kama alivyokuwa akifahamika ndani ya taifa la Tanzania ,Alikuwa akifahamika kwa ina la Aziz Mohamed huyu alikuwa ni moja ya wafanya biashara wakubwa sana kutoka

.

taifa la Tanzania , lakini pia alikuwa ni moja ya wawekezaji wakubwa ndani ya taifa la Rwanda na ndio maana mchango wake ulikuwa ukiheshimika ndani ya taifa hili. “Ndoto yangu yangu kubwa ni kuona Rwanda ikiwa nchi kubwa sana kiuchumi ndani ya bara la Afrika , na haya yote hayawezi kufanikiwa bila ya uwepo wenu”Aliongea. Huku mabwana hawa wakionekana kutingisha vichwa kuashiria kuwa wako pamoja na mheshimiwa na muheshimiwa. “Mheshimiwa sisi tupo tayari kukuunga mkono katika safari ya ndoto yako ya kuifanya Rwanda kuwa kubwa na tutakuwa ni wenye kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha kuinua uchumi wa taifa hili”Alingea Uwimana Kikao hiki kilionesha dhahiri kilikuwa ni cha mipango juu ya kuifanya Rwanda kuwa nchi kubwa kwa miaka ishirini ijayo, mipango ambayo

.

mheshimiwa Jeremy aliona watu pekee wakufanikisha nao swala hilo ni hao mabwana watatu , haikueleweka ni kwanii Mheshimiwa akamwinginza mtu mwingine kutoka taifa la nje yaani Azizi Mohamed. Baada ya kikao hiki kuisha

.

Mheshimiwa huyu alionekana kuwa na maongezi binafsi na Aziz kwani wale mabwana wengine walikuwa washatoka ndani ya ofisi hii. “Asante sana Aziz kwa kufanikisha kurudisha sehemu ya damu yangu mikononi mwangu”. “Jeremy sisi ni marafiki wa muda mrefu sana hupaswi kunishukuru , lakini nisingependa kuona katika Maisha yako unakosa furaha , umemkosa Rahel , lakini naamini zawadi aliokupatia ni kubwa na angalau itakufanya usiishi kwa kujuitia”Aliongea Azizi huku akimtaja Rahel na Jeremy alionekana kukosa furaha mara baada ya kusikia jina la Rahel. “Ni kweli Aziz.. lakini

.

Maisha yangu bado naona kama hayajakamilika kwa kumkosa Rahel , katika Maisha yangu niliamini kwa kuwa raisi hakuna kitu ambacho ninaweza kukosa na kunifanya nisiwe na furaha , lakini Rahel amenifanya nione sikuwa nikifikiria kwa usahihi”. “Ni kweli Jeremy, lakini kwa sasa unatakiwa kumsahau Rahel , yule mwanamke ni mke wa mtu kwa sasa na ni maamuzi ambayo aliyafanye yeye mwenyewe na akakuacha wewe , angalau sasa wekeza nguvu zako katika kulea kichanga alichokuachia kama zawadi”Aliongea Aziz lakini muda huo huo aliingia mwanadada makamu hivi, hakuwa mrembo sana , ila alionekana kuwa mtanashati “Mheshimiwa kuna taarifa mbaya?” “Unamaanisha nini Linda , unamaanisha nini kuhusu taarifa mbaya?” Mwanadada huyu aliefamika kwa jina la Linda alisogelea Rimoti ya Tv na kisha akawasha Runinga na kuweka chaneli ya BBC .

.

BREAKING NEWS: NDEGE YA MALAYSIA AIRLINE ILIOKUWA IKISAFIRI KUTOKA KUAL LAMPUR KUELEKEA BEIJING CHINA YAPOTEZA MAWASILIANO. Taarifa hii ilionekana kumshitua sana

.

mheshimiwa pamoja na Aziz waliouwa wakiangalia Runinga hio lakini kati ya watu hao aliekuwa kwenye hali mbaya Zaidi ni Jeremy. “Linda wasiliana na shirika la ndege la Malaysia wakupe orodha ya majina ya watu waliopanda kwenye hii ndege”Aliongea Mheshimiwa Jeremy huku akiwa ni mwenye wasiwasi mwingi sana. “Jeremy punguza presha naamini huenda kuna tatizo la kawaida tu ambalo limetokea” “Aziz siwezi kutulia kabisa ,unafikiri nitaishije kama kitu kibaya kikimkuta Lorraine ,Nitamwabia nini Rahel , hapana nitaishi kwa majuto makuU kwenye Maisha yangu yote , naomba jambo baya

.

lisitokee”Aliongea Mheshimiwa Jeremy huku akishikilia kifua chake. Ni ndani ya dakika tano Linda alirudi na kuingia ndani ya ofisi , huku wasiwasi ukiwa umejaa kwenye macho yake.

.

“Mheshimiwa hii ndio orodha ya abiria”Aliongea lakini Azizi aliona wasiwasi uliokuwa kwenye macho ya Linda na kwakuwa alikuwa karibu nae alichukua ile karatasi na kuangalia majina hayo na bwana huyu alijikuta akitumbua macho na kumwangalia Rafiki yake Jeremy.

.

“Azizi usiniambie Lorraine ni sehemu ya abiria walikuwepo kwenye hio ndege?” “Jeremy taarifa inasema ndege imepoteza mawasiliano , lakini sio kuanguka tusubirie taarifa kamili , Acha kufikiria mambo mabaya”Aliongea Azizi lakini baada ya kumaliza sentensi yake… “Mheshimiwa..!!”Aliongea linda kwa sauti mara baada ya Mheshimiwa Jeremy kudondoka na kuzimia. SHEMU YA ISHIRINNI NA SABA Taarifa za mheshimiwa Jeremy kuzimia zilikuwa ndani ya ikulu , hazikutoka hata kwa baadhi ya mawaziri Zaidi ya kitengo cha usalama ikulu pamoja na baadhi ya wanafamilia wa mheshimiwa Jeremy. “Nini kimempata mheshimiwa

.

Linda?”Aliuliza mke wa Raisi Jeremy huku akionekana ni mwenye wasiwasi sana , wakiwa nje ya chumba cha matibabu ndani ya ikulu.

.

Lakini Linda hakuwa na jibu la kuongea na kusema hakuwa akijua ni nini kimemkuta mheshimiwa Jeremy Zaidi ya kumwambia First lady huyu wasubiri majibu kutoka kwa daktari.

.

Baada ya masaa kadhaa ya hatimae daktarin wa ikulu alitoka katika chumba cha matibabu. “Inaonekana mheshimiwa kapata mshituko”. “Mshituko , unamaanisha nini mshituko dokta?”Aliuliza mama huyu kwa Jazba huku macho yake yakimgeukia Linda aliekuwa mlinzi wa karibu wa raisi na Linda jasho lilimtoka. “Linda niambie ni jambo gani baya mheshimiwa kakumbana nalo mpaka kupata mshituko?” “Madam ! hata mimi najiuliza swali kama hilo , lakini sina majibu sahihi

.

,maana mheshimiwa nilimkuta akiwa katika hali ya kupoteza fahamu”. Bado haikuwa ikimwingia akilini mwanamama huyu mwenye PhD ya lugha , aliamini kuna jambo ambalo mme wake limemkuta na kumpelekea kupoteza fahamu.

.

Baada ya masaa mawili kadhaa kupita hatimae mheshimiwa Jeremy alirejewa na fahamu zake na swali la kwanza baada ya kuamka lilitoka kwa mke wake aitaka amueleze nini kimemkuta mpaka kupoteza fahamu , lakini mheshimiwa licha ya kuonyesha hali ya wasiwasi hakuwa tayari kuweka wazi ni jambo gani lilimkuta. “Linda nipe taarifa ya kinachoendelea?” “Mheshimiwa taarifa ni zile zile ni Zaidi ya masaa nane sasa ndege haijapatikana kwenye Rada na satelaiti , na wataalamu wa anga wanajaribu kuifatilia kwa ukaribu”Alijibu Linda na kumfanya mheshimiwa chozi la utu uzim limtoke.

.

“No .. no Lorraine you are not dead”Mheshimiwa aliongea kwa uchungu kiasi kwamba Linda alitoa machozi na kumuonea huruma mheshimiwa. ****

.

WHITE HOUSE -USA 1998 MARCH 8.

.

Ndani ya ofisi ya kiserikali ya Marekani ,alionekana mheshimiwa Raisi , mwenye jina maarufu The First Black akiwa ameketi kwenye kiti chake huku akiwa ameshikilia faili lililokuwa na nembo ya ‘Top Confidential’ ikimanaanisha Nyaraka ya Siri sana. ‘Life and Death Operation’(LADO) ndio jina la kichwa cha karatasi kilichokuwa kikisomeka juu kabisa ya karatasi alioshikilia mheshimiwa The First Black(TFB) huku akionekana ni mwenye umakini mkubwa sana kusoma karatasi hio ambayo imetoka kwenye faili lililokuwa mezani .

.

Ni ndani ya dakika kama kumi na moja tu alizotumia Mheshimiwa huyu kusoma , simu yake ilianza kuita mfululizo kiasi cha kumfanya mheshimiwa huyu aichukue na kuipokea . “Yes Rogan whati is news?” “Mr President the plane has landed safely on Life and Death Island”Ilisikika sauti na bwana huyu alitabasamu. “Very Good Rogan Activate Project LADO and all Concealment Protocol should be followed strictly, I will deal with the Rest”Baada ya kuongea maneno hayo simu ilikatwa na mheshimiwa huyu akachukua simu na kupiga na muda huo huo mlango wa ofisi ya mheshimiwa ulifungulikiwa na akaingia mwanadada wa kizungu mwenye umri kati ya miaka therathini hivi kupanda alievalia suti ya zambarau na blazia nyeupe na viatu vyenye kisigino kirefu ‘high heels’ “Christine nipe taarifa ya kinachoendelea huko ulimwenguni” “Mheshimiwa hali sio shwari kwa sasa , mataifa mengi yanahitaji msaada kutoka kwetu , juu ya upoteaji wa ndege ya Malaysia Airlines, ufupi ni kwamba mheshimiwa dunia imesimama kutokana na tukio hili”Mheshimiwa alisimama na kutembea kwa kuzunguka kwenye hii ofisi. “Endelea kutoa taarifa kwa kila anaepiga simu, na waambie serikali yetu itafanya kila namna kuhakikisha ndege hio inapatikana”Aliongea mheshimiwa na kisha Christine alitoka na kwenda kuendelea na kazi .

.

Huyo mwanadada alikuwa ndio msemaji mkuu wa kurugenzi ya White House. Baada ya Christine kutoka . mheshimiwa alivuta faili lingine kwenye droo ya meza , lililokuwa likifanna na lililopo mezani . utofauti wa faili hili na lile ni kwamba juu ya karatasi iliokuwa ndani ya faili hilo ilisomeka kwa jina la ‘The Agrement’ huku kukiwa na baadhi ya orodhesho la mashirika makubwa Duniani ya kijasusi na sahihi za wakurugenzi wakuu wa mashirika hayo. The first Black aliangalia sahihi hizo, lakini kuna jambo moja ambalo lilionekana halikumridhisha. “Shirika la Urusi pekee la kijasusi ndio Saini yao hapa haipo ,Beijing wamenihakikishia kwamba watashughulika na swala hili , lakini bado nina wasiwasi”Aliwaza mheshimiwahuyu na kurudisha mafaili yote kwenye Safe Box ndani ya ofisi yake. **** DAR ES SALAAM ,TANZANIA 1998 -March 8. Ni ndani ya familia moja ya kitajiri maarufu ndani ya Masaki , walionekana wanafamilia hii wakiwa kwenye hali ya furaha sana , na hii yote ni baada ya kiumbe kipya kuja duniani ndani ya familia hio. Rahel pamoja na Bi Salome walionekana furaha ilikuwa imewazidia kiasi kwamba muda wote walikuwa wakipokezana kubeba kitoto kichanga kalikozaliwa. “Rahel umemleta mtoto mzuri sana duniani , anafanana kwa asilimia mia moja na wewe na hili limenifurahisha Zaidi , asante kwa kumlindia mwanangu Adebayo heshima yake”Aliongea mwanamama huyu huku akimwanglia mtoto aliekuwa kwenye mikono yake , muda huu ikiwa yapata saa mbili za usiku. Wakati wanawake hawa wanaendelea kufurahia kiumbe kilichokuja duniani , alionekana kijana wa makamo umri wa Rahel akiingia ndani hapa huku akiwa amelewa chakali , baada ya kuingia ni kama hakuwa akijali waliokuwa sebuleni kwani alipandisha ngazi moja kwa moja. “Adebayo utaacha nini kulewa hivyo wewe”

.

“Mama niache maamuzi ulioyafanya licha ya kwamba nimeyakubali ila ni yenye kuniumiza na njia pekee ya kujipoza ni kunywa”Aliongea kijana huyu na kisha alijikokota na kuingia chumbani kwake huku nyuma akimuacha Raheli aliekuwa akimwangalia kwa huzuni. “Tutampa jina la Edna”Aliongea huyu mama mtu mzima na Raheli alitabasamu. “Ni jina zuri mama”. Upande mwingine mkoani Ruvuma manispaa ya Songea katika familia ya bwana Senga kulikuwa na majonzi makuu , huku mtu aliekuwa akilia kama mtoto alikuwa ni Senga, bwana huyu katika kilio chake alikuwa akitamka neno ‘Mke wangu na mtoto wangu mmeniacha ‘ bwana huyu alionekana watu wake muhimu walikuwa wamapatwa na jambo baya sana. “Yote ni mipango ya Mungu Senga huna budi kumshukuru Mungu”. “Hapana Desmond , ndio kwanza naanza kuyaona mafanikio lakini mafanikio yangu yanasababisha mke wangu na mtoto wangu Denis kufa , bora ningebakia maskini huenda wasingeweza kupanda ndege na haya yote yasingewatokea” Senga alikuwa akilia sana , na katika kilio chake ilionekana yeye ni moja ya familia nyingi duniani ambazo ni wahanga wa upoteaji wa ndege ya Malaysia Airlines. Hakuna alieweza kumfariji bwana huyu akapata unafuu , mapenzi yake kwa watu walipotea na ndege yalikuwa ni makubwa mno

.

, kiasi kwamba hayakuweza kupimika kwa aina yoyote ile ya kipimio, alikumbuka safari ya kimaisha aliopitia na mke wake Blandina ya msoto hatimae kupata pesa na utajiri na Mungu akawabariki mtoto wao wa kwanza , lakini Mugnu huyo huyo akawachukua wote wawili na kumuacha Senga akiwa katika majonzi na machungu makubwa ndani ya moyo wake , hakika maumivu yake hayakuwa ya kupimika hata kidogo na na waliokuwa karibu yake hawakuweza kufanya jambo lolote Zaidi ya kumuonea huruma. Bwana huyu hakujali tena mali alizokuwa nazo , alikuwa radhi kutoa kila kitu alichokuwa nacho iwapo mtu yoyote atatokea na kusema kwamba anaweza kuwarejesha wapendwa wake duniani , lakini bado jambo hilo halikuwa likiwezekana , na tumaini hilo likabakia kuwa ndoto ya mchana.Na waswahili wanakazia kwa msemo wao , alieenda ameenda na waliobaki Maisha yanaendelea,

.

TUKUTANE KESHO SAA NNE NITAWEKA VIPANDE VIWILI KUTIMIZA DENI ..SAA KUMI JIONI NAMALIZIA VITATU KAMA KAWAIDA Ndio kwanza simulizi inaanza , so tuvumiliane ili niendeleee kuhakikisha mnafurahia hii simulizi SURA YA ISHIRINI NA NANE

.

TANZANIA 2013 -JULY Ilikuwa ni mwezi July ndani ya jiji la Dar pilika pilika zilikuwa za hali ya juu ndani ya jiji hili , si kwa wanausalama ,sio kwa majeshi , sio kwa wananchi , kwa mara ya kwanza jiji la Dar linaonekana kuwa safi kuliko siku zote.lakini haikuwa kwa swala la usafi tu , lakini pia ulinzi ulikuwa umeimarishwa kila kona ya jiji hili, huku makachero wa kizungu pia wakionekana kulandalanda huku na huko kuhakikisha hali ya usalama. Naam hii yote nikutokana na ujio wa Raisi wa taifa kubwa duniani , taifa lenye ushawishi kila kona ya dunia , taifa ambalo lina uchumi mkuwa duniani , taifa ambalo linaongoza kwa teknolojia kubwa duniani,Raisi ambaye kwa mara ya kwanza anazuru ndani ya taifa la Tanzania na kufanya dunia isimame na kushangaa tukio hili la kipekee kabisa kutokea ndani ya taifa hili. Ni baada ya masaa kadhaa ya ndege kubwa ya Raisi kutua ndani ya uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na mheshimiwa Raisi Kigombola raisi wa Tanzania akiongozana na viongozi wakubwa wa Tanzania walionekana kuwa katika hali ya furaha maa baada ya kumpokea raisi Barrack Mabo. Mheshimiwa Raisi Kigombola alijisikia fahari sana , na katika Maisha yake ya uongozi alijihisi ni jambo kubwa sana ambalo amelitimiza , kwa kumtoa raisi wa dunia ambaye alikuwa na majukumu mengi duniani na kuja kutembelea taifa dogo la Tanzania. “Ndoto zangu zimetimia nina uhakika maadui zangu ndani ya taifa hili wataelewa uwenzo na nguvu niliokuwa nao.,kumleta raisi wa Dunia Tanzania sio jambo dogo”Aliwaza mheshimiwa huyu wakati wimbo wa Taifa ukiendelea , licha ya kwamba mzee huyu alikuwa akiimba wimbo huu lakini akili yake iilikuwa ikiwaza maadui zake na mipango yake. “Tanzania itakuwa yangu milele na milele ,m nitaacha mizizi ambayo hakuna kiumbe yoyote ambaye ataweza kuingoa”Aliendelea kuwaza. Baada ya shamra shamra za aina yake hatimae safari ya kuelekea ikulu ilianza huku asilimia tisini ya ulinzi wa raisi huyu ulikuwa ukiratibiwa na vikosi vyake ambavyo vilikwisha kutangulia nchini kuhakikisha hali ya usalama. “Karibu sana Rafiki yangu ndani ya Tanzania”Aliongea mheshimiwa Kigombola . “Asante sana Kigombola , nimefurahi na mapokezi ya watanzania”aliongea na kumfanya mheshimiwa Kigombola aendelee kujiona yeye ndio yeye na ndio Raisi wa Tanzania ambaye ana akili nyingi kuliko raisi yoyote yule. Baada ya chakula mheshimiwa Bamo alipewa ofisi yake kwa ajili ya kuendelea na majukumu ya kazi , kwani bwana huyu hakuwa ni mwenye kupumzika kabisa , muda wote alikuwa macho akifanya kazi , alikuwa ni raisi wa Taifa la Marekani , lakini alikuwa akitoa maamuzi na maelekezo yanayoenda kutekelezwa na maraisi wa mataifa mengine na hii yote inaifanya kazi yake kuwa ngumu sana na kumfanya kuwa bize. Wakati akiendelea na kazi ndani ya ikulu ya Tanzania aliingia bwana mmoja alievalia mavazi ya kikachero yenye nembo ya taifa la Marekani, bwana huyu alionekana kuwa kijana mdogo , lakini alikuwa na nafasi kubwa katika kikosi cha ulinzi cha mheshimiwa huyu. “Nipe Ripoti Chriss?”Aliongea mheshimiwa huyu na kisha akampatia mheshiwa Bahasha aliokuwa ameishikilia mkononi na Raisi huyu aliifungua na kuangalia kilichomo ndani , na alikuta ni picha, alizitoa na kuanza kuziangalia na bwana huyu macho yalimtoka. “Wanafanana kwa asiliamia kubwa na Agent no 17, Umefuatilia ni nani baba wa mtoto huyu?” “Mheshimiwa tumekusanya ripoti kadri tulivyoweza , huyo mwanadada anaitwa Edna ni mtoto wa Rahel na Adebayo wanafamilia wanaomiliki kampuni changa ya VEXTO”. “Lakiini imekuwaje huyu Edna akafanana kwa asilimia mia moja na Agent 17?”. “Hilo ndio swali lililofanya tuendelee kufatilia kwa ukaribu kama kuna muunganiko wowte kati ya 17 na Edna na katika uchunguzi tuliofanya tulibaini watu waliohusika kumfanyia matibabu Rahel kipindi cha ujauzito wake , wote walifariki vifo visivyoleweka lakini swala hilo halikuweza kutukwamisha kupata taarifa na kutokana na uwepovyanzo vingi vya taarifa tulivyovipandikiza hapa nchini tumegundua Agent 17 na Edna walizaliwa mapacha wa kufanana”. “Nini, unahakika na hio taarifa Chriss” “Ndio mheshimiwa”. “Sawa Chriss , kazi nzuri kaendelee na majukumu yako mengine , ila hili swala kwa sasa nitampatia mtu mwingine ashughulike nalo , kwasasa hatupaswi kufanya jambo lolote lile”Aliongea Mheshimiwa naChriss alitoka ndani ya ofisi. Baada ya Chriss kutoka mheshimiwa alirudia kuangalia zile picha mezani kwake kwa umakini mkubwa huku akionekana kuwaza sana. “Hapana kwa namna yoyote ile siwezi kuruhusu tundu lolote ambalo litafanya Operation LADO kufichuka, Uwepo wa Edna duniani utamfanya Agent 13 na 17 kutaka kufahamu ukweli uliotokea katika Maisha yao ya nyuma kama watabahatika kumuona Edna na suluhisho la haya yote ni Edna kufa”Aliwaza mheshimiwa huyu huku akiangalia picha hizo. Baada ya lisaa kukaa kwenye ofisi yake hatimae mheshimiwa Kigombola aliingia ndani ya ofisi hio na kukaa kwa ajili ya mazungumzo na mheshimiwa , swala la kwanza ni juu ya mipango yao , ambayo imemfanya bwana huyu mwenye madaraka makubwa duniani kufika ndani ya taifa , lakini pia swala la pili ni jambo binafsi alilokuwa akitaka kuomba msaada kwa Kigombola . “Kigombola , kuna jambo la ziada unapaswa kunisadia”Alianzisha maongezi. “Jambo gani hilo mheshimiwa wewe ni Rafiki yangu na nipo tayari kukusaidia jambo lolote hata kama unataka kasehemu ndani ya hii nchi naweza kukupatia”.Alitabasamu na kisha akatoa picha na kumpa Kigombola. “She need to die and you as my friend utanisaidia katika hili”Aliongea Bamo na kumfanya Raisi wa watanzania ashangae nini tatizo. “Mheshimiwa kuna haja gani ya mtoto kama huyu kufa?”. “Kigombola fanya kama ninavyokuambia huyu msichana lazima afe la sivyo mafanikio yangu ambayo nimeyajenga kwa miaka na miaka yanaweza kuwa hatarini na uwepo wa huyu msichana”Aliongea na kumfanya Kigombola kumwangalia mheshimiwa mwenzake na kutingisha kichwa kwamba jambo hilo atalifanyia kazi. Wakati hayo yakiendelea upande wa pili nchini Rwanda Jeremy anapokea taarifa kutoka kwa shushu wake ikulu iliokuwa kwa mfumo wa ujumbe wa sauti. “Edna yupo hatarini kubaki nchini Tanzania” “Nilitegemea swala hilo , ngoja niwasiliane na upande wa pili wa mpango wetu”Alijibu na simu ilikatwa. “Fu**ck you Amerika , I must pay for what you Did , nitachimba na kuujua ukweli wote”Aliongea kwa hasira Jeremy. **** Edna kama kawaida yake alikuwa amekaa chumba chake cha kujisomea akiwa anafanya baadhi ya kazi za hapa na pale kama ilivyokuwa kawaida ya mwanadada huyu kutokupumzika , lakini ufanyaji kazi wake wa leo mwanadada huyu haukuwa kama wa siku zote , alikuwa ni mwenye kuwaza mambo kadha wa kadha lakini kubwa lililokuw andani ya kichwa chake ni juu ya Roma. Aliinua simu yake na kisha kuangalia picha zilizotumwa na Suzzane zikimuonesha Roma akiwa na Doris siku kadhaa nyuma wakionekana wameshikana viuno , lakini pia picha ya pili ilikuwa ikimuonesha Roma akitoka ndani ya nyumba ya Rose , lakini picha nyingine ikimuonesha Roma akiwa amekumbatiwa na mwanadada ambaye sura yake haikuonekana , lakini pia picha nyingine Roma akibusiana na Nasra kwenye gari , lakini pia picha nyingine Roma akiingia ndani ya chumba cha hoteli na Neema luwazo , Picha zote hizi zilitumwa na mwanadada Suzzane mlinzi wa siri wa Edna. “Suzzane anafanya mambo ambayo sijamwagiza , haikuwa na haja ya kumfatilia Roma , ni mume wangu ndio lakini sio kwa mapenzi ila kwa mkataba na ukiisha tunaachana , sitaki kuyaingilia sana Maisha yake” Aliwaza Licha ya kuona picha hizo lakini kwa Edna hakuonyesha kukasirika alichukulia kawaida tu lakini alionekana kuna kitu hakipo sawa , aliona licha ya Roma kuwa mume wake kisheria ,, lakini hakuwa akiishi kama mume wake ,vitendo ambavyo aliona Roma anafanya vitamletea shida kama watu watagundua kuwa Roma ana mahawala wengi Wakati akiendelea kufikiria mala mlango wake uligongwa na alinyanyuka na kwenda kuufungua na uso kwa uso na Roma. “Honey Darling Chakula tayari , twende tukale”Aliongea Roma huku akiwa ametabasamu na Edna alimwangalia Roma na hakummaliza. “Sijisikii kula” Aliongea na kisha akafunga mlango kwa hasira , ila Roma hakuondoka alisimama na kugonga tena na awamu hii mlango ukafunguliwa tena na mwanadaa huyu huku akionekana ni mwenye kuwa na hasira. “Hivi Roma nini , si nimekuambia sijisikii kula , unaweza kwenda kuendelea” “Namimi siwezi kula peke yangu, na nitaendelea kugonga mlango mpaka ushuke tukale” Edna alimwangalia Roma na kwa alivyokuwa ana muona Roma aliamini bwana huyu alichokiongea alikuwa anaaanisha. “Kale na Bi Wema , kama huwezi kula peke yako” “Bi wema kasema hajisikii vizuri atakula baadae,Mke wangu mbona huna heshima kwa mumeo twende basi” “Yaani Roma wewe sijui ni mwanaume wa aina gani huelewi”Aliongea Edna huku akitoka na kufunga mlango na kuelekea chini akitangulia huku Roma akimwangalia kwa nyuma na kuishia kutabasamu. Bi Wema aliekuwa akiingia kutoka nje alijikuta akitabasamu na moyo wake kuwa wa moto mara baada ya kuona Roma na Edna wakiwa kwenye meza wakila chakula , ilikuwa ni picha ambayo ilimvutia sana, kwake na alitamani iwe kila siku kuona wanandoa hao wanafanya mambo kwa pamoja , hakupenda namna Maisha ambayo Edna alikuwa akiyaishi , alikuwa akiamini mwanamke hawezi kukamilika pasipo ya kuwa na mume na pia Mume hawezi kukamilika pasipo ya kuwa na Mke. “Roma ..!!!”Aliita Edna na Roma alimwangalia Edna. “Ndio mke wangu” “Kwanini haupo kama wanaume wengine”. “Unamaanisha nini mke wangu , usiniambie ushaanza kunifananisha na wanauame wengine?” “Sio kukufananisha na wanaume wengine , lakini wewe upo tofauti kabisa , haupo siriasi na Maisha , kazi umepata lakini unaishai kucheza gemu na kufanya uzinzi”Aliongea Edna huku akionesha yupo siriasi ila Roma hakujali kwanza alitabasamu. “Mke wangu nitakuwaje siriasi na pesa zote hizo ulizonazo , nani wakuzitumbua, wote tukiwa na pesa hainogi bebi , mmoja akiwa tajiri mwingine asiwe na pesa ili kuwe na mtu wa kutumbua pesa na kula bata ,Bebi Edna tuseme wewe umeolewa na mimi na ukanikuta na mipesa kama hii yako, kwanini uanze kujihangaisha na Maisha badala ya kula bata” “Kwa hio wewe kazi yako ni kutumbua pesa zangu ?” “Halafu mke wangu sio pesa zako ni za kwetu , ushasahau sisi ni mwili mmoja”Edna alimwangalia Roma kwa hasira kali mno , alishindwa kuelewa Roma ni mtu wa aina gani yeye yupo siriasi kumwambia mambo ya maana lakini anaanza kuongea ujinga juu ya maswala ya kutumbua hela. “Kama unawaza kutumbua pesa zangu sahau , usipo tafuta zako hutipata chochote kutoka kwangu” “Mke wangu kama hutaki nikitumia pesa zako nani atazitumia ...Halafu mke wangu mbona kama unampango wako kichwani wa sisi kutafuta mtoto halafu huniambii nijiandae”Edna alimwangalia Roma huku akishangazwa na uroppokaji wake , ‘Neno mtoto ‘ ni swala ambalo hakuwahi kulifikiria hapo kabla . “Nani mimi … Mtoto ,, hata kama nitake mtoto siwezi kuzaa na mwanaume asiye siriasi na maisha Watoto wataiga nini”. “Bebi kama hutaki kuzaa na mimi mumeo unataka uzae nje ya ndoa ?”Edna baada ya kuona topic ambayo hakuwa akiipenda Roma kaikomalia , alinyanyuka na kupandisha Ngazi kuelekea chumbani kwake huku Roma akiwa ni mwenye kutabasamu. “Huyu mwanaume muda wote anafikiria ujinga tu , nifanye nini ili angalau kumbadilisha ili hata niwe na kujiamini nikimtambulisha mbele za watu”Aliwaza Edna huku akiwa amesimama kwenye dirisha chumbani kwake. Ukweli ni kwamba kuna muda Edna alitamani kumuona Roma abadilishe mfumo wake wa kimaisha , alitamani awe kama wanaume wengine ambao wako bize na kutafuta Maisha na kuongoza biashara hatimae aweze kujivunia kuwa na mume mwenye mafanikio , lakini haikuwa hivyo , Roma alikuwa Roma kama alivyomtoa kule kwenye kazi yake ya ubeba mizigo , hakuwa amebadilika hata kidogo ,tabia yake ilikuwa vilevile Edna wakati akiendelea kufikiria akiwa anaangalia eno la Nje alimuona mwamba Roma akaitoka tena awamu hii akiwa amepigilia miwani ya jua kabisa na haikueleweka katioa wapi , alimwangalia namna ambavyo anaingia kwenye gari yake na kuwasha na mpaka lilipotokomea nje ya geti. “Lazima anaenda kutafuta mwanamke pale”Aliwaza Edna huku akirudi kitandani na kukaa.

.

ENDELEA KUSOMA ```

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA

Mpya zaidi Nzee zaidi

Ads related

Smartwatchs